Duru za siasa: Matukio nchini na duniani kwa ujumla

KIFO CHA ESCROW KIMEWADIA
WANANCHI WAMEFUNGWA MIDOMO KWA KAMBA ZA MAHAKAMA

CCM IMETEKA HOJA BAADA YA ADHABU YA WANANCHI

http://www.mwananchi.co.tz/habari/K...bani/-/1597296/2589796/-/ysq9pyz/-/index.html

http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=76315

http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=76317

Hii ni sehemuyamabandiko takribani 20 tukieleza kwaundani kuhusu mbinu za serikali za kuficha uozo wa Escrow. Reference ya mada hii ni bandiko 50-54

Tulisema lengo la serikali nikuiteka hoja na kuitumia kwanjia zisizo sahihi
Tulieleza kuwa wapinzani walifanya makosa kushiriki kamati yamaridhiano.

CCM hainahistoriaya maridhiano, lini wanaweza kuja na hoja ya maridhiano ikaaminiwa?
Tulisema Mbowe na Zitto waliuza hoja na
walioshindwa niwananchi.


CCM inatumia vikaovyao inatumia udhaifu wamaridhiano kujijenga baada ya kujeruhiwa uchaguzi serikali mitaa.

Serikali nayo inahakikisha suala la Escrow halisemwi walahalizungumzwi tena.
Leo wamekamatwa watu wawili kwa kutuhuma za kula rushwa ya kupewa mamilioni na Rugemalira.


Huo ni usanii, ukisoma mashtaka yanayowakabili ni pamoja na kuchukua rushwaili kufanikisha suala la IPTL . Inachekesha sana kwasababu sheria za nchi zinakataza kutoaa u kupokea rushwa. Iweje sasa Rugemalira anayejulikana katoa rushwa asifunguliwe mashtaka?

Hili la mahakamani limefanywa makusudi. Tuliwahi kuelezakuwa mbinu itakayotumika kuzima mjadalawa escrow nikukamata watu wawili, ili suala hilo liwe mahakamani na lisiandikwe au kuzungumzwa tena.

Njia ya pili, ni kuwafariji wafadhili , tatizo linashughulikiwa na wapo waliofikishwa mahakamani tayari.

Na tatu, ni kuridishaimanikwawananchi katikamantiki ile ileya kushughulikia tatizo.

Kitendo cha kukubali kulirudisha sualala escrow serikali ilikuwakosa kubwa.
Kitendo
cha kukubali uwepowa kamati yamaridhiano ilikuwa ni kosa kubwa.

Na kitendo chawananchikushangiliakuondolewa kwa Tibaijuka nikosa kwa kuondoa jicho sehemu husika.

Sasa Escrow imezuiliwa kusemwa, ipo mahakamani na kifo chake kimefika rasmi.
Serikali inapumua kama tulivyowahi kuandika huko nyuma.

Wananchi wapigwa changa la macho. Wasubiri khanga na kofia za CCM kwa pesa zao kupitia ufisadi.


Tusemezane
 
MHONGO ANG'OKA

JE, TATIZO LIMEKWISHA? JE, SULUHU IMEPATIKANA?

JK, KAMA SI ''ZA WANANCHI'' HATUA UNAZOCHUKUA NI ZA NINI?

Kwanza,tungeomba wasomaji warejee mabandiko 46-55. Mengine kuhusu Escrow yameelezwa
Tulisema kuirudisha Escrow serikalini ilikuwa ni makosa.

Ni makosa yaliyofanywa na Mbowe na Zitto katika kile wkilichoitwa kamati ya maridhiano ya Bunge. Y
anayotokea ni kutokana na uzembe huo.

Mhongo amejiuzulu kama ilivyo kwa wengine. Kujiuzulu kuna maswali mengi yanayoonyesha kufichwa jambo, au udhaifu wa uongozi

Rais Kikwete alisimama Diamond na kutetea pesa zile hazikuwa za umma na wala hakukuwa na jambo lolote baya

JK akamfukuza Anna Tibaijuka hadharani katika hali inayoonekana sasa hivi kama kumtoa kafara.
Mwanasheria Werema alijiuzulu, ikiwa ni maagizo ya kutakiwa kufanya hivyo.

Mhongo akawekwa kiporo kupisha uchunguzi ukamilike. Na sasa amejiuzulu, bila kujua kama uchunguzi ulimtia matatani au la.

Kwa hali yoyote wananchi wanapaswa kuamini jitihada za kumlinda Mhongo zimeshindikana, na deal nzima ya Escrow ni chafu. Endapo si chafu, kwanini Rais awawajibishe wasadizi wake kwa deal safi?

JK anauambia umma, alichosema Diamond ilikuwa kupitisha upepo wananchi wasahau.Kuna uchafu kuanzia serikali, Mahakamani hadi taasisi za dini bila kusahau Ikulu iliyotajwa mara nyingi tu.

Hatua zinazochukuliwa ni za kuwaridhisha wahisani kwa upande mmoja,kupooza kipigo cha serikali za mitaa kwa upande mwingine.

Hata hivyo, serikali inasahau kuwa suala si kujiuzulu bali waliohusika kufikishwa mbele ya sheria.

Ni kwa mantiki hii, bunge na maazimio yake dhaifu lazima lisimame kutetea hoja ya ''wahalifu'' kuwajibishwambele ya sheria
Hakuna mantiki wananchi kuridhika na hatua za kuwapunzisha watu ili waende kutumia mafao yao kwa starehe.

Utamaduni huu ni dhaifu na hutumiwa na viongozi dhaifu.

Tubadilike na pa kuanzia ni hapa,kuitaka serikali ichukue hatua dhidi ya watuhumiwa. Kazi ya bunge ianze na si kufikia tamati.

CCM INATAFUTA MCHAWI ISIYEMJUA

CCM inatafuta mchawi kwa kudhani Escrow ndiyo chanzo cha kuchukiwa na wananchi

Upo uwezekano Escrow ni sehemu ya sababu na si sababu ya CCM kuchokwa.
Yapo mambo kama katiba na uhuni uliofanyika, na ni bahati mbaya wananchi hawakuwa na uwezo,hilo ndilo liliwakera sana

Ilipokuja escrow ikawa kama chumvi (catalyst) iliyoambatana na uchaguzi

CCM wasidhani hili linaweza kurudisha imani ya wananchi iliyopotea.

Kinachoweza kuwasadia ni kuwasikiliza wananchi wanataka nini.
Mbinu chafu kama za kulazimisha kura ya maoni zitaamsha hisia upya kuelekea 2015.

CCM, MCHAWI WENU MNAYE WENYEWE
Endapo CCM wanadhani escrow ndiye mchawi, hapo watakosea. Mchawi wa CCM ni mwenyekiti wao

Escrow ilipoanza, serikali ilikingia kifua lisizungumzwe bungeni. Hata yalipotolewa majina ya wahusika mwenyekiti alitoka hadharani na kuwatetea, huku akweka wengine viporo.

Leo baada ya CCM kudhurika, mwenyekiti anachukua hatua za kufunika makovu.

Mwenyekiti wa CCM alitakiwa kuwa mstari wa mbele kusafisha chama.

Kwasasa anasafisha kitu gani ikiwa chama kimeshaathirika tayari na uzembe alioufanya?

Udhaifu wa mwenyekiti kuchukua hatua, na ujanja wa kutoa baadhi kafara kama funika kombe, ndio uchawi unaoiponza CCM. Hakuna Mchawi mwingine nje ya CCM.

Tazama, hili la kura ya maoni nalo lipo katika mfano wa escrow.

Mwenyekiti anaelewa kuwa katiba ya Chenge ilianadikwa ili kuhakikisha escrow haijadiliwi.

Ndio maana akina Chenge, Ngeleja, Tibaijuka walikuwa mstari wa mbele kupindisha taratibu, kupiga debe ukiaukwaji wa sheria ili kuhakikisha katiba inachukua nafasi ya mjadala wa escrow.

Kwasasa, tunajua sheria haitoi nafasi hata kura haramu ya maoni kufanyika.

Bado mwenyekiti wa CCM anaendelea na shinikizo licha ya kusaliti makubaliano na wapinzani, kuvurugwa kwa mchakato, na kususiwa kwa katiba pendekezwa.

Itakapofika wakati wa hukumu, CCM watahukumiwa kama CCM na hasa wabunge wao wanaosaliti umma.

Pengine mwenyekiti anajua hana la kupoteza, lakini CCM lazima watambue kuwa kiboko cha wananchi kitawafikia mmoja mmoja pale alipo.

Tutashangaa wakikaa vikao na kutafuta mchawi wakati wanajua mchawi wanaye ndani ya chama chao

Tusemezane
 
Thanks Nguruvi3 kwa uchmbuzi mKini kabisa,
nitakuja baadae tujadili pamoja sual la wapinzani kususia kura ya maoni ya katiba mpya, ambao ni ushauri wako mkuu hapa
 
DURU MATUKIO
Sehemu ya I
GWAJIMA vs PENGO
BVR ZA NIGERIA
Kauli ya kadinali Pengo kuhusu kura ya maoni imeletamtafaruku.

Pengo amepingana na jukwaa la maaskofu linaloundwa na kanisa katoliki,walutheri na Waprotestanti


Kauli ya jukwaa lisema, wakristo wajiandikishe katikadaftari la wapiga kura,waipige kura ya hapana katiba ya Chenge

Sababu walizotoa ni mchakato kutofuatwa, uwepo wa hujuma ndani ya BMLK na kwamba, katiba pendekezwa haina uhalali
Pia walizungumzia mahakamaya
kadhi


Kadinali pengo aliwapinga kwa kusema, jukwaa halina haki yakuamua kwa niaba ya waumini namna ya kupiga kura.

Kauli ya Pengo ina utata kwakuzingati kanisa katoliki lilishiriki katika mkutano wa jukwaa

Haieleweki endapo kauli ya Pengo ni yake binafasi au ni yakanisa

Mchungaji Gwajima ametoa video ikieleza kwa ukali akimtuhumu Pengo kwenda kinyume na kauli za maaskofu wenzake, tena kanisa katoliki likiwa limeshiriki

Gwajima ameitwa Polisi kutoa maelezo

Haieleweki maelezo anyotoa ni kufuatia malalamiko ya kadinali Pengo, au ni serikali inayoona uwepowa tatizo


Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni naye ametoa amri ya Gwajima kufika ofisini kwake kutoa maelezo.

Naye kama Polisi, haielweki amepokea malalamiko ya Pengo au ni mtazamo wake kama mkuu wa Wilaya


UTATA NA USHIRIKI WA SERIKALI


Kauli za Gwajima ilikuwa dhidi ya Kadinali Pengo.

Wote niviongozi wa dini na hivyo wana njia nne za kumaliza tofauti zao

1 Kukaa kimya kati yao kama kukubaliana kutokubaliana

2. Kukaa pamoja meza moja kumaliza tofauti zao

3 Kuwatumia viongozi wenzao wa kiroho kuwapatinisha

4 kwenda katika vyombo ya sheria za nchi, polisi namahakamani


Inaendelea sehemu ya II…..
 
Inaendelea II

UFAFANUZI WA HOJA 1-4 HAPO JUU

Hoja 1-3 zinahitaji maridhiano ya pande husika. Hazina tatizo na zinabaki kwa wahusika
Hoja 4 ina tatizo ambalo kama halitaangaliwa litaweka mtazamo mbaya wa siku za mbeleleni ‘bad precedency'
POLISI NA MKUU WA WILAYA

Hawa huangalia usalama wa raia, mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa kamati ya usalama na ulinzi ya Wilaya na mkoa

Kazi zao zina mapaka. Si kila tukio watatakiwa wawepo hadi washiriki watakapopeleka malalamiko,hoja n.k

Ndio maana hawawezi kwenda kumkamata mtu mtaani kwasababu tu amehitilafiana na swahiba wake, mkewe au wamenyang'anyanyana bia


Katika mazingira yaliyopo, endapo Pengo amekwenda kumshitaki Gwajima Polisi, kazi ya Polisi ni kufanya uchunguzi na kumfikisha mahakamani kama haja itakuwepo

Hadi Polisi watakapoweka wazi chanzo cha malalamiko, sakata linaonekana kushikiwa bango na Polisikwa ushabiki Zaidi ya taratibu na sheria.

Ikiwa hakutakuwepo mlalamikaji, Polisi wakae pembeni.

Kuendelea kushinikiza ni kusimamia haki kwa jicho la kengeza


MKUU WA WILAYA
Kwa upande wa mkuu wa Wilaya ya Kinodoni naye ameita waandishi na kuwaeleza yake.

Akiwa mkuu wa Wilaya suala la Gwajima ni sawa na ugomvi wa watu wawili mtaani, kanisani, msikitini au kwenye Bar. Kazi ya mkuu wa Wilaya ni kusimamia ulinzi na usalama kama mjumbe wa kamati


Si kazi ya mkuu wa Wialaya kuchukua jukumu kuvaa mzozo wa watu wawili.

Pengo na Gwajima ni Watanzania na viongozi wa Kiroho. Alichokisema Gwajima au Pengo havina uhusiano wa aina yoyote wa kuvurugwa Amani au ulinzi na usalama wa Wilaya yake


Makonda kama mkuu wa Wilaya hawezi kusimama kama mwendesha mashtaka kukiwa hakuna mlalamikaji achilia mbali hilo si jukumu lake.

Pengo hajalalamika, iweje Makonda aingilie mzozo huo? Makonda anamwita Gwajima ili iwe nini!


Tunachikiona kwa mkuu wa Wilaya Makonda, ni kile alichosema Rais mstaafu Mkapa.

Majuzi Mkapa amesema, sekta ya utumishi wa umma imevurugwa sana.

Akasema, siku hizi mtu anaweza kuwa yoyote bila kujali historia , uwezo na uzoefu wake kikazi


Mkapa alizungumzia haya ya Makonda. Huyu mkuu wa Wilaya alikuwa mhamasisha wa Chipukizi.

Hajawa na nafasi yoyote katika utumishi wa umma. Tunamjua kwa ‘ushiriki' wake katika kutoa kipigo kwa mzee Warioba, kipigo kilichompa cheo


Inaendelea....
 
Inaendelea III

Matokeo ya kuvurugika kwa utumishi wa umma ni kama haya ya mkuu wa Wilaya kuingilia ugomvi usiomhusu.

Si ajabu ipo siku tutasikia Makonda akigombe Pingu na koplo wa Polisi kwenda kuwafunga mabaa medi wawili wanaogembea buzi


Si ajabu Makonda akaandika barua ya kumtaka mlevi mmoja aliyesahau kitoweo bar aende kutoa maelezo.

Yanawezekana kwasababu haionekani kama anaelewa nafasi yake inamtaka afanye nini


Makonda anamwandikia barua Gwajima na kisha kuongea na vyombo vya habari.

Taratibu za kiofisi hazitaki hilo na huu ni weledi finyu pengine kutokana na uzoefu wa Chipuki.

Makonda anadhani kuongoza watu katikawilaya ni sawa na kuongoza Chipukizi wakijiandaa kwa halaiki uwanja wa taifa


HITIMISHO


Polisi na Makonda kwa pamoja wanaonyesha ushabiki naunafiki.

Haiwezekani wamkemee Gwajima ili hali walikaa kimya wakati waziriLukuvi akihubiri chuki Kanisani kupitia katiba mpya.


Alichokifanya waziri Lukuvi ni jambo la hatari sana kuliko maneno ya Gwajima na Pengo.

Lukuvi alihamasisha mtafarauku wa dini mbili za wakristo na Waislam.

Hatumkusikia mkuu wa Wilaya, mkoa, waziri, waziri mkuu ,mkuu wa Polisi au Rais akimekemea.

Ni kituko ugomvi wa maneno wa Gwajima na Pengo unakuwa tishio la Amani nchini na si tishio halisi la Lukuvi


Tusemezane
 
BVR
Uchaguzi wa Nigeria umemealizika jumapili baada ya kuongezwa siku kutokana na matatizo ya kiufundi ya BVR

Matatizo hayo alikumbana nayo Rais na mgombea bwana J. Goodluck

Mfumo wa bvr haukuweza kutambua alama zake. Huyo ni mkuu wanchi aliyezindua mpango huo na hakuna shaka usahihi na umakini ulikuwepo kwa kiwango cha juu wakati anaandikishwa

Nigeria wanatumia BVR kwa mara ya kwanza. Wameanza uandikishaji kwa muda mrefu.

Hata pale akina Jaji Lubuva walipokwenda kuazimaBVR, Nigeria iliwakatalia kwasababu BVR si chombo cha msimu, ni chombo cha huduma za kila siku


Pamoja na kuwa na BVR kwa muda mrefu, tatizo la uandikishaji na upigaji wa kura limevuruga uchaguzi kwani haukufanyika kama ilivyotarajiwa.

Ikumbukwe, Nigeria wamekuwa na BVR kwa muda mrefu wakitumia kuandikisha wapiga kura


Hakuna shaka, Nigeria walifanyia tathmini na usahihi wa mfumo husika kabla ya kujiridhisha unafaa.
Bado wamepata matatizo


Tunjiuliza, sisi tulipkwenda kuazima BVR kwao tuna hali gani.

Maana muda wa kuandikisha na kufanyia usahihi mfumo husika haupo kwa hesabu zozote za mtu anayetumia fuvu na ubongo wake kikamilifu


Mkoa mmoja tu wa Njombe ndio unasemekana kukamilisha uandikishaji tena bila tathmini.

Tunauliza, muda gani upo kwa mikoa 29 mingine mikubw kama Morogoro, yenye watu wengi kama Mwanza na Kilmanjaro


Hili la Nigeria ni ujumbe kutoka kuzimu kuwa kinachofanywana akina Lubuva ni hatari kubwa kwa taifa.

Kinachofanywa na akina PM ni balaa linalosubiri muda,kinachofanya na Rais ni kuandaa mazingira mazuri kwaajili ya ubovu

Mheshimiwa, kila mara umelalamika kushauriwa vibaya,hatudhani kama tunakushauri vibaya.

Hata kama tunakushauri vibaya si jambo bayakwasababu unashauriwa vibaya kila mara


BVR haiwezekani kwa sasa, hakuna sababu za kuharakisha matatizo.

Zipo sababu za kahirisha matatizo kama si kuyaondoa. Kura ya maoni n itatizo linalosubiri kichochoe


Tusemezane
 
BVR imekuwa haina rekodi nzuri ya performance kwenye nchi nyingi za kiafrika ambapo zimetumika kwenye uchaguzi....
 

2006.
Hayo uliyosema JokaKuu alipaswa kuyajua kuliko wengi jamvini. Makusudi kabisa anapindisha ukweli
 
Last edited by a moderator:
Inaendelea
 
..........
 
..................
 
Endelea kuanzia bandiko 47 hadi hili hapo juu
[QUOTE=Nguruvi3;11588696]RAIS ALIPOWANG'ONGA WABUNGE

KABADILIMSIMAMO WA SERIKALI YAKE KUIPINGA ESCROW

WABUNGE WALIOTETEA SERIKALI WANAONEKANA HAYAWANI NA MAZUZU, RAIS WALIYEMTETEA ANAWASHNGAA

Tunasema anawang'onga wabunge kwasababu Rais anawashangaa wabunge wanaopinga escrokujadiliwa.
Hapa kunasura mbili.

Kwanza, Rais aliagiza serikali yake izuie suala la escrow lisiendebungeni hata kufikia mahali pa kuishinikiza mahakama iandike barua juu yazuio


Je, kunaudhati wa Rais kusema amefurahia suala hilo kujadiliwa?Anafurahi vipi ikiwa hakutaka lijadiliwe bungeni?

Kama Rais alitaka suala hilo lijadiliwe na aliridhika lijadiliwe, ilikuwaje Job Ndugaialiyekuwa anakaimu kiti cha spika apelekwe nje ya nchi naserikali ile ile inayosema imefurahishwa na suala escrow bungeni?

Pili, Raisanasema anashangaa wabunge wa CCM waliopinga suala la escrow lisijadiliwe.
Hawani mawaziri kama Lukuvi na wasira, wabunge akina AsumtaMshama, Luisnde na wengine.



Maana yakauli ya Rais ni kuwafanya waliotetea serikali waonekane mazuzu namazumbuku, na ndivyo
Tatu, Raisanapohoji umakini wa wabunge kuhusu azimio lao ka kutaifisha mitambo ya IPTL,hilo ni tusi.

Bunge lina wasomi walioangalia athari za kufanya hivyo.
Lakinipia, kuwafukuza wahuni ni jambo linalolalamikiwa na wafadhili wa serikali yake.


Hili lilikuwa ni tusi kwa wabunge na bunge kwa ujumla.
Somo kubwawanalopaswa kulipata wabunge na viongozi wengine ni kuwa kauli za Rais huwazina ncha mbili na wala haijulikani ni lini atachukua upande wancha

Wapinzaniwameonja joto la jiwe mara nyingi. Kundi lisiloona ni la wana CCM ambao hatawanapodhalilishwa bado wanabaki kuwa waadilifu. Ni wakati wabunge wajiulize, hivi watatumika kama karatasi za maliwato hadi lini?

Je, wabungehawaoni jinsi wanavyodhalilishwa?

Tusemezane[/QUOTE].........................
King Suleiman Adharusi Alinda Mchambuzi JokaKuu Zitto Bongolander Jasusi Mzee Mwanakijiji Mkandara Ngongo Katavi gfsonwin Pasco
 
Last edited by a moderator:
Kwa mujibu wa mgazeti mh Nchimbi, Mng'ong'o na Maswi wamesafishwa kutokana na tuhuma zinazowakabili

Je, wale waliobaki na ‘uchafu' wamechukuliwa hatua gani na serikali?

Je, mama Tibaijuka hakupaswa kupewa benefit of doubt kama hao wengine?

Je, bunge limetimiza wajibu wake wa kuisimamia serikali ?

Je, kulikuwa na sababu zozote za kuwa na kamati ya bunge kuchunguza tuhuma?

Je, wale waliosimama katika hoja hizo, serikali inawaambia nini? Ni waongo au wazushi?

Je,kuna sababu za bunge kujadili tena tuhuma kama mhimili wa utawala ni mkubwa kimadaraka kuliko ule wa bunge?

Je, akina Mbowe na Zitto waliounda kamati ya majadiliano,hiki ndicho tulitegemea ?


Kwanini wananchi tusiamini bunge letu limejaa waongo, wazushi, wenye wivu kwa vile serikali imeona madai ya bunge hayakuwa na msingi wowote dhidi ya watuhumiwa?

 
.........................
King Suleiman Adharusi Alinda Mchambuzi JokaKuu Zitto Bongolander Jasusi Mzee Mwanakijiji Mkandara Ngongo Katavi gfsonwin Pasco[/QUOTE]

Kuna siku niliwahi kusema kuna baadhi ya wabunge huwa wanadhani Rais wetu mjinga. Naunga mkono maoni ya JK, wabunge wengine kweli maamuzi na busara zao vinatia shaka.

Mkuu nguruvi mchafu ni mchafu tu, hata gazeti likijaribu kumsafisha haliwezi kuondoa uchafu.
 
Something 'might be' unclear on the type of connection forming the chain of Maswi+Mhongo+Mrisho
 
Mkuu Jitegemee , hapa kuna hoja zinachanganya sana

Kwanza, suala la escro liliungwa mkono na wabunge wote wakiwemo CCM.

Maazimio yalikuwa ‘yapo matatizo'yaliyototokana na viongozi husika.


Pili, suala la kampeni ya wanyamapori, mawaziri walijiuzulu na wengine kuondolewa nafasi zao.

Kilichotokea bungeni kwa mujibu wa hansard ni kuwa viongozi waliohusika na waliotajwa na kamati ya bunge hawawezi kushgulikiwa na mhimili huo bali mamlaka zilizo wateua.

Hadi hapo tunajua lilikuwepo tatizo. Na ikumbukwe, TAKUKURU walihusika na vyombo vingine vya umma katika uchunguzi


Leo tunaambiwa tume ya maadili imeona hawana hatia. Wote, wale wa wanyama pori na wa escrow

Katika hali ya kushangaza, yupo waziri aliumbuliwa hadharani.

Jina lake halikupelekwa katika tume ya maadili ya viongozi.


Sasa kama tume ya maadili imeona hawana tatizo, ni tatizo gani ambalo bunge ililiona dhidi ya watuhumiwa?

Na bunge lilikosa uchunguzi upi kiasi cha tume kuja na uchunguzi mkubwa kuliko wakamati ya PAC na bunge kwa ujumla?

Lakini pia tunajiuliza, hivi mhimili upi ni mkubwa kati ya mihimili mitatu ya nchi?

Inawezakanaje bunge liwena hadhi ya kuisimamia serikali, na serikali iwe na hadhi ya kukataa maamuzi yabunge?


Wengine tulishasema katika mabandiko kuanzia 40+ hadi 60 kuwa ilikuwa ni makosa kwa wabunge kukubali suala hilo lirudi serikalini.

Tulijua ni suala la muda kutakuwa na kusafishana. Hebu tazama, taarifa za mawaziri wa maskata mawili tofauti zinatolewa siku moja.Halafu angalia namna taarifa ilivyotolewa.

Kuna tofauti gani na ile ya katibu mkuu aliyegawa rushwa na kuruhusiwa kustaafu?

Katika mwendo huu nani anaweza kusimama jukwaani akaambia wananchi wapambane na rushwa?

Kwa mwendo huu, wizi wa rasilimali, na ufisadi utakomeshwaje?


Tunaendelea kujiuliza kwanini sisini masikini.

Hata sisi wenyewe hatujui kwanini ni masikini ingawa tunajua namna ya kusaidia wale wanaotaka '' kuondokana na umasikini'.

Hatujui kwanini sisi ni masikini!!!!
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…