El Jefe Hillary pamoja na kuonekana anaongoza kwa popular vote lakini bado yeye na Trump wapo chini ya 50% ya popular vote. Hillary hawezi kufikisha 50% ya PV maana Michigan ipo kwa Trump. Trump ana 47.1%, ila tunasubiri matokeo ambayo ni certified.
Rais wa US kutopata 50% ya PV ni kitu cha kawaida kwenye historia ya US.
Ma-Rais wafuatao wa US hawakufikisha 50% ya PV katika miaka yao ya uchaguzi:
Mkuu hapa tena una miss point. Ni kweli Marais wengi tu akiwemo maarufu kama Bill hawakupata 50%
Popular vote si kipimo cha ushindi wa kwenda WH. Hili tumelisema mapema
Hoja ya popular vote ipo katika utawala kwa ujumla wake
Kwa mfano, kila kitu atakachofanya Trump au Republican lazima ki reflect matakwa ya waliowapigia kura na wasiompigia.
Impact ya popular vote ipo katika Congress. Obama aliingia na majority upper and lower house. Midterm akapoteza house na Senate na hilo likamkwaza sana katika sera zake
Ni kwa mtazamo huo, wewe utaiangalia Marekani kwa EV 270.
Senate na Congress inategemea sehemu kubwa popula vote si jumla bali wingi.
Naomba uelewe, si jumpa bali wingi uliosambaa
Nimesoma unavyoiangalia popular vote, EV, Senate na Congress una miss connections kubwa ya vitu hivyo
Ila usisahau, D. Trump ameshinda States 30 wakati Hillary ameshinda States 20 tu na D.C. Ina maana States nyingi zinamkubali Trump
.Mkuu umekosa mengi sana katika nyuzi zetu. Ukweli ni kuwa Trump 'kashinda'state 3 ambazo ni Wisconsin, Penny na Michigan.
Tunasema hivi kwasababu kuna Red states iwe isiwe ni Republican tu
Zipo Blue state ambazo iwe usiwe zitapiga Democrat. Halafu kuna swing states
Tunasema hayo kwasababu moja. Trump alibadilisha Wisconsin na Michigan ambazo ni Blue states na hizo ndizo zimempa ushinda.
Bila state hizo mbili asingefikisha 270, alikuwa na 268 kwa kushinda swing state zote.
Suala si kashinda 30, bali alifanikiwaje kunyakua state 3 za Democrat zilizomfikisha hapo
Nadhani utaelewa hii concept na hata kama hutaelewa sitaweza kukulaumu kwasababu umekosa mengi ya nyuma ikiwemo ramani , EV, Red and Blue states, swing states n.k.
Suala lililopo hapa ni kwamba ikiwa mgombea atatumia mda wake mwingi kufanya kampeni katika majimbo makubwa ili kufikisha EV 270 anaweza kushinda. Ila ushindi wenyewe sio kirahisi kiasi kwamba mgombea anaweza kuacha kufanya kampeni katika States ndogo, maana kwenye hizo States kubwa akizidiwa hata kura mmoja tu kwenye PV ya States anapata EV sifuri haijalishi wanakaribiana kiasi gani.
Issue sio idadi ya Electoral Votes per se, bali uwezekano wa mgombea kupuuza Majimbo madogo na kukomaa na majimbo makubwa ili kufikisha 270. Majimbo madogo huwa nayo yanahusika kubadilisha matokeo. Electoral College is a genious system.
Yes majimbo madogo yanaweza kuamua.
Kwa mfano, Michigan na Wisconsin zingebaki Democrats , New Hampshire ilikwenda kwa Clinton. Jimbo ambalo linge break tie ni Maine ambayo Clinton alishinda.
Hata hivyo Maine haitumii mfumo wa winner takes all, unatumia congressional district.
Lazima uelewe uchaguzi wa Marekani unaambatana na study.
Kwa mfano, Trump alishinda Michigan na Wisconsin ambako hakutumia nguvu.
Alielekeza nguvu Iowa, NC na kwingine kama Arizona na hata Utah.
Clinton alitaka kumbana kwa swing states bila kujua Michigan na Wisconsin zingeweza kubadilisha matokeo kwa kuamini ni blue states tu.
Hivyo kuamka na kukampeni, kuna watu wanajua kazi hiyo kwa miaka nenda Rudi
David Gergen ameshauri Marais 4 wa Marekani. Ukimsikiliza atakueleza mshangao
Hillary amewadhulumu hela watu kibao wakiwemo wa Haiti + Hillary ametumia ofisi ya Secretary of State kujitajirisha na kufanya ufisadi. Sidhani kama utamuweka kwenye list yako ya 'Matajiri wa kweli'.
Mkuu madai mengine jaribu Kuyafanyia utafiti.
Kwa taarifa tu Clinton hayupo katika 'familia' ya matajiri wa US.
Hayo ya wizi unaweza kutusaidia kwa info Zaidi
Hakuna jipya kutoka kwa hao 'watetea uhuru'. Cha ajabu kuna wengine wanaandamana ila hawajui kwanini wanaandamana, mara wengine wanalipwa na akina George Soros, wengine hawakupiga kura, wengine wanafanya uharibifu, wengine wanapigana wao kwa wao, wengine wanafanya fujo, wanaogopa camera za waandishi wa habari n.k yaani vichekesho vitupu. Wafuasi wa Trump pia walikuwa na frustrations zao ila walizimaliza kwenye sanduku la kura na sio barabarani. Rais wa US hachaguliwi barabarani.
Mkuu wanaoandama wana kitu kinaitwa 'anxiety' inayotokana na mambo mengi.
Anxiety yao inazidi wanapoona yanayoendelea. Unajua matamshi ya Trump na misimamo yake ya Xenophobia, Islamophobia, Sexism, racism n.k.
Teuzi zake za washauri wa mambo ya ulinzia na usalama yanaibua hisia kubwa sana
Hao anaoteua hadi sasa wengine wapo katika record za KKK, wengine wametamka maneno makali kuhusu yale aliyosema Trump wakati wa kampeni
Kama unafuatilia appointment zake zote hadi sasa zimekumbana na upinzani mkubwa
Ni Reince Prebius peke yake ambaye hadi sasa anaungwa mkono na pande zote
Rudi Guillian tayari yupo katika matatizo. Mshauri wa kijeshi Gen Flynn ndiye alikuwa katika dinner na Putin na ana mahusiano yenye mashaka achilia mbali kauli yake nzito dhidi ya Waislam na si radical islam kama wengine. Kuna Bannon ambaye ni nationalist, n.k.
Katika frustrations na anxiety za makundi yanatotokea mengine yasiyotarajiwa.
Hapo ulipo-bold inaonekana unaamini waandamanji watamzuia Trump kutimiza ahadi zake. Fuatilia tu kwa karibu anavyoteua team yake pale Trump Tower utagundua Trump sio wa kupelekeshwa na Washington Establishment wala Liberal Media.
Impact za Waandamanaji mbona zinaonekana kwa uteuzi wake wa sasa?
Mkuu nadhani upo behind siku kadhaa. Unadhani kwanini Rudi Guillian yupo pending?
Kama unafuatilia jina lake limejitokeza sana katika maandamano.
Sababu kubwa ni uhusika wake katika kashfa ya Jame Comey. Na Inspector kutoka DOJ anachunguza kuhusu kupata habari za FBI kutoka kwa retired staff waliopata kupitia active staff.
FBI wana kiapo cha maisha, Rudi alipataje? Hilo limemweka kiporo pamoja na madai ya waandamanaji. Trump anaona resistance kubwa kama akimtaja mapema. Down the road atamteua lakini kwasasa anapata upinzani si kutoka makundi, bali Dem na GOP kwa pamoja
Hapo Trump Tower amekutana na Nick Hailey na kesho anakutana na Mitt Romney
Hawa ni the establishment na orodha ya the establishment anaokutana nao ni kubwa
Sina uhakika una maana ipi. Je,Ryan na Mconnel siyo the establishment?
Ni sum up kwa kukumbusha kuwa jitihada za Trump ni ku unite Taifa.
Anajua hawezi kudharau popular vote ambayo leo inasimama kwa 1.1M more.
Hili linatoa picha ya divided nation
Kwa US kuna maana kubwa, si suala la EV ambayo kwasasa haina maana
Maamuzi ya Trump yata impact Republican kwa matokeo mazuri au mabaya mbeleni.
Kwa mfano, antipathy dhidi ya Trump automatically Republican wataathirika.
Kama ujuavyo, GOP wana tatizo na colored people na minority ikiwemo religion
Ni kwa mtazamo huo usidhani majority katika senate na house itampa leeway.
Unakumbuka walivyo repeal executive order ya Obama majuzi kabla ya uchaguzi wakisadiwa na Democrat waliokuwa wanakwenda katika uchaguzi!