Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Soma majibu ya Waziri...Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu inalipa kila mwaka kodi Dar es salaam kiasi gani?
Mheshimiwa Spika, sasa nataka kutoa faida inayotarajiwa kutokana na Mgodi wa Buzwagi katika kipindi cha uhai wake ambayo kama usingesainiwa na Barrick wasiwekeze kwenye mradi huu ingepotea:-(i) Mrabaha na kodi nyingine zinatarajiwa kufikia kiasi cha USD198.9 milioni.(ii) Pay As You Earn kwa wafanyakazi inatarajiwa kufikia USD50.3 milioni.(iii) Ujenzi wa laini ya umeme na matumizi ya umeme ya mgodi na maeneo yanayozunguka mgodi yanategemea kutumia USD30 milioni.(iv) Kununua huduma mbalimbali za wakati wa kujenga miundombinu mingine kwenda mgodini, ujenzi wa mitambo na wakati wa uzalishaji ambao unatarajiwa kugharimu takriban USD568.4 milioni.(v) Jumla ya mapato yote yatakayoingia kwenye uchumi wa Taifa katika kipindi cha uhai wa mgodi yanatarajiwa kufikia takriban USD818.3 milioni.(vi) Mgodi unatarajia kutoa ajira katika fani mbalimbali kwa jumla ya watu 696 watakaopata ajira ya kudumu. Kati yao, 630 au asimilia 91 watakuwa Watanzania ikiwa ni pamoja na maafisa waandamizi.(vii) Mgodi utaongeza mapato ya taifa ya fedha za kigeni kutokana na mauzo ya madini nje.(viii) Mgodi utaendeleza miundombinu ya kiuchumi na kijamii, hasa huduma za jamii kama vile shule na zahanati katika maeneo yanayozunguka mgodi.-(ix) Kufunguliwa kwa mgodi huo kutafungua fursa nyingine za kiuchumi katika maeneo mengi.
Mchambuzi. huu ni mgodi wa Buzwagi peke yake.
Last edited by a moderator: