Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

Kuna hizi hoja tungependa kusikia maoni yako

Mkuu, huenda labda nikawa natoka nje ya mada lakini naamini bado niko ndani ya wigo ule ule wa uchaguzi wa Marekani uliokwisha hivi karibuni.

Unakumbuka kuna wakati nilikuhoji kuhusu baadhi ya kauli za Trump kuhusu Waafrika na watu weusi kwa ujumla ambazo zilikuwa zimeenea sana mtandaoni na nikakuambia hizo habari ni uzushi mtupu?

Naona sasa hilo tatizo limekuwa kubwa kiasi cha kuifanya Facebook kuanza kuchuja habari zote zinazowekwa huko.

Kuna watu wameilalamikia Facebook kuwa iliruhusu mno uwepo wa habari za kizushi ambazo wengine wanadai zilisaidia kumpatia ushindi Bw. Trump.

Kwa habari zaidi bofya hichi kiunganishi Mark Zuckerberg Explains How Facebook Plans to Fight Fake News

Mark Zuckerberg late Friday outlined several steps Facebook Inc. is testing to fight misinformation, an acknowledgment that the social network could be doing more to avoid its proliferation.

Facebook is looking to label certain stories as false, build tools to classify misinformation and work with fact-checking groups, Mr. Zuckerberg, chief executive and co-founder, said in a post.

“We take misinformation seriously,” Mr. Zuckerberg wrote. “We know people want accurate information.”

Halafu kuna hizi nukuu ambazo zinadaiwa ni za Mugabe...umeziona? Yaani ni uzushi mtupu lakini cha kinachosikitisha zaidi ni kwamba kuna watu wanaoziamini kabisa kuwa ni maneno ya huyo mzee.
 
"Mag3, post: 18575583, member: 10873"]Labda tuanzie hapa, hizo unazoita mainstream media ni zipi na ambazo si mainstream ni zipi unazozisikiliza wewe? Je ni katika jamii zipi na wasikilizaji na wasomaji wake ni nani? Je ni mainstream tu ndani ya Marekani ama nje ya Marekani?
Maswali haya nimewauliza magode siku za nyuma na hivi karibuni El Jefe . Hakuna aliyejibu isipokuwa wanaamini tu kitu kinaitwa main stream media. Niliwauliza, New York post, Wall strret Journal na Fox news zinawezaje kuwa tofauti? Hakuna aliyejibu. Nikaendelea kuwauliza, The Telegraph, Herald, The Sun, Hauffington post, Times, CNN zinakuwaje main stream media kwa upande mmoja na zikitengwa kwa baadhi ya nyakati? Hakuna analiyejibu kwasababu wanaamini katika neno mainstream media na si maana yake. Na wataendelea hivyo kwasababu wanataka point za ku justifu ManU na Aresenal nani zaidi.

Mkuu Mgaya D.W, matarajio ya ujio wa Trump ndani ya Marekani ni tofauti kidogo na nje ya Marekani. Ndani ya Marekani tutashuhudia juhudi zaidi za kuwaleta pamoja Wamarekani pamoja bila kujali tofauti zao. Tofauti na huko nyuma juhudi hizo zitaongozwa zaidi na viongozi na hasa wa Democrats kama alivyoanza kuonesha Rais Obama. Hii ni tofauti kabisa na namna Obama mwenyewe alivyopokelewa akiingia madarakani na vituko alivyofanyiwa na Republicans kwa kuapa kutompa ushirikiano. Hali ya baadaye itategemea serikali chini ya Trump itakavyopokea orange leaf kutoka kwa Democrats ila hali inaweza kuwa tete sana kama Trump atajawa kiburi na kuwapuuza.
Tatizo nikuwa rhetoric za Trump zinaanza ku backfire mapema. VP alipoelezwa ukweli 'Hamilton' yeye alikubali hakuna tatizo, Trump akaanza strings za tweets na kulikuza jambo hilo. Kidonda bado ni kibichi. Pamoja na jitihada za Obama kuleta taifa pamoja, kazi ya kulileta taifa inategemea mkono utakaotolewa na Trump na si Republican.

GOP wanaelewa tatizo la divided nation na ukiwasikiliza utaliona hilo. Ninachokiona ni upinzani mkali sana kwa Trump siku za mbeleni kutokana na anxiety na uncertainty kati ya makundi ya jamii.

Mfano, teuzi za watu wanaotiliwa shaka kwa 'moral ethical' zao ni tatizo na mmoja ni Sessions.
Kuna jamii haitakubaliana na kila atakachofanya hata kama ni sahihi kwasababu tu kuna 'prejudice' kuwa Trump anachuki na section ya jamii na ameteua mwenye chuki ili kutimiza lengo lake.
Nje ya Marekani, indiketa zimeshaonesha madhara yanayoweza kutokea na hivyo tusitarajie Trump kutekeleza aliyokuwa akiyahubiri majukwaani. Sana sana anategemewa kupunguza kwa kiasi kikubwa rhetoric zake kwa nchi ambazo zimekuwa marafiki wa Marekani. Kumbuka kwamba pamoja na kuwa Rais, Trump si kila kitu na asitegemee kuungwa mkono na Republicans wakati wote akitoka nje ya mstari. Heri yake iko katika kujenga daraja kuwaleta karibu wahasimu wake kutoka upinzani na anaweza hata kuwashirikisha wengine kwenye serikali yake. Hiyo ndiyo maana ya nchi kuitwa Republic, ukishinda huatamii kila kitu...walioshindwa nao mawazo yao hupewa kipaumbele
Kwa siasa za nje, kuna hamaki kubwa sana kutokana na kile kile kauli zake.

Hivyo kila kauli atakayotoa itakuwa na strings za rhetoric
Nadhani kuungwa mkono 'coalition' kama aliyopata Obama kutakuwa na tatizo sana

Lakini kubwa zaidi anaangaliwa atakavyo deal na trade war na China, au atakavyo counter political clout ya Russia katika global politics.

Nilimsikiliza Lt General Flynn jana, ni wazi suala la ISIS wanaliangalia kwa mtazamo ule ule wa Obama wa kushirikisha ally hasa wa middle east. Si suala la 'Bom the hell' tena kama alivyoahidi

Kwa bahati mbaya ile ''reservation'' kuhusu moslems ipo na atakabiliwa na mistrust kati yake na washirika. Hivyo siasa za nje zitakuwa ngumu kwa upande wake
 
Mkuu, huenda labda nikawa natoka nje ya mada lakini naamini bado niko ndani ya wigo ule ule wa uchaguzi wa Marekani uliokwisha hivi karibuni.

Unakumbuka kuna wakati nilikuhoji kuhusu baadhi ya kauli za Trump kuhusu Waafrika na watu weusi kwa ujumla ambazo zilikuwa zimeenea sana mtandaoni na nikakuambia hizo habari ni uzushi mtupu?

Naona sasa hilo tatizo limekuwa kubwa kiasi cha kuifanya Facebook kuanza kuchuja habari zote zinazowekwa huko.

Kuna watu wameilalamikia Facebook kuwa iliruhusu mno uwepo wa habari za kizushi ambazo wengine wanadai zilisaidia kumpatia ushindi Bw. Trump.

Kwa habari zaidi bofya hichi kiunganishi Mark Zuckerberg Explains How Facebook Plans to Fight Fake News
Halafu kuna hizi nukuu ambazo zinadaiwa ni za Mugabe...umeziona? Yaani ni uzushi mtupu lakini cha kinachosikitisha zaidi ni kwamba kuna watu wanaoziamini kabisa kuwa ni maneno ya huyo mzee.
Niliona habari nyingi sana zilizokuwa fake zikiorodheshwa na kuna mjadala kuhusu hilo
Na si FB, hata tweets ambazo zilitumika ku mislead public in a way

Hapa ndipo tunaona the other side of tech kwamba si lazima iwe positive tu, kuna negative side
Kwa uchaguzi huu, nadhani utabadili sana mtazamo dhidi ya social media
 
"
El Jefe, post: 18575726, member: 387168"]Chris Christie na washirika wake watakapopewa vyeo vikubwa uje urudi kubadilisha hizi statements.
Hoja yako ilikuwa ni transition 'so far so good'
Tukakupa hoja kuwa si nzuri kama unavyodhani.

Suala la Christie ni zito kutokana ushiriki wake kwa Trump, kuondolewa kama chair wa Transition na timbwili la Jared Kushner
Kila anaeteuliwa mnadai ni 'controversial'. Trump ni Rais independent wa kwanza katika historia ya US.
Kama independent ina maana tofauti usemayo ni kweli, kama ina maana tunayojua kuna tatizo
Ben Carson anavyozungumza ni kwamba anaona watu wanavyoweka expectation kubwa kwake kwenye Dept. of Health and Human services na amejipima akaona atulie kwanza. Kwa kifupi anaona kuna wengine wana uwezo wa ku-perform kuliko yeye.
Hizi ni kauli za Ben au ni maoni yako?
Trump anazungumza na watu wengi na nafasi ni nyingi, sio kwamba mtu akikataa ina maana kuna tatizo kwenye Transition. Hawa watu wanajipima.
Unaelewa kwanini anazungumza na watu wengi ?
Inaweza isiwe siku ya kwanza ofisini lakini itakuwa repealed na kuwa replaced kwa namna moja au nyingine.
Trump alisema ata repeal siku ya kwanza. Halafu akashauriwa asema ata repeal and replace.
Hata kwa kutumia Reconcilliation Bills kuimega ACA kidogo kidogo hadi ifike hatua haina maana kuwepo.
Hapa atakuwa ame repeal au amefanyia amendment? Nifahaimishe kidogo upungufu wangu wa kuelewa
Ukuta utajengwa. Kama Hillary aliweza kuipigia kura Secure Fence Bill ya mwaka 2006 na baadae Rais Bush akaisaini, usidhani ni Reps tu ndio wanaoitaka hiyo Border Wall.
Trump kasema ataweka fence na suala la Ukuta ni kama halipo. Inawezekana una habari zaidi, tusaidie
Hivi unafikiri Trump atatoa amnesty kama aliyotoa Obama ya illgegal immigrants millioni 5?
Swali la Mag3 ni kuwa unaamini atafukuza illegal immigrants katika siku 100? Hilo ndilo swali uliloulizwa.

Tulitegemea kusikia kama atafanya hiyo au la
Haya ni maoni ya akina Van Jones, Anderson Cooper, Jake Tapper, Rachel Maddow, na Wolf Blitzer. Umebeba kama yalivyo umeleta huku.
Hoja ya Mag3 ni kuwa Bannon alishiriki katika Braitbart ambayo ni alt-right. Je, hilo ni kweli au sik kweli?

Je madai dhidi ya Session hayana mrengo wa hisia za kibaguzi?

Aliponyimwa u judge 30 yrs na leo kauli inajirudia hakuna hisia za ubaguzi?
Kwa wanaodhani ni hivyo

Kauli zake za 30 yrs zinapolinganishwa na za Trump wakati wa kampeni hapo hakuna hisia za kibaguzi kwa wanaofikiria hivyo?
Usiwe kama Kanye West, Ukimsikiliza vizuri utagundua alivyoenda kwenye voting booth alimtosa bibi kama African Americans wengi walivyofanya
Hivi African-America walimpigia Trump kwa wingi kuliko Hillary? Unazo takwimu za hili maana wengine hatukuona hivyo, tusaidie
 
Kwa maoni hayo inaonekana hata Rep. Trey Gowdy wa South Carolina ni mropokaji.
Nilimtaja Rep. Jason Chaffetz na asante sana kwa kumuongezea na huyo kwenye listi ya waropokaji kama mwenyewe unavyokiri.
Chris Christie na washirika wake watakapopewa vyeo vikubwa uje urudi kubadilisha hizi statements.
Ninalolijua ni kuwa Christie alikuwa fired kama mwenyekiti wa kamati na nafasi yake akapewa mtu mwingine, hayo ya baadaye unayajua wewe.
Kila anaeteuliwa mnadai ni 'controversial'. Trump ni Rais independent wa kwanza katika historia ya US.
Point of correction...la kwanza, Trump anakuwaje Rais independent wa kwanza US? Independent kivipi? Nadhani tatizo ni kwamba ushabiki unakutia upofu. La pili unaposema tunadai, sisi ni akina nani? Je madai yanayotolewa dhidi yao yakiambatanishwa na ushahidi wa video, sauti na maandishi ni uongo?
Ben Carson amejipima akaona atulie kwanza. Kwa kifupi anaona kuna wengine wana uwezo wa ku-perform kuliko yeye.
Siku za Awali Ben Carson alipoulizwa kama atakuwa tayari kujiunga na serikali ya Trump, alijibu akisema yuko tayari kwa nafasi yoyote ile atakayopewa. El Jefe, najua una miezi miwili tu toka umejiunga jamvini lakini kumbuka hii ni JF na inatunza kumbukumbu.
Mwingine ni Jamie Dimon (CEO wa JPMorgan) naye bado anajipima na anasema ikitokea kwamba ni yeye pekee ndiye anayetakiwa kuwa Treasury Secretary atakubali.
Eti bado anajipima...hivi hawa watu wanaongea na wewe saa ngapi maanake sidhani kama unaweza kuthubutu kutamka vitu kama hivi kutoka kichwani tu.
Trump anazungumza na watu wengi na nafasi ni nyingi, sio kwamba mtu akikataa ina maana kuna tatizo kwenye Transition. Hawa watu wanajipima.
Je umejiuliza kwa nini Trump anawaita in the first place...kwamba hajui uwezo wao? Kwamba anaamka tu na kumwita mtu! Kubali usikubali kuna utata mwingi kwenye transition na sasa inaonekana wapo anaowabembeleza wakubali kuingia kwenye serikali yake.
Inaweza isiwe siku ya kwanza ofisini lakini itakuwa repealed na kuwa replaced kwa namna moja au nyingine. Hata kwa kutumia Reconcilliation Bills kuimega ACA kidogo kidogo hadi ifike hatua haina maana kuwepo.
Tatizo kubwa humu ni kwamba wengi mmeanza kuchangia huu uchaguzi wa Marekani juzi juzi tu. Mngekuwa mmefuatilia toka hatua za mwanzo za kampeni na ahadi za wagombea hungesema ulilolisema hapo juu. Kwa nini unaleta mawazo yako binafsi badala ya kujikita kwenye facts?
Ukuta utajengwa. Kama Hillary aliweza kuipigia kura Secure Fence Bill ya mwaka 2006 na baadae Rais Bush akaisaini, usidhani ni Reps tu ndio wanaoitaka hiyo Border Wall.
Trump alieleza wazi kabisa ukuta anaotaka kuujenga na jinsi utakavyogharamiwa. Hata hivyo nakupa benefit of doubt, tusubiri huo ukuta wa Trump ambao urefu wake utakuwa moja katika maajabu ya dunia!
Wewe hukuamini Trump anaweza kuwa Rais na akawa. Hapa umetaja vitu ambayo huamini kama vitafanyika. Vikishafanyika utashikilia vingine na kuanza kudai haviwezi kufanyika.
Nilisema wazi kabisa kwamba Trump hafai kuwa Rais wa Marekani na kwamba Wamarekani ambao nimebahatika kuwafahamu hawawezi kumpigia kura. Msimamo wangu bado ni huo huo...hafai na Wamarekani wengi hawakumpigia kura. Kuhusu kuwa Rais, nakubali Trump ndiye Rais wa 45 wa USA.
Hivi unafikiri Trump atatoa amnesty kama aliyotoa Obama ya illgegal immigrants millioni 5?
Kwanza, huo ni uongo na ni propaganda ya wakurupukaji kama Rep. Chaffetz, Obama hajatoa amnesty kwa illegal immigrants...labda neno amnesty silijui. Pili, Obama amewarudisha makwao illegal immigrants wengi kuliko MaRais wa Marekani waliomtangulia.
Haya ni maoni ya akina Van Jones, Anderson Cooper, Jake Tapper, Rachel Maddow, na Wolf Blitzer. Umebeba kama yalivyo umeleta huku.
El Jefe, una tatizo. Nimetazama sana CNN na hakuna siku imekuwepo panel inayowakilisha upande moja. Sitawataja kwa majina lakini nina hakika unajua naongelea nini. Linapokuja swala la MSNBC pia nawatazama sana ingawa wao si wakati wote wanakuwa na wawakilishi wa pande zote, liberals na conservaties, linapotokea jambo tata wanatafuta maoni ya upande wa pili.
Mbona Megyn Kelly humtaji? au kwa sababu alikuwa upande wa bibi?
Megyn Kelly hakuwa upande wa bibi kama una maana ya Hillary Clinton, alikuwa anapinga unyanyasaji wa wanawake kwa ujumla wao mikononi mwa Trump, yeye naye akiwa muathirika mojawapo.
Mkuu, Hannity amekufanyaje? Inaonekana unamkubali lakini huku mbele za watu hutaki kusema. Nawasikiliza wengi lakini mwisho wa siku napima ukweli upo wapi.
Bila shaka wewe hujui vita alivyoendesha Hannity dhidi ya mtu mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani, Barack Husein Obama. Fukua Jamii Forums ya miaka hiyo ujionee alivyovalia njuga rangi, dini na uraia wa Obama. Ni yeye alikuwa mpiga filimbi wa tapeli Donald Trump na kila mara alikimbilia kwake akitaka kusafishwa madhambi yake.

Lakini la pili ni kwamba Hannity hana sifa ya kuitwa mwandishi wa habari, hakusomea bali alibebwa tu kwa sababu ya msimamo wake wa chuki dhidi ya weusi.
Usiwe kama Kanye West ambaye anajuta kutompigia kura Trump. Alikuwa mshabiki wa Trump lakini hakuweza kusema publicly kabla ya uchaguzi.
Yawezekana Kanye West hakuwa anawakilisha mtu weusi, alikuwa akijiwakilisha yeye na kutafuta namna ya kupata zile bilioni alizokuwa akizihitaji kufanikisha malengo yake na kulipa madeni.
 
Point of correction...la kwanza, Trump anakuwaje Rais independent wa kwanza US? Independent kivipi? Nadhani tatizo ni kwamba ushabiki unakutia upofu.
Mkuu kuna bandiko langu 205 linawasubiri , lipo jingine wamelikimbia

Hapa ndipo tunasema ushabiki unadhuru baadhi yetu

Chief of the sraff ni chair wa RNC bado watu wanaamini Trump alikuwa independent candidate.

Hii hoja ni sawa ni ile waliyosema 'Obama amsamehe Clinton kwasababu anachunguzwa na tume 4 za Bunge''.

Tuliwauliza hiyo inaitwaje kwa sheria za Marekani?

Jibu ni 'presidential pardon' kwamba Rais anaweza kumsamehe Mitch Mconnel au Nancy Pelosi from nowhere na bila kosa.

Obama anatoa 'pres.pardon' kwa watu wasio na hatia. Imagine!

Anaamka na kusamehe watu! kwa 'presidential pardon', sijui ni kitu gani

Akina magode hawafahamu kuwa Trump baada ya ushindi ameona ugumu kule Washington, anawataka the establishment.

Katika hilo anawaita katika interview, ukweli, anataka ukaribu nao kwasababu kuna house na senate ambazo majority ni 'the establishment'

Katika kulaghai akina El Jefe, eti amemwita Rudi Guillian katika interview pia

Hivi Rudi aliyekuwa mshauri mkuu kuanzia debate na mipango mingine Trump hajui uwezo wake? Akina magode wanadhani ni vetting, dah

Obamacare tumewauliza inakuwa repealed and replace, wao wanasema itafanyiwa amendment. Hapa tatizo ni lugha wala siyo Trump kama tunavyoona 'independent'
 
"Hoja yako ilikuwa ni transition 'so far so good'
Tukakupa hoja kuwa si nzuri kama unavyodhani.
Suala la Christie ni zito kutokana ushiriki wake kwa Trump, kuondolewa kama chair wa Transition na timbwili la Jared Kushner

Bado naamini ni so far so good.

Ishu ya Jared Kushner na Christie inaweza kuwa ime-play part kiasi fulani kuhusiana na kuondolewa kwa Christie kwenye nafasi ya juu kwenye Transition.

Lakini pia nilitaja Bridgegate Scandal ya mwaka 2013. Ukiangalia timing ya uondolewaji wenyewe wa Christie kama Chairman utagundua kuwa hiyo scandal ime-play role kubwa kuliko kutokuelewana kwake na Jared.

Wafanyakazi wake wawili walipatikana na hatia siku ya Alhamisi na siku tano baadae (Jumanne) akashushwa cheo.

Kumbuka mfanyakazi wake mmoja kati ya hao wawili alidai Chris Christie anahusika moja kwa moja na hiyo scandal.

Kule kwake New Jersey kukawa kuna watu wanataka kumu-impeach na taasisi zingine zinataka kumfanyia uchunguzi.

Na hiyo ikawa habari Trump Tower, kwamba Chairman wa Transition ana scandal. Na media kila mda walikuwa wanauliza maswali kuhusiana na Christie kwamba kwanini bado ni Chairman wa transition. Media wakaanza kurusha habari kwamba Trump anaaminije watu walioteuliwa na Christie baada ya hiyo scandal ya bridgegate wakati yeye anaenda DC ku-Drain the Swamp?

Ni siku tano tu zilipita ikaamuliwa ashushwe cheo. Ndio maana media hawajabeba bango kuhusiana na Gov. Christie maana wao ndio waliochochea aondolewe.

Hata kipindi cha Transition ya Obama mwaka 2008, Obama alimteua Gavana wa New Mexico Bill Richardson kuwa Secretary wa Commerce lakini aliondolewa kwa sababu ilisemekana anahusika na scandal ya ufisadi huko New Mexico na nafasi yake ikachukuliwa na Gary Locke.

Unaelewa kwanini anazungumza na watu wengi ?

Trump anategemewa kuteua watu kwenye nafasi 1270 zitakazoidhinishwa na Senate na nafasi 363 ambazo sio za kuidhinishwa na Senate. Unategemea azungumze na watu wachache?

Lakini kama mtu anaamini Trump anakutana na wengi kwa sababu anawabembeleza na hawataki kufanya nae kazi, huyo mtu atakuwa na tatizo.

Trump alisema ata repeal siku ya kwanza. Halafu akashauriwa asema ata repeal and replace.Hapa atakuwa ame repeal au amefanyia amendment? Nifahaimishe kidogo upungufu wangu wa kuelewa

Ninachoamini ni kwamba repeal na replace ya ACA haitafanyika day one ila itafanyika baada ya day one.

Trump kasema ataweka fence na suala la Ukuta ni kama halipo. Inawezekana una habari zaidi, tusaidie

Alisema sehemu ndogo itakuwa ni fence na sehemu kubwa ni ukuta na akasema yeye ni mzuri kwenye construction.

Sijui kama una-refer ile interview yake na CBS ya una reference nyingine.

Swali la Mag3 ni kuwa unaamini atafukuza illegal immigrants katika siku 100? Hilo ndilo swali uliloulizwa.
Tulitegemea kusikia kama atafanya hiyo au la

Swali sio kuweza kufukuza bali atafukuza wangapi.

Trump alivyokuwa kwenye debates za primaries alisema atafukuza illegals mil 11+. Binafsi niliona ngumu.

Alivyosema illegals mil 2-3 ambao ni hatari kwa Marekani nadhani inawezekana. Inategemea na sababu atakazotoa mda huo.

Lakini ufukuzwaji mkubwa wa watu wengi nadhani utatokea baada ya ukuta kujengwa.

Hoja ya Mag3 ni kuwa Bannon alishiriki katika Braitbart ambayo ni alt-right. Je, hilo ni kweli au sik kweli?
Je madai dhidi ya Session hayana mrengo wa hisia za kibaguzi?
Aliponyimwa u judge 30 yrs na leo kauli inajirudia hakuna hisia za ubaguzi?
Kwa wanaodhani ni hivyo
Kauli zake za 30 yrs zinapolinganishwa na za Trump wakati wa kampeni hapo hakuna hisia za kibaguzi kwa wanaofikiria hivyo?
Nikipima ukweli kuhusu Bannon ni kwamba naona ni mtu mzalendo na conservative ambaye alikuwa concerned na nchi yake inakoelekea kama ambavyo zaidi ya 60% ya wamarekani hawakuridhika na Obama alikokuwa anawapeleka.

Kwahiyo sio sahihi kutumia brush kubwa kuipaka Braitbart org. kuwa ni alt-right kwa article moja na kuacha kuzungumzia maelfu ya articles ambazo wamezitoa.

Lakini pia mtu anaweza akazungumza jambo fulani halafu waandishi wa habari wakachukua sentensi moja tu wakatengeneza headline na maneno mengine wakaya-ignore, pengine kwa sababu hayo maneno mengine yanaweza kufanya headline ikaonekana ni uongo.

Kama mtu anachukua sample za articles za Braitbart kwa lengo la kuielewa hiyo org., nadhani ni sahihi zaidi kama sample zenyewe zikiwa balanced na sio biased.

Kuhusiana na Sen. Sessions sijakataa kwamba hisia za kibaguzi hazipo kabisa. Ila ukweli ni kwamba hisia zenyewe ni insignificant na zilichochewa na/au zinachochewa na makundi fulani.

January inavyokaribia Sen. Sessions anazidi kupata endorsements nyingi za asasi za kiraia na kiulinzi za US ambazo zina democrats na minorities.

Hivi African-America walimpigia Trump kwa wingi kuliko Hillary? Unazo takwimu za hili maana wengine hatukuona hivyo, tusaidie
Hillary ameongoza kwa African Americans (88% kwa 8%) sikatai ingawa ni kiwango cha chini ukilinganisha na cha Obama 2012 (93%).

Na Trump amepata African Americans wakiume 13% ukilinganisha na wakike 4%. Ukilinganisha na miaka ya nyuma, wanaume weusi wengi wameanza kupita kura bila kufuata mkumbo.
 
Nilimtaja Rep. Jason Chaffetz na asante sana kwa kumuongezea na huyo kwenye listi ya waropokaji kama mwenyewe unavyokiri.

Walim-grill sana Hillary kwenye Congressional Hearing. Hisia zako zinaeleweka.

Ninalolijua ni kuwa Christie alikuwa fired kama mwenyekiti wa kamati na nafasi yake akapewa mtu mwingine, hayo ya baadaye unayajua wewe.
Chris Christie amekuwa 'demoted' na sio 'fired' maana ukisema 'fired' ni kama amefukuzwa kazini.

Chris Christie bado ni Vice Chairman wa Transition Team.

Point of correction...la kwanza, Trump anakuwaje Rais independent wa kwanza US? Independent kivipi? Nadhani tatizo ni kwamba ushabiki unakutia upofu. La pili unaposema tunadai, sisi ni akina nani? Je madai yanayotolewa dhidi yao yakiambatanishwa na ushahidi wa video, sauti na maandishi ni uongo?

Kuna perspective nyingi za kuwa independent:

(i) Trump amejigharamia kampeni zake kwahiyo hana special interests na lobbyists wakumuendesha.

(ii) Trump amekuwa Rais ambaye hana political experience.

(iii) Trump yupo against Washington establishment.

Nikitaka kupaza sauti mbele za watu na kusema mtu fulani yupo hivi au yupo vile inabidi niwe na ushahidi mwingi usio na shaka kuhusiana na huyo mtu. Na kama kuna upande wa utetezi wana cha kuongea huwa nawasikiliza na wao wanasemaje. Huwa sipo quick kum-judge mtu.

Siku za Awali Ben Carson alipoulizwa kama atakuwa tayari kujiunga na serikali ya Trump, alijibu akisema yuko tayari kwa nafasi yoyote ile atakayopewa. El Jefe, najua una miezi miwili tu toka umejiunga jamvini lakini kumbuka hii ni JF na inatunza kumbukumbu.

Ukitaka kujua Ben Carson anajipima juzi alipokuwa kwenye interview kwenye Fox Report Weekend alisema hivi:

“Basically, I’ve said my preference is to be outside and to act as an adviser, but if after going through the process they all conclude it would be much better to have me in the Cabinet, I would have to give that very serious consideration,”

Mi sitaki nim-judge Ben Carson, ila nakuuliza, tutumie hiyo kauli yake ya juzi jumapili au ya siku za awali?

Eti bado anajipima...hivi hawa watu wanaongea na wewe saa ngapi maanake sidhani kama unaweza kuthubutu kutamka vitu kama hivi kutoka kichwani tu.

Sitoi kichwani, hayo ni maneno yao. Wanahojiwa mara kadhaa na wao wanazungumza maoni yao.

Issue hapa ni 'consistency', kama mtu anaweza kuwa na maoni yale yale kila anapohojiwa.

Je umejiuliza kwa nini Trump anawaita in the first place...kwamba hajui uwezo wao? Kwamba anaamka tu na kumwita mtu! Kubali usikubali kuna utata mwingi kwenye transition na sasa inaonekana wapo anaowabembeleza wakubali kuingia kwenye serikali yake.

Unajua ukishaweka hisia zako kwamba kuna tatizo kwenye transition, chochote kikitokea tofauti na ulivyotegemea au mategemeo ya wengi, haraka haraka unaki-link na hizo hisia ulizokwishajenga kwenye mawazo yako na ku-justify hisia zenyewe.

Kwanza ondoa hizo hisia ndipo utakapoweza kuangalia mchakato mzima kwa mawazo huru, huku ukiongozwa na real facts na sio facts za kupikwa.

Rais Obama alivyokuwa akiita watu na kukutana nao kwenye Transition HQ kule Chicago mwaka 2008 hukuwa na tatizo na hilo, Trump akiita watu kukutana nao Trump Tower 2016 unaona kuna tatizo. Hizi ni clear double standards.

Tatizo kubwa humu ni kwamba wengi mmeanza kuchangia huu uchaguzi wa Marekani juzi juzi tu. Mngekuwa mmefuatilia toka hatua za mwanzo za kampeni na ahadi za wagombea hungesema ulilolisema hapo juu. Kwa nini unaleta mawazo yako binafsi badala ya kujikita kwenye facts?

Kuanza kwangu kuchangia huu uzi juzi juzi hakumaanishi moja kwa moja kuwa nimeanza kufuatilia kampeni za US juzi juzi.

Nimefualitia Kampeni za US hata kabla ya primaries za Reps na Dems. Nilivyowasikiliza wote na ahadi zao (Dems na Reps) nikaona atakaeweza kuwafanyia kazi nzuri wamarekani ni Donald John Trump.

Pamoja na kusikiliza ahadi za Trump, ninasikiliza Congressional Reps na Dems wana maoni gani kuhusiana na ahadi hizo maana wao ndio watapitisha mabadiliko ambayo Rais Trump hawezi kufanya kwa kutumia executive orders. Kwa maana hiyo issue ya Reconcilliation Bill sio maoni yangu binafsi.

Nilisema wazi kabisa kwamba Trump hafai kuwa Rais wa Marekani na kwamba Wamarekani ambao nimebahatika kuwafahamu hawawezi kumpigia kura. Msimamo wangu bado ni huo huo...hafai na Wamarekani wengi hawakumpigia kura. Kuhusu kuwa Rais, nakubali Trump ndiye Rais wa 45 wa USA.

Unaanza ku-sound kama watabiri na manabii waliomtabiria Hillary ushindi halafu matokeo yakatoka tofauti.

Wamarekani wengi wamempigia kura Trump kwenye Counties nyingi ukilinganisha na Counties alizoongoza Hillary.

Kwanza, huo ni uongo na ni propaganda ya wakurupukaji kama Rep. Chaffetz, Obama hajatoa amnesty kwa illegal immigrants.

Ni kweli, Rais Obama alitoa amnesty kwa illegal immigrants.

Obama moves to give legal status to 5 million illegal immigrants

Sio sahihi kusingizia watu wengine kuhusika na taarifa zilizotoka kwa Rais Obama mwenyewe.

Ukipenda sera za mgombea A na za mgombea B hujazipenda, automatically unakuwa supporter wa mgombea A hata bila kusema kwa mdomo au kuandika sehemu.

Ukiacha hizo allegations kuhusu wanawake, Megyn alimponda Trump kwenye trade, immigration, security, taxes etc tokea kwenye primaries. Hakuwa against sera za Hillary.

Lakini haijalishi maana currently Megyn ameamua kum-support Trump.

Hannity alishasema yeye sio journalist bali bali ni talk show host, kuna tofauti.

Hannity ni conservative na Fox News ni conservative media kwahiyo chuki zako dhidi ya Fox na Hannity zinaeleweka.

[QUOTE="Mag3, post: 18577712, member: 10873"]Yawezekana Kanye West hakuwa anawakilisha mtu weusi, alikuwa akijiwakilisha yeye na kutafuta namna ya kupata zile bilioni alizokuwa akizihitaji kufanikisha malengo yake na kulipa madeni.[/QUOTE]

Kumbe alikuwa anategemea Trump amlipie madeni yake?. Unaanza kuwa racist.

Sielewi mtu maarufu analipiwaje madeni yake kwa kuonyesha support yake publicly baada ya uchaguzi kwa mgombea aliyeibuka mshindi.

Kanye West hakumpigia kura Hillary. Hilo nalo alilisema baada ya uchaguzi.
 
"El Jefe, post: 18588395, member: 387168"]Bado naamini ni so far so good. Ishu ya Jared Kushner na Christie inaweza kuwa ime-play part kkuondolewa kwa Christie kwenye nafasi Transition.

Lakini pia nilitaja Bridgegate Scandal ya mwaka 2013. Ukiangalia timing utagundua scandal ime-play role kubwa kuliko kutokuelewana na Jared.

Kumbuka mfanyakazi wake mmoja kati ya hao wawili alidai Chris Christie anahusika moja kwa moja na hiyo scandal.

Habari Trump Tower, kwamba Chairman wa Transition ana scandal. Na media kila mda walikuwa wanauliza maswali kuhusiana na Christie kwamba kwanini bado ni Chairman wa transition. Media wakaanza kurusha habari kwamba Trump anaaminije watu walioteuliwa na Christie baada ya hiyo scandal ya bridgegate wakati yeye anaenda DC ku-Drain the Swamp?

Ni siku tano tu zilipita ikaamuliwa ashushwe cheo. Ndio maana media hawajabeba bango kuhusiana na Gov. Christie maana wao ndio waliochochea aondolewe.
Sikiliza, huna info za kutosha, maelezo mengi hayana ukweli.

Bridge gate ilikuwa obvious siku za mwisho na ndiyo maana Christie hakuonekana katika kampeni. Leo ni 2 weeks tangu matokeo na more than 2 weeks tokea kampeni ziishie.

Kilichomuondoa si bridge gate kwasababu alikuwa chair na anaendelea hadi wakati transition team inaundwa ambayo ni less than 10 days

Media hazikuwa concern sana na Christie kwasababu issue ni alijua nini kinaendelea katika scandal wakati akisema hakujua.

Kilichomuondoa chair transition ni Jared Kushner.

Kulikuwa na mtifuano mkubwa sana kiasi cha kutishia vurugu.

Kushner ni kipenzi cha Trump, Christie ni loyal kwa Trump na anawafuasi wengi.

Ikaamuliwa Mike Pence aendelea na nafasi hiyo kwasababu

Akina Newt Gingritch walikuja juu kuhusu Jared kwamba inakuwa family issue.
Hata issue ya Newt na secretary of state Jared ana influence na Newt inaonkena out

Mtifuano ukatoa siri ya Trump kutaka watoto na Jared wapewe security clearance.

Waliofanya hivyo ni wenye uchungu na Christie na wali back stab Trump na Jared

Ugomvi wa transition ni kuhusu Familia ndani ta WH, katika ni Jared Kushner

Usitake kusingizia media wala kuonyesha ulaini wa tatizo
 
"El Jefe, post: 18588395, member: 387168"]
Hata kipindi cha Transition ya Obama mwaka 2008, Obama alimteua Gavana wa New Mexico Bill Richardson kuwa Secretary wa Commerce lakini aliondolewa kwa sababu ilisemekana anahusika na scandal ya ufisadi huko New Mexico na nafasi yake ikachukuliwa na Gary Locke.
Not true, Gavana ali withdraw jina lake mwenyewe.
Trump anategemewa kuteua watu kwenye nafasi 1270 zitakazoidhinishwa na Senate na nafasi 363 ambazo sio za kuidhinishwa na Senate. Unategemea azungumze na watu wachache?
Kumbuka nafasi anazotakiwa kujaza immediate ni Cabinet and key positions. Zingine anajaza kwa vetting itakayofanywa na state organs kwa ushauri na cabinet members

US Rais anapelekewa majina yaliyofanyiwa vetting na anayaangalia kwa vigezo vyake. Hakuna Rais aliyejaza nafasi kwa siku moja,ni process inayoendelea. Please

Teuzi muhimu ni kama zile za Security, Treasury na WH.
Hateui wajumbe wa bodi kama kwetu, hapa unazungumzia United states
Nikipima ukweli kuhusu Bannon ni kwamba naona ni mtu mzalendo na conservative ambaye alikuwa concerned na nchi yake inakoelekea kama ambavyo zaidi ya 60% ya wamarekani hawakuridhika na Obama alikokuwa anawapeleka.
Umeona kilichotokea Washington jana lakini! Pili nilikuuliza approval ya Obama 50% inatoka wapi? Hukujibu
Kwahiyo sio sahihi kutumia brush kubwa kuipaka Braitbart org. kuwa ni alt-right kwa article moja na kuacha kuzungumzia maelfu ya articles ambazo wamezitoa.
Huamini Braitbart ni ya white supremacist
Umesoma na kusikiliza maelezo au unabuni
Lakini pia mtu anaweza akazungumza jambo fulani halafu waandishi wa habari wakachukua sentensi moja tu wakatengeneza headline na a-ignore, pengine kwa sababu headline ikaonekana ni uongo.
Tafadhali hili katika mjadala ni too low.
Kama mtu anachukua sample za articles za Braitbart kwa lengo la kuielewa hiyo org., nadhani ni sahihi zaidi kama sample zenyewe zikiwa balanced na sio biased.
dah!
Kuhusiana na Sen. Sessions sijakataa kwamba hisia za kibaguzi hazipo kabisa. Ila ukweli ni kwamba hisia zenyewe ni insignificant na zilichochewa na/au zinachochewa na makundi fulani.
Alikataliwa kuwa Judge wa federal bado unaamini ni tuhuma insignificant!
January inavyokaribia Sen. Sessions anazidi kupata endorsements nyingi za asasi za kiraia na kiulinzi za US ambazo zina democrats na minorities.
Unajua kuhusu NAACP wanasema nini kuhusiana naye?Tafadhali una adulterate mjadala
Hillary ameongoza kwa African Americans (88% kwa 8%) sikatai ingawa ni kiwango cha chini ukilinganisha na cha Obama 2012 (93%).
Kwahiyo hoja yako ya Trump anaungwa mkono na black wengi inatoka wapi kama unajua ukweli

Tunapokuuliza au kukutaka ufafanue hoja, tunajua kwanini tunafanya hivyo
 
El Jefe said:
Kwahiyo sio sahihi kutumia brush kubwa kuipaka Braitbart org. kuwa ni alt-right kwa article moja na kuacha kuzungumzia maelfu ya articles ambazo wamezitoa.

Tatizo lako El Jefe unaandikia mate na wino upo.
Trump hatainyosha Marekani...ni Marekani itamnyosha.
Marekani na Tanzania ni kama mbingu na ardhi ndugu yangu.​
 
"El Jefe, post: 18588733, member: 387168"]
(i) Trump amejigharamia kampeni zake kwahiyo hana special interests na lobbyists wakumuendesha.
Unajua nini kilichopo katika tax file yake?
Kwanini alikataa kutoa tax return zake?
(ii) Trump amekuwa Rais ambaye hana political experience.
Kwa maana Sanders ambaye ni indpendent katika senate angeamua kugombea kama independent candidate asinge qualify kwasababu ana political experience ambayo si kigezo cha independent candidate! please please!
(iii) Trump yupo against Washington establishment.
Atafanyaje kazi na senate au house? Paul Ryan, Gingrich, Sessions wanatokea wapi?
Issue hapa ni 'consistency', kama mtu anaweza kuwa na maoni yale yale kila anapohojiwa.
Kwahiyo unaaamini Ben Carson kwasababu ya 'consistency'. Well, hakuna mtu aliyekuwa consistent kama Trump na issue ya uzawa wa Obama, hivyo kwako wewe uliamini kwasababu ya 'consistency'
Aisee!
Pamoja na kusikiliza ahadi za Trump, ninasikiliza Congressional Reps na Dems wana maoni gani kuhusiana na ahadi hizo maana wao ndio watapitisha mabadiliko ambayo Rais Trump hawezi kufanya kwa kutumia executive orders.
Siku mbili zilizopita ulituambia Trump atafuta legacy ya Obama kwa exec orders. Tulikuambia si rahisi kiasi hicho, leo unatuambia habari tuliyokueleza siku nyingi. Please
Sielewi mtu maarufu analipiwaje madeni yake kwa kuonyesha support yake publicly baada ya uchaguzi kwa mgombea aliyeibuka mshindi.

Kanye West hakumpigia kura Hillary. Hilo nalo alilisema baada ya uchaguzi.
Kanye West! naye iunamwingiza katika mjadala huu! Yaani Kanye ambaye kila wakati ni tatizo hata kwenye show zake. Hivi unamuona Kanye yupo sawa kweli! Na hili la kumuona Kanye kama mtu muhimu linatueleza mengi kuhusu wewe na si yeye. Please
 
Sikiliza, huna info za kutosha, maelezo mengi hayana ukweli.

Bridge gate ilikuwa obvious siku za mwisho na ndiyo maana Christie hakuonekana katika kampeni. Leo ni 2 weeks tangu matokeo na more than 2 weeks tokea kampeni ziishie.

Kilichomuondoa si bridge gate kwasababu alikuwa chair na anaendelea hadi wakati transition team inaundwa ambayo ni less than 10 days

Media hazikuwa concern sana na Christie kwasababu issue ni alijua nini kinaendelea katika scandal wakati akisema hakujua.

Kilichomuondoa chair transition ni Jared Kushner.

Kulikuwa na mtifuano mkubwa sana kiasi cha kutishia vurugu.

Kushner ni kipenzi cha Trump, Christie ni loyal kwa Trump na anawafuasi wengi.

Ikaamuliwa Mike Pence aendelea na nafasi hiyo kwasababu

Akina Newt Gingritch walikuja juu kuhusu Jared kwamba inakuwa family issue.
Hata issue ya Newt na secretary of state Jared ana influence na Newt inaonkena out

Mtifuano ukatoa siri ya Trump kutaka watoto na Jared wapewe security clearance.

Waliofanya hivyo ni wenye uchungu na Christie na wali back stab Trump na Jared

Ugomvi wa transition ni kuhusu Familia ndani ta WH, katika ni Jared Kushner

Usitake kusingizia media wala kuonyesha ulaini wa tatizo

Twende taratibu,

Unatambua kuwa Jared bado anafanya kazi na Christie kwenye transition? Na kwamba Chris Christie bado ni potential pick kwenye cabinet?

Unadhani Chris Christie anaweza kuchaguliwa kwenye cabinet?
 
Not true, Gavana ali withdraw jina lake mwenyewe.

Kuna kuombwa ku-resign ili usionekane umefukuzwa kazi.

Kumbuka nafasi anazotakiwa kujaza immediate ni Cabinet key positions. Zingine anajaza kwa vetting itakayofanywa na state organs kwa ushauri na cabinet members
US Rais anapelekewa majina yaliyofanyiwa vetting na anayaangalia kwa vigezo vyake. Hakuna Rais aliyejaza nafasi kwa siku moja,ni process inayoendelea. Please

Kuna mtu kasema nafasi zinajazwa kwa siku moja?

Turudi kwenye point yako, unafikiri kwanini Trump anakutana na watu wengi?

Teuzi muhimu ni kama zile za Security, Treasury na WH.
Hateui wajumbe wa bodi kama kwetu, hapa unazungumzia United states

Sir, US ni kawaida, labda niulize, why do you think it is such a big deal to talk about US politics? Again una-assume sijui, too bad.

Ukiassume vitu vingi kuhusu mimi binafsi utajikuta hu-deal na ninachokisema.

Umeona kilichotokea Washington jana lakini! Pili nilikuuliza approval ya Obama 50% inatoka wapi?

Approval rating ya 50% ni ya kushikilia bango kweli?

Hukujibu Huamini Braitbart ni ya white supremacist

Nimejibu

Umesoma na kusikiliza maelezo au unabuni
Nakushauri uwe unaangalia mutliple sources, na sio multiple tu bali multiple in terms ya categories tofauti tofauti.

Tafadhali hili katika mjadala ni too low.
Nani ana-decide kwamba kitu fulani ni too low au too high? Yule ambae hajui kutofautisha Senate na Congress au mwingine?

dah!Alikataliwa kuwa Judge wa federal bado unaamini ni tuhuma insignificant! Unajua kuhusu NAACP wanasema nini kuhusiana naye?Tafadhali una adulterate mjadalaKwahiyo hoja yako ya Trump anaungwa mkono na black wengi inatoka wapi kama unajua ukweli

Umeshikilia kukataliwa kuwa judge kwa Sen. Sessions kiasi kwamba hutaki kusikiliza kitu tofauti.

Unajua kuna Rep. aliyepiga kura ya kumpinga kwenye hiyo 10- 8 decision na amesema anajuta kwa kuwa hakupata maelezo ya kutosha?

Taja asasi 5 zinazompinga Sen. Sessions na mimi nitataja 10 zinazomsupport.

Tunapokuuliza au kukutaka ufafanue hoja, tunajua kwanini tunafanya hivyo
Ninavyoandika hapa ninategemea watu muwe na open mind.
 
Twende taratibu,

Unatambua kuwa Jared bado anafanya kazi na Christie kwenye transition? Na kwamba Chris Christie bado ni potential pick kwenye cabinet?

Unadhani Chris Christie anaweza kuchaguliwa kwenye cabinet?
Sijui unataka kueleza nini hapa ambacho sikielewi pengine

Unakubali kuwa Jared yupo katika transition pamoja na Chris
Unakubali kuwa Chris amekuwa demoted kutoka chair

Jared ni privy wa Trump, Christie ni inner cycle and loyal kwa Trump
Usifikiri ni jambo rahisi kwa Trump kumtupa yeyeote kati ya wawili hao

Kilichotokea ni power struggle and vengeance. Jared anaona ana upper hand katika kumu influence Trump. Chris anamuona Jared ni novice

Kwa mtazamo huo the 'broker' akawa Mike Pence ili kumweka Trump mbali na interest zake kwa wote jambo ambalo lingemkwaza

Yes wanafanya kazi lakini under Pence ili kuondoa nani ni Boss na ku iron out the difference. Christie as loyal member wa Trump lazima atapata post kubwa
Jared as privy and henchman wa Trump ana nafasi no matter what

Haya hayondoi ukweli kuwa tiff miongoni mwao lili derail transition team

What the fuss on this?
 
Hivi kwanini mnapenda ku-assume sana vitu humu?
Siyo ku assume, hiyo ni fact

Na hapa nikupe mfano kidogo tu

Uchaguzi umefanyika , kampeni kali sana zenye kauli nzito

Matokeo yametoka. Hillary ame concede mbele ya dunia
Obama amemwalika Trump kumkabidhi nchi mbele ya dunia

Na wote wanafuata constitution and America's norm and tradition. Period

Utalinganisha na Jecha! please please
 
Unajua nini kilichopo katika tax file yake?
Kwanini alikataa kutoa tax return zake?
Naomba unifahamishe kilichopo katika tax file ya Trump.

Halafu unaniuliza kwanini Trump hakutoa tax return zake? Seriously

Kwanini Hillary hakutoa Scripts za speech zake za Wall Street?

Trump amecomply na FEC. Kama una-insinuate kwamba Trump hajajigharamia kampeni zake, tunaomba ushahidi, please

Maana kila nikiomba evidence hamtoi.

Kwa maana Sanders ambaye ni indpendent katika senate angeamua kugombea kama independent candidate asinge qualify kwasababu ana political experience ambayo si kigezo cha independent candidate! please please!

Kugombea kama independent ni perspective nyingine ya kuwa independent.

Atafanyaje kazi na senate au house? Paul Ryan, Gingrich, Sessions wanatokea wapi?
Kwahiyo mtu akigombea kama independent akaenda akafanya kazi na Senate na House hu-independent wake unaondoka? Jibu umelitaja hapo juu ila hapa ulisahau ku-link tu.

Kwahiyo unaaamini Ben Carson kwasababu ya 'consistency'. Well, hakuna mtu aliyekuwa consistent kama Trump na issue ya uzawa wa Obama, hivyo kwako wewe uliamini kwasababu ya 'consistency'
Sijasema "naamini Ben Carson kwa sababu ya 'consistency' ". Na kuna swali lilifuata pale. Jaribu ku-link lile swali na maelezo ya 'consistency'.

Aisee! Siku mbili zilizopita ulituambia Trump atafuta legacy ya Obama kwa exec orders. Tulikuambia si rahisi kiasi hicho, leo unatuambia habari tuliyokueleza siku nyingi.
Wapi nimesema Trump atafuta legacy ya Obama kwa executive orders?

Please Kanye West! naye iunamwingiza katika mjadala huu! Yaani Kanye ambaye kila wakati ni tatizo hata kwenye show zake. Hivi unamuona Kanye yupo sawa kweli! Na hili la kumuona Kanye kama mtu muhimu linatueleza mengi kuhusu wewe na si yeye. Please
Ukishakuwa African american na ukam-support Trump ujue haupo sawa na una matatizo. Sawa umeeleweka.
 
"El Jefe, post: 18591372, member: 387168"]Kuna kuombwa ku-resign ili usionekane umefukuzwa kazi.
Ok sasa unabadili kauli , awali ulisema alikataliwa. Kumbuka kukataliwa na kuombwa kujitoa ni vitu tofauti
Pamoja na hayo, Richardson alijua hilo na alikataa uteuzi mapema

Ni kama lile la Sen John Edward aliyedhaniwa kuwa VP.
Seneta alikataa mwenyewe kwasababu alijua kashfa ya ufuska inarindima
Kuna mtu kasema nafasi zinajazwa kwa siku moja? Au umeassume tu?
Ndiyo hoja yako kuwa Trump anaita watu wengi ili kujaza nafasi. Ukatoa hadi namba. Tukakueleza si hivyo, kuna nafasi anateua moja kwa moja na nyingine analetewe zikiwa zimefanyiwa vetting.
Approval rating ya 50% ni ya kushikilia bango kweli?
Hiyo approva rate inatolewa na wale wale unaoshikia bango kuwa 60% US haina mwelekeo. Mbona unachagua takwimu na wapi uzitumie?

Kama approval rate ni ndogo, nipe marais 5 na approval rate zao
Umeshikilia kukataliwa kuwa judge kwa Sen. Sessions kiasi kwamba hutaki kusikiliza kitu tofauti.
Bandiko 180 nilikueleza haya

Hillary amehukumiwa kwa makosa yake kama yapo.
Makosa yake hayawezi kufuta makosa ya mtu mwingine.

Jina linalokwenda seneti ni la Sessions

Nimejaribu sana kukueleza lazima uwe na background ya hoja kabla ya kuiweka hapa kwa mtazamo mpana

Historia ya matatizo ya Session
1. Kuna racial remarks unayosema iliyomnyima u judge (confirmed)
2. Kuna tuhuma za kumwita layer mweusi a boy
3. Kuna tuhuma za kuita NAACP un-American

Infact democrat wengi wameonyesha kutaka kufukua mambo hayo kuona kama yana umuhimu kutokana na unyeti wa nafasi anayotarajia kupata

Sen Dianne Feinsten amesema kutakuwa na fair hearing kwa Session wakati wa confirmation akiwa mwenyekiti wa judiciary committee kipindi kijacho.
Hili ni baada ya dep concern ya Democrats

Utetezi
Nilidhani ungetuletea utete kuhusu rekodi ya Sessions na kama kuna elements za kujirudi

Ningalikuwa wewe pengine ningesema haya:
1. Alipiga kura ya kuongeza miaka 30 ya civil rights
2.Aifanya confirmation ya Eric Holder ambaye ni AG wa Obama na mweusi
3. Alipiga kura ya kumpa hadhi mwana mama Rosa Parks katika kupewa medali

Haya ungetueleza kuonyesha anastahili benefit of doubts na si hoja ya 'Clinton alifanya hivyo!

Pamoja na utetezi wa mambo 3 hapo juu, nafasi ya AG inalalamikiwa kuwa ni chanzo cha Injustice katika America.

Ni nafasi nyeti sana ambayo maamuzi yake yanagusa sehemu kubwa ya jamii ya America yenye tension katika mambo ya civil rights

Faida za Sessions
Senate inaweza kumpigia kura 51 bila Democrats na akawa confirmed

Hasara
Atakuwa amekosa bipartisan support na hilo kumfanya aonekane ni AG wa Republican

Political ramifications

Kwavile AG anasimama mambo ya justice , kumuidhinisha kutaangaliwa kwa namna hii;

1. Strong tie na Trump na itaonekana kama yeye ni shoka na Trump ni mpini.
Kumbuka racial remark za Trump zinawiana na Sessions seneta wa kwanza kumuidhinisha Trump

2. Republican watabeba lawama zitakazotokana na Seneti, Trump na Sessions
Hivyo kutakuwa na tatizo la GOP kupata support ya minority kama blacks

3. Kuna political tension kwasababu remark zake na za Trump zina prejudice.

Maamuzi yoyote yawe fair au unfair yatakuwa linked na historia za wawili hao

Ni kwasababu hizo, uteuzi wake una matatizo ya muda mfupi na muda mrefu

At least ungeliangalia jambo hili kwa mtazamo mpana na si 'mbona Clinton alifanya'

Niliwahi kukaribishwa nyumbani kwa rafiki yangu. Ukutani mwa sebule yake kulikuwa na karatasi ilmaneno hayo 'Jesus is a silent listener of all conversations in this house''
Hivi ndivyo suala la Session linaangaliwa, si kirahisi tu 'anaungwa mkono na makundi mengi'
 
Back
Top Bottom