Wakuu wote Salaam,
Nimekuwa mfuatiliaji na msomaji wa mabandiko yenu hapa siku zote,hulka yangu ni kusoma na kuandika kidogo.
Nashukuru sana kwa jitihada zenu katika kushare nasi ujuzi,uzoefu,maarifa pia exposure mlizopata maeneo tofauti,binafsi nafaidika.
Ombi kwenu,ni itakuwa vema mkitusaidia Mara baada ya uchaguzi US kuisha,na Trump kushinda. Nini Mategemeo ya wengi baada ya ushindi wa Trump. Kwakuwa tunajua sera ndizo zinakwenda kufanya kazi.
Marekani Itegemee nini? Na Dunia Itegemee nini baada ya ushindi wa Mh Trump?
Mkuu hili ni swali zuri sana. Nichangie kidogo
Katika mambo yanayoisumbua Marekani na dunia si Trump kama mtu. Ni Trump na sera zake
Tunaposema sera zake hatumaanishi matamashi yake yanayoleta sintofahamu
Tunazungumzia, kwamba, Trump amekwenda katika ushindi kuanzia primaries(kumbu kumbu zipo) hadi uchaguzi mkuu akiwa hana sera specific.
Kumbuka kueleza tishio la ugaidi au kurudisha ajira bila kueleza ni kwa namna gani siyo sera
Kuzungumzia ushiriki wa US katika NATO kwa kutokuwa na specific za nini atafanya ndicho chanzo cha hofu kwa washirika.
Kuzungumzia kujenga ukuta na Mexico watalipa bila kueleza wakikataa atafanya nini, siyo sera
Kuzungumzia ubaya wa Obamacare akiwa hana mbadala siyo sera
Kuzungumzia immigrants kuondoshwa bila kueleza watu milioni 11 atafanyaje, siyo sera
Kuzungumzia kukomesha ISIS bila kueleza ni kwa njia zipi si sera, ni kutisha tu watu
Kuzungumzia law and order katika masuala ya rangi kule US si sera na haielezi suluhu
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa, Trump alitumia anger , frustrations na threat kuteka mawazo ya watu. Ushindi alioputa si kwasababu ya sera, ni kutokana na factors nyingine na akiwa na mwenzake wapo waliomuona ni afadhali au ni bora au walichezewa kiakili
Kwa mfano, katika kila jambo aliloahidi Trump ame back off.
Immigration anasema hatajenga ukuta ataweka uzio baadhi ya maeneo.
Obamacare anasema hata repeal ataifanyia mbadiliko iwe na ubora.
Ushirika wa NATO amewahakikishia kuwa nao n.k.
Hofu ya wananchi na dunia si Trump kama CEO au mtu, ni vague message ambayo dunia na US haijaweza kukaa kitako na kuridhika nayo.
Nitakupa mfano, Obama kwa mara ya kwanza aliingia na sera katika platform yake.
Jambo la kwanza lilikuwa Obamacare iliyomgharimu senate na Congress kiwango cha miaka 50
Alijulikana kuhusu mazingira na mambo ya clean energy ambayo ameyasimamia katika uso wa dunia akiongoza Marekani.
Alijulikana kwa kutopenda kupeleka askari katika vita na utayari wa kumaliza vita zinazoendelea
Waliokubaliana au kutokubaliana na sera zake walikuwa na jambo moja common, kwamba, walitambua anafanya nini au atafanya nini na kwasababu zipi.
Leo haijulikani hatma ya mazingira , mikataba ya biashara , ulinzi na usalama kwasababu Trump hajaweza kuieleza ikaeleweka na sera aliyoahidi sasa anaikana kimya kimya
Hata wakati wa deep recession Markets zilitoa benefit of doubt kwa Obama kwasababu ni mtu calm
Ziliweza kubashiria anaelekea wapi na anatazama vipi mambo na kwa upana upi
Nigel Farage alipoongoza Brexit alichagizwa na nationalist tu. Hakuwa na mtazamo mwingine
Ndiyo maana alikataa nafasi ya kisiasa kwasababu alijua alichokifanya kimetimia, yaani kutimiza matakwa ya nationalist kwa kuwatisha kuhusu hatma ya UK bila kuwaeleza siku za usoni
Obama anachukua jukumu la kuihakikishia dunia kuhusu misimamo ya Marekani akijua washirika wa Marekani katika ulinzi na usalama au biashara wanaweza ku panic na miezi 2 iliyobaki ikawa na legacy mbaya sana kwake