Wanjamvi hebu pitieni hapa
Kwa hisani ya gazeti la Nipashe na MwandishiG.Mushi (tunashukuru)
Wanakijiji Nronga wajifunga kuweka lami barabara yao
Tumeliweka bandiko hili makusudi kuonyesha, tunachozungumza si maneno kuna ushahidi usio na shaka
Kiongozi mkuu anasema '' Kilimanjaro na Arusha ni namba 9 na 7 katika kuchangia pato la taifa, hata hivyo zipo juu kwa maendeleo''.
Kwanza, hakueleza nafasi za mikoa hiyo katika kile anachoamini ni maendeleo.
Amezungumzia jumla tu ili wasikilizaji waamue kama ni namba 1, 2, 3 n.k.
Katika uchangiaji ameonyesha namba ili kuleta hisia kwa wananchi kuwa mikoa hiyo ina mchango mdogo lakini ipo juu
Maana yake, alichotaka kuwaeleza wananchi ni kupanda hisia za kwamba sehemu hizo ima zinapendelewa, zinajaipendelea au zina namna ambayo si njema katika kufikia maendeleo
Katika uzi huu (
Kapwela rudi nyuma ukasome kwanza) tumeeleza dhana nzima ya maendeleo na vichocheo vyake.
Kwa ufupi tumeeleza maendeleo si kitu kinachowekwa katika kontena na kusambazwa.
Ni matokeo ya vigezo vingi, vingine vikiwa nje ya uwezo wetu wanadamu.
Maendeleo hupatikana pale tu fursa iliyopo inapokutana na jitihada.
Dhana ya kusambaza maendeleo sawa nchi nzima kama anavyodai
Mkandara na wengine wanaomtetea kiongozi mkuu inakosa mashiko kwa kuangalia mfano huo wa wananchi wa Nronga.
Ukisoma habari hiyo, kila kaya inachangishwa na wale walioko nje ya mkoa wanachangishwa ili kujenga barabara wakisaidiana na mbunge na Mkandarasi ambaye inaelekea ana ukaribu na maeneo husika. Halmashauri imeshirikishwa pia bila kujali itikadi za kisiasa
Kwa mtazamo wa watu wasio na maono kama kiongozi wetu mkuu, hayo si mambo ya kuzingatia.
Muhimu ni kuangalia nani amechangia nini na amepata nini. Ndio dhana anayohubiri Mkandara hapa pia.
Kuwa wananchi wa Nronga wanaochangia kodi katika hazina, hawapaswi kupata shea yao.
Kinachotakiwa ni kusambaza maendeleo sawa kwa kuchukua wanaokjiletea maendeleo na kusambaza kweingine
Dhana hiyo ina maana ya wananchi wa Nronga wapewe kidogo kwasababu tayari wanajijengea barabara, na kwingine waliko na 'midomo mirefu kama asemavyo kiongozi wetu mkuu'' wapewe zaidi ili wanyanyuliwe
Kwa kipande hicho mnaweza kuona sehemu ndogo ya kwanini sehemu nyingine zimeendelea zingine zipo nyuma.
Mfano wa kijiji cha Nronga ni sehemu tu ya kazi wanazofanya wananchi wa mikoa mingine za kujiletea maendeleo
Hatuwezi kukaa kimya wanapotokea wanasiasa uchwara wakileta takwimu za kupumbaza wananchi, huku wakiwaficha ukweli
Leo wananchi wanakaa wakipiga soga kufyeka barabara wakati wenzao wanapasua miamba kujenga barabara.
Halafu wenzetu wanaamini takwimu zinateremka kama mvua na kwamba sasa ni wakati mikoa yenya maendeleo iwekewe spidi gavana isubiri ile inayoahidiwa pepo na viongozi walaghai.
Watu wamekimbia ukweli wa makala hiyo wakijua ni mwiba unaoua hoja zao za maendeleo, upendeleo na zaidi kuonyessha kuwa kuna chuki inayosambaza na viongozi waliofilisika kisiasa makusudi.
Kwa makala hiyo atokee mtu atuambie tena Shinyanga ina matatizo kwasababu wananchi wa Nronga wanajijengea barabara.
Atokee mtu atuambie matatizo ya Kigoma yanasababishwa na wananchi wa Nronga wanaojenga barabara kwa nguvu zao
Tusemezane