Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

ACA NA GOP

Kuanzia leo na kuendelea CBO itatoa taarifa ya makisio kuhusu nini kitatokea kama Obamacare itafutwa kwa watu waliosajiliwa na walioajiriwa kutoka kwayo

Itatoa gharama zinazotarajiwa kwa ujumla na kwa watu kutokana na proposal mpya

Rep wanaipinga taarifa hiyo wakijua itakuwa mwiba katika kuuza healthcare plan yao.

Wanasema takwimu za CBO zinakuwa off mark mark na si za kuaminika.

Hata hivyo, GOP walitumia takwimu hizo hizo kuisema Obamacare siku za nyuma

Ni mwendelezo wa kukataa taarifa zinapopinga na Republicans na kuzikubali zikionyesha uelekeo mzuri kwao.

Hayo yakiendelea timbwili la tuhuma za Trump dhidi ya Obama linachukua sura mpya.

Wabunge na maseneta wameonyesha mshangao kama kweli jambo hilo limetokea.

Kamati ya Bunge ya intelejensia imetoa hadi leo Jumatatu WH ifikishe ushahidi kupitia wizara ya sheria DOJ ili uchunguzi ufanyike

WH hadi sasa haina ushahidi na ilisema haitazungumzia suala hadi lichunguzwe.
Hii ilikuwa njia ya kukwepa maswali yanayotokana na kauli ya Trump

Kama WH haitafikisha ujumbe, Trump atadhalilika kwa kumdhalilisha mtanguilizi wake.

Ikizingatiwa alihoji uzawa na alitumia muda kum deligitimize Obama, hali si nzuri kwake

Hilo limeendelea kuchagiza uchunguzi kuhusu Russia kuendelea.

Hadi hapo taarifa zitakapotolewa suala hilo tulipe subira.

Muhimu ni kamati ya bunge ya intelejensia imeagiza IC kuwasilisha vielelezo

Kama mtakumbuka IC zilisema Russia iliingilia uchaguzi, zikasema zina ushahidi wa watu waliohusika na kwamba zilinasa mawasiliano uya Russia wakishangilia.

Tusemezane
 
ACA NA GOP

Kuanzia leo na kuendelea CBO itatoa taarifa ya makisio kuhusu nini kitatokea kama Obamacare itafutwa kwa watu waliosajiliwa na walioajiriwa kutoka kwayo

Itatoa gharama zinazotarajiwa kwa ujumla na kwa watu kutokana na proposal mpya
Mkuu Nguruvi3, GOP kwa kutaka kuwachanganya wapenzi wake wenye uelewa mdogo, walikataa katakata kuita ACA kwa jina lake halisi wakaamua kuiita Obama care.

Wanachama wengi katika majimbo mbalimbali wameonekana wakiisifu Affordable Care Act huku wakiiponda Obama Care kama vile ni vitu viwili tofauti. Hii inanikumbusha ulaghai wa CCM waliposifu na kubariki takrima kwenye chaguzi huku wakilaani matumizi ya rushwa na kweli baadhi ya wanachama wao kuunga mkono bila kujua ni kitu kile kile.

CBO, chombo kisichoegemea upande wowote kimetoa ripoti yake ikionesha proposal mpya ilivyo na kasoro nyingi na itakavyoongeza gharama kwa wananchi huku ikiwapa ahueni mabilioneya. Kama kawaida GOP wakiongozwa na Trump wanalaani hii ripoti wakidai inapotosha mambo mengi.

Tutarajie vita baina ya pande mbili kwani yaonekana mstari tayari umechorwa kwani na Democrats nao wameamua kuubatiza hiyo proposal mpya Trump care.

Kamati ya Bunge ya intelejensia imetoa hadi leo Jumatatu WH ifikishe ushahidi kupitia wizara ya sheria DOJ ili uchunguzi ufanyike.

Kama mtakumbuka IC zilisema Russia iliingilia uchaguzi, zikasema zina ushahidi wa watu waliohusika na kwamba zilinasa mawasiliano uya Russia wakishangilia.
Hapa naomba tuzidi kuvuta subira, yapo mambo nyeti yataibuka na jitihada za kuzifagia chini mvunguni huenda zisifanikiwe...tayari GOP diehards wameanza kumtuhumu Obama kuwa ndiye anasuka mpango wa kumuangusha Rais wao mpya, duh! Kuanzia wiki hii huenda tukashuhudia mashambulizi makali kutoka pande zote, je hali itakuwaje? Nunueni tu popcorn!

DOJ seeks more time to respond to Trump's wiretapping assertion...

Justice Dept. seeks more time to respond to congressional inquiry into unproven Trump wiretapping assertion. Earlier the House committee had turned the matter back on the Trump administration and so set today as deadline for the Justice Department to provide evidence.

Mambo yanachemka...
 
WIKI HII KATIKA SIASA ZA US

Tuhuma dhidi ya Obama zabeba uzito
UK wakana taarifa ya WH,Fox wakanusha na Times wakataa

Ni wiki mbili tangu Rais Trump alipotoa madai ya kumtuhumu mtangulizi wake kwa 'wiretapp'
Tuhuma zilizoelekezwa kwa Obama na si utawala wake kwa ujumla

Aliyekuwa mkuu wa usalama wa Taifa Bw Clapper akikanusha kuwape kwa tukio hilo, huku mkuu wa FBI akiitaka idara ya sheria (DOJ) ikanushe madai ya Rais

WH kupitia press sec SeaN Spicer na wapiga debe walibadili tweet kwa kusema ilikuwa ni surveillance
Hoja hiyo imekosa mashiko kwasababu surveillance ni jambo la kawaida lifanywalo na Intel community

Kama ikibidi, kufanya hivyo kwa Raia kunahitaji Rais kuwasilisha hoja mahakamani kabla ya tendo
Hakuna mahali penye ushahidi wa hilo. Na wala hakuna ushahidi mwingine wa intel community

Ushahidi unaotolewa ni ule wa vyombo vya habari kama gazeti la New York times, Fox, na Jaji Napolitano, pia ukihusisha idara ya ujajusi ya UK katika mambo ya electronic ijulikanyo kama CGHQ

Gazeti limeeleza ya kuhusu makala ikieleza surveillance kwa ujumla na si kutokana na tweet za Trump
Television ya Fox imekanushwa kwamba habari ya Napolitano ni maoni yake na si ya kituo
UK kupitia ofisi ya waziri mkuu imeeleza madai hayo kama upuuzi na ya kupuuzwa

Juzi katika mkutano na waandishi wakati wa ziara ya Chancellor Merkel, Rais Trum aliulizwa kuhusu hilo
Kwanza, akasema yeye na Merkel wana kitu common, ikimaanisha sureveillance iliyofanywa na vyombo vya US dhidi ya Ujerumani ni sawa na tapping ya Trump Tower

Pili, akasema asiulizwe kuhusu habari, naye alizisikia kutoka Fox News ambayo imemkana

Hoja za Trump zimetonesha kidonda. Trump alifanya hivyo ili kupoteza mjadala kuhusu ushiriki wa watu wake na Russia katika uchaguzi. Ni kawaida yake kusababisha distractions anapokuwa na jambo

Kama tulivyosema mwaka jana, katika uchaguzi hilo lilifanikiwa. Akiwa Rais kila kauli ina matter
Badala ya kuhamisha mjadala, tweet zake zime mu expose katika hali ngumu sana

Kwanza, kumekuwa na mgogoro wa kidiplomasia na UK, mshirika mkuu. Haitarajiwi UK iiambie WH ni nonsense and ridiculous. Hii ni kauli nzito kwa kuzingatia mahusiano katika nchi hizo
Na kwa ukweli kuwa intel community kama CGHQ hazitoi kauli , kwa hili zimetoa wazi na kukemea

Pili, wengi wanajiuliza, ilikuwaje Rais wa US aiite vyombo vyake ili kupata ukweli kabla ya tweet?
Kwa kunukuu vyombo vya habari, intel community zinaona ni mwendelezo wa dharau dhidi yao

Tatu, Wasgington yote Dems na GOP kwa pamoja wanashangaa madai hayo achilia mbali intel comm

DOJ imefikisha taarifa yake kwa kamati ya bunge baada ya kushindwa Jumapili iliyopita na kupewa muda zaidi wa kufanya hivyo. Taarifa hiyo ni classified kwa maana ya kuwa isitoke nje ya kamati

Huu ni ujanja umma uelewe kuna jambo kama amabvyo Trump anasema wiki 2 zijazo watu watafaham

Inaendelea....
 
Tuhuma.... Inaendelea

Hadi wakati huu hakuna ushahidi wa kuonyesha Obama alitenda hayo kama mtu.

Timbwili limezua majadiliano yakimhusu Rais, mkanganyikao WH, na mataifa

Jumatatu mkuu wa FBI atahojiwa na kamati ya bunge kuhusu suala la Russia
Pamoja na hayo ataulizwa kuhusu wiretapp aliyosema Trump

Ikitokea FBI wakasema kulikuwa na kitu kama hicho, italazimu uchunguzi wa kina
Itakuwa sawa na Watergate. FBI watatakiwa ku prove beyond doubt kuhusu hilo

Ikitokea FBI wakasema hakuna kitu , madai ya Rais Trump yatachukua sura nyingine

Kwanza, kwamba anazoandika ni fake news zinazoleta sintofahamu ndani na nje ya nchi

Pili, atalazimika kuomba radhi, hakuna chombo kingine kilichobaki kuthibitisha madai

Tatu, itaendeleza' Birtherism' ambayo alimshikia bango Obama kwa miaka mingi

Nne, itapunguza credibility ya Rais na taasisi nzima kuhusu kauli zao ndani na nje

Tano, Trump atakuwa amewadhalilisha watumishi wake kama Spicer kwa kutetea uongo

Sita, Intel community zitajiuliza kama bado zina nafasi katika utawala huu

Saba, suala la Russia litapamba moto itahisiwa ni kutaka kulipoteza kwa kutumia wiretap

Wakati Jaji akizuia amri ya 'ban' ya mataifa kama ilivyokuwa ya kwanza, Obamacare ikikabiliwa na upinzani ndani ya Republican, wiki inatokuja ikiwa na Russia na wiretap itakuwa ni nzito kwa upande wa WH

Tusemezane
 
...
Pili, atalazimika kuomba radhi, hakuna chombo kingine kilichobaki kuthibitisha madai...
Sita, Intel community zitajiuliza kama bado zina nafasi katika utawala huu...
Ndio maana nilitoa tahadhari ya muda wa wiki mbili nikiomba tuvute subira, hizo wiki mbili zinayoyoma na kuanzia Jumatatu itakuwa ni kusuka au kunyoa ikitegemea mtu anasimamia lipi. Namsikitikia Rais Trump.
 
Ndio maana nilitoa tahadhari ya muda wa wiki mbili nikiomba tuvute subira, hizo wiki mbili zinayoyoma na kuanzia Jumatatu itakuwa ni kusuka au kunyoa ikitegemea mtu anasimamia lipi. Namsikitikia Rais Trump.
Na hakika kulikuwa na subra kwani mengi yametokea wiki hii.

Watu watakumbuka, tulisema kampeni na transition si sawa na utawala.
Kutawala ni jambo tofauti kabisa

Trick alizotumia kwasasa hazifanyi kazi. Na kibaya, media imezing'amua kikamilifu

Vita na media kwa kusema zina habari fake ili kuzima mijadala haisaidii inawasha moto

Media zinauliza, inakuwaje WH inatumia habari kutoka 'fake news' kuthibitisha madai ?

Inakuwaje Rais akiwa na vyombo asiviite kupata ushahidi kabla ya tweet?

Media zainakumbusha wakati wa Birtherism Trump alisema ametuma ujumbe mkubwa Hawaii na Kenya na kuna habari nzito. Hadi leo hakuna habari zozote

Trump alisema kuna wapiga kura 3-5M ana ushahidi wa kutosha. Hadi leo hakuna

Hili la Obama lina namna mbili zinazomweka mahali pagumu

Kwanza, tuhuma amezipeleka kwa mtu na si mamlaka.
Hakusema admin au WH, bali bad guy! sick Obama.

Hivyo atahitaji kuthibitisha madai yake kwa muktadha huo. Ndipo tunakuja hoja ya pili

Kama kuna surevillance,ni jambo la kawaida na hufanywa na intel community kwa mambo ya nje ya nchi. Ndivyo walivyonasa mawasiliano ya Balozi wa Russia na Flynn.

Surveillance haikumlenga Flynn. Kwa bahati mbaya au nzuri maongezi yalimhusisha Flynn

Kama Obama alifanya surveillance ilibidi awe na ocurt order. Hilo ni kupitia DOJ na FBI

Je, kuna kitu kama hicho ikiwa wiki 2 zimepita na DOJ haikuwa na ushahidi !

Kwa US, intel zinampa Rais taarifa , hazipokei taarifa za nini zifanyie kazi.

Hata kama kutakuwa na taarifa za IC hazimtahusu Obama as person na tuhuma zilivyo

Maana yake ni kuwa lazima kuwe na ushahidi Obama aliagiza vyombo nje ya vya umma

Jaribio la kuihusisha GCHQ ya UK limegonga mwamba na kuwa aibu kubwa.

Lazima WH ithibitishe Obama kama mtu alifanya hivyo kwa ku abuse mamlaka yake!

Jumatatu FBI Comeny ana kazi ngumu. Kumthibitisha Obama kwa mujibu wa tuhuma za tweet, au kumsafisha Obama na kumpaka matope Trump.

FBI waki debunk nadharia za Trump,mpambano na intel utaingia hatua nyingine

Intel zitataka ku prove uwezo wao bila kujali mamlaka ya WH.

Hapa mungu jalia kusiwe na jambo kuhusiana na suala la Russia.

Kama lipo, itakuwa mwaga mboga namwaga ugali
 
Jumatatu ya mahojiano

Bado Dir Comey wa FBI anaendelea na mahojiano

FBI na DOJ wamethibitisha hawana info zozote kuhusu Obama na wiretap
Hili tayari ni habari kwasababu tweet za Trump zimekuwa debunked na idara za serikali

Pili, FBI imethibitisha kuwepo kwa uchunguzi wa Russia hacking, kuhusisha kampeni na wote watakaohusika na uchunguzi

Tathmini zaidi itafuata
 
Donald Trump, the deal maker, had no idea what he was walking into when he decided to run for the presidency. Every day he wakes to that painful fact and oh my, does he regret!
 
Donald Trump, the deal maker, had no idea what he was walking into when he decided to run for the presidency. Every day he wakes to that painful fact and oh my, does he regret!
Mkuu hii ni moja ya habari zitakazo 'sums up' matukio kuanzia Jumatatu iliyopita

Kwa ufupi, hoja ya Obama na tapping imekuwa debunked

Russia na Nunes na michezo ya kuigiza tutaifafanua

Hili la leo la repeal and replace disastrous Obamacare tutalieleza

Tulipokuwa jamvini katika uzi huu tulieleza sana kuhusu ACA na repeal and replace
Wenzetu wengine wakang'ang'ana na 'kufutwa kuko pale pale'

Tulionyesha ugumu, sio geni bali kwa wasioamini it's a reality

Wanabadili goal, inatwa Rynocare, deal maker mitini
 
Breaking news: Healthcare bill pulled!

Naam, imeshindwa...haiwezi kupita.

Mkuu Nguruvi3, nimejizuia sana kukurupuka bila kuwa na habari sahihi lakini nafuatilia kwa karibu sana mambo yanayoendelea huko Marekani. Masikini Paul Ryan, nilidhani ana msimamo lakini, baada ya kusaliti nafsi na msimamo wake na kuamua kula matapishi yake kwa kumuunga mkono Donald Trump, sasa itabidi auguze machungu yake.

Hili la Ryancare ni moja katika mengi ambayo kama hakuangalia huyo huyo Trump atamruka na kumwacha kwenye kikaango. Lingine ni yeye kumshauri Nunes, Mwenyekiti wa kamati ya Intel ya Congress, bila kuwataarifu wajumbe wenzake, kukurupuka na kutoa taarifa nyeti ya INTEL bila kutilia maanani chanzo chake akidhani anaisaidia WH, kumbe!
 
Breaking news: Healthcare bill pulled!

Naam, imeshindwa...haiwezi kupita.

Mkuu Nguruvi3, nimejizuia sana kukurupuka bila kuwa na habari sahihi lakini nafuatilia kwa karibu sana mambo yanayoendelea huko Marekani. !
Mkuu si wewe bali nami niliamua kusubiri kila kitu ili isijeonekana kuna ushabiki

Tunazo habari za kujadili , zimesheheni na kutitia kuhusu politics za US
Kwa wanajamvi, usikae mbali, inaanza soon hadi jumapili ili jumatatu tunafuatilia mpya
 
WIKI HII KATIKA SIASA ZA US

Wiki ilianza kwa kamati ya bunge kuwahoji maafisa wa vyombo vya usalama hasa FBI ya Comey

Kulikuwa na hoja mbili mbele ya meza. Kwanza, tuhuma za Obama wiretapping Trump tower
Hili lilikuwa baada ya tuhuma alizotoa Rais Trump takribani wiki tatu kamili zilizopita

Tuhuma dhidi ya Obama zilimlenga kama mtu na si utawala wake.

Tofauti ya hayo mawili ni kuwa Rais ni taasisi ya umma inafanya kazi na taasisi/idara nyingine
Kusema taasisi zilihusika na wiretapping ni tofauti na kusema Obama kama mtu alihusika

Tafsiri ya wiretapping ni kusikiliza mawasiliano kama simu kutoka eneo kwa siri
Halafu kuna surveillance, ambayo ina sheria zinazoihusu hasa kwa watu wa nje

FBI ya Comey na DOJ zimesema hakuna kitu kama hicho kutokea

Mkurugenzi wa mawakala wa usalama naye kathibitisha hakuna tukio kama hilo

Kamati ya bunge nayo ilisema hakukuwa na ushahidi wa hilo kutokea

Maana yake, taasisi za FBI na DOJ zipo chini ya Rais zinapokataa jambo ni kukanusha

Hivyo madai ya Trump kuwa Obama alifanya wiretapping hayakuwa kweli ni uzushi

Pamoja na hayo, Rais Trump hakuwa na ushahidi wowote kuhusiana na hilo

WH imebadilisha story na kusema kulikuwa na surveillance.

Hili linafanywa chini ya mwneyekiti wa kamati ya bunge ya intelejensia bwana Nunes kama tutakavyoona mbele

Inaendelea
 
SIASA ZA US (Sehemu ya II)

Sehemu ya pili ya mahojiano ya wiki hii baada ya wiretapping ilikuwa suala la Russia

FBI wamethibitisha kuchunguza watu wa kampeni ya Rais Trum, uhusiano wao na Russia
Maswali mengi hayakuwa na majibu kwasababu ya unyeti wa uchunguzi

FBI Dir akasema uchunguzi ulianza muda mrefu na bado unaendelea.
Hilo lilizua maswali, kwamba kwanini hakulisema pamoja na lile la Hillary Clinton?

Kamati iligawanyika, Dems wakitaka kujua ya Trump na Russia, GOP wakiakazinia leaks

Hivyo conclusion haikuapatika zaidi ya kuelewa uchunguzi unaendelea kwa mujibu wa FBI

Tkirudi nyuma, kazi ya kubadili tuhuma dhidi ya Obama na wiretapping iliendelea.
WH ilisema watu subiri jambo litatokea katika wiki moja au mbili ikikataa kuomba radhi

WH ikabadili hadithi, kilichozungumzwa ni surveillance iliyofanya na vyombo vya ulinzi

Katika mazingira ya kushangaza, jumanne , mwenyekiti wa kamati ya Intel Bw Nunes alikwenda WH kumtaarifu Rais habari mpya za wiretapping. Alikuta maandalizi na kuongea na media

Wakati anakwenda, taarifa zake alikataa kusema kazipata wapi bila kupitiwa na wanakamati

Wakati huo huo anakwenda WH kumtaarifu anayetuhumiwa habari za tuhuma zake!!!

Ilikuwa ni mpango ili kumsafisha Trump na tuhuma kuwa alichosema kuhusu surveillance ni kweli.
Hili halikufanikiwa pia kwani media na wachunguzi waliona ilikuwa ni suala la kupangwa

Lakini pia ilikuwa mbinu ya kuzusha mjadala mwingine wa Nunes ili kuondoa focus ya Obamacare na GOP waipitishe kwa mshutuko. Haikfanikiwa

Alhamisi Dems na Schiff katika kamati ya Intel walitoa taarifa katika media kama za Nunes

Wengi wanasema mbona nao wamefanya kosa kama la Nunes na WH

Ukweli ni kuwa Dems wamefanya makusudi ili kuthibitishia umma kamati haiwezi kuwa impartial katika suala la Russia hivyo iundwe kamati maalumu au special prosecutor.

Tayari kuna call ya kamati maalum au special prosecutor kwavile Nunes anaonekana'biased'

Dems wanatambua kamati ikiwa chini ya Nunes hakuna kitakachotokea.
Nunes alikuwa mshauri wa Trump wakati wa transition. Alichofanya ni kosa la kiufundi

Amechagiza uchunguzi nje ya kamati yake ambao hataweza kuu 'cover' na ndiko sakata liendako

Kila uchao habari zinazidi kuvuja zikiwasogeza wasaidizi wa Trump karibu sana na Russia

Uhusiano wa watu hao sasa unazidi kupanuka na kugusa washirika nje ya serikali ya sasa

Watatu wa washirika wakubwa wa Trump wamekubali kufika mbele ya kamati na huenda wa nne akaitwa kwa barua mahususi ya kisheria na lazima

Inaendelea....
 
JARIBIO LA KUONDOA ACA LASHINDWA

Republican waparaganyika
Trump aonja machungu ya kutawala nchi si kampuni

Kwa miaka mingi Rais Trump yupo mstari wa mbele kupinga ACA inayoitwa Obamacare
Kwa miaka 7 Republican wamepinga Obamacare ambayo jana ilitimiza mwaka wa 7 rasmi

Kampeni yote 2016 ku repeal and replace Obamacare ilikuwa ni 'mantra' kila uchao
Jambo moja lililokuwa wazi, hakuna nyaraka iliyowahi kuonekana ikionyesha mbadala wa Obamacare

Rais Obama aliwahi kuhoji kama upo mbadala ili aweze kuunga mkono. Hakuna.
Trump wakatumia kauli nyingi kulaghai umma bila kuwa na mbadala wowote isipokuwa kelele tu

Uchaguzi wa ndani wa Republican wagombea karibu wote walikuwa na sera za namna ya kudeal na Obamacare kwa maana ya mbadala.

Trump hakuwa na hata ukurasa mmoja, lakini alikuwa mzuri sana wa kuponda Obamacare. Hapa jamvini tuliwahi kuhoji sana, kamaACA ni mbaya wapi nzuri ya Trump?

Baada ya kuingia WH Trump alisaini siku ya kwanza kitu kinachoitwa kupunguza maumivu a ACA
Ilikuwa ni kulaghai siku ya kwanza kafuta Obamacare na hapa jamvini wapo wenzetu waliamini

Katika kati ya siku 64 Trump akasema hakujua ni kitu complicated namna hiyo. Mbele ya safari akasema ilikuwa vema kuanza na tax cut kabla ya kufikiria kuiondoa Obamacare

Alichofanya ni kuacha Speaker Paul Ryan aandike bill kwasababu Trump hakuwa na kitu na GOP hawakuwa na blue print kwa miaka 7. Hivyo waliandika kuanzia mwanzo kama kitu kipya

Yote yalifanyika kwa haraka na kusahau factors nyingine zinazoweza kuathiri matokeo ya nyuma

1. Trump alikuwa na vita na 'the establishment' wakati wa kampeni akiwatukuna na kudai kubadilisha Washington. Hakuelewa nguvu ya the establishment ndani ya DC

2. Republican hawakuelewa nguvu na umaarufu wa Obamacare pamoja na mapungufu iliyo nayo

3. Trump hakuelewa Republicans wana makundi makubwa, kwanza, the establishmen,moderates halafu kuna Conservatives ambao ni far right.

Hawa conservatives sasa wanajulikana kama Freedom caucus, lakini ndiyo Tea Party waliompinga Obama na kumdahlilisha kila mara wakiongozwa na akina Hannity, Bannon na Breitbart, Rush Limb.
Hawa ni supremacist kweli kweli na ndio waliongoza sehemu ya kampeni ya Trump katika media

Kwanini wameshindwa kuondoa Obamacare?

Inaendelea........
 
ACA YASHINDWA (Sehemu ya II)

Katika kampeni Republicans walicheza vizuri sana kutoonyesha nini sera yao kuhusu afya
Walitumia Obamacare kuinanga na kuonyesha mapungufu bila mbadala. Walikuwa na sababu

Trump aliahidi kuifuta Obamacare siku ya kwanza, hakuwahi kuonyesha mstari mmoja wa sera yake

GOP na Trump walijua, Obamacare ambayo kimsingi ilijengwa katika misingi ya Republican imesukwa katika hali ambayo ni ngmu kuondoa kipande kimoja bila kuudhi sehemu ya jamii

Mategemeo yao yalikuwa kuifuta pindi wakipata WH, house na seneti amabazo sasa wanazimiliki
Obama aliwaambia Dems, waache GOP waifute wenyewe kama wanataka bila kuwapinga

Trump kama ''deal maker'' akaanza kuita GOP kwa makundi kuwashawishi.
Hii haikuwa bill yake bali imetengenezwa na house Rep chini ya Ryan

Rais Trump alijua jinsi ilivyo complicated akawaambia waahirishe hadi mwaka mmoja upite
Ryan akasema hii ndiyo nafasi wana majority house na seneti na kwamba itapita bila kutegemea 60%

Mswada unaomabatana na bajeti hupitishwa kwa simple majority na walitegemea kufanikiwa
Spika Ryan akatengeneza kinachoitwa America Health care act ili ku repeal and replace Obamacare

Tatizo
Rejea makundi matatu bandiko la awali. The establishment wana msimamo wa kati kwamba kuna mambo yatakayotakiwa marekebisho, lakini wanakubaliana na hoja ya ku repeal and replace
Ndani ya nyoyo zao wana reservation dhidi ya Trump na ubabe aliowafanyia, walimsubiri

Moderates wanatatizika, kwasababu repeal and replace ndiyo msimamo wa GOP.
Wanaona Obamacare inawasaidia hasa upande wa state ambako suala la medcaid ni maarufu

Tea party ambao ni Freedom caucus na ambao ni conservative hawataki kusikia kitu Obamacare
Kumbuka hawa ndio wenye vyombo vya habari na walikataa wazi wazi. Wanataka ifutwe yote

Trump anatambua watu milioni 14-20 watapoteza insurance na wapo wa medcaid, akina mama na wenye maradhi ya muda mrefu wanaonufaika na Obamacare.

Hataki kufuta anataka kbadilisha sehemu kadha wa kadha akiacha mazuri ya Obamacare

Hapo ndipo timwbili lilipoanzia na kuzima jaribio

Inaendelea
 
TIMBWILI NA 'DEAL MAKER' (Sehemu ya II)

Walioangausha Ryancare ni freedom caucus na Trump.
Rais Trump alijaribu kufanya deal za kiutawala kwa mtindo wa deal za biashara zake

Haikuwa rahisi kama alivyodhani na alivyowahi kufanya kwa kuzuia makampuni kuondoka

Wananchi walikuja juu wakitaka kujua masilahi ya kila kundi katika mikutano ya wabunge na maseneta wa Rep. Hii ilikuwa na mkono wa Dems walioeleza wananchi athari zinazofuata

Wabunge na maseneta wa Rep waliona hatari katika miaka miwili ijayo na uchaguzi mkuu
Kuna hali ya kuchanganyikiwa kila mmoja aliona vema asimame na district yake

Najimbo yenye conservatives wengi yaliwalazimisha tea party au freedom caucus kusimama na msimamo wao vinginevyo wangepoteza midterm elections

Moderates na establishment nao walifuata misimamo ya district zao , wakitaka mambo kama ya family health, medcaid, insurance kwa familia yaangaliwe kwasababu yaliathiri district zao

Kuyaleta makundi hayo pamoja ku repeal and replace Obamacare haikuwa kazi rahisi
Trump alijaribu bila maafikiano. Ryancare ikishindikana wakisema ni dead on arrival

Rais Trump ameongea kwa unyenyekevu akieleza jitihada za wabunge wa Republicans na Spika Ryan.

Hakugusia nani waliohusika ikizingitiwa alihitaji Republicans 20 hadi 30 na waliokataa ni zaidi ya hapo. Deal alifanya na GOP hakusumbuka na Dems, GOP wanaweza kupitisha bila kura ya Democrats

Kwanini hakulaumu GOP aliwalaumu Democrats?

Trump alisema mswada umekwama kwasababu hakupa ushirikiano wa kura haa moja ya Democrats
Hili wapiga debe wote wanalizungumzia na kutupa lawama Dems ,mkakati tu wa kukwepa hoja

Trum amekuwa mwangalifu sana kuwaluamu Republicans kama freedom caucus akijua wana nguvu. Hakugusa the est. kwa ushwishi wala moderates, hahitaji upungufu wa kura katika mambo yajayo

1. Kuna tax cut ambayo inaelekea kufeli kabla ya kufika kama Obamacare.
2. Kuna infrastructure spending ambayo inahitaji kura kama Obamacare

Tea party au Freedom caucus au conservatives wanasema tax cut ni nzuri, pesa zitatoka wapi kuendesha serikali? Hawataki kukopa kwasababu deni la taifa ni sehemu ya mambo wasiyotaka

Infrastructure itahitaji trilioni na ushee. Kukiwa na tax cut kiasi hicho kitatoka wapi?
Vinginevyo denilitaongezeka. Hapa moderates na the establishment wataungana na freedom caucus

Mkakati wa kutupa lawama kwa Democrats ni mbaya.
Dems wanasema Trump hakuwafikianamna ya kuboresha Obamacare, kufeli ni mzigo wake.
Wanasema waliompinga Trump na Ryan na freedom caucus.

Kauli hiyo inazidi kuwachonganisha republicans.
Lakini baya zaidi, bado atawahitaji Dems katika kupitisha miswada mingine

Jana Spika Ryan kwa uchungu kaeleza wazi 'Obamacare remains the law in the land'

Pigo la nguvu kwa Trump. Inaendelea
 
MAPIGO MFULULIZO
Siku 65 za mahangaiko

Kufeli kwa repeal and replace Obamacare( ACA) kumemjengea heshima Obama.
Kwamba, pamoja na matatizo aliyokumbana nayo aliweza kutumia fursa vema

Ni failure kwa Trump kwasababu huu ndio mswada wake wa kwanza ndani ya house
Ni campaign signature aliyohubiri miaka 3 ambayo mwisho wa siku hakuweza kufanikisha

Kauli yake ya tweet, Obamacare iachwe itakufa yenyewe ni hali ya kukwepa wajibu
Rais hasubiri jambo lifeli, anapaswa kusimamia masilahi ya nchi na si kujitenga na felia

Pigo hilo linafuatilia lile la 'Wiretapping' lililokanushwa na vyombo vyake mwenyewe
Kilichojitokeza ni kupoteza credibility na kuleta mtafaruku na mataifa kama UK kwa uongo

Pigo la hapo juu linaambatana na kauli ya FBI kuwa kampeni na washirika wake wanachunguza
Kwa Rais aliyepo madarakani kuchunguzwa, si jambo la kawaidia kwa siasa za Marekani

Kabla ya hapo mahakama ilizuia kwa mara nyingine executive order inayopiga marufuku visa
Marufuku hayo ni baada ya yale ya awali yaliyozua maandamano makubwa

Rais Trump amenukuliwa mara nyingi akisema yeye ni 'deal maker' na kwamba hakuna jambo rahisi kutenda kuliko kuingia deal na wanasiasa. Hadi sasa hana deal zaidi ya EO alizotoa

Kuelekea siku 100 kuna hati hati ya kutimizia ahadi alizosema zitafanyika katika muda huo

Katika mkutano leo, seneta Linsey Graham amemhusia kufanya kazi na Dems 'reach the Dems'
Kshindwa ka deal kunatoa hisia 'anawezekana' katika siasa za DC, jambo litakalomsumbua

Trump akiingia madarakani amechagiza masoko ya mitaji kutokana na ukweli wa ahadi zake za deregulation ambazo makampuni na mashirika huzipenda sana

Ni kutokana na ahadi za punguzo la kodi, na kutoa vishawishi kwa wawekazaji ndani ya US

Katika hali ya mapigo yanayomwandama, credibility yake ikiwa mashakani na tuhuma za Russia zikiendelea, wawekezaji wameanza kurudisha kasi nyuma kama ambavyo wiki hii DOJ ilivyoporomoka

Trump anahitaji re-calibration ya siasa zake, kuendesha shirika binafsi si sawa a kutawala Taifa

Tusemezane
 

Breaking News: Former national security adviser tells FBI, the House and Senate intelligence committees he’s willing to be interviewed in exchange for deal, officials say


Mike Flynn, President Trump’s former national security adviser, has told the FBI and congressional committees investigating the Trump campaign’s potential ties to Russia that he is willing to be interviewed in exchange for a grant of immunity from prosecution.

Duh, mambo yanaanza kuwa mambo huko Marekani na viti walivyokalia watu huko Ikulu vinaanza kupata joto. Huyu Michael Flynn tayari anatafuta kinga ili aweze kujitetea mbele ya Kamati za usalama za Senate na House. Je ni yapi hayo anategemewa kuyamwaga? Je watanasa waliomo na wasiokuwamo? Yetu macho, tuvute subira...
 
Back
Top Bottom