Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Awe kasema popote alipo midhali kasema tuna m-hold acconutabe, perfect and square tukizingatia ukweli amepewa benefit of doubt hadi kujaribu kuliangamiza taifa.

Mnachosema wafuasi wake watiifu ni kuwa Kiongozi mkuu hakutoa kauli za kuligawa taifa.

Mnafanya hivyo mkijithadi kuficha ukweli.Nyuma ya pazia katika majadiliano tunaona mnaunga mkono ‘unfair distribution of national cake' Mkiulizwa wekeni hapa ili tuone unfairness ipo wapi , mnakimbiaau kukimbilia hoja za .. dah

Tunajua Mknadara alisema na yupo katika rekodi, mikoa imependelewa kwa kuwa na maji.
Yaani maji yanayotoka ardhini hayakugawanywa vema, sasa sijiu na mungu au serikali.

Kazungumzia umeme n.k.Kasema kuhusu uwezeshwaji ingawa naye kama wewe hakusema uweeshwaji gani na kwanjia zipi.
At least tunajua Mkandara ana fundo tu na anamuunga mkono bila sababu. At least tunajua hilo


Alinda anauliza, ni kwa namna gani na njia zipi au maeneo gani kuna unfair distribution of national cake Bwana Gamba laNyoka?

Jibu haliwezi kuwa Nguruvi bali maelezo yako
 
Last edited by a moderator:
Na hili limejieleza wazi kabisa, si katika ngazi ya serikali tu, hata halmashauri za miji.

Manispaa nyingi zilizopata hata safi ya makusanyo na matumizi, pia zinakiwango kikubwa cha maendeleo.

Hivyo sisuala la GDP tu, Taxation ambayo mchambuzi kasema imewekewa sheria ni muhimu sana katika ku define maendeleo
 
Katika suala la Justice, kundi linaloplipa kodi katika jamii ni wafanyakazi ambao hawana namna ya kukwepa.

Kundi lingine ni la walaji (consumers) ambalo kodi zimefungwa katika bidhaa.
Na kundi lingine ni la ‘essential services' kwamba ni lazima mtu alipe kodi kwa huduma anayoihitaji kwa lazima


Kuna makundi yasiyojulikana yanalipa vipi kodi. Mchambuzi kaongele informal sector.

Hili ni kundi kubwa sana hakuna anayejua linachangia vipi katika kodi.
Kundi hili linahusisha wafanyabiashara, wakulima na watoa huduma ambazo hazina usajili.


Fikria, kuna watu wanafanya biashara bila kulipa kodi ukiachilia mbali ile ya essential services.

Kwa mfano, mfanyabiashara wa mpunga/mahindi n.k., kodi anayolipia ni ile ya mafuta tu kutokana na tozo la mwneye gari.

Hana kodi nyingine na anaweza kuwa na biashara ya mamilioni.

Hapa ndipo suala la efficiency linapoingia. Kwamba hatujui nani anapaswa kulipa kodi, bali tunajua akina nani walipe kodi.

Je, tax system ni effective, absolutely no! Tumeona justice, efficiency zinavyopwaya.

Supreme leader angeweza kuona tax evasion inavyolimaliza taifa.

Unapokuwa na ukwepaji kodi wa Trilioni moja kwa mwaka hilo tu linaeleza wapi tuna matatizo


Supreme leader alipaswa aangalie system nzima ilivyo. Kwamba hatukusanyi kodi, hatuna mfumo wa kubaini nani analipa nani halipi, na kwamba hakuna effectiveness katika suala zima

Kwenda kuongelea mikoa hii ipo hivi ile ipo vile, huu unachangia hivi ule unachangia vile ni kiwango cha chini, dhaifu, dhalili na kisicho na chembe ya busara.

This guy( supreme) is an economist, we expected a lot from him, anapotoka kibubusa majukaani is very unfortunate
 
Awe kasema popote alipo midhali kasema tuna m-hold acconutabe, perfect and square tukizingatia ukweli amepewa benefit of doubt hadi kujaribu kuliangamiza taifa.

Mnafanya hivyo mkijithadi kuficha ukweli.

Supreme leader angeweza kuona tax evasion inavyolimaliza taifa.

Supreme leader alipaswa aangalie system nzima ilivyo.

This guy( supreme) is an economist, we expected a lot from him, anapotoka kibubusa majukaani is very unfortunate

Naamini u mtu mzima kama nilivyo mimi.

Kuendelea KURUDIA HOJA AMBAZO TAYARI ZIMETHIBITIKA KUWA SIO ZA KWELI NI KULIDHARIRISHA JUKWAA HILI.

JIHOJI MWENYEWE!

TUSIMAME KWENYE UKWELI, PROPAGANDA NA UONGO SIO SEHEMU YA JUKWAA LA GREAT THINKERS.

Heshima kwako!




A Lie Can Travel Halfway Around the World While the Truth Is Putting On Its Shoes
 
Umekuja na version yako, ukweli ni upi?
Maana kila mtuanatupa taulo ilimradi supreme aonekane kaokoka. Huko tumewaachia ninyi wabeba viatu.
Wewe ni kada
,sisi ni wananchi

Mchambuzi kaja hapakamuonyesha Gmaba la Nyoka.

Kama utakumbuka
@Gamba la Nyoka alisema mikoa inastahili kupata mgao wa GDP kutokana na inavyochangia teana aimuunga mkono supreme.


Yaani hakujua maana ya GDP na tax na tofauti zake. Mchambuzi kamwekea hadi mfano wa taa za barabarani. Katulia

Takwimu zimewekwa hapa, fanyia kazi kumuokoa si kutafuta teehe 20 guruvi kaandika nini
Mtoeni mtu wenu kweye lindi la tope la majita analoishi na atakaloishi nalo


Huyu supreme leader ni mchumi, mtu aliyewahi kuwa na nyadhifa zinazo mwezesha kuelewa matatizo ya taifa hili.

Anajua wizi unavyoumiza, kukwepa kodi, misamaha ya kodi na kutoka na njia za kukusanya kodi.
Anajua madini na matatizo yake hadi kupelekeakuwa mjumbe wa tume ya Bomani.


Huko ndiko matatizo yalipo si wananchi wa baina ya mikoa.

Mchumi/mbunge/kiongozi mkuu anaposimama na kusema kitutusa tu , inasikitisha sana!

Note: Angalia unachotumbukiza hapa, unaumiza washirika wako.
Nikimwita Wabe itakuwa mbaya. Hivi wewe na Wabe nani senior ki kazi?



Rudi nyuma usome kwanza . Wanapwaya- zumbemkuu
 
Mchambuzi, Mkuu Pato la Taifa ni mzunguko mzima wa biashara kwa kila mkoa wakati Taxes ni makusanyo ya kodi za serikali. Chukulia wewe mshahara wako kwa mwezi ni Tsh Mil.3 hili ndilo pato lako na pengine kuna mkeo, na watoto wanafanya kazi ama vibarua au biashara na jumla yenu ndilo pato la nyuma yako lakini nyote mnalipa kodi asilimia 20 ya mapato yenu kwa serikali na inawezekana mmoja wenu halipi kutokana na shughuli anayoifanya pengine ni NGo ama ina msamaha..

Hivyo, makusanyo ya kodi sio tu inawezekana ila wapo watu wengi wenye kipato lakini hawalipi kodi mfano wenye nyumba za kupangisha na wapo waliosamehewa kodi na wengine hawalipi kabisa kama mawaziri na wabunge. Pia inawezekanauwepo uzembe ama mfumo mbaya wa kukusanya kodi hivyo fedha nyingi hazikusanywi na serikali ilhali Pato la Taifa ni jumla ya fedha zote zinazozungusha uchumi.

Kwa hiyo Tunapozungumzia Pato la Taifa ni jumla ya uzalishaji mzima wa mkoa na kodi ni fedha ambazo serikali imekusanya tokana na mapato ya mishahara ya watu, Corporate Tax, VAT, ushuru na kadhalika na sii jumla ya fedha zinazoendesha shughuli zote za kiuchumi. Sijui tumeelewana au bado una maswali mengine..
 

Jifunze kuwa na uadilifu wa mjadala, uadilifu wa kimjadala ni pamoja na kukubali ulipokosea, huu ni msingi wa majadiliano ya watu wazima,wenye akili timamu.

Kwenye jukwaa kama hili hatupo kUbishana tu, tunajadiliana kwa kithibitisho,kama huna kithibitisho na hutaki kukubali cha mwingine basi unapumzika/hubishi kwanza mpaka utakapopata data zinazoweza kuthibitisha otherwise, ndio ustaarabu.

Sasa wewe kurudi mkavumkavu unabisha na kithibitisho huna utadhani ni walevi waliopo kilabuni ni ishara ya kutoheshimu watu wanaojadili hapa, kumbuka watu hawaji hapa kusoma UONGO wala PROPAGANDA, wanataka taarifa sahihi.

Ni wiki ya tatu sasa nakwambia,hoja ya kusimamaia haiwezi kuwa fulani kasema ni ZITTO KASEMA NINI, Barubaru kaeleza hili
pia

Narudia, hoja ya mjadala ni ZITTO KASEMA,elewa hii principle muhimu.Huna haja ya kujazajaza majina fulani kasema fulani kasema, unapaswa ujue hili.

Otherwise, ukosefu wa uadilifu wa mjadala unaouonyesha ni too low kwa jukwaa hili.

Rejea ushauri wangu hapa chini,CHUKUA HATUA!


A Lie Can Travel Halfway Around the World While the Truth Is Putting On Its Shoes
 
@Kapwela rudi 760. JokaKuualikualika hukuitikia wito Sisi tunaendelea .
Huko kwenye tope ni kwenu,endeleeni kumkwamu,asikutane na hasira za umma


Tumeona takwimu zote zilizowakilisha@Mchambuzi na zile za Mkandara

Hakuna anayetueleza mahusiano yawazi kati ya uchangiaji wa maendeleo na pato la taifa.

Hakukuwa na sababu zakuleta sintofahamu miongoni mwa wananchi ikiwa hakuna maelezo ya kutoshakuhusu nini supreme leader alikusudia


Dhana ya kwamba kuna mgawanyousio sawa wa rasilimali inatokana na matamshi na uenezi wa siasa chafu.Wahusika wameulizwa, ni wapi ambapo kuna walakini katika ugawananaji wa pato lataifa?
Ni eneo gani linalonyimwa na lipilinapewa isichostahili?

Alinda kauliza mara zaidi ya 10,kuna uhusiano gani wa GDP na maendeleo?

Maswali haya yamekuwa yanakimbiwa. Watoa tuhuma hizo kwa dhati ya moyo wao wanaungana na kauli zasupreme leader kuwa ipo mikoa wanayoilenga imeendelea kutokana na mgawanyo usiosawa wa rasilimali

Lakini pia , dhana hii ya chukiimeingia kiasi kwamba wapo wenzetu kama Gamba la Nyoka , wanaamini kwa dhatikuchangia pato la taifa (GDP) ni lazima kwende samba samba na kupewa zaidi.
Nahili pia kalisema Mkandara akieleza ‘wanaomba chao'


Ukiangalia katika suala la kodi,watu hao hao wanaosema GDP iwe kigezo hawawelezi lolote kuhusu kodi.

Mchambuzikaonyesha tofauti ya GDP kama thamani ya uchumi wa eneo husika, na kodi ikiwani makusanyo ya kisheria


Kaeleza, kodi ndizo zinazotoa huduma zinazolalamikiwa kama infrastrure/elimu /afya

Ni wakati sasa wale wanaotete hoja za GDP na supreme wasimame kujibu hoja
 

Upo sawa ndugu?kama ata kusoma na kuelewa kwako ni shida sasa utajadili vipi?maana unafanya kama tupo kilabuni vile.

This is too low kwa Nguruvi yule niliyekuwa namsoma JF!


Rejea ushauri wangu hapa chini,CHUKUA HATUA!


A Lie Can Travel Halfway Around the World While the Truth Is Putting On Its Shoes
 
Nguruv sasa hivi anasema eti, Haijalishi ZZK kasemea wapi, Hiyo yote ni Fair game kumjadili.
Hapa Nguruv anathibitisha yeye mwenyewe kuwa anajipinga. Anajipinga kwa sababu sasa hivi kwake yeye source za Facebook kwake siyo tatizo tena!.
Hawa ndio Ndumilakuwili wenyewe wasio na misimamo thabiti. Wasio na Intellectual honest ya Kujenga hoja kwa kusimamia kile wanchokiamini

Ndo maana ana flip-flop, Anachange position mara kwa mara, Kiufupi hana anachokisimia.
 
Kapwela, Gamba la Nyoka, Ritz,... Nauliza hivi, je mmeamua kukubali kimya kimya kuwa ACT ni mpini wa CCM kuumaliza upinzani nchini na kauli za Supreme Leader wa ACT kuhusu uchangiaji kwenye pato la Taifa zina mapungufu yanayoweza kuhatarisha umoja wa watanzania?

Asante sana Mchambuzi nimeelimika zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Kapwela

Kama nimemsoma Mchambuzi na kumuelewa vizuri kasema kuchugua GPD kama kigezo cha maendeleo katika mikoa husika ni makosa ila kitu ambacho kinakaribiana na uhalisia wa maendeleo husika ni kigezo cha Tax revenues. (naweza kusahihishiwa maana mimi si mchumi)

Ukisoma andishi la Zitto anasema hivi """ Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa. """

Ukisoma hiyo sentensi utaona kuwa anashangaa kwanini Shinyanga iwe no. 4 katika kuchangia pato la Taifa.. na ni masikini wa kutupwa. Nafikirii kama kumbukumbu zangu ziko sawa ni ya 16 katika maendeleo.

Tukirudi katika andishi lake lingine anasema:
Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7."

Hapa anaendelea kuishangaa Kilimanjaro na Arusha mikoa ambayo inachangia no.7 na 9 lakini inamaendeleo zaidi. Kigezo anachotumia ni uchangiaji wa pato la Taifa.

Swali langu kako Je ni kweli kigezo cha maendeleo katika mikoa husika ni uchangiaji wa pato la taifa?


Na je hayo maneno yake huoni yanajenga sintofahamu kuwa baadhi ya watu hasa sie tusio na ufahamu kuhsu uchumi. Maana kutoka na maelezo yake ndo limetokea lile kundi la watu linalosema "kuna baadhi ya mikoa mengine haipati stahiki ipasavyo (kama mkoa haupati stahiki yake ina maana kuna mkoa unaochukua hizo stahiki) ( Kwa bahati mbaya hata mie kabla ya shule ya Nguvuri3 Mchambuzi na wengio nilifikiri kuwa Shinyanga "inanyonywa" ) na ili kundi tulikuwa wengi)

Zitto ni msomi tena ni mchumi huoni kuwa alikuwa na wakati mzuri sana kuelezea hii hali kwa ufasaha kama alivyofanya Mchambuzi, na kutwambia chama chake kina mkakati gani kuhakikisha maeneo kama Shinyanga yanakuwa na maendeleo zaidi kama ilivyo mikoa mengine?




 

Haya tufanye mjadala.. naomba unipe ufafanuzi wako kuhusu "Stahiki"
 
Haya tufanye mjadala.. naomba unipe ufafanuzi wako kuhusu "Stahiki"
Alinda msome hapa chini kwa maneno yakemwenyewe Halafu namnukuu Mkandara '' Alichosema Zitto ni kuwa Kilimanjar na Arusha zinachangia kidogo na zinapata stahiki.
Shinyanga inachangia zaidihaipati stahiki''
Haya ni maneno yaMkandara, akatae


Mchambuzi kaja na takwimu, katuonyesha GDP na tax revune na jinsi gani zinaweza kutumika.

Hakuna hata mmoja miongoni mwa wafuasi anayekataa ukweli huo.


Tunawauliza, GDP na maendeleo vina uhusiano gani?

Kwa maneno mengine, wanakubali kuwa kiongozi alipotosha umma.

Hapo ndipo hoja ilipo, kuwa nia yake katika kuweka takwimu iliongoza na nia ovu ya kusababisha mgongano katika jamii. Ikifika hapo hatukai kimya hataspinning 1000 zikifanywa


 
Last edited by a moderator:
Alinda msome mkuu hapa maana hawakawii kusema nimemwekea maneno

Habari hii ni baada ya JokaKuu kusema , kiongozi mkuu alifanya makosa kulinganisha jamii mojana nyingine.
Alichotakiwa ni kuonyesha matatizo ya jamii kwa ujumla nakwa watu husika.


Mkuu Mkandara kasema hapana , kuna inequality katika kugawa keki tataifa.

Maneno hayo yamerudiwa na Gamba la Nyoka aliyesema kuna unfair distribution of national cake


Wote hawa walikuwa wanatetea hoja za kiongozi mkuu kuhusu mikoa inayochangia na iliyoendelea..

Kiwewe chote kilizushwa na Mchambuzi aliyemwaga data zake alizoombwa na kuzifinga finyanga.
Hoja ikahama kutoka data ikafikia hapa chini
Ukisoma maneno yaMkandara, maana yake ni kuwa mikoa inayochangia kidogo ipate kidogo kwa maana ileile kuwa mikoa inayochangia zaidi ipate zaidi

Hapa napo tunahoji kama wenzetu wanahoja. Wakati wanalalamika unfair distribution of nationa cake, wakati huo huo wana promot unfairness.

Hivi mwananchi wa SIngida akiwasoma atawaelewa kweli.

Hii ndiyo dhana waliyopewa kuieneza, bila kujua wanaeneza sumu ilimradi tu kumpamba maua supreme,hawaangalii athari zake katika umoja wa taifa, wanaangalia masilahi ya mtu katika motive ile ile ya kuandika katiba ya mtu na si watu
.

Katika kuweweseka nawanukuu tena wafuatao

Mkandara- Mikoa yote wanaishi watu wa makabila yote na woteni Watanzania.
Hivyo maendeleo ya eneo moja yanagusa wote


Gamba la Nyoka, Tanzani ni moja, ukiwa Kilimanjaro niTanzania ukiwa Shinyanga ni Tanzania.

Jiulize, kama kweli ndiyo dhamira yao, wapi wanapata ushujaawa kusema hayo hapo juu?
 
Last edited by a moderator:
Alifanya marekebisho baada ya watu kuja juu .. Na kudhibitisha ili lsoma au leta michango ya watu waliochangia.

Kudhibitisha ili msome Al Guido, majibu ya Cristous tena majibu ya Al Guido, na Zitto kaandisha alichokuwa ameandika hapo mwanzo.

Alinda,

Unatuambia kuwa Zitto alibadilisha baada ya kuona anaandamwa na watu. Je wewe ulichotuwekea ni kile alichoandika kabla hajabadilisha au ulichukua baadhwi ya Para na kuacha baadhwi?



Kwa andiko la ZZK aliloliweka kapwela hapa barazani ni SAFI kabisa halina mushkeri wala tatizo lolote kwa mtu yoyote mahiri na mchumi anayefatilia na kujua uchumi wa Tanzania. Lakin sivyo ulivyoliweka wewe lilikuwa ma mashakir na mushker kibaaao kiasi cha kupunguza weledi wa ZZK katika mambo ya uchumi ambao ndio taaluma yake.

Kama ulichukua baadhwi ya para na kuacha nyingine katika maandiko ya ZZK hilo ni kosa kubwa sana na inakupasa
uombe jukwa radhwi na kumuomba ZZK radhwi kwa kumlisha na kumzulia maneno. Lakin kama aliliweka kama ulivyoripoti wewe basi tuwekee kama alivyofanya kapwela ili tuone ukweli na urongo upo wapi?

 
Mchambuzi.

Majibu yako haya hapa juu ni majibu mujarabu kutoka.


Tanzania Human Development Report 2014. Taarifa imesheheni kwa kweli.

Huu utafiti ni wa kisomi siyo porojo.
 
Last edited by a moderator:

Mchambuzi,

Naona umetumia maneno makali sana kwa ZZK.

Je unaweza kunitajia mwanasiasa yoyote huko Tz hususan Tgk kwa wanaokusudia/ kutia nia kugombea uraisi wa Tz ambaye ni msafi asiye LAGHAI na asiyechezea akili za waTz katika kusaka uraisi wake?

Mara nyingi nimekuwa najiuliza mbona ZZK na sio Slaa au JK au Prof Lipumba? Je kunani kwa ZZK?

Naomba jibu lako mkulu.

Ahsantum

 

Mkandara.

Naona umefanya very good Summary. Ahsantum.

Ila palipo niacha HOI hilo hitimisho lako ambalo umeweka bayana bila kificha chochote.

Mimi siku zote nasema yale yaliyofichwa miaka nenda rudi kwa joho la ujamaa ya kugawana umasikini ndio sasa inadhwihiri.

Kabla ya Uhuru yaani wakt wa mkoloni huko Tgk mikoa kama Tanga, Morogoro na Tabora iling'ara sana na ilikuwa na uchumi wa juu sana kuliko Kilimanjaro, Arusha na hata Mwanza leo hii imerudi nyumba kibisaaaaa mpaka inatia huruma. Mimi kama mchumi nikijaribu kujiuliza wamekosea wapi mpaka kila siku hali za mikoa hii inazidi kuwa Duni na kuangalia hio mikoa inayopanda kiuchumi inafanya nini sioni zaidi ya kila mwanasiasa kukumbuka kwao.

Mimi nikiwa wizara ya fedhwa Muungano katika kitengo cha bajeti nilikuwa naoma mashinikizo ya kisiasaa katika kugawana keki ya Taifa. Sisemi mengi lakin kma Mtamuuliza Mz Cleopa Msuya au Mz wangu Edwin Mtei atafafanua mengi sana na wana uwezo mkubwa sana kuizungumzia hiyo keki yenu.

Poleni sana.

 

Napenda kurudia maneno ya Ahali yangu ZAKUMI.

"Siasa ni mchezo wa taifa wa Tanzania. Tanzanian people take pride when they engage in unproductive and endless debates.

Kwa maoni yangu binafsi, mfumo wa kisiasa umeundwa hili kulaghai ulimwengu kuwa Tanzania nayo inajishughulisha kwenye demokrasia. Mpaka pale watu watakapojua kuwa demokrasia ni kwa faida yao wenyewe na sio kuwafurahisha wahisani au kuleta ushabiki wa michezo ndipo watu watakapokuwa serious.
"

Ahsantum
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…