Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Duru za siasa: Chama cha ACT-Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani(?)

Swali lenu nireference za hotuba ya supreme leader. Mumeuliza sana na mara nyingi.
Tuliwajibu kiutu uzima tukidhani mna ufahamu, Sasa mnaona hoja zenu wenyewe zinawanyanyasa mnabadili goli.

Anayehamisha goli ni nani kama sio huyu hapa chini?

Eti mnataka hotuba aliyosema maneno hayo.
Hatuwezi kusoma maneno ya supreme kama msahafu au bibilia au kasuku.

Miezi miwili baada ya mjadala ndio unakiri kuwa hoja sio Zitto aliongea hivyo(kiutu uzima hapa unakiri kuwa msingi wa hoja hii sio hotuba ya ZItto kwa maana hakusema).

Lakini kwani basi hukusema mapema?maana muda wote unabase kwenye ubaguzi, umejikita ZITTO KASEMA, ombeni basi msamaha kwa kuwa-mislead watu kwenye hili.

Ajabu, baada ya kujitoa kuwa issue sio Zitto kasema,unarudi tena

Maana ya mjadala ni kutafuta ukweli wa maneno. Msihamishe goli subirini ni wape reference muonekane viumbe fulani. .

Kuutafuta ukweli wa maneno yepi tena?juu umesema issue sio Zitto kasema nin, hapa tena (kwa lugha yako mwenye unahamisha tena goli), unasema kuutafuta ukweli wa maneno(bila shaka ya Zitto tena juu ya ubaguzi).

Ndio maana nikakwambia kwa kuwa umebase kwenye maneno ya Zitto kueneza chuki kwa mkoa wa Kilimanjaro(kwa lugha yako kama msahafu, kwa reference kuwa Zitto kasema), basi unapaswa ufanye haya ili hoja zako ziwe na nguvu.

1.Thibitisha kuwa Zitto kasema mkoa wa Shinyanga/Tabora unanyonywa na mkoa wa Kilimanjaro.

2. Thibitisha kuwa Zitto kasema umaskini wa Shinyanga/Tabora unatokana na mkoa wa Kilimanjaro.

3. Thibitisha kuwa Zitto kasema kuwa mkoa wa Kilimanjaro unapendelewa.

4. Thibitisha kuwa Zitto kasema mgawanyo wa mapato ya serikali ndio MSINGI PEKEE WA MAENDELEO YA WATU.

KEY HAPA NI PEKEE,huko nyuma umejibu swali hili bila kulielewa.Hakuna sehemu Zitto aliposema kuwa MGAWANYO WA MAPATO YA SERIKALI NDIO MSINGI PEKEE WA MAENDELEO, huu ni mfano wa propaganda mbovu zilizojengwa humu..

Haya hayakwepeki maana ndio reference yako wakati wote.

Najua umeshindwa kuthibitisha maana hakuna yeyote aliyesema hayo, badala ya kukiri hilo unaanza story ndeefu ili kuchanganya watu ili wasijue kuwa umeshindwa kuthibitisha.

Note, Point namba 4: Hii haihusiani na hoja za Mchambuzi na Barubaru na wengine juu ya takwimu na maendeleo, hivyo usije ukasumbuka kuleta data zilizohusika, shika hili neno MGAWANYO WA MAPATO NI MSINGI WA PEKEE WA MAENDELEO?rudia PEKEE, Zitto hajasema hilo.

Ni hivi
Hoja imeanzia jukwaa la siasa. Ikazungumzwa kwa kina duru zasiasa.
Mchambuzi akaleta credible information zake kutoka katika hotuba ya supreme

Mchambuzi kaleta data za uhakika (Bandiko 427)

Mkandara akaunga hoja tena akimlaani supreme kwa kauli chafu(Bandiko433)

Mkandara kaendelea na hoja bandiko 439, 443 akionyesha kutokubaliana na supreme

Mkandara kaja na data zake kutoka serikalini
Zakumi akachangia akilaani maneno ya supreme leader kutokanana vigezo.
Tena akaenda mbali na kuonyesha kwanini mkoa wa KM umeendeleatofauti na kauli za supreme leader
Waberoya katetea hotuba ya supreme leader na kufafanua

Wakuu wafuatao wamechangia hoja na kuchambua data zikihusisha mjadala wa maneno ya supreme.
Nawaomba waje hapa wanisute kama ninawasingizia

Mag3 gfsonwin Waberoya Jasusi JokaKuu Zakumi Alinda TUJITEGEMEE King Suleiman Barubaru
Adharusi kaja na takwimu namaelezo. Ritz kaunga mkono hoja yaAdharusi.

Story zote hizi niliishakujibu kwenye post yangu ile, kama ungeielewe usingerudi tena kujibu kwa story, nilikwambia haya.

Narudia tena, kumbuka wakati wote kuwa msingi wa mjadala huu sio Kapwela kasema nin,sio Mkandara kasema nin, sio Barubaru na sio Ritz kasema nini bali msingi wa thread hii ni either of the two, ACT IMESEMA NINI au ZITTO KASEMA NIN,kutolitambua hilo ni kuzidi kuthibitisha kuwa huna msingi wa hoja.

Hizo story kila mtu humu anazijua, huwezi kuthibitisha Zitto kasema kwa Fulani kasema, out of scope.Kama great thinker unabidi ujue hiyo first principle.

Sisi ni watu wazima, tupo katika jukwaa tunachambua kauli, takwimu na kila jambo. Hatumezi kama wengine.

Kutokana na upuuzi wa kumeza maneno bila kuyachauja, ndio maana watu walikubali katiba iandikwe kwa jina la mtu.
Yaani mtu awe katiba nasi watu.
Hatupendi kucheza nage na mduara wenu ili kupoteza maana ya mjadala.

Nadhani jukwaa litawapuuza si kwasababu tunasema, bali mnajidhihiri.

Msivunje hadhi ya jukwaa, kama hamna hoja kaeni kimya au nendeni mkasome mengine

Samahani wanajamvi, mjadala kuhusu ulaghai na udanganyifu wawanasiasa wa kizazi hiki unaendele.
Chama cha ACT mpini wa kumaliza upinzani

Najua huna hoja ya kujibu, sitashangaa ukikwepa maana huna ujasiri wa kukiri kuwa huna msingi wa hoja zako unazozishupalia kila siku hapa, .

Kumbuka, mjadala haujabase juu ya Uchumi na Maendeleo ujumla wake bali juu ya Zitto alichosema, ndio maana huna budi kuirejea check list ile kama bado unataka kujenga hoja zako juu ya Kilimanjaro,Kilimanjaro,Kilimanjaro.

Hoja uliyoikariri kila siku humu na kuimba kama "kasuku" na kuzifanya msingi wa shutuma zenu kwa ZItto na ACT.

Najua huwezi kuthibitisha ndio maana unajaribu kujificha kwa uwingi wa maneno, ungekuwa mkweli katika mjadala ungefanya nilichokushauri kufanya:

Kukiri udhaifu sio ujinga, kwenye hoja hii hauna msingi wa kuusimamia.

Ukiishakiri hivyo kuwa sio Zitto wala ACT wamesema ubaguzi huo, bali ni mjadala huru juu ya nchi ndipo utakuwa na authority ya kukwepa maswali yale na utatuisaidia nchi kuepukana na mbegu mbaya za Ukanda unazozipanda.

Na ukishakiri hilo tutakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kuendelea na mjadala wa wazi kama alivyoshauri Zitto kwenye hotuba yake ile kuwa
TUJADILIANE NAMNA YA KULETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI,TUJADILIANE!

Sasa hayo yako ya chuki na ubaguzi uliyospecialize nayo, yanayotokana na uzalendo wako kwa mkoa wako wa Kilimanjaro ni yako binafsi, sio ya Zitto wala ya ACT.

Nikushauri tu kuwa man enough kujionyesha wazi na sio kujificha nyuma ya migongo ya wengine.
 
Alinda,

Nafikiri ujaelewa swali hapo ( au labda nikuandikie kwa my mother language Kiarabu labda utanielewa ...joke.)

Dah Kiarabu hapo utanipa mtihani.

Kifupi hayo ulioandika hapo juu ni maneno ya ZZK?
Na kama ya ZZK aliyatoa wapi? utupe reference yako?

Hilo ndilo uliloulizwa na si lingine. Kwani kuna tuhumu Lukuki mnazozitoa zinazomuhusisha ZZK kuwa ni mbaguzi na mchochezi kwa kutoa kauli hizo. sasa kinachohitajika ni ile connection baina ya maneno hayo na tamko la ZZK.

Ndio hayo ni maneno ya Zitto ambayo mimi Alinda niliyaona kwa mara ya kwanza Facebook , Twitter, Instragam (Zitto) na hapa Jf. (hapo nimenyoosha na mkono juu kabisa yaani ninaapa maneno niliyosema ni ukweli na ukweli mtupu)

Na kama mimi ni muongo basi Zitto yuko humu aje akanushe. (huu ni mwenzi mtukufu wa Ramadhan hivyo natumaini atasema ukweli)

Naona hili andishi hata wewe linakutatanisha kama sisi. Na ndo maana tukasema aje atupe maana nyingine alikusudia nini? au hata wewe unaweza kutupa shule jinsi ulivyolielewa.

Pole sana
 
Last edited by a moderator:
Maendeleo na uchumi ni jukumu mtambuka, serikali ina sehemu yake kwenye uchumi na maendeleo, na kuufanya uchumi huo uguze maisha ya watu, kuunganisha shughuli za kiuchumi na shughuli za watu wa maeneo husika, kuna jukumu la uwezeshaji katika nyanja tofauti n.k.

Kuhusu kuubadili mfumo, unachosema hakina tofauti na alichosema Zitto, alisema tuufumue huu mfumo maana haiwezekani sehemu yenye potential kama ile ya Shinyanga ikae kwenye lindi la umaskini.

Haihitaji kuwa mchumi kujua kuwa kama mkoa A una mchango mkubwa wa pato la taifa maana yake una uchumi wa jumla mkubwa, na kama mkoa B wenye mchango mdogo maana yake una uchumi wa jumla mdogo kuliko mkoa A. Sasa kama mkoa wenye uchumi mdogo una maendeleo ya watu makubwa kuliko mkoa wenye uchumi mkubwa maana yake kuna kuna potential ya mkoa A pia kuwa na maendeleo makubwa.Simple!

Maana yake huo uchumi wa A hauna uhusiano na mwananchi wa kawaida, ndio maana akaongeza kuwa miongoni mwa sababu ni kuwa Shinyanga wanategemea dhahabu ambayo haihusiani na mwananchi wa Shinyanga.Ndio maana kama nawe unavyokiri lazima tuboreshe mfumo wetu wa kiuchumi ili huu uchumi umguse pia mwananchi wa kawaida. Hili ni jambo la kimfumo kuliko tulikolipeleka kwa hisia zetu hizi.Hatukuwaza hivi kwa sababu tu ya hisia zetu binafsi kama nilivyosema mwanzo.

Hakuna mwanasiasa yoyote aliyesema wananchi wa mkoa fulani wana shida kwa sababu ya mkoa mwingine na hakuna yoyote aliyesema kuna mikoa inapendelewa.

Hakuna kitu kipya ambacho hatujaeleza hapa.. Tusome huko nyuma uliyoeleza ndicho na sisi tumeeleza haya unayoyafanya ni marudio tu.

Pia epuka hizi lugha,hakuna mkoa wowote ambayo wananchi wake ni wavivu na ambao wananchi wake wana fikra tegemezi, wala hakuna mkoa wowote ambao wananchi wake ni wajuzi na mahiri kudai haki kuliko mkoa mwingine. Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo thread hii imefanikiwa sana na kuishia kukera watu na kujenga chuki ambazo zinaongeza hisia za kuvunja utaifa wetu, kumbuka hakuna mtu atafurahi kusoma hapa kuwa kwao ni wavivu na wenye fikra tegemezi kwa sababu tu hawatoki Arusha au Kilimanjaro.Tuangalie hizi lugha. Kote Tanzania wananchi wanajitafutia maendelo yao binafsi, lakini kuna changamoto mbalimbali na changamoto hizi wakati mwingine ni tofauti kutoka sehemu moja na nyingine, ndio maana solutions zake sio lazima ziwe universal.

Hacha kujenga hoja zako kwa maneno ya kuzusha, ni wapi nimesema watanzani wa wavivu? ni wapi nimesema watanzani ni tegemezi? onyesha ukishindwa kufanya hivyo basi uungwana ni kufuta ulichosema au ni kuomba msamaha kwa wana jukwaa..
Ni aibu kwa mtu nzima kuzusha vitu ambavyo havipo.

Mfano, kijana aliyeishia darasa la 7 arusha au kilimanjaro bado utalii unaweza kumgusa lakini kijana wa darasa la 7 aliye pembezoni mwa katavi nation park hawezi kuguswa kabisa na utalii, mazingira lakini pia priority za serikali kwenye kujenga miundo mbinu ya kuvutia watalii n.k.Hii inaweza kuleta tofauti ya maisha ya vijana hao wawili.

Huu ni mfano tu, kuna maeneo mengi ambayo yanaweza kuboreshwa kuchochea maendeleo pande zote za Tanzania.Kila eneo la Tanzania lina kitu ambacho kinaweza kikashushwa kuwagusa watu.

Kama kijana wa Kili anafaidika na Utali, swali la kujiuliza hapa je vijana wengine wa maeneo mengine wanaweza nao kufaidikaje na utali? Ndo Nguvuri3 kakutolea mfn kuwa vijana wa Katavi na wao wanaweza kufaidika na huu utali kwa kilimo, sanaa, washonaji nguo, Tshirt na nk na hivi vitu vitawezekana pale tu tutakapo kuwa na miundo mbinu. Itakuwa ni maajabu ya ulimwengu vijana wote wa Tanzania nzima kwenda Kili kwa ajili ya kupata ajira katika soko la utalii.Hiki kitu nicho Nguruvi3 alikuwa anaeleza lakini wewe kwa hisia yako na zile spinning zako ukakipeleka sehemu nyingine.
 
Huki face mnapajua wenyewe. Ameeleza hivyo katika face, je ndivyo alivyosema katika mkutano? Kama anajisafisha sisi tuamini tu kama mazuzu

Usibebe kitu bila tafakuri ni hatari sana

Alinda.

Unaweza kuaapa viapo vyote lakini hapa ukumbini bahati mbaya au nzuri hawataki mambo ya Facebook kama anavyosema mkuu Nguruvi3.

Msome kwa makini Nguruvi3 hapo juu anavyotoa angalizo kuhusu Facebook.

Ahsante...
 
Last edited by a moderator:
Dada alinda sikiliza
Maneno ya kupendeza
Mjadala umeongoza
Kwa bandiko la Facebook

Mwenzio Nguruv twamsemeza
Majibu aje kutueleza
Kama ya Facebook hataki
Rejea yake ameipata wapi?

Sisi tuna subira
Twamsubiri bila papara
Ajenge hoja imara
Kwa ushahidi wa rejea!
 
Mimi nafikiri Alinda anaweza kuwa na majibu mujaraab kwa mushkira huu. Labda atuweke wazi maneno haya Chini ameyatoa wapi? atupe ref.

."Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
-16.9% Dar
-9.2% Mwanza kabla haijagawanya
-7.3%. Mbeya
-6%. Shinyanga
-5.3% Iringa
Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa, mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.

[/B]
[/FONT]
Ndio hayo ni maneno ya Zitto ambayo mimi Alinda niliyaona kwa mara ya kwanza Facebook , Twitter, Instragam (Zitto) na hapa Jf. (hapo nimenyoosha na mkono juu kabisa yaani ninaapa maneno niliyosema ni ukweli na ukweli mtupu)

Na kama mimi ni muongo basi Zitto yuko humu aje akanushe. (huu ni mwenzi mtukufu wa Ramadhan hivyo natumaini atasema ukweli)

Naona hili andishi hata wewe linakutatanisha kama sisi. Na ndo maana tukasema aje atupe maana nyingine alikusudia nini? au hata wewe unaweza kutupa shule jinsi ulivyolielewa.

Pole sana

Kwa kuwa source sasa ni facebook/instragram, basi ngoja tukusaidie.

Taarifa kwa ujumla wake hii hapa, ALINDA ALICHOFANYA NI KUUNGANISHA VIPANDE VYA BLUE NA KUACHA SEHEMU ZINGINE ili kujenga taswira aliyoikusudia, sio jambo sahihi kufanywa kistaarabu.Labda ndio maana imekuwa ngumu just kucopy hiyo taarifa na kuiweka hapa.

Barubaru na wengine, sitaki na mimi niwachagulie pa kusoma,someni yote wenyewe bila kukata wala kuongeza popote
.................................................................................................................................................................

Zitto Kabwe

April 5 · Dar es Salam, Tanzani

Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.

Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu

Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.

Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.

Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.

Mikoa 9 nchini ina idadi ya watu zaidi ya 2m. Dar, Mbeya, Tanga, Morogoro, Mwanza, Tabora, Kagera, Dodoma and Kigoma. Mikoa hii ina 52% ya Watanzania wote

Wakati Dar inachangia 16.93% ya katika Pato la Taifa, inaongoza kwa makusanyo ya kodi ambapo inachangia 81% ya Mapato yote ya Serikali. Kwa makusanyo ya Kodi mkoa wa pili ni Arusha na wa tatu ni Tanga.

Dar, Arusha, Tanga, Mwanza na Kilimanjaro huchangia 90% ya mapato yote ya Serikali nchini

Shinyanga inaendelea kushangaza sana. Wakati inashika nafasi ya nne kuchangia Pato la Taifa (6% of Tanzania GDP), inashika moja ya nafasi ya chini kabisa kuchangia Mapato ya Serikali ( 0.46% of total tax ). Unajua sababu? Shughuli nyingi za kiuchumi za Shinyanga hufanyika Shinyanga lakini kodi zake zakusanywa Dar es Salaam. Mfano migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, kodi zake zinalipwa Dar es Salaam

Mkoa wa Njombe ndio unaongoza kwa kuwa na watu wengi virusi vya ukimwi. 15.4% ya watu wa Njombe wenye umri kati ya 14 - 49 wanaishi na virusi vya ukimwi. Mkoa unaofuata ni Iringa wenye 10.9% ya watu wake kuwa na virusi vya ukimwi.

Dodoma, Manyara na Tanga ndio mikoa yenye watu wachache zaidi wanaoishi na virusi vya ukimwi

Mkoa wa Simiyu ndio mkoa wenye watu wachache zaidi wenye elimu ya sekondari ambapo 3.7% ya watu wa Simiyu wenye umri wa zaidi ya miaka 25 wana elimu ya sekondari. Dar es Salaam ndio mkoa wenye watu wengi zaidi wenye elimu ya Sekondari, 29%

Katika kodi zote zinazokusanywa Dar es Salaam, 75% zinatokana na forodha, 16% kodi ya mapato na 9% kodi ya ongezeko la thamani (VAT). Dar inachangia 81% ya makusanyo yote ya kodi nchini. Hii inaonyesha kuwa Watanzania wengi sana hawalipi kodi. Utegemezi kwenye forodha ni hatari sana kwa uhai wa nchi yeyote.

" there appears to be a disconnect between economic growth on the one hand and human development on the other" Tanzania Human Development Report 2014

Takwimu zote ninazoweka hapa toka jana zinatoka katika Tanzania Human Development Report 2014. Taarifa imesheheni kwa kweli

Tofauti ya Kipato miongoni mwa wananchi (Inequality) ni jambo linalokosekana kabisa kwenye uchambuzi wa Taarifa ya Maendeleo ya Watu ( THDR 2014). Ninadhani moja ya hatari kubwa nchini ni kuongezeka kwa pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho. Sifa ya sasa ya uchumi wa Tanzania ni 'kufaidisha wachache na kufukarisha wengi'
.................................................................................................................................................................

Well , hapa ndipo unapizidi kuonyesha uongo , uzushi na jinsi mnavyohangaika kuweka maneno. Kwanza, nuikupongeze unarudi kusoma kama tulivyokushauri.

Tatizo husomi kwa fact unasoma ukiongozwa na hisia za kutaka kuandika tu

Ukweli ni huu

Unasema ;Nguruvi3 ndiye wa kwanza kuandika maneno ya ukabila tarehe 20 April''

Angalia sana hiyo tarehe halafu usome maneno haya ya wakuu wafuatao waliyoandika tarehe 19 April .
Unless sijui maana ya wa kwanza, tarehe zinakueleza
Ahsante @Alinda na King Sleiman

Ritz, haya tafuteni jingine ,mnatusaidia sana kupata ukweli na kujenga hoja

Inaaza tarehe 20 halafu 19 tehe tehe my foot!

[/QUOTE]

Swala la ukabila na Udini. Ni kitu kilichotaka Chadema na kwenda CCM vinginevyo.ila kwa bahati mbaya sana watanzania wengi wanafikri ni kutoka CCM. na kudhibitisha hilo msome Zitto wenyewe hapo juu "Thread ya Mahojiano na Zitto swali kuhusu Ukabila na Udini.. Sitaki kuwaharibia uhondo someni hapo..

Hata hivyo rangi zake hazijifichi, wambie Kapwela , Gamba la Nyoka au hata yeye mwenyewe Zitto walete/ailete video au audio wakati alipokwend Kigoma kwa mara ya pili. video zimefichwa kwa vile aliongea upuuzi mtupu. wakilete wataleta ile ya dk 3 nyingine zimefichwa. Ililetwa humu ndani Moderators waliiondoa haraka sana maana ilikuwa imejaa ukakasi.
Yeye amesema tena bila kupapasa macho kuwa ACT ni chama cha wana Kigoma.. na wanakigoma watembee kifua mbele maana hicho ni chama chao.

Mwaka 2010 wakati wa ubunge, katika wabunge wote zaidi 500 walioshinda na kushindwa hakuna mbunge hata mmoja aliyesema kuwa ameshindwa kwa ajili ya udini, au ameshinda wa kura chache kwa ajili ya udini, Ila ni Zitto pekee aliyesima alipata kura chache kwa ajili ya udini. andishi liko humu humu Jf. Sasa cha kujiuliza kama miaka yote watu wamechangua na kuchanguliwa bila udini, mwaka 2005 ulichanguliwa na watu wote, na katika kipindi cha uongozi wako wewe mwenyewe unaibua hoja ya kutopaka kura nyingi kwa ajili ya udini je swali rahisi tu ni nani kaleta udini ndani ya katika jimbo lako ndani ya miaka 5?

Huyu ndo Zitto

Ukiangalia hata Kapwela yeye aliwahi sana Dr. Slaa (padre) hawezi chakuguliiwa na waislamu.. Ilo neno Padre hakulitumia kwa bahati mbaya bali kwa makusudi yale yale ya udini.. Sasa ukimuuliza ni lini na wapi alikaa na waislamu wakamwambia hilo sijui kama atakuwa na jibu. Lakini cha ajabu huyu ndo anasema sisi ni wabaguzi.

Ritz anayesema wewe ndo mmeanza ubaguzi hakuna hasiyefahamu humu ndani kuwa ni mbaguzi mkuu, ni mchonganishi, yeye huwa anafurahi kuna migorogoro ikishamiri miongozi mwa 'Tanzania na huwa anasema ni mimi ninachochea kuni" na si ajabu huyu ni mtu mzima. Tunarudi kwenye ule msemo kuwa nyani haoni ....

Ukirudi hata kwenye waraka dini ilikuwa ni kigezo kimoja wapo cha yeye kuwa mwenyekiti.

Ila hawa wafuasi wake hayo hawayaoni bali wanachoona ni Alinda na Nguruvi wabaguzi, ukiwambia leta andishi la kibaguzi haina nayefanya hivyo anayejitutumua kufanya hivyo anajitungia maneno yake kichwa na kutulisha.
 
Kwa kuwa source sasa ni facebook, basi ngoja tukusaidie kukuletea hapa.

Taarifa kwa ujumla wake hii hapa, ALINDA ALICHOFANYA NI KUCHAGUA TU VIPANDE VINAVYOUNGA BLUE NA KUACHA SEHEMU ZINGINE ili kujenga hoja mahsusi, sio japo sahihi kufanya.

Barubaru na wengine, ili sitaki na mimi niwachagulie pa kusoma,someni yote wenyewe bila kukata wala kuongeza popote.
.................................................................................................................................................................

Zitto Kabwe

April 5 · Dar es Salam, Tanzani

Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.

Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu

Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.

Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.

Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.

Mikoa 9 nchini ina idadi ya watu zaidi ya 2m. Dar, Mbeya, Tanga, Morogoro, Mwanza, Tabora, Kagera, Dodoma and Kigoma. Mikoa hii ina 52% ya Watanzania wote

Wakati Dar inachangia 16.93% ya katika Pato la Taifa, inaongoza kwa makusanyo ya kodi ambapo inachangia 81% ya Mapato yote ya Serikali. Kwa makusanyo ya Kodi mkoa wa pili ni Arusha na wa tatu ni Tanga.

Dar, Arusha, Tanga, Mwanza na Kilimanjaro huchangia 90% ya mapato yote ya Serikali nchini

Shinyanga inaendelea kushangaza sana. Wakati inashika nafasi ya nne kuchangia Pato la Taifa (6% of Tanzania GDP), inashika moja ya nafasi ya chini kabisa kuchangia Mapato ya Serikali ( 0.46% of total tax ). Unajua sababu? Shughuli nyingi za kiuchumi za Shinyanga hufanyika Shinyanga lakini kodi zake zakusanywa Dar es Salaam. Mfano migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, kodi zake zinalipwa Dar es Salaam

Mkoa wa Njombe ndio unaongoza kwa kuwa na watu wengi virusi vya ukimwi. 15.4% ya watu wa Njombe wenye umri kati ya 14 - 49 wanaishi na virusi vya ukimwi. Mkoa unaofuata ni Iringa wenye 10.9% ya watu wake kuwa na virusi vya ukimwi.

Dodoma, Manyara na Tanga ndio mikoa yenye watu wachache zaidi wanaoishi na virusi vya ukimwi

Mkoa wa Simiyu ndio mkoa wenye watu wachache zaidi wenye elimu ya sekondari ambapo 3.7% ya watu wa Simiyu wenye umri wa zaidi ya miaka 25 wana elimu ya sekondari. Dar es Salaam ndio mkoa wenye watu wengi zaidi wenye elimu ya Sekondari, 29%

Katika kodi zote zinazokusanywa Dar es Salaam, 75% zinatokana na forodha, 16% kodi ya mapato na 9% kodi ya ongezeko la thamani (VAT). Dar inachangia 81% ya makusanyo yote ya kodi nchini. Hii inaonyesha kuwa Watanzania wengi sana hawalipi kodi. Utegemezi kwenye forodha ni hatari sana kwa uhai wa nchi yeyote.

" there appears to be a disconnect between economic growth on the one hand and human development on the other"
Tanzania Human Development Report 2014

Takwimu zote ninazoweka hapa toka jana zinatoka katika Tanzania Human Development Report 2014. Taarifa imesheheni kwa kweli

Tofauti ya Kipato miongoni mwa wananchi (Inequality) ni jambo linalokosekana kabisa kwenye uchambuzi wa Taarifa ya Maendeleo ya Watu ( THDR 2014). Ninadhani moja ya hatari kubwa nchini ni kuongezeka kwa pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho. Sifa ya sasa ya uchumi wa Tanzania ni 'kufaidisha wachache na kufukarisha wengi'
.................................................................................................................................................................

Alifanya marekebisho baada ya watu kuja juu .. Na kudhibitisha ili lsoma au leta michango ya watu waliochangia.

Kudhibitisha ili msome Al Guido, majibu ya Cristous tena majibu ya Al Guido, na Zitto kaandisha alichokuwa ameandika hapo mwanzo.
 
  • MARA YA KWANZA ALIANDIKA HIVI
  • "Dar inaongoza kwa kuchangia pato la Taifa
    -16.9% Dar
    -9.2% Mwanza kabla haijagawanya
    -7.3%. Mbeya
    -6%. Shinyanga
    -5.3% Iringa
    Hata hivyo Shinyanga ni moja ya mikoa yenye Umaskini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia pato la Taifa, mikoa yenye Maendeleo Zaidi ni Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam.Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7 kuchangia Pato la Taifa.
  • BAADA WA WATU KUMBANA HASA AL GUIDO:: NDO AKAJA KIVINGINE NA NDO HAPO IKATOKEA SINTOFAHAMU NDO ZITTO KAANDIKA HAYO MANENO LAKINI KWA KUYATENGANISHA: HIYO ILIKUWA KABLA YA HOTUBA YA YEYOTE ILE: KAMA ANABISHI AJE HAPA ADHIBITISHE:

  • Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.
    Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.
    Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu
  • Na ukisoma michango ya watu wanataja "Kilimanjaro" lakini Kilimanjaro hap juu katika maelezo yake mapya hakuna Kilimanjaro.. Sasa tujiulize kama hakufuta Kilimanjaro katika michango ya watu ilitoka wapi?
  • Like · Comment · Share
  • Mubarak Kibarabara Go Zitto Kabwe Go zitto...always ahead of them all
    5 April at 14:47 · Like · 13
  • Mseeni Merin Erick Arusha haiko tatu bora?
    5 April at 14:48 · Like · 2
  • Alphonce Isangu Mkuu, Kigoma imesimamaje ktk kuchangia pato la serikali na vipi nafasi yake ktk maendeleo ya Watu wake?
    5 April at 14:59 · Like · 11
  • Al Guido Mh Zitto Kabwe, hapa kwa kiasi fulani naona kama unataka kupotosha haswa kwa mkoa wa Kilimanjaro kwa kuweka hisia haustahili maendeleo uliyonayo, nakupa mfano wa mkoa wa Kilimanjaro kwa maana naujua zaidi ya hiyo mikoa mingine.

    Kwanza, ni mkoa mdogo zaidi Tanzania bara ukiacha Dar maana yake mgawanyo wa maendeleo unatapakaa kirahisi zaidi. Ukiacha hayo mahali mkoa huu ulipo ni katika ukanda wa njia kuu za uchumi! Mkoa huu unapakana na Arusha (jiji ambalo lipo ndani ya nafasi za juu za kuingiza mapato Kitaifa), Tanga (bandari) na Kenya (mshirika mkuu wa biashara na Tanzania na pia ukaribu wake na bandari ya Mombasa unarahisisha uchukuzi);

    Pili, una historia pia ya kuchangia mapato makubwa kwa Taifa kipindi cha zao la kahawa kuvuma kipindi cha nyuma kabla na baada ya uhuru mpaka miaka ya sabini kabla ya Brazili na Colombia kuingia rasmi na kunyakua soko la kahawa duniani;

    Tatu, uchumi wake unalalia kwenye kutoa huduma baada ya zao la kahawa na viwanda kufa, yaani elimu, utalii na kwa mbali afya ambazo kwa kiasi kikubwa ni juhudi binafsi za wahusika wa huko! Nyingi ya taasisi zinazotoa huduma hizi ni binafsi zikimilikiwa na madhehebu ya Kilutheri na Katoliki na hata zile za serikali zipo zilizotaifishwa toka taasisi binafsi za kidini na pia hata chama cha Ushirika;

    Nne, kihistoria wamisionari na walowezi wa Kizungu walipenda mandhari za mkoa huu tangu mwanzo na waliweka makazi na kuamsha muamko wa maendeleo toka enzi hizo. Jaribu kufanya siasa safi na usipotoshe hali halisi maana huo mkoa unaojaribu kuweka hisia unapendelewa, hauna wawakilishi katika serikali kuweka upendeleo huo maana uko upinzani.

    Zaidi ya hayo, utuelezee ni mapato yapi unayoongelea kama ni (VAT, royalty tax, revenue tax, income tax, PAYE, corporate tax ama?); maana kwenye list ya TRA 2014-2015 direct tax (million Tshs) hiyo mikoa uliyosema inachangia mapato zaidi haipo. Kumi bora ni Ilala, Kinondoni, Temeka, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma, Iringa na Tanga. Tanzania Revenue Authority - Tax collection statistics

    Tanzania Revenue Authority - Tax collection statistics
    Tanzania Revenue Authority website
    tra.go.tz|By Super User

    5 April at 19:42 · Edited · Unlike · 69
  • Cristous Saprapasen ... Al Guido pamoja na maelezo yako mazuri kuhusu mkoa wa Kilimanjaro.

    1. Hapa Zitto hakuutaja mkoa wa Kilimanjaro zaidi ya kuonesha kutaka kupiga campaign Shinyanga.
    5 April at 18:41
    · Like · 16
  • Al Guido Cristous Saprapasen, nimemjibu kwenye hitimisho alianza hapo https://www.facebook.com/zittokabwe/posts/914235375263827... Na ningefurahi kama angetuonyesha mgao wa hayo mapato ya serikali (Taifa) kwa shughuli za maendeleo kwa kila mkoa katika hii hoja yake!Zitto Kabwe

    Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.

    5 April at 19:02 · Edited · Like · 29
  • Josephat Lotto Zitto jibu sasa umekutana na wenye upeo na takwimu zenye reference
    5 April at 21:30 · Like · 9
  • Manywele Omary Watanzania acheni chuki na dhihaki, hapa suala ni mkoa gani unachangia kiasi gani ktk GDP kupitia kodi, na siyo mkoa gani una nini. So maendeleo yako yawe yanalipiwa kodi pia. Huwezi kuwa tajiri then ukawa was mwisho ktk kutoa kodi hapo lazima kuna walakini...nawaomba muwe mnaangalia jambo kwa kina na siyo kuwa na biased arguments.
    5 April at 21:41 · Like · 7
  • Al Guido Manywele Omary, soma vizuri utaelewa nimemuomba ufafanuzi wa aliyosema, haya ni majadiliano na kama kuna upotoshaji ama wa makusudi au bahati mbaya tutarekebishana! Na kuhusu makusanyo ya kodi kwa mkoa uliotajwa http://www.ippmedia.com/.../functions/print_article.php...
    Why Kilimanjaro regional revenue collection efficient
    Amidst challenges the Tanzania Revenue Authority (TRA) in Kilimanjaro region has success story to be proud of during the 2012/2013 financial year. During the year TRA in Kilimanjaro recorded a tax collection of 90.6 bn/- compared to the previous year of 2011/12 when it collected 77.2 bn/-. This incr…
    ippmedia.com

    6 April at 08:03 · Edited · Like · 12
  • Daniel George Ngwenya Nadhani kunakuchanganya mambo hapa!
    Mikoa iliyo "changamka" inatokana na watu wenyewe kuwa na uchungu wa maendeleo na Siyo wamepewa kiasi gani kutoka kwenye mgawo wa mapato!
    Majengo na kasi ya uchumi mfano Arusha ni watu wenyewe. Nyumba gani unaifahamu...See More
    6 April at 06:47 · Like · 7
  • Manywele Omary Asante Al Guido, umeonesha ni kiasi gani unashiriki kufuatilia mambo muhimu, hii ni report ya individual performance kwa mkoa wa Kilimanjaro only, kuonesha walivyokaribia target ya makusanyo ya 103bn (90.6n collected with PAYE being above VAT). Labda t...See More
    6 April at 07:54 · Edited · Like · 4

  • Max Mushi Zitto acha chuki na ubaguzi
 
Kwa kuwa source sasa ni facebook/instragram, basi ngoja tukusaidie.

Taarifa kwa ujumla wake hii hapa, ALINDA ALICHOFANYA NI KUUNGANISHA VIPANDE VYA BLUE NA KUACHA SEHEMU ZINGINE ili kujenga taswira aliyoikusudia, sio jambo sahihi kufanywa kistaarabu.Labda ndio maana imekuwa ngumu just kucopy hiyo taarifa na kuiweka hapa.

Barubaru na wengine, sitaki na mimi niwachagulie pa kusoma,someni yote wenyewe bila kukata wala kuongeza popote
.................................................................................................................................................................

Zitto Kabwe

April 5 · Dar es Salam, Tanzani

Dar inaongoza kwa kuchangia Pato la Taifa ambapo mchango wake kwenye pato la Taifa ni 16.9%. Inafuatiwa na Mwanza [kabla haijagawanywa] 9.2%, Mbeya 7.3%, Shinyanga 6% na Iringa 5.3%. Hata hivyo Shinyanga ni mmoja wa mikoa yenye umasikini wa kutupwa licha ya kuwa namba 4 katika kuchangia Pato la Taifa.

Ndio maana ni lazima kubomoa mfumo wa sasa wa uchumi. Huwezi kuwa na mkoa unashika namba 5 kuchangia Pato la Taifa lakini unashika namba 16 kati ya mikoa 21 kwa maendeleo ya watu. Shinyanga ina migodi 2 ya dhahabu na migodi 2 ya Almasi. Shinyanga ina Ng'ombe na Pamba.Shinyanga tarehe 17 Aprili, tujadiliane jinsi ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi mkoani mwenu

Mikoa yenye mchango mdogo zaidi kwenye Pato la Taifa ni Pwani (1.85%), Lindi (1.89%) na Singida (1.92%). Hata hivyo Lindi inashika nafasi ya 9 kwa Maendeleo, juu ya Shinyanga inayochangia 6% katika GDP.

Mikoa iliyo nyuma zaidi kimaendeleo nchini ni Kigoma, Singida, Dodoma, Kagera na Tabora. Hata hivyo Tabora ni mkoa wa 10 kwa kuchangia katika Pato la Taifa na Kagera ni mkoa wa 11 katika GDP.

Mikoa yenye Maendeleo zaidi ni Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Hata hivyo Kilimanjaro ni ya 9 katika kuchangia Pato la Taifa na Arusha ni ya 7.

Tanga ni ya 8 katika kuchangia Pato la Taifa. Pia ni mkoa wa 8 kwa kiwango cha maendeleo ya watu wake.

Mikoa 9 nchini ina idadi ya watu zaidi ya 2m. Dar, Mbeya, Tanga, Morogoro, Mwanza, Tabora, Kagera, Dodoma and Kigoma. Mikoa hii ina 52% ya Watanzania wote

Wakati Dar inachangia 16.93% ya katika Pato la Taifa, inaongoza kwa makusanyo ya kodi ambapo inachangia 81% ya Mapato yote ya Serikali. Kwa makusanyo ya Kodi mkoa wa pili ni Arusha na wa tatu ni Tanga.

Dar, Arusha, Tanga, Mwanza na Kilimanjaro huchangia 90% ya mapato yote ya Serikali nchini

Shinyanga inaendelea kushangaza sana. Wakati inashika nafasi ya nne kuchangia Pato la Taifa (6% of Tanzania GDP), inashika moja ya nafasi ya chini kabisa kuchangia Mapato ya Serikali ( 0.46% of total tax ). Unajua sababu? Shughuli nyingi za kiuchumi za Shinyanga hufanyika Shinyanga lakini kodi zake zakusanywa Dar es Salaam. Mfano migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu, kodi zake zinalipwa Dar es Salaam

Mkoa wa Njombe ndio unaongoza kwa kuwa na watu wengi virusi vya ukimwi. 15.4% ya watu wa Njombe wenye umri kati ya 14 - 49 wanaishi na virusi vya ukimwi. Mkoa unaofuata ni Iringa wenye 10.9% ya watu wake kuwa na virusi vya ukimwi.

Dodoma, Manyara na Tanga ndio mikoa yenye watu wachache zaidi wanaoishi na virusi vya ukimwi

Mkoa wa Simiyu ndio mkoa wenye watu wachache zaidi wenye elimu ya sekondari ambapo 3.7% ya watu wa Simiyu wenye umri wa zaidi ya miaka 25 wana elimu ya sekondari. Dar es Salaam ndio mkoa wenye watu wengi zaidi wenye elimu ya Sekondari, 29%

Katika kodi zote zinazokusanywa Dar es Salaam, 75% zinatokana na forodha, 16% kodi ya mapato na 9% kodi ya ongezeko la thamani (VAT). Dar inachangia 81% ya makusanyo yote ya kodi nchini. Hii inaonyesha kuwa Watanzania wengi sana hawalipi kodi. Utegemezi kwenye forodha ni hatari sana kwa uhai wa nchi yeyote.

" there appears to be a disconnect between economic growth on the one hand and human development on the other" Tanzania Human Development Report 2014

Takwimu zote ninazoweka hapa toka jana zinatoka katika Tanzania Human Development Report 2014. Taarifa imesheheni kwa kweli

Tofauti ya Kipato miongoni mwa wananchi (Inequality) ni jambo linalokosekana kabisa kwenye uchambuzi wa Taarifa ya Maendeleo ya Watu ( THDR 2014). Ninadhani moja ya hatari kubwa nchini ni kuongezeka kwa pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho. Sifa ya sasa ya uchumi wa Tanzania ni 'kufaidisha wachache na kufukarisha wengi'
.................................................................................................................................................................

Mkuu Kapwela.

Shukran sana kwa ili bandiko limejaa ukweli mtupu, kuna wengine walikuja na bandiko lao nakutoa viapo kabla ya ili bandiko.

Baada ya kuliona hili bandiko wamebadili kauli kuwa limefanyiwa edit mbona hakusema mwanzo kabla ya kula kiapo chake.

Hili bandiko limefuta kiapo hakina tena maana daa!!!.
 
Last edited by a moderator:
Alifanya marekebisho baada ya watu kuja juu .. Na kudhibitisha ili lsoma au leta michango ya watu waliochangia.

Kudhibitisha ili msome Al Guido, majibu ya Cristous tena majibu ya Al Guido, na Zitto kaandisha alichokuwa ameandika hapo mwanzo.

Alinda unaweza kutupa snapshot/image ya Facebok wall ya ZZK ya bandiko la Zitto kabla ya kufanya editing?
 
Alifanya marekebisho baada ya watu kuja juu .. Na kudhibitisha ili lsoma au leta michango ya watu waliochangia.

Kudhibitisha ili msome Al Guido, majibu ya Cristous tena majibu ya Al Guido, na Zitto kaandisha alichokuwa ameandika hapo mwanzo.

Hisia za watu huwezi kuzitumia wewe great thinker kujengea hoja NZITO kama hii.

Kwani hujasikia kuna watu wanahisi kuwa Benard Membe na Rais Kikwete ni watoto wa Baba mmoja?sasa great thinker ukija hapa na kutuletea data hizo kwa ushahidi wa hisia za watu hatutawashangaa watu hao bali tutakushangaa wewe.

Inabidi uombe msamaha kwa kumislead watu kwa kunyofoa tu kipande wakati ungeweza kuleta taarifa nzima watu wajisomee wenyewe na wakafanya judgement.Hili sio jambo la kiungwana.

NA tena, unatoa kijipande alafu unajifanya kuuliza alimaanisha nin?kwani huwezi kusoma taarifa nzima ukaelewa?na kama huwezi kuielewa si ungewapa watu taarifa nzima wakueleweshe?bu tuache propaganda kwenye mambo muhimu.Vinginevyo tuombe JF waanzishe jukwaa la propaganda ili wanaotaka kufanya propaganda wakafanye huko.
 
Hisia ni za watu huwezi kuzitumia wewe great thinker kujengea hoja NZITO kama hii.

Kwani hujasikia kuna watu wanahisi kuwa Benard Membe na Rais Kikwete ni watoto wa Baba mmoja?sasa great thinker ukija hapa na kutuletea data hizo kwa ushahidi wa hisia za watu hatutawashangaa watu hao bali tutakushangaa wewe.

Inabidi uombe msamaha kwa kumislead watu kwa kunyofoa tu kipande wakati ungeweza kuleta taarifa nzima watu wajisomee wenyewe na wakafanya judgement.Hili sio jambo la kiungwana.

NA tena, unatoa kijipande alafu unajifanya kuuliza alimaanisha nin?kwani huwezi kusoma taarifa nzima ukaelewa?na kama huwezi kuielewa si ungewapa watu taarifa nzima wakueleweshe?bu tuache propaganda kwenye mambo muhimu.Vinginevyo tuombe JF waanzishe jukwaa la propaganda ili wanaotaka kufanya propaganda wakafanye huko.

Naona tunaongelea mabandiko 2 tofauti.. Mimi ninaongelea hilo bandiko no. 1531 hiyo ni facebook page ya Zitto..
 
Mkuu Kapwela.

Shukran sana kwa ili bandiko limejaa ukweli mtupu, kuna wengine walikuja na bandiko lao nakutoa viapo kabla ya ili bandiko.

Baada ya kuliona hili bandiko wamebadili kauli kuwa limefanyiwa edit mbona hakusema mwanzo kabla ya kula kiapo chake.

Hili bandiko limefuta kiapo hakina tena maana daa!!!.

Unajua mambo mengine yanakera sana.

Maana kama hii ndio level yake ya ukweli wake chini ya kiapo,unajiuliza je asipoapa sasa inakuwaje?soma hapo post yake ya kwa Barubaru leo, hajadeclare kuwa ni VIPANDE VYA SEHEMU NZIMA alafu ANAAPA KWELI KWELI TUPU!shame.

Inakera sana, wakati wote ni propaganda propaganda propaganda propaganda.

Hakuna tofauti ya aliyekwenda shule na ambaye hakwenda.

[/B]
[/FONT]
Ndio hayo ni maneno ya Zitto ambayo mimi Alinda niliyaona kwa mara ya kwanza Facebook , Twitter, Instragam (Zitto) na hapa Jf. (hapo nimenyoosha na mkono juu kabisa yaani ninaapa maneno niliyosema ni ukweli na ukweli mtupu)

Na kama mimi ni muongo basi Zitto yuko humu aje akanushe. (huu ni mwenzi mtukufu wa Ramadhan hivyo natumaini atasema ukweli)

Naona hili andishi hata wewe linakutatanisha kama sisi. Na ndo maana tukasema aje atupe maana nyingine alikusudia nini? au hata wewe unaweza kutupa shule jinsi ulivyolielewa.

Pole sana
 
Unajua mambo mengine yanakera sana.

Maana kama hii ndio level yake ya ukweli wake chini ya kiapo,unajiuliza je asipoapa sasa inakuwaje?soma hapo post yake ya kwa Barubaru leo, hajadeclare kunyofoa KWAKE VIPANDE alafu ANAAPA KWELI KWELI TUP!

Inakera sana, wakati wote ni propaganda propaganda propaganda propaganda.

Hakuna tofauti ya aliyekwenda shule na ambaye hakwenda, shame!

Soma hapo juu.. anayekera ni wewe baada ya kuleta kipande kingine kabisa... Lakini sikushangai hii ni jadi yako kumtungia mtu uongo tena wa mchana kweupe.. Ili bandiko ulilota si bandiko tunalolizungumiza.
 
Unajua mambo mengine yanakera sana.

Maana kama hii ndio level yake ya ukweli wake chini ya kiapo,unajiuliza je asipoapa sasa inakuwaje?soma hapo post yake ya kwa Barubaru leo, hajadeclare kuwa ni VIPANDE VYA SEHEMU NZIMA alafu ANAAPA KWELI KWELI TUPU!shame.

Inakera sana, wakati wote ni propaganda propaganda propaganda propaganda.

Hakuna tofauti ya aliyekwenda shule na ambaye hakwenda.

Ni kweli haya ni maneno ya Zitto. Niliyaona Facebook, twitter na Instragam... tarehe 5.4 sasa kama yeye aliedit. hilo haliondoi ukweli kuwa niliyaona.. Nimekupata post hapo juu na nimekuuliza maswali.. Ulichofanya wewe ni kwenda kunga unga kama iliyokawaida yako. Hiki ulicholeta hapa hakipo Facebook.. Labda utwambie umekitoa wapi?
 
Back
Top Bottom