Hizi Mada zimechanganywa au? naona zipo pande mbili katika Duru za siasa - ACT kama mpini wa CCM na hii na Matukio ya dunia. imekuwaje?
Mkuu naomba takwimu za maoni ndani ya CCM maana mnapenda sana kuamini vitu. Ikiwa kweli leo mnaamini chama ni zaidi ya mtu kama Zitto imekuwaje, wanachama wa CCM wamwambie Dr.Slaa ahamie Chadema, chama wanachopingana nacho ili wampe kura zao. Inaingia akiini kweli?
..kilichotokea siyo cha kustaajabisha kama utakuwa umefuatilia historia ya Wambulu tangu enzi za TANU.
..Wambulu wana historia ya kumkataa mgombea wa Tanu Chifu Amri Dodo na badala yake kumchagua independent candidate Herman Elias Sarwatt ktk uchaguzi wa 1960.
..inasemekana Tanu walishaonywa kwamba wasimsimamishe Amri Dodo lakini hawakusikia, hivyo Wambulu wakawapiga chini.
cc
Nguruvi3,
Mchambuzi