TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
TUJITEGEMEE, hayo maneno uliyoyatumia (IN RED) yanaonesha tu usivyoijua Marekani. Tayari baadhi ya wapiga kura wake wanajuta! Kwa sasa sitasema mengi ila nakuomba ufuatilie hali itakavyobadilika katika siku chache zijazo. Halafu naona sana unavyojitahidi kuwatupia lawama media kwamba inampiga vita Trump but are you sure? Nakuhakikishia bila media Trump asingefika alikofika, ni media hiyo hiyo iliyomwibua na kumfikisha hapo alipo.Kikubwa Trump apate EV za kutosha! Vinginevyo moto utawaka, wakimnyima urais hiyo 19 December!
Mkuu naomba utusaidie kidogo kwa haya yafutayo ili tukuelewe vizuri na kwa ufasahaAsante sana Mag3 kwa maelezo mazuri.
Lakini imesemwa kuwa hiyo Electrol Vote ipo kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa majimbo makubwa kuwachagulia rais majimbo madogo. Hivyo popular votes kwa msingi huo haina uhalali wa kutoa rais sahihi wa US kwa mujibu wa taratibu zao. Na hizo petition kuna uwezekano mkubwa zinatengezwa na Mainstream media, na kunauwezekano mkubwa hazionyeshi uhalisia wa Wamarekani wote. hata hivyo naziona petition Sawa na popular votes!!
Kikubwa Trump apate EV za kutosha!Vinginevyo moto utawaka, wakimnyima urais hiyo 19 December!
magode, waliojitokeza kupiga kura wengi wao wamempigia Hillary Clinton na mpaka dakika hii idadi yao ni kama ifuatavyo;magode said:Waliojitokeza kupiga kura ndo wameamua nani awe Rais wao, huwezi kuongelea ambao hawakupiga kura kana kwamba kuna mtu ambae alikuwa anajua watampigia nani!!
TUJITEGEMEE, naona unalikwepa swali la msingi lililoulizwa na Nguruvi3. Ili uchaguliwe kuwa Rais wa Marekani unahitaji kura za wajumbe 270 wa Electoral College. Marekani ina majimbo 50 lakini majimbo manne (California, Texas, Florida na New York) tayari yana EV 152 idadi ambayo ni zaidi ya nusu ya inayotakiwa Hii ina maana kwamba wajumbe 370 waliobaki watatokana na majimbo 46 sawa na wastani wa wajumbe 8 kila jimbo. Hali hii inaondoaje uwezekano wa majimbo makubwa kuwachagulia Rais majimbo madogo?Asante sana Mag3 kwa maelezo mazuri.
Lakini imesemwa kuwa hiyo Electrol Vote ipo kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa majimbo makubwa kuwachagulia rais majimbo madogo.
Wataalamu wote wa Uchumi wanasema hizo mil.200 alizorithi mwaka 1982 kama angeziweka tu kwenye benki ya akiba hivi leo angekuwa na matrilioni ya fedha. Tajiri wa kweli (Warren Buffet) mwenye hisa milioni 2 kwenye benki kubwa ya Wells Fargo hakurithi hela kama hizo alizorithi Donald Trump lakini leo hii utajiri wake unazidi bilioni 30! Pamoja na hayo hajawahi kufilisika ama kumdhulumu mtu yeyote.Huwezi kumbeza mtu aliyerithi mil.200. Lkn akaziendeleza na kufika Bill.4.6. Kwa mujibu wa Forbes huku yeye mwenyewe akisema utajiri wake unafika bill.10.!
Wenzetu wangesema unaishi kwenye bubble...nadhani swali ni je ataweza kumaliza salama hata hiyo awamu yake ya miaka minne? Binadamu aliyekwishaonja uhuru baada ya kuupigania hawezi kukubali tyranny kirahisi rahisi kama inavyotokea kwetu hapa bongo.Nakuhakikishia kinachoendelea ni upepo tu utapita na Amini usiamini trump anashinda tena 2020.
Mkuu Mag3, niliona Tujitegemee alivyokwepa swali nikaachia hapo. Nikushukuru na nichangi kidogomagode,
TUJITEGEMEE, naona unalikwepa swali la msingi lililoulizwa na Nguruvi3. Ili uchaguliwe kuwa Rais wa Marekani unahitaji kura za wajumbe 270 wa Electoral College. Marekani ina majimbo 50 lakini majimbo manne (California, Texas, Florida na New York) tayari yana EV 152 idadi ambayo ni zaidi ya nusu ya inayotakiwa Hii ina maana kwamba wajumbe 370 waliobaki watatokana na majimbo 46 sawa na wastani wa wajumbe 8 kila jimbo. Hali hii inaondoaje uwezekano wa majimbo makubwa kuwachagulia Rais majimbo madogo?
Wataalamu wote wa Uchumi wanasema hizo mil.200 alizorithi mwaka 1982 kama angeziweka tu kwenye benki ya akiba hivi leo angekuwa na matrilioni ya fedha. Tajiri wa kweli (Warren Buffet) mwenye hisa milioni 2 kwenye benki kubwa ya Wells Fargo hakurithi hela kama hizo alizorithi Donald Trump lakini leo hii utajiri wake unazidi bilioni 30! Pamoja na hayo hajawahi kufilisika ama kumdhulumu mtu yeyote.
Wenzetu wangesema unaishi kwenye bubble...nadhani swali ni je ataweza kumaliza salama hata hiyo awamu yake ya miaka minne? Binadamu aliyekwishaonja uhuru baada ya kuupigania hawezi kukubali tyranny kirahisi rahisi kama inavyotokea kwetu hapa bongo.
Tatizo letu Tanzania ni kuwa hatujawahi kuwa huru kwa hiyo hatujui maana ya kuwa huru na hii ndiyo maana wapo wenzetu wanashangilia kukandamizwa. Uhuru wa Marekani ulipatikana baada ya umwagaji wa damu na raia wengi wa Marekani ni watu waliohamia huko wakikimbia ufashisti nchini kwao. Subirini, mtawaona Wamarekani wanavyotetea huo uhuru.
Mkuu ukiangalia ramani, demography ya EU unaweza kupata clue kwanini Marekani ina uzito Europe kabla ya kuangalia mambo mengineMkuu Nguruvi3
Ninashindwa kuelewa nchi mama uingereza inavyopata shida na ushindi WA Trump.Umoja WA ulaya nao unaweeeseka na ushindi wake, najiuliza kwani umoja huu hauna nguvu za kiuchumi zaidi ya Marekani kiasi cha kuogopa hivi?
Nikiangalia nguvu za kiuchumi ya Urusi haiifikii hata Italy.Mkuu ukiangalia ramani, demography ya EU unaweza kupata clue kwanini Marekani ina uzito Europe kabla ya kuangalia mambo mengine
Population ya EU ni 788 millions, wakati USA ni 318Millions
EU ina vinchi vingi sana vikiwa na population ndogo
Kwa mfano, Population ya Los Angels ni 8M, Norway ni 5M na Sweden ni 5M
Kumbuka hapa ni Los Angeles peke yake ni si California yenye 38+M
Kwa ufupi population ya Lativia, Lithuanian, Finland, Malta, Luxembourg combine ni sawa na population ya Los Angels CA
Pili, uchumi wa Marekani ni mkubwa kuliko wa Europe kutokana na advancement na innovation katika mambo yote ikiwemo Military
Tatu, historia inaonyesha nchi za Uropa haziwezi kukabiliana zenyewe na tishio mfano ni vita kuu za dunia kama ya II. Kama si US mataifa kama UK yangalikuwa makoloni pia
Kwasababu ya nguvu za Kiuchumi/kijeshi US ni mshirika mkuu wa NATO 70%
Matishio ya Russia au China zenye nguvu, Uropa inategemea US kwa usalama wao
Pia ni ''quid pro quo'' kwamba nipe nikupe. US inategemea EU kimkakati.
Hili linaipa US upper hand off shore na kuwa na strategic point(s)
Matamshi ya Trump yanatishia NATO.
Trump ana hoja kuwa nchi zote zichangie NATO na si kuipa mzigo US pekee.
Tatizo la kauli yake ilikuwa kuiondoa au kuiona NATO haina masilahi na Marekani.
Ndiyo maana amebadili kauli na kusema zichangie
Nchi kama UK / France na Germany zenye nguvu zinaona tishio vinchi vidogo vikiwa vulnerable kwa mataifa kama Russia na China zitakuwa na tatizo pia
Mfano ni Ukraine ambayo Russia anaingia tu, hii maana yake inaweka mpaka na UK na Germany na France. Russia itawala nguvu za kiuchumi na kijeshi
Hofu ya Uropa, US kuipuuza NATO ni kukaribisha 'maadui' uani.
Hofu kwa Wamarekani ni mataifa ya Uropa yakivurugika,usalama upo matatani
Hofu ya kauli za Trump ipo pande zote, Uropa na USA
Kwanini US ina nguvu? Ni kutokana na sizable population, research, innovation, technology zinazoipa nguvu za kiuchumi na kijeshi.
Hapa kuna swali ninalisubiri!
Haya maswali unajiuliza wewe au wanajiuliza wamarekani!!? Na km wao wamarekani ndo wanajiuliza,ina maana wanajiuliza kuhusu taratibu walizojiwekea!!? Km haya maswali unajiuliza ww,swali hilo ungeweza kujiuliza km yule bibi angeshinda kwa mfumo huu huu!!??As of now this is the Presidential popular votes update...
Difference: 930,824
- Hillary Clinton: 61,781,190
- Donald trump: 60,850,366
Kwa hali inavyoelekea si ajabu Clinton akamshinda Trump kwa kura zaidi ya milioni na kuzidi kuzua maswali kuhusu kushindwa kwake huku akiwa amepata kura nyingi zaidi kutoka kwa wananchi. Utata unaojitokeza ni upi umuhimu anaopewa mwananchi anaposhiriki katika zoezi zima la upigaji kura.
Je ni haki kwa aliyepata kura chache kupewa mandate ya kuamua hatma yataifa la Marekani peke yake kama sheria na kanuni walizojiwekea zinavyotaka? Ni wazi kwamba utaratibu huu haukuzingatia hali kama hii kutokea. Na je katika hali hii sisi Watanzania tuna chochote cha kujifunza kulingana na taratibu zetu?
Wote wapenda uhuru haki za kijamii duniani kote wameumia kwa kiasi fulani kwa ujio wa mtu mbaguzi kama Donald Trump. Kwa sasa sitasema zaidi ila kama wewe ni mfuatiliaji wa matukio duniani naamini utakuwa umeona dunia ilivyopokea ujio wake kwa mshtuko, hofu na shaka. Hali hii imezidi kuchochewa na ukweli kwamba watuhumiwa wote wa ubaguzi wote wa rangi nchini Marekani wamepata hamasa na kumuunga mkono. Kwa msingi huo na mengine mengi, viongozi mbali mbali wameapa kutompa ushirikiano kama ajenda alizozihubiri majukwaani atataka azitekeleze....Mkuu Mag3 najua ww ni sehemu ya walioumia sana juu ya ushindi wa Trump. Kubali matokeo mkuu,ushabiki wa kitu chochote hauna mpaka,hoja kwamba huwezi kuumia kwa vile ww si mmarekani haikusaidii sana kisaikolojia kwa sababu ukweli unakuwa na maumivu kutokana na matokeo kwenda kinyume na matarajio.
Fuatilia wachambuzi wa siasa huko Marekani wanasemaje kuhusu hili.Hata bi clinton mwenyewe sijamsikia akizungumzia idadi ya kura alizopata. Alichoona yeye kimesababisha ashindwe ni FBI kuingilia uchaguzi ktk hatua za lala salama. Angalau hili linaweza kuwa na impact lkn si kuongelea mfumo wa uchaguzi.
Je katika elimu tuliyotoa ni ipi mimi Mag3 nimeikana au ninaikana? Nadhani kote tulisisitiza kwamba kinachoamua nani awe Rais wa Marekani ni idadi ya Electoral Votes anazopata mgombea na kwa msingi huo Donald Trump ndiye Rais mteule wa Marekani.Kabla ya uchaguzi mlitumia muda wenu mwingi sana wewe na mkuu Nguruvi3 kutoa elimu ya jinsi Rais wa us anavyopatikana.
Ni kweli nilionesha upande na kwa hilo sijuti na wala sijabadili msimamo, Donald Trump hafai kuwa Rais wa Marekani au wa nchi yoyote ile nyingine kwa sababu ni mkurupukaji. Najua wapenzi wa Rais wetu hapa Tanzanaia wanaona hiyo ni sifa, mimi siafiki na nadhani nina haki ya kuwa na mawazo tofauti kama wapiga kura wengi wa Marekani walivyoamua, walimkataa Donald Trump!Na kwa vile ww ulionyesha upande wa wazi na kumuita mgombea mwingine ni kichaa na hivyo hawezi kuchaguliwa.
Ni kweli, nisiyempenda kaja lakini hata huko Marekani wasiopenda ni wengi kuliko wanaompenda kwa idadi ya kura zaidi ya milioni!. Naomba nikufahamishe kuwa pamoja na sheria zao kutamka hivyo, hali hii inampa unyonge mkubwa Rais mteule, Donald Trump, na kwa Marekani ninayoijua tukae mkao wa kula...kizaazaa kinapiga hodi na kumbuka Rais wa Marekani si Mungu.Mkuu usiyempenda kaja!!
Mkuu Salam,Projected popular vote update: Unofficial...
Kwa kweli hali hii haikutegemewa...kwamba mshindwa anaongoza kwa kura zaidi ya milioni moja!
- Hillary Clinton: 62,562,377
- Donald trump: 61,332,151
- Difference: 1,230,226
Mkuu hili ni swali zuri sana. Nichangie kidogoWakuu wote Salaam,
Nimekuwa mfuatiliaji na msomaji wa mabandiko yenu hapa siku zote,hulka yangu ni kusoma na kuandika kidogo.
Nashukuru sana kwa jitihada zenu katika kushare nasi ujuzi,uzoefu,maarifa pia exposure mlizopata maeneo tofauti,binafsi nafaidika.
Ombi kwenu,ni itakuwa vema mkitusaidia Mara baada ya uchaguzi US kuisha,na Trump kushinda. Nini Mategemeo ya wengi baada ya ushindi wa Trump. Kwakuwa tunajua sera ndizo zinakwenda kufanya kazi.
Marekani Itegemee nini? Na Dunia Itegemee nini baada ya ushindi wa Mh Trump?
Ahsante sana Mkuu,Mkuu hili ni swali zuri sana. Nichangie kidogo
Katika mambo yanayoisumbua Marekani na dunia si Trump kama mtu. Ni Trump na sera zake
Tunaposema sera zake hatumaanishi matamashi yake yanayoleta sintofahamu
Tunazungumzia, kwamba, Trump amekwenda katika ushindi kuanzia primaries(kumbu kumbu zipo) hadi uchaguzi mkuu akiwa hana sera specific.
Kumbuka kueleza tishio la ugaidi au kurudisha ajira bila kueleza ni kwa namna gani siyo sera
Kuzungumzia ushiriki wa US katika NATO kwa kutokuwa na specific za nini atafanya ndicho chanzo cha hofu kwa washirika.
Kuzungumzia kujenga ukuta na Mexico watalipa bila kueleza wakikataa atafanya nini, siyo sera
Kuzungumzia ubaya wa Obamacare akiwa hana mbadala siyo sera
Kuzungumzia immigrants kuondoshwa bila kueleza watu milioni 11 atafanyaje, siyo sera
Kuzungumzia kukomesha ISIS bila kueleza ni kwa njia zipi si sera, ni kutisha tu watu
Kuzungumzia law and order katika masuala ya rangi kule US si sera na haielezi suluhu
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa, Trump alitumia anger , frustrations na threat kuteka mawazo ya watu. Ushindi alioputa si kwasababu ya sera, ni kutokana na factors nyingine na akiwa na mwenzake wapo waliomuona ni afadhali au ni bora au walichezewa kiakili
Kwa mfano, katika kila jambo aliloahidi Trump ame back off.
Immigration anasema hatajenga ukuta ataweka uzio baadhi ya maeneo.
Obamacare anasema hata repeal ataifanyia mbadiliko iwe na ubora.
Ushirika wa NATO amewahakikishia kuwa nao n.k.
Hofu ya wananchi na dunia si Trump kama CEO au mtu, ni vague message ambayo dunia na US haijaweza kukaa kitako na kuridhika nayo.
Nitakupa mfano, Obama kwa mara ya kwanza aliingia na sera katika platform yake.
Jambo la kwanza lilikuwa Obamacare iliyomgharimu senate na Congress kiwango cha miaka 50
Alijulikana kuhusu mazingira na mambo ya clean energy ambayo ameyasimamia katika uso wa dunia akiongoza Marekani.
Alijulikana kwa kutopenda kupeleka askari katika vita na utayari wa kumaliza vita zinazoendelea
Waliokubaliana au kutokubaliana na sera zake walikuwa na jambo moja common, kwamba, walitambua anafanya nini au atafanya nini na kwasababu zipi.
Leo haijulikani hatma ya mazingira , mikataba ya biashara , ulinzi na usalama kwasababu Trump hajaweza kuieleza ikaeleweka na sera aliyoahidi sasa anaikana kimya kimya
Hata wakati wa deep recession Markets zilitoa benefit of doubt kwa Obama kwasababu ni mtu calm
Ziliweza kubashiria anaelekea wapi na anatazama vipi mambo na kwa upana upi
Nigel Farage alipoongoza Brexit alichagizwa na nationalist tu. Hakuwa na mtazamo mwingine
Ndiyo maana alikataa nafasi ya kisiasa kwasababu alijua alichokifanya kimetimia, yaani kutimiza matakwa ya nationalist kwa kuwatisha kuhusu hatma ya UK bila kuwaeleza siku za usoni
Obama anachukua jukumu la kuihakikishia dunia kuhusu misimamo ya Marekani akijua washirika wa Marekani katika ulinzi na usalama au biashara wanaweza ku panic na miezi 2 iliyobaki ikawa na legacy mbaya sana kwake