ESCROW: KUJIUZULU HAKUKWEPEKI
SERIKALI HAIAMINI VYOMBO VYAKE
RAIS ATABEBA LAWAMA ZITOKANAZO
Utetezi dhidi ya taarifa ya PAC unaendelea. Katika nchi za wenzetu, uwajibika ni sehemu ya maadili ya uongozi. Kutajwa tu katika kashfa inatosha kabisa kwa kiongozi kujiuzulu.
Kujiuzulu kuna maana nyingi kisiasa
- Kukubali kuchukua wajibu kwa kosa
- Kutoa nafasi ya kuchunguzwa ili ukweli ujulikane
- Kuepusha madhara kwa serikali/taasisi au shirika husika
- Kusaidia chombo teuzi kuondokana na lawama
n.k.
Taarifa ya PAC iliyowasilishwa, imenukuu uchunguzi uliofanywa na ofisi ya CAG na PCCB ambavyo ni vyombo vya serikali.
Kila lililosemwa si kutokana na utashi wa watu au mtu bali taarifa ya kitaalamu kutoka katika mamlaka husika
Serikali iliekeza vyombo hivyo vifanye uchunguzi na kuja na taarifa.
Taarifa imeonyesha kuhusika kwa kundi kubwa la watu kutoka kila eneo la jamii, kuanzia mawaziri, wabunge, raia, viongozi wa dini na taasisi kama TANESCO, BRELA n.k.
Kitendo cha mawaziri kuhusishwa na kashfa ni tukio baya hata kabla ya kuangalia ubaya wake.
Kwasasa, serikali ipo mateka kutokana na watu wachache ima kuvurunda au kufanya uhalifu.
Vyovyote iwavyo, hakuna jinsi ya kuisaidia serikali iliyopo madarakani kama si wahusika kujiuzulu nafasi zao.
Hilo sit u litarudisha imani ya wananchi kwa serikali yao, bali pia litaonyesha utawala wa sheria na demokrasia
Katika taratibu za kiutawala, wateuliwa wa Rais wanawajibika kwake.
Makosa yao ni makosa ya mteuzi ambaye ni Rais. Katika hali iliyopo, watuhumiwa wakigoma, watakuwa wanamweka Rais katika wakati mgumu sana.
- Kwamba, alazimike kuwawajibisha ili kuondokana na lawama
- Aendelee kuwa nao, wananchi wapoteze imani na serikali yao
Taarifa ya PAC iliyonukuu CGA na PCCB imeonyesha wazi uwepo wa uzembe ambao ulitetewa kwa uongo ndani ya bunge.
Pia imeonyesha kukiukwa kwa baadhi ya taratibu za utendaji.
Na kibaya zaidi, kuna shaka juu ya maadili ya kiroho ''moral authority'' ya viongozi husika.
Hayo tu yanatosha kabisa kueleza kwanini viongozi husika wanatakiwa kujiuzulu.
Endapo hawakubaliani na hilo, suala na mzigo mzito wa tuhuma utamwangukia Rais wan chi. Hatuwezi kuwa na serikali isyoamini uchunguzi wa vyombo vyake vyenyewe.
Hapo kuna tatizo kubwa sana.
Tusemezane