Duru za siasa - Matukio

Mkuu Nguruvi3

Iran tayari wamepata rais mpya...unadhani msimamo wao kuhusu Syria utabadilika chini ya uongozi mpya?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3Iran tayari wamepata rais mpya...unadhani msimamo wao kuhusu Syria utabadilika chini ya uongozi mpya?
Mwalimu, hili swali lako linahitaji kamjadala kidogo na naomba univumilie kidogo kama sitakwenda kwenye jibu moja kwa moja.

Uchaguzi wa Rouhani kuwa Rais wa Iran umempa ushindi wa kishindo.
Upigaji kura ulifikia asilimia 75-80 huku vijana na wairan waishio nje ya nchi wakimpigia kura mwanamageuzi Rouhani(Reformist).Hamasa kubwa ni kutaka reformist huyo aiondoe nchi katika mtafaruku na dunia jambo linalowaumiza wananchi.

Ushindi wa Rouhani ni dhidi ya wagombea wengine walioungwa mkono na revolutionary guard ambayo ipo chini ya Grand Ayatollah Khamenei.

Ayatollah ni wadhifa na si jina na huyu ndiye aliyemrithi Ayatollah Rohollah Khomeini aliyeleta mapinduzi ya kumuondoa Shah. Ayatollah Khamenei ndiye supreme leader na sheria na mambo yanayohusu katiba aghalab lazima yapate baraka zake.

Rais mtule Rouhani pamoja na njia zote za kidemokrasia bado atahitaji kuthibitishwa na Ayatollah ingawa uwezekano wa kumkataa haupo.

Rouhani anaungwa mkono na aliyekuwa Rais wa Iran Khatami (1997-2005) wote wakiwa ni reformist na liberal ambao wanaamini katika concilliation kuliko confrontaion.
Rouhani ni mwanachama wa green movement ambayo imepewa majina kama 'path' kuepuka mambo ya kisheria.Anajulikana kama Diplomat Sheikh au Sheikh of hope.

Tatizo linaanza kuwa Ayatollah Khemenei yeye si mliberali kama walivyo Khatami na Rouhani.
Ayatollah ni mtu wa revolutonary guard na mrithi wa Khomeni na amewahi kuwa Imam wa Iran, rais na waziri. Kwahiyo anafahamu nguvu zote za kisiasa.

Tukumbuke kuwa Iran ni waislam wa madhehebu ya Shia kwa wingi.
Syria ya Al Asaad ina uhusiano mwembamba na Ushia hata hivyo mahusiano ya Syria na Iran ni ya muda mrefu.

Katika vita vya ghuba wakati nchi za kiarabu zikiitenga Iran, Syria iliunga mkono hata pale chama cha Baathy kilichokuwepo Iraq kilikuwepo Syria ya Hafid Al Asaad baba yake Bashir Al Asaad

Uhusiano wao mwingine ni kuhusu misimamo yao dhidi ya Marekani na Israel.
Wote wanamkakati wa pamoja wa kuipinga Marekani na Israel.

Hata Ayatollah Khameneni ameshwahi kukaririwa akisema penye movement ya kuupinga udhalimu wa Marekani na Israel, Iran itaunga mkono.

Jambo jingine linalowaunganisha ni Hezbollah, kwamba Syria ni njia nzuri ya kupitishia silaha za kwenda kwa Imam Hossein Nasrallah wa Hezboullah dhidi ya Israel.

Hata mpambano wa Hezboullah na Israel ambao Israel alikuwa 'loser' silaha na mikakati ya kijeshi iliwafikia kutoka Iran kupitia Syria.

Kitua kilichostua ni kuhusu Iran kukata misaada kwa Hamas.
Hamas ilikuwa inapokea pound milioni 15 kwa mwezi kutoka Iran.
Hamas wanaunga mkono waasi wa Syria jambo lililowaudhi Wairan na kukata misaada

Hapa naomba niweke sawa, Hamas siyo Shia ni Sunni lakini katika spirit ya Islamic movement, Hamas imeungwa mkono na Iran na Syria. Kiongozi wa Hamas Khali Meshal anaishi Damascus na misaada inatoka Tehran

Equation inakuwa complicated kwasababu kuna element za Hamas kupendela kuwa na watu radical ili wawasaidie katika mpamano na Israel.

Hamas wanaona kama Syria ya Al Saad ni lege lege hasa baada ya kukaa kimya kuhusu Golan height.Wakati huo huo Iman Nasrallah wa Hezboullah ni shia na Ismail Haniya wa Hamas ni sunni.

Iran kama sponsor inajikuta njia panda.
Kwanza kuwasaidia Hezboullah na kwahiyo kuisadia Syria.

Wakati huo huo kuisaidia Hamas ambayo inataka Al Asaad aondoke, na pia kuisadia Hezhboulla inayomuunga mkono Syria.

Wakati huo huo beneficiary wa misaada ya Iran, Hezboullah na Hamas hawaivi kwa mitazamo na upinzani wa kiimani.Unaona palivyo pagumu hapo!!

Kwamintaarafu hiyo rais Rouhani ataingia ofisini akiwa na kibarua kigumu.
Kwanza kuwaridhisha wapiga kura wake kuwa yeye ni reformist na anataka kuirudisha Iran katika utengamano wa dunia.

Rouhan kasema anataka kuondoa mivutano na kushirikiana na dunia kwa kupunguza tension.
Hapa ni kukaa meza moja na western countries!!

Hapo hapo Rouhani anatakiwa alinde masilahi ya revoulationary guard ya Grand Ayatollah Khamenei ambayo ipo chini ya mwenye unasaba mkubwa sana na kiongozi wa awali kabisa shia enzi za Mtume Muhamad(Puh)

Ni kwa mtazamo huo tunasema kuwa ni mapema mno kutabiri au kubashiri mwelekeo wa siasa za mashariki ya kati hata baada ya uchaguzi wa Iran.

Rouhan ni mtu wa siasa za kati na kati (centrist) na mwanamageuzi reformist) ,hata kama anajenda mkononi, je ataweza kuitimiza?

Ugumu ni pale siasa za mashariki ya kati zinapofungamana na dini.
Kwamba kuna nyakati Rouhani itabidi aangalie masilahi ya Shia na Uislam, wakati huo huo akitaka kuiridhisha dunia kwa mambo yanayokinzana na misimamo ya kidini.

Hivyo, Mwalimu, ni ngumu kwakweli kutoa mwelekeo inabidi apewe miezi 3 na hapo ndipo dunia itajua mwelekeo wa Iran na siasa za mashariki ya kati.

Nchi za magharibi zimepokea ushindi wake kwa tahadhari'cautious optimism' kwa kuangalia hali niliyojaribu kuielezea.

Sijui kama nimekidhi japo kidogo kuhusu maoni yako!
 
MLIPUKO WA BOMU ARUSHA NA YATOKANAYO

Sehemu ya kwanza

Wiki hii Watanzania watatu wamepoteza maisha na wengine kubaki majeruhi kufuatia mlipuko wa bomu katika mkutano wa kisiasa Arusha. Tunatoa pole kwa wafiwa na kuwatakia majeruhi wapate afueni ya maumivu na wapone haraka.

Ni tukio la pili la shambulio la Bomu kama lile lililotokea katika kanisa la Olisati hapo hapo Arusha.
Kwa watanzania mambo kama haya ni mageni na hakuna aliyedhani mikusanyiko inaweza kugeuga kuwa uwanja wa vita

Duru tumeshajadili suala hili huko nyuma, kwa mazingira yaliyopo inabidi tulijadili kwasababu njia tunayoelekea si njematu. Kumekuwa na mauaji yasiyoweza kulezeka, matukio yasiyo na majibu na upotoshaji usiojulikana malengo yake ni nini.

Kwa tukio hili la Arusha kuna nadharia zinazozunguka miongoni mwa jamii (Theory).
Tuziangale nadharia hizo na misingi ya hoja zake

1.
(i)Kwamba ni njama za CCM kuvuruga uchaguzi il urudiwe kwa kuelewa kuwa utakatisha wananchi tamaa ya kupiga kura
Msingi wa hoja: Mwaka 1990 uchaguzi ulivurugwa makusudi na uliporudiwa CCM walishinda

(ii)Kujenga hofu miongoni mwa wanachama na wananchi wasijitokeze katika mikutano ya upinzani
Msingi wa hoja:Kujenga hofu ni pamoja a kutumia vyombo vya dola kulipua mabomu hata mahali pasipo na vurugu.

(ii)Kuwaaminisha wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa wapinzani Tanzania ni watu wenye vurugu
Msingi wa hoja :Hata pale Polisi walipokiuka taratibu bado serikali imesimama nao na kushindwa kuwawajibisha wahusika

(iv)Jaribio la kutaka kuwaua viongozi baada ya mbinu za kiusalama kugonga mwamba katika majaribio yaliyopita
Msingi wa hoja: Kwasababu bomu lilielekezwa huko walipokuwa viongozi

2. Nadharia(theory) kuwa Chadema walifanya uhalifu kwa minajili ya kupata kura za huruma.
Msingi wa hoja: Kwamba imeshawahi kutumika kwingine duniani.
Udhaifu wa hoja: Hakuna kiongozi ambaye angeratibu mauaji yake ili ashinde uchaguzi wa vitongoji au kata siku ijayo.

3. Kuna watu wa mataifa hasa jirani wenye ushindani wa kiuchumi wenye kutaka kuvuruga amani ili kuogopesha wawekezaji au watalii kwa kile kinachoonekana kuwa tanzania ni ''politically stable''
Msingi wa hoja: machafuko nchi za jirani yameathiri shughuli za utalii na hivyo Arusha inakuwa target
Msingi wa pili wa hoja hii ni kuwa kuna njama za kuwafakanisha Watanzania. Baada ya jaribio la kanisani kushindwa sasa wanatumia vyama mahasimu vya kisiasa.

Hoja kubwa ya nadharia hii ni kuonyesha kuwa kuna watu wawe wa ndani au nje wanatumia weak point kutaka kuleta machafuko. Sehemu hizo ambazo ni "vulnerable" ni dini ambayo imeleta tension hivi karibu.
Sasa pengine wanajaribu siasa ambayo kama dini nayo ina tension kwa wakati huu.

Uwepo wa nadharia hizo ziwe za kweli au uongo unatokana na mambo yafutayo;
(a)Uongozi dhaifu:
(i)Serikali imeshaonywa kwa vigezo vyote kuwepo kwa uhalifu unaotishia amani ya nchi na hakuna hatua zilizochukuliwa
(ii)Kushindwa kuwawajibisha wenye dhama kwa kushindwa kusimamia amani ya nchi kama Mawaziri na wakuu wa vyombo vya usalama kama Polisi na usalama wataifa
(iii)Kuwakejeli wananchi kwa kuwapa vyeo wale waliosimamia uhalifu au uvunjajiwa sheria na haki za binadamu

(b) Wananchi kupoteza imani na vyombo vya dola
(i)Kunakotokana na kujishirikisha katika siasa, kutoa kauli za kisiasa badala ya utaalam
(ii)Kutumika kisiasa kwa malengo ya wanasiasa

(d)Kuwa na viongozi wanaojadili matumbo yao na wala si taifa la Tanzania
(i)Wasioangalia tatizo kwa undani bali kwa macho na masikio ya kisiasa
(ii)Kutoacha itikadi zao za kisiasa na kujadili mstakabali wa kisiasa

Nini kimetokea Arusha na maswali yatokanayo

Inaendelea
 
Sehemu ya pili

Katika mkutano pale Arusha kulikuwa na walinzi wa usalama.
1. Askari wenye mavazi
2. Askari wa upelelezi (Askari kanzu)

Maana ya kutoa taarifa za mkutano wa kisiasa ni ili kupewa ulinzi na usalama.
Walinzi a usalama si wasikilizaji wa mikutano ya kisiasa. Jukumu la kwanza lilikuwa kuhakikisha kuwa eneo lote linakuwa salama ikiwa ni pamoja na kuangalia vichaka, wabeba vitu visivyoaminika na makundi yenye mijadala inayolenga kuvuruga amani.Bomu limerushwa nyuma ya gari la matangazo karibu na viongozi wa Chadema.
Uslaama wa taifa na askari walikuwa wapi? Hivi hawakujua kuwa katika uhalifu jukwaa kuu ni target?

Hoja ya kuwa askari walizuiliwa na wananchi kumkamata mhalifu ni ya kipuuzi, kitoto na kijinga sana kutolewa na chombo cha usalama achilia mbali kiongozi wa serikali.

Njama za uhalifu hufanywa na kikundi na si wananchi wote.
Haiwezekani iwepo njama iliyopangwa kwa uwanja mzima bila njama hiyo kujulikana.Ni mwedawzimu atakayekubali hilo.

Lakini pia kama Polisi wangejipanga wasingefikia mahali pa kuhitaji kumkimbiza mhalifiu huku wakiwa na silaha.
Wangetumia silaha hizo katika kumdhibiti hata kama kufanya hivyo kungesababisha kifo cha mhalifu.
Polisi wangekuwa na mahali pa kuanzia uchunguzi badala ya kufyatua mirasisi hovyo kwa raia na kumwacha mhalifu atokomee. Leo hakuna clue na inabaki kitendawili.

Pili, Polisi wanasema bomu ni kama lile la kichina lililotumika kanisani Olisait.
Wakati huo huo wanasema mtuhumiwa wa bomu la kanisani alikamatwa kwa msaada wa wanachi waliomkimbiza.
Leo umma unajua kuwa kuna mhalifu magereza anaisadia Polisi.
Je, polisi walitumia mbinu gani kumbana ili ataje chanzo cha upatikanaji wa mabomu hayo?

Mkuu wa jesh la Polisi anakimbilia kutoa namba za kupewa taarifa. Sababu ya kufanya hivyo ni kwa kutambua kuwa hakuna mwananchi atakayetoa taarifa kwa Chagonja anayehusishwa na matukio mabaya wala Kamuhanda au chombo ch dola. Kwa mwendo huo hakuna ushirikiano kati ya jamii na jeshi la Polisi.

Lakini mkuu wa jeshi la Polisi anatakiwa awabane watumishi walioko chini yake ili watimize wajibu.
Hakuna anayewajibika yanapotokea matukio kama haya na kinyume chake wahalifu wanapewa vyeo vya juu kama pongezi. Hivi leo nani atatoa taarifa ya uhalifu kwa IGP,Chagonja au mwingine awaye?

Na pia wananchi wanajiuliza kama Waziri Mwakyembe aliwahi kutaja wahalifu kwa majina na vyombo vyao vya uhalifu, kama mfanyabiashara Mengi aliwahi kutaja majina ya wahalifu muda na mkakati waliopanga na hakuna hatua zilizochukuliwa ni kwanini basi watoe taarifa kwa tukio kama hili na je itakuwa na maana yoyote?

Wananchi bado wanakumbu kumbu za sinema ya Kova ambayo ni uongo uliokithiri na ambao hadi leo hajaweza kulithibitishia taifa kwanini uhalifu ule wa Ulimboka ulifanyika.
Ni katika uhalifu huo Ulimboka alimtaja mtu ambaye leo bado yupo mitaani, sasa namba za simuni za nini na ni ili zisadie kitu gani?

Uhaifu hauishii katika mabomu tu, wananchi wanakumbu kumbu za uundwaji wa tume kuchunguza EPA ambapo mkuu wa Polisi alikuwa mjumbe. Tume hiyo haijulikani imeishia wapi.

Uhalifu kama wa mikataba ulioligharimu taifa mabilioni ya fedha hauna majibu kutoka katika vyombo vya usalama licha ya ushahidi usio na mashaka. Leo IGP anatoa namba za simu ni ili zisadie nini?

Tatizo liko wapi hasa katika vyombo vya usalama?

Inaendelea sehemu ya tatu
 
sehemu ya tatu

Wananchi wanaweweseka na viongozi wanatupiana lawama.
Hakuna ushahidi bali lawama na propaganda za kisiasa.Malumbano yamebaki kati ya Chadema na CCM.

Endapo kungekuwa na vyombo madhubuti vya ulinzi na usalama basi tungeweza kusema Chadema wanaingilia utendaji wa vyombo hivyo. Ni wazi kuwa hakuna ushahidi ambao CDM wataupeleka hata kama wanao ukabaki kama ulivyo.
Ni kwasababu hizo wao kutoa kauli ni sehemu ya kukataa tamaa na pengine hilo linawapa ``benefit of doubt"

CCM ndiyo yenye serikali na inapokuja na malalamiko kuwa tukio hilo limepangwa, si kuwa inatisha bali inasikitisha.
CCM inatakiwa iiagize serikali yake ifanyie kazi tuhuma zao na wala si kufanya kazi kwa njia ya taarifa za magazetini.
CCM ndiyo yenye serikali sasa kama wanalalamika bila ushahidi nani alisadie taifa hili?

Wananchi wameingia katika malumbano hayo ya kisiasa badala ya kuangalia suluhu ya kudumu.

Tatizo siyo mabomu kwasababu yametengenezwa kulipuka
Tatizo siyo mlipuaji kwasababu amedhamiria kufanya uhalifu

Tatizo letu kubwa ni Uongozi dhaifu ulioshindwa kulinda katiba ya nchi kama ilivyokuwa katika kiapo.
Rais aliapa mbele ya umma kuwalinda wananchi wa Tanzania, wao na mali zao.

Rais amekabidhiwa mamlaka ya vyombo vya usalama. Kushindwa kufanya kazi kwa vyombo hivyo ni kushindwa kwa serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi.

Kitendo cha usalama wa taifa kushindwa kubaini chanzo cha matatizo na kuyazuia ni dalili kuwa wakuu wa vyombo hivyo na hapa nasema Waziri wa Mambo ya ndani, IGP na TISS sasa hawawezi tena kusimamia ulinzi na usalama wa Watanzania na mali zao. Na ni dalili pia kuwa rais ameshindwa kutupatia watu watakaosimamia amani na usalama wa taifa

Wananchi hawapaswi kulumbana wakienda katika mazishi ya wapendwa wao. Wanatakiwa waache malumbano ya wanasiasa.

Kazi kubwa wanayotakiwa ni kumwambia mh Rais kuwa viongozi wake wameshindwa kazi.
Talaa Rais hatakubaliana na maoni yao basi wamtake yeye abebe dhamana.

Duru za siasa zinasisitiza kuwa hili si tatizo la chama cha kisiasa hili ni tatizo la Watanzania.
Tuweke tofauti zetu za kiitikadi kwa namna yoyote iwavyo tujinusuru na janga hili la taifa.
Hakuna njia ya makato ni kumtaka Rais awawajibishe wahusika au yeye abebe dhama yao.

Tusemezane
 
MAONI KUHUSU NADHARIA ZA MLIPUKO WA ARUSHA

Nashukuru msomaji wa duru (namhifadhi kama alivyoomba) kaniambia kuwa katika nadharia zote zinazodhaniwa kuwa huenda ndio chanzo cha mlipuko wa Arusha kuna moja ambayo watu wengi hatujaiangalia.

Nadharia hiyo ni kuwa, kwavile upinzani na hasa Chadema wamekuwa mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vya rushwa, kuna uwezekano kabisa ''wenye rushwa'' wanakereka kwani madili yao yanakwama.

Katika hilo wameamua kuwatisha wananchi kwa kutupa bomu (terriorize) na kwamba watu waogope kukiunga mkono chama hicho, alimalizia mchangiaji huo.

Msingi wa nadharia hii ni kuwa watuhumiwa wengi wa ufisadi, ulaji rushwa na wengine mikataba kukatizwa ni matokeo ya upinzani kunyanyua kelele(whistle blower).

Pengine wameamua kufanya hivyo kwa kuogopa kuwa chama hicho kadri kinavyozidi kupata nguvu ndivyo hali za masilahi na maisha yao kiuchumi yanavyokuwa matatani.

Kuna mtuhumiwa mkubwa sana wa ufisadi ambaye sasa amehamia nchi jirani.
Hata wengine waliobaki wapo huru na ‘wanaendelea na shughuli zao' pasi na shaka.

Je haiwezekani kukawa na mkono wa watu hawa kwa kushirikiana na vyombo vya dola?

Tunakumbuka mpango wa kumdhuru Mwakyembe ulihusisha wafanyabiashara maarufu sana waliokuwa katika sakata la Richmond na Dowan wakishirikiana na Polisi ambao walikuwa watumie zana za polisi kukamilisha azma yao.

Tunakumbuka mtego wa madawa ya kulevya wa Mengi ulisukwa na wafanyabiashara maarufu na ulikuwa utekelezwe na Polisi kwa sifa na zana za polisi.

Kwa mifano hiyo miwili, tunaweza kusema hata kama Polisi hawahusiki, bado kuna uwezekano wa polisi kutumiwa kama ilivyoelezwa hapo juu.

Hisia za watu zinakuwa kali kwa kujua kuwa yule mtu aliyemteka Dr Ulimboka na ambaye alitabuliwa kwa jina, cheo na kazi yake bado yupo na serikali haijui nani alifanya uhalifu!!!!!

Hizi bado ni nadhari na hazina ushahidi bali kupanua wigo wa kufikiri lakini huenda moja kati ya hizo ikawa na jibu kama kuna anyefikirisha akili yake katika serikali
 
mkuu nadharia ya mafisadi ipo CCM, kuhusika kwa fisadi yeyote katika mlipuko wa bomu ni kuhusika kwa CCM yote,
hakuna namna yeyote CCM watajinasua kwenye hili tukio.
 
Asante sana mkuu Nguruvi3 kwa kuendelea kutupatia mjadala wa matukio mbalimbali yanayotokea hapa duniani kupitia duru hili la siasa,,,,,,,,,,,,,ubarikiwe sana.
Kwa ishu hii ya bomu la Arusha, bado nipo gizani sielewi ni nini hasa majukumu ya serikali yanapotokea matukio ya mabomu kama haya. Matukio mawili ya mabomu ndani ya muda mfupi na hakuna taarifa yoyote yenye mashiko toka serikalini zaidi ya kauli za kisiasa tu. Ni kama hatuna serikali bali kundi la watu tu waliopo madarakani kwa maslahi yao.
 
Last edited by a moderator:
Katavi, jukumu la kulinda watu na mali zao ni la serikali. Ulinzi na usalama wa raia ni jukumu la serikali.
Matukio mawili yaliyohusisha mabomu si matukio madogo hata kidogo. Ni matukio ya kushtua na kusikitisha sana.
Serikali yoyote duniani lazima itafute chanzo cha tatizo, waliohusika na sababu za wao kufanya hivyo.

Tukio la shambulio la kanisani akiwemo mwakilishi wa papa kwa maana mwanadiplomasia, wakiwepo wakuu wa dini na raia lilikuwa ni zito sana. Lau paa la nyumba lingeanguka basi tungeweza kulipa uzito wa ajali. Hilo haikutokea kilichotokea ni urushaji wa bomu.

Kuna wananchi walimkimbiza mtu mmoja na kumkamata. Kuna watu walioshikiliwa wengine wakaachiwa na wengine bado wapo ndani. Hakuna anayejua sababu na nani hasa alihusika.
Kama isingekuwa busara za Watanzania basi nchi ingekuwa katika machafuko makubwa sana ya kidini.

Tukio la Arusha mkutanoni haliwezi kuchukuliwa kwa namna yoyote ile isipokuwa ugaidi. Matukio mawili yamechukua roho za raia zaidi ya saba kwa masikitiko makubwa. Matukio haya ni ya kigaidi na yanahusisha ugaidi kwa maana ya kutisha watu.

Ugaidi maana yake ni kutisha watu wasifanye jambo au wasifuate taratibu zao za maisha. Kwamba kwenda katika mikutano au makanisani ni tishio. Hilo ndilo mlipuaji alikusudia.

Kinachoshangaza badala ya viongozi wa serikali kuliangalia kama tatizo la usalama wa taifa, wao wanalichulkulia katika mizani ya kisiasa. Tumesikia hata waziri mkuu akiamuru wanaokaidi amri wapigwe. Tumesikia waziri husika akisema kuna sheria zinaruhusu polisi kuua na wala si kulinda, kukamata na kuchunguza chanzo cha tatizo.

Hebu tujiulize, hivi mtoto wa miaka mitatu ana uwezo gani wa kukaidi amri? Hivi ni mtu gani anayeweza kukaidi amri tu kwasababu ameamua pasipo na sabab? Kama yupo mtu huyo kwanini apigwe na asipelekwe hospitali za vichaa?

Kwa nchi za wenzetu mhalifu analindwa ili awe chanzo cha taarifa na uchunguzi. Meja Hassan Nadal aliyeua askari kule Marekani pamoja na kushambuliwa alitibiwa kwa gharama zote ili apone kama ilivyo kwa yule kijana wa Boston, mlipuaji aliyevaa chupi na yule aliyeweka bomu katika viatu. Nivyo ilivyo kwa aliyejaribu kulipua uwanja kule Ireland,magaidi wa UK na kwingineko.

Utawala wa sheria unasema mtu hana hatia hadi pale atakapothibitishwa kuwa anayo. Wakati huo atabaki kama raia na hata akitiwa hatiani anabaki na haki zake za kibindamu. Kuagiza Polisi wapige ni kinyume cha utawala wa sheria na haki za binadamu. Ni kulichochoea jeshi llifanye uhalifu kwa vile tu eti lina haki hiyo ambayo haijaandikwa popote katika katiba ya nchi.

Tumesikia wanasiasa bungeni wakitoa tuhuma za kisiasa. Badala ya Polisi kushirikiana na wahusika hao kutafuta ukweli polisi na serikali zimejikita katika kuficha ukweli kwa kuleta mambo yasiyo na maana. Haiwezekani kesi ya CDM igunga ikawa ya kutisha kuliko Sheikh aliyemwagiwa Tindikali, Padre aliyeuawa, Ulimboka, Mengi, Mwakyembe na marehemu Mwangosi.

Kesi zote hizo zina ushahidi wa kuaminika lakini serikali kwa sababu inazozijua imeamua kufufua kesi za Igunga. Je, kesi ya Igunga ni nzito sana kuliko ile ya kuchinjwa mwanachama wa CDM Marehem Mbwambo kule Tengeru? Tena wahusika walikamatwa na kukimbia wakiwa mahakamani. Si watuhumiwa au Polisi waliochukuliwa hatua.

Ni kwa kuangalia mwenendo huo wananchi wana kila sababu ya kuamini kuwa zipo sababu ambazo serikali inazijua na haitaki kuzifanyia kazi. Hapo ndipo shuku na kunyoshewa kidole kunapokuja na sidhani kama kuna mtu anaweza kukataa

Tatizo linaloonekana hapa ni udhaifu wa vyombo vya usalama ambao umejificha katika mwamvuli tusioujua. Kuna kitu kinaendelea ambacho ni cha hatari sana. Mwenendo huu unaonekana kuwa ndio sehemu ya maisha yetu.

Labda ujiulize, hivi tuhuma za kesi ya Kileo kule Igunga ni nzito kuliko zile za Mwakyembe aliyetaja wahusika kwa majina na vyombo walivyokusudia kumdhuru?

Ni nzito kuliko zile za Mwangosi? Ni nzito kuliko zile za Mengi alizotaja hata askari wahusika ambao badala ya kuchukuliwa hatua walipandishwa vyeo.

Kuna tatizo kubwa sana katika uongozi wa taifa hili. Tatizo hilo litazaa matatizo mengine makubwa siku za usoni.
Serikali inapanda mbegu, pindi zikichanua ni ngumu kuizng'oa.

Inapalilia dhana mbaya na imeondoa imani kwa wananchi. Serikali inawekwa na wananchi, wananchi wakikosa imani na serikali yao, wakiishi kwa hofu na wakishindwa kushiriki shughuli zao, serikali inakuwa imepoteza mamlaka yake.

 
Polisi wameshindwa kusimama katika nafasi yao pia wameshindwa kusimamia wajibu wao kwa nchi na raia wake. Sasa hivi hata lile kauli mbiu yao ua "Usalama wa Raia" haina maana tena bora waibadili kuwa ni "Usalama wa Watawala"
 
MAKWAIA WA KUHENGA AIONGLEA NADHARIA YA TATU

Katika bandiko#203 kipengele cha tatu tumeongelea nadharia ya ugaidi wa Arusha kuwa huenda kuna watu wasioitakia mema nchi hii na hivyo kutumia udhaifu uliopo kupenyeza ajenda zao.

Tumeongelea kuwa tukio la Kanisani na la kwenye mkutano yanafafana kwa kiasi fulani.
Pengine Bomu la kanisani lililenga katika kuleta vurugu kati ya waumini wa dini hapa nchini na hivyo kuitumbukiza nchi katika machafuko.

Watanzania kwa weledi wao waliliangalia tukio hilo kwa mshangao, kitu kilichosadia sana katika kutuliza hasira na kuleta utangamano. Ni weledi tu ndio uliepusha balaa na tunawashukuru sana Watanzania wa imani zote kwa weledi huo wa hali ya juu

Liliposhindikana likatumika la kisiasa ili kuleta mvurugano kwa kuelewa kuwa kati ya CCM na Chadema kuna upinzani mkubwa. Siku zote adui hukushambulia katika eneo dhaifu na hapa ndipo udhaifu wetu ulipo.

Nadharia ya tatu imewahi kuongelewa na Manyerere Jackton hapa JF. Nilipotofautiana na Manyerere ni pale ambapo nimemuuliza kuhusu matukio ya nyuma na kwanini tudhani ni adui wa nje na wala si wa ndani. Matukio ya nyuma hayana maelezo!

Mfano, mauaji ya Mwangosi yalisemwa na jeshi la polisi eti ni matokeo ya mtu kurusha kitu kilicholipuka na kumuua mwangosi.

Picha zinaonyesha kuwa kama ingalikuwa kweli basi askari zaidi ya wanne waliokuwa wamemzunguka marehemu wangekufa kwanza kabla ya Mwangosi.
Ushahidi ulipotoka jeshi la polisi likabaki na aibu na dhalili kubwa sana.

Tukio la Ulimboka eti ni Mkenya alifanya unyama ule.
Hadi leo hakuna ushahidi na jeshi limeshindwa kuendesha kesi yake.
Akatokea askofu na kuliumbua jeshi mchana kweupe!

Tukio la Mwanyembe na Mengi hayana majibu na wala aliyehojiwa achilia mbali kufikishwa mbele ya sheria.

Kwa mtitiriko huo hata kama kuna adui wa nje ni ngumu sana kumuona kwasababu mwenye dhamana ya kuchunguza yeye mwenyewe anapaswa kuchunguzwa.

Leo katika gazeti la Daily news(kwa hisani) mwandishi Makwaia wa Kuhenga ameiangalia nadharia namba tatu kwa jicho kama letu na kwa kutoka angle tofauti http://www.dailynews.co.tz/index.ph...a-bombings-are-they-a-foreign-instigated-plot

Ni kwa msingi huo tunazidi kuonya kuwa hili si suala la kisiasa la mkaidi 'piga'.
Hili si suala la akina Mwigulu Nchemba au Nape na siasa majitaka katika maisha ya wanadamu

Ulinzi na usalama wa taifa ni jambo nyeti linalohitaji nguvu za pamoja, utulivu na fikra.
Kitendo cha wanasiasa kukimbilia kuligeuza ilimradi kukidhi haja za matumbo yao ni cha kulaaniwa, kupuuzwa na kudharauliwa na mtu mwenye akili timamu.

Kwa upande wa jeshi, kwavile linajua kuwa limepoteza maadili (ethics), uaminifu(trust) na uadilifu(moral), hoja yao si kuwatisha akina Chadema walete mkanda.

Jeshi lilitakiwa liwasikilize kuhusu hoja zao za kuundwa tume huru ya kimahakma ili jeshi lijue tatizo liko wapi na pengine lijisafishe kutokana na tuhuma zinazolikabili.

Kinyume chake tumeona jitihada za kuwatumia watu kama mwanasheria mkuu kubadili mwelekeo wa hoja, kukimbilia kuwakamata akina Kilewo kana kwamba hao ndio tatizo na wala si tatizo la ulipuaji wa kanisa au mkutano.

Na kwa upande wa chadema, nao wanawajibu wa kufikisha mkanda wanaodai wanao pindi tume hiyo itakapoundwa.

Kama haitaundwa basi ni vema wakatumia nguvu za kisheria kwa namna nyingine na kuuweka ushahidi huo hadharani.

Hii maana yake ni kuwa itatusaidia kujua kuwa katika nadharia zilizoelezwa ipi inakuwa na mashiko.

Hili ni tatizo la taifa na hakuna anayepaswa kuifanyia mzaha hata kidogo.

Kesho atatumbukizwa nguruwe msikitini, watu wataanza kuumana kumbe anayefanya hivyo anajua udhaifu wetu na wa vyombo vyetu vya usalama.Anayefanya hivyo pengine anataka tuvurugane ili watalii wakimbilie nyumbani kwake.

Na msomaji jaribu kufikiria kidogo kuhusu mkutano wa viongozi wa EAC watatu tu waliokuja na mkakati wa kiuchumi kule Kampala. Fikiria ushindani wa kibiashara kuhusu utalii.

Tunapaswa kusugua vichwa vyetu na si kutoa majibu mepesi kama ya Nchemba, Nape,Lukuvi n.k.

Tusemezane
 
SNOWDEN NA SAKATA LA UVUJISHAJI WA SIRI ZA MAREKANI

Katika bandiko#199 tulielezea sakata la Snowden wakati huo alikuwa Hong Kong ambayo ni sehemu ya china.
Hong Kong ina watu milioni 7 ikiwa ni kituo kikubwa mojawapo cha uchumi duniani(financial centre). Hong Kong inaitwa 'East meet west'

Watu wa Hong Hong ni wachina kwa tamaduni. Kwasababu za ukoloni nchi hiyo imekuwa na tamaduni za magharibi.
Hong Kong inafuta sheria za mkoloni mwingereza ambaye alikirudisha kisiwa hicho kwa China mwaka 1997.

Hong inajitawala isipokuwa kwa mambo ya nje na ulinzi na usalama.
Snowden aliamua kuondoka kwasababu kubwa mbili. Kwanza kuna ushirikiano wa kurudisha wahalifu (extradition)na Marekani na pili China ina uhusiano wa kibiashara na Marekani, isingependelea kuingia katika mzozo wa kidiplomasia(Diplomatic row)

Tayari Marekani ilishafuta passport ya Snowden na sheria zinasema kuwa passport inapofutwa(revoked) mhusika anarudishwa alikotoka. Hii ni tofauti na kumfutia uraia. Kufutwa kwa passport hakuondolei mtu uraia.

Haijulikani ni kwa vipi aliweza kusafiri na watumishi wa WikiLeaks ya Julian Assenge ambaye amejificha katika ubalozi wa Ecuador nchini Uingereza. Snowden alipofika Urusi habari zilisambaa haraka kwasababu tayari makachero wa Marekani walikuwa ndani ya ndege hiyo pamoja naye.

Swali ni kuwa makachero waliwezaje kufika kwa muda mfupi na mazingira hayo? Jibu ni kuwa Marekani ina makachero kila sehemu ya dunia hii. Balozi zao siyo sehemu za wastaafu kwenda kupunzika, ni balozi za kiuchumi, kisiasa, kiulinzi na utamaduni.

Urusi imekiri kuwa yupo katika uwanja wa ndege na si Urusi (technically)kwa maana ya eneo la on transit ili kuunganisha ndege.
Hilo linawasaidia kuwa hayupo katika mamlaka yao ingawa ukweli ni kuwa China na Urusi zinamatamani ili zipate undani wa habari za ulinzi za Marekani.

Njia ya kwanza ya Snowden ilisemwa kwenda Iceland. Pili kwenda Ecuador au Cuba. Cuba na Iceland zinaonekana kujiweka mbali na sakata linalomhusisha mbabe Marekani. Sehemu iliyobaki ni Ecuador. Maafisa wa Ecuador kama walivyompa Assenge hifadhi ubalozini wapo bize kumtafutia hati za uhamiaji kama mkimbizi.

Kutokana na kusua sua kwa Urusi na China kwa interest zao, Ecuador imesema haiwezi kumpa ukimbizi (hifadhi au Asylum)hadi atakapokuwa katika ubalozi au nchini Ecuador. Hii ni kushinikiza Urusi iharakishe kumruhusu aendelee na safari yake.

Kwa upande mwingine taratibu za usafiri zinalamisha njia za anga kupitia karibu na Marekani na uwezekano wa ndege za kijeshi kuilazimisha ndege iliyomo Snowden kutua Marekani ni mkubwa. Kwa kupitia nchi nyingine, nyingi hazipendi kuingia katika mzozo.
Ndio maana Obama alikuwa kimya na amevunja ukimya huo juzi akiwa Senegal pengine kwa kujua mission imeshtukiwa

Snowden ana siri nyingi,nzito na Marekani ina muhitaji sana. Inamtaka kwa tuhuma za ushushu(espionage) katika kesi ya uhalifu(felony).

Ecuador ina watu milioni 15 na uchumi unaotegemea mafuta. Inayoungana na Venezuela na Cuba katika kutunisha misuli.
Kiuchumi hawategemei mataifa ya magharibi zaidi ya wao wa Latin America.
Ni kanchi kanakowatesa sana Wamarekani kwa siasa zake za ''kikaidi'' na huko ndiko Snowden anapotegemea kuelekea.

Safari yake ina vikwazo ambavyo siyo vya kusafiri bali vya kidiplomasia. Nchi za China na Urusi zingependa kumfanya Snowden kama ngazi ya majadiliano. Kuna wahalifu wa China wapo Marekani kama walivyo wa Urusi.
Snowden anatumika kwa sasa kama ''bargaining' ya dili kati ya mataifa makubwa.

Baba yake Snowden ameiandikia idara ya sheria akieleza kuhusu dili ya mwanawe kurudi kwa hairi lakini asifunguliwe mashtaka. Kwamba ni kweli ana makosa lakini hajafanya usaliti kwa wananchi wa Marekani.

Kwa uzito wa tuhuma zake hata kama hilo litatokea CIA haitamuacha na hakika yupo katika wakati mgumu sana wa maisha.

Tusemezane
 
KIKAO CHA BAADHI YA VIONGOZI WA EAC

Sehemu ya kwanza

Wiki hii viongozi wa Keanya, Uganda na Rwanda walikutana mjini Kampala. Nchi za jumuiya zinaundwa na Tanzania na Burundi ambazo hazikuwa na wawakilishi. Kwa taratibu kama ungekuwepo udhuru nchi hizo zingetuma wawakilishi.

Kikao hicho kimekuja wakati kukiwa na mzozo wa kidiplomasia(Diplomatic row) kufuatia kauli ya Rais Kikwete kuzitaka nchi za Rwanda, Uganda na Kongo kuzungumza na waasi ili kupata amani ya kudumu katika eneo la maziwa makuu.

Kauli ya Rais Kikwete ilikuwa ni hoja na ushauri kama ambavyo Tanzania imekuwa inafanya karika eneo hili.
Tanzania imeshiriki kuzileta pamoja pande zilizokuwa zinasigishana kule Angola, muafaka kati ya Mugabe na Nkomo, maongezi ya Frelimo na wapinzani.

Siku za karibuni Tanzania iliwaleta pamoja Raila na Odinga na kupatikana muafaka wa kudumu uliozaa Kenya anayotawala Uhuru Kenyatta sasa hivi.

Na ni Tanzania hiyo hiyo iliyosimama Kidete kuhakikisha kuwa Uhuru Kenyatta anapewa fursa ya kugombea licha ya kesi inayomkabili kule the Hague.Tunakumbuka safari za Uhuru kila wiki mjini Dar es Salaam

Tanzania inasimamia maelewano kati ya wapinzani wa Madagscar, Kongo na kwingineko.
Katika jukumu hilo Tanzania inakuwa mshauri na wala si mwelekezaji ikijua hatima ya nchi ipo katika nchi husika.

Inashangaza kuona rais Kagame akitoa kauli zisizo za kidiplomasia. Kagame alikuwa na hiari ya kukubali au kukataa na wala si kutoa matusi hovyo. Tunajua kuwa hata Kongo na Uganda pengine hawakupendezwa lakini afadhali wao basi wamejaribu kutumia diplomasia katika suala hilo.

Kuna uwezekano kuwa kulikuwa na hali ya sintofahamu ndani ya EAC lakini kuibuka kwa suala hili ndiko kumechochea kikao hicho kwa mtindo wa ''knee jerk reaction'' ikilenga kuiadhibu Tanzania kama ni sahihi kusema hilo.

Maafikiano yaliyofikiwa na viongozi hao watatu ni pamoja na kuwa na vitambulisho vya pamoja, matumizi ya bandari na ujenzi wa reli. Hadi sasa Kenya ina uhusiano na Rwanda wa soko huru la ajira ambao hauhusishi nchi zingine.

Historia ya EAC imejengwa katika nchi 3 ambazo ni Kenya, Uganda na Tanzania.
Rwanda na Burundi ziliomba kujiunga jambo lililoleta upinzani sana. Wengi walikuwa wanaitilia shaka Rwanda ya Kagame kuwa chanzo cha matatizo jambo linaloonekana dhahiri kwa sasa.

Kwa mantiki hiyo kikao hicho hakiwezi kuwa cha EAC bali cha nchi washirika katika mahusiano binafsi.
Rais Museveni anasema EAC si krismas ya mara moja kwa mwaka na kwamba viongozi wanaweza kukutana wakati wowote kama alivyokaririwa na BBC, lakini ukweli unabaki kuwa nchi wanachama zinapaswa kualikwa hata kama hazitahudhuria.

Kuna maswali yanayojitokeza kuhusiana na kikao hicho ambayo tutayajadili
1. Kikao hicho kimelenga nini
2. Je, kuna mafanikio mbele ya safari ya nchi hizo
3. Je, ni mkakati sustainable au umeongozwa na hasira
4. Je, jumuiya ipo imara kama ilivyokuwa siku za nyuma au ndio mwanzo wa mwisho
5. Tanzania ifanye nini na kwanini katika mazingira hayo

Itaendelea......
 
Sehemu ya pili...... inaendelea

Turejee kidogo kuiangalia EAC iliyokufa mwaka 1977. Kenya, Uganda na Tanzania zilikuwa na misimamo tofauti ya kisiasa za ndani na nje. Kwa mfano,Tanzania ikiunga mkono vyama vya ukombozi kusini mwa AfriKa Kenya ilikuwa ikiunga mkono Makaburu na siasa za ubepari tofauti na ujamaa wa Tanzania, Uganda ya Amin ikiwa ipo ipo tu.

Kilichoua EAC ya 1967 siyo tofauti za kisiasa bali ni ubinafsi wa Kenya iliyoamini kuwa uchumi wake ulikuwa mkubwa na hivyo kuzibeba nchi nyingine na ilikuwa bora kwenda 'solo'

Jumuiya ilipovunjika Kenya iliyokuwa na manufacturing industries nyingi ilibaki kuwa na nguvu kiuchumi.
Tanzania na Uganda zilijikuta zikianza upya kujenga mataifa yao kwa kile kilichokuwa hakihamishiki kilichobaki

Mwaka mmoja baadaye nchi hizi mbili zikajikuta katika vita jambo lililozidi kudhoofisha sana uchumi.
Kenya ikabaki kuwa na uchumi wenye nguvu ikivutia wawekezaji kutokana na siasa zake za kimagharibi.

Hali ilibaidilika katika miaka ya 90 na kukawa na ulazima wa kutafuta masoko. Kenya ikapungua nguvu kwa kuwa nje ya sehemu kubwa ya Afrika mashariki na kati. Kenya ikatambua umuhimu wa kufufua tena jumuiya kwa kutambua kuwa soko lake kubwa lipo nje ya nchi hiyo na Tanzania na Uganda zikiwa karibu sana.

Nguvu kubwa ilisukumwa na kuinuka kwa uchumi wa Uganda na Tanzania na hivyo kuleta upinzani.
Ili kwenda n wakati Kenya ikakubali tena kuwa sehemu ya EAC na hapo ndipo EAC ya sasa ilipoibuka

Baada ya rais Mwinyi/Moi/Mkapa kuondoka madarakani huo ukawa mwanya wa Museveni kuwa kaka mkuu wa jumuiya.Museveni alitaka shirikisho liharakishwe ili awe rais wa EA wa kwanza jambo lililoleta malumbano na mzozo

Ili kupata nguvu Museveni akashauri Rwanda na Burundi ziwe ndani ya jumuiya.
Hii maana yake ilikuwa kutaka kuungwa mkono katika agenda zake ndani ya EAC.
Kenya inakubali si kwasababu za kisiasa bali za kiuchumi.

Hata kabla azma ya Museveni na shirikisho la kisiasa haijafikiriwa ugomvi ulizuka kati ya Kenya na Uganda kuhusu kisiwa cha Migingo ambacho ni sq km 1. Kenya wakang'oa reli na kutishia kuingia vitani.

Mzozo huo ulimalizwa kwa spirit ya EAC, ndio maana leo tunashangaa vipi Kagame aje juu kwa Tanzania kisa kuambiwa azungumze na wapinzani.

Huko nyuma Kagame alikuwa na ugomvi na Museveni licha ya kuwa Kagame ni mtoto wa Museveni kisiasa.

Kulikuwa na shutuma za nchi zote kuunga mkono waasi wa nchi nyingine. Kwa sasa uwepo wa south sudan unaisaidia Uganda kutulia.Ni kwa msingi huo Kagame anaona njia rahisi ni kuwa na urafiki na Museveni ili naye awe salama.

Mahali watu hawa walipo na common interest ni Congo (DRC) ambako wote wamejikita kwa mwamvuli wa kupambana na wapinzani lakini ukweli ni kuwa wanashughuli za kiuchumi zaidi kwa kuzingatia kuparaganyika kwa DRC

Tanzania imekubali kupeleka majeshi kule DRC kupitia mamlak aya UN. Kwa maneno mengine majeshi ya washirika wa UN ikiwemo Tanzania yanakwenda kupambana na majeshi ya Rwanda na Uganda ndani ya nchi nyingine. Na hapa ndipo ilipogusa interest za Kagame na Museveni na wao kuamua kumshirikisha Kenya ili kutoa "adhabu"

Na hilo hasa ndilo kiini cha mkutano wa Kampala. Kenya inajikuta ikiingia kati kati kwasababu za kiuchumi. Uganda na Rwanda zinaweza kuisaidia sana kiuchumi kwa kutambua jiografia ya nchi hizo.

Hata hivyo Kenya inacheza karata zake kwa umakini na uangalifu sana kwasababu kiuchumi mshirika na mpinzani wake mkubwa ni Tanzania na wala si Rwanda

Karata kubwa zaidi kwa Kenya ni kushirikiana na Uganda na Rwanda ili kuweka shinikizo kwa Tanzania kukubaliana na matakwa ya washirika hao ndani ya EAC ambayo yataifaidisha kenya kiuchumi zaidi.

Hadi hapa swali la kwanza bandiko#213limejadiliwa.(kutoa adhabu na kuishinikiza Tanzania)

Tuendelee na yaliyobaki........
 
Sehemu ya tatu......inaendelea

Katika mkutano wa Kampala maazimio ni kujenga miundo mbinu, kuwa na visa ya pamoja na kuharakisha(fast track) shirikisho la EAC.

Kujenga miundo mbinu baina ya washirika wa jumuiya si jambo baya, hata Tanzania ikna mpango wa kuunganisha reli ya kati na nchi za Burundi na Rwanda. Kuna makubaliano ya ushirikiano wa nishati kati ya Kenya na Uganda hata miundo mbinu kati ya nchi hizo.

Kitu kibaya kinachotokana na azimio la Kampala ni kutamka kuwa wanataka kujenga reli ili kuacha kuitumia bandari ya Dar es Slaam. Kwa nchi zinazojenga ushirikiano hiyo si kauli ya kidiplomasia na ililenga kupeleka ujumbe Tanzania kuwa wao Uganda na Rwanda wanaacha kuitumia bandari ya Dar kama sehemu ya `adhabu`kutokana na kauli za JK.

Kenya ndiyo itakayofaidika na mpango huo kama utafanikiwa na kuna kila sababu za kuamini kuwa mafanikio yatakuwa kidogo. Kwa mfano,Watanzania wanatumia bandari ya Mombasa kwasababu imekuwa efficient kuliko ya Dar kwa uharaka wa utoaji mizigo, malipo kidogo ukilinganisha na kwa usalama wa mizigo yao.

Hata kama watafanikiwa kuacha kutumia bandari ya Dar hilo litakuwa jambo la muda kwasababu nguvu ya soko haitawaaliwi na serikali bali uchumi. Mfano, utamalazimishaje mfanyabiashara kutumia bandari ya Mombasa kama ya Dar itakuwa efficeint na cost effective.

Na kwa mkakati wa Kampala, wao wanataka soko lao na kusahau kuwa watahitaji soko la Afrika mashariki na kati ambalo Tanzania inapakana nalo kwa nchi 8. Kwa maneno mengine upo wakati miundo mbinu yao itawatosheleza lakini bado watahitaji kuungana na nchi za Tanzania na Burundi walizoziacha ili kuwa na maana ya kiuchumi waliyoikusudia.

Kuhusu single visa: Hili nalo litakuwa tatizo hasa kwa mgawanyo wa mapato. Visa zinazotegemewa ni za watalii ambao destination zao ni Kenya na Tanzania kwa asilimia zaidi ya 80. Kenya, Uganda na Rwanda zikiwa na na single visa msumari utapiga upande wa Kenya ambayo inachangia sana sehemu na Tanzania katika utalii.

Kwa namna yoyote Kenya lazima itatafuta muafaka na Tanzania ili kuboresha soko lake la utalii na hapo italazimika kuwaacha washirika wake wa Kampala. Kenya ingefadika zaidi kwa kuwa na single visa entry na Tanzania kuliko Rwanda

Kwavile uwepo wa Kenya mjini Kampala ulizingatia uchumi zaidi ya siasa, na kwasababu sehemu kubwa ya uchumi wa Kenya kiutalii na kibidhaa inategemea Tanzania kuliko Rwanda na Uganda combine, mbele ya safari lazima kutakuwa na kuachana kwa washirika wa Kampala.

Kuhusu shirikisho la Kisiasa: Hili ndilo hasa linaonekana kichekesho. Kenya inasiasa zinazofungamana sana na Ukabila.Nirahisi sana kwa Waluo kuunga mkono Waganda kuliko Wakikuyu.

Uganda inasiasa tofauti hasa kwa kuzingatia ufalme unaojengwa na Museveni.
Imeripotiwa kuwa mtoto wa Museveni ndiye mrithi mtarajiwa wa kiti.
Hili lita complicate sana siasa na uchumi wakati wa mabadiliko hasa wakati Kagame naye atakapoondoka

Rwanda na Kagame wanasisa za mtutu na sijui ni kwa vipi wanaweza kuwa meza moja na washirika wengine.

Lakini kikubwa sana ni kuwa ushirikiano ni zao la uchumi. Siasa za sikuhizi ni za kiuchumi zaidi kuliko kuhasimiana.

Hivi inawezekanaje kujenga shirikisho bila kuwa na misingi imara ya uchumi. Je, washirika wa Kamapala wamefikiria kuhusu mambo ya mapato, fedha, benki kuu, tofauti za uchumi n.k.

EAC ya 1967 ilikufa kwasababu ya kujengwa katika misingi ya kisiasa zaidi ya uchumi.
Nguvu ya uchumi ilipoelemea sehemu moja ndicho kikawa chanzo cha anguko la kisiasa.
Haoionekani kama akina Uhuru, Museveni na Kagame wamezingatia hilo.

Hapa ndipo tunajibu swali la 2 na la 3 bandiko# 213 kuwa mkakati utakuwa na mafanikio ya muda mfupi sana na umejengwa si kwa sustainable policy bali hasira za kidiplomasia.

Tutaendelea na swali 4 na 5

Itaendelea.....
 
asante sana mkuu,
tunaomba kusikia lolote kuhusu ujio wa rais Obama hapa Afrika na hasa Tanzania, na zaidi sababu za Obama kukutana na Bush hapa Bongo.
 
Misri kumechafuka tena, wananchi hawamtaki rais Morsi. Kuna mkono wa mataifa ya nje yasiyopenda siasa za hawa brotherhood au ni jeshi ndio linataka kurudisha utawala chini yake. Muda utatoa jibu ni nini itakuwa hatma ya utawala wa Morsi. Nguruvi3 tuendelee na habari za akina Museveni na Kagame na hatma ya EAC...
 
Last edited by a moderator:
Tunafuatilia kwa ukaribu sana ziara ya Obama na hali ilivyo Tahariri square ambapo jeshi limetoa ultimatum ya 48 hrs kufikiwa muafaka. Jeshi limesema 'matakwa' ya wananchi yatimizwe.
Tunamalizia sehemu ya EAC, tuendelee na matuio mengine. Ahsanteni
 
EAC Sehemu ya nne

Jumuiya iliyokubaliwa wkati ikizinduliwa upya na Rais Mwinyi/Moi/Museveni ililenga katika uchumi zaidi kuliko siasa.Ililenga kuwashirikisha wananchi kuamua aina ya ushirikiano, faida zinazowagusa kwa hatua kuepuka yaliyotokea mwaka 1967

Wanasiasa wanatakiwa wasimamie yale wananchi yaliyoamuliwa na wa taalamu kwa kubwa tatu za Kenya, Uganda na Tanzania kabla ya kuwashirikisha wengine.

Hatua za awali zilikuwa kutengeneza miundo mbinu ya pamoja kama barabara za Arusha hadi Nairobi na kule Bukoba. Hatua iliyofuata ilikuwa kuimarisha soko la pamoja la ushuru, mitaji na rasilimali watu.
Kuna maeneo yalifikiwa vema.

Halafu ilikuwa kuruhusu watu na mitaji kuhama eneo moja hadi lingine kwa raia EA kusafiri kutoka nchi moja hadi bila tatizo wakiwa na mitaji yao

Tatizo linalojitokeza ni nchi nyingine kutaka kuharakisha mambo kwa manufaa yao.
Kwa mfano ushuru wa forodha na bidhaa ni vyanzo vya mapato vya nchi hizi.
Bila kuwa na mipango ya uwiano wa kibiashara kunakoitwa trade balance kutatokea tatizo

Tatizo la uhamishaji wa mitaji linaambatanishwa na ardhi kama sehemu ya soko huru.
Ukiacha Tanzania nchi zilizobaki zina tatizo kubwa la ardhi.
Tatizo hilo inaonekana linatafutiwa ufumbuzi kwa kupitia Tanzania

Hata kabla ya kuimarisha mambo kama bandari, benki kuu, ushuru, elimu na hata afya nchi nyingine zinaishinikiza Tanzania kufanya ardhi liwe suala la pamoja.
Kwanini ardhi na si elimu, bandari au ushuru wa forodha?

Wakati wakishinikiza hayo wao walikuwa wanagombana kuhusu KM 1 ya ardhi kule Migingo.

Tanzania pia ina tatizo la umiliki wa ardhi na migogoro itoikanayo. Kitendo cha kuingia kichwa kichwa kwa shinikizo la EA ni kuhatarisha usalama wa nchi

Ni vema serikali iliona hilo na kusema wale wenye kuamua kushirikiana na waendelee kwa upande wao. Hadi sasa hakuna ushirikiano wowote kuhusu suala la ardhi kati ya mataifa yaliyokuwa yanashinikiza!!!

Mkutano wa Kampala haugusia suala hilo, lakini wakikaa na Tanzania suala hilo linajitokeza kwasababu kwao ni muhimu.Nchi za wenzetu wameshatoa ardhi na kilichobaki ni kutuletea matatizo ambayo yapo katika nchi zao

Kwa mantiki hiyo ile dhima ya kuwa na EAC iliyojengeka katika misingi ya uchumi imepotea. Tunaona sasa ni matakwa ya kisiasa, kwamba Kagame kachukia jambo basi maamuzi anayafanya ya wana wa Afrika mashiriki.

Tunaanza kuona kutoaminiana tena kwa kufanya mambo katika mtindo wa siasa badala ya utalaam na uchumi.

Mkutano wa Kampala si wa kiutaalam ni wa kisiasa ili kujibu hoja za Kikwete.
Je, hicho ndicho wananchi wanakitaka?

Maagizo yao wakuu waliokaa kampala yatafanyiwa kazi kisiasa na wala siyo kitaalam na mbele ya safari kuna kukwama kwa hali ya juu sana.

Tanzania haitakiwa ku-panic ikifahamu kuwa nayo ni sehemu muhimu sana ya jumuiya. Inatakiwa kulinda masilahi ya nchi na wananchi wake kwanza kama wanavyofanya wengine.

Haitakiwi ikubali kuburuzwa katika mambo yasiyo na tija kwa taifa.
Tanzania inatakiwwa ichukue hatua na baadhi kama:

1. Kuhakikisha kuna political stabiity kwasababu hilo ni muhimu sana kwa wawekezaji.Tanzania ifahamu kuwa kwa mchango wake katika stability ya eneo la maziwa makuu ni jicho la
wawekezaji na wale wanaoliangalia eneo hilo hilo litawalazimu na kuwaghatimu Kampala summit

2. Kuwekeza katika miundo mbinu kwasababu kwa kupakana na nchi 8 bado itakuwa ni 'hub'.
Miundo mbinu kama barabara, bandari na reli ni muhimu sana.
Nguvu ya soko ndiyo itakayoamua uelekeo wa uchumi wa EAC na si mikutano ya siasa.

3. Kuimarisha ulinzi hasa intelligence. Majirani wanaweza kutumia mbinu za kutuvuruga ili kukidhi haja yao ya instability kwa eneo lote na hata kiuchumi. Mathalani, Kenya ipo mbele kuzuia mipango mingi ya Tanzania hasa ya utalii!! ushindani huu ni wa kuangalia.

5. Kuwekeza katika elimu tiukifahamu kuwa hiyo ndio silaha muhimu sana kukabiliana na dunia ya ushindani

6. Kuhusu wanachama wa EAC wanaotaka kuendelea na michakato mbali mbali kufanya hivyo. Hata EU si kila mwanachama anakubaliana na kila jambo.

Wapo waliokataa Euro kama waingereza na wapo waliokataa Shengen visa kwa kuzingatia hali za kiulinzi, usalama na utamaduni.

7. Tanzania ihakikishe kuwa taratibu za kuanzisha EAC zinagutawa na wala si vurugu za Kagame. Ihakikishe Kagame anadhibitiwa kikamilifu ili kuzuia siasa zake za chuki, ubabe na ujuaji ambazo zilipekea nchi katika mauaji ya Kimbari akiwa mshiriki.

Tusemezane



 
ZIARA YA OBAMA AFRIKA

Kipindi cha kwanza cha uongozi wake, Rais Obama hakutaka kuonekana tofauti na marais wengine kwa kuanza safari za Afrika. Matatizo ya uchumi na usalama wa dunia vilimzonga na safari ya Afrika ingeleta maswali kuliko majibu.

Ziara yake ya kwanza ilikuwa Egypt kuongea na ulimwengu wa Kiarabu ambao ni tishio kwa usalama wa USA

Kipindi cha pili amekianza kwa ziara ya Israel ili kuleta utangamano na B.Nyetanyah ambaye ni mkaidi wa maagizo ya US kuhusu mabadiliko mashariki ya kati.

Obama pamoja na kulipa fadhila za Jews waliomuunga sana mkono katika kampeni aliamua kwenda kumpasha B.Nyah kuwa hali ya dunia imebadili na Israel inaendelewa kutengwa.

Safari ya pili ni ya Afrika. Safari hii ni kwa sababu za kiusalama na kiuchumi zaidi kuliko mahusiano ya kawaida.

Katika nchi alizotembea ni South Africa tu ambayo uchumi wake unaweza kugusa uchumi wa Marekani (significant).

Senegal na Tanzania uchumi wake ni mdogo hata kuliko baadhi ya states za Marekani.
Kwanini basi azitembelee?

South Africa ni mwanachama wa BRICS(Brazil, Russia,India, China and South Africa) ambazo ni chumi zinazokua kwa kasi sana dunia hivyo mahusiano na Marekani ni muhimu sana.

Lakini pia kuna wawekezaji wa Marekani nchi Africa kusini na hivyo kuna US interest hasa za kiuchumi. Na kwa ukubwa wa uchumi wa S.Africa ni wazi ina influency kubwa kwa mataifa ya Afrika

Senegal ni nchi masikini, kijiografia imepakana na Mauritania (kaskazini) Mali-mashariki na Guinea kusini bila kusahau .Lakini pia Sengal haipo mbali sana na nchi kama Nigeria au Algeria.

Ziara ya Obama ni kuandaa sehemu muhimu za vituo vya usalama vya Marekani kwa kuangalia hali nchini Mali,Nigeria, Mauritania n.k. Senegal inaonekana kuwa at least politically stable

Senegali ni strategic position kufikia maeneo yanayojulikana kama Magreb region (eneo la magharibi)ambako kuna vikundi vya kigaidi kama 'Alqaeda in Magreb region''.

Obama ameahidi misaada mingi kwa Senegal kwa mwamvuli wa young democracy.
Rais wa Senegal ameahidi kufupisha muda wa urais kutoka miaka 7 hadi 5, pengine kumfurahisha Obama bila kujua lengo la ziara kwa uhalisia

Marekani inataka kutoa misaada ili wana usalama wa nchi hiyo wapate kituo cha kuangalia 'Magreb region' ambako extremists sasa wanatokea kwa ukaribu zaidi

Inaendelea....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…