Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Sawa mkuu labda unifahamishe Yanga inaendeshwa na kina nani? ama hayo yoote ulosema kama ni mchango wa wanachama wa chama cha siasa huwezi kuyaona kwenye chama cha Mpira!
Mkuu ntarudi kufafanua nilichomaanisha
 
Haya usemayo hayana ukweli kabisa kwa sababu hata huko Marekani kwenye wapiga kura zaidi ya millioni 100, wanachama wa vyama vikuu hawafiki asilimia 10. Wanachama ni wajenzi wa chama, unaweza kuwa na wanachama 10 mkaifanya kazi kubwa kuliko wenye wanachama 100 kwa sababu lengo sii kuwa na chama kikubwa chenye jengo kubwa. Lengo la chama ni kuishawishi jamii ya wapiga kura kwamba chama hiki ndicho chenye itikadi, sera la Ilani itakayo waletea maendeleo wananchi. Sasa ili iweze kuwashawishi wananchi wakupe kura zao unatakiwa kufanya nini?

Kwa hiyo unapotangaza Gospel ya Uongo, hata kama utakuwa na wanachama 100,000 haina maana wananchi wengi watakikubali chama hicho kwa maandamano ya kuvaa jezi za Yanga na magwanda, na hili ndilo kosa kubwa wanalolifanya CDM na CCM kwenye majukwaa yao kushindana kuongeza wananchama na kujisifia sijui wangapi wametoka huko na kujiunga huku. Kuna mikoa ambao CDM ina wanachama wengi sana wamepoteza jimbo, na kuna majimbo CCM wana wanachama wengi sana lakini wamepoteza majimbo hayo kwa sababu wananchi wanakikubali chama kingine kwa matumaini walopewa.

Tazama hata Marekani yapo Majimbo yanajulikana kama strong Hold ya Republican lakini sii kwa idadi ya wanachama wake, ila kwa wakazi wake kuamini ktk Uhafidhina. Demokratic vile vile wapo wananchi wanaamini ktk Uliberali haina maana ni wanachama. Canada, Ontario miaka yote ilijulikana kama ni strong hold ya NDP lakini Liberal na Conservative wametokea kuwa washindi sii kwa sababu ya wingi wa wanachama bali sera zao na mikakati yao ktk maandilizi ya chaguzi mbali mbali. Naweza sema kwa uhakika NDP ina wanachama wengi Toronto kuliko vyama vyote lakini hawashindi chaguzi za ndani.

Ikiwa lengo la Chadema ni kukijenga chama kiwe tajiri kama CCM, kiwe na matawi hadi vijijini japo uchaguzi ni 2015 basi wameanza na mguu mbaya sana maana ktk dunia hii ya sayansi unaweza kukitangaza chama kupitia vyombo vya habari, volunteers na na washa mbalimbali ambazo hulenga kuwaelimisha wananchi haki zao za uraia na jins gani chama kimejizatiti kuwapa maisha bora. Hakuna mtu anayejiunga na chama akiasema azma yake imetimia isipokuwa hujiunga na chama kwa malengo ya kusaidia pale anapohitajika.

Mwaka 1995, NCCR ilikuwa na wanachama wachache mara 100 ya CCM lakini wengi wetu tunaamini Mrema alishinda uchaguzi ule, 200 CUF na hata mwaka 2010 nina imani CDM walifanya vizuri zaidi ya matokeo na sii kwa sababu ya wanachama wake isipokuwa CDM iliwavuta wananchi ambao tayari waliisha ichoka CCM yenye wanachama wengi zaidi. Kufikia uchaguzi wa 2010 kusema kweli sikumjua Lema wala Lissu kama majembe (wanasiasa) lakini nimekuja kuwajua kwa sababu ya damage wanaziozifanya kwa sababu sii kila Mpambanaji ni mwanasiasa ila kila Mwanasiasa ni Mpambanaji!
 
Sheria yoyote ama kanuni husimamma haijalishi ufahamu wa wananchi. Kama unaamini ktk Demokrasia ni lazima misingi inayojenga Demokrasioa ifuatwe laa sivyo hakuna demokrasia. Kila nchi inaunda katiba yake pasipo wananchi wake kufahamu yaliyomo. Mwongozo wa chama chochote lazima uwe wazi hata kama wananchi hawafahamu, hii ni kazi ya waasisi wa chama hicho.

Leo hii tunadai katiba mpya itakayo tokana na wananchi japo ni waasisi wetu waloitunga ya kwanza. South Sudan Katiba yao imetungwa na viongozi wao haikutokana na wananchi huu ni mwanzowala rais wao hakupitishwa na wananchi ktk uchaguzi.Sasa nakuona hapa kwa CDM unajenga sababu ambazo hazihusiani na chama ila ufahamu wa wananchi. Hivi kweli unataka mimi niamini kwamba zamani watu walikuwa hawajui kwamba kiongozi au mwenyekiti lazima achaguliwe kwa kura? Ni zamani ipi hiyo hasa unayoongelea maana hatuzingumzii changamoto za kitikadi bali mfumo wa uongozi wa chama cha siasa.

Nilivyowasoma mwanzo mnaonyesha wazi kwamba unapounda chama muasisi hawezi kumteua ama kumchagua mtu ashike mamlaka ya Uenyekiti pasipo kupitia uchaguzi, hlakini tumekuja kwa CDM swala hilo halipo na sababu umezijenga. Hizo sababu nasema hazina maana kabisa kwani Watanzania wana experience kubwa sana ya kuunda vyama toka TAA, ASP, TANU hadi CCM na mfumo huo wa uchaguzi ndani ya chama haujabalika iwe ndani ya demokrasia ama nje. Mwanzo una tofauti kubwa sana ya uchaguzi wa viongozi waa chama na baada ya kujiweka sawa!

Kifupi ni kwamba chama chochote kinapozaliwa kina ruksa ya kuchagua mwenyekiti wake wa muda iwe kwa kuteuliwa kupendekezwa na waasisi wenyewe. Kitila hajafanya kosa lolote zaidi ya sisi kuonyesha jinsi tunavyohaha na ujio wa ACT kama ilivyokuwa kwa wanachama wa CCM pale iliposikika CCJ imesajiliwa. Binafsi sidhani kabisa kama viongozi wa CDM wanakosa usingizi ila sisi wapambe ndio hutembea na MaVuvuzela, homa za nyakati haziishi!
 
Mkandara anaamini katika watu wala si sera za chama. Ndiyo maana tumesema wazi kuwa siasa alizofanya Kitila zinasikitisha sana na inatia majonzi pale akina Mkandara wakimkingia kifua wakati imekuwa ni tamaduni wa Kitila kutoka kiajabu ajabu na kibubusa kila mara

Tumeweka kila kitu wazi, kinachofanyika katika mjadala ni kutuondo katika mada halisi. zumbemkuu kuna njia za kufunika uvundo wa Kitila kwa kutumia vyama vingine.
gfsonwin umesema vyema sana, hapa tulipo tulitegemea makubwa sana, kinachooenekana hata waanzilishi wa African Association (AA) walikuwa na weledi sana kuliko hawa
 
Last edited by a moderator:

Mkuu gfsonwin hili ndio tatizo kubwa kabisa la approach ambayo tunaitumia. Top-Down. Yaani watu wanajengewa imani kali kabisa juu ya nafasi ya ma-initiators katika kufikia malengo yao, na inapotokea jambo lolote lile watu hawa huburuzwa na imani yao iliyogeuka kuwa mahaba kupelekwa huku na huku kama bendera. Inapotokea initiator kuwatupa mkono watu hawa hubaki kutangatanga kama mbuzi malishoni bila mchngaji. Hawawezi tena kujisimamia ila tu kuongozwa, kikubwa watakachobaki nacho ni mahaba na ushabiki.

Ni majanga! Siasa zetuy hazifundishi hivyo, elimu yetu haiko hivyo, mienendo yetu haiko hivyo, na Fikra zetu zitadumu kuwa duni milele Amina.
Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3 Nadhani Kitila Mkumbo siyo mwanachama wa kwanza wa chama cha siasa kumkaribisha kwenye mwanachama mwingine kama utakumbuka Freeman Mbowe alishawahi kumkaribisha Sumaye kujiunga na CDM. kusema Kitila kamteua ZZK kuwa Mwenyekiti ni kumuonea bure kwani pale alikuwa anatoa tu maoni yake ikizingatiwa kuwa ndo kwanza alikuwa anajitambulisha kama mwanachama mpya.

Tanzania Daima
 
Last edited by a moderator:
 
A
 
Mwalimu Nyerere aliwahi tamka kwamba upinzani wa kweli kwa ccm utatoka ccm. Baada ya ujio wa viongozi wa aina ya Zitto nilianza to question iwapo mtazamo wa Mwalimu ulikuwa bado relevant nyakati za leo. Nimekuja gundua kwamba maneno ya Mwalimu bado yanasimama kwani upinzani unaojengwa na ACT unapata nguvu kutokana na kuungwa mkono sana na CCM. Leo Wapo wajumbe wa NEC na hata wa kamati kuu ya CCM ambao wanamuona zitto kama ndiye kiongozi anayefaa kuongoza chama kikuu cha upinzani nchini na wanaweka wazi hilo. Hii maana yake nini kama sio upande mwingine wa shilingi wa hoja ya Mwalimu?

Kuna dalili kwamba ACT kinaelekea kuwa mbadala wa wana ccm kwa wana ccm kuliko mbadala kwa wananchi wanaotafuta mabadiliko.




Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Then kwa logic hiyo unapindisha maana halisi ya alichokusudia Mwalimu, Mwalimu alikusudia upinzani ulio mbadala wa CCM kwa ajili ya manufaa ya umma, na si upinzani kwa CCM for the case ya upinzani tu, ingekuwa hivyo basi hoja ya mwalimu ingekuwa irrelevant!, hata hivyo mwalimu aliyesema CCM siyo mama yake, ni dhahiri hakuwa mnazi wa CCM, bali alikuwa mtetezi wa wananchi, na kwa hiyo basi alikuwa radhi hata CCM imeguke ikiwa tu mmeguko huo ni kwa manufaa ya wananchi. na pia kitu kingine ni kwamba alipigia debe uwanzishwaji wa vyama vya upinzani ili ukipatikana mmbadala bora kwa CCM basi uunde dola!.
Iwapo wana CCM wakiona ACT ina sera nzuri kuliko za chama chao, na ina nidhamu ya kidemokrasia basi si vibaya wakajiunga nacho, au iwapo wataweka upinzani ndani kwa ndani ndani ya chama chao, basi kwa namna hizi ndio muktadha haswa wa hoja ya mwalimu
 

Suala hapa sio "kupindisha" kwani kama ni hivyo, hata wewe naweza sema umepindisha. Suala hapa ni interpretation. You have made some valid points, nitazirudia.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

nyerere had a point kwani alisha one wazi kwamba mtu ndani ya CCM ambaye ameshasoma utendaji kazi wa ccm na amekaa ndani ya serikali anajua utendaji kazi wake in and out ndiye atakayeweza kuwa mpinzani mzuri zaid wa CCM kuliko mtu baki. na hili sina tatizo nalo kwani siku zote anayekujua vyema ndiye anayeweza kuwa adui wako mkubwa hata mwizi wa nyumban kwako ni mtu anayekujua wewe kwa undani.
mwanzoni nilijua kauli hii ya nyerere ilimlenga zaid Mhe Mrema kwakua alikuwa alikuwa mtendaji ndani ya serikali, lkn nilikuja kugundua kwamba kwa kauli hii alikuwa anahofia watu wengi zaid na hata wengine aliwasaababishia mauti kwa alokuwa nayo juu yao.
 
Kwa mujibu wa redio ya sauti uhuru, Katibu Mkuu wa ACT Samson Mwigamba amenukuliwa akisema kwamba - ujio wa Muungano wa UKAWA umevuruga malengo ya chama chake.

Mwigamba ananukuliwa akisema:

"Lengo kubwa la chama cha ACT ni kuwaunganisha wananchi na kuwaeleza ubovu wa chama kikuu cha upinzani nchini Chadema."

"Imekuwa vigumu kueleza uovu wa Chadema wananchi wakaulewa kwa sababu imetokea wananchi wanaiamini UKAWA na hawataki useme chochote kuhusu mshirika wa umoja huo".

"Naamini kwamba UKAWA utasambaratika kabla ya 2015 na hapo ndipo wananchi wataelewa kuhusu vita ya ACT na Chadema."


Maneno haya yanaimarisha hoja iliyopo mbele yetu kwamba chama cha ACT ni mpini wa CCM kumaliza upinzani.


cc Mkandara, JingalaFalsafa, Gamba la Nyoka, Ng'wamapalala, zumbemkuu, Alinda, Kitila Mkumbo
 

Kwa hiyo mpaka hivi sasa hawana strategy yoyote ya kuchukua dola 2015 isipokuwa kusambaratisha chama kikuu cha upinzani?
 
Wakati ndugu yangu Nguruvi3 analeta hii hoja, nilijua ni katika haraka za "kuchokonua" kilicho nyuma ya ACT. sikutarajia kuwa alichoandika ndio ukweli wenyewe! Staki kuamini kuwa Kitilya, Mwigamba na Zitto wanaweza kusaliti umma wa watanzania na kuwa nyuma ya huu mfumo wa chama kimoja (CCM). Nauita mfumo wa chama kimoja kwani CCM haijawahi kupata mshindani tangu kuzaliwa kwake mpaka mwaka 2010 baada ya watanzania kuamuka na kuipa CCM wakati mgumu hasa katika kinyanganyiro cha kiti cha urais..

Sikutarajia hawa wasomi kuanzisha chama ili kushindana na Chadema, nilitegemea wanaanzisha chama ili kumkomboa mtanzania kutoka katika huu ukiritiba wa CCM, Nilitengemea kuona sera za ushindani sio sera za kuua chadema, nilitegemea kusikia malengo ya hiki chama katika swala zima la maendeleo ya nchi yetu, ila kwa bahati mbaya malengo yao ni kuua Chadema, na chadema kikisha kufa basi hata ACT itauwawa maana lengo la kuanzishwa kwake litakuwa limetimia. Kwa bahati mbaya kutaendelea kutawaliwa na watu wale wale na koo zile zile.

CCM wamejipanga....Nikifikiri kuanzia Ugaidi wa Lwakatare, kwenda katika Mabomu Arusha, Kashfa mbali mbali kwa viongozi wa Chadema, Udini, Ukabila, sasa Act hakika ni vema na haki kuwapa pongezi viogozi hawa maana wanapitia mengi.
 
Kwamba tatizo lao ni upinzani si CCM waliodumaza hii nchi kwa miaka 50.

Kuna watu walisema tuna chuki binafsi, nadhani wanaona everything unfolding before their eyes.
Huyu Mwigamba ndiye mshiriki wa wa tatu katika waraka wa Kitila na Zitto.
Haionekani kama hawa watu wanalolote wamejifunza.
 
Alinda , tulipoleta mada tulikuwa tumejiridhisha kabisa kuwa kuna tatizo kwa kuangalia historia, mwenendo na mtazamo wa ACT na viongozi wake. Kuanzisha chama si tatizo wala kujitenga na kuanzisha upinzani mwingine halijawa tatizo. Tatizo ni malengo ya hawa ndugu.

Unapokuwa na chama kilicholenga kuua vingine ili kupata kuungwa mkono, inasikitisha.
Kama ulivyosema Alinda, ilikuwa ni matarajio ya wengi kuwa hawa wasomi wangeweza kutengeneza sera zikajiuza bila wao kusimama katika jukwaa, kutukana mtu au kurusha kejeli.
Imefikia mahali katibu mkuu wa ACT ambaye katika waraka ni MM3 anatangaza kifo cha upinzani ili wao wawe wapinzani.

Waasisi nao wanaibuka na hoja za kutulaghai wakichagua mwenyekiti kabla ya uchaguzi.

Lengo lao si tatizo la umma ambalo ni CCM, wao ni kuhakikisha upinzani unakufa ili mwenyekiti wao mtarajiwa ang'are.

Nao wanaofanya hivyo ni wasomi kabisa ambao hutegemei wakawa na cheap politics kama hizi.
 
Soma hii habari kwanza
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...anzania-kwa-vyama-vyote-vya-siasa-nchini.html

Kinachoonekana ni unafiki wa kusema ni chama cha watu wote wakati ambapo katibu mkuu wao jana kasema kimekuja kupambana na wapinzani.

Halafu, mwandishi anasema kuna watu wanaojifanya ni wa ACT na kuandika habari mitandaoni kuwachafua.
Ukisoma habari hiyo huwezi kujua nani kaandika kwasababu idara ya uenezi haielezi ni nani.
At the same time wanazungumzia uwazi. Uwazi na unafiki siyo synonymous. Uwazi ni jambo moja na unafiki ni lingine.

Tulitegemea basi wangekuja kukanusha au kusahihisha kauli ya Mwigamba kwa hoja, hawajafanya hivyo.
Wanachokifanya ni kuficha alichosema Mwigamba na kutufunika na blanket chafu kana kwamba ni taarifa tu haina uhusiano.
Ukweli utabaki kuwa bila kukanusha maneno ya Mwigamba, hiyo ndiyo dhima na mwelekeo wa ACT

Lakini pia majuzi wametoa kauli iliyoashiria mapambano na upinzani(UTU). Uzi upo na imetolewa na uenezi.
Leo wanataka kutufanya mazuzu kwamba wao hawana vita na upinzani. You can't fool us !

Swali ni kuwa hivi tatizo la Tanzania ni wapinzani au nyangumi CCM?
Wapinzani hawajwahi kushika dola, vipi leo akina Zitto/Kitila na Mwigamba watuaminishe kuwa wao ndio tatizo la nchi hii kwa miaka 50.

Tunarudia tena, chama hakitangazwi kwa uadui wanaofanya ACT. In the end hawataweza kufikisha taifa kule tunakokusudia.
Ni mkakati mbovu sana kiasi cha kuifkiria huu ndio mbadala anaousema Kitila ?
So far wamefanikiwa sana katika kuwasaidia CCM.
ACT politics rahisi kama hizo hazisaidii taifa,tunarudi kwa NCCR, CUF n.k.
 
Mkuu nadhani sasa mnazitafuta sababu kila kona ili kuonyesha kwamba hiki chama ACT sii chama cha wananchi ila ni chama cha kina ZZJK, kitila na wenzake ilihali vyama vyote vya upinzani vimeanzishwa na wasisi wake kuwa viongozi pasipo Uchaguzi wa awali.

Mimi sipendi kupakana choo kwa sababu tu ya ushabiki lakini ukweli utasimama kwamba Maadui wa Mtanzania sasa hivi ni hivi vyama vya Upinzani ambavyo kwa namna moja ma nyingine vinazaliwa kutokana na kutoelewana ndani ya vyama. Na hii imewapotosha sana wananchi hivyo tuliomba kabla ya mwaka 2005 vyama hivi viache tofauti nzao waungane na kuunda nguvu moja dhidi ya CCM lakini majibu tuloyapata toka viongozi wa vyama hivi inadhihirisha wazi kwamba maslahi yao binafsi na ya vyama vyao yalitangulia. Na yalitangulia kwa sababu kila chama kinakula ruzuku toka mfumo wa taifa (wananchi) unachotakiwa ni mtaji tu wa kundi la wapiga kura toka majimbo kadhaa.

Siri kubwa ya demoktrasia ni Upinzani wa fikra za Kitikadi wala sii kutokubaliana na Uongozi, Ukabila, Udini ama Ukanda. Ni aibu kubwa sana leo hii vyama vyetu bado vinapigania kuingia Ikulu kwa mlango wa nyuma baada ya mtafaruku toka vyama walivyokuwepo. Ilisemakana kwamba Chadema iliasisiwa kuivunja CUF na watu wakaamini hivyo hadi pale CDM na CUF walipoungana nguvu. Ikafuatia NCCR na TLP kuingia ktk Mshikamano huo lakini kulikuwa na siri kubwa ya kutoelewana tena ndani ya Muungano huo.

Na nikitazama historia ya siasa za Tanzania naipata picha halisi ya kwamba hao viongozi wetu wote toka vyama vyote wao ndio wa kutazamwa zaidi maana hakuna kati yao anayekubali kuachia kiti iwe kwa kushindwa ama kukubali mtu mwigine aongoze. Tazama CUF na Maalim Seif/ Lipumba, TLP na Mrema na vyama vinginevyo vyote kila mgombea wake kiti cha uenyekiti inabakia kwa waasisi wa chama..N

i NCCR Mageuzi tu ambayo kidogo imeonyesha demokrasia ya kweli nayo imetokana na viongozi wake waasisi kujitoa moja baada ya mwingine ili kuanzisha chama kipya. Kati ya wanasiasa wote wenye vyama vya sisa nchini wametoka CCM ama NCCR kwa sababu zile zile za kutoelewana na wanachama wenzake.

Hivyo, Hii ya ACT sio mwanzo wa kutoelewana bali tunatafuta sababu zetu wenyewe kuonyesha mabaya ya ACT maana hata Mzee wetu Mtei alipoondoka CCM alianzisha chama chake cha CDM pasipo uchaguzi wa ndani kumteuwa yeye kuwa mwenyekiti bali alipendekezwa na wenzake japo ilikuwa Obvious kwa kiswahili safi tunasema - Nani mwingine kama sio yeye!

ACT ni mfululizo wa kutoelewana na kama kweli tunataka kubadilika basi tuanze na hawa viongozi wa vyama vyetu waklubali ushindani, wakubali kukosolewa, wakaubali kuachia ngazi maana sii ajabu kabisa uchaguzi ujao ukasikia wamechukua form kugombea tena nafasi zao walizoshika kwa miaka zaidi ya 20 huku wakiwa bado wameshikilia mpini Kama kweli kuna kiongozi yeyote anayetaka kugombea nafasi hiyo basi aachie ngazi kwanza miaezi sita kabla ya Uchaguzi kisha agombee nafasi hiyo pasipo mamlaka alokuwa nayo kama mwenyekiti maana hawa watu hutumia madaraka walokuwa nayo kufunga milango yote ya Ushindani dhidi yao.

Wadhungu wanasema- Fight the power! Hili neno halina maana moja kwa chama tawala ama utawala bali hata huku chini tulipo kuna nguvu ya viongozi ndani ya vyama ambayo pia huwakwaza watu wengine ktk kuitaka haki na demokrasia ya kweli.
 

Chama chenye zaidi ya wanachama elf 5 hatutegemei kuridhisha kila mtu, tunachotegema ni kufuata msingi waliojiwekea.. Yatakuwa maajabu kama kiongozi atakubalika kwa kila mtu.. kwa maana hiyo kuwazana ni jambo la kawaida muhimu ni kukaa pamoja na kutatua matatizo yao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…