TATIZO LA ESROW SI NANI AMEIBA, BALI NINI KIMESABABISHA WIZI
Tunakumbuka tatizo la madni lililoanza kwa hoja zile za Buzwagi.
Mwisho wa siku kamati iliundwa na hadi leo tatizo lipo pale pale huku serikali iliyosema inashughulikia ikiwa imekalia taarifa hizo makabatini. Wanasiasa wakapanda chati, wananchi wakapoteza!
Ndivyo ilivyokuwa kwa EPA, Richmond n.k. Haiwezekani eti wananchi waambiwe pesa zilitoka hazina bilioni 28 na hakuna anayewajibika au aliyebainika kuzitoa.
Hakuna jibu la mfumo uliotumika na udhaifu wa mfumo kudhbiti tatizo hilo.
Wanasiasa walipanda chati kwa kelele, wananchi wakapoteza kwasababu hawana jjibu.
Tatizo la Escrow si tofauti. Wananchi wasichokitambua ni kuwa huu ni wizi unaofanywa na genge la watu wenye elimu, watu wanaoweza kuiba na kusimama mbele kusema hawakuiba bila kuchukuliwa hatua.
MFUMO MZIMA WA WIZI
Ukitazama kwa undani, suala la Escrow si uzembe wa watu wawili. Ni mfumo mzima uliokufa.
Ndizo sababu za taasisi mbali mbali za kijamii, asasa na watu binafasi kuwa sehemu ya uhalifu huo
Tunasema uhalifu kwa uhakika kwasababu bunge limekubali upo uhalaifu ndio maana limeagiza uchunguzi na hatua za kuchukuliwa. Hivyo, si suala la kusema kuna uhalaifu, bali uhalifu upo tena wa kiwango cha juu sana.
Tumeona mzozo mkali kati ya watu watatu au wane, hasa waziri nishati, katibu mkuu nishati, waziri mkuu na waziri mmoja aliyetuhumiwa kwa uoenvu mama Anna Tibaijuka.
Tuna sababu za kusema Tibajuka katuhumiwa bila sababu za msingi.
Na hapa tufafanue kabla hatujaendelea na ubovu wa mfumo mzima.
Ukisoma orodha ya wahusika na taarifa, hakuna mahali jina la Tibaijuka limejitokeza katika Escrow.
Jina lake limetokea katika wale waliofadika na mgao wa pesa hizo ambaozo bunge limeridhia ni haramu kwa kusema Stanbic inatakatisha.
Orodha iliyotolewa ni ya account moja. Hakuna orodha iliyo wazi ya account zingine na hivyo hatujui wangapi wamefadika na mgao Tibaijuka kapokea kama msaada, hata kama alikuwa na dhamana ya kutulia shaka, na kwamba, ni kiongozi alitakiwa kuwa makini, swali ni kuwa viongozi wangapi wamepokea mgao huo na majina yao hayakutajwa tena pengine moja kwa moja kuliko ''msaada''?
Kwanini ionekana mama
Anna Tibaijuka peke yake na wala si mlololongo mzima uliochukua pesa hizo haramu?
Nani anajua majina yaliyotajwa yalikuwa na uhusiano na viongozi wengine?
Mfano, lingetajwa jina la kachabuseta kupata milioni 600, je tunatakiwa tukae kimya tu kwasababu mtajwa si waziri?
Vipi kama mtu huyo ametumika kama conduit(njia tu) ya kupatishia pesa za wazee?
Mfano mwingine. Ukisoma orodha ya wafaidika utaona watuhumiwa wakubwa kama waziri na katibu au wale wa ofisi nyingine kama BoT na Ikulu hawapo. Kwanini waziri au katibu mkuu apiganie jambo ambalo mgao wake haupo?
Je, tuamini tu kuwa makosa yao ni kufanikisha dili bila ya malipo ya aina yoyote?
Kama walipata mgao, wapi majina yao yaliyopo?
Kwanini Anna aliyepata aoenkane peke yake?
Huko BRELA na BoT hakuna waliosadia kusukuma cheki za pesa za mbele?
Wameyajwa majaji katika mgao na viwango vyao.
Kwanini hakuna anayeona kama kuna ukiukwaji wa maadili, lakini watu wadhani Tibaijuka ndiye pekee aliyekiuka maadili?
Turudi katika mfumo
Ukitazama ripoti, kila sehemu ya serikali, bunge na mahakama ambayo ni mihimili mikuu ya nchi.
Escrow si suala la kisiasa ni la Kiuchumi. Kuzagaa kwa pesa kunaweza kuwa na athari katika mzunguko wa pesa, na anayepokea athari ni mwananchi anayeishi kwa dola 1 si ‘mwenye nchi aliyepata dola 10,000 au zaidi''
Katika nchi yetu tuliko la kampuni hewa liliwahi kujitokeza kwa Richmond.
Ubalozi wetu ukatusaidia kubaini kampuni hiyo hewa.
Tulidhani hilo lilitakiwa liwe funzo kwamba balozi zetu zina nafasi katika usalama wa nchi kiulinzi na kicuhumi.
Inashangaza tatizo limejirudia kwa kuwa na kampuni hewa kutoka Malaysia iliyoingia katika Escrow.
Hatukutumia balozi zetu, tumetuma mtu kwenda kuchunguza badala ya vyombo vya kidiplomasia.
Leo tumetengenezewa umeme na kampuni hewa. Tunaambiwa bora umeme umekuwepo.
Tujiulize katika hali hii, hivi si kweli kuwa ipo siku makundi kama Alshababab yanaweza kuja kuwekeza nchi katika sekta nyeti, yakisoma siri za nchi napengine kuleta hujuma kubwa kwa taifa?
Hivi taasisi ya BRELA kazi yake ni kuorodhesha majina ya kampuni au ni zaidi ya hapo.
Kwanini taarifa hakuonyesha ima kuzembea au kuhongwa kwa viongozi wa BRELA? Hili si tatizo la mfumo kweli!
Usalama wa taifa
Huu kazi zake ni zaidi ya kulinda viongozi. Inapotokea tapeli anaweza kuja na kampuni hewa, akawekeza, akavuna pesa tena akinunua viongozi waliokula kiapo cha umma, hapa hakuna hujuma kutoka taasisi hii muhimu katika uchumi na ulinzi wa taifa kweli!
Mbona hatukuona ushiriki au kutoshiriki au jitihada za taasisi hizi katika suala zima.
Inaendelea mfumo……..