Lugha hazitafsiriwi hivyo, kwa mtazamo wako huo kama nilivyokwisha kwambia mwanzo basi maana ya kipande hiki cha Obama,
"You can put lipstick on a pig. It's still a pig." ― Barack Obama
Kwa tafsiri yako hapo
bold basi ungesema Obama kamtukana mtu kamuita nguruwe.
Hutuitaji kutafsiri "Wakati watu wa Kigoma wanapigwa mabomu kwa kutaka mageuzi watu wa ARusha, Singida, Iringa walikuwa wanakumbatia watawala.. hapa hakuna lugha ya picha bali ni ujumbe wa moja kwa moja kwenda kwa watu wa Iringa na nk.. "Laiti kama angesema baadhi ya watu" "bila kutaja mikoa" hapo walau tungeweza kusema anawalenga wabaya wake ambao ni viongozi wa Chadema. Kitu ambacho ni kawaida kwa siasa zetu za maji taka.
Lakini unapotaja watu wa sehemu fulani wako hivi au vile huwezi kusema hii ni lugha ya picha iwe umeitaja kwa mbaya au kwa mazuri.
Pia bado sijaona uhusihano wa speech ya Obama na speech za Zitto , Obama ametumia msemo na huu msemo ameutumia kwa kumlenga mtu mmoja ambaye kila mtu ni anamfahamu kuwa ni Bi.Hilaly. Hebu niambie kama huu msemo angeutumia kwa kumaanisha wakazi wa Mississipi au Carifornia hali ingekuwaje? Na hapo ndo point yangu ilipo kuwa iwe ni lugha ya picha kama unavyotafsiri yaani uongo au laa swali langu liko pale pale ni kweli watu wa Iringa, Arusha na Singida wanamidomo mrefu au ( waongo) (lugha ya picha)? Na hapa ndio tunarudi kwenye point yangu ya juu, kwamba tatizo si hiyo lugha aliyoitumia, tatizo ni walengewa wa hiyo7hizo kejeri. Laiti kama angesema baadhi, au akamataja Slaa, Mbowe na nk wala kusingekuwa na mjalada wa makabila mengine vs wachaga kama tulivyoona katika jukwaa la siasa au facebook wall ya Zitto.
Thread hii imekuwa ya uhamasishaji na utetezi sio wa taifa bali wa Ukaskazini, ulinzi wa Kaskazini, ndio unaweza ukaona hapo jinsi Lindi iliyotajwa pamoja na Kilimanjaro inavyotupwa ili kujenga Ukaskazini bila kujali kuwa njia hiyo ni hatari kwa taifa.
Hoja nzima imesimama kwenye hisia,hisia zipi..mnaziumba wenyewe, na kuzifinyanga wenyewe..huyu atakuwa ana chuki tu,chuki zipi?hamuwezi kuonyesha.Mtaishia tu kwanin ametaja jina la mkoa wetu?what?ndio maana nimeuliza ni lini kutaja jina la mkoa imekuwa kosa?imetajwa LIndi imekuwa sawa lakini kwanin kataja Kilimanjaro?kwanin kataja Arusha?what??you guys!!
Laiti kama ungetumia lisaa limoja kusoma thread hii kama nilivyokushauri hapo mwanzo (ingawaje lisaa limoja halitakutosha) ungeona ulichoandika hapo juu, ndilo lilikuwa swali letu la msingi, kwamba kama Lindi ni ya 10 kimaendeleo hali katika uchangiaji wa pato la taifa ni kati ya mikoa inayochangia kiasi kidogo sana, sasa kwanini tusiangalie Lindi na Shiyanga na kujiuliza kama wanalindi wameweza kwanini wanaShy wasiweze? Ni point hiyo hiyo uliyotumia hapo kwenye nyekundu tuliyoitumia na sie (unaotuita wabaguzi) na kujikuta tunafikia hitimisho ilo ilo uliyohitimisha kwa maneno kali kwetu sisi badala ya Zitto.
Matokeo yake mkapeleka mjadala sehemu ambako haukuwepo, hakuna sehemu ata moja Zitto kazungumzia mkoa wowote kuunyonya mkoa mwingine?mnatoa wapi?mtasema mmetafsiri..kutafsiri kutoka wapi??..ni kutoka kwenye yaliyojaza moyo yetu na kumsakizia ambaye hajasema popote, hakuna popote,popote Zitto kazungumzia kuna mkoa unaunyonya mkoa mwingine,hakuna!!Mtatoa tafsiri zenu kwa mnayoyataka ninyi,na kuziumba, na matokeo yake mnazidi kuwagawa watu.Hili ni ninyi ndio wenye tatizo.Ni ninyi ndio mnaouumba ukanda humu.Acheni hili jambo
Ni kweli mjadala umekuwa mpana na upana wa huu mjadala umejenga kwa kiasi fulani pale ambapo Zitto alijaribu kupabomoa. Maana tumeona si kweli kwa maendeleo ya Mkoa fulani kigezo chake ni uchangiaji wa pato la taifa pekee, bali ni pamoja na historia na eneo husika,ardhi,mwamko wa maendeleo ktka eneo husika, elimu na nk. Ni matumaini yangu kuwa, wale watu waliokuwa na hisia kuwa "wachaga wanakwapua fedha za mikoa fulani na kuzipeleka makwao na ndo maana wanakuwa na maendeleo zaidi ya maeneo mengine, wameelewa kuwa SI KWELI BALI WATU WA ARU/KILI MAENDELEO YAO YAMELETWA NA JUHUDI ZAO IKISAIDIWA ZAIDI NA HISTORIA YA ENEO LAO.
Hivyo basi utakubaliana na mimi kuwa huu mjadala umejenga zaidi umoja kuliko ule mjadala uliokuwa katika "JUkwaa la siasa" ambao watu walikuwa na hasira za wazi kuhusu "wachaga" , Wamedhalilishwa, kuna watu walienda mbali zaidi na kusema kuwa wanakwapua pesa za maendeleo ya mikoa mingine wanapeleka kwao, kuwa wachaga wamejazana TRA na nk. Kitu walichosahau hawa watu ni kuwa Arusha /Kil hawaishi wachaga tu bali "watanzania wote.
Na jambo la kusikitisha si wewe niliyekuona katika huo mjadala ukikemea kwa ukali ubaguzi wa wazi ulionyeshwa na asilimia kubwa ya wachangiaji ktka mjadala huo bali ulikaa na kunywa Chai, au soda au bia huku huku ukushangilia kuona watanzania wenzako wakidhalilishwa kutokana na kauli za fitina na chuki za Zitto.
Na kwa bahati mbaya sana au kwa makusudi Zitto aliona reaction ya watu juu ya kauli yake si JF peke yake bali hata FB,Instragram na nk. Lakini hakujitokeza kusema "jamani sikumaanisha hivyo au sikujua kuwa watu wangechukulia hivi bali nimaanisha hivi na vile.. Huyu Zitto ambaye ni mzalendo, ambaye ana akili kuliko watanzania wote, ambaya ana siasa za hoja haijawahi tokae Tanzania alikaa kimya akifurahi watu wakibaguana na kudhalilishana.
Ila tatizo lako ni baada ya Nguvuri3 kuona hizo sitofahamu na kuamua kutumia muda wake ambao labda angeutumia kufanya shughuli zake za kujiongeza kipato na kuleta hoja hapa ya kupingana na Zitto juu ya fitina zake na uongo. Ila kwa macho yako huyu mtu amekuwa mbaya na ndo mchongashi, mkanda na nk. Lakini aliyetamka hayo maneno hamgusi.
Hivi kweli wewe unauchungu na ubaguzi au una "act tu???
Nikukubushe aliyeleta kauli ya Arusha Kili vs Shinyanga si Alinda wa Nguruvi3 ni Zitto Kabwe...
Pia nakupata changamoto: Hebu nenda Shinyanga kaa na wazee/vijana na wambie kuwa " Aisee mnafahamu Mikoa yenye maendeleo ni Dar, Arusha na Kilimanjaro, mikoa inayochangia katika pato la taifa Shinyanga inashika No.4 (ok naelewa hawa watu hawaelewa nini maana ya pato la taifa ila wataelewa kinachoongelewa ni kuhusu mambo ya fedha) wakati ARusha inachangia ikiwa no.6 na Kili no.9..ukishamaliza ondoka bila kutoa ufafanuzi unachotaka kueleza ni nini, baada ya hapo rudi tena, majibu utakayo yapata hayatakuwa na tofauti na yale ya jukwaa la siasa "wachaga ni wezi, wanapendelea kwao na nk.
Pia nakupa chamgamoto no.2 (natumaini utakuwa muugwana na kizifanyia kazi ili kupeana darasa) Naomba unionyesha mstari mmoja au paraghafu moja yangu au ya Nguvuri3 ambayo wewe umeisoma kama mwana Tarime (kuhusu Tarime ni mfn tu) na kupata hisia ya kubaguliwa. kikanda au vyovyote vile.