Kutupilia mbali ObamaCare bado kuko juu ya meza, Trump awashauri Dems washiriki kuwanusuru Wamarekani na gharama kubwa za mpango wa bima hiyo!
Mkuu, haya mambo si ya kusikiliza tu, yanahitaji kuyafahamu pia
Kinachozungumzwa kwa ACA kinaonekana kibaya kikawa stigmatized Obamacare
Nilisikia Virginia wakihojiwa na Radio moja, wanasema hawataki Obamacare wanataka ACA kwasababu imewasaidia . Hawa hawajui Obamacare na ACA ni nyaraka moja
Watajikuta wanaingia katika mtego kama ule wa Employment rate
Katika kampeni Trump alisema namba zinazotolewa na bureau of stats ni za kupika, na kwamba unemployment rate ni kubwa. Akaalani job creation ya Obama
Jana, namba kutoka ofisi anayosema ni fake na amekaririwa zaidi ya mara 7, amezisifu
Kwahiyo bureau of stats inafanya kazi, namba nzuri ni kweli kinyume ni mbaya
Hili linaweza kukupa picha hali ilivyo
Ni Trump wiki mbili zilizopita alisema Healthcare ni kitu complicated, leo anasema ata repeal and replace Obamacare unaaamini bila kujiuliza mambo kadhaa
1. Unaweza kutupa cost za proposed healthcare a.k.a Trumpnocare?
2. Kwanini Republicans hawataki kusikia taarifa ya CBO ?
3. Kwanini Republican wanao control Senate, house, magavana na WH wanapata ?
4. Kwanini Dem wamekaa kimya, na Obama aliwaambia nini kabla ya kuondoka?
Ukijiuliza maswali hayo, ukatafuta majibu utaona kauli yako 'Kufutilia mbali Obamacare' si rahisi kama unavyoiona au kudhani.
Hili suala lipo mikononi mwa Republicans na linawapa tabu sana sasa hivi
GOP wanataka kuchanganya Repeal and Replace na Budget ili kutumia 50% kupitisha
Kinyume chake watahitaji 60% ya vote.
Kwa hali ilivyo ndani ya Republicans kuna mpambano
1. Wapo wanaotaka kitu tofauti kabisa kisicho na chembe za Obamacare
2. Wapo wanaotaka improvement ya Obamacare na si kuifuta
3. Wapo wanaotaka kitu kipya lakini kichukue mazuri ya Obamacare
Draft inayozungumziwa sasa imetengenezwa na Paul Ryan si Trump.
Katika draft kuna mambo ya medicaid na coverage ambayo Trump aliyataka
Trump aliacha house itengeneze draft akijua kuna backlash kutoka constituents.
Leo VP alikuwa Kentucky ambako Obamacare imeokoa maisha, kama kule Virginia
Hizi ni Red states na zipo nyingi zinazoona Obamacare ipo mashakani kama maisha yao.
Ni rahisi kusikia Obamacare ni mbaya, kama ambayo nitakuuliza wewe, Ubaya wake ni upi ukilinganisha na draft iliyopo?
Kufuta Obamacare kutaathiri employment na hayo hayaonekani sasa hivi
Mkuu, hili suala Wamarekani wamegawanyika na si la' kubaki mezani au kufutilia mbali'
Ingekuwa rahisi kama unavyosema lingeshamalizika siku 50 zilizopita.
Tusemezane