Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Kuweka kumbukumbu sawa NCCR Mageuzi hawakupata viti hivyo 19.

Uchaguzi wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi 1995, Chama tawala cha CCM kilipata viti 186, CUF viti 24, NCCR MAGEUZI viti 16, CHADEMA viti 3, UDP viti 3 na TLP kiti 1.

Duh nyie watu mnapenda ligi. Kuna tofauti gani kati ya 19 na 16?
 
Hata hueleweki, sijui una haraka gani. Kabla hujabonyeza "submit button" soma uliyoandika, fanya marekebisho kama kuna sehemu umekosea ndipo submit. Mnatupa taabu kwa kuandika kama vile mnakimbizwa!
 

Hilo la mgawanyo wa mapato sina cha ziada maana mshakuwa na mjadala mrefu sana hapa, sina lolote la tofauti.

Ila langu ni dogo tu, tunaweza kuwa na mawazo tofauti lakini sote tuna lengo moja mahsusi, kujenga taifa moja,la watu wamoja, taifa la Watanzania, lenye maendeleo kwenye pande zote za nchi hii.Sina shaka ata kidogo na Zitto juu ya hili, alichosema ni haja ya kusukuma maendeleo PIA kwenye maeneo yaliyo nyuma.

Tatizo ni kuwa baadhi yetu wamekuwa sensitive zaidi na eneo lao/kabila lao, hii ni ishara ya wazi kuwa kuna wengi wetu ambao tu wa eneo letu zaidi kuliko tulivyo Watanzania, kama tungelikuwa ni Watanzania Kwanza basi Tabora ni kwetu kama kulivyo Arusha na kama kulivyo Mtwara, hivyo tatizo la Mtwara linanihusu sana kama linavyonihusu sana la Kagera. Kushindwa kujitafsiri hivyo ndipo lilipo tatizo letu.NI sisi wenye tatizo.Tutoke hapa!!

Kwa kuwa nchi yetu ina central government iliyo na nguvu, ndio yenye almost kila kitu, kwa mfumo huu lazima tuwe na namna ya kusambaza maendeleo pande zote.Jinsi gani?lazima tutatofautiana hapa na pale, lakini tuheshimu mawazo ya wenzetu na kama unaona una wazo bora zaidi unaweza shauri lakini sio kubatizana ubaguzi sehemu ambayo haupo, bila kujijua ni sie tunaochochea hizo hisia na matokeo yake tunasambaza ubaguzi huo.Tuache!!
 

Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi ulifanyika jimbo la Kwahani Zanzibar,nadhan CUF alishinda(sina kumbukumbu nzuri hapa).

Na uchaguzi wa pili ni Kigoma mjini mwaka 1994,aligombea Dr Kabouru na Premji, ambako alishinda Kabouru.Wakati huo ni Kigoma pekee ambako upinzani ulikuwa una nguvu kuliko CCM, Kigoma ndio iliyokuwa symbol ya upinzania wakati huo, ndipo mabomu ya machozi yalipokuwa yanavurumishwa kwa wapinzani kwa mara ya kwanza.Hii ni fact.Bahati mbaya siwezi google hapa na kupata taarifa za Tanzania ya 1994 kutokana na technologia ya zama zile, lakini ndivyo hali halisi ilivyokuwa, ukiandika historia ya vyama vingi nchini huwezi kuliacha hilo.

Kwingine huku wakati huo hakukuwa na nguvu yoyote ya kuishtusha CCM. Nina uhakika ata huyo Mwenyekiti wa Kijiji itakuwa alishinda kwa nguvu zake binafsi sio kwa nguvu ya chama, kama ilivyokuwa kwa Dr Slaa karatu mwaka 1995.Kumbuka mpaka Dr Slaa anagombea ubunge karatu hakukuwa na nguvu yoyote ya Chadema karatu.Chadema Karatu iliibuka na Dr Slaa August 1995.

Maeneo mengine kama nilivyosema juu,upinzani uliibuka ghafla kwa nguvu kuanzia April 1995 lakini Kigoma ilianza kabla ya hapo.
 
Katika wabunge waliochaguliwa mwaka 1995 kutoka Upinzani, wengi kwa ulafi walirudi CCM isipokuwa wanamageuzi wa kweli ambao walikataa vishawishi vya CCM na hadi leo tunao wakiongoza Upinzani katika nyadhifa mbali mbali.

Sijakuelewa hapa, hii inahusianaje na maeneo upinzani upo/umeanzia??sijakupata unamaanisha nin hapa!!
 
Mkuu Kapwela , maendeleo si robota la mitumba unaloweza kugawa nchi nzima baloi ni matokeo ya vitu vingi ikiwemo fursa na jitihada.

Maendeleo hayapelekwi,yana hamasishwa. Mfano, Shule inapofungwakwa kukosa wanafunzi hakuna sababu ya kupeleka makontena ya vitabu, chaki au walimu.

Tatizo si mgawanyo wa vitabu,chaki au walimu. Tatizo ni kukosa hamasa.

Jukumu lakwanza ni kuleta hamasa kwa njia chanya siyo uchochezi


Pili, sehemu zenye maendeleo si kwasababu zilipewa. Ni kutokana na mazingira mbali mbali, tumejadili .

Mazingira yametengeneza fursa,iliyokutana na jitihada.
Unaunga mkono hoja ya maeneo fulani kupewa zaidi, na kwamba ni wakati wa kugawa sawa kama anavyosema Zitto.

Hiyo ndiyo inaamsha hisia,. Huwezi kuwalaumu wananchi wa Kilimanajaro au Arusha kwa mafanikio yao.

Hilo hatukubaliani, halina mantiki,ukweli , akili au mashiko.
Ni cheap politics, tunazilaani


Wengine hatujalalamika daraja la Rufiji kujengwa. Tunalitumia kuliko wananchi wa kusini, ni letu.
Hatujalalamika Maragasi kujengwa, ni daraja letu.


Utaungana nasi kulaani kauli za kuchochea za kiongozi mkuu. Kauli kama za video aliyoleta Alinda inavyoonyesha.

Zitto anaposema ‘Uenyekiti.. kwasababu ni wa Kigoma'' nikauli mbaya sana.

Kwani ubunge alililpwa na wananchi wa Kigoma peke yao. Mbegu anayoipanda ni ya ‘sisi wa Kigomawao wa..''
mbegu chafu na mbaya sana.


Kama unakubali central gov ina nguvu, wapi hoja ya kusambaza maendeleo sehemu zote inatoka? Unachosema, central gov imegawanya kiupande upande.

Endapo ni hivyo, nani wa kulaumiwa? Kwanini wananchi wakaskazini wabebeshwe zigo lisilowahusu?

Kwani wananchi wa kaskazini ndiyo central gov?

Haya ndiyomawazo yanayopigwa vita hapa, hatari Zitto aliyofanikiwa kupanda vichwani mwa watu.


Hatutetei ukabila tunalaani wale wanaotumia umaarufu wao kuchochea ukabila na ukanda.
Zitto hakwepi mkono kwa hili.

Ndiyo maana tunakuomba utuache tukemee, tukuibali ku move on kama unavyoshauri ipo siku watatokea Zittos na hatutaweza tena.

Tumkemee sote kwa kujenga Tanzania yetu, si Ujiji au Isevya,Kadewele au Kicheba.

Ni Tanzania yetu sote


Tusemezane
 
Last edited by a moderator:
Hata hueleweki, sijui una haraka gani. Kabla hujabonyeza "submit button" soma uliyoandika, fanya marekebisho kama kuna sehemu umekosea ndipo submit. Mnatupa taabu kwa kuandika kama vile mnakimbizwa!

SAMAHANI kwa uandishi,wewe na wote,mlioshindwa kuelewa,maana yangu ni kuwa KABURU alishinda uchaguzi Mdogo mwaka 1994,kumbuka uchaguzi MKUU ulikua mwaka 1995,Sasa inawezekanaje historia ianzie 1995 wakati kuna mbunge kashinda uchaguzi Mdogo 1994 na kuingia bungeni kama mbunge wa upinzani kupitia upinzani(CDM),Naamini huyu angetokea KATIKA mikoa mnayoipenda msingebishia,sababu anatokea mkoa anaotoka Zitto imekua tatizo
 

Chadema ndicho chama cha kwanza kuwahi kumwingiza Mwenyekiti wa Kijiji wa Kwanza mwaka 1994 katika kijiji kimoja huko Karatu kinaitwa Gongali na Mwenyekiti mwenyewe anaitwa Simon Kibola.

Uchaguzi wa huyu mwenyekiti ulirudiwa kwa zaidi ya mara nne chini ya usimamizi wa defender za polisi kutoka Arusha Mjini lakini mwishowe kura za wazi ndizo zilizomfanya ashinde.
 
Wewe kazi yako kufuata mkumbo tu msikilize Zitto mwenyewe kwenye hiyo video aliyoleta Alinda.

Siwezi kununua uongo wake, kama wewe unaamini maneno yake amini hivyo, nitamsoma kiduchu, nitamsikiliza kiduchu ila siwezi kukubali maneno yake bila kuhoji
 
Last edited by a moderator:

Nakubaliana na wewe juu ya vichocheo vya maendeleo ila natofautiana na wewe kuhusu role ya serikali.Serikali ina nafasi yake ya kufanya, iwe ni kwenye fursa, iwe ni kwenye hamasa, elimu n.k, kuna mengi serikali inaweza kufanya. Sasa tunaweza kutofautiana hapo ni kipi kifanyike, ni kipi kisifanyike. Ni tofauti ya kawaida.Kama kuna jambo tulipaswa tujitite ni hapo, kwamba mbona kwangu naona option nzuri zaidi ingekuwa A na sio B, ni C na sio D. Ndipo tulipotakiwa kuhangaika nako sasa.

Lakini kuitafsiri unavyotafsiri kauli ya kisera na kimfumo kwa namna tunavyotafsiri hapa bila shaka tatizo sio kwa Zitto bali lipo ndani yetu sie.Kutafsiri hivi kunahitaji kwanza kuwa na huo "u-kaskazini kwanza", kwani hakuna sehemu Zitto kazungumzia kanda yoyote.Hakuna sehemu Zitto kawasema wananchi wa Kaskazini, ata sehemu moja, kazungumzia hali ya maendeleo ya kiuchumi nchi nchini, na umuhimu wa kuboresha mfumo wa kiuchumi ili kuboresha hali hii kwa mfano wa maeneo yaliyo nyuma, hajasema maeneo yaliyo mbele yarudishwe nyuma au yatengwe, note hilo!!

Kwenye kauli ileile ileile alisema


  • Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP."

Naamini kuna watu wa LIndi pia hapa, hawajashtuka lolote kwa sababu ni suala la kisera tu, ni suala la Tanzania, na kote ni kwao.

Sasa huu utafsiri wa Ukaskazin umetoka wapi?huu utafsiri wa "wananchi wa Kaskazini umetoka wapi"?
Hii ishara ya wazi kuwa bado tuna kazi ya kufanya kuujenga huu Utaifa huu. Hii ni wazi sasa kuliko kabla kuwa Nyerere hakumaliza kazi ya kuujenga Utanzania wetu, hii ni ishara kuwa tunao akina Nassari humu (refer kauli yake ya kujenga nchi ya Kaskazini),wenye Ukaskazini mioyoni mwao, na ndio maana wanalazimisha kutafsiri Ukaskazini ata ambapo hakuna mtu kataja Ukaskazini.

Na hapa ndipo lilipo tatizo na wala sio kauli ya Zitto, tuna kazi nzito sana ya kufanya hapa, na jitihada hizi zinapaswa zifanywe na kila mmoja wetu, tutoke hapa,tuujenge Utanzania mioyoni mwetu.


 
Siwezi kununua uongo wake, kama wewe unaamini maneno yake amini hivyo, nitamsoma kiduchu, nitamsikiliza kiduchu ila siwezi kukubali maneno yake bila kuhoji
Sipo hapo kukulizamisha wewe kuamini ninachoandika nipo hapa kuwafahamisha wale wote wanaofuatilia huu mnakasha.

Narudia tena Zitto kujiunga Chadema mwaka 1993 wakati huo yupo kidatu cha tatu.

Wakati huo Dr.Slaa alikuwa amewakumbatia watawala CCM huo ndiyo ukweli ingawa kuna watu inawauma kisikia haya.
 
Last edited by a moderator:

Huwezi kubadilisha historia leo. Upinzania wa chama kuwa na nguvu dhidi ya CCM umeanzia Kigoma.

Ata kama unawachukia lakini huwezi kubadilisha historia.
 
Sijui mnachopinga nini mnaleta mfano wa Mwenyekiti wa Kijiji wakati Kigoma walitoa mbunge wa kwanza wa Chadema 1994 kwenye Bunge ili kwenu siyo kubwa, kubwa ni la Mwenyekiti wa kijiji kuchaguliwa.

Halafu unapotosha siyo kweli kuwa uchaguzi ulirudiwa mara nne hii sijui umeipata wapi au unameza tu kila unachoambiwa na Mag3.

Baada ya kuanza kwa vyama vingi vya siasa, na karatu kuwa jimbo la uchaguzi ndani ya wilaya ya mbulu, historia nyingine inakuja pale ambapo katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kijiji cha Gongali ilipo msimamisha mgombea wa mwenyekiti wa kijiji kupitia Chadema mwaka 1994 na kushinda kwa kura nyingi sana na kuandika katika historia ya nchi kuwa kijiji cha kwanza kuongozwa na upinzani na ndio kijiji ambacho anaishi Dr. W.P.Slaa.
 
Last edited by a moderator:
Nishakujibu huko mwanzo, juu ya "midomo mirefu", sitaki kuamini kama bado lugha ya picha hiyo haieleweki.


Kwa hiyo ni haki watu wa Arusha, Singida na Iringa kuitwa wana midomo mrefu?? Hivi kama alimaanisha Lissu je alishindwa kusema Lissu ana mdomo mrefu? na kama alimaanisha Lissu na wengineo, Je alishindwa kusema "baadhi ya watu wa Singida wana midomo mrefu? (angesema hivi wala nisingeleta hiyo video maana ningekuja anamaanisha "baadhi ambao ni chadema") kulikuwa na mantiki gani ya kusema watu (Wote) wa hiyo mikoa wana midomo mrefu iwe kwa tafsiri yako (lugha ya picha) au iwe kwa tafsiri yangu.




Nafikiri hapa kumbukumbu zako haziko sawa hii siwezi kukulaumu maana hatuna info za kutosha kumhusu Dr. Amani Kabourou. Baada ya kupekua pekua huku na kule ndo nimepta info za kuwa :

Ni kweli kuwa Mwaka 1994 kulikuwa na uchaguzi wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi Tanzania bara,
Ni kweli Dr. Amani Kabourou aligomea na Premj
Na ukweli ni kuwa Premji alimshinda Kabourou,
Na ukweli ni kuwa matokeo yalitenguliwa na mahakama hivyo Kigoma mjini ikawa haina mbunge mpaka Mwaka ulifuata yaani 1995.

Hivyo ni uongo kuwa Mbunge wa kwanza Tangayika kukaa katika bunge la Jamhuri ni Dr. Amani Kabourou. (ninaweza kusahihishwa maana info ni tatizo Tanzania)


..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…