Duru za siasa: Matukio nchini na duniani kwa ujumla

Duru za siasa: Matukio nchini na duniani kwa ujumla

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
Wanajamvi
Huu ni mwendelezo wa uzi wa https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/308989-duru-za-siasa-matukio-20.html
Tutaangalia matukio mbali mbali yanayotokea nchini na dunia kwa nyakati tofauti.
Tutaendelea na nyuzi nyingine mahususi kama zilivyo sasa.

MTAFARUKU WA IRAQ NA SOMO KWA VIONGOZI WA TANZANIA

Sehemu ya I


Katika siku za karibuni kumetokea uasi nchini Iraq unaoelekea kuangusha utawala wa waziri Mkuu Nuur Maliki.
Maliki ni kiongozi anaytokana na sehemu ya tawi la Waislam la Shia. Waasi wa serikali wanatoka katika tawi la sunni

Kwa faida tu ya wasomaji na kwa ufupi wa habari, matawi hayo yana matawi mengine madogo mengi.
Kwa mfano, sunni wana matawi (madehebu) ambao yanatokana na mitazamo na tafsiri kutoka kwa wasomi waliobobea(scholars).

Matawi madogo ndani ya tawi moja hayana tofauti kubwa kimtazamo.
Tofauti kubwa ipo katika matawi makubwa kama Shia, Sunni, Sufi na Ahamdiyya.

Kundi kubwa ni la Sunni likifuatiwa na Shia na mengine yote yakiwa yameenea katika sehemu za dunia, kutokana na kuenea kwake. Mathalan, nchini Saudia, sehemu kubwa ni Sunni tofauti na eneo kama Iran ambako ni Shia Islam.

Kwa nchi kama Iraq, matawi Makuu ya Waislam yamegawanyika kutokana na jiografia ya eneo.
Nchi ya Iraq inapakana na nchi za Iran na Saudia na hivyo kuwa na influenced na waislam wa pande zote.

MAREKANI ILVYOLIKOROGA NA SASA IPO NJIA PANDA

Utawala wa Saadam Hussein ulitumia mkono wa chuma kiutawala.
Kwa upande mmoja ilionekana Sunni walikuwa wanatawala,upande mwingine Saadam aliweza kuyaunganisha makundi hayo katika utaifa mmoja.

Baada ya kuvamia Iraq, Marekani ilifanya kosa moja la kihistoria linaloiandama nchi hiyo hadi tunavyoandika.
Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuungwa mkono na wananchi wa Iraq kwa kutumia siasa na dini.

Marekani ndiyo iliyoanzisha kauli mbinu ya Saadam aliwaonea Shia na kuendelea kujenga hali hiyo vichwani mwa watu.Matokeo yake yalikuwa kuungwa mkono na viongozi kama Murtada el Saada wa kundi la Shia.

Hali hiyo iliigawa nchi kwa Sunni kuhisi kuwa kuondolewa kwa Saadam kulikuwa na siri zaidi ya ile iliyosemwa. Tukaanza kuona makundi ya upinzani wa kidini yakizuka kati ya Sunni na Shia.

Wakati huo huo, Shia walikuwa wanaungwa mkono na Iran ambaye ni hasimu Mkubwa Marekani kwa sasa.
Ghafla tukaona akina Mortada el Sada wakiungwa mkono na Iran na kuleta upinzani kwa Marekani

Kwa uchache, aliyechochea mgawanyiko wa makundi katika nchi ya Iran ni uvamizi wa Marekani kwa kutumia siasa maeneo yenye watu wenye mitazamo tofauti ya kiimani.

Kabla hatujaangali jinsi ugumu ulivyo kwa Marekani nchini Iraq, tuangalie kwa uchache siasa za mashariki ya kati.
Siasa za mashariki ya kati ni za kuchanganya sana(complicated).
Unaweza kutafuta suluhu ya tatizo moja, wakati huo huo ukazua tatizo jingine kubwa zaidi.

Kwa mfano, wakati Hezbollah chini ya Imam Hussein Nasrallah wanapigana na Israel, misaada yao ilitoka Iran kwenye Shia wengi na kuwafikia kupitia baadhi ya sehemu za Syria yenye Sunni.
Wakati huo huo, Hamas hawakuwa katika maelewano na Hezbollah na walipata misaada yao kutoka Saudia na Syria.

Marekani ingependelea kumsaidia Israel, na ili kufanikiwa ni lazima isaidie kundi moja.
Endapo itamsaidia Hezbollah basi ni wazi itaungana na Iran ambaye ni tishio kubwa kwa Israel.
Endapo wataunga Mkono Hamas, watakuwa wanawatosa Waisrael.
Na hayo yakiendelea ni ima Marekani itaudhi Saudia au Israel achilia mbali Iran.

Na ugumu huo upo Syria kwa sasa. Marekani inashindwa kuingilia mzozo huo kwasababu wanaopigana Syria ni Sunni.
Sunni wanafanya takriban asilimia zaidi ya 60 ya watu wa Syria.

Wapinzani wa Al Asaad wanatokana na tawi la Sunni linaloojulikana kama Wahab au Wahabia.
Wahabia ni kundi la harakati (movement) ambalo linatengeneza makundi mengine yenye misimamo mikali zaidi na yanayopigana dhidi ya Marekani.

''Inasemekana'' makundi yote kama Alshabab na Alqaida yanaundwa na watu wenye msimamo au wanaofuata mafunzo ya Wahabia (Shool of thought).

Hivyo Marekani kuunga mkono kwa uwazi ni jambo la hatari kwa kutokujua nini hatima ya makundi hayo yatakapochukua nchi ya Syria.

Wakati huo huo kuna shinikizo la chini kwa chini kutoka Saudia likiitaka Marekani iunge mkono wapinzani.
Tunaona Marekani ikifanya hivyo kwa tahadhari kubwa bila kuingilia mapambano.

Ndivyo siasa za mashariki ya kati zilivyo na utata. Ni ngumu kuwa na balanced equation kutoka na jiografia na historia ya eneo hilo kwa ujumla wake

Inaendelea....
 
Sehemu ya II

MAKUNDI KUTOKA SYRIA YATISHIA AMANI YA IRAQ

Kutokana na mapambano yanayoendelea Syria, na mgawanyiko wa kimakundi (sect) uliopo Iraq, kumetokea uasi unaotishia kuanguka kwa serikali ya Iraq.

Katika kupambana na hali hiyo, kiongozi wa kundi la Shia(Ayatollah) amewaapisha wafuasi wake kuingia vitani ili kukabiliana na upinzani wa kundi la Sunni linalosemwa kuwa ni sehemu ya Wahabia.
Kilichopo Iraq ni kile wanachokisema 'full fledged religion war' katika mfumo wa sects i.e Shia Vs Sunni.

Kwa muda wote Marekani imepata taabu kuingilia kwasababu kuu mbili.
Kwanza, kukwepa kuonekana inapendelea upande mmoja.
Kwa mfano, itakapoamua kuwasaidia Shia na Nuur Al Malik ni wazi itaudhi nchi zenye Sunni na hapa ni Saudia na wengine.

Saudia haipendi kuona Iraq ikitawaliwa na Shia kwa hofu ya kuwakaribisha Iran karibu nao.
Na kwamba, hiyo itaongeza influence ya Shia katika eneo hilo la mashariki ya kati.
Na kufanya hivyo ni kuwa karibu na Iran ambaye ni hasimu wake mkuu.

Kukaa kimya na serikali ya Shia kuanguka ni kuunga mkono makundi hatari ya Sunni kwa mujibu wao.
Kumbuka hawa ndio Wahabia kama inavyosemwa na hilo ni kikwazo kwa Marekani.

Njia Marekani inayotumia kwasasa ni kupata 'assurance' kutoka serikali ya Nuur Malik kuhusu ruhusa ya kushambulia na kwamba serikali yake itawahusisha Wasunni ili kumaliza mzozo unaohusisha makundi ya dini.

Mzozo wa Iraq umetengenezwa na Marekani kwa kuanzisha siasa kwa kutumia dini, kwamba Saadam aliwaone Shia na sasa inakula upande wa pili Marekani akiwa njia panda.

Hofu kubwa ya Marekani ni kuwa kuna masilahi yake katika nchi washirika kama Saudia, na hivyo kuudhi kundi moja au kupendelea kundi jingine ni kuhatarisha masilahi hayo hasa majeshi yake yenye vituo katika nchi husika.
Hilo lnaweza kuwakaribisha mahasimu wa Marekani na kulea ukinzani wa nguvu za kibabe katika mashariki ya kati.

Lakini pia Marekani inaangali mustakabali wa mshirika wake mkuu Israel. Serikali za mashariki ya kati zina maana kubwa kwa usalama wa Israel na Marekani isingependa kuwaweka Waisrael njia panda.

FUNZO KWA TANZANIA

Hali inayoendelea mashariki ya kati kama tulivyoijadili kwa uchache inapaswa kuwa funzo kwa Tanzania.
Siku za karibuni waziri Lukuvi wa serikali ya JK alikwenda kuhubiri siasa akitaka kuungwa mkono na makanisa.

Ni rahisi kutumbukiza mbegu hiyo katika maeneo ya dini, lakini gharama zake ni kubwa sana mbele ya safari.
Hakuna aliyejua(ingawa Marekani ilionywa) nini kitatokea miaka 10 baada ya vita ya Iraq.
Leo Marekani ipo njia panda kuleta pamoja makundi iliyoyatengeneza kwa gharama kubwa za kiuchumi na kiusalama

Ni kwa kuangali hali hiyo, duru za siasa tunasema, waziri Lukuvi alipaswa kuwa amejiuzulu nafasi yake siku nyingi.
Huyu ni mshauri mkuu katika ofisi ya rais anayeshughulikia utawala bora.
Watu wanajiuliza, kuendelea kwake na wadhifa kuna maana gani kwa serikali na Rais Kikwete.

Tulidhani kwamba rais Kikwete alipaswa kuonyesha mfano kwa kumwajibisha kiongozi anayemuwakilisha kwa mambo ya hatari kama hayo.

Bado tunasisitiza kuwa kutomwajibisha kunaleta hisia kuwa kiongozi huyo alitumwa na serikali.
Hata pale waziri mkuu alipokemea, hilo halitoshi.
Kosa la waziri Lukuvi ni kubwa na la hatari sana kwa mustakabali wa taifa.

Endapo kutazauka makundi mengine yenye msimamo tofauti na wa waziri, serikali iliyopo madarakani itawezaje kushughulikia bila kuonekana haitendi haki au uonevu kwa baadhi ya Raia wa nchi moja?

Mbegu anayoipanda Lukuvi inapaswa ivunjwe kabla ya kuchomoza ardhini.
Hakuna mtu mwingine anayeweza kuivunja bali rais Kikwete.

Kimya na huruma za rais kwa kiongozi kama Lukuvi zinapeleka ujumbe mbaya kwa jamii.
Mwisho wa siku Kikwete atabeba lawama iwe leo au miaka 10 ijayo(mungu aepushe).
Historia ndivyo ilivyo, haindikwi inajiandika na Kikwete atajikuta akitajwa na historia kwa njia asiyoweza kujitetea.

Bado kuna nafasi ya kuonyesha kukasirishwa na kitendo cha Waziri Lukuvi, na kitendo anachotakiwa kukifanya ni kumfukuza kazi mara moja umma ukiona kama funzo na kama sehemu ya kuponya kovu hilo.

Tusemezane.
 
Mkuu Nguruvi3, asante kutupa mwanga kwa hili. Mimi nakiri siasa za Masshariki ya Kati ni ngumu!, ila the Master Minder ni US ndie alimtengenreza Osama!, kibao kilipogeuka, Osama akawageuka kwa September 11!. Na katika kumsaka, huko Afghanistan, Wamarekani wamewaua innocent civilians 100 times more than waliouliwa na Osama!. Kwao roho zenye thamani ni roho za Wamerekani tuu!. Ni Marekani ndio waliomtengeneza Saadam enzi za vita ya Iraq na Iran na ujio wa Ayatollah Ruhola Komein, ili Iraq iidhibiti Iran!, kibao kilipogeuka, wakamshukia Saadam kwa kisingizio cha kuzisaka WMD hewa na ulimwengu ikishuhudia!. Wakamyonga Saadam!. Jumla ya Wairaki innocent waliouwawa na Wamarekani ni mara 100 ya Wairaki wote waliouwawa na Saadam!.Libya nako ni hivyo hivyo, ni Wamerakani ndio waliomtengeneza Ghadafi!, alipotaka kuwaunganisha Waafrika tuunde USA yetu, wakamshukia!.To me the real devil ni Americans!.Kwa vile wao ni super power!, hakuna wa kuwaadabisha only "Karma" ya all innocent souls ilizosababisha zikapotea, itawashukia!.Pasco
 
Mkuu Nguruvi3, asante kutupa mwanga kwa hili. Mimi nakiri siasa za Masshariki ya Kati ni ngumu!, ila the Master Minder ni US ndie alimtengenreza Osama!, kibao kilipogeuka, Osama akawageuka kwa September 11!. Na katika kumsaka, huko Afghanistan, Wamarekani wamewaua innocent civilians 100 times more than waliouliwa na Osama!. Kwao roho zenye thamani ni roho za Wamerekani tuu!. Ni Marekani ndio waliomtengeneza Saadam enzi za vita ya Iraq na Iran na ujio wa Ayatollah Ruhola Komein, ili Iraq iidhibiti Iran!, kibao kilipogeuka, wakamshukia Saadam kwa kisingizio cha kuzisaka WMD hewa na ulimwengu ikishuhudia!. Wakamyonga Saadam!. Jumla ya Wairaki innocent waliouwawa na Wamarekani ni mara 100 ya Wairaki wote waliouwawa na Saadam!.Libya nako ni hivyo hivyo, ni Wamerakani ndio waliomtengeneza Ghadafi!, alipotaka kuwaunganisha Waafrika tuunde USA yetu, wakamshukia!.To me the real devil ni Americans!.Kwa vile wao ni super power!, hakuna wa kuwaadabisha only "Karma" ya all innocent souls ilizosababisha zikapotea, itawashukia!.Pasco
Pasco siasa za eneo la mashariki ya kati kwakweli zinachanganya sana. Kuna mambo mengi ya kijiografia, historia na dini yanayoingia kwa pamoja.

Kwa mfano, unaoongelea Palestina lazima uingize Lebanon, Israel na Jordan.
Kuna kitu kinaitwa black september kilichowahusu Wapalestina na wajordan. In fact sehemu kubwa sana ya population ya Jordan ni Wapalestina.

Black September iliwaondoa Wapalestina wengi kutoka Jordan kwenda Lebanon. Kumbuka, Israel iliwaondoa Wapalestina waliokimbiia Jordan na wengine Lebanon. Black September ikaongeza idadi ya Wapalestina waliohamia Lebanon.
Hali hiyo ikabadilisha 'demography' ya Lebanon in favor of Muslims.

Serikali ipo kati ikitawaliwa na Wakristo na kusini ni Waislam wa Shia chini ya Imam Hussein Nasorallah, wakati pwani ni Waislam wa Sunni.

Majadiliano yoyote yanayohusu Palestina na Israel lazima yawashirikishe Jordan.
Ndiyo maana King Hussein wakati huo alikuwa mshiriki wa amani ya mashariki ya kati, sasa King Abdullah anashika kiti cha enzi.

Israel inashikilia milima ya Golan(Golan Height) kwa muda mrefu.
Milima hiyo si kuwa ni chanzo cha huduma kama maji, bali pia ni sehemu muhimu sana kiulinzi ya Israel.
Ugomvi uliopo ndani ya Syria si Arab spring tu, bali wasuni wa madhehebu ya Wahabia wanadhani kuwa Al Asaada amewaachia Israel sehemu yao na wao wangependa kuikomboa.

Hadi hapo unaona kuwa Mmarekani akiwasiaida waasi wa Syria, in future itabdi ahangaike na Milima ya Golan aliyoshikilia swahiba wake Israel.Kusita sita kwa Marekani kupo katika mantiki hiyo ingawa wao wanasema waasi wanaundwa na kundi la Ugaidi. Ukweli ni kuwa hofu ya siku za baadaye kuhusu Israel ndiyo inayotawala ingawa hawasemi.
 
Vip issue ya BokoHaramu
Marekani ndio hasa walioanzisha na kukuza kikundi cha Aqaeda kwa kukipa promotion. Alqaeda ilikuwepo muda mrefu na lengo lake hasa linasukumwa na uvamizi na uonevu dhidi ya Wapalestina. Wanaamini Marekani ndiye anayemtetea Israel ili kuhujumu Palestina.

Baada ya kupata umaarufu, kila kundi linalozuka sasa linahitaji kujiweka karibu au kujinasisibisha na Aqaeda ili kupata attention ya dunia kama si kuogopwa.

Kutokana na hali hiyo kuna kundi linaloitwa Alqaeda islamic in Maghreb(AQIM) kwa maana ya alqaeda ukanda wa magaharibi. Ni kutokana na umaarufu unaokuzwa wa AQIM makundi kama Boko Haram nayo yanazuka na kujinasibisha nayo.

Boko harama haina maana sahihi isiokuwa ni neno la Kihausa likimaanisha kupinga umagharibi ikiwa ni pamoja na elimu ya nchi za magaharibi. Hapo katika sura ya dunia, wao ni local kule Nigeria kasakazini katika majimbo kama Kano, Bauchi n.k. Kano ni moja ya majimbo yanayoongozwa na Sharia.

Boko kwa asili ni wana wa jihadi wanaotaka eneo la kaskazini litawaliwe kwa sharia. Hata hivyo matendo yao yanavuka mipaka kiasi cha makundi mengine kama Alqaeda kujiweka mbali nao. Boko ilianzishwa 2002 na Mohamed Yusufu.
Inasemwa kuwa chanzo cha Boko si suala la imani, bali sababu za ukabila, na za kidini.

Nigeria ina migogoro mikubwa sana ya ukabila. Katika eneo la Boko wapo Wahausa, Wafulani n.k Kulikuwa na hisia za uonevu kutoka kwa viongozi wa dini nyingine na hivyo kuanzisha movement ya kukabliana na uonevu huo.
Boko haikuanza kama ilivyo, ilianza kama movement ya vijana wa madhehebu ya Salafi.
Wakati huo ilijulikana kama Shabaab. Neno hilo lina maana ya vijan, na hivyo kuna ukaribu sana wa Alshabaab ya Somalia na Boko kwa mtazamo na fikra.

Kwa mfano, boko hawkaubaliani na watu kutazama vitu kama mpira, jambo ambalo Alshabaab waliwahi kulitekeleza.
Tunakumbuka Alshabaab waliwahi kugomea mbole na kuzuia watu wasichukue mbolea za nchi za mgaharibi wala misaada.
Hali hiyo ilisababisha njaa sana maeneo ya Somalia vijijini na watu wengi walipoteza maisha.

Kiongozi wake bwana Yusuf aliuawa akiwa chini ya ulinzi wa Polisi jambo lililochochea zaidi ghasia.
Boko si kundi linaloungwa mkono na waislam wengi kutokana na matendo yake hata ndani ya Nigeria.
Wamekwenda mbali na kuvuka misingi ya kile wanachokitetea. Tunaona mauaji, ubakaji n.k. vitu ambavyo ni kinyume na sheria za dini yao na hata kufikia mahali wengi kuliona kundi hilo kama linadhalilisha dini ya Kiislam.

Labda niseme kuwa Boko hawana taathira kubwa katika uso wa dunia. Shughuli zao ni local hasa eneo la kaskazini mwa Nigeria. Uhusiana wake na makundi mengine ni kwa ajili ya umaarufu. Malengo ya kuanzishwa kwake ni pamoja na ukabila 'ethenicity' na dini. Hakuna sababu maalumu zinazoweza kuanishwa kama chanzo chake kwasababu mambo yote yamechanganyika.
 
ENEO LA MASHARIKI YA KATI LIPO KATIKA HALI YA WASI WASI
VITA KUBWA YAWEZA KUTOKEA
MAREKANI IPO NJIA PANDA


Katika mabandiko yaliyotangulia tumeeleza jinsi siasa za mashariki ya kati zilivyo ngumu.
Siasa hizo zinahusisha makabila, dini, madheebu n.k.
Ni siasa ambazo ukipata ufumbuzi wa jambo moja, lingine linazuka

Tumeeleza jinsi Marekani ilivyosita kuwasaidia waasii wa Syria, jinsi inavyosita kumsaidia Waziri mkuu wa Iraq na jinsi inavyosita kujiingiza eneo la mashariki ya kati ingawa tayari ipo.Tulizungumzia mvutano wa Shia na Sunni na makundi yanayowafuata.

Hali imezidi kuwa mbaya na kusukuma hali ya usalama katika ''ukingo wa vita'' kubwa mashariki ya kati.
Kabla hatujaeleza hali ipoje, ni vema tukakurudisha nyuma kidogo ili mwana duru uweze kutufuatilia kwa ukaribu.

Marekani ililazimika kuunga mkono wapinzani wa Syria ingawa haikupendelea.
Hiyo ilifuatia msukumo wa Arab Spring ambayo Marekani imesisitiza ni haki ya watu kuamua hatima ya nchi zao na kwamba, ni muda madikteta kuondoka.

Marekani hakupenda Al Asaad aondoke, ni mazingira yanyowalazimisha.
Al Asaad anaonekana kutokuwa na tatizo kubwa na Israel kama tulivyoeleza kuhusu Golan Heights.

Hofu ya Marekani ni kutojua nani anakuja baada ya Al Asaad.
Marekani ina mafunzo mazuri kama la kuanguka kwa USSR (Urusi ya zamani), Egypt, Libya, Aghanistan n.k.

Kwa mfano, kusambaratika kwa USSR hakukuwa na plan ya nini kitafuata.
Matokeo yake ni wanasayansi wa Kirusi kuhamia katika nchi za Pakistan n.k kufundisha namna ya kutengeneza nyuklia.

Zana hizo zimezusha mashindano ya silaha na India. Kwasasa Marekani inalipa gharama kubwa kuwaweka Pakistan karibu ili silaha hizo zisije angukia katika mikono ya magaidi na extremist. Hii ni sababu kubwa sana kwanini Marekani ipo karibu sana na Pakistan.

Funzo lingine ni lile la Misri, kuondoka kwa Hussein Mubarak kuliacha ombwe la uongozi na kuwaweka Waisrael katika wakati mgumu sana. Hadi sasa hali haijatulia,ukweli ni kuwa kuondolewa Kwa Mohamed Morsi ulikuwa mpango wa Marekani kukabiliana na Muslim Brotherhood. Huyu Rais Sisi ni zao la Marekani kwa ushirikiano wa muda mrefu.

Hali ni kama hiyo kule Libya ambako uwezekano wa kupata waasisi na matawi ya Aqaeda ni mkubwa kuliko eneo lingine.
Kule Afghanistan hali ni mbaya na itachukua miaka mingi kuimarika.
Lakini funzo kubwa ni la Marekani kumfunza Osama ambaye aligeuka kuwa mwiba mkali wenye sumu kwa upande wao.

SYRIA
Syria ni nchi inayoogopwa sana na Israel. Wao wanaJulikana kama Warrior wa vita.
Hata katika uduni wa silaha bado ni wazuri na wapo eneo linalowapa taabu Waisrael.
Utulivu wa Syria ni muhimu kwa eneo zima.

Syria ina sehemu kubwa ya Sunni, na wanaoipinga kwa sasa ni Sunni wa madhehebu ya Wahabia.
Kama tulivyosema nyuma, Wahabia na Sufi muundo wao ni wa movement na huongozwa zaidi na matendo kama yalivyoainishwa.Mara nyingi huingiwa na ukereketwa hata kupita kipimo cha kile wanachokifuata.

WanAompinga Al Saad wengi ni Wahabia ambao makundi mengine ya extremist yanahusiana nao.
Marekani ilisita kuwapa silaha wapinzani wa Al Asaad kwa hofu ya kutokujua hawa wapinzani hasa ni akina nani.
Je, ikiwa ni sehemu ya Alqaeda Maekani itafanya nini?

Ukweli umejitokeza.....
 
Inaendelea...

Jana Syria imeshambulia waasi wanaoishambulia Iraqi wanaojulikana kama ISIS (Islamic state in Iraq and Syria).
ISIS inadai eneo la levant ikimaanisha eastern Mediterranean ambayo Jordan, Israel, Turkey na Egypt zipo.

Ni eneo kubwa linalokwenda hadi jimbo maarufu la Allepo kule Syria ambako ni ngome ya wapinzani wa Al Asaad.
Hii Syria pia inajulikana kama Bilad al Sham. Na hilo neno Sham ndio mwendelezo wa bahari ile ya pembe ya Afrika.

Syria wameshambulia ISIS walioko nchi Iraq kwa sasa wakielekea Baghdad.
Waziri mkuu wa Iraq ni Shia na ruhusu ya kwenda kutetea nchi kwa imani ilitolewa na Ayatollah Sistan wa Iran.
Hii ina maana kuwa Iran wanahusika vema katika vita ya Iraq wakiunga mkono Shia wa Iraq.

Kilichotokea ni kuwa Syria inashambulia ISIS huku Marekani ikipanga kumsaidia Nur Al Maliki kuwapiga ISIS.
Ni kwa mtazamo huo ile hofu ya kuwasaidia Wapinzani wa Syria aliyokuwa nayo Marekani ni kweli.

Leo Alqaeda wa Syria wamekula kiapo cha utiifu kwa Al Baghdad ambaye ni mkubwa wa ISIS.
Marekani ingewapa wapinzani wa Syria silaha ingekuwa imetoa kwa mahasimu wao Alqaeda kiani.

Kwa uapnde mwingine, Iran na Shia walioko nchi zote za Mashariki wanaona Iraq inashambuliwa na Syria na Marekani inawashambulia ISIS. Picha nzima inabadilika na kuwa, ISIS wanaonekana ni Sunni badala ya ISIS.
Hivyo vita ni kati ya Shia na Sunni.

Lakini pia Marekani inajikuta katika wakati mwingine mgumu. Kuwasaidia ISIS ni sawa na kumsaidia Al Asaad aendelee kuua. Marekani imeshawatambua wapinzani wa Al Asaad wa Syria ingawa haijatoa silaha.

Kumsaidia Nur Al Mailki wa Iraq ni kumsaidia Iran kwa namna nyingine. Iran yupo katika vikwazo vya uchumi vya Marekani na hivyo ni kituko kucheza timu moja. Marekani inajikuta ikicheza timu moja na Al Asaad wa Syria na Iran katika kiwanja kimoja.

NJIA ILIYOBAKI KWA MAREKANI

John Kerry secretary of states alikuwa Baghdad kujadiliana uwezekano wa Marekani kupeleka washauri wa kijeshi.
Washauri hao wapatao 60 wameshawasili.
Hata hivyo, kauli ya Kerry ya kumtaka Nur Al Malik aongee na Sunni kupata muafaka leo imepingwa na waziri mkuu huyo.

Hapa pia Marekani ipo njia panda. Nur Almalik alichaguliwa kwa kura na Marekani kupongeza demokrasia iliyomweka madarani.
Leo kumlazimisha aondoke ni kula matapishi yao ya kuhubiri demokrasia.

Kumtaka atafute suluhu na Sunni mezani ni kwenda kinyume na matakwa ya wapiga kura na ni kuchochea uasi maeneo mengine kwa kutegemea matokeo kama hayo.

KITAKACHOTOKEA

Ushiriki wa Marekani unaweza kulitia eneo la mashariki ya kati katika hali ya vita ya dini kati ya makundi makubwa ya Shia na Sunni, huku vikundi vidogo visivyo na udhibiti kama Wahabia,sufi n.k vikijichukulia hatua mikononi.

Tayari mzozo umeshaingia Lebanon ambapo sympathizer wa ISIS wameshambulia eneo la Imam Hussein Nasrallah (Mshia).
Hasira za Nasrallah zinaweza kuishia kwa Israel.

Israel itakapojibu mapigo, katika hali ya vurugu ya sasa, kuna mawili yanyoweza kutokea.
1. Watakaofaidika na vipigo vya Israel watakaa kimya. Nchi kama Syria na Egypt zinaweza kuwaka moto tena
2. Israel inaweza kuwaunganisha Shia na Sunni kwa vile ni adui ya common na wao wanafungwa na Iman.

Mtakumbuka vita ya kwanza ya Ghuba, Saddam alimshambulia Israel, lakini Israel haiukjibu mapigo.
Ule ulikuwa mkakati mzuri kwasababu Israel ingejibu, basi nchi zote za kiarabu zingeungana, na Marekani angeweza kunyimwa military base ya kumshambulia Saddam.

Katika hali kama tuliyoieleza, eneo la mashariki ya kati lipo katika uwezekano mkubwa sana wa kuingia vitani.
Hata hivyo wataalam wa mambo ya kisiasa wanasema, Marekani ina uwezo wa kuzuia tafran yoyote na kwamba ni suala muda tu hali itarejea.

Hadi muda huo suluhu itakapopatikana, vita vya mashariki ya kati vinafika hadi kijijini kwako, uwe mlali, Nakapanya, Naliendele, Machame, Kicheba, Isevya, au Bugalika.
Leo bei ya mafuta imefikia dollar 106 kwa pipa kutoka dollar 91 za mwezi jana. Hiyo ni kwasababu ya vita inayoendelea nchini Iraq.

Tusemezane
 

MATUKIO YA NCHINI TANZANIA
MSIMAMIZI WA SHERIA ANAPOVUNJA SHERIA
ESCROW YAKWEPESHWA KIAINA, LENGO KUFICHA UOVU

Bado tunafuatilia suala la mashariki ya kati kwa ukaribu.
Hadi sasa Marekani imepeleka wanajeshi 800 kwa walichosema ni kulinda ubalozi na interest za Marekani
Kwa sababu hizo, itabidi walinde uwaanja wa ndege, wanadai.

Inachoogopa Marekani ni mashambulizi dhidi ya Sunni, au kuwasaidia Shia.
Pia wanataka kumuondoa Nur Al Malki kwa namna ambayo haitwaudhi Mashia. Tutaendelea kuhabarisha k

Hapa nyumbani kuna tukio lisilo la kawaida katika siasa za nchi. Mwanasheria mkuu alitaka kumpiga mbunge. Mtunza sheria anaposimama mbele ya chombo cha kutunga sheria ili avunje sheria alizopewa azisimamie ni jambo lisilo la kawaida kwani halijatokea tangu tumepata Uhuru.

Mashaka zaidi ni weledi wa Mwanasheria Werema anayeanatoka 'kimtaani' kwa kuudhi na kudhalilisha.
Ni Jaji kwa wadhifa, matarajio ya umma ni uwezo mzuri wa kutambua, kuchambua na kuamua kuliko raia
Inapotokea majibu yake hayalingani na Kiwango, inatia shaka sana.
Hasira zake zilizopelekea ''ngumi mkononi '' zimetokana na suala la kutiwa Mtuhumiwa.

Utuhumiwa unatokana na mazingira tata ya pesa za Escrow ambazo hazina majibu ya kueleweka.
mbunge Kafulila kauliza baada ya kulindana kusiko na sababu. Escrow, ni sehemu ya tatizo la IPTL.

Spika Anne Makinda akazuia kuundwa tume huru ya bunge. Walichokifanya ni suala linapelekwa kwa uchunguzi PCCB, CAG na Polisi.Hivi ni vyombo vya dola haviwajibiki kwa bunge.
Taarifa zake zinapelekwa serikalini ambako kuna watuhumiwa wakubwa.

Mtandao kufisadi kiasi umeenea serikalini kama alivyotajwa katibu mkuu Maswi, bunge kwa Mwanasheria mkuu, BoT n.k. Hao wote wametajwa tu kama tuhuma na duru tunabaki kusema ni tuhuma.

Hii inatoa picha kuwa hakuna PCCB,CAG au Polisi anayeweza kuvuka uzio uliotengenezwa.
Suala la Richmond, PCCB walitetea uhalifu. Leo tunajua uchafu ule na watu waliohusika.

Njia ya kufunika uhalifu huu wa Escrow ni taarifa na uchunguzi unafanywa na serikali inayotuhumiwa.
Ni mazingaombwe yanaendelea, utajulikanamiaka mingi ijayo si leo

Mwanasheria Werema alipoombwa atoe ufafanuzi, alikimbilia hoja ya kumwita mbunge Tumbili.
Hilo tu kwa mtu wa hadhi yake ni dhalili sana. Mzee wa umri hapaswi kuzungumza matusi hata kama ni sehemu ya malezi au utamaduni. Nafasi yake ni ya kimataifa na kitaifa, anapaswa kujua neno la kawaida kwa raia kwakwe ni habari.

Hata alipofanya hivyo Spika alimkingia kifua, dalili kuwa mtandao wa kulindana ni mpana sana.
Spika hawezi kusimamia kanuni, mwanasheria hawezi kusimamia sheria, nchi inajiendea kama boya.

Hoja hapa ni kuwa wakati umefika hatua za makusudi za kurudisha serikali yenye nidhamu na heshima mbele ya umma zichukuliwe.

mawaziri kusotana vidole, wabunge kuchoma madole, waziri naye kusema mbovu kwa waingereza, mwanasheria kutaka nafasi ya tyson na upuuzi mwingine ambao hauhitaji microscope kuubaini.

Matukio ya namna hii yanazidi kuonyesha, udhaifu, ombwe na dhalili ya serikali ya leo.

Tusiposema uchafu huu unaofumbiwa macho na JK utageuka kuwa utamaduni.
Tayari watu kwama katibu mkuu Maswi hawajibu hoja wala kufafanua, ni kuonyesha ubingwa wa kutukana . Rais yupo kimya, why?

Werema na Maswi wanapeleka ujumbe kuna kulindana. Kinyume chake watmishi hawa wa umma wasingekuwa na jeuri ya kuudhalilisha umma.
Unapotukana mbele ya kipaza sauti ukiwa mwanasheria au katibu mkuu unaudhalilisha umma wa Watanzania.

Tusemezane
 
Nguruvi3, wakati mnaendelea na mjadala, naomba nitoe ufafanuzi huu tu kiduchu;

  • Taifa la USA lilizaliwa tarehe July 4, 1776 baada ya kujitangazia uhuru kutoka mikononi mwa Wakoloni wa Kiingereza.
  • Taifa la USA lilitambulika rasmi kama nchi huru tarehe September 3, 1783 miaka minane baada ya kuasi.
  • Taifa la USA linajulikana kama la wahamiaji na ndilo taifa linalowajumuisha watu wengi wenye nasaba tofauti duniani.
Tofauti kati ya nchi zilizojulikana kama Mesopotamia zilikuwepo kabla ya USA na zitaendelea kuwepo hata USA ikisambaratika leo na kupotea katika uso wa dunia...they are more deep-rooted kuliko wengi wetu tunavyodhani. Nawatakieni mjadala mwema.
 
Wana duru
Katika wiki hii tutaangalia mizozo miwili mikubwa inyaotikisa dunia kwa sasa
Ndege iliyotunguliwa
Mzozo wa Palestina.

Ahsanteni
 
KUTUNGULIWA KWA NDEGE YA ABIRIA MH17

Ni tukio lililotisha na kuusikitisha ulimwengu. Ndege ya abiria 298 ilitoka Amsterdam kwenda Malaysia ilitunguliwa na kombora ikiwa katika anga la kimataifa nchini Ukraine.

Ndege hiyo kama zilivyo nyingine ilikuwa katika njia za kimataifa na haikuwa yenyewe. Dakika 25 baada ya kutunguliwa ndege nyingine kama Air India zilizpita eneo hilo ikionyesha njia ilikuwa salama

MH17 ilipita njia ya kaskazini kwavile ile ya kusini ilikuwa na radi na ingekuwa ni hatari kuitumia.
Waasi wa Ukraine wanaoungwa mkono na Russia wakaitungua.

Haieleweki hadi sasa ni wao hasa au ni Warusi, isipokuwa jumuiya ya kimataifa haina shaka kuwa wote wawili walishirikiana.

Eneo la jali linamilikiwa na waasi hao ambao walitamba kuangusha ndege katika mazungumzo yaliyonaswa na kuwekwa hadharani. Ingawa walibadili msimamo, ukweli unabaki kuwa walishatamba kuhusu hilo na ndio waliokuwa na kifaa cha black box.

Shinikizo la kimatifa limefaulu kuishinikiza Urusi kuwashawishi waasi warudishe kifaa hicho ili habari zipatikane kuhusiana na ajali. Hata hivyo kifaa hicho hakiwezi kutoa taarifa zozote za nani amefanya nini isipkuwa tu kueleza hatua za mwisho ndege ilipoanguka.

Utetezi wa waasi ni kuwa teknolojia yao haiwezi kutumia makombora kufika zaidi ya km 13 angani.
Hapo kuna ukweli kwa kuelewa waasi wanatumia makombora ya kawaida na wala si wazoefu.

Hata hivyo teknolojia inaonyesha kuwa ndege inayosafiri kwa mwendo wa KM 500 au zaidi kwa saa ikiwa angani umbali wa km 13 inahitajika teknolojia ya hali ya juu sana kuifikia.

Hapo ndipo Urusi inayowaunga waasi mkono inapoingia. Inasemwa na wataalam kuwa kombora lililotumika linakwenda kwa kasi ya zaidi ya km 1500 kwa saa, likiwa linaongozwa kutoka ardhini.

Utetezi huo unaonekana kuiweka Urusi katika mazingira magumu isiyoweza kuyakana.
Hivyo suala si kuwa ndege imetunguliwa, suala ni nani anahusika kati ya Ukraine, Waasi wanaosaidiwa na Urusi au Warusi. Pamoja na kukana, zipo picha zikionyesha waasi wakiondoa magari yaliyobeba makombora kuelekea Urusi

Jumuiya a kimatifa imewanyoshea kidole Urusi bila kificho, Putin anajitahidi kuosha mikono kutokana na tukio hilo. Wataalam wa mambo ya kisiasa wanasema hiyo inaweza kuwa ajali isiyokusudiwa, kwamba lengo halikuwa kutungua ndege ya abiria bali ndege zinazoelekea Ukraine.

Kwa vyovyote vile ajali hiyo iliyoua Waholanzi 198 na wengine 100 wa mataifa mbali mbali inabaki kuwa mwiba mkali kwa Rais Putin. Nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zimekaza uzi wa vikwazo vilivyoanza siku za nyuma.

Tatizo la vikwazo lipo katika ufungamano wa kiuchumi. Kwa mfano, Marekani inasita sita kuweka vikwazo wazi kutoka na biashara za nchi hizo na washirika wengine. Mgogoro huo unaonekana kuyumbisha masoko ya mitaji duniani.
Katika hali tete ya uchumi unaozinduka kufuatia mdororo, uangalifu unahitajika sana kutoka mataifa ya magharibi.

Hofu mojawapo ni kuwa Urusi ambayo majuzi tu imetoka Brazil katika mkutano wa BRICS inaweza kuleta ushawishi wa kiuchumi utakaoidhuru Marekani kwa kutumia mataifa mengine hasa yanyoinukia kicuhumi.

Mkutano wa BRICS(Brazil,Russia, India, China na South Africa) uliofanyika Brazil, ulikuwa katika muda ambao Breton institution ilianzishwa baada ya vita kuu ya pili kule Washintong Hotel, New Hampshire.

Bretton insitution ndio ilizaa hizi WB na IMF. Hivyo mkutano wa Brics ulionekana kama kutaka kuanzisha chombo kingine kwa nchi zinazoinukia zikilenga nchi masikini.

Kwa upande wa Ulaya, kuna tatizo la vikwazo pia. Uingereza ina matajiri wengi wa Urusi na wengi wakiweka fedha zao katika visiwa vilivyo na uhusiano na nchi hiyo kama ilivyokuwa kwa sakata la 'vijisenti' Tanzania.
Nchi za ulaya zinapata energy zao kama gesi na mafuta kutoka Urusi.

Kwa mfano, kuna uhusiano mkubwa sana wa kiuchumi kati ya Uholanzi na Urusi, Ufaransa na Urusi na mataifa mengine.
Hivyo suala la vikwazo ingawa linaongelewa, bado utekelezaji wake unakuwa na matatizo kwa kila nchi ikiangalia mustakabali wake. Vikwazo vya uchumi vinaweza kubadili hali za maisha za wakazi wengi wa Ulaya kama vitakuwepo.

Suala ni je, nchi hizo ziendelee na vikwazo au zifanye nini kuhusu Urusi na gogoro hili.

Vikwazo vya kiuchumi vimelenga kuongeza shinikizo la ndani ya Urusi kutoka kwa matajiri na wananchi watakaoteseka.
Suala la matumizi ya nguvu halipo. Urusi pamoja na mtatizo makubwa yaliyoikumba bado ni taifa lenye nguvu sana kijeshi. Kuimarika kwa uchumi kwa miaka ya karibu na kuziweka nchi zilizojitenga karibu nao kunaipa nguvu sana.

Lakini pia Urusi inawashirika katika maeneo muhimu ya kijeshi kama Iran na Israel.

Nchi za ulaya zinaitegemea Urusi kwa nishati na hilo si jambo la kuamua usiku mmoja kuanza mapambano.
Linahitaji mbadala ambao si wa siku au miaka michache.

Mgogoro huu utaendelea kwa muda mrefu. Dunia inaiangalia Urusi kama sehemu ya tatizo la Ukraine na amani ya dunia.
Urusi inazingalia nchi za magharibi kama tishio linalotaka kujenga kambi ukumbini mwao.

Tusemezane.
 
MZOZO WA MASHARIKI YA KATI

Wanajamvi, duru inafuatilia kwa ukaribu mzozo unaorindima kati ya Israel na Hamas

Tutaongelea kwa uchache kuhusu Jews, Zionist, Palestina, Israel, Mr Gurion, Henry Durant, Apartheid, Mahatman Gandhi, Africa charter of human right na mambo yanayoambata na mzozo kwa ujumla.

Mzozo huu si wa kuangaliwa kwa jicho moja, ni mpana kuliko unavyooenakana kuanzia karne nyingi.

Vijana wengi wanavutwa na 'emotion' hasa za kidini badala ya kuangalia historia nzima na utamaduni wa eneo lenyewe.
Mfano, ni rahisi kusikia mtu akisema kwanini hatuna ubalozi wa Israel, lakini mtu huyo hawezi kueleza kwanini uliokuwepo ulifungwa.

Sehemu kubwa ya tatizo la vijana wa sasa ni kukosa 'curiosity' na ipo sehemu inayochangiwa na uongozi wetu wa leo.
Tanzania imekuwa nchi ya kujificha nyuma ya taasisi za kikanda badala ya kuongoza kama ilivyokuwa.

Lakini pia teknoloji ina sehemu yake katika hili. Watu wanasoma 'headings' badala ya kuchimba kwa undani.

Wanabeba vichwa vya habari vya TV na magazeti bila chembe ya ufahamu kuwa wanaoandika au kuzunguza ni wanadamu wenye mitazamo yao pia.

Kwa mfano, wengi wanaamini kutekwa kwa vijana wa Israel na kisasi cha kijana wa Kipalestina ndilo chimbuko la mzozo.

Tutaendelea tukiwa tayari.
 
MZOZO WA MASHARIKI YA KATI

ISRAEL YAANZA KUTENGWA NA MATAIFA

HAMASI WASUSIWA NA NCHI ZA KIARABU


Sehemu ya I

Kwa takriban wiki 3 kmekuwa na mapambano kati ya Israel na kundi la Wapalestina la Hamas.
Hamas wanatawala ukanda wa Gaza, na chama cha Fatah katika ukingo wa magharibi.

Mpambano ulianza baada ya vijana 3 wa Kiisrael kutekwa na kuuawa ikihisiwa kuwa Hamas ndoio waliofanya tendo hilo.
Hakuna ushahidi wa aina yoyote kuthibitisha hilo na kwa mara ya kwanza Hamas walikanusha tendo kama hilo.
Kwa kawaida matendo ya namna hiyo Hamas hupenda kuchukua credit.

Watu kutoka Israel nao walimteka mtoto wa kiume wa kipalestina na hatimaye kumuua.
Huo ndio ukawa mwanzo wa kurusha maroketi kuelekea Israel na kujibiwa na makombora ya ndege na vifaru.

Mapambano yamekuwa makali kwa pande zote huku Israel ikilazimika kuita askari wake 16,000 wa akiba, kutumia ndege za drone na zile za kivita kushambulia gaza. Hamas nao wamewaweka Israel roho juu kwa makombora ya mfululizo kuelekea miji ya nchi hiyo.

Idadi ya vifo ni kubwa hasa kwa upande wa Wapalestina ambao sehemu kubwa ya waliopoteza maisha ni raia wa kawaida.
Eneo la Gaza ni dogo sana ukilinganisha na idadi ya wakazi wake. Imeandikwa ni sawa na maili za mraba 156.

Gaza imekuwa chini ya vikwazo vya anga, nchi kavu na majini vilivyowekwa na Israel tangu wachukue madaraka ya bunge la Palestina. Kiwango cha ukosefu wa ajira ni takriban asilimia 90-95 ikimaanisha katika watu 100 ni watu 5 wenye ajira.
Idadi ya wakazi wengi wa Gaza takribani asilimia 56 wana umri wa chini ya miaka 20.

Hali ni tofauti kidogo na ukingo wa magharibi unaongozwa na chama cha Fatah.
Kumekuwa na mgawanyiko mkubwa miongoni mwa Fatah na Hamas.

Kumekuwepo na jitihada za kumaliza mzozo, hata hivyo kila baada ya makubaliano kumekuwa na kukiukwa kwa makubaliano husika. Israel iliingia Gaza kwa sababu ya kumaliza mashambulizi ya makombora ya Katusha.
Ni kwa bahati njema teknolojia ya iron dome imezuia makombora hayo kutua maeneo yenye makazi.

Hata hivyo, kila kombora linaporushwa ving'ora hulia kuashiri watu waingie katika maeneo maalumu ya kujificha.
Hali hiyo nayo imawaweka Waisrael katika wakati mgumu wa kukimbia kila baada ya dakika kadha.

Kwa safari hii makombora yaliweza kufika katika uwanja wa ndege wa Gurion mjini Tel Avivu.
Gurion ni jina la mwisrael maarufu sana katika uanzishwaji wa taifa hilo na jina la uwanja ni kwa heshima yake.
Tutaeleza nani Gurion na nini mchango wake katika Israel kadri tunavyosonga mbele.

Kila kunapotokea makombora ya katusha, Hamas hulaumiwa ima kwa kukiuka mkataba wa makubaliano au kubeba lawama zinazotokana na hilo.

Hamas ni kikundi kimoja tu kati ya makundi mengi yenye harakati kule Gaza. Yapo makundi ya Mujaheedina na mengine yenye itaikadi za kidini. Hivyo Hamas sio kundi linalobeba dhamana yote, vipo vikundi vidogo vidogo ambavyo ushiriki wake ni mkubwa ingawa matokeo yote mabaya au mazuri hutupiwa Hamas.

Katika mzozo huu, Hamas wanaonekana kubaki wenyewe bila kuungwa mkono na nchi za kiarabu.

Hilo halitokei kwa bahati mbaya kuna makusudi kabisa ya kufanya hivyo kutokana na mwenendo na ushawishi wa Hamas katika eneo la mashariki ya kati. Nalo tutalijadili kwa mara ya nyingine huko mbele ya mjadala.

Kwa upande mwingine, Israel inalaaniwa kutumia nguvu kupita kiasi katika kukabiliana na Hamas.
Nchi za Ulaya zinaonekana kukereka na tabia ya Israel hasa ya kukaidi hata sheria za kimataifa achilia mbali maazimio mbali mbali.

Ikumbukwe kuwa Israel ni wahanga wa vita na kubaguliwa sana katika historia yao.
Mauaji ya Holocust ya Hitler ni sehemu ya mauaji mengi yaliyowahi kuwakuta huko siku za nyuma.
Hivyo wengi walitaraji kuona nguvu ya Israel kukabliana na Hamas ikiwa katika wastani.

Zoezi la kukabliana makombora likageuka kuwa la kubomoa mahandaki ya Hamas. Mahandaki hayo yamejengwa kitaalamu na yalikuwa tishio kwa Israel. Pamoja na ukweli huo, bado Israel inaendelea kutengwa na mataifa hasa ya Ulaya kwa namna tofauti.

Kuna pande mbili hapa za kuangalia.
Kwanza Hamas waliosusiwa na wenzao wa Uarabuni na nchi za jirani
Israel wanaosusiwa na mataifa yaliyowaunga sana mkono siku za nyuma.

Swali, kulikoni haya yakatokea?

Tutaendelea kuingia kwa undani kuhusu mzozo huu. Huu ni utangulizi wa kutoa picha ya haraka na sehemu zinazofuata tutaangalia kundi, na kila eneo kwa upana zaidi.

Itaendelea........
 
Mkuu Nguruvi3

Israel imezoea kushutumiwa kuhusiana na mgogoro huu na sidhani kama shutuma za sasa zitaleta utofauti wowote kwao....kwa kifupi ni kwamba hawajali dunia inasema nini juu yao.
Kwa upande wa mataifa makubwa kama Marekani sioni mwenye ubavu wa kuchukua hatua zaidi dhidi ya Israel ukiondoa shutuma zinazotolewa...mfano Marekani hana ubavu wa kuvunja uhusiano na Israel, vivyo hivyo kwa mataifa mengine ya ulaya!

Mgogoro huu unazidi kuwa mgumu sababu ya vikundi kama Hamas ambao moja ya maazimio yao ni kuangamiza taifa la Israel...ambao nao kwa upande mwingine hawako tayari kukaa meza ya mazungumzo na kikundi ambacho wameapa kuwamaliza.

Hamas wanaendesha vita hii kutoka maeneo ya raia huku wakitambua fika kwamba majeshi ya Israel hawatojali hilo na watashambulia popote pale watakapoona ni tishio hata kama raia wasio na hatia watapoteza maisha! Mwisho wa siku Hamas wanatambua kwamba raia wengi wanavyozidi kupoteza maisha pengine itawapatia kuungwa mkono na wapalestina wengi zaidi wenye hasira kutokana na kupigwa na waisrael.
 
Last edited by a moderator:
SAKATA LA ESCROW

Marejeo ya tarehe 2 July.
Mabandiko yanafuata

MATUKIO YA NCHINI TANZANIA
MSIMAMIZI WA SHERIA ANAPOVUNJA SHERIA
ESCROW YAKWEPESHWA KIAINA, LENGO KUFICHA UOVU

Bado tunafuatilia suala la mashariki ya kati kwa ukaribu.
Hadi sasa Marekani imepeleka wanajeshi 800 kwa walichosema ni kulinda ubalozi na interest za Marekani
Kwa sababu hizo, itabidi walinde uwaanja wa ndege, wanadai.

Inachoogopa Marekani ni mashambulizi dhidi ya Sunni, au kuwasaidia Shia.
Pia wanataka kumuondoa Nur Al Malki kwa namna ambayo haitwaudhi Mashia. Tutaendelea kuhabarisha k

Hapa nyumbani kuna tukio lisilo la kawaida katika siasa za nchi. Mwanasheria mkuu alitaka kumpiga mbunge. Mtunza sheria anaposimama mbele ya chombo cha kutunga sheria ili avunje sheria alizopewa azisimamie ni jambo lisilo la kawaida kwani halijatokea tangu tumepata Uhuru.

Mashaka zaidi ni weledi wa Mwanasheria Werema anayeanatoka 'kimtaani' kwa kuudhi na kudhalilisha.
Ni Jaji kwa wadhifa, matarajio ya umma ni uwezo mzuri wa kutambua, kuchambua na kuamua kuliko raia
Inapotokea majibu yake hayalingani na Kiwango, inatia shaka sana.
Hasira zake zilizopelekea ''ngumi mkononi '' zimetokana na suala la kutiwa Mtuhumiwa.

Utuhumiwa unatokana na mazingira tata ya pesa za Escrow ambazo hazina majibu ya kueleweka.
mbunge Kafulila kauliza baada ya kulindana kusiko na sababu. Escrow, ni sehemu ya tatizo la IPTL.

Spika Anne Makinda akazuia kuundwa tume huru ya bunge. Walichokifanya ni suala linapelekwa kwa uchunguzi PCCB, CAG na Polisi.Hivi ni vyombo vya dola haviwajibiki kwa bunge.
Taarifa zake zinapelekwa serikalini ambako kuna watuhumiwa wakubwa.

Mtandao kufisadi kiasi umeenea serikalini kama alivyotajwa katibu mkuu Maswi, bunge kwa Mwanasheria mkuu, BoT n.k. Hao wote wametajwa tu kama tuhuma na duru tunabaki kusema ni tuhuma.

Hii inatoa picha kuwa hakuna PCCB,CAG au Polisi anayeweza kuvuka uzio uliotengenezwa.
Suala la Richmond, PCCB walitetea uhalifu. Leo tunajua uchafu ule na watu waliohusika.

Njia ya kufunika uhalifu huu wa Escrow ni taarifa na uchunguzi unafanywa na serikali inayotuhumiwa.
Ni mazingaombwe yanaendelea, utajulikanamiaka mingi ijayo si leo

Mwanasheria Werema alipoombwa atoe ufafanuzi, alikimbilia hoja ya kumwita mbunge Tumbili.
Hilo tu kwa mtu wa hadhi yake ni dhalili sana. Mzee wa umri hapaswi kuzungumza matusi hata kama ni sehemu ya malezi au utamaduni. Nafasi yake ni ya kimataifa na kitaifa, anapaswa kujua neno la kawaida kwa raia kwakwe ni habari.

Hata alipofanya hivyo Spika alimkingia kifua, dalili kuwa mtandao wa kulindana ni mpana sana.
Spika hawezi kusimamia kanuni, mwanasheria hawezi kusimamia sheria, nchi inajiendea kama boya.

Hoja hapa ni kuwa wakati umefika hatua za makusudi za kurudisha serikali yenye nidhamu na heshima mbele ya umma zichukuliwe.

mawaziri kusotana vidole, wabunge kuchoma madole, waziri naye kusema mbovu kwa waingereza, mwanasheria kutaka nafasi ya tyson na upuuzi mwingine ambao hauhitaji microscope kuubaini.

Matukio ya namna hii yanazidi kuonyesha, udhaifu, ombwe na dhalili ya serikali ya leo.

Tusiposema uchafu huu unaofumbiwa macho na JK utageuka kuwa utamaduni.
Tayari watu kwama katibu mkuu Maswi hawajibu hoja wala kufafanua, ni kuonyesha ubingwa wa kutukana . Rais yupo kimya, why?

Werema na Maswi wanapeleka ujumbe kuna kulindana. Kinyume chake watmishi hawa wa umma wasingekuwa na jeuri ya kuudhalilisha umma.
Unapotukana mbele ya kipaza sauti ukiwa mwanasheria au katibu mkuu unaudhalilisha umma wa Watanzania.

Tusemezane
 
KASHFA YA ESCROW

SERIKALI INATAFUTA MBINU ZA KUFUNIKA UOZO

MBINU ZA SIKU ZA NYUMA, ZIMEKWAMA! ZITATUMIKA

Kwa mara nyingine kashfa ya Escrow inarindima kwa kishindo kama ilivyokuwa ya Richmond. Kuna sababu za kisiasa zinazoplekea msukumo wa kashfa hii.
Katika mazingira ya kawaida, CCM wangefunika kombe, lakini inaonekana hali ngumu

Tutapitia mbinu na sababu za kisiasa zinazoplekea suala hili kuwa na hisia.

Sehemu ya I

Kashfa zilizotangulia
Tunakumbuka kashfa zilizotangulia zilivyozimwa na serikali ,bila majibu hadi leo.
Yote yalifichwa kwa mwamvuli wa bunge lenye CCM wengi.

Mfano, hadi leo hakuna anayejua pesa za rada zilitokaje na akina nani walihusika.
Ndivyo ilivyo kwa EPA na kashfa nyingine. Mara zote uongozi wa bunge umeleta hoja za kubabaisha na mijadala inakufa kifo cha kudumu.

Nini kimebadilika?
Safari hii kashfa imeibuliwa na vyombo vya habari vya nje, na kupelekea wahisani kusitisha misaada. Hilo tu linaweka uwezekano wa kufunika kashfa kuwa mgumu.

Pili, sababu za kisiasa
Mbio za urais zinawaunganisha wapinzania na mahasimu ndani ya CCM dhidi ya mahasimu wenzao.

Mgombea mmoja mtarajiwa aliondolewa kwa kashfa na imebaki doa la kudumu.
Hivyo, wengi wanatakiwa kuwa na madoa ili suala la kashfa lisiwe kigezo tena cha kuwania au kumwengua mtu katika kinyang'anyiro

Miongoni mwa jina yanayotajwa katika kashfa, mengine yanatajwa katika kugombea Urais. Endapo majina hayo yatabainika, hiyo itasaidia kambi ya mtarajiwa anayepigiwa debe kuwa na upinzani hafifu.

Ni kwa mantiki hiyo, wabunge wa CCM wanaosimamia kashfa hii, si kwa masilahi ya taifa, bali ya mgombea wanayempigia debe.

Hicho ndicho kinawaunganisha baadhi ya wabunge wa CCM na upinzani, na kuweka kikwazo katika kuzuia mjadala


Tatu, presha ya wananchi
Kashfa imekuja wakati hali ya maisha ya Watanzania hasa katika sekta ya afya ni mbaya.
Hivyo inatafsiriwa kuwa presha ya wananchi inaunganisha matukio haya mawili
 
Sehemu ya II

MBINU ZILIZOTUMIKA SIKU ZA NYUMA

Mbinu za kuzuia zilizotumika siku za nyuma hazifanyi kazi kwasababu tatu tulizoeleza. Serikali inatafuta namna ya kunusuru mjadala huo unaohusisha viongozi wakubwa serikali ndani ya chama

Mbinu iliyokuwa imepangwa ni kumtumia CAG na PCCB kufikisha taarifa serikalini ili watafutwe watu wa kutolewa kafara. Kwa bahati mbaya, habari zimevuja kuvilazimu vyombo hivyo kufanya kazi angalau kwa weledi wa woga.

PCCB
Mkuu wake anakumbuka alivyotetea kashfa ya Richmond kwa taarifa za kupika. Haijulikani kama alijifunza kutokana na hali hiyo au la.

CAG
Naye ana makando kando, na haionekani kama anaweza kwenda kinyume na kupika habari hii ambayo imeshavuja katika vyombo vya kitaifa na kimataifa kwa uhakika

Kitendo cha mawaziri kujitokeza na kukiri kuchukua mgao kinaeleza jinsi ambavyo ugumu wa kuficha. Katika hali ya kawaida hilo lisingetokea, katika mazingira ya vithibitisho hilo limetokea.

WAZIRI MKUU
Matarajio ya waziri mkuu kupokea taarifa hiyo na kuifanyia namna isifike bunge yanakwama kwa kuzingatia sababu ya pili hapo juu.

Kwamba, presha ndani ya chama chake kutoka kwa wapinzani wanagombea nafasi ya urithi wa kiti cha enzi.Mbinu ya kuficha taarifa imekwama, si suala la wapinzani tu bali sasa lina CCM ndani yake.

MWANSHERIA MKUU
Huyu aliamsha hisia baada ya kutaka kumzaba makonde mbunge Kafulila.
Hilo lilikuwa kiashirio kuna jambo linafichwa. Sambamba na mwanasheria mkuu, katibu mkuu na wazari wa wizara husika nao walionekana kuwa wakali badala ya kujenga hoja.

MAHAKAMA
Tayari suala hili lilishamalizika mahakamani. Ushahidi ni jinsi waziri mkuu alivyoruhusu uchunguzi tena mwanasheria mkuu akiwa amekubali.

Ni jinsi PCCB ilivyoruhusiwa kufanya uchunguzi kwa kujiridhisha hakukuwa na uingiliaji wa shughuli za mahakama



MBINU MPYA
Katibu mkuu kiongozi kasimama kidete kutetea taarifa hiyo ifikishwe bungeni mwishoni mwa kikao cha bunge.

Awali, katibu mkuu kiongozi alihoji uhalali wa suala hilo kuongelewa na bunge.

Hapa alimaanisha ile mbinu ya kutumia CAG na PCCB kupeleka taarifa serikalini ili DPP afanyie kazi ilikuwa muafaka ili kuficha yasiyotakiwa kuonekana

Inaendelea
 
Sehemu ya III

BUNGE KUBADILI RATIBA

Kashfa ilikuwa ijadiliwe mapema, bunge limeweka utaratibu wa kubadili ratiba kulingana na mazingira na mweleko wa kashfa.

Ilipangwa bunge lijadili tarehe 26 ikiwa ni siku mbili kabla ya kikao kuahirishwa.

Taarifa zinaonyesha bunge litajadili kwa siku 1 ambayo ni tarehe 27.
Na pengine kutojadiliwa kutokana na mbinu zinazoendelea kusukwa

UKUBWA WA TAARIFA
Kutokana na ukubwa, unyeti na hisia za wananchi, ni jambo la kushangaza taarifa hiyo inaweza kujadiliwa katika siku moja. Lakini hili limefanyika makusudi.

1.Ili serikali ipate muda wa kuahirisha bunge kwa kisingizio cha kukosa muda. Maana yake jambo hili lijadiliwe kwa siku moja.

2.Serikali kupitia bunge inaanda mbinu za kuwapanga wasemaji watakaohakikisha wanababisha zaidi ya kujadili taarifa.

KITAKACHOFANYIKA
Baada ya mjadala mfupi, itatolewa rai kuwa limeagiza serikali ishughulikie suala hilo na wote waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Hadi hapo mjadala utakuwa unaahirishwa kwasababu

  1. Serikali haina pesa za kikao kingine siku inayofuata
  2. Wazungumzaji wa kupangwa watakuwa wamechukua nafasi ya siku moja.


UKWELI
Itakuwa ni ngumu kujua ukweli wa nani kahusika nani hakuhusika.
Suala litarudi serikali na kubaki kabatini kama ilivyokuwa siku za nyuma.

UGUMU UNAPOTOKEA

Suala hili limegusa viongozi wa mihimili mikuu.

Ni kwa mantiki hiyo. Wapo watumishi waandamizi wa mahakama waliotajwa .
Kurudi suala hili mahakamani hakutatoa matokeo yoyote ya maana kwasababu kulindana itakuwa ndio utaratibu.

Kwa upande mwingine, serikali itakuwa na kazi ya kurudisha imani kwa wafadhili.
Ili kufanikiwa ni lazima ionyeshe wazi kuwa haki imetendeka na waliohusika wamewajika kikazi na kisheria.

Kwa kuzingatia kashfa ina sura ya kimataifa, na imehusisha mataifa mengine hili litaitesa sana serikali ya CCM.

Kukosekana kwa ufadhili kutachagiza hali mbaya katika huduma kwa wananchi.
Lawama zitaiendea CCM hasa tukielekea 2015.

Kashfa inaweza kuwa haina matokeo tofauti katika chaguzi kama zilizotangulia, hata hivyo kadri siku zinavtyosonga mbele wananchi wanabadilika na haijulikana hiyo inaweza kuiathiri CCM kwa namna ipi.
 

Sehemu ya IV

MSUKUMO KUTOKA KWA WANANCHI


Kumekuwepo na hoja za wahusika kujiuzulu nafasi zao.
Huo ni utamaduni unaonekana kukomaa.

Wananchi wengi hawakubaliani na suala la kuiba na kupewa likizo.
Wangependa wahusika wafike mbele ya sheria.

Hata hivyo, ipo hoja kuhusu serikali ya CCM na hasa Rais Kikwete.
Katika kipindi cha miaka takribani 9 serikali yake imekumbwa na kashfa nyingi.

Swali wanalouliza wananchi ni kuwa ilikuwaje serikali yenye vyombo vya dola haikuweza kubaini uhalifu huu ambao hujirudia kila mwaka kwa njia tofauti?

Huu utaratibu wa kujiuzulu unamweka wapi Rais wa nchi.
Haiwezekani kila mara kukawa na uhalifu na serikali kujitoa huku watendaji wake wakiwa ni sehemu muhimu ya kashfa hizo.


SERIKALI INAKWEPA, CCM INA KAZI

Serikali inaweza kukwepa kwa kuzingatia muda uliobaki.
Ingalikuwa sehemu nyingine kama Japan,hata siku moja iliyobaki, serikali ingewajaibika

Msukumo wa suala zima utahamia CCM.
Kwa bahati nzuri sana, wapinzani wa Tanzania si wazuri wa kutumia kashfa kama hizi kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa ushawishi wa kura za wananchi.

Hili litakuwa jambo la muda na kama wanavyosema ni upepeo utapita tu.


WANANCHI NA WABUNGE WAFANYE NINI

Kama kweli wananchi wamedhamiria kashfa hii ifike mwisho basi wanatakiwa watie shinikizo bunge lijadili kwa siku si chini ya tatu.
Hapo ndipo uozo wote na wahusika wote watakapoweza kujulikana.

Tarehe iliyowekwa ni mtego tu, na upo uwezekano likazushwa jambo ili kufifisha mjadala husika.

Hoja kwamba serikali haina pesa haina mashiko.
Haiwezekani siku nzima wabunge wakakaa bila kujadili jambo halafu serikali hiyo hiyo ikasema haina pesa.

Haiwezekani serikali isiyo na pesa itenge kiasi cha bilioni 2 kuhonga waandishi na wasomi kwa kupitisha katiba mpya.

Hapa ndipo wananchi wanapaswa kuhoji, iwapo serikali haina pesa za kujadili suala hili, wapi serikali imepata pesa za kuhonga waaandishi na wasomi?

Na inakuwaje serikali isiwe na pesa za kuweka wabunge siku mbili ili kuweza kurudisha bilioni 320 zilizopotea?

Hata kama wabunge watatumia bilioni 2 kwa siku mbili, kiuchumi ina maana zaidi kwa kuokoa bilioni 320.

Tunarudia tarehe 27 inaweza kutotoa matoke yanayotarajiwa.

Watakaopoteza ni wananchi wanaolipa kodi za umeme za juu kwa ajili ya kundi dogo la watu.Hili si suala la mtu au watu ni suala la wananchi.

Tusemezane
 
Back
Top Bottom