Duru za siasa: Matukio nchini na duniani kwa ujumla

Duru za siasa: Matukio nchini na duniani kwa ujumla

KIFO CHA ESCROW KIMEWADIA
WANANCHI WAMEFUNGWA MIDOMO KWA KAMBA ZA MAHAKAMA

CCM IMETEKA HOJA BAADA YA ADHABU YA WANANCHI

http://www.mwananchi.co.tz/habari/K...bani/-/1597296/2589796/-/ysq9pyz/-/index.html

http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=76315

http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=76317

Hii ni sehemuyamabandiko takribani 20 tukieleza kwaundani kuhusu mbinu za serikali za kuficha uozo wa Escrow. Reference ya mada hii ni bandiko 50-54

Tulisema lengo la serikali nikuiteka hoja na kuitumia kwanjia zisizo sahihi
Tulieleza kuwa wapinzani walifanya makosa kushiriki kamati yamaridhiano.

CCM hainahistoriaya maridhiano, lini wanaweza kuja na hoja ya maridhiano ikaaminiwa?
Tulisema Mbowe na Zitto waliuza hoja na
walioshindwa niwananchi.


CCM inatumia vikaovyao inatumia udhaifu wamaridhiano kujijenga baada ya kujeruhiwa uchaguzi serikali mitaa.

Serikali nayo inahakikisha suala la Escrow halisemwi walahalizungumzwi tena.
Leo wamekamatwa watu wawili kwa kutuhuma za kula rushwa ya kupewa mamilioni na Rugemalira.


Huo ni usanii, ukisoma mashtaka yanayowakabili ni pamoja na kuchukua rushwaili kufanikisha suala la IPTL . Inachekesha sana kwasababu sheria za nchi zinakataza kutoaa u kupokea rushwa. Iweje sasa Rugemalira anayejulikana katoa rushwa asifunguliwe mashtaka?

Hili la mahakamani limefanywa makusudi. Tuliwahi kuelezakuwa mbinu itakayotumika kuzima mjadalawa escrow nikukamata watu wawili, ili suala hilo liwe mahakamani na lisiandikwe au kuzungumzwa tena.

Njia ya pili, ni kuwafariji wafadhili , tatizo linashughulikiwa na wapo waliofikishwa mahakamani tayari.

Na tatu, ni kuridishaimanikwawananchi katikamantiki ile ileya kushughulikia tatizo.

Kitendo cha kukubali kulirudisha sualala escrow serikali ilikuwakosa kubwa.
Kitendo
cha kukubali uwepowa kamati yamaridhiano ilikuwa ni kosa kubwa.

Na kitendo chawananchikushangiliakuondolewa kwa Tibaijuka nikosa kwa kuondoa jicho sehemu husika.

Sasa Escrow imezuiliwa kusemwa, ipo mahakamani na kifo chake kimefika rasmi.
Serikali inapumua kama tulivyowahi kuandika huko nyuma.

Wananchi wapigwa changa la macho. Wasubiri khanga na kofia za CCM kwa pesa zao kupitia ufisadi.


Tusemezane
 
MHONGO ANG'OKA

JE, TATIZO LIMEKWISHA? JE, SULUHU IMEPATIKANA?

JK, KAMA SI ''ZA WANANCHI'' HATUA UNAZOCHUKUA NI ZA NINI?

Kwanza,tungeomba wasomaji warejee mabandiko 46-55. Mengine kuhusu Escrow yameelezwa
Tulisema kuirudisha Escrow serikalini ilikuwa ni makosa.

Ni makosa yaliyofanywa na Mbowe na Zitto katika kile wkilichoitwa kamati ya maridhiano ya Bunge. Y
anayotokea ni kutokana na uzembe huo.

Mhongo amejiuzulu kama ilivyo kwa wengine. Kujiuzulu kuna maswali mengi yanayoonyesha kufichwa jambo, au udhaifu wa uongozi

Rais Kikwete alisimama Diamond na kutetea pesa zile hazikuwa za umma na wala hakukuwa na jambo lolote baya

JK akamfukuza Anna Tibaijuka hadharani katika hali inayoonekana sasa hivi kama kumtoa kafara.
Mwanasheria Werema alijiuzulu, ikiwa ni maagizo ya kutakiwa kufanya hivyo.

Mhongo akawekwa kiporo kupisha uchunguzi ukamilike. Na sasa amejiuzulu, bila kujua kama uchunguzi ulimtia matatani au la.

Kwa hali yoyote wananchi wanapaswa kuamini jitihada za kumlinda Mhongo zimeshindikana, na deal nzima ya Escrow ni chafu. Endapo si chafu, kwanini Rais awawajibishe wasadizi wake kwa deal safi?

JK anauambia umma, alichosema Diamond ilikuwa kupitisha upepo wananchi wasahau.Kuna uchafu kuanzia serikali, Mahakamani hadi taasisi za dini bila kusahau Ikulu iliyotajwa mara nyingi tu.

Hatua zinazochukuliwa ni za kuwaridhisha wahisani kwa upande mmoja,kupooza kipigo cha serikali za mitaa kwa upande mwingine.

Hata hivyo, serikali inasahau kuwa suala si kujiuzulu bali waliohusika kufikishwa mbele ya sheria.

Ni kwa mantiki hii, bunge na maazimio yake dhaifu lazima lisimame kutetea hoja ya ''wahalifu'' kuwajibishwambele ya sheria
Hakuna mantiki wananchi kuridhika na hatua za kuwapunzisha watu ili waende kutumia mafao yao kwa starehe.

Utamaduni huu ni dhaifu na hutumiwa na viongozi dhaifu.

Tubadilike na pa kuanzia ni hapa,kuitaka serikali ichukue hatua dhidi ya watuhumiwa. Kazi ya bunge ianze na si kufikia tamati.

CCM INATAFUTA MCHAWI ISIYEMJUA

CCM inatafuta mchawi kwa kudhani Escrow ndiyo chanzo cha kuchukiwa na wananchi

Upo uwezekano Escrow ni sehemu ya sababu na si sababu ya CCM kuchokwa.
Yapo mambo kama katiba na uhuni uliofanyika, na ni bahati mbaya wananchi hawakuwa na uwezo,hilo ndilo liliwakera sana

Ilipokuja escrow ikawa kama chumvi (catalyst) iliyoambatana na uchaguzi

CCM wasidhani hili linaweza kurudisha imani ya wananchi iliyopotea.

Kinachoweza kuwasadia ni kuwasikiliza wananchi wanataka nini.
Mbinu chafu kama za kulazimisha kura ya maoni zitaamsha hisia upya kuelekea 2015.

CCM, MCHAWI WENU MNAYE WENYEWE
Endapo CCM wanadhani escrow ndiye mchawi, hapo watakosea. Mchawi wa CCM ni mwenyekiti wao

Escrow ilipoanza, serikali ilikingia kifua lisizungumzwe bungeni. Hata yalipotolewa majina ya wahusika mwenyekiti alitoka hadharani na kuwatetea, huku akweka wengine viporo.

Leo baada ya CCM kudhurika, mwenyekiti anachukua hatua za kufunika makovu.

Mwenyekiti wa CCM alitakiwa kuwa mstari wa mbele kusafisha chama.

Kwasasa anasafisha kitu gani ikiwa chama kimeshaathirika tayari na uzembe alioufanya?

Udhaifu wa mwenyekiti kuchukua hatua, na ujanja wa kutoa baadhi kafara kama funika kombe, ndio uchawi unaoiponza CCM. Hakuna Mchawi mwingine nje ya CCM.

Tazama, hili la kura ya maoni nalo lipo katika mfano wa escrow.

Mwenyekiti anaelewa kuwa katiba ya Chenge ilianadikwa ili kuhakikisha escrow haijadiliwi.

Ndio maana akina Chenge, Ngeleja, Tibaijuka walikuwa mstari wa mbele kupindisha taratibu, kupiga debe ukiaukwaji wa sheria ili kuhakikisha katiba inachukua nafasi ya mjadala wa escrow.

Kwasasa, tunajua sheria haitoi nafasi hata kura haramu ya maoni kufanyika.

Bado mwenyekiti wa CCM anaendelea na shinikizo licha ya kusaliti makubaliano na wapinzani, kuvurugwa kwa mchakato, na kususiwa kwa katiba pendekezwa.

Itakapofika wakati wa hukumu, CCM watahukumiwa kama CCM na hasa wabunge wao wanaosaliti umma.

Pengine mwenyekiti anajua hana la kupoteza, lakini CCM lazima watambue kuwa kiboko cha wananchi kitawafikia mmoja mmoja pale alipo.

Tutashangaa wakikaa vikao na kutafuta mchawi wakati wanajua mchawi wanaye ndani ya chama chao

Tusemezane
 
Thanks Nguruvi3 kwa uchmbuzi mKini kabisa,
nitakuja baadae tujadili pamoja sual la wapinzani kususia kura ya maoni ya katiba mpya, ambao ni ushauri wako mkuu hapa
 
DURU MATUKIO
Sehemu ya I
GWAJIMA vs PENGO
BVR ZA NIGERIA
Kauli ya kadinali Pengo kuhusu kura ya maoni imeletamtafaruku.

Pengo amepingana na jukwaa la maaskofu linaloundwa na kanisa katoliki,walutheri na Waprotestanti


Kauli ya jukwaa lisema, wakristo wajiandikishe katikadaftari la wapiga kura,waipige kura ya hapana katiba ya Chenge

Sababu walizotoa ni mchakato kutofuatwa, uwepo wa hujuma ndani ya BMLK na kwamba, katiba pendekezwa haina uhalali
Pia walizungumzia mahakamaya
kadhi


Kadinali pengo aliwapinga kwa kusema, jukwaa halina haki yakuamua kwa niaba ya waumini namna ya kupiga kura.

Kauli ya Pengo ina utata kwakuzingati kanisa katoliki lilishiriki katika mkutano wa jukwaa

Haieleweki endapo kauli ya Pengo ni yake binafasi au ni yakanisa

Mchungaji Gwajima ametoa video ikieleza kwa ukali akimtuhumu Pengo kwenda kinyume na kauli za maaskofu wenzake, tena kanisa katoliki likiwa limeshiriki

Gwajima ameitwa Polisi kutoa maelezo

Haieleweki maelezo anyotoa ni kufuatia malalamiko ya kadinali Pengo, au ni serikali inayoona uwepowa tatizo


Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni naye ametoa amri ya Gwajima kufika ofisini kwake kutoa maelezo.

Naye kama Polisi, haielweki amepokea malalamiko ya Pengo au ni mtazamo wake kama mkuu wa Wilaya


UTATA NA USHIRIKI WA SERIKALI


Kauli za Gwajima ilikuwa dhidi ya Kadinali Pengo.

Wote niviongozi wa dini na hivyo wana njia nne za kumaliza tofauti zao

1 Kukaa kimya kati yao kama kukubaliana kutokubaliana

2. Kukaa pamoja meza moja kumaliza tofauti zao

3 Kuwatumia viongozi wenzao wa kiroho kuwapatinisha

4 kwenda katika vyombo ya sheria za nchi, polisi namahakamani


Inaendelea sehemu ya II…..
 
Inaendelea II

UFAFANUZI WA HOJA 1-4 HAPO JUU

Hoja 1-3 zinahitaji maridhiano ya pande husika. Hazina tatizo na zinabaki kwa wahusika
Hoja 4 ina tatizo ambalo kama halitaangaliwa litaweka mtazamo mbaya wa siku za mbeleleni ‘bad precedency'
POLISI NA MKUU WA WILAYA

Hawa huangalia usalama wa raia, mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa kamati ya usalama na ulinzi ya Wilaya na mkoa

Kazi zao zina mapaka. Si kila tukio watatakiwa wawepo hadi washiriki watakapopeleka malalamiko,hoja n.k

Ndio maana hawawezi kwenda kumkamata mtu mtaani kwasababu tu amehitilafiana na swahiba wake, mkewe au wamenyang'anyanyana bia


Katika mazingira yaliyopo, endapo Pengo amekwenda kumshitaki Gwajima Polisi, kazi ya Polisi ni kufanya uchunguzi na kumfikisha mahakamani kama haja itakuwepo

Hadi Polisi watakapoweka wazi chanzo cha malalamiko, sakata linaonekana kushikiwa bango na Polisikwa ushabiki Zaidi ya taratibu na sheria.

Ikiwa hakutakuwepo mlalamikaji, Polisi wakae pembeni.

Kuendelea kushinikiza ni kusimamia haki kwa jicho la kengeza


MKUU WA WILAYA
Kwa upande wa mkuu wa Wilaya ya Kinodoni naye ameita waandishi na kuwaeleza yake.

Akiwa mkuu wa Wilaya suala la Gwajima ni sawa na ugomvi wa watu wawili mtaani, kanisani, msikitini au kwenye Bar. Kazi ya mkuu wa Wilaya ni kusimamia ulinzi na usalama kama mjumbe wa kamati


Si kazi ya mkuu wa Wialaya kuchukua jukumu kuvaa mzozo wa watu wawili.

Pengo na Gwajima ni Watanzania na viongozi wa Kiroho. Alichokisema Gwajima au Pengo havina uhusiano wa aina yoyote wa kuvurugwa Amani au ulinzi na usalama wa Wilaya yake


Makonda kama mkuu wa Wilaya hawezi kusimama kama mwendesha mashtaka kukiwa hakuna mlalamikaji achilia mbali hilo si jukumu lake.

Pengo hajalalamika, iweje Makonda aingilie mzozo huo? Makonda anamwita Gwajima ili iwe nini!


Tunachikiona kwa mkuu wa Wilaya Makonda, ni kile alichosema Rais mstaafu Mkapa.

Majuzi Mkapa amesema, sekta ya utumishi wa umma imevurugwa sana.

Akasema, siku hizi mtu anaweza kuwa yoyote bila kujali historia , uwezo na uzoefu wake kikazi


Mkapa alizungumzia haya ya Makonda. Huyu mkuu wa Wilaya alikuwa mhamasisha wa Chipukizi.

Hajawa na nafasi yoyote katika utumishi wa umma. Tunamjua kwa ‘ushiriki' wake katika kutoa kipigo kwa mzee Warioba, kipigo kilichompa cheo


Inaendelea....
 
Inaendelea III

Matokeo ya kuvurugika kwa utumishi wa umma ni kama haya ya mkuu wa Wilaya kuingilia ugomvi usiomhusu.

Si ajabu ipo siku tutasikia Makonda akigombe Pingu na koplo wa Polisi kwenda kuwafunga mabaa medi wawili wanaogembea buzi


Si ajabu Makonda akaandika barua ya kumtaka mlevi mmoja aliyesahau kitoweo bar aende kutoa maelezo.

Yanawezekana kwasababu haionekani kama anaelewa nafasi yake inamtaka afanye nini


Makonda anamwandikia barua Gwajima na kisha kuongea na vyombo vya habari.

Taratibu za kiofisi hazitaki hilo na huu ni weledi finyu pengine kutokana na uzoefu wa Chipuki.

Makonda anadhani kuongoza watu katikawilaya ni sawa na kuongoza Chipukizi wakijiandaa kwa halaiki uwanja wa taifa


HITIMISHO


Polisi na Makonda kwa pamoja wanaonyesha ushabiki naunafiki.

Haiwezekani wamkemee Gwajima ili hali walikaa kimya wakati waziriLukuvi akihubiri chuki Kanisani kupitia katiba mpya.


Alichokifanya waziri Lukuvi ni jambo la hatari sana kuliko maneno ya Gwajima na Pengo.

Lukuvi alihamasisha mtafarauku wa dini mbili za wakristo na Waislam.

Hatumkusikia mkuu wa Wilaya, mkoa, waziri, waziri mkuu ,mkuu wa Polisi au Rais akimekemea.

Ni kituko ugomvi wa maneno wa Gwajima na Pengo unakuwa tishio la Amani nchini na si tishio halisi la Lukuvi


Tusemezane
 
BVR
Uchaguzi wa Nigeria umemealizika jumapili baada ya kuongezwa siku kutokana na matatizo ya kiufundi ya BVR

Matatizo hayo alikumbana nayo Rais na mgombea bwana J. Goodluck

Mfumo wa bvr haukuweza kutambua alama zake. Huyo ni mkuu wanchi aliyezindua mpango huo na hakuna shaka usahihi na umakini ulikuwepo kwa kiwango cha juu wakati anaandikishwa

Nigeria wanatumia BVR kwa mara ya kwanza. Wameanza uandikishaji kwa muda mrefu.

Hata pale akina Jaji Lubuva walipokwenda kuazimaBVR, Nigeria iliwakatalia kwasababu BVR si chombo cha msimu, ni chombo cha huduma za kila siku


Pamoja na kuwa na BVR kwa muda mrefu, tatizo la uandikishaji na upigaji wa kura limevuruga uchaguzi kwani haukufanyika kama ilivyotarajiwa.

Ikumbukwe, Nigeria wamekuwa na BVR kwa muda mrefu wakitumia kuandikisha wapiga kura


Hakuna shaka, Nigeria walifanyia tathmini na usahihi wa mfumo husika kabla ya kujiridhisha unafaa.
Bado wamepata matatizo


Tunjiuliza, sisi tulipkwenda kuazima BVR kwao tuna hali gani.

Maana muda wa kuandikisha na kufanyia usahihi mfumo husika haupo kwa hesabu zozote za mtu anayetumia fuvu na ubongo wake kikamilifu


Mkoa mmoja tu wa Njombe ndio unasemekana kukamilisha uandikishaji tena bila tathmini.

Tunauliza, muda gani upo kwa mikoa 29 mingine mikubw kama Morogoro, yenye watu wengi kama Mwanza na Kilmanjaro


Hili la Nigeria ni ujumbe kutoka kuzimu kuwa kinachofanywana akina Lubuva ni hatari kubwa kwa taifa.

Kinachofanywa na akina PM ni balaa linalosubiri muda,kinachofanya na Rais ni kuandaa mazingira mazuri kwaajili ya ubovu

Mheshimiwa, kila mara umelalamika kushauriwa vibaya,hatudhani kama tunakushauri vibaya.

Hata kama tunakushauri vibaya si jambo bayakwasababu unashauriwa vibaya kila mara


BVR haiwezekani kwa sasa, hakuna sababu za kuharakisha matatizo.

Zipo sababu za kahirisha matatizo kama si kuyaondoa. Kura ya maoni n itatizo linalosubiri kichochoe


Tusemezane
 
BVR imekuwa haina rekodi nzuri ya performance kwenye nchi nyingi za kiafrika ambapo zimetumika kwenye uchaguzi....
 
Mnajua nyie mna tatizo sana kwa sababu mnaipenda sana Chadema mkashindwa kutazama ukweli. Ebu turudi nyuma kidogo tuachane na chama ila tuzungumze WATU.. Ebu tumchukue Dr.Slaa, huyu mwaka 1995 alijiandikisha kugombea Ubunge Karatu kwa tiketi ya CCM akashindwa na mwenzake ndani ya CCM, akahamia CDM kabla ya uchaguzi na kujiandikisha upya kama mgombea wa CDM jimbo hilo hilo la Karatu.

Mnafikiri CCM walimtazama vipi? kama wewe ungekuwa mpenzi wa CCM na kwa haki mnayoizungumzia hapa unadhani alichokifanya kilikuwa sawa au ni Usaliti? na isitoshe alipokuja CDM akashinda uchaguzi kumshinda ya chaguo la CCM wenyewe dhidi yake. Na ghafla akaruka vyeo hadi kuwa katibu mkuu wa Chama kuwapita kina Zitto alowakuta.

Sasa ikiwa historia imeonyesha kwamba Dr.Slaa alipendwa na wananchi wa Karatu na miscalculation walofanya ni chama CCM na kwa nini isiwe leo ni Chadema au msifikirie yeye Dr. ni Pandikizi? Kwa Zitto kila kitu kimepinduliwa, hakilaumiwi chama, isipokuwa yeye ndio msaliti kwa nyendo zile zile alizofanya Dr.Slaa, Lissu, Lema, Shibuda, Prof. Safari - The list is too long, watu walishindwana ktk vyama vyao wakahamia Chadema na sababu ni kama hizi hizi iweje leo Zitto kutoka Chadema imekuzwa kiasi hiki. Kama hawa wote walikuwa na sababu kama za Zitto huko walikotoka imekuwaje wamepokelewa Chadema?

Je hamuoni kama mna sura mbili hapa mnashindwa kujitazama wenyewe nyuma kama Manyani. Fear is the key na nawahakikishieni kwa hofu alowatia, Chadema itajimaliza yenyewe baada ya kuchonga mpini.

Mkandara,

..naomba nikusahihishe kidogo.

..Dr.Slaa alishinda ktk kura za maoni za CCM huko Karatu.

..sasa CCM wakamfanyia mzengwe kwa kukata jina lake na kumpa ushindi mgombea aliyeshika nafasi ya pili.

..wananchi waliokuwa wakimuunga mkono Dr.Slaa wakamwelekeza achague chama kingine watamuunga mkono. Dr akahamia CDM and the rest is history.

..Dr.Slaa hakupewa nafasi za uongozi haraka kama ulivyoeleza. alikaa bungeni na michango yake mle ndiyo iliyopelekea yeye kupewa nafasi za uongozi CDM.

..pamoja na hayo, huyu mzee wa watu ana uwezo na ni mpambanaji kwelikweli. hakuna shaka kwamba ametoa mchango mkubwa sana ktk kuijenga CDM.[/QUOTE Mkandara ukiangalia profile yake yupo kuanzia
2006.
Hayo uliyosema JokaKuu alipaswa kuyajua kuliko wengi jamvini. Makusudi kabisa anapindisha ukweli
Anapindisha ukweli ili kukidhi haja ya kuonyesha supreme leader hajafanya makosa

Ndio Mkuu JokaKuu ahsante sana kwa ufafanuzi wako.

Tulikaa kimya tukijua ukimuuliza kauli ya Shinyanga/Mwanza kuporwa na K’njaro/Arusha ni shihi?
Jibu lake mbona Mbowe kasema ABCD


Tazama uongo alioueleza hapo juu. Anasema Slaa alipanda ngazi kiajabu ajabu ili kuhalalisha supreme kupewa nafasi haraka haraka.

Katiba ya CDM iliandikwa na akina Kitila na Zitto. Nafasi ya katibu mkuu ilielezwa namna inavyopataikana. Haikuwaihi kuundwa ili kukidhi haja.

Alikuwepo Aman Kaborou na wengine. Nafasi ya supreme imeundwa 24hr ili kukidhi haja ya kumsimika supreme


Kwa mtazamo huo unawezaje kufananisha watu hao wawili na mazingira yao?

Kama livyosema Mchambuzi, lengo ni ku-derail mjadala uondoke kwa wahusika.

Hilo tunalijua. Sababu kubwa ni kushindwa kukabiliana na hoja zinazomkabili supreme na ACT.

Mkandara hawezi kufanisha ‘unyemela’ wa kubadilisha katiba ya CDM na unyemela wa kuweka cheo cha supreme kwa kubadili katiba ndani ya saa 24 just to accommodate individual interest.


Hawezi kukemea kauli ya ACT ya kuwagawa Watanzania kwasababu tu mbona fulani kasema!

Hoja ya ukanda iliyowakimbiza ndio hiyo wanayoihubiri.

Alichokifanya supreme ni kuwaeleza wananchi wa Shinyanga/Mwanza kataeni hao kutoka eneo fulani.

Hoja ya CCM sasa imepata mpiga debe. Ndio maana tunasema huu ni mpini, shoka lenyewe lipo kimya


Sehemu ya I

WANANCHI WAMESHINDWA NA MAFISADI

KAtika sakata la Escrow, wananchi wameshindwa vita dhidi ya ufisadi. Kushindwa kwao kunaelezeka kwa namna tofauti.

  1. Kwamba, hawajaweza kuzuia madhara ya mafisadi kutokana na kujirudia
  2. Mategemeo ya kuwa na suluhu ya kudumu (durable solution) dhidi ya ufisadi yamekwisha
  3. Wameendelea kuamini vyombo vya umma vilivyowajifisha walipo sasa
  4. Wanaendelea kuumia kwa gharama za ufisadi na mafisadi
  5. Wameendelea kudanganywa na wanasiasa wakitumiwa kama ngazi za kufikia malengo ya kisiasa
  6. Hali zao zinazidi kudumaa, huku wakimenyeka kulipa kodi wasizostahili
  7. Wanasalitiliwa na wale waliowaamini kwa mjaina ya viongozi

Kuhsindwa kwa wananchi kunatokana na mambo kadha wa kadha

  1. Wananchi kutojitambua na kutotambua haki zao wakidhani kutendewa ubaya ni haki yao na kutendewa wema ni fadhila.
  2. Woga uliojengwa na wahuni , kwamba, kudai haki zao ni kuvunja amani na utulivu. Kwamba amani na utulivu ni zao la wao kukaa kimya hata wakiumia.
  3. Kuamini serikali licha ya kudanganywa miaka nenda rudi
  4. Kutokuwa na ari ya kuwajibisha waliowaweka madarakani
  5. Kuamini wanasiasa badala ya kuamini hoja za nguvu zao wenyewe

KUTOJITAMBUA
Hili ni tatizo zito sana. Kwa miaka zaidi ya 7 na mingine ya nyuma, wananchi wameshuhudia mafisadi wakipora rasilimali zao huku wakiaminishwa serikali inachukua hatua dhidi ya rushwa na ufisadi.

Hadi leo hakuna jibu la kashfa yoyote kubwa iliyowahi kutokea. Kila wanapouliza, jibu ni serikali kuendelea na uchunguzi.
Haiwezekani serikali yenye vyombo vyote ikashindwa uchunguzi kwa miaka 7.

Haiwezekani wananchi wasijue nani aliingia hazina akachota pesa za rada, pesa zimerudi kwa nani na zinafanya kazi gani.

Muhimu zaidi ni kuwa hata wanapofunguliwa vichwa , bado hawaamini wanachokiona.
Tumeona jinsi pesa zilivyoandaliwa na Ikulu kuhonga wana habari na wasomi ili katiba ambayo basically ni ya wananchi ipite.
Hii ndiyo ofisi inayomiliki vyombo vyote, sasa kama inatoa rushwa, ni lini na kwa vipi inawza kushughulikia rushwa?

AMANI NA UTULIVU
Kauli hiyo uinatumiwa kuwatisha wananchi wasidai haki zao au kuwawajibisha wahusika.
Kwa mfano, mwezi mzima hospitali hazina dawa, watu wanalala sjkafuni mahospitalini wakisubiri hatima za maisha yao.

Wananchi hawajitambui kwa kujiuliza, kama hakuna pesa, zile walizojipangia wabunge na maafisa wa serikali kwenda kutibiwa nje zinatoka wapi?

Wanachoambiwa ni kuwa kuzungumzia haki zao ni kuvunja amani na utulivu.

Labda wajiulize, wakati kuna mtu hawezi kununua dozi ya malaria, inakuwaje kiongozi wa serikali apewe milioni 40 bila sababu?
Ili kuzuia kuhojia, wananchi wanaambiwa kuuliza ni kuvuruga amani na utulivu.
Kwamba, amani ipo wkiteseka kimya, wakidai haki zao ni kuvuruga amani.

KUAMINI SERIKALI NA VYOMBO VYAKE
Wananchi hawajitambui, kwamba haiwezekani wezi wakatumia njia zile zile kila siku kuiba na serikali isiwe na jibu. Hakuna kesi au tatizo lolote ambalo wananchi wanaweza kusimama na kusema serikali imelipatia ufumbuzi.
Lakini, bado wanaamini kuwa ipo siku serikali itakuja na majibu ya jumla ya matatizo yote. Miaka inasonga mbele….

KUAMINI WANASIASA
Hili nalo ni tatizo. Katika sakata la Escrow, wengi tulisema hoja si pesa za umma kurudishwa.
Hoja ni kupata majibu ya kudumu ya kukomesha hali iliyojitokeza.
Escrow si suala la watu wachache, ni tatizo la mfumo mzima.

Wanasisasa hawakueleza wananchi ubovu huo, walitumia hoja dhiafu za uzalendo, upigananaji na kutaja majina ya wapiganaji hata kama ilikuwa wazi hiyo ilikuwa ni kujijenga kisiasa ’’political stunt’

Ndio maana tumeona suala la Escrow likiwa limelenga zaidi watu badala ya mfumo.
Likiongelewa kama hoja za viongozi ABCD badala ya hoja ya wananchi.
Likalenga baadhi ya watu na kuacha sehemu kubwa sana ya tatizo kama tunatakvyoeleza.

Kwasasababu lengo la wanansiasa ni kujenga majina yao, maazimio yaliyofikiwa na bunge hayana msingi wowote wa kumaliza tatizo, wala hayakuleta matarajio yaliyokusudiwa na wananchi.

Wananchi wajiulize, inawewzakanje kukawa na maazimio ya maridhiano katika ya wezi na waliobiwa?
Kitu gani kinaridhiwa? Kwamba kuna majadiliano ya wahalifu na uhalifu.

Baada ya aazimio ya wezi na walioibiwa, wanasiasa sasa wanatoka na kuaminisha umma tatizo limepatiwa jawabu! Wanajifaragua kwa majina yao kutajwa kama vinara na wapiganaji. Kipi walichokipagania hadi wakaja na maridhiano na wezi?

Inaendelea……
Kisha endelea
 
Last edited by a moderator:
TATIZO LA ESROW SI NANI AMEIBA, BALI NINI KIMESABABISHA WIZI

Tunakumbuka tatizo la madni lililoanza kwa hoja zile za Buzwagi.
Mwisho wa siku kamati iliundwa na hadi leo tatizo lipo pale pale huku serikali iliyosema inashughulikia ikiwa imekalia taarifa hizo makabatini. Wanasiasa wakapanda chati, wananchi wakapoteza!

Ndivyo ilivyokuwa kwa EPA, Richmond n.k. Haiwezekani eti wananchi waambiwe pesa zilitoka hazina bilioni 28 na hakuna anayewajibika au aliyebainika kuzitoa.

Hakuna jibu la mfumo uliotumika na udhaifu wa mfumo kudhbiti tatizo hilo.
Wanasiasa walipanda chati kwa kelele, wananchi wakapoteza kwasababu hawana jjibu.

Tatizo la Escrow si tofauti. Wananchi wasichokitambua ni kuwa huu ni wizi unaofanywa na genge la watu wenye elimu, watu wanaoweza kuiba na kusimama mbele kusema hawakuiba bila kuchukuliwa hatua.

MFUMO MZIMA WA WIZI

Ukitazama kwa undani, suala la Escrow si uzembe wa watu wawili. Ni mfumo mzima uliokufa.
Ndizo sababu za taasisi mbali mbali za kijamii, asasa na watu binafasi kuwa sehemu ya uhalifu huo

Tunasema uhalifu kwa uhakika kwasababu bunge limekubali upo uhalaifu ndio maana limeagiza uchunguzi na hatua za kuchukuliwa. Hivyo, si suala la kusema kuna uhalaifu, bali uhalifu upo tena wa kiwango cha juu sana.

Tumeona mzozo mkali kati ya watu watatu au wane, hasa waziri nishati, katibu mkuu nishati, waziri mkuu na waziri mmoja aliyetuhumiwa kwa uoenvu mama Anna Tibaijuka.

Tuna sababu za kusema Tibajuka katuhumiwa bila sababu za msingi.
Na hapa tufafanue kabla hatujaendelea na ubovu wa mfumo mzima.
Ukisoma orodha ya wahusika na taarifa, hakuna mahali jina la Tibaijuka limejitokeza katika Escrow.

Jina lake limetokea katika wale waliofadika na mgao wa pesa hizo ambaozo bunge limeridhia ni haramu kwa kusema Stanbic inatakatisha.

Orodha iliyotolewa ni ya account moja. Hakuna orodha iliyo wazi ya account zingine na hivyo hatujui wangapi wamefadika na mgao Tibaijuka kapokea kama msaada, hata kama alikuwa na dhamana ya kutulia shaka, na kwamba, ni kiongozi alitakiwa kuwa makini, swali ni kuwa viongozi wangapi wamepokea mgao huo na majina yao hayakutajwa tena pengine moja kwa moja kuliko ''msaada''?

Kwanini ionekana mama Anna Tibaijuka peke yake na wala si mlololongo mzima uliochukua pesa hizo haramu?
Nani anajua majina yaliyotajwa yalikuwa na uhusiano na viongozi wengine?

Mfano, lingetajwa jina la kachabuseta kupata milioni 600, je tunatakiwa tukae kimya tu kwasababu mtajwa si waziri?
Vipi kama mtu huyo ametumika kama conduit(njia tu) ya kupatishia pesa za wazee?

Mfano mwingine. Ukisoma orodha ya wafaidika utaona watuhumiwa wakubwa kama waziri na katibu au wale wa ofisi nyingine kama BoT na Ikulu hawapo. Kwanini waziri au katibu mkuu apiganie jambo ambalo mgao wake haupo?

Je, tuamini tu kuwa makosa yao ni kufanikisha dili bila ya malipo ya aina yoyote?
Kama walipata mgao, wapi majina yao yaliyopo?

Kwanini Anna aliyepata aoenkane peke yake?
Huko BRELA na BoT hakuna waliosadia kusukuma cheki za pesa za mbele?

Wameyajwa majaji katika mgao na viwango vyao.
Kwanini hakuna anayeona kama kuna ukiukwaji wa maadili, lakini watu wadhani Tibaijuka ndiye pekee aliyekiuka maadili?

Turudi katika mfumo
Ukitazama ripoti, kila sehemu ya serikali, bunge na mahakama ambayo ni mihimili mikuu ya nchi.

Escrow si suala la kisiasa ni la Kiuchumi. Kuzagaa kwa pesa kunaweza kuwa na athari katika mzunguko wa pesa, na anayepokea athari ni mwananchi anayeishi kwa dola 1 si ‘mwenye nchi aliyepata dola 10,000 au zaidi’’

Katika nchi yetu tuliko la kampuni hewa liliwahi kujitokeza kwa Richmond.
Ubalozi wetu ukatusaidia kubaini kampuni hiyo hewa.
Tulidhani hilo lilitakiwa liwe funzo kwamba balozi zetu zina nafasi katika usalama wa nchi kiulinzi na kicuhumi.

Inashangaza tatizo limejirudia kwa kuwa na kampuni hewa kutoka Malaysia iliyoingia katika Escrow.
Hatukutumia balozi zetu, tumetuma mtu kwenda kuchunguza badala ya vyombo vya kidiplomasia.

Leo tumetengenezewa umeme na kampuni hewa. Tunaambiwa bora umeme umekuwepo.

Tujiulize katika hali hii, hivi si kweli kuwa ipo siku makundi kama Alshababab yanaweza kuja kuwekeza nchi katika sekta nyeti, yakisoma siri za nchi napengine kuleta hujuma kubwa kwa taifa?

Hivi taasisi ya BRELA kazi yake ni kuorodhesha majina ya kampuni au ni zaidi ya hapo.
Kwanini taarifa hakuonyesha ima kuzembea au kuhongwa kwa viongozi wa BRELA? Hili si tatizo la mfumo kweli!

Usalama wa taifa

Huu kazi zake ni zaidi ya kulinda viongozi. Inapotokea tapeli anaweza kuja na kampuni hewa, akawekeza, akavuna pesa tena akinunua viongozi waliokula kiapo cha umma, hapa hakuna hujuma kutoka taasisi hii muhimu katika uchumi na ulinzi wa taifa kweli!
Mbona hatukuona ushiriki au kutoshiriki au jitihada za taasisi hizi katika suala zima.

……..
Inaendelea
 
Shemu ya III

Mfumo

Tunaendeleakuangalia mfumo unaozaa ufisadi. Eneo jingine ni BoT, chombo huru, (Gavana) akiwa mteule wa Rais kama Mwanasheria mkuu,mkuu wa taasisi ya usalama au awaye.

Hoja ya PAC: BoT ilisita kuidhinisha malipo. Utetezi ni hafifu kwasababu PAC inasema, baadaye BoT ikabidi itoe pesa kwa shinikizo la mwanasheria mkuu.

Haiwezekani AG akamshinikiza Gavana wa benki kuu. Ilikuwepo nafasi ya Gavana kuonana na waziri mkuu au mkuu wanchi kueleza wasi wasi kwa kuzingatia kiasi cha pesa na athari zake katika uchumi kwa mzunguko


Inajulikana katibu wa Rais naye alishinikiza. Bado Gavana kama mteule mwingine alikuwa na nafasi ya kuonana na mh Rais kueleza wasi wasi.

Aidha,kulikuwa na nafasi ya kutaarifu vyombo vya usalama.
PAC haukueleza jitihada zaBoT ziliishia wapi. Wanachosema, BoT walijaribu sana kuzuia.
Well, hawakujaribu kwasababu wizi umetendeka on their watch.


Wizara yafedha
Nayo inahusika na mambo ya fedha kwa kuhusiana na benki kuu na mabenki mengine.
Haionekani kama wizara ilikuwa na ushiriki au la, tunachojua PAC haikueleza kwa kina upande huo.
Ni kwanini, linabaki kuwa swali la kujiuliza


TANESCO
Zimekuwepo tuhuma kuwa mwenyekiti wa bodi alikuwa anashirikiana na wafanyabiashara kutengeneza mgao ili kuagiza mafuta. Tuhuma hizi na mikataba ya haraka harak ailipaswa kutiliwa shaka kuanzia mwanzo.
Leo tunafahamu Tanesco imeshiriki vema katika wizi kwa namna nyingi, kuanzi mikataba n.k.


Mwenyekiti au mkurugenzi mtendaji walikuwa na nafasi ya kuonana na uongozi wa nchi ilikueleza wasi wasi kuhusu malipo, au capacity charges zisizolingana na mkataba, kiashirio kizuri sana cha hujuma.

Ofisi yawaziri mkuu
PAC imeelezawaziri mkuu alikuwa na taarifa za kinachoendelea.
PAC haikuenda mbali kutafuta endapo PM alikuwa na mawasiliano na bosi wake ambaye ni Rais.

Hatuelewi kwanini PAC haikuenda mbali Zaidi kutafuta ukweli na kuishia katika hoja yaofisi ya waziri mkuu kushiriki.

Ofisi ya PMhaikutumia vyombo vyake kubaini ukweli. Walichofanya ni kutoa kauli za uongokuhusu pesa.
Ofisi ya PM ilikuwa na kila sababu za kushtuka tukizingatia uzembe wa vyombo vingine tulivyoeleza.

Ukifikiria kuwa katibu wa Rais alishinikiza, inakuwaje ofisi ya waziri mkuu na oifisi ya Rais visiwe na mawasiliano ingawa wantu mmoja mmoja wana mawasiliano? Nini kilitokea hapo haijaelezwa.

Inaendelea...
..........
 
sehemu ya IV

BUNGENI
Ni eneo lilionyesha udhaifu mkubwa wakati wa kujadili suala la Escrow
Bunge lilikuwa tayari kuuza nafasi yake kwa kutumia mhimili wa sheria ili kulinda watuhumiwa.

Watoa hoja walipata nafasi ya kuungwa mkono na wenzao wa UKAWA
Pengine hilo lingeanza mapema , kutokana na migogoro wote wakaunganishwa na Escrow

Wapinzania waliungwa mkono na mkundi ya CCM yenye masilahi tofauti yaliyotaka kuona ‘mahasimu wao’’ wakianguka tukielewa safari ya kuelekea 2015 inachezwa rafu.

Hata wale CCM waaminifu, ilikuwa ni dhahiri hawakutaka kuhusishwa na sakata hilo.
Ndio maana CCM ikawatuma watu vituko kwenda kutetea serikali.

Ule utamaduni wa CCM kuwafunga midomo wabunge wako nao ulitumika.
Ndio hasa msingi wa manung’uniko ya chini kwa chini.

Wabunge wa CCM walikuwa na hofu iliyosababishwa na

  1. Ugomvi unaoweza kukigawa chama, hata katika masuala yanayohitaji umoja wao kama yale ya katiba ya CCM wanaotaka kusikumiza kwa wananchi
  2. Chuki kuendelea na kudhoofisha nafasi za watarajiwa, kukiweka chama katika wakati mgumu
  3. CCM kuchafuka na huenda ikawa ndio mwanzo wa anguko kwa hasira za wananchi

Ni kwa mtazamo huo, upinzani ulikuwa na nguvu kubwa kuliko ilivyowahi kutokea huko nyuma.

Ni kwa bahati mbaya, wapinzani si watu wa kusoma kutokana na makosa ya nyuma.

UDHAIFU WA WAPINZANI
Hakukuwa na shaka kuwa CCM ilitambua uwepo wa hujuma.
Kutokana na watu mbali mbali kukingia kifua Escrow isijadiliwe bungeni, wapinzani walitakiwa kuelewa na tuliwahi kuwaambia wasiruhusu jambo hilo likarudi serikali.

Nia ya serikali ni kuficha escrow na kutumia mjadiliano ya bunge kama muafaka kabla ya kwenda kwa wafadhili.

Inajulina PCCB, DPP, Police na sasa mahakama ni vyombo vya serikali.
Haiwezekani serikali ikatumia vyombo hivyo kujikaanga.

Wapinzania walitakiwa kuelewa taarifa ya CAG na PCCB ilikuwa ni mwanzo mzuri wa uchunguzi na mashtaka kwa wahusika bila kuanza mlolongo wa urasimu utakaohusisha serikali.

Hadi leo hakuna kashfa hata moja iliyotanzuliwa.
Kila mara serikali inasema uchunguzi unaendelea, wapinzani wanaamini ni muafaka kurudi serikalini.

NJIA ZILIZOTUMIWA
Kwamba, waliotuhumiwa ni wateule na hivyo bunge halina njia ya kuwawajibisha isipokuwa kumshauri rais atengeue uteuzi wao. Ukisangalia majadiliano, hilo ndilo lililokuwa kubwa sana kwa CCM na serikali

Wapinzani wamesahau huko nyuma waliwahi kutoa mapenedekezo kama hayo na hayakufanyiwa kazi. Watuhumiwa wa rushwa kama katibu mkuu Jairo wakapewa nafasi ya kustaafu.
Bunge likapoteza, wananchi wakapoteza.

MBOWE
Wapinzani walipotaka kuondoka bungeni, kiongozi wa upinzania aliwazuia.
Hili lilikuwa kosa kubwa. Lini CCM imekubali majadiliano na wapinzani?

Mbowe amesahau miswada imepitishwa kwa nguvu huko nyuma tena kukiwa na wabunge 100 wa CCM.

Mbowe amaesaahu Bunge la katiba CCM haikutaka kujadiliana kama alivyosema Makinda
Mbowe alipaswa kuwaacha wapinzani watoke, ili CCM wabaki wenyewe.

Kitendo cha CCM kumuomba Mbowe wabaki ilikuwa ni dalili ya kutafuta mahala pa kutokea.
Kwamba mazimio ni ya bunge na wala si ya CCM.


Inaendelea …..
..................
 
Endelea kuanzia bandiko 47 hadi hili hapo juu
[QUOTE=Nguruvi3;11588696]RAIS ALIPOWANG'ONGA WABUNGE

KABADILIMSIMAMO WA SERIKALI YAKE KUIPINGA ESCROW

WABUNGE WALIOTETEA SERIKALI WANAONEKANA HAYAWANI NA MAZUZU, RAIS WALIYEMTETEA ANAWASHNGAA

Tunasema anawang'onga wabunge kwasababu Rais anawashangaa wabunge wanaopinga escrokujadiliwa.
Hapa kunasura mbili.

Kwanza, Rais aliagiza serikali yake izuie suala la escrow lisiendebungeni hata kufikia mahali pa kuishinikiza mahakama iandike barua juu yazuio


Je, kunaudhati wa Rais kusema amefurahia suala hilo kujadiliwa?Anafurahi vipi ikiwa hakutaka lijadiliwe bungeni?

Kama Rais alitaka suala hilo lijadiliwe na aliridhika lijadiliwe, ilikuwaje Job Ndugaialiyekuwa anakaimu kiti cha spika apelekwe nje ya nchi naserikali ile ile inayosema imefurahishwa na suala escrow bungeni?

Pili, Raisanasema anashangaa wabunge wa CCM waliopinga suala la escrow lisijadiliwe.
Hawani mawaziri kama Lukuvi na wasira, wabunge akina AsumtaMshama, Luisnde na wengine.



Maana yakauli ya Rais ni kuwafanya waliotetea serikali waonekane mazuzu namazumbuku, na ndivyo
Tatu, Raisanapohoji umakini wa wabunge kuhusu azimio lao ka kutaifisha mitambo ya IPTL,hilo ni tusi.

Bunge lina wasomi walioangalia athari za kufanya hivyo.
Lakinipia, kuwafukuza wahuni ni jambo linalolalamikiwa na wafadhili wa serikali yake.


Hili lilikuwa ni tusi kwa wabunge na bunge kwa ujumla.
Somo kubwawanalopaswa kulipata wabunge na viongozi wengine ni kuwa kauli za Rais huwazina ncha mbili na wala haijulikani ni lini atachukua upande wancha

Wapinzaniwameonja joto la jiwe mara nyingi. Kundi lisiloona ni la wana CCM ambao hatawanapodhalilishwa bado wanabaki kuwa waadilifu. Ni wakati wabunge wajiulize, hivi watatumika kama karatasi za maliwato hadi lini?

Je, wabungehawaoni jinsi wanavyodhalilishwa?

Tusemezane[/QUOTE].........................
King Suleiman Adharusi Alinda Mchambuzi JokaKuu Zitto Bongolander Jasusi Mzee Mwanakijiji Mkandara Ngongo Katavi gfsonwin Pasco
 
Last edited by a moderator:
Kwa mujibu wa mgazeti mh Nchimbi, Mng'ong'o na Maswi wamesafishwa kutokana na tuhuma zinazowakabili

Je, wale waliobaki na ‘uchafu' wamechukuliwa hatua gani na serikali?

Je, mama Tibaijuka hakupaswa kupewa benefit of doubt kama hao wengine?

Je, bunge limetimiza wajibu wake wa kuisimamia serikali ?

Je, kulikuwa na sababu zozote za kuwa na kamati ya bunge kuchunguza tuhuma?

Je, wale waliosimama katika hoja hizo, serikali inawaambia nini? Ni waongo au wazushi?

Je,kuna sababu za bunge kujadili tena tuhuma kama mhimili wa utawala ni mkubwa kimadaraka kuliko ule wa bunge?

Je, akina Mbowe na Zitto waliounda kamati ya majadiliano,hiki ndicho tulitegemea ?


Kwanini wananchi tusiamini bunge letu limejaa waongo, wazushi, wenye wivu kwa vile serikali imeona madai ya bunge hayakuwa na msingi wowote dhidi ya watuhumiwa?

 
Endelea kuanzia bandiko 47 hadi hili hapo juu
[QUOTE=Nguruvi3;11588696]

RAIS ALIPOWANG'ONGA WABUNGE

KABADILIMSIMAMO WA SERIKALI YAKE KUIPINGA ESCROW

WABUNGE WALIOTETEA SERIKALI WANAONEKANA HAYAWANI NA MAZUZU, RAIS WALIYEMTETEA ANAWASHNGAA

Tunasema anawang'onga wabunge kwasababu Rais anawashangaa wabunge wanaopinga escrokujadiliwa.
Hapa kunasura mbili.

Kwanza, Rais aliagiza serikali yake izuie suala la escrow lisiendebungeni hata kufikia mahali pa kuishinikiza mahakama iandike barua juu yazuio


Je, kunaudhati wa Rais kusema amefurahia suala hilo kujadiliwa?Anafurahi vipi ikiwa hakutaka lijadiliwe bungeni?

Kama Rais alitaka suala hilo lijadiliwe na aliridhika lijadiliwe, ilikuwaje Job Ndugaialiyekuwa anakaimu kiti cha spika apelekwe nje ya nchi naserikali ile ile inayosema imefurahishwa na suala escrow bungeni?

Pili, Raisanasema anashangaa wabunge wa CCM waliopinga suala la escrow lisijadiliwe.
Hawani mawaziri kama Lukuvi na wasira, wabunge akina AsumtaMshama, Luisnde na wengine.



Maana yakauli ya Rais ni kuwafanya waliotetea serikali waonekane mazuzu namazumbuku, na ndivyo
Tatu, Raisanapohoji umakini wa wabunge kuhusu azimio lao ka kutaifisha mitambo ya IPTL,hilo ni tusi.

Bunge lina wasomi walioangalia athari za kufanya hivyo.
Lakinipia, kuwafukuza wahuni ni jambo linalolalamikiwa na wafadhili wa serikali yake.


Hili lilikuwa ni tusi kwa wabunge na bunge kwa ujumla.
Somo kubwawanalopaswa kulipata wabunge na viongozi wengine ni kuwa kauli za Rais huwazina ncha mbili na wala haijulikani ni lini atachukua upande wancha

Wapinzaniwameonja joto la jiwe mara nyingi. Kundi lisiloona ni la wana CCM ambao hatawanapodhalilishwa bado wanabaki kuwa waadilifu. Ni wakati wabunge wajiulize, hivi watatumika kama karatasi za maliwato hadi lini?

Je, wabungehawaoni jinsi wanavyodhalilishwa?

Tusemezane
.........................
King Suleiman Adharusi Alinda Mchambuzi JokaKuu Zitto Bongolander Jasusi Mzee Mwanakijiji Mkandara Ngongo Katavi gfsonwin Pasco[/QUOTE]

Kuna siku niliwahi kusema kuna baadhi ya wabunge huwa wanadhani Rais wetu mjinga. Naunga mkono maoni ya JK, wabunge wengine kweli maamuzi na busara zao vinatia shaka.

Mkuu nguruvi mchafu ni mchafu tu, hata gazeti likijaribu kumsafisha haliwezi kuondoa uchafu.
 
Something 'might be' unclear on the type of connection forming the chain of Maswi+Mhongo+Mrisho
 
Bongolander;12684911]

Kuna siku niliwahi kusema kuna baadhi ya wabunge huwa wanadhani Rais wetu mjinga. Naunga mkono maoni ya JK, wabunge wengine kweli maamuzi na busara zao vinatia shaka.

Mkuu nguruvi mchafu ni mchafu tu, hata gazeti likijaribu kumsafisha haliwezi kuondoa uchafu.
Mkuu Jitegemee , hapa kuna hoja zinachanganya sana

Kwanza, suala la escro liliungwa mkono na wabunge wote wakiwemo CCM.

Maazimio yalikuwa ‘yapo matatizo'yaliyototokana na viongozi husika.


Pili, suala la kampeni ya wanyamapori, mawaziri walijiuzulu na wengine kuondolewa nafasi zao.

Kilichotokea bungeni kwa mujibu wa hansard ni kuwa viongozi waliohusika na waliotajwa na kamati ya bunge hawawezi kushgulikiwa na mhimili huo bali mamlaka zilizo wateua.

Hadi hapo tunajua lilikuwepo tatizo. Na ikumbukwe, TAKUKURU walihusika na vyombo vingine vya umma katika uchunguzi


Leo tunaambiwa tume ya maadili imeona hawana hatia. Wote, wale wa wanyama pori na wa escrow

Katika hali ya kushangaza, yupo waziri aliumbuliwa hadharani.

Jina lake halikupelekwa katika tume ya maadili ya viongozi.


Sasa kama tume ya maadili imeona hawana tatizo, ni tatizo gani ambalo bunge ililiona dhidi ya watuhumiwa?

Na bunge lilikosa uchunguzi upi kiasi cha tume kuja na uchunguzi mkubwa kuliko wakamati ya PAC na bunge kwa ujumla?

Lakini pia tunajiuliza, hivi mhimili upi ni mkubwa kati ya mihimili mitatu ya nchi?

Inawezakanaje bunge liwena hadhi ya kuisimamia serikali, na serikali iwe na hadhi ya kukataa maamuzi yabunge?


Wengine tulishasema katika mabandiko kuanzia 40+ hadi 60 kuwa ilikuwa ni makosa kwa wabunge kukubali suala hilo lirudi serikalini.

Tulijua ni suala la muda kutakuwa na kusafishana. Hebu tazama, taarifa za mawaziri wa maskata mawili tofauti zinatolewa siku moja.Halafu angalia namna taarifa ilivyotolewa.

Kuna tofauti gani na ile ya katibu mkuu aliyegawa rushwa na kuruhusiwa kustaafu?

Katika mwendo huu nani anaweza kusimama jukwaani akaambia wananchi wapambane na rushwa?

Kwa mwendo huu, wizi wa rasilimali, na ufisadi utakomeshwaje?


Tunaendelea kujiuliza kwanini sisini masikini.

Hata sisi wenyewe hatujui kwanini ni masikini ingawa tunajua namna ya kusaidia wale wanaotaka '' kuondokana na umasikini'.

Hatujui kwanini sisi ni masikini!!!!
 


Mkandara,

..naomba nikusahihishe kidogo.

..Dr.Slaa alishinda ktk kura za maoni za CCM huko Karatu.

..sasa CCM wakamfanyia mzengwe kwa kukata jina lake na kumpa ushindi mgombea aliyeshika nafasi ya pili.

..wananchi waliokuwa wakimuunga mkono Dr.Slaa wakamwelekeza achague chama kingine watamuunga mkono. Dr akahamia CDM and the rest is history.

..Dr.Slaa hakupewa nafasi za uongozi haraka kama ulivyoeleza. alikaa bungeni na michango yake mle ndiyo iliyopelekea yeye kupewa nafasi za uongozi CDM.

..pamoja na hayo, huyu mzee wa watu ana uwezo na ni mpambanaji kwelikweli. hakuna shaka kwamba ametoa mchango mkubwa sana ktk kuijenga CDM.[/QUOTE Mkandara ukiangalia profile yake yupo kuanzia
2006.
Hayo uliyosema JokaKuu alipaswa kuyajua kuliko wengi jamvini. Makusudi kabisa anapindisha ukweli
Anapindisha ukweli ili kukidhi haja ya kuonyesha supreme leader hajafanya makosa

Ndio Mkuu JokaKuu ahsante sana kwa ufafanuzi wako.

Tulikaa kimya tukijua ukimuuliza kauli ya Shinyanga/Mwanza kuporwa na K’njaro/Arusha ni shihi?
Jibu lake mbona Mbowe kasema ABCD


Tazama uongo alioueleza hapo juu. Anasema Slaa alipanda ngazi kiajabu ajabu ili kuhalalisha supreme kupewa nafasi haraka haraka.

Katiba ya CDM iliandikwa na akina Kitila na Zitto. Nafasi ya katibu mkuu ilielezwa namna inavyopataikana. Haikuwaihi kuundwa ili kukidhi haja.

Alikuwepo Aman Kaborou na wengine. Nafasi ya supreme imeundwa 24hr ili kukidhi haja ya kumsimika supreme


Kwa mtazamo huo unawezaje kufananisha watu hao wawili na mazingira yao?

Kama livyosema Mchambuzi, lengo ni ku-derail mjadala uondoke kwa wahusika.

Hilo tunalijua. Sababu kubwa ni kushindwa kukabiliana na hoja zinazomkabili supreme na ACT.

Mkandara hawezi kufanisha ‘unyemela’ wa kubadilisha katiba ya CDM na unyemela wa kuweka cheo cha supreme kwa kubadili katiba ndani ya saa 24 just to accommodate individual interest.


Hawezi kukemea kauli ya ACT ya kuwagawa Watanzania kwasababu tu mbona fulani kasema!

Hoja ya ukanda iliyowakimbiza ndio hiyo wanayoihubiri.

Alichokifanya supreme ni kuwaeleza wananchi wa Shinyanga/Mwanza kataeni hao kutoka eneo fulani.

Hoja ya CCM sasa imepata mpiga debe. Ndio maana tunasema huu ni mpini, shoka lenyewe lipo kimya


Kisha endelea
Hizi Mada zimechanganywa au? naona zipo pande mbili katika Duru za siasa - ACT kama mpini wa CCM na hii na Matukio ya dunia. imekuwaje?

Mkuu naomba takwimu za maoni ndani ya CCM maana mnapenda sana kuamini vitu. Ikiwa kweli leo mnaamini chama ni zaidi ya mtu kama Zitto imekuwaje, wanachama wa CCM wamwambie Dr.Slaa ahamie Chadema, chama wanachopingana nacho ili wampe kura zao. Inaingia akiini kweli?
 


Hizi Mada zimechanganywa au? naona zipo pande mbili katika Duru za siasa - ACT kama mpini wa CCM na hii na Matukio ya dunia. imekuwaje?

Mkuu naomba takwimu za maoni ndani ya CCM maana mnapenda sana kuamini vitu. Ikiwa kweli leo mnaamini chama ni zaidi ya mtu kama Zitto imekuwaje, wanachama wa CCM wamwambie Dr.Slaa ahamie Chadema, chama wanachopingana nacho ili wampe kura zao. Inaingia akiini kweli?
Nimeangalia sijaona mahali panapochanganya, kama kupo basi mada zirudishwe kule kwa ACT mpini.

Kuna uwezekano mtu akachangia katika uzi tofauti, naomba kama imetokea basi bandiko lirudishwe eneo husika

Ahsante kwa angalizo
 
Back
Top Bottom