Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Hapana sijasema mnafahamiana ila mnaonyesha kuyajua yya Chadema kama watu wa ndani maana mnasema kwa uhakika exactly what where and how it started, ilihali mtu wa nje hawezi kuyajua haya isipokuwa kwa tulosimuliwa na kuunganisha dots. Mimi kila nachoandika ni kuwasoma, kuwasikia viongozi wa Chadema lakini siwezi kusema kilichotokea ndani ya Chadema mawati sikuwepo..
 

Hebu nipe mfano nilichoongea kama wanandani..Sio kwa nia mbaya inawezekani ulinielewa vibaya au nilishindwa kujieleza.
Swala la urais hilo ni 100% ndicho kilichotoka mdomoni mwa Zitto..
 
Alinda , siku zote hoja zinapomuelemea mkuu Mkandara, kunanjia tatu anazotumia.

Moja, atachomeka hisia za udini, pili atahamisha mada (ref jitegemee) na mwisho atafanya character assassination


Bandiko lake anasema sisi wengne ni Chadema tunajua kwa undani na tunatumika.

Kwawasomaji wa duru wataelewa udhaifu wa hoja hii kwani hoja za duru zipo wazi na zinalikana.

Hakuna aliyeachwa au kusamehewa. Kinachojadiliwa ni hoja kwa mustakabali wa nchi na taifa

Pengine angesema sisi ni ACTtungemwelewa maana tumeeleza ‘movie' nzima ya Zitto ikiwa studio, sasa hivi watu wapo theatre wanaangalia na kubaini script yetu ilikuwa sahihi 100.


Tumechambua kuanzia siasa za ndani, nje na popote.
Ningemuomba apitie nyuzi za duru aone tunavyosimama katika issue na si watu au gengela wahuni


Kama ulivyosema, hatufahamiani wengi tu,ingawa pia ningefurahi kama tungekutana.

Mkandara atakumbuka mabandiko tunayokubaliana ninasemahivyo, tunayopishana ninasimama na anasimama kwa
anachokiamini.


Mawazo mbadala tunayapenda na kuyakaribisha sana.

Tusichokipenda ni spinning, maana akina Kitila na Zitto wanapofanya hivyo,halafu tukubali JF itufanyie hivyo, hatujitendei haki.

Tutaita spade kama spadena si kijiko kikubwa.


Nawaomba nirudi kwenye mada hasa kupitia hoja zawachangiaji, na kisha kuzama katika siasa mpya za ACT za kuligawa taifa.
Siasa za ukanda ambazo walizipiga vita na sasa ndio vinara
Tutaeleza kwa kina kwanini Zitto ameamua kwenda kwenyeUkanda na hoja dhaifu
Tuteleza kwa kuangalia anachopotosha na ukweli wa mambo
Inaendelea…

JokaKuu
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana
 

Umeeleza vema sana mkuu. Kitila anadhani watu hawaoni alichokifanya.

Kwanza, kitendo cha kuvuta uchaguzi mwezi march ili kumu accommodatemtu mmoja ni udikteta.

Chama ni watu si mtu, ile dhana ya Waraka badoinafanya kazi nje ya ‘adui' yao. Dhana ya kuamini hakuna siasa bila Zitto


Katiba ya ACT inasema, ‘kiongozi mkuu ndiye atakayegombea nafasi ya Urais'

Kwa maana nyingine mgombea wa ACT kwasasa ni Zitto.
Nafasi hiyo imeundwa masaa 24 kabla ya mkutano mkuu.

Kwa maana nyingine wajumbe hawakujua katiba inabadilishwaje na kwasababu zipi.

Kitila na Mwigamba ndio taasisi na taasisi ndio wao


Ule udikteta waliokukimbia CDM, wanautekeleza .Wana supreme leader kwa sababu za Zitto na si mahitaji ya taasisi.
Anachokifanya Kitila ni kudanganya umma.

Umma unafahamu nafasi ya supreme imeundwa kimagumashi ilikumu accommodate Zitto.

Haikuwa nafasi iliyo rasmi hata wajumbe wa kamat ikuu achilia mbali wanachama hawaelewi maana ya supreme.

Wanachoelewa ni kuwa wamepigwa pini kwa nafasi ya Urais kama itakuwepo


Siyo CCM , NCCR, TLP wala CDM yenye katiba inayosema, ‘supreme'wao ndio wana nafasi ya kugombea.

Hoja za Kitila ndio msingi wa sisi wengine kusimama hapa.

Tunajua anachokitaka ni kutumia weledi finyu wa wananchi kuwalaghai.


Wamekula wanatapika sasa wanameza matapishi yao, wakiwalaghai wananchi ni uji wa mchanganyiko.

 
Mkuu sasa hivi si suala la kura, wameanza ''vita vya ukabila''

Zitto kaanza mkakati wa kupambana na mikoa na si mahasimu wake wa kisiasa

Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro sasa ni ‘vita' tu. Mkakati huu ni mzuri sana maana Zitto atakuwa ametangaza ‘vita' na mikoa inayojiletea maendeleo. Sijui akienda Kagera na Mbeya atawaeleza nini

Tutafafanua kwa kina upotofu wa hoja za Zitto.

Kinachotia hofu ni mbegu ya chuki anayoipanda.

Tulitegemea Mwalimu Kitila mkumbo aone hatari hii, kama ndiye anayemshauri basi lipo tatizo kubwa sana nchini


Baada ya Waraka sasa wanashambulia makabila. Wamechukua sera za CCM rasmi

CCM wapo pembeni, mpini unafanya kazi. CCM wanateswa na ukabila na udini walioanzisha, sasa wamekabidhi mafaili wao wanaendelea na ziara za chama
 

Wapi Zitto kataja MAKABILA
 
Last edited by a moderator:
Anachokifanya Nguruvi3 na wenzake kujifanya mtabiri(ablakadabla) wa maisha ya kisiasa ya Zitto.ni sawa mimi niwe naandika kuhusu CDM na UKAWA,
Nianze hivi,huu Muungano wa ukawa naamini hauna maisha,najua kabla au baada ya uchaguzi lazima watagombana,hawateelawana,pia swala la uchaguzi wa Rais na wabunge ukawa linateletta mtifuano,alafu likitokea nije kusema mnaona script yangu imetimia tulisema haya...(ablakadabla)
 
Hebu nipe mfano nilichoongea kama wanandani..Sio kwa nia mbaya inawezekani ulinielewa vibaya au nilishindwa kujieleza.
Swala la urais hilo ni 100% ndicho kilichotoka mdomoni mwa Zitto..

  • Hapa sijui unataka kusemaje? kwamba tunatunga sheria lakini wakati wa kuzitumia basi tuangalie huyu mtu anayetaka kushurutiwa ana cheo gani? na ushawishi gani katika chama na nchi kwa ujumla? yaani kwa maana nyingine sheria zetu ni kwa ajili ya wanyonge tu? Kweli? Kama ni hivyo basi hatuna haja ya kuwalaumu CCM kuwa wanashindwa kushughulikia mafisadi papa, wauza uga na nk.. wanadeal na vidagaa visivyo na ushawishi wowote katika jamii... au nielewa vingine.



 
 
 
Tutaangalia kuhusu kauli za supreme leader aliposhambulia mikoa ya kaskazini

Kauli ya kuchangia pato na maendeleo ya sehemu ni ya hatari na ina hitaji mjadala

Tutakuwa na mfulululizo wa mabandiko tukiangalia kauli za supreme na lengo lake katika taifa hili

Inafuata usiku huu
 
Juzi CCM wamemtimua mkongwe Mzee Nassor Moyo kwa sababu eti anashirikiana na CUF... Timua timua hii ingetokea CHADEMA watu wangepiga kelele za "UDIKTETA" ila kwa kuwa imetokea Lumumba hakuna shida!

Ndio mnapokosea hapo wadau wa mabadiliko(demokrasia),jambo likiwa baya ata kama linafanywa na CCM halitoi uhalali wa kuwa jambo jema....sababu ya watu kuunga mkono mabadiliko ni kuichoka CCM( chama changu).na kuhitaji mabadiliko,hatuwezi kuitoa CCM alafu tukaweka mbadala wa hovyo ilo haliwezekani,mmi nipo tayali kwa mabadiliko lakini si ya kuingiza CDM madarakani,chama kinachosigina kanuni na taratibu zake zilizojiwekea,chama kinapata hati yenye mashaka kutoka kwa CAG,kama CCM,ni kujidanganya kuwa wakishika dora kwa bahati mbaya watabadilika ni uongo..nimegundua kitu waliounda vyama vingi vya upinzani walikua CCM ndio mana wanaviendesha Kkama CCM,bora ACT KIMEANZISHWA NA VIJANA,NAZANI HIKI KITAKUA NA MABADILIKO MAKUBWA naweza kujiunga nacho siku moja kama kitafuata mabadiliko ya kweli na demokrasia
Samahani kutoka nje ya mada nilibidi nimjibu huyu kijana
 

ACT pia imefanya timua timua kwa kina Limbu so nao ni wale wale tu... shida yangu kubwa ni kwamba huku kwingine zikifanyika hakuna makelele yanayopigwa isipokuwa kwa CHADEMA tu!
 
Ndugu yangu, umeshindwa kuelewa hoja ya wadau

Mkandara alisema kuwa mambo ya chama yanamalizwa katika vikao kama CCM wanavyofanya.
Wadau wanauliza, kama ndivyo hivyo, je Mansour na Naossoro Moyo mbona hayakumalizwa katika vikao?

Mkandara anasema, ACT-Waraka hawakutenda kosa linalopaswa kufukuzwa.
Wadau wanauliza, je kusema serikali tatu ni tatizo kubwa kuliko Waraka wa Zitto na kundi lake waliokwenda mbali na kuporomosha matusi kwa mwenyekiti wao?

Washabikii wa ACT wanasema waraka ni mkakati wa ushindi ndio maana ulikuwa siri na hilo si kosa
Je, Manosur na Nassoro moyo wanayoyasema hadharani bila makundi wana makosa gani?

Hoja si kuiga mfumo wa CCM, bali kuonyesha kuwa hoja za utetezi wa ACT kwa kutumia CCM ni muflisi.

Nadhani utakuwa umeelewa
 
Mkuu wambo ya chama humalizwa ndani ya Chama kwa maana kwamba Mansour na Moyo wamewafukuza ndio tukatangaziwa. Chadema swala la Zitto na Kitila lilikuwa mitandaoni wakihukumiwa hata kabla ya vikao vya chama. hapakuwa na sababu ya kufanya hivyo inaonyesha utoto na kutojua siasa.
 
Nadhania tu sina uhakika. Chadema walituhumiwa siku nyingi kumhujumu Zitto kwa ukanda na hata ukabila. Ikaelezwa, na wewe ni mmojawapo kuwa kutangaza nia ya kugombea uenyekiti ndicho chanzo cha mgogoro

Tuhuma hizo ziliaminika kwa wengi, sisi tupo katika rekodi hapa jamii forum tukisema 'kutangaza nia halikuwa tatizo, tatizo ni busara na muda'

Tukaongeza kusema haiwezekani CDM wawe na mgombea wa Urais halafu Zitto anatangaza nia wakati huo huo.
Hii ilikuwa kumfanya mgombea wao 'useless''

Madai hayo ya uenyekiti na Urais ndiyo yaliovuma na kutumika kama hoja ya kumkweza na kumtetea Zitto
Chadema wakaona hakukuwepo njia nyingine isipokuwa kuelewesha umma yaliyotokea

Mwigamba(Mkulima masikini) akiwa ndani ya kikao alikuwa anaandika na tunasoma hapa JF live.

Mwigamba hakutumia kikao kueleza hisia au asichoridhishwa nacho.

Wala waandika waraka hawakutumia vikao kumaliza matatizo yao.

Hakukuwepo njia nyingine ya kuaminisha umma kuwa zipo hujuma dhidi ya CDM ispokuwa kuweka waraka hadharani.

Leo tunajua kumbe ACT si chama kichanga, ni chama kilichoanza ndani ya Chama. Waraka unatuleza bila kificho
Nadhani ilikuwa ni muhimu kufanya hivyo, vinginevyo CDM ingeshaporomoka siku nyingi kwa mbinu za ACT-WARAKA

Unakumbuka mambo ya vikao waliyafanya sana. Tuliwatahadharisha kuwa Zitto ataleta tatizo. Hiyo ilikuwa 2011, leo yanatokea.

Kuna wakati radical intevention inahitajika. Si katika siasa tu hata maisha ya mwanadamu

Daktari anapotumia dawa bila matokeo mazuri, kuna nyakati hutumia kisu kufanya operation.

Hiyo ndiyo inaitwa radical intervention.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…