"Hoja yako ilikuwa ni transition 'so far so good'
Tukakupa hoja kuwa si nzuri kama unavyodhani.
Suala la Christie ni zito kutokana ushiriki wake kwa Trump, kuondolewa kama chair wa Transition na timbwili la Jared Kushner
Bado naamini ni so far so good.
Ishu ya Jared Kushner na Christie inaweza kuwa ime-play part kiasi fulani kuhusiana na kuondolewa kwa Christie kwenye nafasi ya juu kwenye Transition.
Lakini pia nilitaja Bridgegate Scandal ya mwaka 2013. Ukiangalia timing ya uondolewaji wenyewe wa Christie kama Chairman utagundua kuwa hiyo scandal ime-play role kubwa kuliko kutokuelewana kwake na Jared.
Wafanyakazi wake wawili walipatikana na hatia siku ya Alhamisi na siku tano baadae (Jumanne) akashushwa cheo.
Kumbuka mfanyakazi wake mmoja kati ya hao wawili alidai Chris Christie anahusika moja kwa moja na hiyo scandal.
Kule kwake New Jersey kukawa kuna watu wanataka kumu-impeach na taasisi zingine zinataka kumfanyia uchunguzi.
Na hiyo ikawa habari Trump Tower, kwamba Chairman wa Transition ana scandal. Na media kila mda walikuwa wanauliza maswali kuhusiana na Christie kwamba kwanini bado ni Chairman wa transition. Media wakaanza kurusha habari kwamba Trump anaaminije watu walioteuliwa na Christie baada ya hiyo scandal ya bridgegate wakati yeye anaenda DC ku-Drain the Swamp?
Ni siku tano tu zilipita ikaamuliwa ashushwe cheo. Ndio maana media hawajabeba bango kuhusiana na Gov. Christie maana wao ndio waliochochea aondolewe.
Hata kipindi cha Transition ya Obama mwaka 2008, Obama alimteua Gavana wa New Mexico Bill Richardson kuwa Secretary wa Commerce lakini aliondolewa kwa sababu ilisemekana anahusika na scandal ya ufisadi huko New Mexico na nafasi yake ikachukuliwa na Gary Locke.
Unaelewa kwanini anazungumza na watu wengi ?
Trump anategemewa kuteua watu kwenye nafasi 1270 zitakazoidhinishwa na Senate na nafasi 363 ambazo sio za kuidhinishwa na Senate. Unategemea azungumze na watu wachache?
Lakini kama mtu anaamini Trump anakutana na wengi kwa sababu anawabembeleza na hawataki kufanya nae kazi, huyo mtu atakuwa na tatizo.
Trump alisema ata repeal siku ya kwanza. Halafu akashauriwa asema ata repeal and replace.Hapa atakuwa ame repeal au amefanyia amendment? Nifahaimishe kidogo upungufu wangu wa kuelewa
Ninachoamini ni kwamba repeal na replace ya ACA haitafanyika day one ila itafanyika baada ya day one.
Trump kasema ataweka fence na suala la Ukuta ni kama halipo. Inawezekana una habari zaidi, tusaidie
Alisema sehemu ndogo itakuwa ni fence na sehemu kubwa ni ukuta na akasema yeye ni mzuri kwenye construction.
Sijui kama una-refer ile interview yake na CBS ya una reference nyingine.
Swali la
Mag3 ni kuwa unaamini atafukuza illegal immigrants katika siku 100? Hilo ndilo swali uliloulizwa.
Tulitegemea kusikia kama atafanya hiyo au la
Swali sio kuweza kufukuza bali atafukuza wangapi.
Trump alivyokuwa kwenye debates za primaries alisema atafukuza illegals mil 11+. Binafsi niliona ngumu.
Alivyosema illegals mil 2-3 ambao ni hatari kwa Marekani nadhani inawezekana. Inategemea na sababu atakazotoa mda huo.
Lakini ufukuzwaji mkubwa wa watu wengi nadhani utatokea baada ya ukuta kujengwa.
Hoja ya
Mag3 ni kuwa Bannon alishiriki katika Braitbart ambayo ni alt-right. Je, hilo ni kweli au sik kweli?
Je madai dhidi ya Session hayana mrengo wa hisia za kibaguzi?
Aliponyimwa u judge 30 yrs na leo kauli inajirudia hakuna hisia za ubaguzi?
Kwa wanaodhani ni hivyo
Kauli zake za 30 yrs zinapolinganishwa na za Trump wakati wa kampeni hapo hakuna hisia za kibaguzi kwa wanaofikiria hivyo?
Nikipima ukweli kuhusu Bannon ni kwamba naona ni mtu mzalendo na conservative ambaye alikuwa concerned na nchi yake inakoelekea kama ambavyo zaidi ya 60% ya wamarekani hawakuridhika na Obama alikokuwa anawapeleka.
Kwahiyo sio sahihi kutumia brush kubwa kuipaka Braitbart org. kuwa ni alt-right kwa article moja na kuacha kuzungumzia maelfu ya articles ambazo wamezitoa.
Lakini pia mtu anaweza akazungumza jambo fulani halafu waandishi wa habari wakachukua sentensi moja tu wakatengeneza headline na maneno mengine wakaya-ignore, pengine kwa sababu hayo maneno mengine yanaweza kufanya headline ikaonekana ni uongo.
Kama mtu anachukua sample za articles za Braitbart kwa lengo la kuielewa hiyo org., nadhani ni sahihi zaidi kama sample zenyewe zikiwa balanced na sio biased.
Kuhusiana na Sen. Sessions sijakataa kwamba hisia za kibaguzi hazipo kabisa. Ila ukweli ni kwamba hisia zenyewe ni insignificant na zilichochewa na/au zinachochewa na makundi fulani.
January inavyokaribia Sen. Sessions anazidi kupata endorsements nyingi za asasi za kiraia na kiulinzi za US ambazo zina democrats na minorities.
Hivi African-America walimpigia Trump kwa wingi kuliko Hillary? Unazo takwimu za hili maana wengine hatukuona hivyo, tusaidie
Hillary ameongoza kwa African Americans (88% kwa 8%) sikatai ingawa ni kiwango cha chini ukilinganisha na cha Obama 2012 (93%).
Na Trump amepata African Americans wakiume 13% ukilinganisha na wakike 4%. Ukilinganisha na miaka ya nyuma, wanaume weusi wengi wameanza kupita kura bila kufuata mkumbo.