Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Huwezi kubadilisha historia leo. Upinzania wa chama kuwa na nguvu dhidi ya CCM umeanzia Kigoma.

Ata kama unawachukia lakini huwezi kubadilisha historia.

Hakuna mtu mwenye chuki wa wanaKigoma, na naomba utuombe radhi kwa hilo wanakigoma ni ndugu zetu tena wengine tumechangia damu na wanakigoma na pia unapobishana na mtu ondoa kwanza hisia za chuki huu ni mjadala wa kujenga si wa kutenganisha.

Hakuna mtu anayepiga kuhusu upinzani na Kigoma ila tunachopiga ni uongo wa kutuaminisha kwa Tanzania nzima tulikuwa tumelalal ila ni Kigoma tu ndo kulikuwa na upinzani.. Huu naweza kuita upuuzi..

Na pia inawezekana ni mazingira ya wakati ule yanakufanya uamani kuwa mageuzi ni Kigoma tu. Nanivyofahamu kwa kipindi cha nyuma vyombo vya habari vilikuwa vya kuhesabu, kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine ilikuwa ni "issue" hivyo kupata habari za vyama vya siasa ilikuwa tabu kidogo na ndo maana unaamini kuwa ni Kigoma peke yake iliyopokea mageuzi. (Kwa vile ulikuwa unaishi Kigoma)

Pili kupigwa mabomu Kigoma haifanyi mkoa mingine hisiwe na vuguvugu la mabadiliko. Ni kama leo Lema asimame pale Arusha wambie kuwa nyie ndo wanamageuzi wa kweli maana nyie ndo mmepigwa mabomu sana, na mikoa mingine bado wanakubatia watawala. Swali kwako je hii kauli itakuwa na ukweli wowote?
 
Huko sahihi Mbunge wa kwanza kukaa upande wa upinzani baada ya vyama vingi kuruhusiwa ni Kaburu, mwaka 1994 Alinda amelisishwa ubishi na wenzake,maana ukisoma maelezo yake,anataja wabunge wa upinzani wa Arusha,Kilimanjaro,ila kwa kigoma hajataka kujishughulisha,wakati hizo amegoogle,kwanini hasigoogle na kigoma,nilichogundua,baada ya kutuvutiwa na Zitto,sasa hivi wanaichukia hata na historia ya upinzani kutoa mbunge wa upinzani kutoka kigoma,wanatamani angetoka mikoani kwao huko,huzi ulishapotea njia huu,tokea Zitto alipo amia ACT[/QUOTE

Hii mipasho huwa sina "comment"
 
Kwa hiyo ni haki watu wa Arusha, Singida na Iringa kuitwa wana midomo mrefu?? Hivi kama alimaanisha Lissu je alishindwa kusema Lissu ana mdomo mrefu? na kama alimaanisha Lissu na wengineo, Je alishindwa kusema "baadhi ya watu wa Singida wana midomo mrefu? (angesema hivi wala nisingeleta hiyo video maana ningekuja anamaanisha "baadhi ambao ni chadema") kulikuwa na mantiki gani ya kusema watu (Wote) wa hiyo mikoa wana midomo mrefu iwe kwa tafsiri yako (lugha ya picha) au iwe kwa tafsiri yangu..

Alinda, hili la midomo mirefu wala lisikusumbue na wala halihitaji attension kiasi hicho, ni lugha ya kawaida kabisa kifasihi, unanogesha lugha badala ya kueleleza direct.
.................................................................................................................................................................
"midomo mirefu" maana yake "anayeongea sana maneno ya uongo".

Sasa huishii hapo, hii ni lugha inayokurejesha kwenye tukio la "wanaongea sana uongo", inakuleta ni nani hao??anasema "ni hao wanaosema kuwa yeye ni msaliti na kuwa wao ndio wapinzani sanaaa", kuondoa doubt ya ni nani hao ndio anamalizia "yule anayetokea mkoa wa Arusha, Iringa n.k).

.................................................................................................................................................................
Wanasiasa wote wazuri hawaongei kila kitu direct badala yake hujenga picha kuongeza tafakari, na hiyo unogesha zaidi maongezi/hotuba kuliko kusema direct, kwa lugha ya kawaida wakati mwingine ukisema direct inaonekana ni harsh zaidi kuliko ukisema kwa kutumia picha.
 
Alinda, hili la midomo mirefu wala lisikusumbue na wala halihitaji attension kiasi hicho, ni lugha ya kawaida kabisa kifasihi, unanogesha lugha badala ya kueleleza direct.
.................................................................................................................................................................
"midomo mirefu" maana yake "anayeongea sana maneno ya uongo".

Sasa huishii hapo, hii ni lugha inayokurejesha kwenye tukio la "wanaongea sana uongo", inakuleta ni nani hao??anasema "ni hao wanaosema kuwa yeye ni msaliti na kuwa wao ndio wapinzani sanaaa", kuondoa doubt ya ni nani hao ndio anamalizia "yule anayetokea mkoa wa Arusha, Iringa n.k).

ni dk ya ngapi anatamka neno "yule anayetokea Arusha" Yaani unaongopa kwa vitu vidogo ambavyo kila mtu anasikiliza na kuelewa mwenyewe? Je kikija kitu kikubwa ambacho hatuwezi kusikiliza/au kusoma na kuelewa tutakuaminije?

Wakati mwingine jamani kuweni na aibu.. Wewe ni watu wazima, kaka au baba hivi unapokuja kwenye mtandao na kumuekea mtu maneno mdomoni ambayo hajasema unakuwa na nia gani?

.................................................................................................................................................................
Wanasiasa wote wazuri hawaongei kila kitu direct badala yake hujenga picha kuongeza tafakari, na hiyo unogesha zaidi maongezi/hotuba kuliko kusema direct, kwa lugha ya kawaida wakati mwingine ukisema direct inaonekana ni harsh zaidi kuliko kusema kwa kutumia picha.

Ukiangalia vizuri maelezo yako mwenyewe hapo yanathibitisha kuwa Dr Aman Kabour ni mbunge wa kwanza kukaa katika bunge la Jamhuri mwaka 1994.

Kwanin unalithibitisha hilo? ni kwa sababu matokeo ya uchaguzi yanapopingwa hupelekwa mahakamani, wakati wote wa kesi ya kupinga matokeo hayo, yule aliyeshinda uchaguzi (kwa hapa Kabouru) uwa ni mbunge halali wa jimbo husika na hushiriki vikao vyote vya Bunge kama wabunge wengine.

Unaweza kukumbuka pia Makongoro Nyerere na Steven Wasira, walikuwa wabunge kwa muda mrefu mpaka pale kesi zao zilipoamuliwa.Ndivyo ilivyokuwa kwa kabouru.

Hivyo, hili nina uhakika nalo, 100%, Dr Aman Kabouru ndiye alikuwa Mbunge wa kwanza wa upinzani sio kuchaguliwa tu bali pia kukaa na kushiriki vikao vya bunge kwa upande wa Tanganyika.Nasema Tanganyika kwa sababu sina kumbukumbu nzuri kama Kwahani kweli alishinda CUF.

Kama umenisoma vizuri.. Nimeandika hivi Dr. Amani HAKUSHINDA NA NDO MAANA ALIKWENDA MAHAKAMANI NA MAHAKAMA IKATENGUA HAYO MATOKEO.
 
Kama umenisoma vizuri.. Nimeandika hivi Dr. Amani HAKUSHINDA NA NDO MAANA ALIKWENDA MAHAKAMANI NA MAHAKAMA IKATENGUA HAYO MATOKEO.

Nimekusoma.Sasa Alinda umeniwekea maneno ndani ya Quote yangu itaonekana kama ni maneno yangu wakati siyo.

Moja, kama nilivyosema lugha ya picha hauitafsiri direct, maana yake inapatikana kwa kuitafsiri picha.

Imenibidi nirudi kusoma na nimekutana na hili!!Hivyo kwenye la ubunge nakubali kukosea.Lakini hii pia inathibitisha nguvu ya Chadema wakati huo.

In Kigoma thecandidate selected by the opposition party CHADEMA was a well-respected political economist,Dr. Kabouru,. After a brief campaign marred by allegations of registration irregularities andgovernment favoritism shown the CCM candidate, the election resulted in a victory for the rulingparty. Following the election there were charges that the opposition candidates had receivedvirtually no media coverage on the government-controlled radio station, and that opposition partieswere often denied permits to hold meetings and rallies. It was also pointed out that the [mal votecount had been stopped before it was completed and later a CCM victory was declared with Dr.Kabouru protesting that he and his agents had not been able to see and verify the ballots talliedafter the resumption of counting.

Just for fun,politics:
Tutakapoweza kutofautiana kama hivi bila kuchukiana na tukaendelea kuheshimiana na kukubaliana kutokukubaliana,ndio njia ya kwenda!
https://www.youtube.com/watch?v=lhh7SvDIWGk
https://www.youtube.com/watch?v=laCoCJaHtEM 😀K YA 0.48 mpaka 0.59 Obama anaongea exactly kama alivyoongea Zitto juu ya wapinzani wake
 
Nakubaliana na wewe juu ya vichocheo vya maendeleo ila natofautiana na wewe kuhusu role ya serikali.Serikali ina nafasi yake ya kufanya, iwe ni kwenye fursa, iwe ni kwenye hamasa, elimu n.k, kuna mengi serikali inaweza kufanya. Sasa tunaweza kutofautiana hapo ni kipi kifanyike, ni kipi kisifanyike. Ni tofauti ya kawaida.Kama kuna jambo tulipaswa tujitite ni hapo, kwamba mbona kwangu naona option nzuri zaidi ingekuwa A na sio B, ni C na sio D. Ndipo tulipotakiwa kuhangaika nako sasa.

Lakini kuitafsiri unavyotafsiri kauli ya kisera na kimfumo kwa namna tunavyotafsiri hapa bila shaka tatizo sio kwa Zitto bali lipo ndani yetu sie.Kutafsiri hivi kunahitaji kwanza kuwa na huo "u-kaskazini kwanza", kwani hakuna sehemu Zitto kazungumzia kanda yoyote.Hakuna sehemu Zitto kawasema wananchi wa Kaskazini, ata sehemu moja, kazungumzia hali ya maendeleo ya kiuchumi nchi nchini, na umuhimu wa kuboresha mfumo wa kiuchumi ili kuboresha hali hii kwa mfano wa maeneo yaliyo nyuma, hajasema maeneo yaliyo mbele yarudishwe nyuma au yatengwe, note hilo!!

Kwenye kauli ileile ileile alisema

  • Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP."

Naamini kuna watu wa LIndi pia hapa, hawajashtuka lolote kwa sababu ni suala la kisera tu, ni suala la Tanzania, na kote ni kwao.

Sasa huu utafsiri wa Ukaskazin umetoka wapi?huu utafsiri wa "wananchi wa Kaskazini umetoka wapi"?
Hii ishara ya wazi kuwa bado tuna kazi ya kufanya kuujenga huu Utaifa huu. Hii ni wazi sasa kuliko kabla kuwa Nyerere hakumaliza kazi ya kuujenga Utanzania wetu, hii ni ishara kuwa tunao akina Nassari humu (refer kauli yake ya kujenga nchi ya Kaskazini),wenye Ukaskazini mioyoni mwao, na ndio maana wanalazimisha kutafsiri Ukaskazini ata ambapo hakuna mtu kataja Ukaskazini.

Na hapa ndipo lilipo tatizo na wala sio kauli ya Zitto, tuna kazi nzito sana ya kufanya hapa, na jitihada hizi zinapaswa zifanywe na kila mmoja wetu, tutoke hapa,tuujenge Utanzania mioyoni mwetu.

Kapwela, mnajitahidi sana kuigeza geuza kauli ya Zitto.
Wewe unaongelea Lindi, huongelei jinsi alivyokula sahani moja na mkoa ya Arusha/ Kilimanjaro

Hili linaonyesha. kauli ya Zitto hata ninyi watetezi wake mnaiona si sahihi.
Msichotaka kukifanya ni kukemea uhuni. Ndivyo ilivyo video ya Alinda inavyoeleza.

Zitto kaenda sambamba na mikoa yenye midomo mirefu, mnatafuta justifications za kauli zake hata kama nyoyo zenu zinajua kasema ubaya.

Hatuna sababu kuingilia ugomvi wa Zitto na Viongozi wenzake, tunachokataa ni kutaka kulimega taifa kwa misingi ya Ukigoma, ukanda, Utabora, U-Tanga ili anufaike kisiasa.

Kauli kama '..kuna ubaya gani mtu wa Kigoma kuwa mwenyekiti' ililenga kuonyesha kuna watu wa maeneo fulani wanaodhani wana haki. Ukiangalia mgogoro ndani ya Chama hapa alimaanisha kitu kibaya sana. Kibaya sana

Yaani hasimami kama Zitto anasimama kwa Ukigoma! msikilize anasema' kwanini watu wa Kigoma waone aibu.. kujitambulisha''
Yaani matatizo ya kisiasa ameyafanya ya mkoa wa Kigoma, sasa anashawishi wananchi wa Mikoa hiyo wachukie wa Mikoa mingine

Unakumbuka alianza na kanda ya kaskazini, sasa anaingia central zone, tayai Singida na Iringa zimejumuishwa .

Yote haya hamuyaoni, mantushauri tukae kimya, taifa linamwega, who is he kiasi cha kuleta mifarkano ya kijamii namna hii.
 
Hivi Alinda humjui Mkandara? Anajua kabisa katiba ilibadilidhwa lini na wakati huo Zitto alikuwa nani ndani ya Chadema. Anajua kabisa ni lini Zitto alitaka kugombania uenyekiti wa Chadema na kushauriwa asubiri na wazee. Anajua ni lini waraka wa usaliti ulitayarishwa. Anajua timeline ya Chadema toka kuanzishwa kwake. Anajua yote hayo.

Lakini kwa makusudi yasiyoeleweka ukimsoma ni kama vile anadai katiba ilibadilishwa baada ya Zitto kushauriwa asigombee. Kama humjui Mkandara unaweza kuumia ukijiuliza nini hasa ni lengo lake lakini kwa ambao tumebahatika kumfahamu japo kidogo, hatushtuki. Ukijaribu kumbana hapo atakuja na mengine na kuzua mapya ambayo hajaulizwa.

Mathalani ukimuuliza wakati Dr. Slaa anajiunga na Chadema na kuchaguliwa mbunge mwaka 1995, Zitto alikuwa nani ndani ya Chadema na mchango gani aliweza kuutoa kulinganisha na Mbunge Dr. Slaa. Katika uchaguzi uliofuatia mwaka 2000 Zitto alikuwa nani ndani ya Chadema na mchango wake ulikuwa upi katika kukiimarisha chama kipindi hicho.

Sasa humu unamkuta mtu kama Ritz anarukia hata vile asivyovijua kwa kumuunga mkono eti akina Dr. Slaa walikuwa wamelala wakati Zitto anajenga chama. Kugombea Uraisi kwa Mbowe mwaka 2005 ndiko kulikozidi kukitangaza chama hadi Zitto kuukwaa ubunge kwani mashina tayari yalikuwepo Kigoma toka wakati wa Dr. Kabourou.

Katika jukwaa hili la GT tungejitahidi kupunguza ulaghai kwa kutoandika tunayojua moyoni kwamba si ya kweli lakini kwa makusudi tunafanya hivyo. Tukumbuke kwamba wwaka 1995 Chadema haikutoa mgombea wa Uraisi na hivyo hivyo mwaka 2000. Ushupavu wa wabunge kama Dr. Slaa ndiko kulifanikisha kukiimarishana na kukijenga chama zaidi.
Mkuu kama una swali unauliza kisha upate jibu langu kuliko kubuni vitu kwa sababu unataka tu kujenga hoja ya nguvu. Nisome hapo nyma nimeeleza vizuri Katiba iliandikwa lini ya mwaka gani na ilikuwa na kipengele hicho.

Kwa hiyo Mbowe pamoja naviongozi wengine wote walikuwa na vipindi viwili yaani toka 2004 ilipoandikwa Katiba hiyo. Mimi nilikuwa mmoja wa watu waloamini Mbowe alitakiwa kupewa mihula miwili kwa sifa na uwezo wake dhidi ya Zitto na tuliyasema hapa JF yakaisha baada ya Zitto kukubali ushauri wa wazee na yote haya yalikuwepo hapa JF.

Mwaka 2006 ikabadilishwa na kuandikwa Katiba Mpya. Kinachowatatiza wengi ni kwamba baada ya kuandikwa na kupitishwa na vikao vyote vya chama, bado katiba hiyo ilifanyiwa marekebisho mengine katika vifungu kadhaa ikiwemo hicho. Hapo ndipo madai yalipokuja ya kwamba mabadiliko hayo hayakutakiwa kwa sababu hayakupitishwa na vikao na ndio maana ya kuitwa Kinyemela. Wengine wanadai hata kama hayakutakiwa swala la UKOMO wa viongozi haukuwepo katika ile katiba ilopitishwa yaani ya mwaka 2006. Wengine wanasema (kina Kitila) Jamani kwanza uandishi wa Katiba ya 2006 swala la UKOMO halikuguswa liliachwa vile vile kama lilivyokuwa 2004 isipokuwa mwelekeo na DIRA ya chama Kiitikadi ndicho kilichobadilishwa.

Kinachonipa shaka miye ni kwamba haiwezekani viongozi wengi wa chama mikoani wakubaliane na upande wa Zitto, isipokuwa tunasikia viongozi wa kamati kuu tu wale waloshukiwa ndio wanaotetea kutokuwepo kwa UKOMO wa viongozi wakati wao ni viongozi kana kwamba wanatetea nafasi zao. Kwa nini asiwe mtu wa nje ya kamati kuu, mjumbe alokuwepo kupitisha katiba ile na anakumbuka kwa uhakika kwa kiifungu hicho hakikuwepo/kilikuwepo. Haya zaidi ya hapo watu wamekuja fanya vile vile kama ilivyokisiwa kuwa ndio lengo lao, afadhali hata wangekubali kuachia nafasi zao wakachukua uongozi mwingine ingetupa picha tofauti.

Hayo mengine wewe endelea kufikiri unavyotaka maana hata miye niklikuwa mbishi hivyo hivyo sikuamini kina Zitto hadi nilipokuja gundua walokuwa nyuma ya mambo haya.. Siwezi andika hapa na wala sii mahala pake..Amini usiamini mimi nimeshafikia ukomo wa kujieleza.
 
    • Je ni kweli wakati Kigoma upinzani umekomaa Arusha, Singida na Iringa walikuwa wanashangilia watawala?

      Jibu ni hapana ila ni kweli kuwa kuna baadhi ya mikoa mpaka leo wao ni CCM damu damu.

    Na kwa ili sitegemea kiongozi msomi kama Zitto kuwakashfu watu kwa vile tumetofautiana kimtazamo na pia si haki pale watu wanapoona umuhimu wa vyama vya upinzani na kujiunga havyo , wauulizwe/wasimangwe/wakweke daraja la pili kwa vile tu majiunga le hawakujiunga miaka 20 iliopita. Vyama havijengwi kwa kutazama ni lini umejiunga bali kwa kutazama unakitumikiaje chama.Na hizi ndo argument za kijinga kutoka kwa Zitto. (kwamba mie nimejiunga nikiwa na miaka 16 na nyie umejiunga jana.. au sie tulipigwa mabomu wakati nyie mnashangilia watawala) .

    Nakubaliana na wewe kuhusu kimbuga cha Mrema lakini Mrema alikuta mageuzi yapo ila alipojiunga na upinzani ni kama alileta chachu za mabadiliko na hizi chachu za mabadiliko zilienea Tanzania nzima ikiwemo na Kigoma. Hivyo basi huwezi kusema kuwa Kigoma hawakufaidika na Mrema maana wao walishapiga hatua kwenda mbele kuliko mikoa yote.

..

Wala hakuna masimango hapo, ni lugha za kawaida kabisa hizo kisiasa.Nimeweka hapo juu video za Obama na Clinton utaona wanachosema ni hicho hicho anachosema Zitto, ni argument ya kawaida kujenga uhalali wa maelezo yako.

Ni kweli kimbunga cha Mrema kilivuma kote, lakini kabla ya kimbunga kile hakukuwa na upinzani wowote wa kuweza kuishinda CCM, iwe ni Iringa, iwe ni SIngida, iwe ni Arusha, ongeza jimbo lingine lolote nje ya Kigoma Mjini. Majimbo mengine yalifufuka ghafla na kimbunga kile na kugeuka tishio kwa CCM kuelekea uchaguzi wa 1995.

Lakini kingine cha kuzingatia, hapa argument hii ni Zitto dhidi ya "wanaosema kuwa yeye ni kibaraka", ndio maana akawataja kwa picha ya wanakotokea yaan Iringa (Msigwa), Arusha(Dr Slaa na Lema) na Singida (Lissu), je ni kweli kuwa walikuwa wamekumbatia watawala?ni kweli Dr Slaa alikuwa kada wa CCM wakati huo, sina uhakika bali yawezekana Tindu Lissu, Lema na Msigwa walikuwa CCM au hawakuwa na mpango wala kushiriki kwenye struggle hii wakati huo.

Na unaweza kuthibitisha hilo kuwa anazugumzia "watu" na sio "mkoa" kwa kuangalia hapo choice yake, kwanin hajataja Kilimanjaro wakati Mbowe nae yupo kundi hilo juu? ni kwa sababu wakati huo Mbowe tayari alikuwa upinzani tayari.Hii ndio picha ya wazi kabisa inayotoka kwenye clip hiyo.
 
Kapwela,

..Tundu Lissu anajulikana kuwa ni mwanaharakati toka yuko JKT.

..aligombea ubunge mara ya kwanza mwaka 95 kupitia chama cha NCCR.

..kwenye suala la kutetea haki za wananchi kuna watu wachache sana wanaolingana na Tundu Lissu.

..kwa mtizamo wangu ktk suala la harakati za kutetea maslahi ya wananchi, Tundu Lissu ni mlima kilimanjaro na Zitto ni kichuguu.

cc Alinda, Mkandara, Mchambuzi, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Kapwela, mnajitahidi sana kuigeza geuza kauli ya Zitto.
Wewe unaongelea Lindi, huongelei jinsi alivyokula sahani moja na mkoa ya Arusha/ Kilimanjaro

Hatuna sababu kuingilia ugomvi wa Zitto na Viongozi wenzake, tunachokataa ni kutaka kulimega taifa kwa misingi ya Ukigoma, ukanda, Utabora, U-Tanga ili anufaike kisiasa.

Unakumbuka alianza na kanda ya kaskazini, sasa anaingia central zone, tayai Singida na Iringa zimejumuishwa.

Hivi u Ukaskazini mnautoa wapi?maana nautafuta siuoni, nimesoma maelezo ya Zitto sioni, ndio maana nazidi kupata mashaka sana na Utanzania wa baadhi yetu, maana kutafsiri jambo la kisera na kimfumo kwa muktadha wa Ukaskazini?hii inasikitisha sana.

Na kingine hiki kinanishangaza zaidi, kwanini Lindi isiwe issue?maana alipotaja Kilimanjaro ndipo alipotaja Lindi pia?sasa kwanin iibuke hoja tu ya Ukaskazini lakini isiibuke hoja ya Ukusini?kuna tatizo kubwa hapa.

Ni wazi kuwa kuna watu wanatafuta excuse ya kuonyesha jinsi wasivyo wa-taifa kwa kulazimisha ata kisichokuwepo.Tunahitaji kuondoa hii kitu mioyoni mwetu, maana wakati mwingine unaweza ukakiona kitu sio kwa sababu kipo kwa mwingine bali ni kwa sababu kipo ndani yako.Hiki tukiondoe!!

Na pia tusiwawekee watu maneno ambayo hawajayasema, mfano wa Ukaskazini na chuki kwa Ukaskazini, kama tunahitaji Ukaskazini tuseme wazi kama Nassari, tusiwasingizie wengine. Ebu tulishike neno hili la busara la Alinda hapa chini.

  • Wakati mwingine jamani kuweni na aibu.. Wewe ni watu wazima, kaka au baba hivi unapokuja kwenye mtandao na kumuekea mtu maneno mdomoni ambayo hajasema unakuwa na nia gani?
.

Hatuna sababu kuingilia ugomvi wa Zitto na Viongozi wenzake,

Kauli kama '..kuna ubaya gani mtu wa Kigoma kuwa mwenyekiti' ililenga kuonyesha kuna watu wa maeneo fulani wanaodhani wana haki. Ukiangalia mgogoro ndani ya Chama hapa alimaanisha kitu kibaya sana. Kibaya sana.

Hayo ya power struggle ndani ya Chadema sio rahisi kwetu ku-conclude lolote.

Kwenye taasis yeyote kuna vitu vya ndani ambayo kwa mtu asiye kwenye inner-cycle hawezi kujua. Ndivyo ilivyo ngumu kwangu na labda kwetu juu ya hayo ya chumba cha ndani cha Chadema.

Ni vizuri tu tuweke benefit of doubt kwa pande zote kisha tusonge mbele.

Unakumbuka alianza na kanda ya kaskazini, sasa anaingia central zone, tayai Singida na Iringa zimejumuishwa .

Yote haya hamuyaoni, mantushauri tukae kimya, taifa linamwega, who is he kiasi cha kuleta mifarkano ya kijamii namna hii.

Hakuna mtu yeyote utamsikia analalamikia Usingida wala U-Iringa.Mtu yeyote atatambua kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa dhidi ya Msigwa na Lissu.

Nguruvu, Alinda: Najua mu watu makini sana, na yawezekana kabisa mna Utanzania ndani yenu.Lakini kauli hizi humu ndani badala ya kujenga zitazidi kujenga utengano wa kijamii.

Kuna watu humu wanaosoma ambao kwa maelezo ya humu watapata picha tofauti na badala ya kujenga ndio kwanza tunabomoa zaidi.Tusiwe watetezi wa Kanda.Tuwe wa Tanzania kwanza.
 
Ni mkoa gani huo ambao ulikuwa chini ya CCM na watu wote wakishangilia?

Katika kumbukumbu zangu, uchaguzi wa vyama vingi Mwaka 1995 Nccr ndicho chama kilichokuwa kina nguvu Tanzania bara na CUF Zanzibar na katika uchaguzi huo vyama vya upinzani viliweza kupata wabunge 55.

Nccr wabunge 19, CUf wabunge 22, UDP 3, Chadema 3 na 10 viti maalum.

Miongoni mwa wabunge hawa kuna Makongoro Nyerere Arusha mjini, Mabere Marando Rorya, James Mbatia Vunjo, Makidara - Siha, Kibaso Iringa, Joseph Mtui Moshi na nk. Sina kumbukumbu kuwa 1995 Kigoma waliweza kupata mgombea kutoka Upinzani.

Sasa swali kwako Je ni kweli wakati wanakigoma wako atika harakati za mageuzi, Arusha, Iringa na Singida walikuwa wamelalal?

Na kama walikuwa wakishangilia CCM ilikuwaje Makongoro na Kibaso wakachanguliwa kuwa wabunge kutoka Nccr?

Na katika kura za urais Mrema alipata asilimia 27.7 wakati Ben Mpaka akiwa na asilimia 61.... Je unataka kusema hizi kura alizopata Mrema zilitoka Kigoma tu?
Bibie Kama unataka kubishana juu ya Mikoa hiyo angalia harakati za mageuzi na sio ushabikia vyama. Zitto anazungumzia CHADEMA na jinsi wananchi walivyokuwa bado wakiichagua CCM wakati wananchi wa Kigoma wakipigwa kwa kutoichagua CCM kama tunavyoweza jenga hoja juu ya CUF Zanzibar.

Hata leo hii bado Mikoa ya Pwani inashikiliwa na CCM na ndizo ngome zao , hivyo chama cha Upinzani kushinda jimbo moja ama mawili katika mkoa mmoja haiwezi jenga hoja ya mkoa mzima. Leo CCM wanaweza kabisa sema mikoa ya kanda ya Ziwa na Kaskazini wananchi wake wamelewa na Upinzani, japo wanashinda baadhi ya majimbo lakini ukweli unabakia kuwa mikoa hiyo ndio ngome ya Chadema..

Siasa lazima uipime kisiasa na sio kutafsiri maneno kwa emotions, siasa hazitaki emotions bali kuelewa ujumbe unamlenga nani na kwa sababu gani na UWAZI ndio utoa picha kamili. Tunapozungumzia Mabepari haina maana kila tajiri ni bepari isipokuwa lengo ni kuzungumzia UNYONYAJI, isiwe kia tajiri achukie hoja pasipo kutazama walengwa.
 
Wala hakuna masimango hapo, ni lugha za kawaida kabisa hizo kisiasa.Nimeweka hapo juu video za Obama na Clinton utaona wanachosema ni hicho hicho anachosema Zitto, ni argument ya kawaida kujenga uhalali wa maelezo yako.

kwanza nashukuru kwa kuweka hiyo video, ila kwa bahati mbaya sioni mantiki ya kuweka hizo video za Obama.

Kwanza hatuko Amerika, Pili Zitto si Obama, Tatu sio lazima analolifanya Obama na Zitto afanye hilo hilo, Tano nimesikiliza hazo video mara mbili mbili hakuna niliposikia Obama anasema "Watu wa Chigaco au LA ni waongo "yaani ile tafsiri yako ya midomo mirefu.
Sit
a hata kama Obama amesema hivyo haifanyi Zitto na yenye kukashfu watu wa mikoa fulani.

Ni kweli kimbunga cha Mrema kilivuma kote, lakini kabla ya kimbunga kile hakukuwa na upinzani wowote wa kuweza kuishinda CCM, iwe ni Iringa, iwe ni SIngida, iwe ni Arusha, ongeza jimbo lingine lolote nje ya Kigoma Mjini. Majimbo mengine yalifufuka ghafla na kimbunga kile na kugeuka tishio kwa CCM kuelekea uchaguzi wa 1995.

Umesema Kigoma walifanya uchaguzi wa kwanza mwaka 1994, na kwa bahati mbaya Dr. Amani alishindwa na premji tena kwa kura nyingi tu. Sasa huo uchanguzi ambao ungefanyika na Kigoma wakaibuka kidedea ni changuzi upi hali Dr. Aman alishashindwa 1994 (hapa ni kabla ya Mrema) So baada ya Mrema mwaka 1995 kuleta hiyo chachu kwa Tanzania nzima ikiwemo Kigoma ndo Dr. Amani akashida uchanguzi. Jamani tubishanie hata vitu vilivyo wazi kiasi hiki.

Lakini kingine cha kuzingatia, hapa argument hii ni Zitto dhidi ya "wanaosema kuwa yeye ni kibaraka", ndio maana akawataja kwa picha ya wanakotokea yaan Iringa (Msigwa), Arusha(Dr Slaa na Lema) na Singida (Lissu), je ni kweli kuwa walikuwa wamekumbatia watawala?ni kweli Dr Slaa alikuwa kada wa CCM wakati huo, sina uhakika bali yawezekana Tindu Lissu, Lema na Msigwa walikuwa CCM au hawakuwa na mpango wala kushiriki kwenye struggle hii wakati huo.

Husitake kubalisha maneno hakuna sehemu Zitto aliposema "Wanaosema Kibaraka" hebu sikiliza vizuri hiyo clip tena na tena.. "anasema wakati Kigoma wanapigania mageuzi watu wa Singida, Arusha, Iringa walikuwa wanawakumbatia watawala". Sasa wewe hayo meneno mengine unayatoa wapi?? na after all hata hivyo Lissu alianza harakati za kumkoboa myonge hata kabla ya Zitto hajaanza siasa ila tatizo la Lissu si mtu wa kutaja mafanikio yake au si mtu wa media. Ni nadra sana kumsikia Lissu akisema "nimefanya hiki au kile" ila watu tunamfahamu tangu akiwa NCCR.

Lema huyu alikuwa NCCR kabla ya kwenda Chadema (mwaka gani sina uhakika)

Dr.Slaa Mwaka 1995 alikuwa kati ya wale wabunge 3 wa Chadema. Kwa hapa ukiangalia mageuzi yameaanza mwaka 1992 hivi kweli mtu mwenye akili unaweza kumsimanga mtu aliyejiunga na mageuzi miaka 3 baada ya mageuzi kuruhusiwa? na ukimsimanga huyu je yule aliyejiunga mwezi leo au jana si ndo dalaja la 2.

Hivyo basi ukichukua hayo maelezo yangu hapo juu si kweli kuwa Lissu alikumbatia watawala tena Lisssu amekula virungu zaidi ya Zitto. (sina kumbukumba kama Zitto alishakula virungo sasa sijui wakati wenzake huko Kigoma wanakula virugu yeye alikuwa wapi)

Na unaweza kuthibitisha hilo kuwa anazugumzia "watu" na sio "mkoa" kwa kuangalia hapo choice yake, kwanin hajataja Kilimanjaro wakati Mbowe nae yupo kundi hilo juu? ni kwa sababu wakati huo Mbowe tayari alikuwa upinzani tayari.Hii ndio picha ya wazi kabisa inayotoka kwenye clip hiyo.

Hapa sijui unataka kusema nini?
 
Bibie Kama unataka kubishana juu ya Mikoa hiyo angalia harakati za mageuzi na sio ushabikia vyama. Zitto anazungumzia CHADEMA na jinsi wananchi walivyokuwa bado wakiichagua CCM wakati wananchi wa Kigoma wakipigwa kwa kutoichagua CCM kama tunavyoweza jenga hoja juu ya CUF Zanzibar.

Hata leo hii bado Mikoa ya Pwani inashikiliwa na CCM na ndizo ngome zao , hivyo chama cha Upinzani kushinda jimbo moja ama mawili katika mkoa mmoja haiwezi jenga hoja ya mkoa mzima. Leo CCM wanaweza kabisa sema mikoa ya kanda ya Ziwa na Kaskazini wananchi wake wamelewa na Upinzani, japo wanashinda baadhi ya majimbo lakini ukweli unabakia kuwa mikoa hiyo ndio ngome ya Chadema..

Siasa lazima uipime kisiasa na sio kutafsiri maneno kwa emotions, siasa hazitaki emotions bali kuelewa ujumbe unamlenga nani na kwa sababu gani na UWAZI ndio utoa picha kamili. Tunapozungumzia Mabepari haina maana kila tajiri ni bepari isipokuwa lengo ni kuzungumzia UNYONYAJI, isiwe kia tajiri achukie hoja pasipo kutazama walengwa.

Mwanzo ulisema alikuwa anamaanisha Lissu, Lema na Msingwa!

Sasa hivi umebadilika tena imekuwa mikoa. Haya sasa swali kwako

Kigoma waliacha lini kutoichagua CCM na mikoa mingine iliacha lini?
 
Hivi u Ukaskazini mnautoa wapi?maana nautafuta siuoni, nimesoma maelezo ya Zitto sioni, ndio maana nazidi kupata mashaka sana na Utanzania wa baadhi yetu, maana kutafsiri jambo la kisera na kimfumo kwa muktadha wa Ukaskazini?hii inasikitisha sana.

Na kingine hiki kinanishangaza zaidi, kwanini Lindi isiwe issue?maana alipotaja Kilimanjaro ndipo alipotaja Lindi pia?sasa kwanin iibuke hoja tu ya Ukaskazini lakini isiibuke hoja ya Ukusini?kuna tatizo kubwa hapa.

Ni wazi kuwa kuna watu wanatafuta excuse ya kuonyesha jinsi wasivyo wa-taifa kwa kulazimisha ata kisichokuwepo.Tunahitaji kuondoa hii kitu mioyoni mwetu, maana wakati mwingine unaweza ukakiona kitu sio kwa sababu kipo kwa mwingine bali ni kwa sababu kipo ndani yako.Hiki tukiondoe!!

Na pia tusiwawekee watu maneno ambayo hawajayasema, mfano wa Ukaskazini na chuki kwa Ukaskazini, kama tunahitaji Ukaskazini tuseme wazi kama Nassari, tusiwasingizie wengine. Ebu tulishike neno hili la busara la Alinda hapa chini.

Hayo ya power struggle ndani ya Chadema sio rahisi kwetu ku-conclude lolote.

Kwenye taasis yeyote kuna vitu vya ndani ambayo kwa mtu asiye kwenye inner-cycle hawezi kujua. Ndivyo ilivyo ngumu kwangu na labda kwetu juu ya hayo ya chumba cha ndani cha Chadema.

Ni vizuri tu tuweke benefit of doubt kwa pande zote kisha tusonge mbele.

Hakuna mtu yeyote utamsikia analalamikia Usingida wala U-Iringa.Mtu yeyote atatambua kuwa kauli hiyo ni ya kisiasa dhidi ya Msigwa na Lissu.

Nguruvu, Alinda: Najua mu watu makini sana, na yawezekana kabisa mna Utanzania ndani yenu.Lakini kauli hizi humu ndani badala ya kujenga zitazidi kujenga utengano wa kijamii.

Kuna watu humu wanaosoma ambao kwa maelezo ya humu watapata picha tofauti na badala ya kujenga ndio kwanza tunabomoa zaidi.Tusiwe watetezi wa Kanda.Tuwe wa Tanzania kwanza.

Nilitegemea huu ushauri umpe mtoa matamshi.. kumbe ushauri tunapewa sisi ambao tunataka kujua ukweli wa hizo kauli. Kama mpaka hivi sasa hata wewe uelewi nini madhumuni ya hizo kauli ndo hivyo hvyo wananchi wa Kigoma, Iringa, Singida na Arusha nao wako gizani.

Kapwela,

..Tundu Lissu anajulikana kuwa ni mwanaharakati toka yuko JKT.

..aligombea ubunge mara ya kwanza mwaka 95 kupitia chama cha NCCR.

..kwenye suala la kutetea haki za wananchi kuna watu wachache sana wanaolingana na Tundu Lissu.

..kwa mtizamo wangu ktk suala la harakati za kutetea maslahi ya wananchi, Tundu Lissu ni mlima kilimanjaro na Zitto ni kichuguu.

cc Alinda, Mkandara, Mchambuzi, Nguruvi3

JokaKuu,

Kwako Zitto uwa ana jema hata moja sijawahi kukusoma ukimuandika kwa mema hata siku moja wakati mwingine uwa nacheka peke yangu.

Kwako Zitto anaweza kuzidiwa hata na Dovutwa.
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu,

Kwako Zitto uwa ana jema hata moja sijawahi kukusoma ukimuandika kwa mema hata siku moja wakati mwingine uwa nacheka peke yangu.

Kwako Zitto anaweza kuzidiwa hata na Dovutwa.

..Zitto ana akili, ila tatizo lake ni papara.

..pia nadhani he is very poor at choosing his friends.

..alifanya makosa kujiweka karibu na makundi yanayoporomosha matusi na kashfa dhidi ya CDM na mwenyekiti wake.

..CCM kuna maprofesa na ma-dr wa kimataifa, lakini hata siku moja hutasikia wakiandika majarida kwamba mwenyekiti wa CCM ana akili ndogo na elimu ya hovyo-hovyo kulinganisha na wao.

..kwa nafasi aliyofikia Zitto ndani ya CDM angeacha madaraka yamfuate na siyo kuanza kutafuta madaraka ktk chama.

..mfano mzuri wa kuigwa ni Dr.Slaa. Yeye amechapa kazi tu ktk nafasi yake kiasi he is more influential ndani na nje ya chama kuliko hata mwenyekiti wa CDM.

cc Alinda, Mkandara
 
Last edited by a moderator:
[/COLOR]Nilitegemea huu ushauri umpe mtoa matamshi.. kumbe ushauri tunapewa sisi ambao tunataka kujua ukweli wa hizo kauli. Kama mpaka hivi sasa hata wewe uelewi nini madhumuni ya hizo kauli ndo hivyo hvyo wananchi wa Kigoma, Iringa, Singida na Arusha nao wako gizani.
Maneno yako hapa chini ni maneno sahihi sana nawe pia kuyashika.
Alinda

  • Wakati mwingine jamani kuweni na aibu.. Wewe ni watu wazima, kaka au baba hivi unapokuja kwenye mtandao na kumuekea mtu maneno mdomoni ambayo hajasema unakuwa na nia gani?

Nimetoa mifano ya Obama kwa sababu inaendana na tunachofanya hapa, siasa za dunia zinafanana sana, ni kama tu copy and paste kutoka sehemu moja kwenda nyingine, https://www.youtube.com/watch?v=DLgm1I8bVVE, watu wanachukua vitu visivyo vya msingi wanavitafsiri wanavyotaka alafu wanavifanya ndio issue na kuvikomalia,ili siasa zetu ziishie hapo hapo, kwenye vitu vyepesivyepesi.

Hili suala la maendeleo kwa mfano, lilikuwa la msingi sana, na lingepaswa kuibua mjadala wa namna bora ya kuleta maendeleo, la msingi sana, sasa sijui mtu anawezaje kuja na Ukaskazini kwenye hoja ya kitaifa kama hii? nani kalileta hili?ni mioyo ya baadhi yetu ambayo either ina upungufu wa Utanzania na walioujaza ukanda mioyoni mwao. Na kwakuwa hawawezi kujisema wazi, wanasingizia hoja ata isiyohusika ili kujipa uhalali wa kuzungumzia matamanio ya mioyo wao.

Bahati mbaya sana, badala ya kujadili juu ya namna gani nzuri ya kusambaza maendeleo hayo mikoani, tunabaki hapa tunajadili Ukaskazini wetu, hatujisaidii sisi,hatuzisaidii siasa zetu, na hatulisaididi taifa letu.Tuache njia hii, inapanda mbegu mbaya.

Kuna watu waliokuwa hawajui kama kuna kitu kinaitwa Ukaskazini, humu ndani wamejengwa moyo wa uzawa wa Kaskazini.

Kuna watu ambao Tabora ni wako, Moshi ni kwao, Mtwara ni kwao, hapa wameonyeshwa kuwa labda sio sahihi sana kulazimisha mikoa yote iwe na maendeleo, wameambiwa mikoa mingine iridhike iwe ilivyo, watajiuliza maswali,kwanin??kwanini watu hawataki hiki??

Yawezekana kabisa ata hatuna mawazo haya, lakini bila kujijua hizi mbegu zinapandika.Tunaambukiza watu.Tuepuke kutenganisha watu.

Yawezekana kabisa kuwa hatupendi kabisa siasa za Zitto,ni haki ya kila mtu,yawezekana tunataka kila hoja yake ionekane ni mbaya, ni haki yetu kabisa.Lakini ebu tujue sehemu ya kupambana nae kwenye siasa bila kujenga chuki na kugawanya watu.hapa mlipopachagua kupambana nae sipo.Panabomoa taifa letu.Mtafuteni angle zingine kisiasa.Sio hii.

Nakumbuka Mwalimu Nyerere na story yake ya Geroge Kahama(sio direct quotation)
.................................................................................................................................................................
George kahama alikuwa amepanda ndege, kaenda mikutano ya kimataifa
ndege ikatikisika mara ya kwanza, George Kahama akaguna...My God...(mtu wa kimataifa)...
ndege ikatikisika zaidi mara ya pili -- George Kahama akaguna ..(Mungu wangu)..(karudi kwenye Utanzania)
Ndegu ikatikisika kwa nguvu zaidi mara ya tatuu -- nikamsikia george akipiga kelele -- maweeeee(kaisharudi kwenye kabila lake)!!!!!

JK Nyerere
................................................................................................................................................................
Kwenye mambo ya kutetea Kanda zetu badala ya taifa ebu tupige break.Hayatusaidii kama taifa.

Ata hilo la lugha ya picha, watanzania wanajua sana lugha yao ya kiswahili, na wanajua jinsi lugha hizi zinavyotumika kufikisha ujumbe kwa hadhira.Wala haiwasumbui, na ndio maana ata Lema aliposema wa dar es salaam, waliishia kucheka tu, ndivyo Watanzania tulivyo, Watanzania hawa mioyo yao ni misafi sana, hawawezi haya tunayotaka kuyapanda.
 
Mwanzo ulisema alikuwa anamaanisha Lissu, Lema na Msingwa!

Sasa hivi umebadilika tena imekuwa mikoa. Haya sasa swali kwako

Kigoma waliacha lini kutoichagua CCM na mikoa mingine iliacha lini?
Ni kituko kusema 'wananchi wa Mara'' ukimaanisha Wasira

Ni kituko kusema ' wazanzibar'' ukimaanisha Maalim Seif

Ni kituko kusema Wananchi wa Pwani' ukimaanisha JK

Hapa watu wakubali kuwa Zitto hakuchgua maneno vizuri. Na kwamba, ni wachache katika jamii wanaoweza kutafsiri kauli yake. Tumeona jinsi kauli yake ya Shinyanga ilivyopokelewa kule jukwaa la Siasa. Mambo yalikuwa Uchaga, usukuma, unyiramba badala ya Utanzania.

Nadhani Kapwela angetenda haki kwa kusimama katika ukweli na si kuficha uvundo chini ya kapeti

Hivi Zitto anaweza kusimama katika jukwaa Singida akawananga wananchi wa Singida au iringa na kisha wananchi wakaelewa anazungumzia Msigwa na Lissu? Jamani spedi iitwe spedi na siyo kijiko kikubwa
 
Back
Top Bottom