[/COLOR]Nilitegemea huu ushauri umpe mtoa matamshi.. kumbe ushauri tunapewa sisi ambao tunataka kujua ukweli wa hizo kauli. Kama mpaka hivi sasa hata wewe uelewi nini madhumuni ya hizo kauli ndo hivyo hvyo wananchi wa Kigoma, Iringa, Singida na Arusha nao wako gizani.
Maneno yako hapa chini ni maneno sahihi sana nawe pia kuyashika.
Alinda
- Wakati mwingine jamani kuweni na aibu.. Wewe ni watu wazima, kaka au baba hivi unapokuja kwenye mtandao na kumuekea mtu maneno mdomoni ambayo hajasema unakuwa na nia gani?
Nimetoa mifano ya Obama kwa sababu inaendana na tunachofanya hapa, siasa za dunia zinafanana sana, ni kama tu copy and paste kutoka sehemu moja kwenda nyingine,
https://www.youtube.com/watch?v=DLgm1I8bVVE, watu wanachukua vitu visivyo vya msingi wanavitafsiri wanavyotaka alafu wanavifanya ndio issue na kuvikomalia,ili siasa zetu ziishie hapo hapo, kwenye vitu vyepesivyepesi.
Hili suala la maendeleo kwa mfano, lilikuwa la msingi sana, na lingepaswa kuibua mjadala wa namna bora ya kuleta maendeleo, la msingi sana, sasa sijui mtu anawezaje kuja na Ukaskazini kwenye hoja ya kitaifa kama hii? nani kalileta hili?ni mioyo ya baadhi yetu ambayo either ina upungufu wa Utanzania na walioujaza ukanda mioyoni mwao. Na kwakuwa hawawezi kujisema wazi, wanasingizia hoja ata isiyohusika ili kujipa uhalali wa kuzungumzia matamanio ya mioyo wao.
Bahati mbaya sana, badala ya kujadili juu ya namna gani nzuri ya kusambaza maendeleo hayo mikoani, tunabaki hapa tunajadili Ukaskazini wetu, hatujisaidii sisi,hatuzisaidii siasa zetu, na hatulisaididi taifa letu.Tuache njia hii, inapanda mbegu mbaya.
Kuna watu waliokuwa hawajui kama kuna kitu kinaitwa Ukaskazini, humu ndani wamejengwa moyo wa uzawa wa Kaskazini.
Kuna watu ambao Tabora ni wako, Moshi ni kwao, Mtwara ni kwao, hapa wameonyeshwa kuwa labda sio sahihi sana kulazimisha mikoa yote iwe na maendeleo, wameambiwa mikoa mingine iridhike iwe ilivyo, watajiuliza maswali,kwanin??kwanini watu hawataki hiki??
Yawezekana kabisa ata hatuna mawazo haya, lakini bila kujijua hizi mbegu zinapandika.Tunaambukiza watu.Tuepuke kutenganisha watu.
Yawezekana kabisa kuwa hatupendi kabisa siasa za Zitto,ni haki ya kila mtu,yawezekana tunataka kila hoja yake ionekane ni mbaya, ni haki yetu kabisa.Lakini ebu tujue sehemu ya kupambana nae kwenye siasa bila kujenga chuki na kugawanya watu.hapa mlipopachagua kupambana nae sipo.Panabomoa taifa letu.Mtafuteni angle zingine kisiasa.Sio hii.
Nakumbuka Mwalimu Nyerere na story yake ya Geroge Kahama(sio direct quotation)
.................................................................................................................................................................
George kahama alikuwa amepanda ndege, kaenda mikutano ya kimataifa
ndege ikatikisika mara ya kwanza, George Kahama akaguna...My God...(mtu wa kimataifa)...
ndege ikatikisika zaidi mara ya pili -- George Kahama akaguna ..(Mungu wangu)..(karudi kwenye Utanzania)
Ndegu ikatikisika kwa nguvu zaidi mara ya tatuu -- nikamsikia george akipiga kelele -- maweeeee(kaisharudi kwenye kabila lake)!!!!!
JK Nyerere
................................................................................................................................................................
Kwenye mambo ya kutetea Kanda zetu badala ya taifa ebu tupige break.Hayatusaidii kama taifa.
Ata hilo la lugha ya picha, watanzania wanajua sana lugha yao ya kiswahili, na wanajua jinsi lugha hizi zinavyotumika kufikisha ujumbe kwa hadhira.Wala haiwasumbui, na ndio maana ata Lema aliposema wa dar es salaam, waliishia kucheka tu, ndivyo Watanzania tulivyo, Watanzania hawa mioyo yao ni misafi sana, hawawezi haya tunayotaka kuyapanda.