Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Mkuu nadhani tumwache tu aamini kuwa Qorro alishinda! Hakuna namna unaweza kumbadilisha au kumwelewesha

Ni katika kuchepuka na kuondoa focus. Facts zinaonyesha Slaa alikuwa mbunge, sijui nini tatizo
 
Mkuu nadhani tumwache tu aamini kuwa Qorro alishinda! Hakuna namna unaweza kumbadilisha au kumwelewesha

Ni katika kuchepuka na kuondoa focus. Facts zinaonyesha Slaa alikuwa mbunge, sijui nini tatizo
No, facts zinaonyesha Qorro alikuwa mgombea wa CCM. Unachepuka wewe sio mimi.. Jokakuu kesha elewa
 

Mlitaka alichosema Zitto na Takwimu nimewapa hamtaki,nawapi kazitoa,mnaendelea kumlisha maneno KLM inapora Mali za Shy..naendelea kusisitiza ulistahili Ban kwa kumlisha maneno Zitto..Takwimu ni Takwimu,hata zisipo wafurahisha nyinyi hizi zitabaki kua Takwimu,tena zimerahisishwa na THDR 2014,kuwekwa katika asilimia,zile zingine ni mbwembwe za Excel tu
 
Adharusi hizo si takwimu! Ni kitu ulichoona kinafanana na takwimu

Hujaeleza kasema nini umeumba umba maneno.

Angalia za mchambuzi uliangnishe na asilimia (siyo takwimu) halafu rudi jamvini

Mkuu, nenda ukajipange, kwa hili tunapata taabu sana hata kuzungumzia achilia mbali kujadili namba tu
 
Mkuu wakati mwingine mnabisha vitu kiupuuzi sana wakait mnajua tofauti baina ya GDP na Renevue..Sielewi kwa nini mnataka takkwimu wakati mnaweza zipata kirahisi kabisa. haya nenda hapa tafuta table namba 26 kisha angalia mwaka 2010.

Na hata hadi kufikia 2014 au kesho, bado Shinyanga inachangia sana GDP kutokana na madini lakini kidogo tu kinaingia kama revenue kwa sababu madini hayatoi ajira nyingi wala kuanzishwa miradi mingine itknayo na madini hayo.. Kuna mengi unaweza jifunza pia kupitia hapa
 

Hebu basi tusaidie ni kwanini Shinyanga hiko nyuma kimaendeleo hali ni wachangiaji wakubwa ukilinganisha na Arusha na Kilimanjaro?
 


Naomba ufafanuzi wako, Uchangiaji wa pato la taifa unahusikaje na maendeleo ya mkoa husika?

Na ili kujua mkoa huu una maendeleo zaidi ya mkoa ule ni vigezo gani vimetumika( yaani ni vitu gani wameangalia mf. km wameangali idadi ya watu, shule na nk)

Natumaini nikipata ufafanuzi nitaelewa zaidi maana naanza kuchangaya "madesa" Nilipomsoma Mchambuzi nilifikiri nimeelewa kumbe bado...
 
Last edited by a moderator:
Hebu basi tusaidie ni kwanini Shinyanga hiko nyuma kimaendeleo hali ni wachangiaji wakubwa ukilinganisha na Arusha na Kilimanjaro?
Swali muhumi sana hili.

Lakini pia tuelewe kuwa hizo si takwimu zalizotumia supreme. Angalia zile zinazofanana na takwimu(Adharusi) na hizo.

Hapa wanakwepa kuweka zile za Zitto

Hata hivyo twende nao taratibu maana Mchambuzi alipoweka walikataa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ni katika upuuzi wetu tunafaidika na huduma za ujanja wako.

Mkuu tusaidie sasa, ingawa hizo si takwimu alizotumia supreme na hata unaona WanaMahaba wake mnavyopingana, tungependa utufahamishe, kipi hasa kimetumika katika kauli ya supreme, Revenue au GDP?

Usichoke tusiadie, ndilo lengo la elimu kwa umma

cc Mchambuzi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara Alinda anauliza hayo hapo juu
Anasema data za Mchambuzi alizielewa, hizi anazosingiziwa Zitto zinamuondolea uelewa.
Alinda anaomba msaada, tafadhali tufananulie maana tunaelekea vizuri sana.

Tusaidie
 
Mkuu Mkandara Alinda anauliza hayo hapo juu
Anasema data za Mchambuzi alizielewa, hizi anazosingiziwa Zitto zinamuondolea uelewa.
Alinda anaomba msaada, tafadhali tufananulie maana tunaelekea vizuri sana.

Tusaidie

anazingiwa Zitto nini,wakati ata katika ukurasa wake wa Facebook kaweka hizo,nenda utaona
 

niliyoyasema yote yapo katika ukurasa wake Facebook Zitto
 
niliyoyasema yote yapo katika ukurasa wake Facebook Zitto
Huki face mnapajua wenyewe. Ameeleza hivyo katika face, je ndivyo alivyosema katika mkutano? Kama anajisafisha sisi tuamini tu kama mazuzu

Usibebe kitu bila tafakuri ni hatari sana
 
anazingiwa Zitto nini,wakati ata katika ukurasa wake wa Facebook kaweka hizo,nenda utaona
Kama ndizo alizowawekea vema, endeleeni kumeza tu

Kwanini anaongelea huko haji hapa! Pengine anajua mazuzu wanazoleka kirahisi sana huko

Endelea naye, Mkandara katua na zake. Tumasubiri Wabe na Rit nao waje na zao.
Alhasiri kushika kila ujani unaoelea! kwa lugha ya mlimani city, shoot any moving object
 

Hicho ndio alichokisema,alianza kuweka Takimwi katika mitandao,na akaongelea katika mikutano,Mimi nataka ushahidi wa maneno yako, wapi alisema KLM inaipokonya Shy...ukinipa ushahidi neno kwa kwa neno...nahama CCM nahamia ADC
 
My take

Kwanza ni ngumu sana kukujibu kwa vile umekiri hoja zako zinatoka facebook ya Zitto.

Huko fb tunakuachia na pengine utupe nafasi kwavile hatufiki maeneo yako. Hoja zako zinajieleza wazi ni za kifb.

Ukisoma maelezo ya Zitto hapo juu, bila kujali alisema nini katika mkutano, bila kujali ana takwimu gani, tayari umeshamtia matatani na unazidi kuueleza umma kuhusu uhuni, uchochezi na uongo wa supreme. Yaani unamwanika hasa.

1 Huwezi kuweka asilimia ukasema ni data bila kutueleza zimepatikana kwa kuangalia nini

Kuna vitu vingi sana umeshindwa kujua havipo, na supreme alijua watu wa aina yako huko fb hawawezi kuona.
Wala sitajaribu kukueleza maana nitakuwa nakutwisha mzigo mzito.


2 Soma maelezo yako ambayo unasema ni ya supreme.
Hivi kuna uhusiano gani kati ya uchangiaji wa pato la taifa, umasikini na maendeleo ya mikoa ya Shinyanga, Kilimanjaro na Arusha?

Kama Arusha ni wa 7 na K'njaro ni wa 9, kipi kilikuwa bora, kulinganisha Shinyanga na namba 1 hadi 6 au kulinganisha Shinyanga na namba 7na 9. Kuna motive gani ya kuruka mikoa iliyotangulia kimaendeleo zaidi ya Kilimanjaro na Arusha?


Tatu, Kwa maneno yako, supreme alikuwa na maana gani aliposema ‘kujenga uchumi shirikishi?
Alimaanisha nani anamyonya nani na kwanini suluhu iwe shirikishi. Wapi kuna ombwe la shirikishi.


Nadhani unaona jinsi unavyozidi kuleta ushahidi kuhusu kauli za supreme za uchochezi, kuligawa taifa na shambulio kali la kisiasa dhidi ya mikoa miwili ya K'njaro na Arusha

Kwakweli kama ni wakili, basi utakuwa umemsaidia mwendesha mashtaka kumtia hatiani supreme.
Huko fb endeleeni, mkija huku mnamtafutia matatizo.


Soma tena maneno yake mwenyewe uliyomnukuu hapo juuhalafu fikiria mtu mwenye akili timamu atafikia conclusion gani.
Ni mbaya sana ndugu yangu, umemtia pabaya bora ungekaakimya! Rejea fb na ahsante sana kwa kushiriki nasi
 

Al Akhiy naomba nikukumbusha hapo naona ulisahau.

Na Mnyika alisema wazi katika mkutano wa hadhwara kuwa ADUI WAO NAMBA ONE NI ZITTO KABWE.

 

Alinda.

Hapa nilitaka nikupe darsa kiduuuchu kuhusu masuala yako hapo juu.

Uchangiaji wa mkoa katika pato la Taifa hauhusiani kabisa na maendeleo ya mkoa. Bali Maendeleo ya nchi yote yanawekwa katika Vipaumbele vya nchi husika na hivyo ndivyo vinavyotoa dira ya bajeti ya mwaka au kipindi fulani ya nchi.

Kama umesoma bajeti pendekezwa ya Tz ya mwaka huu 2015/2016 yenyewe imeonyesha vipaumbele vyake kuwa ni Uchaguzi mkuu, Kura ya maoni ya Katiba Mpya, Kilimo, Afya na Ilmu. Sasa kwa hilo pesa nyingi za bajeti yenu mwaka huu itaelekezwa katika mambo hayo na mengine yanawekwa kama matengenezo / ukarabati na dharula.

Nikiwa kama mchumi kama Tz ingeweka mkazo katika Bandari ambayo ndio njia kuu ya kukusanya mapato yake ( mfano Dar wao hawalimi zao lolote lakin wanaongoza kwa ukusanyaji wa kodi ni kwa sababu ya Bandari tu. Kwani kwanza bandari yenyewe ina makusanyo mengi na makubwa lakin pia viwanda vinatumia uwepo wa bandari hiyo katika kuagizia mitambo na vipuri lakin pia hata kuuza biashara zao nje. Na mwisho ni wafanyabiashara wanavyotumia bandari hiyo kusafirishia bidhaa zao za kuja kuuza Tz na kwengineko).

Sasa kama ingeweka mkazo katika Bandari kama wanavyofanya Kenya au nchi zote Duniyani basi Bandari ya Mtwara na Tanga zingeinua sana makusanyo ya kodi kwani ndanimwe mizigo kama ya Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi na Zambia ingepita humo bila usumbufu.Na kwa ujio wa hiyo Gas huko Mtwara basi saa hizi Mtwara ingekuwa ya kwanza mbele ya Dar katika kukusanya kodi.

Tatizo lililopo kwa Tz ni ubinafsi na siasa kushika hatamu za uchumi ndio maana vipaumbele vyake vinalenga baadhwi ya mikoa kisiasa na sio kiuchumi na hivyo nchi nzima kuzama katika umasikini.

 

Mkuu Nguruvi3,

Supreme leader Zitto aidha 'aliteleza', ni 'mchumi kihiyo' au anafanya makusudi akidhania kwamba watanzanai wote ni wajinga. Cha kustaajabu ni kwamba hata wafuasi wake humu wameamua kuanguka nae katika hoja. Kwa kweli inakuwa vigumu sana kujibu hoja zao humu, hoja ambazo wao wanadhania wanamtetea supreme leader, kumbe ndio wanazidi kumuangamia nae. Takwimu za Adharusi ambazo amezinukuu kutoka kwa zitto zinazidi kudhihirisha hilo.

Tuseme basi tumeamua kukubaliana nao kwamba GDP ni kigezo sahihi cha kupima mchango wa mikoa katika pato la taifa, hivyo kila mkoa upate mgao kutokana na mchango wake katika GDP ya taifa. Hapo juu Adharusi kaleta data zile zile za supreme leader Zitto, data ambazo Nguruvi3 upo sahihi kabisa kusema kwamba zinazidi kuwaangamiza. Kwa mujibu wa data za Adharusi copied and pasted from supreme leader Zitto, mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa yenye mchango mkubwa sana in terms of GDP ya taifa. Kwa mfano, Mbeya ni mkoa wa tatu kwa mchango wake katika GDP ya nchi, ukitanguliwa na DSM na Mwanza. Shinyanga ni Mkoa wa nne. Je:

1. Supreme leader na wafuasi wake humu wanajua mgao unaoenda Mbeya ni kiasi gani relative to mikoa mingine kama vile Shinyanga?

2. Supreme leader akienda Mbeya atawaeleza wananchi wa Mbeya (mkoa wa tatu GDP wise) kwamba Shinyanga (mkoa wa nne GDP wise) unawanyonya kiuchumi?

Rukwa (kwa swahiba wa zitto - Arfi), ni mkoa jirani wa Kigoma, mkoa wa Zitto. Mkoa wa Rukwa mchango wake kwa GDP ya taifa, ni mkubwa kuliko Kigoma. Lakini mapato ya Kigoma (Tax Revenues) ni makubwa kuliko Rukwa. Je:

3. Supreme leader anaweza kutuambia ni mkoa upi kati ya Rukwa na Kigoma ambao unapata mgao mkubwa zaidi? Kwanini?

Tabora inachangia zaidi ya Kigoma kwa kila kitu (GDP & Tax Revenues). Je:

4. Supreme leader anaweza kutuambia ni mkoa upi kati ya hii miwili unatapa mgao mkubwa zaidi kuliko mwenzake? Kwanini?
 

Siku zote unapopata DATA ni vizuri kuzi analyse vizuri na kujiuliza kwanini awe wa kwanza na sio wa mwisho? ana kitu gani cha ziada kuliko wengine ? n.k


Sasa labda tujiulize kwanini Dar es Salaam inaongoza kwa makusanyo ya kodi za TRA? Je wana kitu gani cha ziada kuliko mikoa mingine kiasi cha kuweza kuongoza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…