Hata sikuelewi mkuu wangu unaposema hii link ni dhana! Kama ni dhana sasa tunachobishania hapa nini maana kila kitu ukikichukulia kuwa ni dhana ina maana hakuna Uhalisia wake.
Kwanza ungesoma swali la
Alinda hapo juu kisha ukasoma nilichokiweka badala ya kuelezea vitu vya ajabu kabisa kuwa hii ni dhana halafu unasema ni somo la Uchumi kwa nadharia. Kuna kitu hapa duniani kisichokuwa nadharia hata afya yako ni nadharia unaweza pima mzima wa Afya na ukakatika usiku kwa kansa ya mapafu wakait huvuti sigara, Ila inaposema Sigara inasababisha Kansa usianze kupinga ati ni nadharia. Ukipanda mbegu za shamba la hekari 10 utategemea kuvuna magunia kadhaa hii ni dhana ambayo inatangulia mahala popote. Ukivuna kidogo ya ile dhana ndivyo kiuchumi hata GDP yenyewe ina Positive na Negative.. ndio dunia tuishio lakini haian maana tusielimike na uwezekano wa kuvuna ulichopanda.
Na Hivi, kuwepo kwa multiple choice ndiko kunabadilisha makuzi ya Uchumi au una maana gani? Swali linapokuwa na Multiple choice au isiwe jibu la swali ni moja tu, Wangweza kuweka swali hilo na kutoa jibu posipo Multiple choice kwa sababu link hiyo imeanza kwa kufundisha kisha ndio unatihaniwa na majibu. Maana ama sababu za kuweka multiple choice ni kutazama kama msomaji ama mtihaniwa ameelewa vizuri alichokisoma.
Nikiuliza 2+2 =? halafu nikaweka A.3, B 6, C22 na D. 4, haina maana nafundisha ila namtihani msomaji hata kama chini kuna jibu. Na mtihaniwa akajibu ni 3 ina maana huyu mtu haelewi hesabu anahitaji kuelimishwa kwa nini 2+2 inakuwa 4. Mara zote Multiple choice huwa mtego mzuri wa kutazama weredi wa mtihaniwa. Usitafute sababu za kubishana juu ya makuzi ya Uchumi yanaweza vipi kubadilisha matokeo.
Swala la Brazil, hivi unataka kunambia kwamba Makuzi ya Uchumi (economic growth) maadam link inajadili Brazil kwa dhana basi ingekuwa tofauti Tanzania? je unajua kwamba hizo namba zilizotumiwa ni dhana tu hakuna uhalisia kwa sababu huu ni mtihani haufuati uhalisia? Hata mahesabu naweza sema Gari linalokwenda kasi ya km 100 kwa saa, litachukua muda gani kufika mita 200 ni dhana maana gari linaweza kuzimika kabla haklijafika mita 100.
Mkuu haya maswali sio somo la kufundishia ila ni jinsi gani Uchumi unakua iwe mahala popote kwa sababu hata ukiwapa maswali hayo wasomi wa uchumi kwa nchi za Urusi, Uingereza, Tanzania, Kenya au Marekani wote majibu yao yatakuwa sawa kwa kutoa majibu yalowekwa hapo, na akiweka jibu tofauti atakuwa maekosea, sasa sielewi unachopinga hapa maana muda wote humu tunazungumzia makuzi ya Uchumi, na somo la Economics haijalishi kama unazungumzia nchi au kijiji majibu yake ni yale yale halafu leo unauliza inatusaidia nini?...