Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwalimu, hili swali lako linahitaji kamjadala kidogo na naomba univumilie kidogo kama sitakwenda kwenye jibu moja kwa moja.Mkuu Nguruvi3Iran tayari wamepata rais mpya...unadhani msimamo wao kuhusu Syria utabadilika chini ya uongozi mpya?
Katavi, jukumu la kulinda watu na mali zao ni la serikali. Ulinzi na usalama wa raia ni jukumu la serikali.Asante sana mkuu Nguruvi3 kwa kuendelea kutupatia mjadala wa matukio mbalimbali yanayotokea hapa duniani kupitia duru hili la siasa,,,,,,,,,,,,,ubarikiwe sana.
Kwa ishu hii ya bomu la Arusha, bado nipo gizani sielewi ni nini hasa majukumu ya serikali yanapotokea matukio ya mabomu kama haya. Matukio mawili ya mabomu ndani ya muda mfupi na hakuna taarifa yoyote yenye mashiko toka serikalini zaidi ya kauli za kisiasa tu. Ni kama hatuna serikali bali kundi la watu tu waliopo madarakani kwa maslahi yao.
Tunafuatilia kwa ukaribu sana ziara ya Obama na hali ilivyo Tahariri square ambapo jeshi limetoa ultimatum ya 48 hrs kufikiwa muafaka. Jeshi limesema 'matakwa' ya wananchi yatimizwe.asante sana mkuu,
tunaomba kusikia lolote kuhusu ujio wa rais Obama hapa Afrika na hasa Tanzania, na zaidi sababu za Obama kukutana na Bush hapa Bongo.Misri kumechafuka tena, wananchi hawamtaki rais Morsi. Kuna mkono wa mataifa ya nje yasiyopenda siasa za hawa brotherhood au ni jeshi ndio linataka kurudisha utawala chini yake. Muda utatoa jibu ni nini itakuwa hatma ya utawala wa Morsi. Nguruvi3 tuendelee na habari za akina Museveni na Kagame na hatma ya EAC...