Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Asante sana Mag3 kwa maelezo mazuri.

Lakini imesemwa kuwa hiyo Electrol Vote ipo kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa majimbo makubwa kuwachagulia rais majimbo madogo. Hivyo popular votes kwa msingi huo haina uhalali wa kutoa rais sahihi wa US kwa mujibu wa taratibu zao. Na hizo petition kuna uwezekano mkubwa zinatengezwa na Mainstream media, na kunauwezekano mkubwa hazionyeshi uhalisia wa Wamarekani wote. hata hivyo naziona petition Sawa na popular votes!!

Kikubwa Trump apate EV za kutosha!Vinginevyo moto utawaka, wakimnyima urais hiyo 19 December!
 
Kikubwa Trump apate EV za kutosha! Vinginevyo moto utawaka, wakimnyima urais hiyo 19 December!
TUJITEGEMEE, hayo maneno uliyoyatumia (IN RED) yanaonesha tu usivyoijua Marekani. Tayari baadhi ya wapiga kura wake wanajuta! Kwa sasa sitasema mengi ila nakuomba ufuatilie hali itakavyobadilika katika siku chache zijazo. Halafu naona sana unavyojitahidi kuwatupia lawama media kwamba inampiga vita Trump but are you sure? Nakuhakikishia bila media Trump asingefika alikofika, ni media hiyo hiyo iliyomwibua na kumfikisha hapo alipo.

Mpaka dakika hii Clinton anaongoza kwa kura (popular votes) zaidi ya nusu milioni! (566,434) Generation Y hawakuwepo kanuni za uchaguzi zilipowekwa na kwa kawaida mshindi wa popular votes anategemewa kushinda na Electoral votes na hata ikitokea (imewahi kutokea mara mbili tu katika miaka karibu200) tofauti inakuwa ndogo na si kubwa kiasi hiki.
 
Ha haa haaa! Mag3 najua ni sehemu ya walioumia,ndo maana unajitahidi kutafuta habari za kufariji. Lkn hakuna kitakachobadilika,Donald J.Trump ndo Rais wa marekani anayesubiri kuapishwa.

Unachosema ww ni kilekile kinachosemwa na wasiompenda Trump hasa vyombo vya habari. Huko nyuma tulishasema,ukiacha mambo mengine mabaya ya Trump,mambo km ya uhamiaji aliyokuwa anayasema trump ndo hasa wamarekani walikuwa wanataka kusikia.

Hilo la kupata kura nyingi za jumla kwa nini liwe kwenye mjadala sana leo wakati Al gore alishinda kwa zaidi ya kura laki 5.? Hizi ni hasira tu za wale ambao hawakupenda Trump ashinde. Waliojitokeza kupiga kura ndo wameamua nani awe Rais wao,huwezi kuongelea ambao hawakupiga kura kana kwamba kuna mtu ambae alikuwa anajua watampigia nani!!

Wengine tulijua tangu mwanzo HC hawezi kushinda,lkn mkuu mag3 kwa sababu ya sumu uliyokuwa umelishwa na vyombo vya habari ulikuwa unatubeza sana na kuna bandiko lako hapa ukisema ukimtukana kabisa trump..!! Utajitahidi sana hata sasa kutafuta habari zenye kukuonyesha kuwa Trump hafai,lkn hazitabadili ukweli!

Huwezi kumbeza mtu aliyerithi mil.200. Lkn akaziendeleza na kufika Bill.4.6. Kwa mujibu wa Forbes huku yeye mwenyewe akisema utajiri wake unafika bill.10.! Nakuhakikishia kinachoendelea ni upepo tu utapita na Amini usiamini trump anashinda tena 2020.
 
magode hakuna sehemu nimesema Trump hataapishwa kuwa Rais ila nimesema ni lazima apigiwe kura na electoral college. Toka mwanzo tumeeleza kwamba kushinda popular votes peke yake hakumpi mtu Urais na hivyo ndivyo ilivyo kulingana na taratibu walizojiwekea.

Nilichojaribu kuelezea Ni changamoto ambazo tayari zimeanza kujitokeza kabla hata hajaapishwa. Obama alichaguliwa bila mizengwe lakini angalia changamoto alizokutana nazo lakini baada ya kuapishwa. Watu wale wale walioapa kumkwamisha ndio hao hao sasa watakuwa madarakani na sasa itakuwa zamu Yao.

Donald Trump ndiye Rais wa 45 wa Marekani na Hilo halina ubishi na hakuna niliposema hatakuwa. Hata hivyo kwa dalili zinazojitokeza atapata wakati mgumu sana kutoka pande zote. Ahadi alizotoa na ambazo zimemwezesha kupata kura kutoka sehemu moja tu kubwa ya jamii moja ndizo zitamsulubu.
 
Asante sana Mag3 kwa maelezo mazuri.

Lakini imesemwa kuwa hiyo Electrol Vote ipo kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa majimbo makubwa kuwachagulia rais majimbo madogo. Hivyo popular votes kwa msingi huo haina uhalali wa kutoa rais sahihi wa US kwa mujibu wa taratibu zao. Na hizo petition kuna uwezekano mkubwa zinatengezwa na Mainstream media, na kunauwezekano mkubwa hazionyeshi uhalisia wa Wamarekani wote. hata hivyo naziona petition Sawa na popular votes!!

Kikubwa Trump apate EV za kutosha!Vinginevyo moto utawaka, wakimnyima urais hiyo 19 December!
Mkuu naomba utusaidie kidogo kwa haya yafutayo ili tukuelewe vizuri na kwa ufasaha

1. Je, hayo unayosema kuhusu electoral vote ilivyowekwa ni maoni yako au ni facts?
2. Electoral college inaundwa na watu wa kundi/makundi gani?
3. Kwanini unadhani Trump anaweza kukosa EV za kutosha?
4. Texas, California, na Florida zina EV 122 sawa na 45% ya EV zote. Je hizi hazichagui Rais kwa majimbo mengine madogo?

Tuanzie hapa kwanza
 
Nguruvi3 Asante kwa maswali yako. Majibu nimeamua kutumia nukuu za humu humu J F.

swali namba 1 na 4 majibu yapo post namba 1 ya uzi huu hapa chini pamoja na baadhi ya post zetu humu kwenye thread zinazohusu uchaguzi Marekani kwenye jukwaa hili.

ELECTORAL VOTES NA NAMNA RAIS WA MAREKANI ANAVYO PATIKANA

swali namba 2. jibu linapatikana kwenye nukuu ya The bold post namba moja ya uzi huu. Je, unajua maana halisi ya Electoral College inayotumika kuchagua Rais Marekani? Jifunze

swali namba tatu, jibu lake ni kuwa hao wenye hizo EV hawalazimishwi kuchagua rais anayetokana na chama chake. Ingawa kufanya hivyo unaweza kuonekana ni usaliti.
 
magode said:
Waliojitokeza kupiga kura ndo wameamua nani awe Rais wao, huwezi kuongelea ambao hawakupiga kura kana kwamba kuna mtu ambae alikuwa anajua watampigia nani!!
magode, waliojitokeza kupiga kura wengi wao wamempigia Hillary Clinton na mpaka dakika hii idadi yao ni kama ifuatavyo;
  • Hillary Clinton: 61,313,976
  • Donald trump: 60,537,336
Ni wazi kuwa kulingana na waliojitokeza kupiga kura Clinton kapata kura 776,640 zaidi ikiwa na maana kwamba wananchi wengi zaidi hawakumtaka Trump. Idadi hii inategemewa kufika na pengine kuvuka milioni hesabu zote zitakapokuwa tayari.

Asante sana Mag3 kwa maelezo mazuri.
Lakini imesemwa kuwa hiyo Electrol Vote ipo kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa majimbo makubwa kuwachagulia rais majimbo madogo.
TUJITEGEMEE, naona unalikwepa swali la msingi lililoulizwa na Nguruvi3. Ili uchaguliwe kuwa Rais wa Marekani unahitaji kura za wajumbe 270 wa Electoral College. Marekani ina majimbo 50 lakini majimbo manne (California, Texas, Florida na New York) tayari yana EV 152 idadi ambayo ni zaidi ya nusu ya inayotakiwa Hii ina maana kwamba wajumbe 370 waliobaki watatokana na majimbo 46 sawa na wastani wa wajumbe 8 kila jimbo. Hali hii inaondoaje uwezekano wa majimbo makubwa kuwachagulia Rais majimbo madogo?
Huwezi kumbeza mtu aliyerithi mil.200. Lkn akaziendeleza na kufika Bill.4.6. Kwa mujibu wa Forbes huku yeye mwenyewe akisema utajiri wake unafika bill.10.!
Wataalamu wote wa Uchumi wanasema hizo mil.200 alizorithi mwaka 1982 kama angeziweka tu kwenye benki ya akiba hivi leo angekuwa na matrilioni ya fedha. Tajiri wa kweli (Warren Buffet) mwenye hisa milioni 2 kwenye benki kubwa ya Wells Fargo hakurithi hela kama hizo alizorithi Donald Trump lakini leo hii utajiri wake unazidi bilioni 30! Pamoja na hayo hajawahi kufilisika ama kumdhulumu mtu yeyote.
Nakuhakikishia kinachoendelea ni upepo tu utapita na Amini usiamini trump anashinda tena 2020.
Wenzetu wangesema unaishi kwenye bubble...nadhani swali ni je ataweza kumaliza salama hata hiyo awamu yake ya miaka minne? Binadamu aliyekwishaonja uhuru baada ya kuupigania hawezi kukubali tyranny kirahisi rahisi kama inavyotokea kwetu hapa bongo.

Tatizo letu Tanzania ni kuwa hatujawahi kuwa huru kwa hiyo hatujui maana ya kuwa huru na hii ndiyo maana wapo wenzetu wanashangilia kukandamizwa. Uhuru wa Marekani ulipatikana baada ya umwagaji wa damu na raia wengi wa Marekani ni watu waliohamia huko wakikimbia ufashisti nchini kwao. Subirini, mtawaona Wamarekani wanavyotetea huo uhuru.
 
magode,

TUJITEGEMEE, naona unalikwepa swali la msingi lililoulizwa na Nguruvi3. Ili uchaguliwe kuwa Rais wa Marekani unahitaji kura za wajumbe 270 wa Electoral College. Marekani ina majimbo 50 lakini majimbo manne (California, Texas, Florida na New York) tayari yana EV 152 idadi ambayo ni zaidi ya nusu ya inayotakiwa Hii ina maana kwamba wajumbe 370 waliobaki watatokana na majimbo 46 sawa na wastani wa wajumbe 8 kila jimbo. Hali hii inaondoaje uwezekano wa majimbo makubwa kuwachagulia Rais majimbo madogo?

Wataalamu wote wa Uchumi wanasema hizo mil.200 alizorithi mwaka 1982 kama angeziweka tu kwenye benki ya akiba hivi leo angekuwa na matrilioni ya fedha. Tajiri wa kweli (Warren Buffet) mwenye hisa milioni 2 kwenye benki kubwa ya Wells Fargo hakurithi hela kama hizo alizorithi Donald Trump lakini leo hii utajiri wake unazidi bilioni 30! Pamoja na hayo hajawahi kufilisika ama kumdhulumu mtu yeyote.

Wenzetu wangesema unaishi kwenye bubble...nadhani swali ni je ataweza kumaliza salama hata hiyo awamu yake ya miaka minne? Binadamu aliyekwishaonja uhuru baada ya kuupigania hawezi kukubali tyranny kirahisi rahisi kama inavyotokea kwetu hapa bongo.

Tatizo letu Tanzania ni kuwa hatujawahi kuwa huru kwa hiyo hatujui maana ya kuwa huru na hii ndiyo maana wapo wenzetu wanashangilia kukandamizwa. Uhuru wa Marekani ulipatikana baada ya umwagaji wa damu na raia wengi wa Marekani ni watu waliohamia huko wakikimbia ufashisti nchini kwao. Subirini, mtawaona Wamarekani wanavyotetea huo uhuru.
Mkuu Mag3, niliona Tujitegemee alivyokwepa swali nikaachia hapo. Nikushukuru na nichangi kidogo

Tatizo ni wengi kuangalia mambo kwa jicho la ushabiki na ku ignore facts
Electoral votes ilivyoanzishwa kulikuwa na idea Zaidi ya 3 na zote zilionekana zina matatizo

Kama inavyoelewekwa, Philadelphia ndiko mkataba wa federal uliposianiwa na 13 states
Kwa maana hiyo electoral votes ilianzia hasa Atlantic kwa undani wake

Katika hatua mbali mbali kuna fifteenth Ammendment iliyofautiwa na Ammendment nyingi

Kwanza, kulikuwa na ushirikishwaji wa blacks ambao walikuwa disfranchised kwa bases za literacy etc. Kwamba, ili kupiga kura mzungu alisamehewa mweusi alifanyiwa test

Halafu likawepo suala la 3/5 ambapo kura ya mweusi ilikuwa ndogo kuliko whites

Na mwisho kuruhusu wanawake kupiga kura, iliyotokea chini ya miaka 100 iliyopita(920)

Electroal votes ime evolve kama ambavyo constitution ya USA imekuwa inafanyika

Hivyo mkuu Tujitegemee aitengeneza hoja bila kuwa na background ndiyo maana nilimuuliza kama yaikuwa maoni yake au facts. Laiti angefuatilia nyuzi zote angetuelewa vema

Kuhusu tatizo kwa Trump

Wengi wanadhani tatizo ni maandamano yanayoendelea. Haya yatapita tu lakini influence yake itakuwa kubwa sana. Kwa mfano, katika congress majority ni GOP, wanahitaji 51%

Katika seneti inahitajiwa 51% lakini hakuna ukomo wa kujadili. Hili ndilo linaitwa filibuster

Kwahiyo bill inaweza kupita congress ikajadiliwa na seneti kwa muda mrefu tu.

Ili kuweza kumaliza mlolongo wa mjadala kunahitajika cloture kwa kura 60.
Kwa mantiki hiyo GOP itahitaji Democrat

Kundi linaloandamana lina send message kwa Congress na seneti watakaokuwa na midterm elections mwaka 2018. Kuzidharau sauti za sasa ni kujichimbia kaburi.

Hili ndilo litalazimisha kukosa majority ya GOP, watu huhukumiwa kwa kura zao

Pili, tatizo linalotokana na waandamanaji linaelezwa vema na constitution amendment zilizofanyika ku accommodate madai mbali mbali kama wanawake kupiga kura, 3/5 ya balack kuwa 1 vote n.k.

Hivyo, si jambo la kupuuza maana Wamarekani wanaelewa haki zao na wanajua kuzidai

Tatu, waandamanaji wameanza kwa kuonyesha mashaka juu ya agenda za Trump.

Ili kupunguza kupingwa Trump ame back off mambo 3, Obamacare, immigration na Birth control.

Obamacare haitakuwa repealed itafanyiwa amendment kuacha pre existing conditions

Immigration anasema ata fence part of southern border na si kujega ukuta tena

Na suala la abortion litafanyiwa 'mjadala' kwa mujibu wa GOP

Suala la waandamanaji lina impact kubwa na Trump kampeni inalielewa ndiyo maana tone inakuwa polite na wanahangaika kutafuta the ground kabla ya kuingia oval office
 
Mkuu Nguruvi3
Ninashindwa kuelewa nchi mama uingereza inavyopata shida na ushindi WA Trump.
Umoja WA ulaya nao unaweeeseka na ushindi wake, najiuliza kwani umoja huu hauna nguvu za kiuchumi zaidi ya Marekani kiasi cha kuogopa hivi?
 
Mkuu Nguruvi3
Ninashindwa kuelewa nchi mama uingereza inavyopata shida na ushindi WA Trump.Umoja WA ulaya nao unaweeeseka na ushindi wake, najiuliza kwani umoja huu hauna nguvu za kiuchumi zaidi ya Marekani kiasi cha kuogopa hivi?
Mkuu ukiangalia ramani, demography ya EU unaweza kupata clue kwanini Marekani ina uzito Europe kabla ya kuangalia mambo mengine

Population ya EU ni 788 millions, wakati USA ni 318Millions
EU ina vinchi vingi sana vikiwa na population ndogo

Kwa mfano, Population ya Los Angels ni 8M, Norway ni 5M na Sweden ni 5M
Kumbuka hapa ni Los Angeles peke yake ni si California yenye 38+M

Kwa ufupi population ya Lativia, Lithuanian, Finland, Malta, Luxembourg combine ni sawa na population ya Los Angels CA

Pili, uchumi wa Marekani ni mkubwa kuliko wa Europe kutokana na advancement na innovation katika mambo yote ikiwemo Military

Tatu, historia inaonyesha nchi za Uropa haziwezi kukabiliana zenyewe na tishio mfano ni vita kuu za dunia kama ya II. Kama si US mataifa kama UK yangalikuwa makoloni pia

Kwasababu ya nguvu za Kiuchumi/kijeshi US ni mshirika mkuu wa NATO 70%
Matishio ya Russia au China zenye nguvu, Uropa inategemea US kwa usalama wao

Pia ni ''quid pro quo'' kwamba nipe nikupe. US inategemea EU kimkakati.
Hili linaipa US upper hand off shore na kuwa na strategic point(s)

Matamshi ya Trump yanatishia NATO.
Trump ana hoja kuwa nchi zote zichangie NATO na si kuipa mzigo US pekee.

Tatizo la kauli yake ilikuwa kuiondoa au kuiona NATO haina masilahi na Marekani.
Ndiyo maana amebadili kauli na kusema zichangie

Nchi kama UK / France na Germany zenye nguvu zinaona tishio vinchi vidogo vikiwa vulnerable kwa mataifa kama Russia na China zitakuwa na tatizo pia

Mfano ni Ukraine ambayo Russia anaingia tu, hii maana yake inaweka mpaka na UK na Germany na France. Russia itawala nguvu za kiuchumi na kijeshi

Hofu ya Uropa, US kuipuuza NATO ni kukaribisha 'maadui' uani.
Hofu kwa Wamarekani ni mataifa ya Uropa yakivurugika,usalama upo matatani

Hofu ya kauli za Trump ipo pande zote, Uropa na USA

Kwanini US ina nguvu? Ni kutokana na sizable population, research, innovation, technology zinazoipa nguvu za kiuchumi na kijeshi.
Hapa kuna swali ninalisubiri!
 
Popular votes update...
  • Hillary Clinton: 61,313,976
  • Donald trump: 60,537,336
Difference: 776,640
 
Nikiangalia nguvu za kiuchumi ya Urusi haiifikii hata Italy.
UK, German, France na Italy zinauwezo wa kuunganisha nguvu hata hao Urusi asifanye chochote.

Sema unakuta Urusi amewekeza rasilimali zake nyingi kwenye Jeshi kwa muda mrefu.
 
As of now this is the Presidential popular votes update...
  • Hillary Clinton: 61,781,190
  • Donald trump: 60,850,366
Difference: 930,824

Kwa hali inavyoelekea si ajabu Clinton akamshinda Trump kwa kura zaidi ya milioni na kuzidi kuzua maswali kuhusu kushindwa kwake huku akiwa amepata kura nyingi zaidi kutoka kwa wananchi. Utata unaojitokeza ni upi umuhimu anaopewa mwananchi anaposhiriki katika zoezi zima la upigaji kura.

Je ni haki kwa aliyepata kura chache kupewa mandate ya kuamua hatma yataifa la Marekani peke yake kama sheria na kanuni walizojiwekea zinavyotaka? Ni wazi kwamba utaratibu huu haukuzingatia hali kama hii kutokea. Na je katika hali hii sisi Watanzania tuna chochote cha kujifunza kulingana na taratibu zetu?
 
Haya maswali unajiuliza wewe au wanajiuliza wamarekani!!? Na km wao wamarekani ndo wanajiuliza,ina maana wanajiuliza kuhusu taratibu walizojiwekea!!? Km haya maswali unajiuliza ww,swali hilo ungeweza kujiuliza km yule bibi angeshinda kwa mfumo huu huu!!??

Sioni sababu ya watu kuhoji mfumo waliojiwekea wenyewe. Wakati huo huo unatuhoji watanzania tumejifunza nini ktk huo mfumo wa uchaguzi wa marekani. Tafsiri yake sijui ni nini,unaponda huo mfumo uliompa ushindi Trump,lkn wakati huo huo unaponda mfumo wetu wa uchaguzi wingi wa kura.

Kule marekani kwenyewe hakuna mjadala mkubwa kuhusu mfumo wa uchaguzi na hata wanaoandamana,hawapingi mfumo,bali wanampinga Trump hasa kutokana na misimamo yake aliyoonyesha wakati wa kampeni. Ndo maana sote tunajua ameshaanza kulegeza msimamo ktk mambo mengi tu..!!

Mkuu mag3 najua ww ni sehemu ya walioumia sana juu ya ushindi wa Trump. Kubali matokeo mkuu,ushabiki wa kitu chochote hauna mpaka,hoja kwamba huwezi kuumia kwa vile ww si mmarekani haikusaidii sana kisaikolojia kwa sababu ukweli unakuwa na maumivu kutokana na matokeo kwenda kinyume na matarajio.

Hata bi clinton mwenyewe sijamsikia akizungumzia idadi ya kura alizopata. Alichoona yeye kimesababisha ashindwe ni FBI kuingilia uchaguzi ktk hatua za lala salama. Angalau hili linaweza kuwa na impact lkn si kuongelea mfumo wa uchaguzi.

Kabla ya uchaguzi mlitumia muda wenu mwingi sana wewe na mkuu nguruvi3 kutoa elimu ya jinsi Rais wa us anavyopatikana. Na kwa vile ww ulionyesha upande wa wazi na kumuita mgombea mwingine ni kichaa na hivyo hawezi kuchaguliwa. Na km vyombo vingine vilivyokuwa vinaonyesha,clinton alikuwa na uhakika wa EV-268 kutoka blue state na alihitaji kushinda battle state moja tu ili awe Rais. Kilichotokea kila mtu anajua hapa cha kujifunza ni kuwa uchaguzi ni uchaguzi tu,mpaka ufanyike ndo utajua mshindi mengine huwa ni maoni tu lkn hayabadilishi hali halisi. Mkuu usiyempenda kaja!!
 
magode, kabla sijajibu naomba usome huu utangulizi niliowahi kuutoa kuhusu taifa la Marekani...

Kila mwaka Marekani hupokea maelfu kwa maelfu ya wageni kutoka mataifa karibia yote duniani wenye lengo moja tu; kutafuta fursa na maisha bora...kielimu, kiuchumi, kiafya na kiusalama kisiasa. Hakuna taifa lolote lingine hapa duniani lenye raia wenye asili tofauti, rangi tofauti, lugha tofauti na tamaduni tofauti kama Marekani huku wote wakiona fahari kuitwa Wamarekani. Hata Watanzania wa kila jinsia, rangi, dini, kabila, shule na maumbile wako Marekani na wengine wameamua kuchukua na uraia kabisa!

Marekani pia ni taifa pekee linalojulikana kama taifa la wahamiaji ambako ni vigumu kumkuta mtu asiye na ndugu ambaye ni raia wa taifa lingine. Ukifika Marekani umeiona dunia nzima na huna tena haja ya kujua Mrusi anafananaje, Msukuma anaongeaje, Mhindu anaabudujee, Mzulu yukoje, Mwarabu anavaaje, Mchina anakulaje...hapana, umewaona wote. Huyo aanayeitwa Mmarekani anaweza kuwa babu yako, bibi yako, babako mdogo/mkubwa, mamako mdogo/mkubwa, kakako, dadako, mwanao wa kufikia au hata shemeji yako.

Idadi ya wahamiaji wanaoishi Marekani, wasio raia, pamoja na watoto wao kwa sasa wanafikia milioni 82 (82,000,000) karibu mara mbili ya Watanzania wote. Wahamiaji hawa wengi wangefurahi kupewa uraia wa Marekani na kuachana kabisa na nchi zao za asili. Kati ya hawa asilimia 20%, pamoja na kutokuwa na vibali vya kuishi nchini humo, wako radhi wabangaize hivyo hivyo kuliko kurejea makwao na ukweli ni kwamba wanaishi vizuri zaidi kuliko awali. Hiyo ndiyo Marekani kimbilio la wenye kuelemewa na matatizo.

Kwa mwaka idadi ya watu wanaohamia Marekani ni wastani wa milioni 1.2 (1,200,000) ama kwa kuzikimbia nchi zao au kutafuta maisha bora zaidi. Nchi ya India kwa sasa ndio inaongoza ambapo mwaka 2014 idadi ya wahamiaji kutoka huko walifikia 147,500 ikifuatiwa na China watu 131,800 kwa mwaka! Idadi ya wahamiaji kutoka Afrika Mashariki peke yake inafikia 500,000! Hawa ni watu waliozikimbia nci zao na hata ukiwashawishi namna gani hawako tayari kurudi kwenye hali zao duni za awali kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mwaka 2014 asilimia 48% ya wahamiaji Marekani walikuwa Wazungu, asilimia 26% Waasia, asilima 7% Waafrika na waliobaki ama hawaeleweki au ni mchanganyiko. Asilimia 79% ya Wamarekani huongea majumbani kwa lugha ya Kiingereza, ikifuatiwa na Kihispania, Kichina na lugha zingine ndogondogo kutoka kila sehemu ya dunia pamoja na Kiswahili kwa mbaaali! Katika watu wasioweza kuongea Kiingereza kwa ufasaha, asilimia 64% huongea Kihispania (Latino), asilimia 7% huongea Kichina (Mandarin na Cantonese), Vitnamese na vilugha vidogo dogo.

Baada ya huo utangulizi, naomba nijibu baadhi ya hoja zako ambazo naamini umezitoa kwa kutoijua Marekani kama taifa la wahamiaji lililojengwa katika misingi imara ya uhuru na haki. Ni kweli imewahi kutokea misukosuko iliyosababishwa na mapungufu ya kibinadamu na ambayo kwa nyakati tofauti zimeweza kuitikisa misingi hii, lakini Marekani haikuweza kutetereka...ujio wa Trump ni moja katika hiyo misukosuko.
...Mkuu Mag3 najua ww ni sehemu ya walioumia sana juu ya ushindi wa Trump. Kubali matokeo mkuu,ushabiki wa kitu chochote hauna mpaka,hoja kwamba huwezi kuumia kwa vile ww si mmarekani haikusaidii sana kisaikolojia kwa sababu ukweli unakuwa na maumivu kutokana na matokeo kwenda kinyume na matarajio.
Wote wapenda uhuru haki za kijamii duniani kote wameumia kwa kiasi fulani kwa ujio wa mtu mbaguzi kama Donald Trump. Kwa sasa sitasema zaidi ila kama wewe ni mfuatiliaji wa matukio duniani naamini utakuwa umeona dunia ilivyopokea ujio wake kwa mshtuko, hofu na shaka. Hali hii imezidi kuchochewa na ukweli kwamba watuhumiwa wote wa ubaguzi wote wa rangi nchini Marekani wamepata hamasa na kumuunga mkono. Kwa msingi huo na mengine mengi, viongozi mbali mbali wameapa kutompa ushirikiano kama ajenda alizozihubiri majukwaani atataka azitekeleze.
Hata bi clinton mwenyewe sijamsikia akizungumzia idadi ya kura alizopata. Alichoona yeye kimesababisha ashindwe ni FBI kuingilia uchaguzi ktk hatua za lala salama. Angalau hili linaweza kuwa na impact lkn si kuongelea mfumo wa uchaguzi.
Fuatilia wachambuzi wa siasa huko Marekani wanasemaje kuhusu hili.
Kabla ya uchaguzi mlitumia muda wenu mwingi sana wewe na mkuu Nguruvi3 kutoa elimu ya jinsi Rais wa us anavyopatikana.
Je katika elimu tuliyotoa ni ipi mimi Mag3 nimeikana au ninaikana? Nadhani kote tulisisitiza kwamba kinachoamua nani awe Rais wa Marekani ni idadi ya Electoral Votes anazopata mgombea na kwa msingi huo Donald Trump ndiye Rais mteule wa Marekani.
Na kwa vile ww ulionyesha upande wa wazi na kumuita mgombea mwingine ni kichaa na hivyo hawezi kuchaguliwa.
Ni kweli nilionesha upande na kwa hilo sijuti na wala sijabadili msimamo, Donald Trump hafai kuwa Rais wa Marekani au wa nchi yoyote ile nyingine kwa sababu ni mkurupukaji. Najua wapenzi wa Rais wetu hapa Tanzanaia wanaona hiyo ni sifa, mimi siafiki na nadhani nina haki ya kuwa na mawazo tofauti kama wapiga kura wengi wa Marekani walivyoamua, walimkataa Donald Trump!
Mkuu usiyempenda kaja!!
Ni kweli, nisiyempenda kaja lakini hata huko Marekani wasiopenda ni wengi kuliko wanaompenda kwa idadi ya kura zaidi ya milioni!. Naomba nikufahamishe kuwa pamoja na sheria zao kutamka hivyo, hali hii inampa unyonge mkubwa Rais mteule, Donald Trump, na kwa Marekani ninayoijua tukae mkao wa kula...kizaazaa kinapiga hodi na kumbuka Rais wa Marekani si Mungu.
 
Projected popular vote update: Unofficial...
  • Hillary Clinton: 62,562,377
  • Donald trump: 61,332,151
  • Difference: 1,230,226
Kwa kweli hali hii haikutegemewa...kwamba mshindwa anaongoza kwa kura zaidi ya milioni moja!
 
Mkuu Salam,
Naomba nisaidie kuelewa juu ya hizo kura(Popular votes) Ambazo wachambuzi wazijadili.

Kura hizo zinatoka katika majimbo aliyoshinda Donald Trump au Hilary Clinton?

Ipi ni athari,ikiwa kura za majimbo aliyoshinda Donald Trump tayari yametoa Electoral votes za kumpa ushindi na kumkabidhi Dola Trump na majimbo machache kuja na kura za popular kuzidi?

Je,kwa mujibu wa Sheria za US kuna shida gani mtu aliyekidhi vigezo na kushinda,kutizamwa kwenye popular vote is isiyokuwa na impact kwake?
 
Wakuu wote Salaam,
Nimekuwa mfuatiliaji na msomaji wa mabandiko yenu hapa siku zote,hulka yangu ni kusoma na kuandika kidogo.

Nashukuru sana kwa jitihada zenu katika kushare nasi ujuzi,uzoefu,maarifa pia exposure mlizopata maeneo tofauti,binafsi nafaidika.

Ombi kwenu,ni itakuwa vema mkitusaidia Mara baada ya uchaguzi US kuisha,na Trump kushinda. Nini Mategemeo ya wengi baada ya ushindi wa Trump. Kwakuwa tunajua sera ndizo zinakwenda kufanya kazi.

Marekani Itegemee nini? Na Dunia Itegemee nini baada ya ushindi wa Mh Trump?
 
Mkuu hili ni swali zuri sana. Nichangie kidogo

Katika mambo yanayoisumbua Marekani na dunia si Trump kama mtu. Ni Trump na sera zake

Tunaposema sera zake hatumaanishi matamashi yake yanayoleta sintofahamu

Tunazungumzia, kwamba, Trump amekwenda katika ushindi kuanzia primaries(kumbu kumbu zipo) hadi uchaguzi mkuu akiwa hana sera specific.

Kumbuka kueleza tishio la ugaidi au kurudisha ajira bila kueleza ni kwa namna gani siyo sera

Kuzungumzia ushiriki wa US katika NATO kwa kutokuwa na specific za nini atafanya ndicho chanzo cha hofu kwa washirika.

Kuzungumzia kujenga ukuta na Mexico watalipa bila kueleza wakikataa atafanya nini, siyo sera

Kuzungumzia ubaya wa Obamacare akiwa hana mbadala siyo sera

Kuzungumzia immigrants kuondoshwa bila kueleza watu milioni 11 atafanyaje, siyo sera

Kuzungumzia kukomesha ISIS bila kueleza ni kwa njia zipi si sera, ni kutisha tu watu

Kuzungumzia law and order katika masuala ya rangi kule US si sera na haielezi suluhu

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa, Trump alitumia anger , frustrations na threat kuteka mawazo ya watu. Ushindi alioputa si kwasababu ya sera, ni kutokana na factors nyingine na akiwa na mwenzake wapo waliomuona ni afadhali au ni bora au walichezewa kiakili

Kwa mfano, katika kila jambo aliloahidi Trump ame back off.

Immigration anasema hatajenga ukuta ataweka uzio baadhi ya maeneo.
Obamacare anasema hata repeal ataifanyia mbadiliko iwe na ubora.

Ushirika wa NATO amewahakikishia kuwa nao n.k.

Hofu ya wananchi na dunia si Trump kama CEO au mtu, ni vague message ambayo dunia na US haijaweza kukaa kitako na kuridhika nayo.

Nitakupa mfano, Obama kwa mara ya kwanza aliingia na sera katika platform yake.
Jambo la kwanza lilikuwa Obamacare iliyomgharimu senate na Congress kiwango cha miaka 50

Alijulikana kuhusu mazingira na mambo ya clean energy ambayo ameyasimamia katika uso wa dunia akiongoza Marekani.

Alijulikana kwa kutopenda kupeleka askari katika vita na utayari wa kumaliza vita zinazoendelea

Waliokubaliana au kutokubaliana na sera zake walikuwa na jambo moja common, kwamba, walitambua anafanya nini au atafanya nini na kwasababu zipi.

Leo haijulikani hatma ya mazingira , mikataba ya biashara , ulinzi na usalama kwasababu Trump hajaweza kuieleza ikaeleweka na sera aliyoahidi sasa anaikana kimya kimya

Hata wakati wa deep recession Markets zilitoa benefit of doubt kwa Obama kwasababu ni mtu calm
Ziliweza kubashiria anaelekea wapi na anatazama vipi mambo na kwa upana upi

Nigel Farage alipoongoza Brexit alichagizwa na nationalist tu. Hakuwa na mtazamo mwingine
Ndiyo maana alikataa nafasi ya kisiasa kwasababu alijua alichokifanya kimetimia, yaani kutimiza matakwa ya nationalist kwa kuwatisha kuhusu hatma ya UK bila kuwaeleza siku za usoni

Obama anachukua jukumu la kuihakikishia dunia kuhusu misimamo ya Marekani akijua washirika wa Marekani katika ulinzi na usalama au biashara wanaweza ku panic na miezi 2 iliyobaki ikawa na legacy mbaya sana kwake
 
Ahsante sana Mkuu,
Nimekupata vizuri sana.
Moja: "Make America Great Again" ni slogan ya Trump na Republican yake,je slogan hii haikujengwa katika misingi ya nini kinakwenda kufanyika na Kwa namna gani? Ili kufanya America Great Again?

Pili: Hakuna utaratibu wa kuwa na sera Ambazo zimeandikwa kwaajili ya wananchi kujisomea na Mara wafanyapo maamuzi wana hakika juu ya maamuzi yao pasi kutegemea maneno ya majukwaani pekee?
 
Back
Top Bottom