Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Ni wakati sasa tuyaweke maelezo haya katika 'simple terms' zinazoeleweka na wengi.

Na si kutafsiri tu, bali pia tueleze uhusiano uliopo kati ya Mikoa inayochangia pato la taifa (Dar, Mwanza, Shinyanga, Iringa) kwa mujibu wa wale wanaotetea hoja za supreme, na uhusiano wa maendeleo katika mikoa ya Dar, Arusha, Kilimanjaro. Tuangalie pia ni namna gani sehemu moja inaweza kukwaza nyingine


Yaliyojadiliwa

Kuna mambo tumeyaongea.
Nguruvi3 aliongelea uhusiano kati ya umasikini na elimu.

Mchambuzi akaongelea population growth rate akieleza jinsi family planning inavyochangia kurudisha watu nyuma

JokaKuu akongelea hoja ya mwisho ya UN kuhusu ukweli kuwa hakuna mantiki ya kuzuia sehemu moja kwa ajili ya nyongine akionyesha kuwa maeneo ya nchi yetu hakuna eneo lilovuta jingine nyuma

Alinda akaomba sana uhusiano wa kuchangia pato, mgawanyo wa pato na maendeleo.

Tuendelee


Kuhusiana na hoja yako ya umasikini na elimu. Hii hoja haina nguvu sana. Hiyo ilitolewa kutafuta njia ya mkato ya kutafuta maendeleo. Waliotoa hoja hii walidai kuwa ukiwapa watu elimu, watatumia elimu kuondoa umasikini. Huu umekuwa wimbo na watu tunaamini bila kufikiri nini chanzo cha maendeleo.

Jamii inapotaka maendeleo ni lazima iwe na Economic engines ambazo zinaweza ku-sustain social services, mojawapo ikiwa ni utoaji wa elimu. Kilimo cha kahawa kilikuwa ni engine ya waendeleo kilichosaidia kunyanyua maendeleo ya mkoa wa kilimanjaro. Na kilimo kilisaidia zaidi kwa sababu uzalishaji na mzunguko wa mapato ulikuwa chini ya wananchi.

Tukirudi kwenye mkoa wa Shinyinga, pamoja na kuwa inatoa mchango mkubwa, shughuli nyingi hazipo mikononi mwa mwananchi. Kwa mfano Shinyanga inaweza kuwa na makampuni ya kimataifa ya kuchimba madini. Lakini kutokana na matumizi ya technologia, kampuni hizo zinaweza kufanya kazi zake bila kuajiri watu wanaoishi Shinyanga. Matokeo yake ni kuwa hizo kampuni sio chachu au engine za maendeleo kwa watu wa Shinyanga.

Tukiachana na ubishi kwa sababu unamuhusu Zitto. Ukweli wa mambo, hakuna hata mkoa mmoja Tanzania unaoweza kujinyanyua wenyewe kielimu kwa wazazi kutegemea bajeti ya elimu kutoka serikali kuu.

Kitu kimoja kikubwa kwa sisi watanzania tunachoweza kuiga kutoka kwa wachagga ni kuwa na economic engines ni muhimu kwa maendeleo ya jamii. Watu wakiwa na economic engines watawapeleka watoto wao shule na umuhimu wa elimu utakuwepo.
 
Mkuu Nguruvi3.

Wala mimi sijisikii vibaya kwa chochote dhidi ya Pro-Chadema na Bavicha kunitukana mimi nimeishakuwa sugu na matusi ya Bavicha ukinitajia huyo mfuasi wako zumbemkuu sidhani kama anaweza kuja na matusi mapya dhidi yangu.

Nampa offer serous akija na matusi mapya nampa zawadi ya dollar 100.

Najua mkuu wewe ndiyo supreme leader wa ili jukwaa tuvumiliane tu mimi sugu wa matusi.

Tuendelee na ACT Mpini...

Mkuu niwie radhi, hili jukwaa sijawahi kukuita lumumba buku 7fc au vyovyote vile, jukwaa hili halina ushabiki wa vyama zaidi ya hoja tu, ukiona hoja haikutoshi ni kunyamaza na kuwasoma wengine, lugha unayotumia ni ya jukwaa la siasa, humu watu wanatambuana kwa hoja na sio lugha kama pro chadema au bavicha, huo ni utomvu wa nidhamu kwa jukwaa hili, jifunze kwa watu kama mkandala na wengine.
Mjadala unakupwaya huu, ndo maana kila mara unakuja na nukuu za facebook na tweeter ulizo'edit ili kuvuruga mjadala,
 
Last edited by a moderator:
Mkuu niwie radhi, hili jukwaa sijawahi kukuita lumumba buku 7fc au vyovyote vile, jukwaa hili halina ushabiki wa vyama zaidi ya hoja tu, ukiona hoja haikutoshi ni kunyamaza na kuwasoma wengine, lugha unayotumia ni ya jukwaa la siasa, humu watu wanatambuana kwa hoja na sio lugha kama pro chadema au bavicha, huo ni utomvu wa nidhamu kwa jukwaa hili, jifunze kwa watu kama mkandala na wengine.
Mjadala unakupwaya huu, ndo maana kila mara unakuja na nukuu za facebook na tweeter ulizo'edit ili kuvuruga mjadala,
Tatizo lako wewe roho inakuuma sana mimi ninapo wajibu mabwana zako.

Sisi kuitwa wafuasi wa Zitto sawa lakini nyie kuambiwa pro-Chadema mnakasirika.

Mkuu mbona wewe hatuoni mchango wako wowote kwenye hii mada zaidi ya kubeba mikoba ya mabwana zako, naona umeamua kujipa majukumu ya Moderate.

Najua unaumia sana kunisoma lakini vumilia JF siyo mali ya Chadema. Nimecheka sana unataka kunipangia cha kuandika sisi ndiyo tunafanya mjadala unakuwa na changamoto, kama navuruga mjadala niripoti kwa Mods nichukuliwe hatua kupingana na hoja za mabwana zako ndiyo kuharibu mjadala? Nguruvi3 kumtukana Mkandara ulikuwa wapi kusema anaharibu mjadala unampaka mafuta Mkandara siyo.

Kamanda nivulimie tu hamna namna ingine kama haupendi michango yangu pita mbali tu au usinisome.
 
Last edited by a moderator:
Ritz acha upuuzi wako, sijui una maana gani kudai nimetengeneza maneno yangu, nimenukuu maneno yako word for word! Soma tena niliyoyaandika kama hayamo kwenye post yako. Halafu hii ya kusema sisi ni wana Chadema ni muendelezo tu wa upuuzi wenu; mimi naunga mkono msimamo wa Chadema lakini sijawahi hata kukutana na kiongozi wao hata moja, nasoma na kufuatilia tu harakati zao katika kuwaelimisha wananchi juu ya chama cha kilaghai cha CCM na kitoto chake ACT...I dont even know which is which!

Hayo maneno unayodai source, naomba utafute gazeti la Mwananchi la Februari, 2010 wakimhoji Zitto...sina hakika ni tarehe gani au ukipenda fukua humu JF, tuliuongelea sana uropokaji wakati huo. Nitatafuta reference nikuletee, kumbuka JF inatunza kumbu kumbu na kama mtu aliwahi kuropoka hovyo huko nyuma, imetoka hiyo, haifutiki. Najua kuna mbinu zimefanywa watu kujaribu kurekebisha, kusahihisha na hata kufuta kauli zao za awali huko nyuma; kisiki ni kwamba iwapo kuna watu walishakunukuu hata ukirekebisha ulichoandika, juhudi zako ni bure.

Nitajie Mbunge aliyewahi kuandikiwa barua kutoka majimbo mbali mbali akiombwa agombee majimbo zaidi ya moja.
Kukwambia ukweli unanitukana mimi sugu wa matusi, mkuu tuwekee link au maadishi ya maneno ya Zitto siyo kujiandikia tu kisha unataka tumeze Hapana watameza pro-Chadema wenzako ambao hawana uwezo wa kuhoji.
 
Last edited by a moderator:
Kukwambia ukweli unanitukana mimi sugu wa matusi, mkuu tuwekee link au maadishi ya maneno ya Zitto siyo kujiandikia tu kisha unataka tumeze Hapana watameza pro-Chadema wenzako ambao hawana uwezo wa kuhoji.

Wewe uliweka link?
Kweli ujinga ni mzigo, mkuu cheki tena halmashauri yako ya kichwa kama ipo sawa. Sishangai ukisema wewe ni sugu wa matusi, hahaha, chongolo bwana
 
Last edited by a moderator:
Tatizo lako wewe roho inakuuma sana mimi ninapo wajibu mabwana zako.

Sisi kuitwa wafuasi wa Zitto sawa lakini nyie kuambiwa pro-Chadema mnakasirika.

Mkuu mbona wewe hatuoni mchango wako wowote kwenye hii mada zaidi ya kubeba mikoba ya mabwana zako, naona umeamua kujipa majukumu ya Moderate.

Najua unaumia sana kunisoma lakini vumilia JF siyo mali ya Chadema. Nimecheka sana unataka kunipangia cha kuandika sisi ndiyo tunafanya mjadala unakuwa na changamoto, kama navuruga mjadala niripoti kwa Mods nichukuliwe hatua kupingana na hoja za mabwana zako ndiyo kuharibu mjadala? Nguruvi3 kumtukana Mkandara ulikuwa wapi kusema anaharibu mjadala unampaka mafuta Mkandara siyo.

Kamanda nivulimie tu hamna namna ingine kama haupendi michango yangu pita mbali tu au usinisome.

Mkuu mchango wangu utafute humu kuanzia mwanzo wa mjadala,
Bilashaka umenielewa Mr. Sugu wa matusi
 
Last edited by a moderator:
Wewe uliweka link?
Kweli ujinga ni mzigo, mkuu cheki tena halmashauri yako ya kichwa kama ipo sawa. Sishangai ukisema wewe ni sugu wa matusi, hahaha, chongolo bwana
Huu ndiyo mchango wako nimekubali upo vizuri sana Wanaukumbi wanakusoma.
 
Nianze na Swala la JokaKuu kuhusu Lindi kuwa mkoa wa 10 kimaendeleo. Nafikiri kinachofanya Lindi kuendelea zaidi ya Shinyanga ni kilimo cha Korosho na Ufuta, Utaona kuwa kilimo cha korosho/ufuta kinachangia ukuaji wa maendeleo katika mkoa husika kwa sababu wakulima wanapouza mazao yao ulipwe wao hivyo kufanya wananchi wa maeneo hayo kuwa na pesa mfukoni za kujiletea maendelo wao kama wao. Na kipindi hiki cha mavuno mzunguko wa hela kuwa mzuri kiasi ambacho hufanya hata biashara kwenza vizuri,tunavyofahamu kama biashara inakwenda vizuri inamaana na viwanda vya kutengeneza hizo bidhaa vitapata order nyingi, kama order zinaongezeka inamaana wafanyakazi kufanya "overtime" /au kuajiri wafanyakazi zaidi kama wafanyakazi wakifanya muda waziada inamaana na wao pesa inaongezeka mifukoni mwao/wakiajiri watu inamaana unakuwa na watu wachache wasio na kazi, mtu akiwa na pesa ni rahisi kuchangia maendeleo kuliko asiye na kitu mfukoni. Na serikali upata kodi zaidi..

Tukija kwa Shinyanga ingawaje wao wanautajiri mkubwa tena kuzidi watu wa Lindi, lakini utajiri walionao hawanufahishi wao unamnufaisha zaidi "mgeni" ambayo ni makampuni ya kingeni na kuuacha mkoa wa Shinyanga masikini wa kutupwa.. Hii yote ni uzembe wa viongozi wetu na ufinyu wa "maono" wa viongozi wetu,
Nasema hivyo kwanini? Kwa sababu ukiangali ubinafsishaji wa migoni ni kitu ambacho kama taifa hatukujiaandaa.

Hatukujiandaa kivipi? Hatukujianda si kwa upande wa wataalumu tu bali hatukujiandaa kupokea wageni ambao wangeingia katika mkoa wa Shinyanga.. Viongozi walifahamu kuwa tunapokwenda kubinafsisha tunakwenda kuwa na wageni wa mataifa mbali mbali ,watanzania kutoka kila sehemu, hivyo hawa hawa watu wanahitaji vitu muhimu ili kuhufanya huu mkoa kupata vichecho vya maendeleo si kutonana na kodi ya malighafi tu, bali hata pesa ya hawa wageni kuangalia uwezekano kuwa stahiki zao wanazolipwa zinabaki hapa hapa nchini.

Sasa basi swali lili ni vipi tutahakikisha pesa za hawa wageni zinabiki hapa nchini?

Serikali ilikuwa na wajibu kushawishi wafanyabaishara kuwekeza katika huu mkoa pale ambapo wangejenga mahotel, kumbi za mikutano/starehe,kujenga "arpatments, kujenga mashule,kujenga vyuo vya "mineral resource ili wafanyakazi kuweza kujiendeleza wakati huo huo anafanya kazi,kujenga barabara ili iwe rahisi kusafirisha bidhaa kama vyakula vinywaji na nk.. kuelemisha wakulima wafugaji juu vya kilimo cha kisasa na vyakula vyenye ubora, hivyo hivyo kwa wakulima kufunga mifugo yenye ubora,. Kuwabana "Foreigners" kulipwa mashahara yao hapa hapa nchi, kuhakikisha hatuajiri wageni hali watu wetu wanaweza kufanya hiyo kazi, kufungua vyuo vya lugha na kuwabana hawa watu kabla hujaanza kazi ni lazima ujifunze lugha, mila na desturi walao 4wks na kn. Kama taifa tungefanya hivi nafahamu kuwa leo tungekuwa kunaonge vitu vingine kuhusu Shinyanga.

Lakini Taifa la watu wa kusadikikika waliacha kila kitu mikononi mwa foreigners, Nitatoa ushuhuda kidogo kuhsu "Bulyanhulu" Kwanza walichofanya hawa wawekezeji walichukua eneo, wakajenga Camps kwa watu wao (na kampuni iliyokuwa inashughulika na malazi ikuwa ni kampuni kutoka Ufarasa) Wakatafuta kampuni nyingine kwa ajili ya chakula na vinywaji yaani ndani ya Camp kulikuwa (kwa wakati huo kwa sasa sijui) kulikuwa na bar, vyakula kuanzia chai asubuhi, chakula cha mchana, chakula cha jioni, Juice mbali mbali na aina zote, matunda mbali mbali na ya aina zote wafamyakzi waliokuwa wanaishi ndani walikula na kunywa bure kasoro pombe tu ndo ulinunua (Yaani Barrick ilipia fanyakazi wao chakula malazi) lakni cha ajabu hakuna chakula cha aina yoyote ile kilichotoka in our county. Kila kitu kilitoka South afrika, Ndege ilitoka SA na kutua Kahama, hivi vyakula havikutozwa ushuru au havikukaguliwa..

Hawa watu walitaka kufanya utalii hapa nchini, lakini kulikuwa hatuna ofisi za kupata information, walitaka kuleta familia zao lakini kulikuwa hakuna hotel ya maana ya kuleta familia, walitaka kuenjoy weekend ziwa vicotoria lakini kulikuwa hakuna info mbali mbali, yaani utafikiri "kulivurumumshwa katika swala zima la uwekezaji..

Lakini kama tungejiandaa basi wakulima wetu wangeweza kulisha "Bulyahulu", hizo camps zilizojengwa na wafarasa zingeweza kujengwa na watanzania, kama tungejenga apartment basi wafanyakazi wangeweza kuleta familia zao na kuspend pesa nyingi pale badala ile ya kila baada ya siku 70 watu wanarudi makwao na kupeleka pesa zote huku, kama kutungewabana wa "wazungu kabla kuanza kazi kuchukua kozi ya kiswali, kujifunza mila na desturi zetu, basi tungeongeza ajira zetu, kama tungejenga chuo mkoani shinyanga basi watu wetu angeweza kufanya kazi na kwenda shule hivyo kupunguza kuwaajiri wageni ambao wananufaisha mataifa yao na nk. Na kama hayo yote yangefanyika leo hii tungekuwa tunaongea utajiri wa wanashinyanga kuliko umasikini wa wanashinyanga.

Sasa hayo yote ni tisa kumi ni kosa ile ile tulilofanyika Shinyanga ndolo tunakwenda kufanya tena Mtwara, na baada ya hapo atakuja tena Zitto na kutwambia tena kuwa Mtwara inachangia ikiwa ya 1 katika pato la taifa lakini ya mwisho katika maendeleo hali Arusha ni 7 kimaendeleo..Sasa hapa kama kuna ukweli au ni kutaka kuchonganisha watu ilo ninamwachia nyie..
 
Last edited by a moderator:
Niende tena kwa Zakumi ulisema kuwa kwanini wachagga hawachangii maendeleo ya wasukuma na nk..

Sijui hapa ulisema kuchangia maendeleo wa jinsi gani.. Ila ninavyoelewa ni kuwa kila mtanzania ambaye ni mfanyakazi, mfanyabiashara, mkulima au mfugaji anawajibu wa kulipa kodi, na Serikali yake ambayo inakusanya hizi kodi inawajibu wa kuwaletea wananchi wake huduma ambazo zitafanya kuwa kichocheo cha wananchi wa eneo husika kujiletea maendeleo.

Ni wajibu wa serikali inayokusanya kodi, kujenga barabara, kujenga mashule,kujenga vyuo, kutengeneza ajira kwa waitimu wake,kujenga mahospital, kuleta umeme, kuvuta maji na nk. Pale serikali inaposhindwa kupeleka hivi vitu katika mikoa husika either kwa kutokuwa na pesa ya kutosha ua kwa ufisadi jambo ambalo limezooeleka hapa nchini mwetu hilo si kosa la mchanga au mhaya au kabila lolote lile. Maana wao kwa umoja wao kama watanzania wametimiza wajibu wao wa kulipa kodi. Na iwepo ikotoke mkoa fulani kwa kona muhimu wa barabara, na kuona kuwa serikali haina uwezo, au haioni muhimu wa kujenga barabara mkoa husika,na watu wa mkoa ule wakaamua wao kuchangishana pesa, na wakajenga barbara kwa nguvu zao basi ili ni jambo la kujivunia na jambo la kuigwa. Si lazima wa mtu kutoka mkoa fulani kwenda mkoa mwingine kwa minajiri ya kujengea watu wa mkoa husika barabara, au kisima cha maji, au kuwaimiza kupeleka watoto wao bali ni wajibu wa watu wa mkoa fulani kuona muhimu wa kujiletea wao maendeleo kwa kuiga mkoa uliofanya hivyo. (ok hapa viongozi wanahusika zaidi katika kushawishi watu kujiletea maendeleo). Hiyo basi utaona kuwa Mchagga /msukuma/Mhaya anasaidia maendeleo pale anapotimiza wajibu wake wa kulipa kod.


Linapokuja swala la nchi za nje kutusaidia kuleta maendeleo hili nalo linahitaji uzi wake, Maana kwa uelewa wangu hakuna nchi yeyote ile ambayo imewahi kupata maendeleo kwa misaada. Hawa watu wanachofanya ni kutupa pesa, hii haitusaidi bali inatufanya kuwa na akili tegemezi, (ni kama unapokuwa nyumbani kuna akiba fulani hiko kabati, basi utakapopata shida yeyote ya pesa akili itakutuma kwenda kwenye kabati kuchua hiyo pesa, huwezi kuwaza zaidi ya hapo) wanatakiwa kutupa ujuzi, kutufundisha jinsi ya kupata pesa si kwa kutuletea pesa. Hebu angalia miaka 50 kila siku ya Mungu tunapokea misaada ya pesa kutoka mataifa mbali mbali hebu niambie mbona bado matatizo yetu yako pale pale? Sasa kama 50 yumepewa misaaada/tumesaidiwa katika maendeleo na mpaka sana safari bado ni ndefu je hii misaada ni muhimu wowote katika swal zima la kujiletea maendeleo? Kwanini wasitupe ujuzi, wakatujengea viwanda,wakatujenga vyou na nk? si kwamba hawawezi bali wakikujengea viwanda na kukupa elimu hawataweza kukutalawa tena kupita mlango wa misaada.
 
Last edited by a moderator:
wana ukumbi naomba radhi kwa kutokuwepo na kushiriki kwenye mijadala kwa muda ila kazi ndizo zimenibana sana hasa ukizingatia mwaka wa fedha ndo unaishia ivyoo.
Alinda asante sana kwa majibu mazuri sana uliyoyatoa.

mie naomba niseme kidogo kuhusu hali ya umaskin na nitachukulia mfano zaid kwa maeneo ambayo nimetemebelea kwa muda huu mfupi wa mwez mmoja.

nitaanzia tabora, hii nchi ni nchi pekee inayolima tumbaku kuliko mikoa mingine yote kwa tanzania. cha ajabu zaid wanachi wake wengi ni maskini sana ingawa lile gap kati ya maskin na tajiri ni dogo. nilichojionea binafsi ni kwamba ndani ya tabora utajiri uko vijijin zaidi kuliko mjini na sabb kubwa ni kwamba vijijin ndiko kunakolimwa sana. huko kumkuta mkulima anaingiza faida ya mil 10 katika msimu w akilimo ni kawaida sana ila sasa hakuna maendeleo interms of tangible effects.

nadhan kukosekena kwa reli kumeathiri zaid mkoa huu ukafikia wakati kwamba mwenye pesa ataeka zake benki na kuhusu maendeleo ata yake mwenyewe iyo sio kazi yake kabisa.

hali kama hii nimeikuta kwenye wilaya ya mbarali, kwamba wananchi wa RUJEWA ni wakulima wazuri sana wa mpunga tena wana mashamba makubwa zaid ya hekta 3500 lkn jaman kuna umaskin uliokithiri, hali ya maisha ni duni hasa kwenye vitongoji vyake hata huduma za vyoo kwenye kaya ni ngumu, wasukuma walioko kwenye hili bonde wana ng'ombe kila mmoja zaid ya 30 lkn jaman eti waanshindwa ata kujijengea vyoo tu ama hata kuhamasishana kuweza kuwa nakashule.

kuna baadhi ya maeneo utajikuta mtu hajali hata mwanae anavaa nini lkn eti kuna uwekezaji mkubwa kwenye tumbaku na mpunga. unashindwa kuelewa.

ilifika mahali nikasema labda kwasabb ya wale waarabu waliobaki tabora ndio walioshikilia huu mkoa yaani zaid ya urambo huko vijijin sijaona cha kusema mkoa wa tabora unamiliki uchumi mkiubwa. yaani watu mmoja mmoja ni maskin sana.

kadhalika huko RUJEWA yaani hali ni duni sanaaa ya maisha ya mtu binafsi.

nafkiri kama tukiwa tunapima maendeleo kwa kiwango cha upatikanaj wa maji safi, hali ya maisha ya mtu binafsi na upatikaj wa huduma muhimu basi kuna maeneo ambayo itabidi tuwaulize wenyeji je kwann hawabadiliki ilihali vipato vyao ni vikubwa na vinatosha kabisa kubadili hali ya umaskini.

ipo shida kwa serikali lkn pia naiona shida kwa wananchi wenyewe kwamba wamekaa kungojea utakuja msaada wa kujengea choo, na shule wakati wao tu wenyewe wanaweza kuyafanya haya. mabadiliko huanzia ndani sasa wasipotaka kubadilika awataishia kusubiri misaada miaka 900
 
Nimekusoma gfsonwin hasa swala la vyoo nimenigusa sana maana umelenga pale pale utafiiiri ulikuwa kichwni mwangu...Nitarudi tulijadili kwa mapana yake.
 
Mkuu Nguruvi3, nakujibu kwa kumnukuu Zitto mwenyewe mwaka huo wa 2010;

Zitto alifafanua kwamba uamuzi wa kugombea moja kati ya majimbo hayo utategemeana na utafiti na uchunguzi ambao amekwisha uanza kuufanya kupitia watu wake maalumu pamoja na ushauri kutoka kwa viongozi wa chama chake, ndugu, jamaa na marafiki zake.

Huo ni ulaghai at its best ingawa bado watu wanamwamini kama Mkandara wakitetea eti huo ndio ukomavu wa kisiasa na kwamba wengine tunaongozwa tu na wivu.
Mkuu kwani Dr.Slaa hakutangaza kutogombea Urais awamu ya pili au Mbowe kutogombea Uenyekiti 2013, hadi akaombwa na Kamati kuu, wanachama na wazee? Ni lazima tufahamu kitu kimoja kwamba uongozi wa kisiasa ni nia ya dhati kuwatumikia WATU sio maisha yako, hivyo unaweza kufikiri kwamba huna uwezo ama sababu za kuongoza wakati wananchi wanakuhitaji hivyo kama mpambanaji wa kweli itakubidi ukubali maombi ya watu wako. Kumbuka maneno ya mwalimu Nyerere pia aliwahi kusema:- Kila mara nilipotaka kung'atuka watu walinifuata na kunambia bado nahitajika....." Exactly kama Nyerere haya yamemkuta Mbowe na mimi naelewa vizuri..

Kwa hiyo mimi sioni makosa yoyote ikiwa kanuni za chama zinaruhusu..Mawazo ya binadamu yanaweza badilika dakika moja lakini kanuni pekee ndio inalinda mfumo mzima wa viongozi kugombea ama kutogombea dhidi ya kung'ang'ania madaraka.
 
Pamoja na juhudi za kututoa kwenye mada ya Nguruvi3 inayosema; Re: Duru za siasa: Chama cha ACT - Mpini wa CCM kumaliza upinzani, naomba nikuulize Mkandara, kwa nini unaamini hayo ndiyo maneno aliyoyatamka Supreme Leader akiwa Shinyanga? Sijui kwa nini leo umwamini Ritz kwa kutoa nukuu anayodai ni ya Zitto...huu ushikaji umeanza lini! Kabla sijarudi kwenye mada na mimi naomba nikukumbushe kidogo onyo lililotolewa na Kamati ya Usaliti chini ya Samson Mwigamba na Dr. Kitila Mkumbo, nanukuu;



Mkuu Mkandara, mtu anayeongelewa hapa ni huyo huyo aliyekuwa anatengenezewa njia ili siku akitua chamani moja kwa moja atawazwe kuwa Kiongozi Mkuu (hata katiba ilikuwa inamsubiri!). Hapo tahadhari inatolewa jinsi asivyokuwa na busara na alivyo mwepesi katika kutoa matamshi bila kufikiria madhara yake katika jamii. Lakini kama nilivyotahadharisha hapo mwanzo haya tuyaache turudi kwenye mada iliyoko mezani...Re: Duru za siasa: Chama cha ACT - Mpini wa CCM kumaliza upinzani!

Supreme Leader hakuitaja mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kwa bahati mbaya, aliitaja kwa kukusudia lakini kama kawaida yake hakuzingatia ni jinsi gani matamshi yake yangepokelewa katika jamii. Ni katika mikakati hiyo hiyo aliwaita wana UKAWA wasakatonge bila kufikiria athari zake kwa watu wanaopigania mabadiliko ya kweli katika nchi hii. Yeye alichokusudia ni kuzidi kuwafurahisha wale ambao alikuwa na hakika wangempigia vigelegele kwa matamshi yake hayo...nasikia sasa anajuta, kasahau majuto ni mjukuu!
Unajua mnapo laumu mtu juu ya jambo inatakiwa kwanza mjipime wenyewe. kwa sababu mnapenda kunilaumu mimi kumuamini Ritz wakati nyie wenyewe hamna nukuu halisi ya hotuba ya Zitto akiwa Shinyanga, hata nyie sielewi mliipata wapi japo nilikubali mloyaandika kama hotuba ya Zitto na tukajadili nikitoa mfano wa hotuba ya Mbowe vile vile akiwa Shinyanga. Kama mnapinga aloyaandika Ritz vizuri wekeni hotuba halisi na tuonyesheni link yake maana unapotaka Ritz atoe Link inawabidi nanyi katika madai yenu mtoe Link ya madai yenu kuwa ndio halali.

Nimejaribu kupitia hotuba yake ilowekwa humu JF sikuona mahala wameiweka hotuba kamili kama mlivyosema. Maelezo ya mkutano huo haya Hapa, na ukisoma imeelezwa kwa ufafanuzi mzuri sana. Nje ya hapo nachukua maelezo yenu (iwe wewe au Ritz) na kuyajengea Hoja maana tupo ktk mjadala. Sikuwepo Shinyanga na wala sikuiona Hotuba hiyo. Na unaposema ati Zitto hakuitaja mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kwa bahati mbaya ni swala lako wewe kukataa ukweli maana kama kuna ukweli katika maelezo yake kuna ubaya gani. Ubaya ni kutunga kitu ambacho hakina Ukweli na ukweli tumeupata HDR kuwa takwimu zipo kama alivyoonyesha Mchambuzi takwimu za TRA siwezi kumpinga kwa sababu ati kwa sababu sio zake kanukuu TRA.

Kosa ni pale anaposema kitu ambacho sii kweli. HDR wametuonyesha takwimu zao na mchango wa Shinyanga iweje kuitaja mikoa hiyo iwe tatizo? mngependa aitaje mikoa gani na isingekuwa tatizo ikiwa fikra zenu hazikujenga hoja ya Ukabila. Je, kwa fikra hizo hizo mlokuwa nazo angesema Shinyanga inachangia kuliko Dodoma lakini Dodoma wanapewa zaidi isingekuwa Ukabila dhidi ya Wagogo?. Au Dodoma kidogo haina nguvu ya hoja kuliko mikoa mloitaja?

Nauliza:- Kwa nini mnafikiria ni Ukabila kuitaja Arusha na Kilimanjaro kama sio lengo lenu kuhakikisha ACT haikubaliki Arusha na Kilimanjaro kwa kuzua fitna hii mapema. Maana sioni sababu zaidi ya kwamba nyie ndio wenye nia ya kuichafua ACT isipate wanachama mikoa ambayo Chadema inaweka ngome yake. Ama nyie wenyewe mna hisia za ukbaila na mpo tayari kuilinda mikoa yenu dhidi ya maneno yyote yanayohusu Mikoa hiyo au Chadema, maana rahisi kwenu kuizungumzia vibaya Kigoma na ACT lakini isiwe Kilimanjaro na Chadema - Kwa nini? kama watanzania kwanini mnakuwa na mipaka ktk nchi hii kuzungumziwa.

Maswala ya Zitto kuwa Supreme huo ni mtazamo wenu kwa sababu hata Mbowe alikuwa na ambition toka nimjue na kafika mbali kwa juhudi zake na sii kuyataka madaraka tu bali he worked for it. Dr.Slaa pia nimeonyesha huko nyuma na wengine wengi tu wameingia katika Siasa kwa nguvu kubwa wakitaka kuwa watu fulani na wamefanikiwa wengine imebuma. Kwa hiyo kila mtu ana malengo yake, Ningependa sana kuwa tajiri isipokuwa sioni njia rahisi na halali lakini kama ipo na pasipo kukiuka sheria why not follow that right path hata kama kuna watu wataona wivu.
 
Jokakuu;

Katika michango yako mingi unachanganua mambo bila kuwa biased. Kama tungeweza kutumia sifa zako, tungeweza kumwangalia Zitto kama mwanasiasa na kupima maneno yake kama yanasaidia jamii, taifa, na yeye mwenyewe.

Matatizo yaliopo ni kuwa toka Zitto awe na migogoro na Chadema na toka aondoke CDM, kuna watu kwa sababu wanazozijua wenyewe wamehamua kucheza na Zitto bega kwa bega. Wanafuatilia anachosema. Wanafuatilia anapokwenda. They are obsessed with him 24/7. He's their number one enemy. I think he doesn't deserve that.

Kwa maoni yangu, Zitto anao uhuru wake wa kikatiba. Kuondoka kwake CDM, kusitufanye tumnyime haki yake ya kikatiba. Uhuru wa katiba unampa ruhusa ya kuitisha mikutano na kuzungumza. Katika mambo atakayozungumza, mengine hatutapendezwa nayo. Lakini hiyo isitufanye kumnyima haki yake. Nchi imehamua kufuata western democracy na hizo ndizo gharama zake.

..nakubaliana na wewe 100% kuhusu uhuru wa kutoa maoni.

..hakuna mahali nimesema Zitto asitoe maoni yake.

..nilichofanya mimi ni kutoa mtizamo wangu kuhusu maoni aliyoyatoa Zitto.

..sikubaliani na hii dhana ya Zitto kudai kwamba kuna jamii au mikoa fulani inanyonya na kudhulumu jamii na mikoa mingine hapa Tz.

..naamini natumia haki yangu kama Zitto alivyotumia haki yake.

cc Mkandara, Alinda, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Alinda,

..asante kwa michango yako.

..kwasababu ya muda mchache tulionao naomba nisii-quote.

..huu mjadala siyo mpya hapa JF. nakushauri upitie archives za JF.

..hata maelezo uliyoyatoa siyo mapya, yalishatolewa huko zamani tena kwa watu hawahawa unaojaribu kuwajibu ktk thread hii.

..pamoja na hayo nakuomba usikate tamaa. nasema hivyo kwasababu naamini umesimama ktk ukweli.
 
Last edited by a moderator:
..kuna maneno vs hoja.

..hoja nzima ya Zitto inajenga dhana kwamba kuna mikoa na jamii fulani zinadhulumu mikoa na jamii nyingine.

cc Mkandara, Nguruvi3, TRUVADA
Kabla hatujafika huko tupe hotuba iloinukuu maneno hayo tuyasome sote maana inaonyesha kuna sintofahamu juu ya hotuba hiyo. Kila mtu anasema lake hivyo ili tuwe mstari mmoja yaweke maneno ya Zitto yanayoonyesha kuwa mikoa fulani huinyonya Shinyanga!
 
Back
Top Bottom