Nianze na Swala la
JokaKuu kuhusu Lindi kuwa mkoa wa 10 kimaendeleo. Nafikiri kinachofanya Lindi kuendelea zaidi ya Shinyanga ni kilimo cha Korosho na Ufuta, Utaona kuwa kilimo cha korosho/ufuta kinachangia ukuaji wa maendeleo katika mkoa husika kwa sababu wakulima wanapouza mazao yao ulipwe wao hivyo kufanya wananchi wa maeneo hayo kuwa na pesa mfukoni za kujiletea maendelo wao kama wao. Na kipindi hiki cha mavuno mzunguko wa hela kuwa mzuri kiasi ambacho hufanya hata biashara kwenza vizuri,tunavyofahamu kama biashara inakwenda vizuri inamaana na viwanda vya kutengeneza hizo bidhaa vitapata order nyingi, kama order zinaongezeka inamaana wafanyakazi kufanya "overtime" /au kuajiri wafanyakazi zaidi kama wafanyakazi wakifanya muda waziada inamaana na wao pesa inaongezeka mifukoni mwao/wakiajiri watu inamaana unakuwa na watu wachache wasio na kazi, mtu akiwa na pesa ni rahisi kuchangia maendeleo kuliko asiye na kitu mfukoni. Na serikali upata kodi zaidi..
Tukija kwa Shinyanga ingawaje wao wanautajiri mkubwa tena kuzidi watu wa Lindi, lakini utajiri walionao hawanufahishi wao unamnufaisha zaidi "mgeni" ambayo ni makampuni ya kingeni na kuuacha mkoa wa Shinyanga masikini wa kutupwa.. Hii yote ni uzembe wa viongozi wetu na ufinyu wa "maono" wa viongozi wetu,
Nasema hivyo kwanini? Kwa sababu ukiangali ubinafsishaji wa migoni ni kitu ambacho kama taifa hatukujiaandaa.
Hatukujiandaa kivipi? Hatukujianda si kwa upande wa wataalumu tu bali hatukujiandaa kupokea wageni ambao wangeingia katika mkoa wa Shinyanga.. Viongozi walifahamu kuwa tunapokwenda kubinafsisha tunakwenda kuwa na wageni wa mataifa mbali mbali ,watanzania kutoka kila sehemu, hivyo hawa hawa watu wanahitaji vitu muhimu ili kuhufanya huu mkoa kupata vichecho vya maendeleo si kutonana na kodi ya malighafi tu, bali hata pesa ya hawa wageni kuangalia uwezekano kuwa stahiki zao wanazolipwa zinabaki hapa hapa nchini.
Sasa basi swali lili ni vipi tutahakikisha pesa za hawa wageni zinabiki hapa nchini?
Serikali ilikuwa na wajibu kushawishi wafanyabaishara kuwekeza katika huu mkoa pale ambapo wangejenga mahotel, kumbi za mikutano/starehe,kujenga "arpatments, kujenga mashule,kujenga vyuo vya "mineral resource ili wafanyakazi kuweza kujiendeleza wakati huo huo anafanya kazi,kujenga barabara ili iwe rahisi kusafirisha bidhaa kama vyakula vinywaji na nk.. kuelemisha wakulima wafugaji juu vya kilimo cha kisasa na vyakula vyenye ubora, hivyo hivyo kwa wakulima kufunga mifugo yenye ubora,. Kuwabana "Foreigners" kulipwa mashahara yao hapa hapa nchi, kuhakikisha hatuajiri wageni hali watu wetu wanaweza kufanya hiyo kazi, kufungua vyuo vya lugha na kuwabana hawa watu kabla hujaanza kazi ni lazima ujifunze lugha, mila na desturi walao 4wks na kn. Kama taifa tungefanya hivi nafahamu kuwa leo tungekuwa kunaonge vitu vingine kuhusu Shinyanga.
Lakini Taifa la watu wa kusadikikika waliacha kila kitu mikononi mwa foreigners, Nitatoa ushuhuda kidogo kuhsu "Bulyanhulu" Kwanza walichofanya hawa wawekezeji walichukua eneo, wakajenga Camps kwa watu wao (na kampuni iliyokuwa inashughulika na malazi ikuwa ni kampuni kutoka Ufarasa) Wakatafuta kampuni nyingine kwa ajili ya chakula na vinywaji yaani ndani ya Camp kulikuwa (kwa wakati huo kwa sasa sijui) kulikuwa na bar, vyakula kuanzia chai asubuhi, chakula cha mchana, chakula cha jioni, Juice mbali mbali na aina zote, matunda mbali mbali na ya aina zote wafamyakzi waliokuwa wanaishi ndani walikula na kunywa bure kasoro pombe tu ndo ulinunua (Yaani Barrick ilipia fanyakazi wao chakula malazi) lakni cha ajabu hakuna chakula cha aina yoyote ile kilichotoka in our county. Kila kitu kilitoka South afrika, Ndege ilitoka SA na kutua Kahama, hivi vyakula havikutozwa ushuru au havikukaguliwa..
Hawa watu walitaka kufanya utalii hapa nchini, lakini kulikuwa hatuna ofisi za kupata information, walitaka kuleta familia zao lakini kulikuwa hakuna hotel ya maana ya kuleta familia, walitaka kuenjoy weekend ziwa vicotoria lakini kulikuwa hakuna info mbali mbali, yaani utafikiri "kulivurumumshwa katika swala zima la uwekezaji..
Lakini kama tungejiandaa basi wakulima wetu wangeweza kulisha "Bulyahulu", hizo camps zilizojengwa na wafarasa zingeweza kujengwa na watanzania, kama tungejenga apartment basi wafanyakazi wangeweza kuleta familia zao na kuspend pesa nyingi pale badala ile ya kila baada ya siku 70 watu wanarudi makwao na kupeleka pesa zote huku, kama kutungewabana wa "wazungu kabla kuanza kazi kuchukua kozi ya kiswali, kujifunza mila na desturi zetu, basi tungeongeza ajira zetu, kama tungejenga chuo mkoani shinyanga basi watu wetu angeweza kufanya kazi na kwenda shule hivyo kupunguza kuwaajiri wageni ambao wananufaisha mataifa yao na nk. Na kama hayo yote yangefanyika leo hii tungekuwa tunaongea utajiri wa wanashinyanga kuliko umasikini wa wanashinyanga.
Sasa hayo yote ni tisa kumi ni kosa ile ile tulilofanyika Shinyanga ndolo tunakwenda kufanya tena Mtwara, na baada ya hapo atakuja tena Zitto na kutwambia tena kuwa Mtwara inachangia ikiwa ya 1 katika pato la taifa lakini ya mwisho katika maendeleo hali Arusha ni 7 kimaendeleo..Sasa hapa kama kuna ukweli au ni kutaka kuchonganisha watu ilo ninamwachia nyie..