Mkandara,
Kama alivyojadili
Mwalimu,
Alinda,
Nguruvi3, Mwakalinga na wengine, mkakati wako umekuwa katika derailing hoja Ya msingi ili mpate fursa Ya Kukwepa maswali ambayo bado Hamna majibu. Wenzako kwa maana Ya walio upande wa hoja, Akina
Ritz,
Adharusi,
Waberoya, wamekimbia. Sana sana wanachungulia thread na wanakuja na "like" kwa post za ovyo zisizojibu hoja, au kusingizia kwamba takwimu wanazo Lakini Wapo kibiti na laptop wameacha msoga. Tunaelewa kwamba hiyo ni lugha Ya kistaarabu kusema kwamba hoja zimewalemea.
Tumeuliza kuhusu takwimu za Zitto katika ziara Zake, Hamna majibu. Tumeuliza kwanini ukawa wamkubali Msaliti Zitto, tumeambiwa kwamba hana nia Ya kujiunga ukawa badala yake anatafuta namna Ya kupata upendo wa kugeuza kibao kwamba alitaka kujiunga na ukawa Lakini ukawa umemgomea. Hii ni tafsiri nyepesi kabisa kwa hoja yako mkandara.
Mkilemewa na hoja, mnakuja na hoja za kumfananisha Zitto na Mbowe et al. As if Mbowe, Slaa ndio Chadema. Kama hawa wangekuwa Chadema, Iringa, Dsm, Singida, mwanza, etc wasingeunga Mkono Chadema. Chadema inazidi kuimarika kama taasisi na ndio maana kiongozi kama Zitto kutokea Kigoma alifanikiwa sana ndani ya Chama hiki. Usaliti ndio umemwangusha. Anatumika, anatumika, anatumika. Tumejenga hoja juu Ya hilo, hamjibu hoja.
Unamwalika lowassa wa CCM kujiunga na ACT Wazalendo, kwa maana gani? Unaunga mkono hoja ya Chenge bungeni kuwatetea mafisadi ndani ya CCM dhidi ya escrow kwa maana gani? Unalalamika kwamba Chadema haikuwa na demokrasia, halafu unaenda kuiba Chama cha watu ACT Tanzania na kujipachika usultani Kwa maana gani?
Unaita ukawa wasaka tonge, una washutumu kwamba wana nia Ya kuvunja muungano, halafu unasema upo tayari kujiunga nao kwa maana gani? Hapo ni Baada Ya mwenyekiti Anna kutamka kwamba kufanya hivyo ni usaliti kwa mujibu wa katiba Ya ACT Wazalendo, huku mkandara akisema kwamba Zitto analaghai wananchi, hana nia ya dhati kujiunga na ukawa.
Zitto anadai kwamba ACT ni Chama kinachotaka kurudisha Azimio la Arusha Na misingi yake, Akasema kwamba anataka kuvaa viatu vya Nyerere, tukahoji hatua kwa hatua anatosha vipi kivigezo? Hamna majibu zaidi Ya Kuja na comparative analysis Ya Zitto na Slaa, Mbowe.
Mkuu, Chadema kama upinzani umepiga hatua kubwa. Hata Slaa na Mbowe wakiamua kuacha Siasa, ACT na CCM hawawezi tena kupambana na Chadema kwa hoja. Chadema sasa ni Chama cha kitaasisi na ni Chama ambacho wananchi wengi wameamua kukikubalia kama Tumaini Lao, angalau kwa sasa. Hata wana CCM wenye kuweka maslahi Ya taifa mbele wanaona hilo mchana kweupe. Lakini nyie, kila kitu Chadema "safi" kasoro uwepo wa Zitto.