Mchambuzi,Nguruvi, Alinda, mnaweza mkaliepuka hilo leo kwa kufuatilia mkutano LIVE kutokea Mwembeyanga Temeke kupitia Azam TV, Channel 10, na EFM Radio kuanzia saa 10 jioni.
Aksanteni sana na Kwaherini!
Hahah Mmeshaacha habari za Facebook, leo mmegeukia MwembeYanga na kwamba mmekuwa washauri wa ZZK acheni chuki zenu binafsi
Turudi kwenye Mada acheni hii intoxication ya Zittophobia
Gamba la Nyoka , kwanza tunaitikia wito wa Kapwela.Hahah Mmeshaacha habari za Facebook, leo mmegeukia MwembeYanga na kwamba mmekuwa washauri wa ZZK acheni chuki zenu binafsi
Turudi kwenye Mada acheni hii intoxication ya Zittophobia
Hili swala la kuwataja wenye account Uswiss kusema kweli binafsi yangu sikufurahia hata kuahidi kuwataja kwa sababu hizi kelele za mlangoni kusema kweli haziwezi kutusaidia kitu. Akiwataja kama Dr.Slaa ingesaidia nini zaidi ya kutafuta umaarufu maanake tumeisha ona mifano huko nyuma kuwa serikali yetu haifuatilii kabisa maswala haya. Kama wangekuwa viongozi waliopo ama walopita hapo kidogo ninge shukuru kwa sababu unawaondolea kura za uchaguzi kwa wenye uchungu..
He mara hii Zitto mwenye kulaumiwa kwa kusema Kilimanjaro kuinyonya shinyanga, eti anazungumzia na Kilimanjaro Kunyonywa pia.
je hii si ni ushahidi wa Wazi wa Zitto kutaka fair distribution ya keki ya taifa? na si issue ya ubaguzi?.
Tupe ufafanuzi hapo, kivipi unataka fair distribution na kwa vigezo vipi? tupe shule kwa uelewa wako..Lakini kabla ya hapo pata shule kutoka kwa Mchambuzi..
Umeona sasa mkuu Ritz, hii disparity sijui kwa nini Mchambuzi haioni. Kutokana na weakness katika taxation regime, ambapo kodi kutoka sehemu moja ya nchi zinakusanywa sehemu nyingine,ni vigumu kuchukulia kodi ya mahala pekee as an indicator ya sehemu hiyo ya kuchangia katika mapato ya serikali compared na sehemu nyinginezo.
Indicator nzuri zaidi, ni kutumia kipimo cha overall production of goods and services ya sehemu fulani kwa mwaka
The GDP disparity is obvious. But what are you trying to imply - that the GDP disparity is a result of weaknesses in taxation system?
Haujaeleweka vyema.
Indicator nzuri kufanya nini? Pia katika Hili haujaeleweka vyema.
Hakuna aliyesema tatizo ni Kodi na siyo GDP, Usiwalishe wana Ukumbi Maneno.
Again, Tatizo siyo Kilimanjaro kama mkoa na watu wake, Tatizo ni serikali isiyo Fair, ambayo ina mipango mibovu katika ugawaji wa pato la taifa, Serikali ambayo hapo juu Ritz amekuonyesha hata Mbunge wa Shinyanga akilalamika kuwa Serikali imeuacha nyuma mno huo mkoa ktk suala la afya na Elimu.
QUOTE=Alinda;13172595]
Gamba la Nyoka tuko pamoja katika mjadala huu? Pato la Taifa linagawiwa na Serikali?? Hebu tupe ufafanuzi jinsi serikali inavyogawa pato la taifa..
Gamba la Nyoka natumaini utakuwa umeishapata sehemu tulivu ili tupate majibu/ufafanuzi wa maswali yetu.. Karibu Gamba la Nyoka..Kama swala ni kuomba msamaha ili wanaukumbi tupate shule ya uhakika kutoka kwako.. Basi Gamba la Nyoka naomba msamaha kwa kutaka ufafanuzi wa neno Stahiki badala la Stahili.. Natumaini msamaha wangu umepokelewa.. Hivyo wanaduru tukae mkao mzuri shule yaja.. Haya Gamba la Nyoka uwanja ni wako...
Mkandara,Alinda,
Mimi nakuomba pitia haya maswali na majibu HAPA, yasome taratibu yakuingie kisha fikiria upya swali lako..
Baada ya muda utasikia wanarudi na madai 'acheni chuki'' Tuliuliza chuki zi wapi, hakuna hojaMkandara,
Hiyo link inajadili dhana ya "economic growth", yani kasi ya kukua kwa uchumi. Ni PDF file ambalo Lina kurasa "98" za maswali ya multiple choice na majibu yake kwa mtindo wa jibu Ni "A", "B", "C" au "D". Ni content ambayo inaweza kuwa iliandaliwa Brazil, India, marekani, au nchi yoyote kwa nia ya kufundisha wanafunzi uchumi kwa nadharia, hasa economic growth, tena kwa mtindo wa multiple choice, wala sio discussion or analysis.Hii PDF file inatusaidia nini? Inajibu maswali gani humu?
Kwa kweli Huku Ni kuchanganyikiwa. Acheni ushabiki kwenye masuala nyeti Kama uchumi wa wananchi. Siasa hazina nafasi katika mijadala ya Aina hii. Kiongozi wenu mkuu aliteleza. Kwa pamoja tumsahihishe na tujenge mjadala wa kusaidia taifa.
Hata sikuelewi mkuu wangu unaposema hii link ni dhana! Kama ni dhana sasa tunachobishania hapa nini maana kila kitu ukikichukulia kuwa ni dhana ina maana hakuna Uhalisia wake.Mkandara,
Hiyo link inajadili dhana ya "economic growth", yani kasi ya kukua kwa uchumi. Ni PDF file ambalo Lina kurasa "98" za maswali ya multiple choice na majibu yake kwa mtindo wa jibu Ni "A", "B", "C" au "D". Ni content ambayo inaweza kuwa iliandaliwa Brazil, India, marekani, au nchi yoyote kwa nia ya kufundisha wanafunzi uchumi kwa nadharia, hasa economic growth, tena kwa mtindo wa multiple choice, wala sio discussion or analysis.Hii PDF file inatusaidia nini? Inajibu maswali gani humu?
Kwa kweli Huku Ni kuchanganyikiwa. Acheni ushabiki kwenye masuala nyeti Kama uchumi wa wananchi. Siasa hazina nafasi katika mijadala ya Aina hii. Kiongozi wenu mkuu aliteleza. Kwa pamoja tumsahihishe na tujenge mjadala wa kusaidia taifa.
Alinda,
Mimi nakuomba pitia haya maswali na majibu HAPA, yasome taratibu yakuingie kisha fikiria upya swali lako..
Mkandara,Hata sikuelewi mkuu wangu unaposema hii link ni dhana! Kama ni dhana sasa tunachobishania hapa nini maana kila kitu ukikichukulia kuwa ni dhana ina maana hakuna Uhalisia wake.
Kwanza ungesoma swali la Alinda hapo juu kisha ukasoma nilichokiweka badala ya kuelezea vitu vya ajabu kabisa kuwa hii ni dhana halafu unasema ni somo la Uchumi kwa nadharia. Kuna kitu hapa duniani kisichokuwa nadharia hata afya yako ni nadharia unaweza pima mzima wa Afya na ukakatika usiku kwa kansa ya mapafu wakait huvuti sigara, Ila inaposema Sigara inasababisha Kansa usianze kupinga ati ni nadharia. Ukipanda mbegu za shamba la hekari 10 utategemea kuvuna magunia kadhaa hii ni dhana ambayo inatangulia mahala popote. Ukivuna kidogo ya ile dhana ndivyo kiuchumi hata GDP yenyewe ina Positive na Negative.. ndio dunia tuishio lakini haian maana tusielimike na uwezekano wa kuvuna ulichopanda.
Na Hivi, kuwepo kwa multiple choice ndiko kunabadilisha makuzi ya Uchumi au una maana gani? Swali linapokuwa na Multiple choice au isiwe jibu la swali ni moja tu, Wangweza kuweka swali hilo na kutoa jibu posipo Multiple choice kwa sababu link hiyo imeanza kwa kufundisha kisha ndio unatihaniwa na majibu. Maana ama sababu za kuweka multiple choice ni kutazama kama msomaji ama mtihaniwa ameelewa vizuri alichokisoma.
Nikiuliza 2+2 =? halafu nikaweka A.3, B 6, C22 na D. 4, haina maana nafundisha ila namtihani msomaji hata kama chini kuna jibu. Na mtihaniwa akajibu ni 3 ina maana huyu mtu haelewi hesabu anahitaji kuelimishwa kwa nini 2+2 inakuwa 4. Mara zote Multiple choice huwa mtego mzuri wa kutazama weredi wa mtihaniwa. Usitafute sababu za kubishana juu ya makuzi ya Uchumi yanaweza vipi kubadilisha matokeo.
Swala la Brazil, hivi unataka kunambia kwamba Makuzi ya Uchumi (economic growth) maadam link inajadili Brazil kwa dhana basi ingekuwa tofauti Tanzania? je unajua kwamba hizo namba zilizotumiwa ni dhana tu hakuna uhalisia kwa sababu huu ni mtihani haufuati uhalisia? Hata mahesabu naweza sema Gari linalokwenda kasi ya km 100 kwa saa, litachukua muda gani kufika mita 200 ni dhana maana gari linaweza kuzimika kabla haklijafika mita 100.
Mkuu haya maswali sio somo la kufundishia ila ni jinsi gani Uchumi unakua iwe mahala popote kwa sababu hata ukiwapa maswali hayo wasomi wa uchumi kwa nchi za Urusi, Uingereza, Tanzania, Kenya au Marekani wote majibu yao yatakuwa sawa kwa kutoa majibu yalowekwa hapo, na akiweka jibu tofauti atakuwa maekosea, sasa sielewi unachopinga hapa maana muda wote humu tunazungumzia makuzi ya Uchumi, na somo la Economics haijalishi kama unazungumzia nchi au kijiji majibu yake ni yale yale halafu leo unauliza inatusaidia nini?...
Mkuu, sio wewe ulokataa link hiyo ukisema haina maana yoyote kwa sababu ni dhana? sasa iweje tena useme Economics ni nadharia ambayo kumbe unakubaliana nayo? ndio maana nikakwambia kila kitu hapa duniani ni dhana iwe hata maisha yako mwenyewe, na nikakupa mifano ya 2+2 hadi mwendo wa gari. Equation yoyote inajibiwa kama ilviyo.Mkandara,
Kwa uelewa wangu, dhana maana yake ni concept au kitu Kama hicho. Ulichowasilisha in PDF ni concept of economic growth, au sio Sawa?
Economic growth as a concept is based on models and theories of growth - kwa maana rahisi? Nadharia. Kwanini unakataa na Nini ngumu kuelewa hapo?
Hizi theories and models ndio huwa tested and applied to give us uelewa wa masuala husika ya kiuchumi in contemporary terms.
The PDF file you presented lengo la aliyelitayarisha ilikuwa ni aidha mtihani au somo kwa wanafunzi wa uchumi. Somo hapo ni dhana ya economic growth au kukua kwa uchumi. Presentation hiyo ya PDF haina discussion wala analysis, ni multiple choice questions, basi.
Mimi sikupinga dhana ya economic growth. Na sijapinga kwamba Kama lengo ni kujielimisha, lipo la kujifunza kwenye Hilo PDF file. Vile vile, kutaja kwangu Brazil, india etc maana yangu ilikuwa kwamba hili document linaweza kuwa limeandaliwa in any country kufundisha au kuwapa mtihani walengwa kuhusu dhana ya economic growth. In a global sense, pia the said knowledge applies anywhere where they are practicing neo liberal economics. I didn't dispute any of that.
Nachopinga ni kitendo Chako Cha kutafuta tu document ya uchumi kiholela holela na kuitupia humu kwa madai eti inajibu maswali ya alinda. Je, ulielewa maswali yake? Economic growth inayajibu vipi? How do the 98 questions and answers in the PDF answer maswali ya alinda?
Binafsi I don't see any meaningful relationship between maswali Yale na hiyo copy and paste yako. Otherwise Kwa nini usije na analysis and discussion badala ya copy and paste?