Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Duru za siasa: Bunge la Katiba, upotoshaji na kiwewe cha kuzinduka Tanganyika

Mchambuzi
Hili suala la JFC linazidi kutupa maeneo ya kungalia na kufikiri.
Washabiki wa S2 kama Mkandara wanasema S3 ni tatizo kwasababu hiyo serikali ya shirikisho itakuwa inaelea.
Itakuwa haina vyanzo vya uhakika vya mapato na hivyo kukosa nguvu.

Katika JFC tunaona suala la mikopo na misaada linachukuliwa kama sehemu ya muungano.
Ni jambo hatari sana muungao kuendeshwa kwa kutumia vyanzo visivyo na uhakika kama misaada na mikopo.
Na znz wapo katika muungano kwa hilo tu, nje ya hapo hawana sababu na muungano.

Kwa ajili ya mjadala, tufanye assumption kuwa wahisani wamegoma kutoa misaada na mikopo kbaisa kama ilivyowahi kutokea.

Mapato
Kwa Tanganyika itakuwa ni trillion 11
Kwa Zanzibar itakuwa 400 Billion

Matumizi
JFC haielezi matumizi kwa 'specifics' kwamba hizo pesa za account ya pamoja zinatumika kwa mambo gani ikzingatiwa kuwa hakuna mambo ya Tanganyika isipokuwa Tanzania na Zanzibar

Mgawanyo
JFC imekuja na formula ya 21% ya ajira.
Ni formula gani inatumika kugawana mapato na matumizi kwa kila upande.

Hakuna formula inayoonyesha hiyo account ya pamoja inagawanywa vipi.
Lakini muhimu sana ni kuwa Tanganyika itachangia na znz kwa Billion 400 hata bila kutoa senti moja bado haitakuwa na uwezo wa kuchangia

Hii maana yake nini?
Chanzo cha uhakika cha mapato ya S2 ni kodi za Watanganyika. Ni makusanyo ya Tanganyika yanayopigiwa mahesabu ya kugawana na Zanzibar kama chanzo cha uhakika cha S2.
Huu nao ni aina ya upuuzi ambao Watanganyika lazima wauangalie kwa macho mawili.

Ni kwa msingi huo, washabiki wa S2 hawataki kuzungumzia kabisa chanzo cha mapato cha uhakika wa S2 isipokuwa wanahoji cha S3. Kwa mfano wa JFC tunaona instability kubwa sana ya muungano kinyume na inavyoaminishwa.

Kwamba, ili muungano uwepo ni lazima Tanganyika itoe kila ilicho nacho.
Wakati huo huo znz haina mchango wowote wa maana kama si hakuna kabisa.

Sidhani kama Tanganyika inahitaji JFC. Kuna sababu gani za msingi ikiwa hakuna mchango kwa upande mwingine.
Kwamba, tunachukua chetu na tunaita majirani wa nchi jirani ya znz kugawana. If this is not insanity, I don't know what it is.

Hoja ya chanzo cha uhakika cha mapato ya S2 inafia hapa, na haisemwi kwa kujua itaudhi wznz ambao hawana cha kuchangia
 
Ndugu Mchumi, hapa hujatueleza kitu ndiyo maana tunakuomba sana ukae kimya.
Kama unatumia data basi tunakuomba uweke kando misaada na mikopo. Hivyo ni vitu ambavyo huwezi kusema unavyo hadi uwe nacho. Ukisema mkopo wa bilioni 100 ni hadi uupate, na hata ukiupata ni wehu kushangilia mkopo kwasababu riba yake hasa kwa nchi masikini ni tatizo.

Kilichowasukuma akina Nyerere kuanzisha South South commission ni pamoja na kutaka kujikwamua kwa uhsirikiano wa nchi masikini na si kupitia Washinton n.k.

Tukirudi kwa data zako, mapato ya znz ni 400B na ya Tanganyika ni 12T.

Tunapokuwa na JFC:
1. Znz inachangia nini ikiwa mapato hayo tu,ambayo bila kuondoa hata senti tano hayatoshi kuendesha wizara moja ya muungano.

2. JFC inahudumiwa na mapato ya wanchama au inategemea misaada na mikopo? Na je ikiwa hakuna hiyo ina maana JFC haina kazi.

3. Kwa vile JFC imetoa kiwango cha ajira kama 21%, tuambie JFC inasema viwango gani viingine katika account kutoka kwa pande mbili zilizotajwa na sheria husika.

Kama hujui %, basi ukae kimya maana huna data. In fact kaa kimya tu hii iwe taarifa ili usije vuruga zaidi.

Nguruvi3,

Naona una nung'unika sana kiasi cha kujitoa ufahamu.

Kukusaidia nimekupa vigezo hapo vinavyotumiwa kiuchumi na nikabainisha Population na eneo la kila nchi. lakin pia nikakuwekea bajeti za kila nchi.
sasa kwa akili yako inawezekana kuchangia 50/50 kwa mazingira kama hayo? nafikiri hata mtoto mdogo hawezi kufikiria kama wewe. Naomba nikupe pole.

Haya ili kuunogesha huu mnakasha ambao watu wengi wameni PM kwa uchambuzi wangu naomba sasa kwa kuwa tuna bajeti za nchi zote mbili (JMTz na Znz )za 2014/2015 na Figure zake tuingie kwenye uchumi halisi sasa kwa kuweka data
. Naomba unijibu yafuatayo:

1. JE ZNZ INATAKIWA ICHANGIE KIASI GANI KATIKA MUUNGANO?
2. Sema wazi TGK inachangia kiasi gani katika muungano?
3. Lakin pia sema Znz achangie wapi na katika mfuko gani hizo pesa zake kwa huo muungano?.
4. Sema TGK inachangia katika mfuko gani huo mchango wake wa muungano?
5. Ni nani anayedhibiti matumizi na mapato ya huo mfuko na kuhakikisha haki inatendeka katika mgao wao.

Nafikiri tukipata majibu ya haya tutaweza kwenda vizuri katika mnakasha. Kwani hilo ndilo tatizo lililopo kwako kutoweka DATA hizo tokea awali zaidi ya wewe kunung'unika bila kutoa Data.

Tuweke wazi ili tuendeleze mnakasha.

Tuweke DATA hapo ili tuwweze kujadili tukiwa na takwimu au Data halisi. Kwani mwisho wake tunaweza kujua ni kama kweli ni kibri cha Znz kukataa kulipia Muungano au kuna namna ya baadhwi kujipendekeza kujitwika mzogo wote kama walivyo jitwika joho la Mvungano?

Jasusi kasema vizuri sana hapo juu. Naomba umsome.
Haieleweki unasimamia hoja zipi na za msingi gani. Huko JFC huna hoja, sasa unarukia mambo mengine kabisa.
Kumbuka jamvi na jukwaa hili haliendeshwi hovyo. Unadhani unaweza kutuchochea tuseme hovyo. Huko hatupo!
Narudia tena, tafadhali sana usiharibu mijadala kwa trivial na useless arguments kama hiyo.

Tunakushukuru sana, na tunaomba nafasi ya kujadili mambo yetu bila kuvurugwa. Ahsante sana, inatosha na tumekusikia

Nguruvi3,

Haya ni masuala muhimu sana kuweza kujua chimbuko la JFC na ili kuweka kuunogesha mnakasha huu naomba majibu yako. Tuache siasa hapa kwani uchumi ni DATA. hebu mwaga data mtaalamu wetu.

1. JE ZNZ INATAKIWA ICHANGIE KIASI GANI KATIKA MUUNGANO?
2. Sema wazi TGK inachangia kiasi gani katika muungano?
3. Lakin pia sema Znz achangie wapi na katika mfuko gani hizo pesa zake kwa huo muungano?.
4. Sema TGK inachangia katika mfuko gani huo mchango wake wa muungano?
5. Ni nani anayedhibiti matumizi na mapato ya huo mfuko na kuhakikisha haki inatendeka katika mgao wao.

Tuweke DATA hapo ili tuwweze kujadili tukiwa na takwimu au Data halisi. Kwani mwisho wake tunaweza kujua ni kama kweli ni kibri cha Znz kukataa kulipia Muungano au kuna namna ya baadhwi kujipendekeza kujitwika mzigo wote kama walivyo jitwika joho la Mvungano?

nasubiri majibu yako mtaalamu.

Mchambuzi
Hili suala la JFC linazidi kutupa maeneo ya kungalia na kufikiri.
Washabiki wa S2 kama Mkandara wanasema S3 ni tatizo kwasababu hiyo serikali ya shirikisho itakuwa inaelea.
Itakuwa haina vyanzo vya uhakika vya mapato na hivyo kukosa nguvu.

Katika JFC tunaona suala la mikopo na misaada linachukuliwa kama sehemu ya muungano.
Ni jambo hatari sana muungao kuendeshwa kwa kutumia vyanzo visivyo na uhakika kama misaada na mikopo.
Na znz wapo katika muungano kwa hilo tu, nje ya hapo hawana sababu na muungano.

Kwa ajili ya mjadala, tufanye assumption kuwa wahisani wamegoma kutoa misaada na mikopo kbaisa kama ilivyowahi kutokea.

Mapato
Kwa Tanganyika itakuwa ni trillion 11
Kwa Zanzibar itakuwa 400 Billion

Matumizi
JFC haielezi matumizi kwa 'specifics' kwamba hizo pesa za account ya pamoja zinatumika kwa mambo gani ikzingatiwa kuwa hakuna mambo ya Tanganyika isipokuwa Tanzania na Zanzibar

Mgawanyo
JFC imekuja na formula ya 21% ya ajira.
Ni formula gani inatumika kugawana mapato na matumizi kwa kila upande.

Hakuna formula inayoonyesha hiyo account ya pamoja inagawanywa vipi.
Lakini muhimu sana ni kuwa Tanganyika itachangia na znz kwa Billion 400 hata bila kutoa senti moja bado haitakuwa na uwezo wa kuchangia

Hii maana yake nini?
Chanzo cha uhakika cha mapato ya S2 ni kodi za Watanganyika. Ni makusanyo ya Tanganyika yanayopigiwa mahesabu ya kugawana na Zanzibar kama chanzo cha uhakika cha S2.
Huu nao ni aina ya upuuzi ambao Watanganyika lazima wauangalie kwa macho mawili.

Ni kwa msingi huo, washabiki wa S2 hawataki kuzungumzia kabisa chanzo cha mapato cha uhakika wa S2 isipokuwa wanahoji cha S3. Kwa mfano wa JFC tunaona instability kubwa sana ya muungano kinyume na inavyoaminishwa.

Kwamba, ili muungano uwepo ni lazima Tanganyika itoe kila ilicho nacho.
Wakati huo huo znz haina mchango wowote wa maana kama si hakuna kabisa.

Sidhani kama Tanganyika inahitaji JFC. Kuna sababu gani za msingi ikiwa hakuna mchango kwa upande mwingine.
Kwamba, tunachukua chetu na tunaita majirani wa nchi jirani ya znz kugawana. If this is not insanity, I don't know what it is.

Hoja ya chanzo cha uhakika cha mapato ya S2 inafia hapa, na haisemwi kwa kujua itaudhi wznz ambao hawana cha kuchangia

Mkuu Nguruvi3,

Kwa kuongezea, Kama tulivyojadili awali, muungano unagharamiwa na Mapato ya muungano ambayo vyanzo vyake ni kodi yanatokana na:

1. kodi ya Mapato kwa Watu binafsi na mashirika, ambayo zaidi ya 80% yapo Tanganyika),
2. Ushuru wa forodha,
3. Ushuru wa bidhaa Zinazizalishwa nchini (mostly Tanganyika). Hapa pia JFC ikawasaidia wapate kodi ya bidhaa Zote zinazozalishwa Tanganyika na kuwa consumed Zanzibar. Zote hizi ni fedha zinabaki znZ, ingawa kwa Tanganyika, kodi zilizokatwa Katika uzalishaji wake - personal income and corporate tax on vibarua Tanganyika na viwanda Tanganyika, Mapato yake yanaenda kwenye kapu la muungano.

Kwa pamoja, Mapato haya ni Kama 92% ya Mapato yote.

Kiasi kilichobakia (12%) Kama Mapato ya muungano ni Yale yasiyotokana na kodi Kama vile tozo na Ada mbalimbali zinazotokana na utekelezaji wa mambo ya muungano Katika idara, na mashirika mbalimbali. Kwa mfano:

1. WiZara ya uchukuzi (tcaa, TPA, tma, ATC). Cha ajabu ni Kwamba hii sio wizara ya muungano, znZ wana ya Kwao lakini Mapato ya watanganyika kutoka idara chini ya wizara hii znZ nao wanafaidi.

2. Wizara ya viwango na biashara, Brela wanakusanya Mapato, na mengi ni ya Tanganyika lakini yanaenda kwenye kapu la muungano ingawa wizara ya viwanda sio ya muungano.

3. Fedha na uchumi - Hapa kuna Mapato pale benki ya posta, nmb, BOT,NIC, CHC, haya yote kimsingi ni Tanganyika lakini Mapato yake znZ wanafaidi.

4. Wizara ya nishati na madini, kuna Mapato ya tpdc, ewura etcetera, wizara hii sio ya muungano lakini znZ wanafaidi kwani Mapato ya idara hizi yanaenda kwenye kapu la muungano.

5. Sayansi na tekinolojia, hii sio ya muungano, lakini kitengo chake cha tcra, Mapato yake yanaenda muungano.

6. Wizara ya katiba na Sheria - Mapato Mahakama ya rufani, yanaenda kwenye kapu la muungano ingawa znZ hawaitambui Mahakama hii.

7. Wizara ya mambo ya ndani - Hapa kuna Mapato ya uhamiaji, idara ya polisi (fines etc). Hii tunaweza sema ni ya muungano lakini ukitazama, ni Mapato ya Tanganyika zaidi.

8. Ofisi ya waziri mkuu (msajili wa vyama vya siasa), Shughuli karibia zote za vyama hivi ni Tanganyika, in terms of wanachama etc.
Takwimu zilizopo ni Kwamba zanzibar wanakusanya asilimia 1.4% tu ya Mapato yenye vyanzo vya muungano, 98.6% ya Mapato ya muungano kwa maana hii yanatokana na juhudi na jasho la watanganyika. Chini ya mazingira haya, upo sahihi Kuhoji umuhimu wa JFC.
Barubaru anahoji Tanganyika inachangia kiasi gani kuendesha muungano. Tulitarajia kwamba kutokana na elimu yake ya uchumi anayojitapa nayo, Angekuwa na majibu Kwamba makusanyo ya fedha kuendesha muungano yanatokana na vyanzo vya kodi na non tax sources nilizojadili hapo juu. Kwa mfano, Mapato ya kodi kutoka kwa employees na corporate taxes Ndio yanaongoza, kwa zaidi ya miaka mitano sasa. Leo, Mapato haya stand at about shillingi trilioni 4.4. Ushuru wa forodha ni karibia trilioni moja, na ushuru wa bidhaa pia karibia trilioni moja shillingi. Jumla ya tax based revenues vyanzo vya muungano kwahiyo Leo ni Kama 6.4 trillion shillings. Tukija kwenye vyanzo ambavyo ni non taxed based, haya ni karibia shillingi bilioni Mia Tisa. Kwa takwimu hizi, ni wazi Kwamba Tanganyika inaendesha muungano kwa vyanzo vyake vya ndani tofauti na hoja ya barubaru Kwamba bajeti yetu ni tegemezi on donors . Kweli ni tegemezi lakini Fedha hizo nyingi zinaenda kwenye miradi ya maendeleo, including znZ kupitia framework ya mkukuta I and II, sio masuala ya muungano.

Hapo awali nilijadili Kwamba muungano unaendeshwa sio tu na Mapato ya muungano Bali pia Mapato yasiyo ya muungano kwa upande wa bara//Tanganyika Kama vile:

1. VAT
2. Ushuru wa stempu.
3. Kodi ya bidhaa za Mafuta.
4. Kodi za hoteli.
5. Kodi ya vyombo vya moto.
6. Ada ya viwanja vya ndege.
7. Ada ya bandari.
8. Mapato yasiyotokana na kodi (rejea tozo na Ada za idara mbalimbali hapo juu ambazo ni za Tanganyika lakini Mapato ni ya watanzania).
9. Mikopo na misaada ambayo mlipaji ni Tanganyika.
10. Mikopo ya ndani kutoka mabenki na pension funds za watanganyika.

Kwa vile bajeti ya muungano ni hiyo hiyo bajeti ya Tanganyika, priority kwa watanganyika haipo, badala yake kipaumbele cha bajeti moja kila mwaka ni utaifa wa Tanzania (muungano). Kina barubaru Hawaoni Hilo.

Je kwa Zanzibar, mapato ya kodi yasiyo ya muungano ni yepi?

1. VAT
2. Ushuru wa stempu.
3. Kodi ya bidhaa za Mafuta.
4. Kodi za hoteli.
5. Ada ya viwanja vya ndege.
6. Ada uwanja wa ndege.
7. Mapato ya ZRA.

Je Mapato yasiyo ya kodi ZnZ ni yepi?
1. Ada na tozo mbalimbali toka idara na asasi mbalimbali zisizo za muungano. Hakuna revenues za maana Hapa.
2. Mikopo ya nje - mdhamini mtanganyika.
3. Mikopo ya ndani.

Je, matumizi ya serikali ya Zanzibar ni yepi?

1. Kugharamia mambo ya znZ nje ya muungano. ZnZ wana fiscal autonomy na pia independence in policy and strategies in economic and social development terms kwa wazanzibari, watanganyika Hawana Lao. Lakini kupitia serikali ya muungano, mtanganyika ameweka priorities kwa utaifa wa Tanzania huku mZanzibari akijalia zaidi utaifa wa Zanzibari.

2. Kulipia madeni yake ya nje yaliyochukuliwa na serikali ya muungano kwa ajili ya kutekeleza masuala nje ya muungano. Swali linalofuata ni je, Zanzibar wanalipa the 12% au 88% ya Deni lake? Binafsi Sidhani Kama inalipa any of the two kwani bajeti yake ya kila mwaka ingekuwa inatueleza kiasi gani kinatengwa kulipia Deni la nje. Pengine Barubaru Ana takwimu hizo, Vinginevyo za Tanganyika Zipo kwenye kila bajeti.

Katika muktadha wa Akaunti ya pamoja, znZ Hawana hoja kwani tu kuitazama hoja zangu hapo juu, awali ni je, huo "upamoja" ni upi? znZ hawataki upamoja, wanataka vyake viwe vyake ndani ya utaifa wa Zanzibar na hapo hapo, vya mtanganyika viwe vya wote.

ZnZ has it's own national strategy planning na policies ambazo haziwi implemented chini ya serikali ya muungano, Kama vile afya, elimu, Kilimo, na Ndio maana awali nilijadili Kwamba wanacholenga znZ kwenye Foreign Aid ni fedha za miradi ya maendeleo ambayo haina uhusiano na muungano. Kwa maana nyingine, wakifanikiwa Kupata fedha za nje, haina maana Kwamba watazitumia kuchangia muungano kwa mia ya kumpunguzia mtanganyika mzigo wa gharama kwa miaka 50.

Katika muktadha wa kudai uhuru wake juu ya ushirikiano wa kimataifa, lengo la znZ ni kuendelea kujenga institutions za kuimarisha mikakati Yao Huko Mbeleni ya kujitoa kwenye muungano. Katiba Yao ya 2010 imewekeza Katika misingi muhimu juu ya Hilo, kinacho wakwamisha ni uwezo Mdogo kifedha na kiuchumi. Wakifanikiwa to take full control of fiscal and monetary matters, including aid and loans za nje, nia itakuwa to strengthen their hand in negotiations na serikk ya muungano (Tanganyika) na kuwapa comfort Katika uimarishaji wa taasisi zake Kama taifa ili iwe Rahisi Kwao kujitoa kwenye muungano baada ya kuwatumia watanganyika Kama tishu ya chooni. Huko Ndio tuendako.

I

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Watetezi wa Zanzibar wanakwepa Ukweli Kwamba:

1. Serikali ya muungano imekuwa ikigharamia mambo ya muungano kutokana na Mapato ya muungano lakini pia na Mapato yasiyo kuwa ya muungano kwa upande wa Tanzania bara/Tanganyika. Kwa upande wa Zanzibar, serikali hii haichangii moja kwa moja Kama Tanganyika, badala yake inachangia kupitia Mapato ya muungano ambayo yanakusanywa na serikali ya jamhuri ya muungano, of which zaidi ya 75% ni Mapato ya Tanganyika.

2. Kwa miaka 50, bajeti ya JMT haitenganishi vyanzo vya Mapato na matumizi kwa utaratibu wa mambo ya muungano na mambo ya Tanganyika. Tunapozungumzia bajeti ya Tanzania, maana yake ni bajeti ya serikali moja - inayoshughulikia muungano (tanganyika na Zanzibar) huku znZ ikiwa na bajeti yake (fiscal autonomy) na vipaumbele vyake. Kwa upande wa Tanganyika, bajeti yake ni hiyo hiyo ya muungano Katika kapu moja. Kuwa na bajeti
Moja - ya Tanganyika na muungano inaathiri sana vipaumbele vya Tanganyika. Wazanzibari Hawaoni hili.

Given yote haya na niliyojadili awali,
Kati ya hoja hizi Mbili, ipi holds more water?

•Hoja ya kwanza ni ya znZ ambao wanalalamika hawapati mgao unaostahili kutokana na Mapato ya serikali ya muungano.

•Hoja ya pili ni ya upande wa Tanganyika Kwamba Zanzibar haichangii kuendesha muungano.

Definitely hoja ya pili.
Ibara ya 133 ya katiba inaelekeza serikali Mbili zilizopo kuchangia gharama za muungano, Zanzibar kwa miaka zaidi ya 20 sasa haichangii moja kwa moja Bali kupitia Mapato ya muungano of which kimsingi ni Mapato ya Tanganyika.

Mwisho wazanzibari wanasahau Kwamba masuala ya misaada na mikopo haipo Katika katiba ya jmt, hivyo hayatambuliki kisheria. Sasa Kujadili Kwamba JFC Ipo kwa Mujibu wa Sheria (which is correct) lakini hapo hapo kusingizia suala la mikopo na misaada kwa znZ Kama kikwazo cha JFC kutekeleza majukumu yake ya kikatiba Wakati masuala ya fedha za nje (mikopo na misaada) sio masuala ya muungano, lakini pia hayapo kisheria ni kukosa umakini wa hoja.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mchambuzi,
1. Swala la mapato na uchangiaji wake haujalishi kiasi gani bali asilimia ngapi ya pato lako unachangia. Sasa ikiwa zanzibar ina watu wasiozidi mil 1 wakati bara ina watu mil.40 ulitegemea vipi mchango wa Zanzibar ulingane na ule wa bara? hizi hesabu gani mnatumia ili uupata Ukweli? na Je, umejiuliza pia Tanganyika hutumia kiasi gani cha mchango huo kwa ajili ya Tanganyika? Hivi kweli wewe kama mshahara wako ni mil. 5 na mkeo ni laki 3 lakini anachangia kwa asilimia sawa na wewe (toka pato lake) kuingia mfuko wa familia, basi ina maana mkeo hana mchango ktk familia kwa kutazama kachangia Tsh ngapi? jamani acheni hizi mtakuwaje wachumi wazuri ikiwa mna fikra kama hizi na inasikitisha zaidi pengine ndio yanatokea ktk nyumba zenu.

2. Wewe mwenyewe umesema wazi ktk wazo lako la kwanza, hivyo unachoshangaa kipi haswa ktk swala hili? kwanza thibitisha maelezo yako kuhusu michango ya Tanganyika kwa Zanzibar ktk mambo yasokuwa ya Muungano halafu tuendelee (tupe takwimu zako)..

Mkuu ikiwa bajeti ya taifa (muungano) inawahusu Zanzibar kwa asilimia 5 tu yaani yale mambo 22 ambayo hayana gharama kubwa wala mapato makubwa ukilinganisha na yale yasokuwa ya Muungano, iweje bajeti hii inaposomwa isemekane kuwa inachangia Zanzibar zaidi ilihali bajeti hiyo kuna mambo mengi hayahusu muungano? Nguruvi3 kisha sema asilimia 95 ya bajeti nya JMT ni mambo ya Tanganyika Wazanzibar wanafanya nini humo?. Sasa leo hayo mambo madogo ndio yamekuwa yanazalisha kuliko yale makubwa ya asilimi 95 kweli? mapato ya taifa yako wazi GDP na michango yake inajulikana wazi kuwa ni Kilimo, madini, services, usafiri, utalii, n.k haya yashindwe na kodi ama ushuru wa vitu gani?

Kuwa na bajeti moja kunaiumiza vipi Tanganyika kama sio Tanganyika kufaidika zaidi pale michango ya Kimataifa (karibu asilimia 50 kutoka nje) kwa ajili ya Bandari, Elimu, Mabarabara, Afya, Miundombinu, vifaa na zana za kilimo na kadhalika, mambo yasokuwa ya Muungano Tanganyika hutumia jina la Tanzania na Zanzibar isifaidike na matumizi ya jina hlo. Kodi na ushuru kuwepo ktk mambo ya muungano ni lazma isipokuwa hizo kodi zinakusanywa toka wizara gani ndilo tunalotakiwa kutazamwa.

Kama Zanzibar na Tanganyika zote zinatakiwa kuchangia asilimia 20 ya kodi hizo ktk mfuko wa Taifa haijalishi Zanzibar wamechangia kiasi gani bali tutazame tofauti ya kodi hizo ktk mchango wa mfuko. Kwa mfano, Unapoingiza gari Tanganyika unatozwa Tsh mil.5 na kati ya hizo laki 5 zinakwenda mfuko wa Taifa, na Zanzibar unapoingiza gari unatozwa mil.2 lakini pia laki 5 zinakwenda mfuko wa Taifa. Hapa panakuwa hakuna tatizo la mchango wa nchi na wala haitazamwi ni kiasi gani nchi moja imechangia dhidi ya nyingineyo kutokana na sababu millioni za uwekezaji wetu wenyewe ktk maeneo hayo.

Mnashindwa kipi kuliona hili nanyi ni wasomi mlobobea ktk uchumi na taaluma za utawala bora. Cha kujiuliza wewe ni hili - 'inakuwaje bandari za Tanganyika tunalipa kodi kubwa kuliko Zanzibar?, je hiyo ziada ya mil.3 (toka 5 kwenda 2) huwa inakwenda wapi? Jamani kama tumeweza kuendesha serikali ya Tanganyika ndani ya bunge hili kwa miaka 50, leo mnakuja kuidai Tanganyika ambayo ipo na imekuwepo kwa miaka 50 ikipitishwa bajeti yake kwa mambo ya Muungano na yasokuwa ya Muungano ndani ya Bunge hili hili, inakuwaje leo mshindwe kuelewa kwamba mambo yote yakiwa ya Muungano, ati hilo bunge la Tanganyika litatoka wapi? Kwani miaka yote lilikuwa wapi? Miaka yote mnajua ni bunge la Muungano ndilo limekuwa bunge la Tanganyika sasa tuseme mambo yote yawe ya Muungano mnaanza kudai na bunge la Tanganyika kama vile halipo!.

Nachokisema mimi ni kwamba haitakiwi kuwepo mambo yasokuwa ya Muungano laa sivyo ndio maana tunapata watu kama nyie mnaopima vitu kwa mchango wa nchi kama zanzibar lakini hamtaki kuzisoma nchi kama Singida, Rukwa na Dodoma zina mchango gani ktk serikali ya tanganyika. Kesho ni wa tu kama nyie mtakao kuja na hoja kama hii juu ya mikoa kama Mtwara, Mwanza, Mara na Geita kuchangia zaidi ya Singida na Dodoma ili kutafuta mkataba mpya wa Uhuru wa Tanganyika. Ikiwa leo hii mnashindwa kuelewa maana ya Muungano mtaweza vipi kufikiri hata Utanganyika wenyewe nani alouwekea mkataba!

Nchi zinapoungana haitazamwi nini mchango wake bali sehemu husika zinafaidika vipi na rasilimali za taifa, kufikiri nje ya Utaifa ni gonjwa sugu la waafrika ambao Ukabila na utumwa vimewaathiri hadi keshokutwa. Nchi kama Marekani au canada kuna watu wa kila kabila, kila asili na wote hutambuliwa kwa haki sawa na mtu mwingine yeyote. Hakuna fikra za sisi Texas tunazalisha kuliko Maryland au hizi siasa za WAO against SISI. Hao Wazenji waloanzisha hizi fikra za kujitenga hawana tofauti kabisa na kundi hili la Ukawa, hivyo wamekutana wendawazimu wawili na watu mnawashangilia kwa sababu Ubaguzi kwetu ni asili baada ya kutumikia Utumwa kwa karne 500. Kwa nini mnatuletea hizi habari za Uzanzibar na Utanganyika!

Hapa jawabu ni moja tu kila jambo lazima liwe la Muungano tuvunje fikra hizi za pande zote mbili na kama hamtaki tafuteni mahala engine mkaishi lakini ubaguzi huu hauwezi kupongezwa wala kuvumiliwa..sitoendelea na fikra za Utanganyika wala Uzanzibar ni upuuzi ambao nashindwa kabisa kuutetea kwa hali wala mali..
 
Mkandara, pitia pia Uzi #405 , nadhani nimejadili baadhi ya hoja zako.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3,

Kwa kuongezea, Kama tulivyojadili awali, muungano unagharamiwa na Mapato ya muungano ambayo vyanzo vyake ni kodi yanatokana na:

1. kodi ya Mapato kwa Watu binafsi na mashirika, ambayo zaidi ya 80% yapo Tanganyika),
2. Ushuru wa forodha,
3. Ushuru wa bidhaa Zinazizalishwa nchini (mostly Tanganyika). Hapa pia JFC ikawasaidia wapate kodi ya bidhaa Zote zinazozalishwa Tanganyika na kuwa consumed Zanzibar. Zote hizi ni fedha zinabaki znZ, ingawa kwa Tanganyika, kodi zilizokatwa Katika uzalishaji wake - personal income and corporate tax on vibarua Tanganyika na viwanda Tanganyika, Mapato yake yanaenda kwenye kapu la muungano.

Kwa pamoja, Mapato haya ni Kama 92% ya Mapato yote.

Kiasi kilichobakia (12%) Kama Mapato ya muungano ni Yale yasiyotokana na kodi Kama vile tozo na Ada mbalimbali zinazotokana na utekelezaji wa mambo ya muungano Katika idara, na mashirika mbalimbali. Kwa mfano:

1. WiZara ya uchukuzi (tcaa, TPA, tma, ATC). Cha ajabu ni Kwamba hii sio wizara ya muungano, znZ wana ya Kwao lakini Mapato ya watanganyika kutoka idara chini ya wizara hii znZ nao wanafaidi.

2. Wizara ya viwango na biashara, Brela wanakusanya Mapato, na mengi ni ya Tanganyika lakini yanaenda kwenye kapu la muungano ingawa wizara ya viwanda sio ya muungano.

3. Fedha na uchumi - Hapa kuna Mapato pale benki ya posta, nmb, BOT,NIC, CHC, haya yote kimsingi ni Tanganyika lakini Mapato yake znZ wanafaidi.

4. Wizara ya nishati na madini, kuna Mapato ya tpdc, ewura etcetera, wizara hii sio ya muungano lakini znZ wanafaidi kwani Mapato ya idara hizi yanaenda kwenye kapu la muungano.

5. Sayansi na tekinolojia, hii sio ya muungano, lakini kitengo chake cha tcra, Mapato yake yanaenda muungano.

6. Wizara ya katiba na Sheria - Mapato Mahakama ya rufani, yanaenda kwenye kapu la muungano ingawa znZ hawaitambui Mahakama hii.

7. Wizara ya mambo ya ndani - Hapa kuna Mapato ya uhamiaji, idara ya polisi (fines etc). Hii tunaweza sema ni ya muungano lakini ukitazama, ni Mapato ya Tanganyika zaidi.

8. Ofisi ya waziri mkuu (msajili wa vyama vya siasa), Shughuli karibia zote za vyama hivi ni Tanganyika, in terms of wanachama etc.
Takwimu zilizopo ni Kwamba zanzibar wanakusanya asilimia 1.4% tu ya Mapato yenye vyanzo vya muungano, 98.6% ya Mapato ya muungano kwa maana hii yanatokana na juhudi na jasho la watanganyika. Chini ya mazingira haya, upo sahihi Kuhoji umuhimu wa JFC.
Barubaru anahoji Tanganyika inachangia kiasi gani kuendesha muungano. Tulitarajia kwamba kutokana na elimu yake ya uchumi anayojitapa nayo, Angekuwa na majibu Kwamba makusanyo ya fedha kuendesha muungano yanatokana na vyanzo vya kodi na non tax sources nilizojadili hapo juu. Kwa mfano, Mapato ya kodi kutoka kwa employees na corporate taxes Ndio yanaongoza, kwa zaidi ya miaka mitano sasa. Leo, Mapato haya stand at about shillingi trilioni 4.4. Ushuru wa forodha ni karibia trilioni moja, na ushuru wa bidhaa pia karibia trilioni moja shillingi. Jumla ya tax based revenues vyanzo vya muungano kwahiyo Leo ni Kama 6.4 trillion shillings. Tukija kwenye vyanzo ambavyo ni non taxed based, haya ni karibia shillingi bilioni Mia Tisa. Kwa takwimu hizi, ni wazi Kwamba Tanganyika inaendesha muungano kwa vyanzo vyake vya ndani tofauti na hoja ya barubaru Kwamba bajeti yetu ni tegemezi on donors . Kweli ni tegemezi lakini Fedha hizo nyingi zinaenda kwenye miradi ya maendeleo, including znZ kupitia framework ya mkukuta I and II, sio masuala ya muungano.

Hapo awali nilijadili Kwamba muungano unaendeshwa sio tu na Mapato ya muungano Bali pia Mapato yasiyo ya muungano kwa upande wa bara//Tanganyika Kama vile:

1. VAT
2. Ushuru wa stempu.
3. Kodi ya bidhaa za Mafuta.
4. Kodi za hoteli.
5. Kodi ya vyombo vya moto.
6. Ada ya viwanja vya ndege.
7. Ada ya bandari.
8. Mapato yasiyotokana na kodi (rejea tozo na Ada za idara mbalimbali hapo juu ambazo ni za Tanganyika lakini Mapato ni ya watanzania).
9. Mikopo na misaada ambayo mlipaji ni Tanganyika.
10. Mikopo ya ndani kutoka mabenki na pension funds za watanganyika.

Kwa vile bajeti ya muungano ni hiyo hiyo bajeti ya Tanganyika, priority kwa watanganyika haipo, badala yake kipaumbele cha bajeti moja kila mwaka ni utaifa wa Tanzania (muungano). Kina barubaru Hawaoni Hilo.

Je kwa Zanzibar, mapato ya kodi yasiyo ya muungano ni yepi?

1. VAT
2. Ushuru wa stempu.
3. Kodi ya bidhaa za Mafuta.
4. Kodi za hoteli.
5. Ada ya viwanja vya ndege.
6. Ada uwanja wa ndege.
7. Mapato ya ZRA.

Je Mapato yasiyo ya kodi ZnZ ni yepi?
1. Ada na tozo mbalimbali toka idara na asasi mbalimbali zisizo za muungano. Hakuna revenues za maana Hapa.
2. Mikopo ya nje - mdhamini mtanganyika.
3. Mikopo ya ndani.

Je, matumizi ya serikali ya Zanzibar ni yepi?

1. Kugharamia mambo ya znZ nje ya muungano. ZnZ wana fiscal autonomy na pia independence in policy and strategies in economic and social development terms kwa wazanzibari, watanganyika Hawana Lao. Lakini kupitia serikali ya muungano, mtanganyika ameweka priorities kwa utaifa wa Tanzania huku mZanzibari akijalia zaidi utaifa wa Zanzibari.

2. Kulipia madeni yake ya nje yaliyochukuliwa na serikali ya muungano kwa ajili ya kutekeleza masuala nje ya muungano. Swali linalofuata ni je, Zanzibar wanalipa the 12% au 88% ya Deni lake? Binafsi Sidhani Kama inalipa any of the two kwani bajeti yake ya kila mwaka ingekuwa inatueleza kiasi gani kinatengwa kulipia Deni la nje. Pengine Barubaru Ana takwimu hizo, Vinginevyo za Tanganyika Zipo kwenye kila bajeti.

Katika muktadha wa Akaunti ya pamoja, znZ Hawana hoja kwani tu kuitazama hoja zangu hapo juu, awali ni je, huo "upamoja" ni upi? znZ hawataki upamoja, wanataka vyake viwe vyake ndani ya utaifa wa Zanzibar na hapo hapo, vya mtanganyika viwe vya wote.

ZnZ has it's own national strategy planning na policies ambazo haziwi implemented chini ya serikali ya muungano, Kama vile afya, elimu, Kilimo, na Ndio maana awali nilijadili Kwamba wanacholenga znZ kwenye Foreign Aid ni fedha za miradi ya maendeleo ambayo haina uhusiano na muungano. Kwa maana nyingine, wakifanikiwa Kupata fedha za nje, haina maana Kwamba watazitumia kuchangia muungano kwa mia ya kumpunguzia mtanganyika mzigo wa gharama kwa miaka 50.

Katika muktadha wa kudai uhuru wake juu ya ushirikiano wa kimataifa, lengo la znZ ni kuendelea kujenga institutions za kuimarisha mikakati Yao Huko Mbeleni ya kujitoa kwenye muungano. Katiba Yao ya 2010 imewekeza Katika misingi muhimu juu ya Hilo, kinacho wakwamisha ni uwezo Mdogo kifedha na kiuchumi. Wakifanikiwa to take full control of fiscal and monetary matters, including aid and loans za nje, nia itakuwa to strengthen their hand in negotiations na serikk ya muungano (Tanganyika) na kuwapa comfort Katika uimarishaji wa taasisi zake Kama taifa ili iwe Rahisi Kwao kujitoa kwenye muungano baada ya kuwatumia watanganyika Kama tishu ya chooni. Huko Ndio tuendako.
Mkandara , kabla sijajibu hoja zako, naomba upitie hoja za Mchambuzi halafu ukubali au ukanushe kuwa hazina ukweli.
Kama unaona zina ukweli basi huo ubaki ukweli. Kinyume chake huwezi kutuaminisha kuwa tuna 'upamoja' wakati ambapo chao ni chao, chetu ni chao. Wakati umefika wa ndama kuacha kunyonya, no more no less.
Ndama mwenyewe angekuwa na adabu japo haijambo!
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

Haya ni masuala muhimu sana kuweza kujua chimbuko la JFC na ili kuweka kuunogesha mnakasha huu naomba majibu yako. Tuache siasa hapa kwani uchumi ni DATA. hebu mwaga data mtaalamu wetu.

1. JE ZNZ INATAKIWA ICHANGIE KIASI GANI KATIKA MUUNGANO?
2. Sema wazi TGK inachangia kiasi gani katika muungano?
3. Lakin pia sema Znz achangie wapi na katika mfuko gani hizo pesa zake kwa huo muungano?.
4. Sema TGK inachangia katika mfuko gani huo mchango wake wa muungano?
5. Ni nani anayedhibiti matumizi na mapato ya huo mfuko na kuhakikisha haki inatendeka katika mgao wao.

Tuweke DATA hapo ili tuwweze kujadili tukiwa na takwimu au Data halisi. Kwani mwisho wake tunaweza kujua ni kama kweli ni kibri cha Znz kukataa kulipia Muungano au kuna namna ya baadhwi kujipendekeza kujitwika mzigo wote kama walivyo jitwika joho la Mvungano?

nasubiri majibu yako mtaalamu.
Jibu lako ni rahisi, JFC imeundWa kwa ajili gani. Pili, 21% ya ajira imetoka katika hesabu gani jwa nani na msingi upi. Mbona hoja zako ni shallow na trivial? Hujulikani unajadili nini. Nitakutendea haki ya kutoadili hoja zisizo na mashiko na za kiwango hiki.
 
Mkandara;9817706]Mchambuzi,
1. Swala la mapato na uchangiaji wake haujalishi kiasi gani bali asilimia ngapi ya pato lako unachangia. zanzibar ina watu wasiozidi mil 1 wakati bara ina watu mil.40 ulitegemea vipi mchango wa Zanzibar ulingane na ule wa bara?
Hizi hesabu gani mnatumia ili uupata Ukweli? Hivi kweli wewe kama mshahara wako ni mil. 5 na mkeo ni laki 3 lakini anachangia kwa asilimia sawa na wewe (toka pato lake) kuingia mfuko wa familia, basi ina maana mkeo hana mchango ktk familia kwa kutazama kachangia Tsh ngapi?
Mkuu, kwanza niseme tunachokitaka ni kumaliza utegemezi wa Zanzibar kwa hila na mbinu. Kama unakubali Zanzibar ina watu milioni 1,ukubali wao kudai usawa katika muungano ni ujuha. Tume ya Warioba wznz walidai 50-50 wakisema ni wabia sawa wa muungano na wakapewa.
Hao wznz 15 wa tume wanawakilisha watu milioni 1 unaosema. Vipi mbona hilo hulioni?

Kule Dodoma kuna wabunge 81 wanaowakilisha watu milioni 1.
Mbunge mh Mnyika anawakilisha watu zaidi ya milioni 1. Huo udogo wa znz upo wapi?
Kwenye ulaji wanahitaji usawa, kwenye kuwajibika ni wadogo na wachache. Hilo halikubaliki tena.

Kumbuka hawa watu wamevunja katiba ya JMT kwa kutumia watu wao 50. Huo udogo wa znz unatoka wapi.
Misaada na mikopo wanataka zaidi ya mkoa wa Dar es salaam. Huo udogo unatoka wapi.
Znz inatengewa pesa nyingi kuliko halmashauri 54 za Tanganyika kwa wakati mmoja. Huo udogo unatoka wapi.

Kila wanapotakiwa wawajibike wanakimbilia suala la udogo. Mambo yakiwa tayari wanadai haki na usawa.
Hili lazima lifike mwisho, haiwezekani udogo usiwe katika kuwajibika bali kuomba,nataka,na mimi pia!

Kuhusu mfano wa mke, huyo mke angekuwa na pato anachangia hapo ingeeleweka. Znz haina mchango katika JMT ya Tanzania. Mchango mkubwa wa znz ni kutaka, kuomba na kudai. Kwa bajeti ya bilioni 400 hakuna chochote kinachoweza kuchukuliwa kutoka hapo. Kuchukua ni sawa na dhambi kwasababu unamkamua ng'ombe mgonjwa asiye na kiwele.
2. Wewe mwenyewe umesema wazi ktk wazo lako la kwanza, hivyo unachoshangaa kipi haswa ktk swala hili? kwanza thibitisha maelezo yako kuhusu michango ya Tanganyika kwa Zanzibar ktk mambo yasokuwa ya Muungano halafu tuendelee (tupe takwimu zako)..
Mwaka wa bajeti wa 2013/2014 znz ilipewa bilioni 32 kupitia ofisi ya makamu wa Rais. Pesa hizo hazijulikani ni za nini. Bilioni 30 ni sawa na 7.5% ya bajeti yao. Bado wana 4.5% na wana pesa za bajeti achilia mbali madeni ya ndani na nje.

Nakisi ya bajeti ya znz inafidiwa na hazina Dar. Tundu Lissu kalisema mbele yao na waziri Aboud kaunga mkono.
Elimu ya juu isiyo ya muungano inagharamia wznz 1700 bila mkopo, I mean bure huku watoto wa walipa kodi wa Tanganyika wakihangaika kwa mikopo na hata kunyimwa kwasababu hawana uzanzibar.

Deni la ndani la znz linafidiwa na JMT. Mfano mzuri ni wao kupitisha bili za umeme kulipwa na JMT wakati hawakusanyi bill zao. Wizara ya mambo ya nje na ndani hawana bajeti. Mchango wao ni sifuri katika hayo.

Ndiyo maana hutasikia hata siku moja wakidai ulinzi na usalama., wanataka mkataba.
Mikataba ni pamoja na kuendelea kufaidika na free ride.

Na mwisho, mishahara ya SMZ imekuwa inatoka hazina kuanzia enzi za komandoo.
Waulize waganyakazi wa SMZ, mishahara inapochelewa huwa wanasubiri itoke wapi.

Orodha ni ndefu, kwa bilioni 400 hatuhitaji kuorodhesha kila kitu. Kama hukubali utegemezi wa hali ya juu, utakuwa uanajidanganya. Habari ndio hiyo.
Mkuu ikiwa bajeti ya taifa (muungano) inawahusu Zanzibar kwa asilimia 5 tu yaani yale mambo 22 ambayo hayana gharama kubwa wala mapato makubwa ukilinganisha na yale yasokuwa ya Muungano, iweje bajeti hii inaposomwa isemekane kuwa inachangia Zanzibar zaidi ilihali bajeti hiyo kuna mambo mengi hayahusu muungano? Nguruvi3 kisha sema asilimia 95 ya bajeti nya JMT ni mambo ya Tanganyika Wazanzibar wanafanya nini humo?. Sasa leo hayo mambo madogo ndio yamekuwa yanazalisha kuliko yale makubwa ya asilimi 95 kweli? mapato ya taifa yako wazi GDP na michango yake inajulikana wazi kuwa ni Kilimo, madini, services, usafiri, utalii, n.k haya yashindwe na kodi ama ushuru wa vitu gani?
Mkuu narudia tena, ni mambo ya Tanganyika kwasababu wameondoa kila jambo kwa kutumia katiba yao.

Leo tunajadili jini kuhusu baraza la mitihani ikiwa wameondoa?
Tutajadili nini kuhusu bandari ikiwa wameondoa.
Ndivyo ilivyo kwa TRA ambapo makusanyo yao yanabaki huko na wala hayaji muungano.

Tutajadili nini kuhusu znz ikiwa wana wizara zao ambazo waziri wa muungano hana nafasi.
Hata waziri mkuu wa JMT hawmjui leo tunajadili nini nao.

Ni kwa msingi huo hata wale wabunge 81 wanakuja kupoteza muda maana hakuna tunachojadili. Katiba yao ya 2010 imeshavunja muungano, ni heri watuache nasi tujadili mambo yetu bila bughudha.

Lini tuliwaomba tuwe na mwakilishi BLW. In short mambo ya Tanganyika ni ya Tanganyika na wao kuingia katika mjadala ni haramu. Inakuwa halali kwasababu tu ya mshiko, kimantiki hakuna muungano, wznz walishauvunja siku nyingi.

Leo tujadili kujenga vyoo vya shule halafu tuwapelekee waidhinishe. Please, this must come to an end.
Wewe umesema ni milioni 1. Huo uwezo wa ku dictate terms za watu milioni 43 wanaupata wapi.
Kuwa na bajeti moja kunaiumiza vipi Tanganyika kama sio Tanganyika kufaidika zaidi pale michango ya Kimataifa (karibu asilimia 50 kutoka nje) kwa ajili ya Bandari, Elimu, Mabarabara, Afya, Miundombinu, vifaa na zana za kilimo na kadhalika, mambo yasokuwa ya Muungano Tanganyika hutumia jina la Tanzania na Zanzibar isifaidike na matumizi ya jina hlo. Kodi na ushuru kuwepo ktk mambo ya muungano ni lazma isipokuwa hizo kodi zinakusanywa toka wizara gani ndilo tunalotakiwa kutazamwa.
Hapa napo unashindwa kuangalia mambo kwa upana wake.
Tueleze bajeti ya ulinzi ambayo ni zaidi ya Trilion moja znz inaweza kuchangia nini.
Bajeti ya mambo ya ndani inachangia nini. Ada za mashirika na taaisisi za kimataifa znz inachangia nini.

Madeni ya ndani znz inalipa kwa kutumia nini. Kumbuka ni bilioni 400 ambazo ni sawa na makusanyo ya TRA ya Tanganyika ya wiki mbili kama si mwezi.
Huoni mambo yote hayo unaangalia misaada ya Washington.
Huu ni utumwa mkubwa sana wa kuamini pesa za washington ni nzuri kuliko free ride wanayokula sasa hivi.

Lakini pia kumbuka, waziri wao wa fedha amesema asilimia 88 ya mikopo ya znz ya nje inadhaminiwa na JMT.
Sasa tuambie katika bajeti yao ya 2014/2015 kama alivyosema Mchambuzi, wapi katika hizo bilioni 400 kuna kifungu cha kulipa deni.

Hivi Mkandara hawa wasioweza kulipa bill za umeme wanawezaje kulipa madeni ya nje.
Ni wazi deni la nje analibeba Mtanganyika. Hapa tunaongelea bilioni 400 tu, ambazo nusu ni Mishahara

Hivi kweli Mkandara unaamini kwa dhati kabisa kuwa misaada na mikopo ndio msingi wa muungano huu.
Ikitokea Paris club wanagoma kutoa misaada na mikopo basi muungano utakufa.

Muungano utakufa kwasababu ni kwa kutumia jina la Tanzania, mchango wa znz unaonekana na si kutumia chanzo kingine. Huu utumwa wa akili ni mbaya kuliko umasikini wowote ule.
Kama Zanzibar na Tanganyika zote zinatakiwa kuchangia asilimia 20 ya kodi hizo ktk mfuko wa Taifa haijalishi Zanzibar wamechangia kiasi gani bali tutazame tofauti ya kodi hizo ktk mchango wa mfuko. Kwa mfano, Unapoingiza gari Tanganyika unatozwa Tsh mil.5 na kati ya hizo laki 5 zinakwenda mfuko wa Taifa, na Zanzibar unapoingiza gari unatozwa mil.2 lakini pia laki 5 zinakwenda mfuko wa Taifa. Hapa panakuwa hakuna tatizo la mchango wa nchi na wala haitazamwi ni kiasi gani nchi moja imechangia dhidi ya nyingineyo kutokana na sababu millioni za uwekezaji wetu wenyewe ktk maeneo hayo.
Tlliwahi kufanya hivyo znz wakasema wana nyonywa. Ndio msingi wa madai yao.
Walichokifanya ni kuacha kuchukua kodi ili bidhaa ziingie Tanganyika bure.

Wakatumiwa na wafanyabiashara kudhoofisha ukusanyaji wa kodi.
Kuendelea ku entertain upuuzi huo ni kuliumiza taifa letu. Katiba yao ya 2010 haitambui ZNZ kama sehemu ya Tanzania.
Lakini basi huwezi kuchukua nusu nusu. Kama wao wameondoa mambo ya muungano, wapi tunategemea kodi itapatikana? Mfano, utakusanya vipi kodi ikiwa wameshaondoa bandari. Hili ni tatizo walilozua wao.
Nchi zinapoungana haitazamwi nini mchango wake bali sehemu husika zinafaidika vipi na rasilimali za taifa, kufikiri nje ya Utaifa ni gonjwa sugu la waafrika ambao Ukabila na utumwa vimewaathiri hadi keshokutwa. Nchi kama Marekani au canada kuna watu wa kila kabila, kila asili na wote hutambuliwa kwa haki sawa na mtu mwingine yeyote. Hakuna fikra za sisi Texas tunazalisha kuliko Maryland au hizi siasa za WAO against SISI. Hao Wazenji waloanzisha hizi fikra za kujitenga hawana tofauti kabisa na kundi hili la Ukawa, hivyo wamekutana wendawazimu wawili na watu mnawashangilia kwa sababu Ubaguzi kwetu ni asili baada ya kutumikia Utumwa kwa karne 500. Kwa nini mnatuletea hizi habari za Uzanzibar na Utanganyika!
Singida hawajatengewa nafasi maalumu wala hawapewi upendeleo maalumu. Mtwara hawana katiba yao na ni Watanzania. Mtu anaweza kuishi popote bila kuulizwa wewe ni Mkilimanjaro au Mwarusha. Ubaguzi umeletwa na Zanzaibar na tunataka tukomesha mbegu hii chafu.
Wznz si raia bora kuliko wasumbawanga au wa Iringa. Huu upendeleo wa kuwafanya ni raia bora ndio hasa unatuletea matatizo.
Hapa jawabu ni moja tu kila jambo lazima liwe la Muungano tuvunje fikra hizi za pande zote mbili na kama hamtaki tafuteni mahala engine mkaishi lakini ubaguzi huu hauwezi kupongezwa wala kuvumiliwa..sitoendelea na fikra za Utanganyika wala Uzanzibar ni upuuzi ambao nashindwa kabisa kuutetea kwa hali wala mali.
.Mkandara, sio wewe umesema mambo yameingizwa kinyemela ili kuwaonea wznz.

Leo unageuka na kusema kila jambo ni la muungano.
Si tumefanya hivyo miaka 50, mbona wakati wznz wanaondoa mambo bila kushauriana na sisi hujawakemea.
Yaani unawapa hata haki ya kuvunja katiba ukitaka tukae kimya kwasababu ni wznz unaodhani ni watu bora sana duniani.

Mkandara, katiba ya 2010 ya znz haiwatambui kama raia wa Tanzania bali wznz.
Leo unataka mambo yawe ya muungano, kwa lipi na sababu zipi.
Je, nani wa kunyooshewa kidole, yule anayejitoa kwa kuvunja katiba au huyu kondoo Tanganyika aliyekaa kimya miaka 50.

Lakini pia Mkandara kasema Tanganyika imevaa koti la muungano. Leo anarudi na kusema tuweke mambo yote katika koti lile lile analosema ni chafu. Mkandara where do you stand on issues. Flip flop si jambo jema.
Huwezi kusema neno kesho ukalibadilisha tukakaa kimya. Unapotosha mkuu.

Mwisho, huwezi kuwalumu UKAWA. 2010 ZNZ walibadili mwelekeo wa siasa za nchi na muungano.
Wamevunja katiba, wametudhalilisha sana na wametukana kuwa wao si Watanzania.

Hatuwezi kuendelee na hali hiyo.tunataka Tanganyika ili tuendelee kufanya mambo yetu bila bughudha.
Hatuwezi kubeba zigo la samadi na kukaa kimya kwasababu tu zigo hilo lina miaka 50.
Sasa muda umefika, tunawatua chini. Zipo njia mbili tu.

1. Wakubali kukaa mezani ili tuafikiane tunawasidia wapi. Tunawasaidia maana hawana msaada the least to say. Uisogope kuwaambuia ukweli. Na siku hizi tunawaambia njia nyeupe hakuna anayefungua mdomo.
Wanajua ukweli kuwa tunaelekea kuwatua waendelee na katiba yao.

2. Ima hawataki kukaa mezani, tutaizindua Tanganyika kwa gharama zao. They will pay for it.
Wao ndio watakaoizindua Tanganyika, unfortunate kwa gharama kubwa sana.
 
Mkandara , kabla sijajibu hoja zako, naomba upitie hoja za Mchambuzi halafu ukubali au ukanushe kuwa hazina ukweli.
Kama unaona zina ukweli basi huo ubaki ukweli. Kinyume chake huwezi kutuaminisha kuwa tuna 'upamoja' wakati ambapo chao ni chao, chetu ni chao. Wakati umefika wa ndama kuacha kunyonya, no more no less.
Ndama mwenyewe angekuwa na adabu japo haijambo!
Ukweli ni upi? maana nimeuliza maswali vizuri ktk uzi wangu kufuatia uzi wake.

Kwanza kabisa mnachanganya vitu maana mnatakiwa kuanza na hayo mambo 22 ya Muungano kisa ndio uzungumzie yasokuwemo. Hivyo basi tuorodheshe kwanza ya Muungano ambayo ni:-

MAMBO 22 YA MUUNGANO KWA MUJIBU WA NYONGEZA YA KWANZA YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO NA KAMA ILIVYO TAJWA KATIKA IBARA YA 4 YA KATIBA 1977

1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.
9. Kodi na Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
10. Utumishi katika Serikali ya Jamuhuri ya Muungano.
11. Bandari,mambo yanayohusika na usafiri wa Anga,Posta na Simu.
12. Mambo yote yanayohusisha na sarafu ya Fedha kwa ajili ya malipo halali(pamoja na noti)mabenki na shughuli zote za benki,fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.
13. Leseni ya Viwanda na Takwimu.
14. Elimu ya juu.
15. Utafiti wa Hali ya Hewa.
16. Usafiri na Usafirishaji wa Anga.
17. Utafiti.
18. Utafiti wa Hali ya Hewa.
19. Takwimu.
20. Mahakama ya Rufani ya Jamuhuri ya Muungano.
21. Uandikishaji wa Vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo.
22. Maliasili ya Mafuta pamoja na mafuta yasiyochujwa ya matokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia.

Sasa mtu anambie hapa serikali ya JMT inawezaje kufaidika na mambo hayo yaloorodheshwa ikiwa baadhi ya mambo haya Mchambuzi kayasema sii ya Muungano? Mfano Usafiri ni utaratibu gani uliopo kulingana na hilo ambao unawekwa ili pato lake liwe la muungano! Kifupi nipeni majibu kwa yote niloya Highlight kuwa ni ya muungano, hiyo serikali ya JMT inategemea vipi ukusanyaji wa mapato yake ilihali Mchambuzi kasema sii ya Muungano.

Mkuu wangu, swala la katiba ya zanzibar ni baada ya kuchoshwa na chenga zetu, tuliitumia serikali ya JMT kwa faida yetu sasa tumefikia kudai kwamba hata mikopo ya nje tunailipa sisi kuwa sababu ya kutowahusisha Zanzibar. Alaa hivi kweli wewe ukichukua mkopo benki kwa jina la Mr& Mrs, basi unaweza kataa kumjulisha wala kujadili na mkeo unazikopa kwa ajili gani? ati kwa sababu tu mlipaji ni wewe?. Huo mkopo una malengo gani kama sii kuinufaisha nyumba uachiwe tu pasipo kwa sababu bwana kasema. Hii ndio maana halisi ya Kuvaa koti la Muungano kutokana na mambo yasokuwa ya Muungano ilihali huko nje tunakokopa inajulikaa ni ya Muungano.

Haya mawazo haya sii ndio ya Nyerere alokuwa akikopa kwa wazungu kisha anawaambia msiniulize nitazitumiaje maana mkopo ni wangu nitatumia nitakavyo, nyie mjali zitarudi kwa dhamana ya nchi yangu - Tukanyiomwa mikopo!.. Dunia ya Kibepari haiendi hivyo jamani lazima mkopeshwaji ajieleze mkopo ni wa nini na fedha hizo zitarudishwa vipi na kwa muda gani. Ile habari ya Misaada ya Kisoshalist ambayo haina masharti haipo tena dunia nyingine hii.

Hoja zenu zote ni za kipuuzi maana mnatuweka sisi tuamini kwamba kuna kitu Watanganyika na Wazanzibar kama wanavyoamini wajinga wachache wa Zanzibar sasa wamepata manazi toka bara na Utanganyika jambo ambalo tumelikataa toka tuanze mjadala huu. Hatutaki kitu Utanganyika wala Uzanzibar isipokuwa kwa pride ya uzawa tu ambayo hata mimi siku zote hujiita Mkerewe haina maana nyingineyo. Kesho mtaanza na Uislaam vs Ukiristu maadam ujinga unapobebwa na huzaa adha kubwa zaidi!

Hayo ulozungumza ktk uzi #409, ni makosa tunayoendelea nayo toka tuingie Ubepari. Yaliwezekana wakati ule wa Ujamaa ili kujenga usawa wa hoja (kisiasa) na sii kiuchumi na ndipo wengi wenu mnapotea. Swala la utawala wakati wa Nyerere lilikuwa ni la Kisiasa zaidi ya Kiuchumi, sasa hivi tunahitaji kuwa na mambo yote ni ya Muungano ili kuziwezesha nchi hizi zikabiriane na uwajibikaji kwa kila upande badala ya kusubiri maagizo toka Ikulu ambapo rais alikuw ahana mamlaka bila kushauriana na rais wa Zanzibar!. Hii haiwezekani tena ndani ya mfumo wa vyama vingi kuiendeleza ni kukubali CCM watawale milele..

Ili kukomesha makundi haya yote mawili ni lazima MAMBO YOTE YAWE YA MUUNGANO hivyo kila nchi itashiriki kikamilifu ktk ukusanyaji wa kodi zake na kuchangia asilimia 60 au 70 ya pato ktk mfuko wa Taifa bila kuwepo na jambo la hii sio ya Muungano. Na mapato yake yataitazama Tanzania nzima ktk maendeleo ya sehemu muhimu za uwekezaji hata kama mkopo mzima utakwenda Zanzibar kujenga bandari kubwa na bora kuliko zote Afrika, maana mwisho wa siku mapato yake yatainufaisha Tanzania, na sii kujenga Fast Transit Dar es Salaam mradi wa watu binafsi (white elephant) kwa jina la Mradi wa Kitaifa (Muungano) toka benki kuu ya dunia!. Kisha Mayor wa Dar hana mamlaka na Transit hiyo, hana mamlaka na sewer na drain system (
majitaka), barabara, recreaction management (bustani na viwanja) wala Parking lots za mji wake isipokuwa kwa maelekezo kutoka kwa waziri au Ikulu. huu ni Upuuzi mtupu. Wapeni mamlaka Zanzibar kama nchi, wapeni mamlaka Ma - Meya, Wakuu wa mikoa na hata viongozi wa serikali za mitaa ambao watachaguliwa na wananchi ili kila mkoa uwe na mamlaka ya kupanga na kuchagua maendeleo yao sii kusubiri ahadi za rais.
 
Ukweli ni upi? maana nimeuliza maswali vizuri ktk uzi wangu kufuatia uzi wake.

Kwanza kabisa mnachanganya vitu maana mnatakiwa kuanza na hayo mambo 22 ya Muungano kisa ndio uzungumzie yasokuwemo. Hivyo basi tuorodheshe kwanza ya Muungano ambayo ni:-

MAMBO 22 YA MUUNGANO KWA MUJIBU WA NYONGEZA YA KWANZA YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO NA KAMA ILIVYO TAJWA KATIKA IBARA YA 4 YA KATIBA 1977

1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.
9. Kodi na Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
10. Utumishi katika Serikali ya Jamuhuri ya Muungano.
11. Bandari,mambo yanayohusika na usafiri wa Anga,Posta na Simu.
12. Mambo yote yanayohusisha na sarafu ya Fedha kwa ajili ya malipo halali(pamoja na noti)mabenki na shughuli zote za benki,fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.
13. Leseni ya Viwanda na Takwimu.
14. Elimu ya juu.
15. Utafiti wa Hali ya Hewa.
16. Usafiri na Usafirishaji wa Anga.
17. Utafiti.
18. Utafiti wa Hali ya Hewa.
19. Takwimu.
20. Mahakama ya Rufani ya Jamuhuri ya Muungano.
21. Uandikishaji wa Vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo.
22. Maliasili ya Mafuta pamoja na mafuta yasiyochujwa ya matokaa na mafuta ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia.

Sasa mtu anambie hapa serikali ya JMT inawezaje kufaidika na mambo hayo yaloorodheshwa ikiwa baadhi ya mambo haya Mchambuzi kayasema sii ya Muungano? Mfano Usafiri ni utaratibu gani uliopo kulingana na hilo ambao unawekwa ili pato lake liwe la muungano! Kifupi nipeni majibu kwa yote niloya Highlight kuwa ni ya muungano, hiyo serikali ya JMT inategemea vipi ukusanyaji wa mapato yake ilihali Mchambuzi kasema sii ya Muungano.

Hivi Unaelewa mantiki yangu kujadili masuala yanayoketa mkanganyiko Katika suala Zima la uchambuzi wa Mapato na gharama za muungano? JFC kazi yake ni kushauri juu ya haya, lakini inajikuta ikikumbana na Mapato ya muungano ambayo yapo Katika wizara za Tanganyika (zisizo za muungano) Katika Mapato ya muungano yasiyotokana na kodi ambayo ni karibia shillingi trilioni moja. Ni dhahiri Kwamba Katika hili hauna uelewa wa kina juu ya nini kinaendelea.

Hoja zenu zote ni za kipuuzi maana mnatuweka sisi tuamini kwamba kuna kitu Watanganyika na Wazanzibar kama wanavyoamini wajinga wachache wa Zanzibar sasa wamepata manazi toka bara na Utanganyika jambo ambalo tumelikataa toka tuanze mjadala huu. Hatutaki kitu Utanganyika wala Uzanzibar isipokuwa kwa pride ya uzawa tu ambayo hata mimi siku zote hujiita Mkerewe haina maana nyingineyo. Kesho mtaanza na Uislaam vs Ukiristu maadam ujinga unapobebwa na huzaa adha kubwa zaidi!

Tangia lini upuuzi unajibiwa na upuuzi?

Ili kukomesha makundi haya yote mawili ni lazima MAMBO YOTE YAWE YA MUUNGANO hivyo kila nchi itashiriki kikamilifu ktk ukusanyaji wa kodi zake na kuchangia asilimia 60 au 70 ya pato ktk mfuko wa Taifa bila kuwepo na jambo la hii sio ya Muungano. Na mapato yake yataitazama Tanzania nzima ktk maendeleo ya sehemu muhimu za uwekezaji hata kama mkopo mzima utakwenda Zanzibar kujenga bandari kubwa na bora kuliko zote Afrika, maana mwisho wa siku mapato yake yatainufaisha Tanzania, na sii kujenga Fast Transit Dar es Salaam mradi wa watu binafsi (white elephant) kwa jina la Mradi wa Kitaifa (Muungano) toka benki kuu ya dunia!. Kisha Mayor wa Dar hana mamlaka na Transit hiyo, hana mamlaka na sewer na drain system (
majitaka), barabara, recreaction management (bustani na viwanja) wala Parking lots za mji wake isipokuwa kwa maelekezo kutoka kwa waziri au Ikulu. huu ni Upuuzi mtupu. Wapeni mamlaka Zanzibar kama nchi, wapeni mamlaka Ma - Meya, Wakuu wa mikoa na hata viongozi wa serikali za mitaa ambao watachaguliwa na wananchi ili kila mkoa uwe na mamlaka ya kupanga na kuchagua maendeleo yao sii kusubiri ahadi za rais.

Hakika unaishi in utopia. Ni akili gani kusema Kwamba "mambo yote yawe ya muungano" kaisha hapo hapo unasema "
Hivyo kila nchi itashiriki Katika ukusanyaji wa kodi zake"? Ni kitu gani unazungumza hapa Kama sio kuchanganyikiwa.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Jibu lako ni rahisi, JFC imeundWa kwa ajili gani. Pili, 21% ya ajira imetoka katika hesabu gani jwa nani na msingi upi. Mbona hoja zako ni shallow na trivial? Hujulikani unajadili nini. Nitakutendea haki ya kutoadili hoja zisizo na mashiko na za kiwango hiki.

Nguruvi3,

Nilijuwa tu huwezi kunipa majibu hapo kwani wewe unafikiri uchumi ni bla bla wakti wanaojua uchumi tunajuwa fika kuwa UCHUMI ni DATA na sio maneno matupu kama wewe unavyofikiria.

Lakin pia unapenda kulalamika bila kuwa na DATA za kile unacholalamikia hivyo mnakasha utakuwa taabu kama mtu anataka kuujadili mnakasha kitaaluma na kutumia data kwani DATA ZOTE ZIPO KATIKA BAJETI ZENU ZA NCHI ZENU ZA 2013/2014 NA ILE YA 2014/2015.

Namekupa masuala very basic ili tuanze kucheza na DATA kuona mushkira upo wapi.

Nakupa pole sana
 
Mkandara;9822341]Mkuu wangu, swala la katiba ya zanzibar ni baada ya kuchoshwa na chenga zetu, tuliitumia serikali ya JMT kwa faida yetu sasa tumefikia kudai kwamba hata mikopo ya nje tunailipa sisi kuwa sababu ya kutowahusisha Zanzibar. Alaa hivi kweli wewe ukichukua mkopo benki kwa jina la Mr& Mrs, basi unaweza kataa kumjulisha wala kujadili na mkeo unazikopa kwa ajili gani? ati kwa sababu tu mlipaji ni wewe?. Huo mkopo una malengo gani kama sii kuinufaisha nyumba uachiwe tu pasipo kwa sababu bwana kasema. Hii ndio maana halisi ya Kuvaa koti la Muungano kutokana na mambo yasokuwa ya Muungano ilihali huko nje tunakokopa inajulikaa ni ya Muungano.
Huyo mke wakati unadaiwa anasema huyu si mume wangu, mimi ni zanzibar, huyo simjui. Nilikuwa naitwa Mrs sasa nimerudi kwenye jina la asili 'binti zanzibar'. Usiku anakuja na kudaia vitenge na khanga na sasa anataka kubebwa apelekwe maliwato.
Bado mume anasema ninaye mke, kama si limbwata ni nini.

Hapa Mkandara unatuunga mkono kuwa lazima yawepo mambo ya Tanganyika na ya zanzibar ili kuondoa sintofahamu.Hakuna namna znz inaweza kuwa na mambo yake halafu tukawa na JMT ambayo znz ipo tukasema tuna muungano.Ndio upuuzi wa watu kulala wameshawasha taa bili wanamtupia Mpogoro kwa jina la Tanzania. Huyo mpogoro wa kidatu morogoro analipa umeme, vipi huyu mtanzania mwingine kwanini yeye apewe ubwete tu, kwa ubora gani.

Asilimia 88 ya mikopo inadhaminiwa na JMT, znz hailipi halafu unasema mikopo. Lakini pia nimekuuliza lile deni la ndani la znz linalipwa na nani? Au kwavile halitoki washington! Deni la ndani la znz ni zaidi ya nusu ya bejti yao, nani analipa.Bajeti yao haina fungu la kulipa deni, bajeti yao haina fungu la ulinzi na usalama, bajeti yao haina mambo ya ndani n.k.Leo unazungumzia mkopo na kusahau kuwa kuna mambo kama hayo hayashugulishi akili kwasababu hawana gharama
Haya mawazo haya sii ndio ya Nyerere alokuwa akikopa kwa wazungu kisha anawaambia msiniulize nitazitumiaje maana mkopo ni wangu nitatumia nitakavyo, nyie mjali zitarudi kwa dhamana ya nchi yangu - Tukanyiomwa mikopo!.. Dunia ya Kibepari haiendi hivyo jamani lazima mkopeshwaji ajieleze mkopo ni wa nini na fedha hizo zitarudishwa vipi na kwa muda gani. Ile habari ya Misaada ya Kisoshalist ambayo haina masharti haipo tena dunia nyingine hii.
Ndio maana tunataka Tanganyika ili tuhangaike na matatizo yetu tuwaache wznz wakakope Paris kwa raha zao. Hatuhitaji wznz wakati wa kukopa na wala hatuna sababu za kuwahitaji kwasababu hawana asset zozote za kutusaidia. Kama watatuhitaji waje kwa adabu kwasababu sisi hatuna sababu za kuwafunga mikono. Mkandara bilioni 400 ukiwa huna wizara ya ulinzi, mambo ya nje, ya ndani na bill zingine, unakwenda kuomba nini hapo? Unadhulumu nini?Usikatae ukweli wala kuwaambia wazi kuwa znz siTanganyika hata siku moja na wala hakuna ukaribu wa aina yoyote kiuchumi
Hoja zenu zote ni za kipuuzi maana mnatuweka sisi tuamini kwamba kuna kitu Watanganyika na Wazanzibar kama wanavyoamini wajinga wachache wa Zanzibar sasa wamepata manazi toka bara na Utanganyika jambo ambalo tumelikataa toka tuanze mjadala huu. Hatutaki kitu Utanganyika wala Uzanzibar isipokuwa kwa pride ya uzawa tu ambayo hata mimi siku zote hujiita Mkerewe haina maana nyingineyo. Kesho mtaanza na Uislaam vs Ukiristu maadam ujinga unapobebwa na huzaa adha kubwa zaidi!
Well kama hoja ni za kipuuzi jisome hapa chini
Hayo ulozungumza ktk uzi #409, ni makosa tunayoendelea nayo toka tuingie Ubepari
Labda nikukumbushe kuwa katiba ya znz ya 2010 iliyoridhiwa na wazanzibar wote wakiwemo CCM na CUF chini ya Pandu Kificho, ikariwa saini na Aman Karume haitambui mznz kama Mtanzania. Hakuna sehemu inayomtambua au kumtambulisha mzn kama Mtanzania. Leo wamefikia mahali wanavunja katiba, mkandara anaamini hawa ni Watanzania.
Kama wangekuwa Watanzania kama wale wa Singida na Lindi, znz isingeomba upendeleo maalumu kwa kila jambo.

Hawa si Watanzania, kwasababu wanapata upendeleo na wao wamekana kwa maandishi kuwa si Watanzania na wala hawatki utanzania. Mkandara usiwang'ang'anie wanatusumbua bure.
Waache waende zao sisi tutabaki kama Tanganyika, hawatutaki hawa.

Hakuna sababu ya kufuga watu wanaotusumbua. Huo ni ukweli na wameutambua.
Siku hizi hatusemi kwa haya tena, tunawaambia njia nyeupe. Wametambua hilo wala husikii tararira, wameufyata na hiyo ni hatua ya kwanza tu
Ili kukomesha makundi haya yote mawili ni lazima MAMBO YOTE YAWE YA MUUNGANO hivyo kila nchi itashiriki kikamilifu ktk ukusanyaji wa kodi zake na kuchangia asilimia 60 au 70 ya pato ktk mfuko wa Taifa bila kuwepo na jambo la hii sio ya Muungano. Na mapato yake yataitazama Tanzania nzima ktk maendeleo ya sehemu muhimu za uwekezaji hata kama mkopo mzima utakwenda Zanzibar kujenga bandari kubwa na bora kuliko zote Afrika, maana mwisho wa siku mapato yake yatainufaisha Tanzania
Mkandara mzanzibar akipata mafao hakutaki wewe Mtanganyika. Na siku wakikua kiuchumi hawatataka kusikia hata jina Tanganyika.

Nini kiliwafanya wakimbize mafuta na gesi. Nini kiliwafanya waondoe bandari, Anga, baraza la mitihani, shirika la viwango, shirika la maritime n.k. Pale penye mafao mzanz ana roho mbaya tu.
Hatutegemei wakipata watatusaidia lolote lil. Ni wabinafsi, wachoyo na wana umimi.

Hatuhitaji bandari huru znz, tunajenga Tanga. Wao waendelee na mpiango ya bandari yao.
Hatuhitaji chochote kutoka kwao, na tunachokitaka ni kuondokana na hizi adha za kubeba watu mgongoni wakicheza msewe.

Kila siku nataka, na mimi, ongeza. Imetosha, hakuna mawazo ya kujenga isipokuwa nafasi za ubalozi na znz ni nchi au si nchi!!

Kuna mambo 7 tunaweza kuwasaidia, kinyume chake watatusaidia kuizundua Tanganyika.
Mkandara hapa tulipo hakuna tena Utanzania, wznz wameshaharibu na wala usiwasingizie Watanganyika.

Miaka 50 tumekubali kupoteza ID yetu, kinyume chake wznz wanatufanya shamba la bibi la ID wasolipia au kuchangia isipokuwa wanapotaka, naomba, nipe namimi, ongezeka baba, na voilio vya kitoto.

Watatusaidia kwa gharama zao kuirudisha Tanganyika.
 
Huyo mke wakati unadaiwa anasema huyu si mume wangu, mimi ni zanzibar, huyo simjui. Nilikuwa naitwa Mrs sasa nimerudi kwenye jina la asili 'binti zanzibar'. Usiku anakuja na kudaia vitenge na khanga na sasa anataka kubebwa apelekwe maliwato.
Bado mume anasema ninaye mke, kama si limbwata ni nini.

Mkuu hapa ndipo unaposhindwa kuelewa ya kwamba wewe ulipochukua mkopo kwa jina la familia ulienda kununua suti sasa iweje mkeo awe mlipa deni ambalo kwanza hakuambiwa, hakuombwa na baada ya hapo kaambiwa maswala ya suti yeye anajua nini?. Kosa ni kutumia jina la familia unapotaka kukunua suti zako maana hizo suti hazimfaidishi mke bali ni ktk mambo yasokuwa ya ndoa. Kwa nini usitumie jina lako mwenyewe uukaingia gharama hizo?
Hapa Mkandara unatuunga mkono kuwa lazima yawepo mambo ya Tanganyika na ya zanzibar ili kuondoa sintofahamu.
Siwaungi mkono kwa sababu kama kuna mambo yasiyokuwa ya muungano basi Tanganyika ingechukua mikopo kwa kutumia jina la tanganmyika ambalo halipo wala halijulikani.. Hivyo ni muhimu kuwahusisha Zanzibar ktk kila mradi wa KIMATAIFA hasa pale jina la JMT linapotumika kama vile wao wanawajinika kupitia bunge la JMT kupewa misaada ya maendeleo kupitia Ubalozi wetu wa nje. Tanganyika haihitaji ridhaa ya wabunge wetu na ndio maana hata mikataba yote ni siri kwa sababu bado tunatumia mfumo wa Kijamaa ulotanguliwa na Usir wa kujificha upo upande gani wakati huo umekwisha ni wakati wa UWAZI na UWAJIBIKAJI, hakuna longolongo. Ikiwa mambo yote ni ya Muungano basi hii mikataba lazima ingepitishwa na bunge kwa kutambua manufaa yake kwa TAIFA hata kama inawekeza zanzibar au bara.
Hakuna namna znz inaweza kuwa na mambo yake halafu tukawa na JMT ambayo znz ipo tukasema tuna muungano.
Bado huelewi mkuu makosa ni kuwepo mambo yasokuwa ya Muungano. Mapendekezo yangu ni kutokuwa na mambo yasiyokuwa ya Muungano hivyo Tanganyika haiwezi kuendelea kutumia jina la Tanzania wakati inachukua miradi ya Kimataifa ambayo sii ktk mambo ya muungano... Hivyo kwa kila mradi wowote ule Tanganyika na Zanzibar watafaidika na hivyo kuleta wepesi ktk hoja za wabunge kuelewa kwamba kwa kila kodi inayokusanywa ipo fedha kwa pande zote 2..
Ndio upuuzi wa watu kulala wameshawasha taa bili wanamtupia Mpogoro kwa jina la Tanzania. Huyo mpogoro wa kidatu morogoro analipa umeme, vipi huyu mtanzania mwingine kwanini yeye apewe ubwete tu, kwa ubora gani.
Mkuu wangu ebu nambie kwani mkoa wa Mwanza wanalipia Umeme au ni waanchi wanalipa Tanesco. Kuna vungu lolote la fedha toka bajeti ya Mwanza ilokwenda kulipia uwekezaji wa Umeme ambao mkopo wae umetokana na jina Tanzania?. Halafu je, unataka kunambia wananchi wa Zanzibar hawalipi Umeme Tanesco? hii habari ya kupewa uemme bure mnaitoa wapi?.. Songea wanalipia? mbona leo mnataka kuchukua gas toka Mtwara kwenda dar hiyo dara italipia kiasi gani?

Asilimia 88 ya mikopo inadhaminiwa na JMT, znz hailipi halafu unasema mikopo. Lakini pia nimekuuliza lile deni la ndani la znz linalipwa na nani? Au kwavile halitoki washington! Deni la ndani la znz ni zaidi ya nusu ya bejti yao, nani analipa.
Bajeti yao haina fungu la kulipa deni, bajeti yao haina fungu la ulinzi na usalama, bajeti yao haina mambo ya ndani n.k.
Leo unazungumzia mkopo na kusahau kuwa kuna mambo kama hayo hayashugulishi akili kwasababu hawana gharamaNdio maana tunataka Tanganyika ili tuhangaike na matatizo yetu tuwaache wznz wakakope Paris kwa raha zao. Hatuhitaji wznz wakati wa kukopa na wala hatuna sababu za kuwahitaji kwasababu hawana asset zozote za kutusaidia. Kama watatuhitaji waje kwa adabu kwasababu sisi hatuna sababu za kuwafunga mikono. Mkandara bilioni 400 ukiwa huna wizara ya ulinzi, mambo ya nje, ya ndani na bill zingine, unakwenda kuomba nini hapo?
Mkuu unaelewa maana ya deni la ndani? sasa ikiwa sio serikali ya JMT kulipi ulitaka nani alipie iwapo Tanganyika nayo inalipiwa na JMT au unataka kusema Benki kuu na wizara ya fedha sio wizara za muungano. tatizo lako huelewi jinsi gani serikali 2 au 3 au 50 zinavyoendeshwa ila unafikiria Kitanganyika zaidi.
Unadhulumu nini?Usikatae ukweli wala kuwaambia wazi kuwa znz siTanganyika hata siku moja na wala hakuna ukaribu wa aina yoyote kiuchumi
Well kama hoja ni za kipuuzi jisome hapa chini Labda nikukumbushe kuwa katiba ya znz ya 2010 iliyoridhiwa na wazanzibar wote wakiwemo CCM na CUF chini ya Pandu Kificho, ikariwa saini na Aman Karume haitambui mznz kama Mtanzania. Hakuna sehemu inayomtambua au kumtambulisha mzn kama Mtanzania. Leo wamefikia mahali wanavunja katiba, mkandara anaamini hawa ni Watanzania.
Kama wangekuwa Watanzania kama wale wa Singida na Lindi, znz isingeomba upendeleo maalumu kwa kila jambo.
Hawa si Watanzania, kwasababu wanapata upendeleo na wao wamekana kwa maandishi kuwa si Watanzania na wala hawatki utanzania. Mkandara usiwang'ang'anie wanatusumbua bure. Waache waende zao sisi tutabaki kama anganyika.
Hakauna sababu ya kufuga watu wanaotusumbua. Huo ni ukweli na wameutambua. Siku hizi hatusemi kwa haya tena, tunawaambia njia nyeupe. Wametambua hilo wala husikii tararira, wameufyata na hiyo ni hatua ya kwanza tu Mkandara mzanzibar akipata mafao hakutaki wewe Mtanganyika. Ni siku wakikua kiuchumi hawatataka kusikia hata jina Tanganyika. Nini kiliwafanya wakimbize mafuta na gesi. Nini kiliwafanya waondoe bandari, Anga, baraza la mitihani, shirika la viwango, shirika la maritime n.k. Pale penye mafao mzanz ana roho mbaya kuliko nyoka. Hatutegemei wakiapata watatusaidia lolote lil. Ni wabinafsi, wachoyo na wana umimi.

Hatuhitaji bandari huru znz, tunajenga Tanga. Wao waendelee na mpiango ya bandari yao.
Hatuhitaji chochote kutoka kwao, na tunachotakitaka ni kuondokana na hizi adha za kubeba watu mgongoni wakicheza msewe. Kila siku nataka, na mimi, ongeza. Imetosha, hakuna mawazo ya kujenga isipokuwa nafasi za ubalozi na znz ni nchi au si nchi.

Kuna mambo 7 tunaweza kuwasaidia, kinyume chake watatusaidia kuizundua Tanganyika.
Mkandara hapa tulipo hakuna tena Utanzania, wznz wameshaharibu na wala usiwasingizie Watanganyika.

Miaka 50 tumekubali kupoteza ID yetu, kinyume chake wznz wanatufanya shamba la bibi la ID waisolipia au kuchangia isipokuwa wanapotaka, naomba, nipe namimi, ongezeka baba, na voilio vya kitoto.

Watatusaidia kwa gharama zao kuirudisha Tanzania. They have to pay the cost!
Madudu matupu yaani hata sikuelewi! anyway poa endeleeni na Utanganyika wenu tuone kama mwaka huu Mtafika popote.. Ni watu kama nyie mnaopotezea fikra sahihi na kueleta ujinga wa kiafrika kila siku Ukabila na Udini ndio malezi mlofundishwa makanisani na misikitini.. I am out!..nimechoka!
 
Mkandara;9824960]Mkuu hapa ndipo unaposhindwa kuelewa ya kwamba wewe ulipochukua mkopo kwa jina la familia ulienda kununua suti sasa iweje mkeo awe mlipa deni ambalo kwanza hakuambiwa, hakuombwa na baada ya hapo kaambiwa maswala ya suti yeye anajua nini?. Kosa ni kutumia jina la familia unapotaka kukunua suti zako maana hizo suti hazimfaidishi mke bali ni ktk mambo yasokuwa ya ndoa. Kwa nini usitumie jina lako mwenyewe uukaingia gharama hizo?
Mkuu si ndio maana tunataka tutumie jina letu la Tanganyika ili tusitumie jina la familia? Huoni unatuunga mkono kwa dhati kabisa. Tena unaeleza vizuri sana hapa chini
Siwaungi mkono kwa sababu kama kuna mambo yasiyokuwa ya muungano basi Tanganyika ingechukua mikopo kwa kutumia jina la tanganmyika ambalo halipo wala halijulikani
..
Bado huelewi mkuu makosa ni kuwepo mambo yasokuwa ya Muungano. Mapendekezo yangu ni kutokuwa na mambo yasiyokuwa ya Muungano hivyo Tanganyika haiwezi kuendelea kutumia jina la Tanzania wakati inachukua miradi ya Kimataifa ambayo sii ktk mambo ya muungano
.Hayo yasiyokuwa ya muungano yanasimamiwa na nani?
Ndiyo maana tunataka Tanganyika ili tusimamie yasiyo ya muungano. Huoni logic inavyokubali hapo?

Halafu unapiga kona bila indicator unasema 'yasiyo ya muungano' huko nyuma katika bandiko hilo umesema mambo yote ni ya muungano.Mkuu unaelekea wapi unasimamia nini. Huwezi kuwa na position mbili katika wakati mmoja.
Hivyo kwa kila mradi wowote ule Tanganyika na Zanzibar watafaidika na hivyo kuleta wepesi ktk hoja za wabunge kuelewa kwamba kwa kila kodi inayokusanywa ipo fedha kwa pande zote 2.
Znz hawataki kodi yao ikusanywe na JMT, wanasema ni kuwanyonya.
Mkuu wangu ebu nambie kwani mkoa wa Mwanza wanalipia Umeme au ni waanchi wanalipa Tanesco. Kuna vungu lolote la fedha toka bajeti ya Mwanza ilokwenda kulipia uwekezaji wa Umeme ambao mkopo wae umetokana na jina Tanzania?. Halafu je, unataka kunambia wananchi wa Zanzibar hawalipi Umeme Tanesco? hii habari ya kupewa uemme bure mnaitoa wapi?.. Songea wanalipia? mbona leo mnataka kuchukua gas toka Mtwara kwenda dar hiyo dara italipia kiasi gani?
Well, wananchi wa Mwanza wanalipa, wa znz hawalipi.
Wangekuwa analipa deni lingetoka wapi. Uwekezaji tumewasaidia sana.
Mwezi Jamuary zimetoka bilioni 11 kupeleka umeme znz, je hiyo si sehemu ya uwekezaji?
Mkuu unaelewa maana ya deni la ndani? sasa ikiwa sio serikali ya JMT kulipi ulitaka nani alipie iwapo Tanganyika nayo inalipiwa na JMT au unataka kusema Benki kuu na wizara ya fedha sio wizara za muungano. tatizo lako huelewi jinsi gani serikali 2 au 3 au 50 zinavyoendeshwa ila unafikiria Kitanganyika zaidi.
Katika bandiko hili umesema Tanganyika imefutika na haijulikani wakati wa kuomba misaada. Wapi unaipata tena ? Huo mantiki inavyokufunga kiasi cha kusahahu umeandika nini within a minute or two.
Well, kuna wizara ya fedha znz, sasa sijui unamaanisha nini. Again logic inakataa kabisa hata ukivuta kwa kamba.
Madudu matupu yaani hata sikuelewi! anyway poa endeleeni na Utanganyika wenu tuone kama mwaka huu Mtafika popote.. Ni watu kama nyie mnaopotezea fikra sahihi na kueleta ujinga wa kiafrika kila siku Ukabila na Udini ndio malezi mlofundishwa makanisani na misikitini.. I am out!..nimechoka
Well, ungesema wznz waendelee na uzanzibar wao.
Mwaka 2010 wamekataa wao si Watanzania kupitia katiba yao.
Walioanza ubaguzi ni wznz ambao hawataki hata kuitwa Watanzania.
Leo unataka kuwakungumiza katika muungano wasioutaka, kwa lipi.

Njia ni moja, Tanganyika izinduke mezani kwa yale tutakayokubaliana kuwasaidia.
Kinyume chake, watatusaidia kuizundua kwa gharama zao.

Mkuu huwezi kunielewa kwasababu ninasimamia ukweli wewe unasimamia uhalifu.
Kwa Watanganyika wanaelewa ninaandika nini, kwa wznz haya ni madudu kwasababu yanachoma.

Hata hivyo sitapunzika kuonyesha uhuni wa kundi la watu laki kadhaa dhidi ya milioni 43.
Hatuna tatizo na znz, tunataka Tanganyika tusimamie mambo yetu, tuache kuwanyonya na kuwategemea kwa jina.

Hapa tulipofika, hakuna njia, lazima Tanganyika izinduke. Ikishindikana Dodoma wzanz watatusaidia kwa gharama zao.
 
Swala la utawala wakati wa Nyerere lilikuwa ni la Kisiasa zaidi ya Kiuchumi, sasa hivi tunahitaji kuwa na mambo yote ni ya Muungano ili kuziwezesha nchi hizi zikabiriane na uwajibikaji kwa kila upande badala ya kusubiri maagizo toka Ikulu ambapo rais alikuw ahana mamlaka bila kushauriana na rais wa Zanzibar!. Hii haiwezekani tena ndani ya mfumo wa vyama vingi kuiendeleza ni kukubali CCM watawale milele..

Ili kukomesha makundi haya yote mawili ni lazima MAMBO YOTE YAWE YA MUUNGANO hivyo kila nchi itashiriki kikamilifu ktk ukusanyaji wa kodi zake na kuchangia asilimia 60 au 70 ya pato ktk mfuko wa Taifa bila kuwepo na jambo la hii sio ya Muungano. Na mapato yake yataitazama Tanzania nzima ktk maendeleo ya sehemu muhimu za uwekezaji hata kama mkopo mzima utakwenda Zanzibar kujenga bandari kubwa na bora kuliko zote Afrika, maana mwisho wa siku mapato yake yatainufaisha Tanzania
s.
then
Mkandara: Bado huelewi mkuu makosa ni kuwepo mambo yasokuwa ya Muungano. Mapendekezo yangu ni kutokuwa na mambo yasiyokuwa ya Muungano hivyo Tanganyika haiwezi kuendelea kutumia jina la Tanzania wakati inachukua miradi ya Kimataifa ambayo sii ktk mambo ya muungano...
well!
 
Zanzibar. The Zanzibar Higher Education Loans Board (ZHELB) will only sponsor new 1,000 students in the next academic year down from 1,400 in the current academic year. Presenting his ministry's budget estimates in the Zanzibar House of Representatives (ZHR) yesterday, the Minister for Education Ali Juma Shamhuna said the reduction follows minimal funds which have been allocated for the forthcoming financial year.He said the board is now putting more energy in debt collection from graduates and beneficiaries of the loans and up to March this year they had managed to get Sh166 million. "We hope this initiative will help to boost the number of new beneficiaries in the near future," he said.

He told the House that in order for the process to be a success, the government has decided that no beneficiary of ZHELB working for the Revolutionary Government of Zanzibar will be allowed to go for further studies before clearing their debts.

According to Shamhuna, ZHELB will have Sh8.7 billion in its pocket to spend for the new and continuing students from Zanzibar in the 2014/2015 academic year.

In the current 2013/2014 academic year ZHELB managed to cater for 2,823 new and continuing students from the isles
ZHELB Imepunguza idadi ya wanafunzi kutoka 1400 hadi 1000.

Wakati huo huo wamelalamika na JK kuwaongezea nafasi kutoka 1000 hadi 1700.
Kumbuka hili si katika yale ya 1964 na hivyo halipo katika mambo ya muungano.
Nasisitiza kwa dhati kabisa kuwa halipo katika mambo ya muungano. Mwenye hoja aje hapa apinge!

Znz inasema haitaruhusu wanafunzi wasiomaliza kulipa madeni yao kuendelea na masomo ya juu.
Wale 1700 waliokuja bara ambao hawapewi mikopo bali zawadi wanaruhusiwa kuendelea kupata zawadi hadi uprofesa.

Hii maana yake ni kuwa znz wanatumia fiscal autonomy yao katika uchumi wao.
Matatizo yao wanayasukuma bara kwenye shamba la bibi kwasababu hatuna fiscal autonomy. Chetu ni chao, chao ni chao!

Waziri anasema, kipindi kijacho watakusanya bilioni 8.. kusaidia wanafunzi wengine wa znz.
Sisi tunaochukua 1700 ya wanafunzi wao pesa hizo zinakwenda na maji 'under the bridge'.

Hakuna tatizo wao kuwa na mipango yao, lakini mipango yao isiathiri maisha ya walipa kodi wa Tanganyika.
Hii ni nchi kamili na ina vyombo vyake na haitambui uwepo wa JMT hivyo wapewe nafasi ya kutumikia watu wao, na wasiwe mzigo kwa mlipa kodi wa Tanganyika.

Ni hawa hawa wanaosema misaada na mikopo hawapati. Hizo pesa za wanafunzi 1700 zingetoka Washington au Paris pengine wangejisikia burdani zaidi. Leo kuna watu wanatuaminisha kuwa znz wanaonewa!
watu wanasema znz ina mchango katika muungano huu.
Angalia ubaguzi wa nafasi za masomo na kazi, kwamba utapata ZHESL Ukiwa mzanzibar na ukiwa na utapata ajira SMZ.
Huku kwetu shamba la bibi. Wapo wanaosema eti hakuna ubaguzi, huu wa kizanzibar ni nini kama is ubaguzi.

Wapo wanaolaumu Tanganyika kwa kujitoa miaka 50 kwa kila jambo, eti wanatuaminisha mambo yote ni ya muungano.
Mambo yote kwa maana mambo ya Tanganyika, ya znz ni znz na hapo juu ni mfano mzuri.

Unawezaje kuwa na mambo yote ya muungano ukiwa na mengine pembeni? Hawa watu wasio na uchungu na kodi za mama na baba zao wanaamini kuwa znz kufanya ujahili wa kuvunja katiba, kuleta ubaguzi na kujiweka katika daraja zaidi ya wengine ni sawa kabisa. Watanganyika kuomba fiscal autonomy ni upuuzi!!!

Tunaposimama kutetea nchi na watu wetu tunaambiwa wapuuzi.
Hate me, love me, I will stand for what is right.
I will stand for mother Tanganyika and my allegiance is unwavering!
 
Nguruvi3 - Nachosema mimi ni kwamba inatakiwa iwe -Hakuna mambo yasokuwa ya Muungano, unaendelea kuuliza yale yasokuwa ya muungano yatasimamiwa na nani? na sababu ni kwamba huelewi napoandika maswala ya mfumo wa utawala uliyopo sasa hivi ambao unatakiwa kubadilishwa na mfumo ninaopendekeza utakuwaje! wewe unachanganya hoja zangu juu ya mfumo uliyopo na unatakiwa uwe vipi, vyote unaviweka pamoja.

Mkuu ktk mchango wangu kila upande na kila mkoa, kila jimbo watasimamia shughuli za serikali zao. Mfumo huu haukomi kwa nchi za bara na visiwani tu bali unashuka hadi serikali za chini kuwa na mamlaka ya kuendesha shughuli zao kupitia vyama walivyochgua kuendesha shughuli za serikali. Ni mgawanyo wa kazi hakuna uhasama wa nchi wala Ukanda, kiasi kwamba hata madiwani wanapokaa na kufanya maamuzi yanaheshimiwa na kutekelezwa na wao sio kusuburi serikali kuu na kila jimbo litafaidika na rasilimali walizowekeza ktk mapato ya kila mwaka..

NB: Unaona mnavyodanganywa ya kwamba wananchi wa Zanzibar hawalipii umeme? yaani ujinga mtupu unatembezwa kwa sababu ukweli ni kwamba wanalipia Tsh 160 kwa Unit ilikuwa Tsh.120 zamani, lakini mnachotaka ni ati serikali ya Zanzibar iwalipe tanganyika kwa mkopo wa Kimataifa ulotumia jina la Tanzania..sasa sijui kama umeuliza hizo wizara zetu, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya ofisi zao za serikali ya Tanganyika wanadaiwa kiasi gani na Tanesco! je wanalipa au ndio mali ya Umma!
 
Mkuu kuna vitu viwili umechanganya,naomba nikuwekee sawa ili ujadili bila kupoteza unguli wako unaoheshimika jamvini.

Kuhusu umeme, hakuna msaada wa nje unaotumiwa kulipa bili za Tanesco.
Tanesco inafanya kazi Tanganyika na inakusanya mapato yake huko.
Zanzibar wana Zesco, inauziwa umeme na Tanesco.
Kwamba Zesco wanakusanya kwa unit sh ngapi hilo ni juu yao.
Tunachojua kwa unit moja znz inalipa chini ya Mtanganyika.

Deni la Zesco kwa Tanesco ni baina ya mashirika mawili. Zesco wanakusanya mapesa na hayajulikani yanakwenda wapi.
Kuna scandal ya bilioni 20 kutoweka kiaina huko Zesco ambayo imefukiwa.

SMZ inachukua deni la Zesco na kuitupia serikali ya muungano. Sasa mznz analipa umeme jibu ni hapana.
Laiti wangekuwa wanalipa basi wasingegoma kulipa deni la bilioni zaidi ya 70. Deni linatoka wapi kama wznz wanalipa?

Hapo utakuja na hoja kuwa Zesco wanakula pesa. Well,walipojiondoa Tanesco ilikuwa ni kuwa na shirika lao.
Sisi tunawauzia umeme wao na ndiyo maana SMZ inatakiwa ilipe.
Mgomo wa kulipa,walitaka walipe kiwango cha chini cha unit za Tanganyika. Hiyo ndiyo akili ya ZNZ.

Pili, SMZ ilikuwa inatumia milioni 800 kwa mwezi kwa umeme wa Pemba.
Kwa mujibu wa waziri wao sasa hali itakuwa njema baada ya kuungwa na Tanesco kutokea Tanga.
Hali nzuri maana yake ni ile ile, watagoma kulipa na deni litapelekwa JMT. Wanaogoma ni znz kumbuka.

Tatu, kuhusu suala la misaada, umeme wa kwenda znz wa mwanzo ulikuwa mkopo na msaada uliolipiwa na JMT.
Mwezi Jan 2014 wamepeleka umeme kwa msaada wa nchi za nje ambzo zimetoa kiasi bilion 39? na SMZ bilioni 5. Kiaisi kilichotakiwa ambacho SMZ haikuweza kukilipia ni bilioni 11 walizoomba kutoka JMT.
Hadi hapo unaona jinsi gani mikopo na misaada inavyowafikia. Hivyo usichanganye kati ya bill na gharama za kupeleka umeme.

Unatakiwa ujiulize, kama mambo yote ni ya JMT, ZESCO imeundwa kumhudumia nani na kwanini.
Haya yote ni katika narcissism na nepotism, kwamba wanataka kutumia ubinafsi kujinufaisha kwa gharama za wengine.
Haiwezekani SMZ yenye kila chomba ipitishe matatizo yake kwa Mtanganyika kwa kisingizio cha jina.

Ili kuondoa kuvaa koti, tunataka Tanganyika yetu tushughulikie umasikini wa Watanganyika.
Znz wabaki huru waende kukopa na wapewe misaada kama Syechelles, Mauritius, Comoro, Haiti, Vnanuata, Fiji na Jamica.

Sijui mkuu kwanini hutaki tuweke equation sawa sawa.
Tunasema kama tumevaa koti basi tunaomba tulivue ili wenzetu nao wapate upande wa kujifunika. Hilo hutaki.

Usipoanza na kuwalaani wznz kwa ujahilia wao wa kudharau katiba yetu, na kuandika katiba yao ya kibaguzi ya 2010, unapoteza nguvu za hoja za kuwasemea.

Kwavile kuna dana dana za kuwapendeza, sisi tunasema they will pay the cost. Wana nafasi moja tu, kukubali uwepo wa Tanganyika. Wakiichezea hiyo tutawataka watusaidie kuizindua Tanganyika kwa gharama zao.
 
Back
Top Bottom