Kapwela uchaguzi wa kwanza kabisa kufanyika baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi na upinzani kushinda ulikuwa ni wa serikali za mitaa mwaka
1994. Aliyeshinda uchaguzi huo na kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa kijiji kupitia chama cha Chadema aliitwa
Simon Kibola aliyeshinda na kuwa Mwenyekiti wa Kijiji kinachoitwa
Gongali huko
Karatu.
Chama cha Mapinduzi hakikuamini kwamba kingeweza kushindwa na hivyo uchaguzi kurudiwa mara nne chini ya usimamizi wa defenda za polisi kutoka Arusha. Ilibidi uchaguzi wa wazi ufanyike baada ya wana Karatu kukomaa na kumkataa kabisa mgombea wa CCM.
Kwa kumbukumbu Dr. Slaa mwaka
1995 alichaguliwa kuwa mbunge pia kupitia Chadema alikohamia baada ya chama chake cha CCM kumletea mizengwe. Katika uchaguzi huo wabunge machachari
Masumbuko Lamwai na
Mabere Marando walichaguliwa kupitia chama cha NCCR Mageuzi.
Sijui hii ya Kabourou kuchaguliwa mwaka 1994 unaipata wapi lakini ni wazi watu wa Karatu ndio wanaweza kupewa sifa kwa kuvunja mwiko wa CCM kushindwa kwenye uchaguzi wowote ule. Sasa na wewe naomba uje hapa na facts jinsi wana Kigoma walivyopigwa virungu kwa kuunga mkono mageuzi.
Katika wabunge waliochaguliwa mwaka 1995 kutoka Upinzani, wengi kwa ulafi walirudi CCM isipokuwa wanamageuzi wa kweli ambao walikataa vishawishi vya CCM na hadi leo tunao wakiongoza Upinzani katika nyadhifa mbali mbali.