Hutuitaji kutafsiri "Wakati watu wa Kigoma wanapigwa mabomu kwa kutaka mageuzi watu wa ARusha, Singida, Iringa walikuwa wanakumbatia watawala.. hapa hakuna lugha ya picha bali ni ujumbe wa moja kwa moja kwenda kwa watu wa Iringa na nk.. "Laiti kama angesema baadhi ya watu" "bila kutaja mikoa" hapo walau tungeweza kusema anawalenga wabaya wake ambao ni viongozi wa Chadema. Kitu ambacho ni kawaida kwa siasa zetu za maji taka.
Lakini unapotaja watu wa sehemu fulani wako hivi au vile huwezi kusema hii ni lugha ya picha iwe umeitaja kwa mbaya au kwa mazuri.
Pia bado sijaona uhusihano wa speech ya Obama na speech za Zitto , Obama ametumia msemo na huu msemo ameutumia kwa kumlenga mtu mmoja ambaye kila mtu ni anamfahamu kuwa ni Bi.Hilaly. Hebu niambie kama huu msemo angeutumia kwa kumaanisha wakazi wa Mississipi au Carifornia hali ingekuwaje? Na hapo ndo point yangu ilipo kuwa iwe ni lugha ya picha kama unavyotafsiri yaani uongo au laa swali langu liko pale pale ni kweli watu wa Iringa, Arusha na Singida wanamidomo mrefu au ( waongo) (lugha ya picha)?
Niliishatoa maelezo marefu sana juu ya hili,dunia haisimami,tuangalie mengine.
wale watu waliokuwa na hisia kuwa "wachaga wanakwapua fedha za mikoa fulani na kuzipeleka makwao na ndo maana wanakuwa na maendeleo zaidi ya maeneo mengine, SI KWELI BALI WATU WA ARUSHA/KILIMANJARO MAENDELEO YAO YAMELETWA NA JUHUDI ZAO
"wachaga" , Wamedhalilishwa, kuna watu walienda mbali zaidi na kusema kuwa wanakwapua pesa za maendeleo ya mikoa mingine wanapeleka kwao, kuwa wachaga wamejazana TRA na nk.
Kama u mkweli utakubaliana nami kuwa Zitto hajasema popote kuwa kuna mkoa wowote unaounyonya mkoa mwingine,hajataja kabisa kanda yoyote, alitoa takwimu za nchi nzima,akitoa mifano ya baadhi ya mikoa,alitaja mikoa ya pande zote za nchi, huwezi kurasimisha kwenye KANDA MOJA,unless una lako jambo.
Kama u mkweli wa nafsi yako utakubaliana na mimi Zitto hajaongea neno/maneno yoyote ya kuwabagua watu wengine (juu ya mapato), wewe mwenyewe unasema hapa kuwa ni tafsiri za baadhi ya watu ndio zilikwenda huko, na mbaya zaidi ata ma-great thinker hapa wakazitafsiri kwa tafsiri zao hizohizo zilizosukumwa na chuki za kisiasa na kuzipa jina la "ZItto kasema".Hili ni kosa. Mjadala wote huu umejikita kwenye msingi huu mbovu.
Na jambo la kusikitisha wewe niliyekuona katika huo mjadala ukikemea ubaguzi wa wazi ulionyeshwa bali ulikaa na kunywa Chai, au soda au bia huku huku ikushangilia kuona watanzania wenzako wakidhalilishwa kutokana na kauli za fitina na chuki za Zitto.
Hapa kweli siwezi kushangaa kuhusu tafsiri za hayo ya Zitto maana napata picha hapa jinsi ulivyo na uwezo wa kudhania, mpaka kwenye keyboard yako ukaweza "kuniona nikishangilia"!!hisia hisia hisia
kwa makusudi Zitto aliona reaction ya watu juu ya kauli yake Lakini hakujitokeza kusema "jamani sikumaanisha hivyo au sikujua kuwa watu wangechukulia hivi bali nimaanisha hivi na vile.. Zitto alikaa kimya akifurahi watu wakibaguana na kudhalilishana.
Na Zitto nae katu hakuwezi kujificha, kupitia keyboard yako uliweza kumuona jinsi anavyokuwa akifurahia watu wakibaguana!!hisia hisia hisia.
Yaan tupo page ya 66 lakini msingi wa hoja yenyewe upo kwenye hisia, tunahisi "alimaanisha hivi", "tunahisi anauchukia na mkoa wa nyumbani kwetu", "tunahisi analichukia kabila letu","tunahisi hatupendi sisi watu wa huku", "tunahisi anaona sisi tunapendelewa", "tunahisi kuwa alimaanisha kuwa mchango wa mapato wa mkoa ndio KIGEZO PEKEE cha maendeleo", msisitioz "KIGEZO PEKEE".
Hoja kubwa kama hii haiwezi ikasimama kwenye jukwaa la great thinkers kwa muda wote huu na msingi wake TUNAHISI TU.
Sasa kama wewe ambaye akina Nguruvi ndio wanakufanya msahafu wa kutoa habari za "ndani" za Zitto(refer Udini/Ubaguzi) na hapa unahisi tu sasa vip wao?maana wewe ndio reference ati.
Ila tatizo lako ni baada ya Nguvuri3 kuona hizo sitofahamu na kuamua kutumia muda wake ambao labda angeutumia kufanya shughuli zake za kujiongeza kipato na kuleta hoja hapa ya kupingana na Zitto juu ya fitina zake na uongo.
Nikukumbushe aliyeleta kauli ya Arusha Kili vs Shinyanga si Alinda wa Nguruvi3 ni Zitto Kabwe...
Zitto kaleta pambano la Arusha Vs Shinyanga? ajabu hii, unarudia kumaanisha kuwa Zitto hakupaswa kutaja jina la Kilimanjaro kwenye mfano wake lakini angetaja Lindi sio kosa, maana hakuna mtu kalalamika kutajwa kwa Lindi na hatujaona watu wa Lindi wakilalamika kutajwa mkoa wao, vip Kilimanjaro?kuna nini mpaka ilete maneno yote hayo kwa kutajwa tu Kilimanjaro?hii ndio inaleta picha ya tatizo mahsusi.
Tatizo sio mfano huo bali tatizo ni kuutaja mkoa wa Kilimanjaro, kuwa mwanasiasa asiyetoka Kilimanjro haruhusiwi kutoa mfano wa mkoa wa Kilimanjaro?hizi hisia zenu za uzalendo kwa mkoa badala ya taifa mnapaswa ni ishara ya upungufu wa Utanzania na ndio maana mnaspin kila kitu ili kutafuta excuse ya kujenga hisia kupitia mgongo wa mtu mwingine, kwenye hii thread Zitto, ili kuepuka kuonyesha sura zenu halisi.
Muda huu ungetumika vizuri zaidi kujenga utaifa badala ya kujenga Ukaskazini kulikoshamiri kwenye thread hii, muda huu ungetumika vizuri sana kuitambua mipaka ya nchi ya Tanzania, tanzania moja, isiyo na mipaka ndani yake, thread hii imeonyesha "uzalendo wa dhati" wa baadhi ya watu kwenye maeneo wanayotokea, miaka 54 baada ya Uhuru bado watu hawajaweza kujitambua kwa taifa lao bali wapo sensitive zaidi na kutajwa tu kwa eneo lao na kitu kitu kiwe ata cha kisera wanakitafsiri kwanza kwa mkoa wao.
Hii ni aibu, tutoke huko.