Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Mchambuzi,Nguruvi, Alinda, mnaweza mkaliepuka hilo leo kwa kufuatilia mkutano LIVE kutokea Mwembeyanga Temeke kupitia Azam TV, Channel 10, na EFM Radio kuanzia saa 10 jioni.

Aksanteni sana na Kwaherini!

Inasemekana mwembeyanga, Zitto amegairi kutaja majina ya mafisadi wa mabilioni ya uswisi, je ni kweli? Kama ni kweli, kwanini tusiamini hoja ya Nguruvi3 bandiko #1745 ?
Waberoya, Mkandara, Ritz, Adharusi.
 
Last edited by a moderator:
Inasemekana mwembeyanga, Zitto amegairi kutaja majina ya mafisadi wa mabilioni ya uswisi, je ni kweli? Kama ni kweli, kwanini tusiamini hoja ya Nguruvi3 hapo juu?

Yaani hakuna siku niliyosikitika kama siku ya leo.. Masikini Zitto Hivi huyu ndo yule Zitto wa Buzwagi?

Nakumbuka hata swala la Buzwagi ilikuwa aende kuomba Bunge msamaha, Ila washauri wake walikesha naye wakimshauri kamwe hasithubutu kuomba msamaha, maana kwa kufanya hivyo atakuwa ameonyesha kuwa yeye si mtu wa kuaminiwa. Wazee hawa walifika mbali na kumwambia kama ni posho ya vikao basi "chama kitakulipa" lakini kamwe na katu husiombe msamaha. Kilichotokea kila mtu anakifahamu.

Sasa kijana aliyejijenga na kuaminiwa na umma (ingawaje baadhi ya umma huu ulianza kupata mashaka naye) leo hii anaharibu hata kile kidogo tu alichokuwa amebaki nacho.

Katika kipindi hiki, kipindi ambacho unajaribu kurudisha imani yako kwa umma unawezaje kufanya ujinga wa namna hii? Unautangazia umma kuwa unakwenda kutaja list ya watu kwenye A/c Uswis mwisho wa siku unawambia watu unaogopa sheria? Mbona unampa Nguruvi3 nguvu ya kudhibitisha kile alichotabiri hapo mwanzo? Mbona unawapa watetezi wako wakati mgumu? Hivi washauri wako ni akina nani?

Ushauri: Siku nyingine kabla hujaenda kwenye pablic na kutangaza/kusema kitu kikubwa kuwa na uhakika na kile usemacho, ikibidi washirikishe washauri wako (tena achana na washauri kama akina@Kitila Mkumbo , akina Mchange na nk tafuta wale washauri wako wa mwanzo kabisa) na wanasheria wako.
 
Hahah Mmeshaacha habari za Facebook, leo mmegeukia MwembeYanga na kwamba mmekuwa washauri wa ZZK acheni chuki zenu binafsi

Turudi kwenye Mada acheni hii intoxication ya Zittophobia
 
Hahah Mmeshaacha habari za Facebook, leo mmegeukia MwembeYanga na kwamba mmekuwa washauri wa ZZK acheni chuki zenu binafsi

Turudi kwenye Mada acheni hii intoxication ya Zittophobia
Gamba la Nyoka , kwanza tunaitikia wito wa Kapwela.
Pili tuna haki ya kusikiliza na kuzungumza.

Tatu, mjadala unaoendelea na hili la mwembe yanga vina link na mwisho hatuna phobia tuna utapeliphobia.

Baada ya kutoa benefit of doubt kwa miaka 15 tukitaraji makuzi, tunachokiona ni kuvia tena kwa hatari kubwa ya utaifa. Hatuendi mahali popote tupo hapa

Baada ya kubaini madai yake ya ubaguzi yamegonga mwamba, kila tawkimu inakataa na kila hoja haikubaliani naye, na baada ya kukumbana na hukumu ya wananchi, kiongozi mkuu anatafuta mahali pa kutokea

Kilichotokea ni kutaka kuua mada husika kwa kutumia ukubwa wa Dar,kugeuza mada kutoka ubaguzi kwenda uswiss apate nafasi ya kuingia anakohisi ni hotbed .

Kule anakosubiriwa aulizwe kuhusu umasikini, utajiri, unyonyaji na unyonywaji

Orodha ya Mwembe yanga anayo miaka mingi. Ni kutokana na sababu za kisheria hakuweza kuitaja.
Inashangaza aksema sababu za kisheria zinamzuia ili hali alijua hilo

Hakuwa na jipya, alitumia orodha ya Uswiss kama ‘sensational ad' ili watu wahudhurie mikutano na kujenga hoja anakubalika.

Bila hivyo, alijua mkuatano unaweza kuwa na watu 69 au 300, kati yao wakimzomea kwa abaguzi anayouchomeka nchini.

Hakuna jipya mwembeyanga, pengine la kuliangansha Shinyanga Arusha na Kilimanjaro ilikuwa jipya zaidi. Soma zaidi #1720
 
Inasemekana mwembeyanga, Zitto amegairi kutaja majina ya mafisadi wa mabilioni ya uswisi, je ni kweli? Kama ni kweli, kwanini tusiamini hoja ya Nguruvi3 bandiko #1745 ?
Waberoya, Mkandara, Ritz, Adharusi.
Hili swala la kuwataja wenye account Uswiss kusema kweli binafsi yangu sikufurahia hata kuahidi kuwataja kwa sababu hizi kelele za mlangoni kusema kweli haziwezi kutusaidia kitu. Akiwataja kama Dr.Slaa ingesaidia nini zaidi ya kutafuta umaarufu maanake tumeisha ona mifano huko nyuma kuwa serikali yetu haifuatilii kabisa maswala haya. Kama wangekuwa viongozi waliopo ama walopita hapo kidogo ninge shukuru kwa sababu unawaondolea kura za uchaguzi kwa wenye uchungu..

Niliposoma ile list nikakuta hakuna viongozi isipokuwa wafanyabiashara ambao kati yao sijui 95 na fedha zenyewe ni Millioni 113, kila mmoja ni millioni 1 na ushee, halafu hana hakika kama ni fedha haramu au laa sikufurahishwa na ahadi yake kabisa kwa sababu pale Bongo penyewe kuna watu wana acoount ya mamillioni na ziko benki zetu hawafuatiliwi kama wamelipa kodi stahiki, iweje hawa wanafanya biashara ambao huna hakika iwe issue kuba kiasi kile.

Pamoja na yote haya sioni sababu ya kuunganisha kutowataja wenye fedha Uswiss na mada hii ama alichosema Nguruvi3. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. hata sisi tunatetea haki zake tu na kwenye unyonge wake tutawapa ruksa ya kumnyonga.. Ila nanyi kubalini tunapowatundika kamba ya shngo msianze kulia tuanzishe mada nyingine..
 
Ili kuweka Rekodi Sawa hii ndiyo hotuba ya ZZK Mwembeyanga
Dar Es Salaam 04.07.2015

Ndugu Wanadar es salaam

Kwanza nianze kwa kutoa shukran kwa kuitikia wito wetu wa kujitokeza kwa wingi kuja kutusikiliza leo hii katika Viwanja hivi vya Mwembeyanga, TUNAWASHUKURU SANA.

Kwetu nyie mna umuhimu wa kipekee, maana mnatokea katika Jiji ambalo misingi ya ujenzi wa Taifa hili ilianzia, kuanzia kuasisiwa kwa Chama cha Tanganyika African Association mpaka harakati za Chama hicho cha Kijamii kurithiwa na Chama cha Siasa za TANU.

Siku zote historia inawaonyesha watu wa Dar es salaam kuwa ndio waasisi wa harakati hizi za siasa za kizalendo nchini. Kutokea nyakati zile za kina Mwalimu Nyerere, Bibi Titi Mohammed, kina Sykes, Dossa Aziz Ally, John Rupia na Zuberi Mtemvu mpaka leo bado wanadar es salaam mnao umuhimu wa kipekee katika siasa za nchi hii. Kwa kutambua umuhimu wenu huo, tumeona leo tufanye Mkutano huu Maalum viwanjani hapa ili kukitambulisha tena chama hiki kwenu, na pia kukikabidhi mikononi mwenu ili harakati hizi za kurudisha misingi ya Uzalendo wa Taifa hili mzishike nyie wenyewe waasisi wa harakati husika.

Na hili tunalolifanya leo si jambo geni kwenu, labda niwakumbushe tu, ni kwa huo umuhimu wenu Rais wetu wa kwanza na baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alijenga Utamaduni wa kuzungumza na Taifa juu ya mambo yote mazito ya nchi hii kupitia wazee wetu wa Jiji hili, utamaduni ambao umeendelea kurithiwa, nasi tunaona ni utamaduni mwema wa kuuendeleza. Japo sisi tunakwenda mbele zaidi, kwamba tumekuja kwenu Vijana, Wanawake na Wazee wetu wa Dar es salaam kuzungumza nanyi juu ya jambo hili zito, kukikabidhi kwenu chama chetu cha ACT Wazalendo.

Ndugu Wanadar es salaam

Tumewaiteni leo tukiwa na mambo Machache Muhimu kwa chama chetu na Taifa kwa ujumla ambayo tungependa kuyaeleza kwenu na kwa Umma wa Watanzania wenzetu kwa ujumla.

Kama mnakumbuka Machi 29 mwaka huu tulizindua chama chetu hapa jijini Dar es salaam na baada ya uzinduzi huo tulifanya ziara katika mikoa 22 na baadhi ya majimbo nchini, pia tokea wakati huo operesheni mbali mbali za chama zimekuwa zikifanyika wakati wote huo, ikiwa ni pamoja na kuzindua Azimio la Tabora – Tamko la Kimuongozo, Kiitikadi, Kisera na Kimaadli la Chama chetu ambalo limehuisha Azimio la Arusha. Tunawashuku sana wananchi wa Mikoa mbalimbali kwa mapokezi yao makubwa waliyotupa pamoja na kulipokea kwao kwa mikono miwili Azimio la Tabora.

Ndugu Wana-Dar es salaam

Tuna uchumi unaojenga Matabaka. Hivi sasa uchumi wetu umeshikwa na watu wachache hususan wafanyabiashara ambao pia wameshika siasa au kwa wao kushiriki kwenye siasa moja kwa moja au kufadhili wanasiasa wa kutetea maslahi yao.

Tuna kansa ya ufisadi ambapo watu hutumia nafasi zao za uongozi kujilimbikizia mali. Ufisadi ni tatizo zaidi la viongozi walioshika madaraka ya umma. Tunahuisha Azimio kwa lengo la kusimika miiko ya Uongozi wa Umma ambayo itakuwa msingi mkuu wa mapambano dhidi ya ufisadi.

Azimio la Tabora kwa kiasi kikubwa linakuja kuleta Mwarobaini wa Kimaadili juu ya suala husika, kwa kuwa linahuisha Azimio la Arusha kwa kurudisha miiko ya Uongozi na Utumishi wa Umma, na pia kujenga misingi ya uchumi wa Ujamaa wa kisasa utakaojikita katika kuongeza uzalishaji mali na ugawaji sawa wa keki ya Taifa na hivyo kupunguza matabaka nchini kwetu.

Ndugu Wanadar es salaam

Mtakumbuka kuwa Mwezi Novemba mwaka 2012 Bunge lilipitisha Azimio namba Tisa la Mwaka 2012 ambalo lilielekeza Serikali kufanya uchunguzi kuhusu Watanzania na makampuni ya kitanzania waliotorosha na kuficha fedha kwenye mabenki ughaibuni. Uchunguzi pia ulikuwa uhusike na Mali za Watanzania zilizopo nje ya nchi katika juhudi za kuhakikisha kuwa fedha chafu na ufichwaji wake vinakomeshwa. Bunge lilitoa muda wa miezi sita kwa Serikali kufanya uchunguzi huo. Mwaka mzima ulipita Serikali haikutoa maelezo yeyote na baada ya kubanwa ndani ya Bunge Serikali ikaomba miezi sita zaidi. Hata hivyo mpaka leo Serikali haijatoa kauli yeyote kuhusu taarifa hiyo ya uchunguzi.

Takwimu zinazohusu fedha za Watanzania nje ya nchi bado sio za uhakika sana. Kwa mfano, Taarifa ya Serikali ya kisiwa cha Jersey kilicho chini ya himaya ya Uingereza inaonyesha kuwa Fedha na Mali za Watanzania katika mabenki kisiwani humo ni paundi za Uingereza 440 milioni ambazo kwa bei ya sasa ni sawa na shilingi za kitanzania 1.4 trilioni. Vile vile taarifa rasmi ya Benki Kuu ya Uswiss inaonesha kuwa Watanzania wenye akaunti katika mabenki ya nchi hizo imefikia dola za kimarekani 304 milioni kutoka dola 213 milioni mwaka 2012. Hatuna takwimu kwa nchi nyingine duniani.

Fedha hizi zaweza kuwa halali ama haramu. Kuna watu ama ni Watanzania wanaishi ughaibuni na kufanya kazi huko ni lazima wawe na akaunti za benki. Pia kuna Watanzania ambao ni wafanyabiashara na masharti ya biashara zao ni lazima wawe na akaunti katika mabenki ya nje. Hata hivyo mfumo mzima wa ufunguaji na ufungaji wa akaunti katika mabenki ya nje umewekewa masharti ya kisheria na kibali cha Benki Kuu kinahitajika. Kuna Watanzania wenye kuficha fedha ambazo zimepatikana kwa rushwa na biashara haramu mbalimbali kama vile madawa ya kulevya na biashara ya nje ambayo haingii kwenye rekodi za Benki Kuu. Iwapo Serikali ingefanya uchunguzi na kuukamilisha tungeweza kujua kwa hakika katika orodha ya watu wenye akaunti nje ni wepi wana fedha zao halali na wepi wana fedha haramu. Serikali imetunyima haki hiyo kwa zaidi ya miaka miwili na nusu sasa. Bunge la Kumi linavunjwa mnamo tarehe 9 Julai mwaka huu na hakuna dalili yeyote ya Serikali kutoa taarifa ya uchunguzi ndani ya bunge kama ilivyoagizwa na Bunge.

Ndugu Wanadar es salaam

Mara baada ya Azimio la Bunge kutolewa mwaka 2012 nilipata mialiko kutoka sehemu mbalimbali za dunia kwenda kushirikiana nao katika jambo hili. Jambo hili sio changamoto ya Tanzania peke yake. Nchi mbalimbali duniani kama Marekani, India, Nigeria, Ujerumani nk zinahangaika na jambo hili. Kila nchi ilichukua hatua inavyoona yenyewe inafaa ili kukabiliana na suala hili. Hatua ya Tanzania kufanya uchunguzi kufuatia agizo la Bunge ilikuwa ni ya kipekee na wachunguzi wengi wa kimataifa wakashawishika kuwa Tanzania itakuwa nchi ya mfano katika kupambana na tatizo la utoroshwaji wa fedha na ukwepaji wa kodi.

Katika safari hizo mbalimbali nilizofanya duniani nilipata taarifa ambazo niliziwasilisha Serikalini kwa ajili ya kusaidia uchunguzi wetu. Jaji mmoja wa Mahakama ya Ufaransa ambaye anafanya uchunguzi dhidi ya Benki ya HSBC alinipa ushirikiano wa kutosha na taarifa muhimu ambazo niliziwasilisha Serikalini ili waweze kuchukua hatua. Serikali haijafanya kitu. Miongoni mwa taarifa hizo ni orodha ya Watanzania 99 wenye akaunti 288 katika tawi moja la Benki ya HSBC nchini Switzerland. Orodha hiyo niliiwasilisha kwa Gavana wa Benki Kuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya uchunguzi. Serikali mpaka sasa ninapozungumza nanyi haijatoa Taarifa licha ya kupewa kila aina ya ushirikiano.

Nimeamua leo kuiweka orodha hii wazi kama shinikizo kwa Serikali kutoa taarifa ya uchunguzi kabla ya Bunge kuvunjwa wiki ijayo. Kila mwandishi wa habari aliyepo kwenye mkutano huu nimempatia bahasha yenye majina 99 ya Watanzania au watu wenye mahusiano na Tanzania ambao wana akaunti HSBC ya Uswiss. Jumla ya akiba katika akaunti Benki hii pekee ni dola za kimarekani 114 milioni.

Narejea kusema kuwa sisi hatuna uhakika kama fedha hizi ni halali au haramu. Kuna ambazo zinahusiana na washirika 2 wa kashfa ya rada ambao ni Sailesh Vithlani aliyetuhumiwa kumhonga Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi na mmiliki wa kampuni ya Shivacom. Hizi zaweza kuhusishwa na ufisadi wa rada. Hata hivyo nyingine ni ngumu sana kusema zinatokana na nini kama vyombo vyetu vya uchunguzi vikiendelea kukalia kimya taarifa ya uchunguzi. Wito wangu ni kwa Serikali kuwasilisha taarifa ile Bungeni ili wenye fedha halali watofautishwe na wenye fedha haramu na wale wenye haramu wachukuliwe hatua kali za kisheria ikiwemo fedha hizo kurejeshwa nchini.

Ndugu Wanadar es salaam

Suala hili ni tone tu ya namna tatizo la kimaadili lilivyo kubwa nchini, na pia namna lilivyo na athari kisiasa na kiuchumi, ni suala ambalo kama Taifa tunapaswa kulitafutia dawa, Chama cha ACT Wazalendo tumewaletea dawa ya tatizo – Miiko ya Uongozi kama ilivyoainishwa katika katika Azimio la Tabora.

Ahsanteni sana.
 
Ahsante sana Gamba la Nyoka. Tulipouliza rekodi za Shinyangana Mwanza tuliletewa vipande na sihotuba nzima.
Na hadi leo tunatuhmiwa tu, washabiki hawana full text. Anyways tuendelee

Hapo juu umesema tuache intoxication ya Zphobia. Naona kamaupo nervous kidogo

Haonewi mtu na pia hahurumiwi hasa masilahi mapana ya taifa yanapoguswa

Tuendelee na mnakasha, haya yalikuwa by the way tu
 
Mkandara #17206 upo uhusiano wa mada na hotuba ya leo. Kiongozi mkuu wa ACT amezungumza kama chama.
Rejea 1720 na 1725

Mada inasema ACT ni mpiniwa kumaliza upinzani. Katika tarehe ya leo, fikra za wananchi ni kuondoa udhia wa miaka 50 kama si kudhibiti udhia huo kwa siku zaijazo.

Tumeona miswada ya dharura iliyolenga uchaguzi, sheria za mitandao, wapiga zumari(whistleblower)na mafuta na gesi zikikimbizwa. Tunajua ni silaha za uchaguzi.

Kwa mfano,sheria ya mafuta na gesi imelenga kutuliza hasira za wananchi wa kusini(Mtwarana Lindi) kwa kuwaambia ipo sheria kulinda masilahi yao. Vifungu zaidi ya 200 havitapitiwa kwa uyakinifu. Hilo ni danganya tu kwa ajili ya uchaguzi

Tumeona wabunge wakifukuzwa kwa kukataa kusimamia kanuni na masilahi ya nchi.
CCM wanataka kupitisha kila wanachotaka kwa masilahi yao si taifa

Katika nyakati hizi ambapo bunge lina siku 7 au chini, ni ujinga kudhani kuna hoja inayoweza kujadiliwa tena na kuzaa matunda. Hoja ya pesa za Uswiss ilikuwepo siku nyingi. Inashangaza kiongozi mkuu akiizungumza leo tukijua hakuna kitakachofanyika. Ni too little toolate.

Kwa maana hiyo kiongozi mkuu alikuwa anatafuta political stunt. Katika hilo anaondoa focus ya wananchi kuhusu uchaguzi mkuu. Anapunguza hoja muafaka kama hii ya kufukuzwa wabunge ambayo ni ushahidi wa ubabe wa CCM

Hadi hapo ACT inatumika kuondoa focus dhidi ya CCM ndiyo maana tunasema ni mpini wa kumaliza upinzani.
Huwezi kuchomeka hoja bila kuangalia nyakati.

Kwanini imefanyika hivyo, tafadhali rejea bandiko 1720 na 1725

Tunazidi kuona, hoja ya Shinyanga imeondoa focus na hii inazidi , kulikoni?

Kwanini ACT wanatoa nafuu kwa CCM ya namna hii? Kulikoni?

Tusemezane
 
He mara hii Zitto mwenye kulaumiwa kwa kusema Kilimanjaro kuinyonya shinyanga, eti anazungumzia na Kilimanjaro Kunyonywa pia.

je hii si ni ushahidi wa Wazi wa Zitto kutaka fair distribution ya keki ya taifa? na si issue ya ubaguzi?.

Tupe ufafanuzi hapo, kivipi unataka fair distribution na kwa vigezo vipi? tupe shule kwa uelewa wako..Lakini kabla ya hapo pata shule kutoka kwa Mchambuzi..

Umeona sasa mkuu Ritz, hii disparity sijui kwa nini Mchambuzi haioni. Kutokana na weakness katika taxation regime, ambapo kodi kutoka sehemu moja ya nchi zinakusanywa sehemu nyingine,ni vigumu kuchukulia kodi ya mahala pekee as an indicator ya sehemu hiyo ya kuchangia katika mapato ya serikali compared na sehemu nyinginezo.

Indicator nzuri zaidi, ni kutumia kipimo cha overall production of goods and services ya sehemu fulani kwa mwaka

The GDP disparity is obvious. But what are you trying to imply - that the GDP disparity is a result of weaknesses in taxation system?

Haujaeleweka vyema.

Indicator nzuri kufanya nini? Pia katika Hili haujaeleweka vyema.

Hakuna aliyesema tatizo ni Kodi na siyo GDP, Usiwalishe wana Ukumbi Maneno.

Again, Tatizo siyo Kilimanjaro kama mkoa na watu wake, Tatizo ni serikali isiyo Fair, ambayo ina mipango mibovu katika ugawaji wa pato la taifa, Serikali ambayo hapo juu Ritz amekuonyesha hata Mbunge wa Shinyanga akilalamika kuwa Serikali imeuacha nyuma mno huo mkoa ktk suala la afya na Elimu.

QUOTE=Alinda;13172595]
Gamba la Nyoka
tuko pamoja katika mjadala huu? Pato la Taifa linagawiwa na Serikali?? Hebu tupe ufafanuzi jinsi serikali inavyogawa pato la taifa..

Kama swala ni kuomba msamaha ili wanaukumbi tupate shule ya uhakika kutoka kwako.. Basi Gamba la Nyoka naomba msamaha kwa kutaka ufafanuzi wa neno Stahiki badala la Stahili.. Natumaini msamaha wangu umepokelewa.. Hivyo wanaduru tukae mkao mzuri shule yaja.. Haya Gamba la Nyoka uwanja ni wako...
Gamba la Nyoka natumaini utakuwa umeishapata sehemu tulivu ili tupate majibu/ufafanuzi wa maswali yetu.. Karibu Gamba la Nyoka..
 
Last edited by a moderator:
Kapwela bado nasubiri majibu ya haya maswali hapa chini.

Ukisoma andishi la Zitto anasema hivi """ Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa. """

Ukisoma hiyo sentensi utaona kuwa anashangaa kwanini Shinyanga iwe no. 4 katika kuchangia pato la Taifa.. na ni masikini wa kutupwa. Nafikirii kama kumbukumbu zangu ziko sawa ni ya 16 katika maendeleo.

Tukirudi katika andishi lake lingine anasema:
Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7."

Hapa anaendelea kuishangaa Kilimanjaro na Arusha mikoa ambayo inachangia no.7 na 9 lakini inamaendeleo zaidi. Kigezo anachotumia ni uchangiaji wa pato la Taifa.

Swali langu kako Je ni kweli kigezo cha maendeleo katika mikoa husika ni uchangiaji wa pato la taifa?

Na kama ndivyo vipi kuhusu Lindi?

Na je hayo maneno yake huoni yanajenga sintofahamu kuwa baadhi ya watu hasa sie tusio na ufahamu kuhsu uchumi. Maana kutoka na maelezo yake ndo limetokea lile kundi la watu linalosema "kuna baadhi ya mikoa mengine haipati stahiki ipasavyo (kama mkoa haupati stahiki yake ina maana kuna mkoa unaochukua hizo stahiki) ( Kwa bahati mbaya hata mie kabla ya shule ya Nguvuri3 Mchambuzi na wengio nilifikiri kuwa Shinyanga "inanyonywa" ) na ili kundi tulikuwa wengi)

Zitto ni msomi tena ni mchumi huoni kuwa alikuwa na wakati mzuri sana kuelezea hii hali kwa ufasaha kama alivyofanya Mchambuzi, na kutwambia chama chake kina mkakati gani kuhakikisha maeneo kama Shinyanga yanakuwa na maendeleo zaidi kama ilivyo mikoa mengine?

[/QUOTE]
 
Alinda,
Mimi nakuomba pitia haya maswali na majibu HAPA, yasome taratibu yakuingie kisha fikiria upya swali lako..
 
Mkandara , Gamba la Nyoka Mbona hojaza Alinda zipo wazi kabisa na hazihitaji maelezo marefu?

Alinda anauliza

Unfair distribution ya kekiya taifa ipoje wapi na inafanyikaje?

Kama Shinyanga haipatai ‘stahiki' au stahili, je haki yake inabaki au inakwenda wapi?

Je, pato la taifa linagawiwaje na serikali?

Je Kigezo cha maendeleo ya mkoa ni uchangiaji wa GDP?

Nyongeza ya hoja za Alinda

Mchambuzi alionyesha, Sumbawanga ina GDP kubwa kuliko Kigoma. Kigoma ina tax evenue kubwa kuliko Sumbawanga.

Gamba la Nyoka na Mkandara hili mnaliuzungumziaje mkifikiria kauli ya kiongozi mkuu ya kulinganisha mikoa?

Kama GDP ni indicator ya maendeleo kwa mujibu wa Gamba laNyoka, je anaeleza nini ukumbi kuhusu Lindi yenye GDP ndogo lakini ni ya 10 katika maendeleo?
 
Alinda,
Mimi nakuomba pitia haya maswali na majibu HAPA, yasome taratibu yakuingie kisha fikiria upya swali lako..
Mkandara,
Hiyo link inajadili dhana ya "economic growth", yani kasi ya kukua kwa uchumi. Ni PDF file ambalo Lina kurasa "98" za maswali ya multiple choice na majibu yake kwa mtindo wa jibu Ni "A", "B", "C" au "D". Ni content ambayo inaweza kuwa iliandaliwa Brazil, India, marekani, au nchi yoyote kwa nia ya kufundisha wanafunzi uchumi kwa nadharia, hasa economic growth, tena kwa mtindo wa multiple choice, wala sio discussion or analysis.Hii PDF file inatusaidia nini? Inajibu maswali gani humu?

Kwa kweli Huku Ni kuchanganyikiwa. Acheni ushabiki kwenye masuala nyeti Kama uchumi wa wananchi. Siasa hazina nafasi katika mijadala ya Aina hii. Kiongozi wenu mkuu aliteleza. Kwa pamoja tumsahihishe na tujenge mjadala wa kusaidia taifa.
 
Baada ya muda utasikia wanarudi na madai 'acheni chuki'' Tuliuliza chuki zi wapi, hakuna hoja
Tukiliuza tueleweshwe wanapotea ! Sasa hilo pdf sijui kama linajibu au linatetea hoja za kiongozi wao mkuu

Hoja zipo hapo waungwana, simameni mtetee rekodi bila tuhuma, na wala msionyeshe chuki
 
Mkandara,
Hiyo link inajadili dhana ya "economic growth", yani kasi ya kukua kwa uchumi. Ni PDF file ambalo Lina kurasa "98" za maswali ya multiple choice na majibu yake kwa mtindo wa jibu Ni "A", "B", "C" au "D". Ni content ambayo inaweza kuwa iliandaliwa Brazil, India, marekani, au nchi yoyote kwa nia ya kufundisha wanafunzi uchumi kwa nadharia, hasa economic growth, tena kwa mtindo wa multiple choice, wala sio discussion or analysis.Hii PDF file inatusaidia nini? Inajibu maswali gani humu?

Kwa kweli Huku Ni kuchanganyikiwa. Acheni ushabiki kwenye masuala nyeti Kama uchumi wa wananchi. Siasa hazina nafasi katika mijadala ya Aina hii. Kiongozi wenu mkuu aliteleza. Kwa pamoja tumsahihishe na tujenge mjadala wa kusaidia taifa.
Hata sikuelewi mkuu wangu unaposema hii link ni dhana! Kama ni dhana sasa tunachobishania hapa nini maana kila kitu ukikichukulia kuwa ni dhana ina maana hakuna Uhalisia wake.

Kwanza ungesoma swali la Alinda hapo juu kisha ukasoma nilichokiweka badala ya kuelezea vitu vya ajabu kabisa kuwa hii ni dhana halafu unasema ni somo la Uchumi kwa nadharia. Kuna kitu hapa duniani kisichokuwa nadharia hata afya yako ni nadharia unaweza pima mzima wa Afya na ukakatika usiku kwa kansa ya mapafu wakait huvuti sigara, Ila inaposema Sigara inasababisha Kansa usianze kupinga ati ni nadharia. Ukipanda mbegu za shamba la hekari 10 utategemea kuvuna magunia kadhaa hii ni dhana ambayo inatangulia mahala popote. Ukivuna kidogo ya ile dhana ndivyo kiuchumi hata GDP yenyewe ina Positive na Negative.. ndio dunia tuishio lakini haian maana tusielimike na uwezekano wa kuvuna ulichopanda.

Na Hivi, kuwepo kwa multiple choice ndiko kunabadilisha makuzi ya Uchumi au una maana gani? Swali linapokuwa na Multiple choice au isiwe jibu la swali ni moja tu, Wangweza kuweka swali hilo na kutoa jibu posipo Multiple choice kwa sababu link hiyo imeanza kwa kufundisha kisha ndio unatihaniwa na majibu. Maana ama sababu za kuweka multiple choice ni kutazama kama msomaji ama mtihaniwa ameelewa vizuri alichokisoma.

Nikiuliza 2+2 =? halafu nikaweka A.3, B 6, C22 na D. 4, haina maana nafundisha ila namtihani msomaji hata kama chini kuna jibu. Na mtihaniwa akajibu ni 3 ina maana huyu mtu haelewi hesabu anahitaji kuelimishwa kwa nini 2+2 inakuwa 4. Mara zote Multiple choice huwa mtego mzuri wa kutazama weredi wa mtihaniwa. Usitafute sababu za kubishana juu ya makuzi ya Uchumi yanaweza vipi kubadilisha matokeo.

Swala la Brazil, hivi unataka kunambia kwamba Makuzi ya Uchumi (economic growth) maadam link inajadili Brazil kwa dhana basi ingekuwa tofauti Tanzania? je unajua kwamba hizo namba zilizotumiwa ni dhana tu hakuna uhalisia kwa sababu huu ni mtihani haufuati uhalisia? Hata mahesabu naweza sema Gari linalokwenda kasi ya km 100 kwa saa, litachukua muda gani kufika mita 200 ni dhana maana gari linaweza kuzimika kabla haklijafika mita 100.

Mkuu haya maswali sio somo la kufundishia ila ni jinsi gani Uchumi unakua iwe mahala popote kwa sababu hata ukiwapa maswali hayo wasomi wa uchumi kwa nchi za Urusi, Uingereza, Tanzania, Kenya au Marekani wote majibu yao yatakuwa sawa kwa kutoa majibu yalowekwa hapo, na akiweka jibu tofauti atakuwa maekosea, sasa sielewi unachopinga hapa maana muda wote humu tunazungumzia makuzi ya Uchumi, na somo la Economics haijalishi kama unazungumzia nchi au kijiji majibu yake ni yale yale halafu leo unauliza inatusaidia nini?...
 
Alinda,
Mimi nakuomba pitia haya maswali na majibu HAPA, yasome taratibu yakuingie kisha fikiria upya swali lako..

Mkandara asante sana kwa hiyo link. Kwa vile sijaweza kupata muda wa kusoma pg zote, na kwa faida ya wasomaji (maana kinachoandikwa hapa si chetu tu bali kuna watu wanakuja na soma) basi maandam wewe umesoma yote tena kwa umakini ningepeda utupe ufafanuzi kuhusiana na ulichokisoma na maswali ya hapo juu yaani no.#1730 and 1731

Asante
 
Hata sikuelewi mkuu wangu unaposema hii link ni dhana! Kama ni dhana sasa tunachobishania hapa nini maana kila kitu ukikichukulia kuwa ni dhana ina maana hakuna Uhalisia wake.

Kwanza ungesoma swali la Alinda hapo juu kisha ukasoma nilichokiweka badala ya kuelezea vitu vya ajabu kabisa kuwa hii ni dhana halafu unasema ni somo la Uchumi kwa nadharia. Kuna kitu hapa duniani kisichokuwa nadharia hata afya yako ni nadharia unaweza pima mzima wa Afya na ukakatika usiku kwa kansa ya mapafu wakait huvuti sigara, Ila inaposema Sigara inasababisha Kansa usianze kupinga ati ni nadharia. Ukipanda mbegu za shamba la hekari 10 utategemea kuvuna magunia kadhaa hii ni dhana ambayo inatangulia mahala popote. Ukivuna kidogo ya ile dhana ndivyo kiuchumi hata GDP yenyewe ina Positive na Negative.. ndio dunia tuishio lakini haian maana tusielimike na uwezekano wa kuvuna ulichopanda.

Na Hivi, kuwepo kwa multiple choice ndiko kunabadilisha makuzi ya Uchumi au una maana gani? Swali linapokuwa na Multiple choice au isiwe jibu la swali ni moja tu, Wangweza kuweka swali hilo na kutoa jibu posipo Multiple choice kwa sababu link hiyo imeanza kwa kufundisha kisha ndio unatihaniwa na majibu. Maana ama sababu za kuweka multiple choice ni kutazama kama msomaji ama mtihaniwa ameelewa vizuri alichokisoma.

Nikiuliza 2+2 =? halafu nikaweka A.3, B 6, C22 na D. 4, haina maana nafundisha ila namtihani msomaji hata kama chini kuna jibu. Na mtihaniwa akajibu ni 3 ina maana huyu mtu haelewi hesabu anahitaji kuelimishwa kwa nini 2+2 inakuwa 4. Mara zote Multiple choice huwa mtego mzuri wa kutazama weredi wa mtihaniwa. Usitafute sababu za kubishana juu ya makuzi ya Uchumi yanaweza vipi kubadilisha matokeo.

Swala la Brazil, hivi unataka kunambia kwamba Makuzi ya Uchumi (economic growth) maadam link inajadili Brazil kwa dhana basi ingekuwa tofauti Tanzania? je unajua kwamba hizo namba zilizotumiwa ni dhana tu hakuna uhalisia kwa sababu huu ni mtihani haufuati uhalisia? Hata mahesabu naweza sema Gari linalokwenda kasi ya km 100 kwa saa, litachukua muda gani kufika mita 200 ni dhana maana gari linaweza kuzimika kabla haklijafika mita 100.

Mkuu haya maswali sio somo la kufundishia ila ni jinsi gani Uchumi unakua iwe mahala popote kwa sababu hata ukiwapa maswali hayo wasomi wa uchumi kwa nchi za Urusi, Uingereza, Tanzania, Kenya au Marekani wote majibu yao yatakuwa sawa kwa kutoa majibu yalowekwa hapo, na akiweka jibu tofauti atakuwa maekosea, sasa sielewi unachopinga hapa maana muda wote humu tunazungumzia makuzi ya Uchumi, na somo la Economics haijalishi kama unazungumzia nchi au kijiji majibu yake ni yale yale halafu leo unauliza inatusaidia nini?...
Mkandara,

Kwa uelewa wangu, dhana maana yake ni concept au kitu Kama hicho. Ulichowasilisha in PDF ni concept of economic growth, au sio Sawa?

Economic growth as a concept is based on models and theories of growth - kwa maana rahisi? Nadharia. Kwanini unakataa na Nini ngumu kuelewa hapo?
Hizi theories and models ndio huwa tested and applied to give us uelewa wa masuala husika ya kiuchumi in contemporary terms.

The PDF file you presented lengo la aliyelitayarisha ilikuwa ni aidha mtihani au somo kwa wanafunzi wa uchumi. Somo hapo ni dhana ya economic growth au kukua kwa uchumi. Presentation hiyo ya PDF haina discussion wala analysis, ni multiple choice questions, basi.

Mimi sikupinga dhana ya economic growth. Na sijapinga kwamba Kama lengo ni kujielimisha, lipo la kujifunza kwenye Hilo PDF file. Vile vile, kutaja kwangu Brazil, india etc maana yangu ilikuwa kwamba hili document linaweza kuwa limeandaliwa in any country kufundisha au kuwapa mtihani walengwa kuhusu dhana ya economic growth. In a global sense, pia the said knowledge applies anywhere where they are practicing neo liberal economics. I didn't dispute any of that.

Nachopinga ni kitendo Chako Cha kutafuta tu document ya uchumi kiholela holela na kuitupia humu kwa madai eti inajibu maswali ya alinda. Je, ulielewa maswali yake? Economic growth inayajibu vipi? How do the 98 questions and answers in the PDF answer maswali ya alinda?

Binafsi I don't see any meaningful relationship between maswali Yale na hiyo copy and paste yako. Otherwise Kwa nini usije na analysis and discussion badala ya copy and paste?
 
Last edited by a moderator:
Duh I thought this issue was dead and buried na nina hakika hata mhusika mwenyewe hawezi kuthubutu tena kurudia kauli kama hizo. Sasa hapa kinachoshangaza ni kwamba kama hata yeye inaonekana amekiri kukurupuka, mnaondeleza mjadala kwa kumtetea mnatakaje? Do you guys really believe that by so doing you are helping him out au ndio mnazidi kumtosa tu baharini kwenye mawimbi na upepo mkali? Kulikoni?

Oneni sasa alivyozidi kujidhalilisha juzi huko Mwembeyanga! Hivi tunapoilalamikia CCM kwamba imetekwa na mafisadi, kumbe ni hawa wafanya biashara wa Kiasia ndio culprits wetu! Je ni sera za hawa wafanya biashara ndio zinatekelezwa na serikali ya CCM! Kwamba ni hawa ndio wamesababisha mikoa mingine ibaki nyuma kimaendeleo kuliko mingine! Kwamba uongozi wa CCM na serikali yake uko mikononi mwa hawa Waasia!

Jamani tujaribu kuwa wa kweli kwa nafsi zetu, Supreme Leader anahitaji kuchukua time out apumzike kidogo ili aweze kupoa. Kwa vitendo vyake hivi utetezi wowote atakaoupata kutoka kwa mtu yeyote yule ndani ya taifa hili linalohitaji ukombozi hauwezi kuwa unasukumwa na uzalendo. Sijui safari hii lengo lake kuu lilikuwa ni nini lakini kwa vyovyote vile this was really bad timing UKAWA wakipigania maslahi ya taifa.
 
Mkandara,

Kwa uelewa wangu, dhana maana yake ni concept au kitu Kama hicho. Ulichowasilisha in PDF ni concept of economic growth, au sio Sawa?

Economic growth as a concept is based on models and theories of growth - kwa maana rahisi? Nadharia. Kwanini unakataa na Nini ngumu kuelewa hapo?
Hizi theories and models ndio huwa tested and applied to give us uelewa wa masuala husika ya kiuchumi in contemporary terms.

The PDF file you presented lengo la aliyelitayarisha ilikuwa ni aidha mtihani au somo kwa wanafunzi wa uchumi. Somo hapo ni dhana ya economic growth au kukua kwa uchumi. Presentation hiyo ya PDF haina discussion wala analysis, ni multiple choice questions, basi.

Mimi sikupinga dhana ya economic growth. Na sijapinga kwamba Kama lengo ni kujielimisha, lipo la kujifunza kwenye Hilo PDF file. Vile vile, kutaja kwangu Brazil, india etc maana yangu ilikuwa kwamba hili document linaweza kuwa limeandaliwa in any country kufundisha au kuwapa mtihani walengwa kuhusu dhana ya economic growth. In a global sense, pia the said knowledge applies anywhere where they are practicing neo liberal economics. I didn't dispute any of that.

Nachopinga ni kitendo Chako Cha kutafuta tu document ya uchumi kiholela holela na kuitupia humu kwa madai eti inajibu maswali ya alinda. Je, ulielewa maswali yake? Economic growth inayajibu vipi? How do the 98 questions and answers in the PDF answer maswali ya alinda?

Binafsi I don't see any meaningful relationship between maswali Yale na hiyo copy and paste yako. Otherwise Kwa nini usije na analysis and discussion badala ya copy and paste?
Mkuu, sio wewe ulokataa link hiyo ukisema haina maana yoyote kwa sababu ni dhana? sasa iweje tena useme Economics ni nadharia ambayo kumbe unakubaliana nayo? ndio maana nikakwambia kila kitu hapa duniani ni dhana iwe hata maisha yako mwenyewe, na nikakupa mifano ya 2+2 hadi mwendo wa gari. Equation yoyote inajibiwa kama ilviyo.

Unachopinga ni mimi kutafuta document ya Uchumi kiholela? ndio nini kiholela ikiwa hukusoma swali la Alinda ambalo majibu yake yapo katika link hiyo kwa sababu aliuliza swali hili:- Je ni kweli kigezo cha maendeleo katika mikoa husika ni uchangiaji wa pato la taifa?

Swali la tatu linauliza hivi:- 3) We are interested in long-term growth primarily because it bringsA) higher price levels.B) lower price levels.C) higher standards of living.D) trade wars with our trading partners. Answer: C

Mnachotaka nyie kusema ni kwamba kupanda mbegu haina maana utavuna zaidi na hata ukipata mavuno zaidi haina maana ndio utaendelea kwa sababu hizi ni dhana tu. Mnachojaribu kupinga ni kuhusisha GDP na maendeleo ya nchi ama Mkoa, jambo ambalo wachumi wote duniani wanaafiki isipokuwa nyie tu.

Hiii hii Tanzania yetu Uchumi wake umekuwa sana tu kutokana na uwekezaji mkubwa ulofanyika miaka ya nyuma na muda wote GDP halisi imepanda na ilitegemewa kuwepo na maendeleo makubwa lakini maendeleo hayo hayakuwafikia wananchi ina maana kuna mapungufu fulani. Maendeleo yetu yamejenga madaraja ya walokua nacho wa wasokuwa nacho, na wala sio kosa la walokuwa nacho bali mfumo uliopo. Vivyo hivyo sisi tunasema kwa udogo wake tunaitazama Shinyanga kwa sababu maendeleo ya nchi ama ujenzi wa nchi unaanzia chini. Kama mikoa yetu haiwezi kuwa mfano bora wa maendeleo yatokanayo na makuzi ya uchumi ina maana kuna mapungufu makubwa ya kimfumo.

Alinda,
Juu ya fikra za kwamba mkoa haupati stahiki nimeshakwambia mara mia kidogo ya kuwa ikiwa wewe hupewi mshahara stahiki haina maana unamshitakia Mchambuzi unayefanya naye kazi ndiye kachukua chako kwa sababu analipwa zaidi yako, hapana - Unacholalamikia ni kulipwa haki yako wewe kwa kazi uloifanya na kuwepo mfumo bora unaotazama uzalishaji. Sasa wewe ukianza kusema unapunjwa mshahara kwa sababu wewe ni mwanamke hapo tena itakuwa hoja ya Uwezekano wa shirika kutumia mfumo huo wa kulipa mishahara midogo wanawake bila kujali uzalishaji wao, bado hii haina maana unamshtaki Mchambuzi kachukua stahiki yako bali policies za shirika lenyewe ndizo kandamizi. Huna ugonvi na wanaume bali unatumia kigezo cha wanaume kuonyesha what they get paid na wewe unalipwa nini..

Kwa Kuelewa huko ndio maana napingana nanyi juu ya maelezo ya Zitto.
 
Back
Top Bottom