Mkandara;9817706]Mchambuzi,
1. Swala la mapato na uchangiaji wake haujalishi kiasi gani bali asilimia ngapi ya pato lako unachangia. zanzibar ina watu wasiozidi mil 1 wakati bara ina watu mil.40 ulitegemea vipi mchango wa Zanzibar ulingane na ule wa bara?
Hizi hesabu gani mnatumia ili uupata Ukweli? Hivi kweli wewe kama mshahara wako ni mil. 5 na mkeo ni laki 3 lakini anachangia kwa asilimia sawa na wewe (toka pato lake) kuingia mfuko wa familia, basi ina maana mkeo hana mchango ktk familia kwa kutazama kachangia Tsh ngapi?
Mkuu, kwanza niseme tunachokitaka ni kumaliza utegemezi wa Zanzibar kwa hila na mbinu. Kama unakubali Zanzibar ina watu milioni 1,ukubali wao kudai usawa katika muungano ni ujuha. Tume ya Warioba wznz walidai 50-50 wakisema ni wabia sawa wa muungano na wakapewa.
Hao wznz 15 wa tume wanawakilisha watu milioni 1 unaosema. Vipi mbona hilo hulioni?
Kule Dodoma kuna wabunge 81 wanaowakilisha watu milioni 1.
Mbunge mh Mnyika anawakilisha watu zaidi ya milioni 1. Huo udogo wa znz upo wapi?
Kwenye ulaji wanahitaji usawa, kwenye kuwajibika ni wadogo na wachache. Hilo halikubaliki tena.
Kumbuka hawa watu wamevunja katiba ya JMT kwa kutumia watu wao 50. Huo udogo wa znz unatoka wapi.
Misaada na mikopo wanataka zaidi ya mkoa wa Dar es salaam. Huo udogo unatoka wapi.
Znz inatengewa pesa nyingi kuliko halmashauri 54 za Tanganyika kwa wakati mmoja. Huo udogo unatoka wapi.
Kila wanapotakiwa wawajibike wanakimbilia suala la udogo. Mambo yakiwa tayari wanadai haki na usawa.
Hili lazima lifike mwisho, haiwezekani udogo usiwe katika kuwajibika bali kuomba,nataka,na mimi pia!
Kuhusu mfano wa mke, huyo mke angekuwa na pato anachangia hapo ingeeleweka. Znz haina mchango katika JMT ya Tanzania. Mchango mkubwa wa znz ni kutaka, kuomba na kudai. Kwa bajeti ya bilioni 400 hakuna chochote kinachoweza kuchukuliwa kutoka hapo. Kuchukua ni sawa na dhambi kwasababu unamkamua ng'ombe mgonjwa asiye na kiwele.
2. Wewe mwenyewe umesema wazi ktk wazo lako la kwanza, hivyo unachoshangaa kipi haswa ktk swala hili? kwanza thibitisha maelezo yako kuhusu michango ya Tanganyika kwa Zanzibar ktk mambo yasokuwa ya Muungano halafu tuendelee (tupe takwimu zako)..
Mwaka wa bajeti wa 2013/2014 znz ilipewa bilioni 32 kupitia ofisi ya makamu wa Rais. Pesa hizo hazijulikani ni za nini. Bilioni 30 ni sawa na 7.5% ya bajeti yao. Bado wana 4.5% na wana pesa za bajeti achilia mbali madeni ya ndani na nje.
Nakisi ya bajeti ya znz inafidiwa na hazina Dar. Tundu Lissu kalisema mbele yao na waziri Aboud kaunga mkono.
Elimu ya juu isiyo ya muungano inagharamia wznz 1700 bila mkopo, I mean bure huku watoto wa walipa kodi wa Tanganyika wakihangaika kwa mikopo na hata kunyimwa kwasababu hawana uzanzibar.
Deni la ndani la znz linafidiwa na JMT. Mfano mzuri ni wao kupitisha bili za umeme kulipwa na JMT wakati hawakusanyi bill zao. Wizara ya mambo ya nje na ndani hawana bajeti. Mchango wao ni sifuri katika hayo.
Ndiyo maana hutasikia hata siku moja wakidai ulinzi na usalama., wanataka mkataba.
Mikataba ni pamoja na kuendelea kufaidika na free ride.
Na mwisho, mishahara ya SMZ imekuwa inatoka hazina kuanzia enzi za komandoo.
Waulize waganyakazi wa SMZ, mishahara inapochelewa huwa wanasubiri itoke wapi.
Orodha ni ndefu, kwa bilioni 400 hatuhitaji kuorodhesha kila kitu. Kama hukubali utegemezi wa hali ya juu, utakuwa uanajidanganya. Habari ndio hiyo.
Mkuu ikiwa bajeti ya taifa (muungano) inawahusu Zanzibar kwa asilimia 5 tu yaani yale mambo 22 ambayo hayana gharama kubwa wala mapato makubwa ukilinganisha na yale yasokuwa ya Muungano, iweje bajeti hii inaposomwa isemekane kuwa inachangia Zanzibar zaidi ilihali bajeti hiyo kuna mambo mengi hayahusu muungano?
Nguruvi3 kisha sema asilimia 95 ya bajeti nya JMT ni mambo ya Tanganyika Wazanzibar wanafanya nini humo?. Sasa leo hayo mambo madogo ndio yamekuwa yanazalisha kuliko yale makubwa ya asilimi 95 kweli? mapato ya taifa yako wazi GDP na michango yake inajulikana wazi kuwa ni Kilimo, madini, services, usafiri, utalii, n.k haya yashindwe na kodi ama ushuru wa vitu gani?
Mkuu narudia tena, ni mambo ya Tanganyika kwasababu wameondoa kila jambo kwa kutumia katiba yao.
Leo tunajadili jini kuhusu baraza la mitihani ikiwa wameondoa?
Tutajadili nini kuhusu bandari ikiwa wameondoa.
Ndivyo ilivyo kwa TRA ambapo makusanyo yao yanabaki huko na wala hayaji muungano.
Tutajadili nini kuhusu znz ikiwa wana wizara zao ambazo waziri wa muungano hana nafasi.
Hata waziri mkuu wa JMT hawmjui leo tunajadili nini nao.
Ni kwa msingi huo hata wale wabunge 81 wanakuja kupoteza muda maana hakuna tunachojadili. Katiba yao ya 2010 imeshavunja muungano, ni heri watuache nasi tujadili mambo yetu bila bughudha.
Lini tuliwaomba tuwe na mwakilishi BLW. In short mambo ya Tanganyika ni ya Tanganyika na wao kuingia katika mjadala ni haramu. Inakuwa halali kwasababu tu ya mshiko, kimantiki hakuna muungano, wznz walishauvunja siku nyingi.
Leo tujadili kujenga vyoo vya shule halafu tuwapelekee waidhinishe. Please, this must come to an end.
Wewe umesema ni milioni 1. Huo uwezo wa ku dictate terms za watu milioni 43 wanaupata wapi.
Kuwa na bajeti moja kunaiumiza vipi Tanganyika kama sio Tanganyika kufaidika zaidi pale michango ya Kimataifa (karibu asilimia 50 kutoka nje) kwa ajili ya Bandari, Elimu, Mabarabara, Afya, Miundombinu, vifaa na zana za kilimo na kadhalika, mambo yasokuwa ya Muungano Tanganyika hutumia jina la Tanzania na Zanzibar isifaidike na matumizi ya jina hlo. Kodi na ushuru kuwepo ktk mambo ya muungano ni lazma isipokuwa hizo kodi zinakusanywa toka wizara gani ndilo tunalotakiwa kutazamwa.
Hapa napo unashindwa kuangalia mambo kwa upana wake.
Tueleze bajeti ya ulinzi ambayo ni zaidi ya Trilion moja znz inaweza kuchangia nini.
Bajeti ya mambo ya ndani inachangia nini. Ada za mashirika na taaisisi za kimataifa znz inachangia nini.
Madeni ya ndani znz inalipa kwa kutumia nini. Kumbuka ni bilioni 400 ambazo ni sawa na makusanyo ya TRA ya Tanganyika ya wiki mbili kama si mwezi.
Huoni mambo yote hayo unaangalia misaada ya Washington.
Huu ni utumwa mkubwa sana wa kuamini pesa za washington ni nzuri kuliko free ride wanayokula sasa hivi.
Lakini pia kumbuka, waziri wao wa fedha amesema asilimia 88 ya mikopo ya znz ya nje inadhaminiwa na JMT.
Sasa tuambie katika bajeti yao ya 2014/2015 kama alivyosema
Mchambuzi, wapi katika hizo bilioni 400 kuna kifungu cha kulipa deni.
Hivi Mkandara hawa wasioweza kulipa bill za umeme wanawezaje kulipa madeni ya nje.
Ni wazi deni la nje analibeba Mtanganyika. Hapa tunaongelea bilioni 400 tu, ambazo nusu ni Mishahara
Hivi kweli Mkandara unaamini kwa dhati kabisa kuwa misaada na mikopo ndio msingi wa muungano huu.
Ikitokea Paris club wanagoma kutoa misaada na mikopo basi muungano utakufa.
Muungano utakufa kwasababu ni kwa kutumia jina la Tanzania, mchango wa znz unaonekana na si kutumia chanzo kingine. Huu utumwa wa akili ni mbaya kuliko umasikini wowote ule.
Kama Zanzibar na Tanganyika zote zinatakiwa kuchangia asilimia 20 ya kodi hizo ktk mfuko wa Taifa haijalishi Zanzibar wamechangia kiasi gani bali tutazame tofauti ya kodi hizo ktk mchango wa mfuko. Kwa mfano, Unapoingiza gari Tanganyika unatozwa Tsh mil.5 na kati ya hizo laki 5 zinakwenda mfuko wa Taifa, na Zanzibar unapoingiza gari unatozwa mil.2 lakini pia laki 5 zinakwenda mfuko wa Taifa. Hapa panakuwa hakuna tatizo la mchango wa nchi na wala haitazamwi ni kiasi gani nchi moja imechangia dhidi ya nyingineyo kutokana na sababu millioni za uwekezaji wetu wenyewe ktk maeneo hayo.
Tlliwahi kufanya hivyo znz wakasema wana nyonywa. Ndio msingi wa madai yao.
Walichokifanya ni kuacha kuchukua kodi ili bidhaa ziingie Tanganyika bure.
Wakatumiwa na wafanyabiashara kudhoofisha ukusanyaji wa kodi.
Kuendelea ku entertain upuuzi huo ni kuliumiza taifa letu. Katiba yao ya 2010 haitambui ZNZ kama sehemu ya Tanzania.
Lakini basi huwezi kuchukua nusu nusu. Kama wao wameondoa mambo ya muungano, wapi tunategemea kodi itapatikana? Mfano, utakusanya vipi kodi ikiwa wameshaondoa bandari. Hili ni tatizo walilozua wao.
Nchi zinapoungana haitazamwi nini mchango wake bali sehemu husika zinafaidika vipi na rasilimali za taifa, kufikiri nje ya Utaifa ni gonjwa sugu la waafrika ambao Ukabila na utumwa vimewaathiri hadi keshokutwa. Nchi kama Marekani au canada kuna watu wa kila kabila, kila asili na wote hutambuliwa kwa haki sawa na mtu mwingine yeyote. Hakuna fikra za sisi Texas tunazalisha kuliko Maryland au hizi siasa za WAO against SISI. Hao Wazenji waloanzisha hizi fikra za kujitenga hawana tofauti kabisa na kundi hili la Ukawa, hivyo wamekutana wendawazimu wawili na watu mnawashangilia kwa sababu Ubaguzi kwetu ni asili baada ya kutumikia Utumwa kwa karne 500. Kwa nini mnatuletea hizi habari za Uzanzibar na Utanganyika!
Singida hawajatengewa nafasi maalumu wala hawapewi upendeleo maalumu. Mtwara hawana katiba yao na ni Watanzania. Mtu anaweza kuishi popote bila kuulizwa wewe ni Mkilimanjaro au Mwarusha. Ubaguzi umeletwa na Zanzaibar na tunataka tukomesha mbegu hii chafu.
Wznz si raia bora kuliko wasumbawanga au wa Iringa. Huu upendeleo wa kuwafanya ni raia bora ndio hasa unatuletea matatizo.
Hapa jawabu ni moja tu kila jambo lazima liwe la Muungano tuvunje fikra hizi za pande zote mbili na kama hamtaki tafuteni mahala engine mkaishi lakini ubaguzi huu hauwezi kupongezwa wala kuvumiliwa..sitoendelea na fikra za Utanganyika wala Uzanzibar ni upuuzi ambao nashindwa kabisa kuutetea kwa hali wala mali.
.Mkandara, sio wewe umesema mambo yameingizwa kinyemela ili kuwaonea wznz.
Leo unageuka na kusema kila jambo ni la muungano.
Si tumefanya hivyo miaka 50, mbona wakati wznz wanaondoa mambo bila kushauriana na sisi hujawakemea.
Yaani unawapa hata haki ya kuvunja katiba ukitaka tukae kimya kwasababu ni wznz unaodhani ni watu bora sana duniani.
Mkandara, katiba ya 2010 ya znz haiwatambui kama raia wa Tanzania bali wznz.
Leo unataka mambo yawe ya muungano, kwa lipi na sababu zipi.
Je, nani wa kunyooshewa kidole, yule anayejitoa kwa kuvunja katiba au huyu kondoo Tanganyika aliyekaa kimya miaka 50.
Lakini pia Mkandara kasema Tanganyika imevaa koti la muungano. Leo anarudi na kusema tuweke mambo yote katika koti lile lile analosema ni chafu. Mkandara where do you stand on issues. Flip flop si jambo jema.
Huwezi kusema neno kesho ukalibadilisha tukakaa kimya. Unapotosha mkuu.
Mwisho, huwezi kuwalumu UKAWA. 2010 ZNZ walibadili mwelekeo wa siasa za nchi na muungano.
Wamevunja katiba, wametudhalilisha sana na wametukana kuwa wao si Watanzania.
Hatuwezi kuendelee na hali hiyo.tunataka Tanganyika ili tuendelee kufanya mambo yetu bila bughudha.
Hatuwezi kubeba zigo la samadi na kukaa kimya kwasababu tu zigo hilo lina miaka 50.
Sasa muda umefika, tunawatua chini. Zipo njia mbili tu.
1. Wakubali kukaa mezani ili tuafikiane tunawasidia wapi. Tunawasaidia maana hawana msaada the least to say. Uisogope kuwaambuia ukweli. Na siku hizi tunawaambia njia nyeupe hakuna anayefungua mdomo.
Wanajua ukweli kuwa tunaelekea kuwatua waendelee na katiba yao.
2. Ima hawataki kukaa mezani, tutaizindua Tanganyika kwa gharama zao. They will pay for it.
Wao ndio watakaoizindua Tanganyika, unfortunate kwa gharama kubwa sana.