Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Kwa hiyo hoja yangu baso ipo palepale, Uzalendo kwa viongozi na wananchi umepotea na hili linatugharimu sana iwe kwa Viongozi, Madaktari, walimu na hata mitaani kwa sababu hatuwandaa watu ktk misingi ya kibiashara. Kutoka Ujamaa kuingia Ubepari ni sawa na mtu alokwenda kuhbadilisha dini kutoka Uislaam kuingia Ukristu au kinyume lazima atakuwa na tafisri mbovu za faradhi za sunna za imani aloingia. Kwa hiyo nitaenbdelea kupinga mfumo huu wa Afya nchini na pengine nitasema Madkatri ni victims wa mfumo huu uloanzishwa na Mwinyi na Lowassa in 1992 and we are paying for that. the one

Nianze kuomba samahani kwa kuwa sijapitia thread zote, ila nitachangia kwa kutoa uzoefu wangu.

Ninachokiona ni viongozi kujaribu kukidhi matakwa ya kisiasa kwenye uendeshwaji wa serikali kitaalam. Ukidodosa kabla ya 1967 civil service chini ya Central establishment hapakuwepo tofauti ya mishahara kwa misingi ya taalum badala yake kigezo kilikuwa ni "qualifications and experience". Promotions zilikuwa scheduled. Lakini kilichokuwa wazi wakati huo lazima ukidhi na kujipambanua kwa ufanisi.

1972 nchi yetu ilikumbwa na ombwe la Mwongozo (Ambao in a nutshell uliondoa Technical Management based on evidence and delivery) ambao ulijenga dharau kwa baadhi ya taaluma. Lakini wakati huo huo ukasimika chama kushika hatamu na maamuzi ya kichama yaliyojitenga na utendaji wa kitaalamu (professional) pamoja na maamuzi yenye misingi ya mantiki kwa ajili kujikidhi uwezo duni na mdogo wa washika hatamu. (Mlinzi getini ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama alikuwa na madaraka ya kuamua hatma ya taasisi zaidi ya Meneja (nimebana ieleweke ni mfano wa kweli). Maana yake hapo ilipandwa mbegu ya kuanza kubagua na kutoheshimu taaluma.

Kilichofuatia ni kusomeshwa na kulipwa kulingana masomo yako. Nakumbuka vizuri mimi binafsi 1972 nilipata scholarship ya Jeshi kwenda Canada kuwa Fighter Pilot. Kulingana na mahitaji ya nchi kwa walimu wa hisabati, nilichuliwa na FFU toka uwanja wa ndege na kupelekwa UD nikasomee ualimu wa hisabati. Nilipomaliza walimu wa hesabu tulikuwa tunalipwa mshahara wa juu kuliko mtu ye yote (Tshs 1400 1974/5). Yaani hata Mkuu wa Mkoa hakutufikia. Mwanzo wa ubaguzi huo.

1977 ikazaliwa CCM ndani ya misingi ya kibaguzi ya taaluma. Akaingia mdudu anaitwa "Rare Profession" pamoja na Registration za Professional Cadres zilizojibainisha na kujipambanua kuwa ni Rare Profession. Hapo zikauondoa msingi wote wa utumishi serikalini. Kwa mfano nina ushahidi kuwa kwa sasa kuna kada zinapaa kwa promotions pamoja na ngazi za mishahara kwa sababu wao wanaaccess ya mafaili ya maamuzi kwa hiyo kwao ni lazima wawe juu. Hoja hapa ni kuwa when the center can not hold things fall apart.

Kwa hoja namantiki ya uzoefu nilioutoa ona yafutayo:-

1. Mind set ya utumishi imebadirika kuwa rare professionalism yaani ubora wa kimimi kwa fani yangu. Swali mind set hii inarandana vipi na utumishi wa umma? Jibuni wenyewe

2. Wanasiasa wamefanikiwa kuonekana wao ndio watumishi wa umma wasiolala kwa vile wanafanya maamuzi yanayohusu mstakabali wa nchi kwa hiyo they are rarest professional lazima walipwe tofauti na wengine na hasa kwa vile wao ni waamuzi wa mwisho Swali kibinadamu matumizi ya msingi yanatofautiana? Kwa nini tutofautiane kwa kigezo ambacho si kazi bali nani ana nafasi gani ya kuamua juu ya mwingine? Hii inajidhihirisha na maumbile ya kibinadamu kutaka haki na usawa.

3. Kama vilivyo viungo vya mwanadamu hakuna kisicho na umuhimu. Hata vidole pamoja na utofauti wake vinaheshimiana wakati wa utendaji. Serikali hufanya kazi kama mwili wa mwanadamu kila kiungo kina umuhimu wake na mchango wake. Si msomi wa biolojia ila najua mahitaji ya kila kiungo cha mwanadamu yanakidhiwa sawa sawa vinginevyo kiungo kitakachopungukiwa kitasababisha mwili kuuma. Hoja na swali hapa maana halisi ya utumishi bado ipo? Na kila mtumishi anaielewa sawa sawa na mwenzake? Na watumikiwa nao wanaonaje kinachoendelea? Ni wazi kunahitaji ku redifine utumishi wa umma (naomba nieleweke utumishi wa umma ni regardless na utumishi wa serikali kwa maana ya delivery ya service kwa public)

Changamoto

Mwalimu ambaye ni daktari, injinia na kiongozi kwa taaluma zote hizo adai mshahara kiasi gani? Na mwananchi uelewa wake wa huduma za kiumma (afya, elimu, usafiri, biashara/uchumi) azilinganishe na fani na kuzigharamia kifani.

Hitimisho

Kuna kujiona fani fulani ni bora kuliko nyingine. Hili limejengeka kwa historia ya utawala wa nchi yetu. Pia kuna maamuzi yanayofanywa kisiasa kwenye masuala ya kitaalamu k.m. kuendesha serikali kama serikali ni taaluma na kama taaluma haitofautiani sana duniani. Tulichokosea ni kufanya na kuruhusu maamuzi bila kuzingatia mahitaji ya kitaalamu ambayo hayatofautiani kwa serikali makini dunia nzima. Tusisahau mtoto umleavyo ndivyo akuavyo

KWA VILE WATAWALA WAMELIKOROGA LAZIMA WALINYWE HATA KAMA CHUNGU mKWA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU
 
Mimibaba,

Kusema kweli sijakuelewa ktk baadhi ya sehemu lakini pengine niseme tu ya kwamba nchi za wenzetu za Kibepari ukifanya kazi serikalini unalipwa mshahara mkubwa kuliko sekta binafsi. Yaani ukipata kazi serikalini umeula na kama serikali haiwezi ulipa mishahara hiyo kufanya contract na shirika au hata madaktari wenyewe huwa private working under contract..

Na sababu ukiitazama ni kwamba kila msomi nchi hizi amekopesha fedha ili kujisomesha au mzazi wake aliweka fungu la kumsomesha mwanaye hivyo at operating level ni all business.. Hata iwe nchi za kutoa huduma hizi bure huwa sii bure maana kodi ya kila mfanyakazi ni kubwa sana kiasin kwamba ina cover mahitaji mengi ktk sura za kibiashara...

Rudi kwetu sisi Ni watu wangapi wanalipa kodi haswa, sidhani kama tuna hesabu ya maana. Ni watu wangapi hawana kazi au ni kiasi gani cha kazi wakati wa JK zimezalishwa - hatujui. Nakumbuka wakati wa Nyerere akimaliza form six au chuo cha certificate unaenda Jeshini na kabla ya kumaliza tayari umeshapangiwa sehemu ya kazi au kwenda chuo kikuu. Tayari serikali hujiandaa kupokea vijana walomaliza shule kwa kuanda nafasi hizo sehemu husika wakati vijana hawa hawapotezi muda kusubiri..

Leo hii tunazalisha vijana kwa maelfu na hawajui kesho watakwenda wapi..Hivyo markst kubwa sii vijana wa kazi bali uhaba wa kazi yenyewe na ndio ina determine price maana kila mtu anaituta kazi..WE tend to work the otherway around - Kinyumenyume.

Halafu unaposema wakati wa Nyerere ndio tuliacha kuthamini professionalism, mkuu wangu sidhani isipokuwa sisi ndio hatukufahamu ya kwamba kuwa waziri wa Afya sio lazima uwe daktari maana hii ni nafasi ya leadership. Waziri ni sawa kabisa na CEO mtu anayejua kuongoza WATU ktk mazingira alopewa iwe biashara au utoaji huduma. Watu wanataka kuona waziri wa Afya awe daktari ndio hayo yale ya kina Nkya..wakati tuna MAT mbona zamani hatukuwa na matatizo kama haya ya leo wakati wa kina Sarungi?

Na Sikumbuki kama tulipishana sana mishahara maana nakumbuka enzi zetu sisi Ukimaliza Chuo Kikuu au IMF mshahara ulikuwa unaanzia Tsh 2020 na 2050 tofauti ilikuwa ndogo sana sema tu umuhimu wa mtumushi huyo ndio alipewa nyumba na pengine kupangiwa gari na dereva wa kumfuata kwenda kazini na kumrudisha nyumbani..Nakumbuka sana zile landrover za SLK au SU zikitupitia asubuhi kila siku wakati watu wakihangaika na UDA.

Amini maneno yangu mkuu wangu tulivurunda baada ya kungia Azimio la Zanzibar, pale chama CCM kilipowakabidhi wahuni mkuki na ngao ndipo tulipokwisha na kama unamkumbuka ndio Mwinyi alianza na shule za kulipia toka Prinmary school, mara hatujakaa sawa shule na mahopital yakawa ya kulipia..Hapo ndipo tulipokuwa at the lowest level hadi Mwalimu akaanza kupiga kelele, lakini it was too late. Tanzania imekwisha ingia ktika Ubepari tukiwa na zigo la maadui wetu Umaskini, Ujinga namaradhi mgongoni..Haya ya leo ni mavuno ya kile tulichopanda!
 
Wakuu Mkandara na JingalaFalsafa,
Mmenigusa sana na hoja zenu za UTU na KITU; kila kimoja kina sehemu yake katika jamii; tukianza na UTU ni ukweli usiopingika watanzania tumelelewa kwenye maadili ya UTU ni rahisi sana kwa huku ughaibuni kumtofautisha mtanzania na waafrika wa mataifa mengine, nikija kwenye KITU nacho kinasehemu yake kwenye jamii; swali la msingi tunachopaswa kujiuliza UTU na KITU ni kipi bora kwenye maisha ya mwanadamu? Kuporomoka kwa maadili ya UTU miongoni mwetu watanzania imechangiwa sana na UBINAFSI miongoni mwetu; ukianzia kwa wanasiasa, wafanyakazi na wafanyabiashara wote wapo mstari wa mbele kutafuta KITU kwa njia zote halali na zisizo halali; katika vita hii vita ya kutafuta KITU wathirika ni watanzania wa kawaida ambao wengi wao hawajui kesho wakiamka riziki wataipata wapi; Hivi ni kweli Tanzania tuna wanasiasa au matajiri wa kweli? Mwasiasa wa kweli ni yule anayepigania watu wake na tajiri wa kweli yule anayejitolea hali na mali; ipo mifano ya kina Bill Gate, Warren Buffet wanajitolea mabilioni kusaidia kupunguza umasikini Afrika, sisemi kuwa hao tunaowaita matajiri nao watoe kwa kiwango cha kina Bill Gate najua hawana uwezo huo; wanaweza kuchangia kwa kiasi chao; inafurahisha na kuchekesha sana kwa hao tunaowaita matajiri kwenda kwenye vituo vya mayatima kutoa gunia la mchele na kupiga picha lukuki kwenye magazeti, hiyo dhihaka kubwa wanachotafuta ni popularity tu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mimibaba,

Kusema kweli sijakuelewa ktk baadhi ya sehemu lakini pengine niseme tu ya kwamba nchi za wenzetu za Kibepari ukifanya kazi serikalini unalipwa mshahara mkubwa kuliko sekta binafsi. Yaani ukipata kazi serikalini umeula na kama serikali haiwezi ulipa mishahara hiyo kufanya contract na shirika au hata madaktari wenyewe huwa private working under contract..

Na sababu ukiitazama ni kwamba kila msomi nchi hizi amekopesha fedha ili kujisomesha au mzazi wake aliweka fungu la kumsomesha mwanaye hivyo at operating level ni all business.. Hata iwe nchi za kutoa huduma hizi bure huwa sii bure maana kodi ya kila mfanyakazi ni kubwa sana kiasin kwamba ina cover mahitaji mengi ktk sura za kibiashara...

Rudi kwetu sisi Ni watu wangapi wanalipa kodi haswa, sidhani kama tuna hesabu ya maana. Ni watu wangapi hawana kazi au ni kiasi gani cha kazi wakati wa JK zimezalishwa - hatujui. Nakumbuka wakati wa Nyerere akimaliza form six au chuo cha certificate unaenda Jeshini na kabla ya kumaliza tayari umeshapangiwa sehemu ya kazi au kwenda chuo kikuu. Tayari serikali hujiandaa kupokea vijana walomaliza shule kwa kuanda nafasi hizo sehemu husika wakati vijana hawa hawapotezi muda kusubiri..

Leo hii tunazalisha vijana kwa maelfu na hawajui kesho watakwenda wapi..Hivyo markst kubwa sii vijana wa kazi bali uhaba wa kazi yenyewe na ndio ina determine price maana kila mtu anaituta kazi..WE tend to work the otherway around - Kinyumenyume.

Halafu unaposema wakati wa Nyerere ndio tuliacha kuthamini professionalism, mkuu wangu sidhani isipokuwa sisi ndio hatukufahamu ya kwamba kuwa waziri wa Afya sio lazima uwe daktari maana hii ni nafasi ya leadership. Waziri ni sawa kabisa na CEO mtu anayejua kuongoza WATU ktk mazingira alopewa iwe biashara au utoaji huduma. Watu wanataka kuona waziri wa Afya awe daktari ndio hayo yale ya kina Nkya..wakati tuna MAT mbona zamani hatukuwa na matatizo kama haya ya leo wakati wa kina Sarungi?

Na Sikumbuki kama tulipishana sana mishahara maana nakumbuka enzi zetu sisi Ukimaliza Chuo Kikuu au IMF mshahara ulikuwa unaanzia Tsh 2020 na 2050 tofauti ilikuwa ndogo sana sema tu umuhimu wa mtumushi huyo ndio alipewa nyumba na pengine kupangiwa gari na dereva wa kumfuata kwenda kazini na kumrudisha nyumbani..Nakumbuka sana zile landrover za SLK au SU zikitupitia asubuhi kila siku wakati watu wakihangaika na UDA.

Amini maneno yangu mkuu wangu tulivurunda baada ya kungia Azimio la Zanzibar, pale chama CCM kilipowakabidhi wahuni mkuki na ngao ndipo tulipokwisha na kama unamkumbuka ndio Mwinyi alianza na shule za kulipia toka Prinmary school, mara hatujakaa sawa shule na mahopital yakawa ya kulipia..Hapo ndipo tulipokuwa at the lowest level hadi Mwalimu akaanza kupiga kelele, lakini it was too late. Tanzania imekwisha ingia ktika Ubepari tukiwa na zigo la maadui wetu Umaskini, Ujinga namaradhi mgongoni..Haya ya leo ni mavuno ya kile tulichopanda!

Ungenitaka nikueleweshe zaidi hayo maeneo ungenurahisishia. Hata hivyo nisifiche sura yangu ili isaidie kueleweka. Nashukuru Mungu nina elimu si haba na uzoefu wa utendaji wa umma wa miaka 40.

Historia

Enzi zetu 60s kulikuwa na tathmini endelevu ya maendeleo ya mwanafunzi kupitia SEL FORMS ambazo zilikuwa zinajazwa na walimu wenye taaluma siyo wa kuteuliwa. Hawa waliweza kumtambua mtoto (hasa wa sekondari) kuwa ana mwelekeo wa fani gani. Ndiyo maana mtu alikuwa anachaguliwa kwenda kidato cha tano kabla ya matokeo ya mtihani; na yalipotokea ambao hawakukidhi kwa kutopata matokeo mazuri walikuwa kama 0.01%. Nalieleza hili kwa sababu serikali ilikuwa haisiti kuwekeza kumwendeleza mtoto kwa sababu ya usahihi wa taarifa zake.

Kwa utaratibu huo baada ya kidato cha sita pia tulichaguliwa kujiunga na chuo kutokana na taarifa za uwezo wa awali kama zilivyokusanywa. Baadhi yetu hatukujua kuwa mwelekeo na uwezo wetu ni fani fulani (Mimi binafsi ualimu wa hisabati). Wizara husika na sekta hiyo ilikuwa na orodha ya wahusika kujiunga na fani hiyo. Kwa hiyo kama mimi (yatima) nilikuwa napata barua tu kuwa umechaguliwa kidato cha sita, chuo kikuu unaenda bomani kuchukua warrant na vitu vingine vinavyohusiana na masomo. Chuo kikuu tulikuwa na kitu kinaitwa Bursary. Mwalimu mwanafunzi aliyekuwa anasoma chuo kikuu alikuwa tayari ameajiliwa na Wizara ya elimu kwa kima na utaratibu wa serikali kwa barua yenye stahili zinazoambatana.

Hapo hapakuwa na issue ya mkopo ila mkataba wa utumishi wa miaka mitano. The catch ilikuwa baada ya miaka mitano kama ulikuwa mtendaji mzuri lazima utapanda ngazi kwa hiyo haikuwa rahisi kulalamika au kuitosa kazi yako.

Kwa mwalimu kama mimi naamini elimu ni kioo cha taifa ndiyo maana nimeeleza haya yote. Kama utanisoma nina maana tuangalie historia ya nchi yetu upande wa elimu. Ni kwa sababu serikali ni establishment inayoendeshwa kwa manpower inayozalishwa na sekta ya elimu. KWA SASA IMESAMBATAIKA HAKUNA PA KUSHIKA. Kwenye thread ya kwanza nilijaribu kueleza disparity za malipo kuwa zina hitoria gani na zimesababishaje mind set ya sasa ambayo inazaa migogoro. Hili pia ni zao la mfumo uliosambaratika wa elimu.

Tuje kwenye kusambaratika kwa uongozi wetu. Umejenga hoja kuhusisha Azimio la Zanzibar (Hiyo ni fact). Lakini kwangu mimi hili azimio halikukusudia uhai na dhamira ya taifa; bali manufaa ya watawala. Mifano ni mingi lakini moja kubwa ni kuruhusu viongozi wamiliki mali (kosa ni kuwa, wamiliki kwa namna gani kihalali au kiharamu azimio halikusema kitu). Ushahidi ni tofauti ya kujilimikizia mali tofauti na kunufaisha taifa. Viongozi wengi ni tabaka la juu la wenye nacho tofauti na wananchi. Hii imezaliza mawazo ya kunyoosheana vidole kuwa wanakula sehemu kubwa ya taifa siyo waadilifu. Kibaya zaidi hata maamuzi yao kwa dhamana tuliyowapa yanaelemea kivyao.

Upande mwingine je wananchi tumelifahamuje hili azimio la zanzibar? Kweli hakuna fursa yo yote kwetu? Majibu yangu wengi hatulifahamu kabisa kwa hiyo hatujui linatupa fursa gani. Ni donda sugu la kutojielimisha lililojengeka kutokana na mfumo wa elimu uliosambaratika. Kimaisha kama umebahatika kuvinjari duniani watu wanaoendelea hujikita kwenye kuwa informed; hapa kwetu kuna jitihada za kutowainform public kwa elimu iliyokengeuka (skewed). Ushahidi hata elimu ya katiba haipo kama sehemu ya maisha ya mtanzania mimi nikiwemo.

TULIVURUGA WAPI.

Naona umejitwisha jukumu zito sana kujiuliza tulipovuruga ambalo ni jambo jema. Ila pamoja na hilo umetaja uwezekano wa awamu husika katika kuvuruga. Ni sawa lakini na sisi tujiulize hatujachangia kwenye uvurugaji huo? Kama ndiyo tunajikomboaje? Na hapa ndipo penye kiini cha yote. Tumejisalimisha muda mrefu kwa watawala wetu bila sisi wenyewe kujishirikisha kwenye kujiamulia na kuchangia mstakabali wa maisha yetu kama wananchi wa nchi hii. We are to blame first. Vitabu vyote vya dini vinasisitiza kujielimisha; wengi wetu tumechukua role ya maamuma kwa hiyo imam akikupotoka ndiyo basi tena. Sisemi tuwe maimamu, ninachosema tutafune/tutafakari tunachoambiwa tusimeza tu, ndiyo tunameza shubiri sasa.

FURSA

Fursa ya kwanza ni sisi wenyewe kudefine mstakabali wetu. Hapo itatusaidia kutambua mahitaji yetu na kujipangia mahitaji yetu. Hapo tutawauliza (kwa maana hatukatazwi) watawala tuna makubaliano gani nao watatumia raslimali zipi na mkakati upi utakaopimika kwa matokeo yapi yenye viashiria vipi tulivyokubaliana. Haya yote yapo kwenye uwezo wetu. Labda nijisemee mimi kwenye masuala ya kitaifa siamini BLAME GAME. Naamini wote ni wadau wenye majukumu sawa na wajibu sawa. Tunatofautishwa na maeneo tu ya kutekelezea majukumu yetu bila kumtegemea mtu chini ya utaratibu wa mfumo imara wa uongozi.

Finger pointing si nzuri kwa sababu unajitenga na mchakato mzima.

Changamoto

Tumekengeuka katika uongozi na mstakabali wa nchi yetu. Migogoro imetukwama kooni, haturidhiki na hatua mbali mbali zinazochukuliwa na watawala kukabili hali hii. Ni kweli tumeingia kwenye matabaka ya kipato, ya fikra na zaidi tumeingia kwenye kulaumiana bila kujitambua. Je tumeainisha fursa tulizo nazo kukabili hali hii na changamoto hizi? Hapa mchakato ninaouamini ni ule unaoanzia na mimi, baadae sisi baadae nchi nzima.

Hitimisho

Tuheshimu historia ya nchi yetu kwani ina majibu ya kuainisha mwanzo wa matatizo yetu. Hapa mimi napendekeza tutafakari sana kusambaratika kwa mfumo wa elimu. Halafu tusimame kidete kutetea kwa busara yale yanayotugusa binafsi kwa sababu yako ndani ya uwezo wetu na tujenge uwezo wa kuwasilisha hoja zetu kwa data.

Uongozi umekuwa ombwe lakini kuna historia ambayo na sisi tumechangia. Hapa kuna msemo kuwa kwa uwezo ulionao unaweza kuleta maabadiko yanayolingana na uwezo wako. Yanapokuwa nje ya uwezo ulionao shirikiana/shikamana na wenzio wenye uwezo na nia kama yako kuleta mabadiriko hayo.

NIMEOGELEA TU LAKINI NAAMINI HISTORIA YA NCHI YETU KISIASA, KIUCHUMI, KIELIMU INA MAJIBU YA MENGI TUNAYOJIULIZA
 
Mkuu Mkandara;
Azimio la Zanzibar halikuhalalisha watu wawe wezi, hatari ya kubwa ya hiki kinachofanyika sasa hivi sio wizi ni transfer of wealth from the Government to public officials and their inner cronies; hata ukiangalia mikataba mingi iliyoingia serikali sio kweli kwamba hawajui ni nini walichosaini yale yalikuwa ni makusudi kwa nia moja tu wizi, mimi si mwanasheria lakini huitaji kuwa digrii ya sheria kujua nini kilichofanyika; haikuwa sera ya CCM hayo yafanyike bali tamaa na ubinafsi wa wahusika, Azimio la Zanzibar liliruhusu viongozi wamiliki nyumba na si vijiji vya mahekalu, liliruhusu viongozi kuwekeza lakini sio kwa njia za wizi. Sasa hivi watu wanaingalia sana CCM kutokana na matendo machafu ya viongozi wake; kimsingi tatizo hili lipo ndani ya vyama vyote; ukianzia Chadema viongozi kujipa tenda kwa njia ya mlango wa uani, ununuzi wa magari yaliyotumika kwa mil. 350,000,000, ukienda CUF jiulize kwa nini ni Lipumba na Maalim tu; ukienda UDP ni Cheyo na kampuni yake hali kadhalika TLP. Watanzania wanawajibika kuchagua viongozi wataosimamia maslahi yao, bado tunao viongozi waadilifu wenye nia ya kweli ya kuomboa mtanzania kwenye umaskini uliokithiri.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu Mkandara;
Azimio la Zanzibar halikuhalalisha watu wawe wezi, hatari ya kubwa ya hiki kinachofanyika sasa hivi sio wizi ni transfer of wealth from the Government to public officials and their inner cronies; hata ukiangalia mikataba mingi iliyoingia serikali sio kweli kwamba hawajui ni nini walichosaini yale yalikuwa ni makusudi kwa nia moja tu wizi, mimi si mwanasheria lakini huitaji kuwa digrii ya sheria kujua nini kilichofanyika; haikuwa sera ya CCM hayo yafanyike bali tamaa na ubinafsi wa wahusika, Azimio la Zanzibar liliruhusu viongozi wamiliki nyumba na si vijiji vya mahekalu, liliruhusu viongozi kuwekeza lakini sio kwa njia za wizi. Sasa hivi watu wanaingalia sana CCM kutokana na matendo machafu ya viongozi wake; kimsingi tatizo hili lipo ndani ya vyama vyote; ukianzia Chadema viongozi kujipa tenda kwa njia ya mlango wa uani, ununuzi wa magari yaliyotumika kwa mil. 350,000,000, ukienda CUF jiulize kwa nini ni Lipumba na Maalim tu; ukienda UDP ni Cheyo na kampuni yake hali kadhalika TLP. Watanzania wanawajibika kuchagua viongozi wataosimamia maslahi yao, bado tunao viongozi waadilifu wenye nia ya kweli ya kuomboa mtanzania kwenye umaskini uliokithiri.

Chama
Gongo la mboto DSM
Chama sijakuelewa hapa. Unaposema Azimio la Zanzibar halikuwa wizi wakati huo huo unasema ilikuwa transfer wealth kutoka government kwenda kwa hawa viongozi sii wizi wenyewe?. Mimi najua vizuri jinsi walivyjipangia Utajiri huu kugawana maana hawa wote walikuwa maskini kamamsisi sasa unapoingia Ubepari huna mtaji ingekuwa aibu kubwa kwao maana hawakuwa na kitu. Unapoondoa mamlaka ya uchumi mikononi mwao ni sawa na kuputa mkono uendao kinywani, hivyo they worked out a system ambayo itawapa wao mamlaka ya kuiba mali hizo na kuweka mikataba..

Haiwezekani kabisa mnapoanzisha vyama vingi na Ubepari bado maamuzi ya mikataba na manunuzi yabakie mikononi mwa viongozi badala ya bunge. Ni Azimio hilo lilowauzia nyumba, mashamba na hata kugawana nyumba za NHC na Msajili. Kuuziana viwanda na mashirika hata utajiri wa Bakhresa na wahindi matajiri kama Manji, Jeetu binafsi yangu nina mashaka nao sana kama hakuna ubia wa viongozi. Baada ya kuuza vitu vyote wakavunja commission na chombo cha kubinafsisha ili mafaili yake yapotee..

Hivyo nakubaliana na wewe sana tu ktk hili na naelewa wazi ni Azimio la Zanzibar lilotuondoa ktk Uzalendo, lilovunja miiko yote na maadili ya uongozi bora ikiwa kila mtu anatazama ataweza vipi kujinufaisha. Na ni katika wakati huo huo kina Lowassa wakajenga majina yao, wafanyabiashara wakubwa wakawa lobbiest wa CCM na wabunge wengine wakaingia wenyewe kupata nguvu hadi bungeni na serikalini. Chama cha Mapinduzi kimepoteza wanachama wake na sasa kimejaa mafisadi japokuwa ukiwauliza wao watasema mna wivu, chuki na fitna..
 
Mkuu wangu Chama:
WIZI NI NINI KWANI?
Hivi unatambua kuwa watanzania wote wanastahili kufaidika sawa kutokana na rasilimali zetu zilizopo? Yaani kama ni pato lipatikanalo kwa utalii ml. Kilimanjaro ligawanywe sawa kwa kila mtanzania, vile sawa kwa litokanalo na mbuga zetu, madini yetu, aridhi, maji yetu n.k. LINAFANYIKA HILO? Jibu liwazi kuwa, kama ilipasa kila mtanzania apate 10, basi yupo atakayepata 19 na mwingine akapata 1. JE, HUO SIO WIZI? Azimio la Zanzibar halikuhalalisha hilo?
Kwani hujui kwamba hatuwezi kumfungulia mashtaka Reginad Mengi kwa kuchukua na kuhodhi fungu la watanzania wa Tandale kutokana mgawanyo wa mapato yetu, kwanini asishtakiwe? Je, sio Mfumo uliohalalisha hilo? Je, sio wizi huo?
Au tunajifanya hatujui kuwa kuna watanzania wamejilimbikizia hisa za wenyewe wenye hisa hizo wanakufa njaa, magonjwa, hawana mavazi wala pakulala? Utajiri wa Mengi ungejenga Zahanati ngapi vijijini? Rostam naye? Lowasa na Manji je? Ndesamburo nae, Mbowe na Abood nao? Riz 1 na Sumaye je? Mnadhani utajiri wao una chanzo tofauti zaidi ya mito, aridhi, milima, watu, mbuga, misitu,n.k. ambavyo ni mali za watanzania wote? Au mnataka tafsiri ya neno "WIZI" iwe ile ya mzungu?
"HAKUNA UHALALI WA KUFICHA CHAKULA ULE KESHO, HALI JIRANI YAKO HAJALA SIKU YA PILI"
UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO.
Mungu wetu anaita sasa!
 
Mkuu wangu Chama:
WIZI NI NINI KWANI?
Hivi unatambua kuwa watanzania wote wanastahili kufaidika sawa kutokana na rasilimali zetu zilizopo? Yaani kama ni pato lipatikanalo kwa utalii ml. Kilimanjaro ligawanywe sawa kwa kila mtanzania, vile sawa kwa litokanalo na mbuga zetu, madini yetu, aridhi, maji yetu n.k. LINAFANYIKA HILO? Jibu liwazi kuwa, kama ilipasa kila mtanzania apate 10, basi yupo atakayepata 19 na mwingine akapata 1. JE, HUO SIO WIZI? Azimio la Zanzibar halikuhalalisha hilo?
Kwani hujui kwamba hatuwezi kumfungulia mashtaka Reginad Mengi kwa kuchukua na kuhodhi fungu la watanzania wa Tandale kutokana mgawanyo wa mapato yetu, kwanini asishtakiwe? Je, sio Mfumo uliohalalisha hilo? Je, sio wizi huo?
Au tunajifanya hatujui kuwa kuna watanzania wamejilimbikizia hisa za wenyewe wenye hisa hizo wanakufa njaa, magonjwa, hawana mavazi wala pakulala? Utajiri wa Mengi ungejenga Zahanati ngapi vijijini? Rostam naye? Lowasa na Manji je? Ndesamburo nae, Mbowe na Abood nao? Riz 1 na Sumaye je? Mnadhani utajiri wao una chanzo tofauti zaidi ya mito, aridhi, milima, watu, mbuga, misitu,n.k. ambavyo ni mali za watanzania wote? Au mnataka tafsiri ya neno "WIZI" iwe ile ya mzungu?
"HAKUNA UHALALI WA KUFICHA CHAKULA ULE KESHO, HALI JIRANI YAKO HAJALA SIKU YA PILI"
UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO.
Mungu wetu anaita sasa!
MKuu wangu katika falsafa hii kidogo tutatofautiana na mimi maana naamini kwamba kila mtu atalipwa kwa nguvu ya mazao atakayo panda. Zipo sekta ambazo ni za Kitaifa na zipo sekta binafsi ambazo zinakubalika ktk utajirisho. Ikiwa kuna tajiri ambaye kaanza na shilingi 10 kulima nyanya na kavuna nyanya 100 haya na mafao yake tofauti na yule anayelima mahindi na kavuna vile vile.. Kinachoweza kutokea ni hawa watu kuuziana kwa njia halali mwenye nyanya akamuuzia mkulima wa mahindi na mwingine na mwingienkila mmoja wetu kutumia pato lake kununua huduma au mali za mwenzake.
Nisichokubali mimi ni pale mtu anapoingia shambani kwako akachukua shamba kwa sababu linazalisha akidai yeye ndiye kiongozi na ana haki ya kumiliki shammba alitakalo. Yale ya Zimbabwe wazungu asilimia 10 kumiliki asilimia 70 ya ardhi wakati wenyeji asilimia 90 wanamiliki asilimia 30.

Kama watu wote watapewa nafasi sawa ya kumiliki na nafasi sawa ya kujiendeleza bila shaka watatokea walio bora zaidi ya wengine. kama Shule hatuwezi kuwazawadia watoto wote nafasi za kuendelea na masomo hata kama wanashindwa lakini tunawapa nafasi sawa wanafunzi wote wapate kushinda mtihani..

KLwa hiyo bninafsi yangu sina karaha na utajiri wa mtu alowekeza ktk biashara mabyo mimi siiwezi wala haikuwa chaguo langu la pia watu wote hatukuumbwa sawa maana ukipendacho wewe sii lazima nikipende mimi na utajiri uutakao sii lazima nami niwe kama wewe..

Muhimu ni kuwepo uwanja huru na sawa kwa watu wote kuweza kujinufaisha na nguvu waliyoiweka ktk kupanda, kupalilia na kuvuna mapato yao uwekezaji wao. Hatuwezi kuendeleza fikra za Kikumunist maana hazifanyi kazi. hakuna usawa wa binadamu ktk malengo na maisha isipokuwa tuna mahitaji ya huduma sawa, haki, sawa, uhuru sawa na kadhalika maadam uwanja na tambarare. Tunachopigana nacho ni Ukoloni, ukoloni mamboleo, Ubeberu na unyonyaji..Nje ya hapo ruksa kila mtu kutajirika maadam wote tunapewa nafasi sawa ya kujiendeleza.

I hate to say that napinga sana mawazo ya kuwapa nafasi sawa hata wageni ambao sio wazawa na raia wa Tanzania. Hii inatokana na historia ya kukoloniwa maana walikuja kutuibia kiuchumi na sii kutawala mipaka na watu wake hizi zilikuwa enzi za Utumwa wakati watu ndio biashara ya nguvu kazi Ulaya na Amerika. Fikra hizi za kutawaliwa kiuchumi bado zipo kichwani hivyo kumruhusu fisi ktk zizi la ndama kwa fikra za kwamba anakuja kulinda kusema kweli hali linanipa shida sana kulielewa. lakini pia hatuwezi kumkubali paka shume au mbwa koko kwa sababu tu ni mnayama wa nyumbani..

Kama mgeni anataka kuwekeza nchini lazima awe raia au ana residence permit na account zake zipo nchini, kinyume cha pale ataingia ktk mkataba ambao masharti ya ndani ktk Ubia na wananchi yatatumika.
 
Mkuu Mkandara:
Hiki unapaswa kukijua! Nilishasema huko juu kuwa...
1. Ubepari=pigania kunyonya kwa namna yoyote.
2. Ubepari upo wa namna mbili.
(a) Ule wa taifa kunyonya taifa(nauita External Capitalism)
(b) Ni ule wa mzawa kumnyonya mzawa( Internal Capitalism)
Mkuu wangu:
1. Kipi kinakufanya uamini kwamba watanzania tuliachwa kwenye tambarale kushindania mkate km.1 mbele? Hivi hujui kwamba kuna watu Shule na Hospitali wamekuja kuzijua miaka hii na wapo waliozijua kabla ya ukoloni, na wapo ambao hawataijua leo wala kesho? Kipindi anahangaika na malaria eti anambiwa ashindanie mbio na yule ambaye yuko "mentally and phisically fit" je ni Fair Competetion hiyo, kweli inaingia akilini? Tambarale gani unalosema tuliachwa humo? Au kwa vile wakubwa wametuambia hivyo basi nasi tuamini tu?
Ni UBINAFSI UBINAFSI KILA KONA!
2. Unadai unachojali wote tupate huduma sawa. Unadhani wodi anayolazwa tajiri ni sawa na ile nayolazwa mimi? Hata kama ugonjwa wake wake ni mdogo kuliko wangu, lakini kinachojaliwa ni KITU. Pia huoni uwepo wa International Schools na zile zetu sisi za St. Kayumba? Mnaita HALALI-HAKI, najua ni kwakuwa wazungu wamewaambia hivyo. Unadhani huduma sawa zitawezekana vipi hali tumetofautiana kipato? Lakini tujiulize, magonjwa yawapatayo masikini huwa ya makali madogo kulinganisha na yale ya tajiri? Maradhi yanapima kipato cha mtu na kumfanyia "consideration"? Malaria ya Tandale ni tofauti na ile ya Masaki?
3. Cha kushangaza unakubali kuwe na uhuru wa Local Competetion. Lakini unakataa International competetion...nakiri sijakuelewa! UHURU upi unaodai uwepo kwenye uchumi wetu? Hata wasipokuja wao, hujui kwamba Wewe au mimi naweza kupokea mtaji mkubwa kutoka kwa hao wageni nikawekeza hapa kwetu, nikagawana nao faida? Si tumeruhusu kila mtu kupigania maslahi binafsi, unadhani nitamfikiria mtanzania asiyekuwa na rafiki wa nje ili ampe mtaji?
Hii ni mitego mkuu wangu.
Maisha ni Furaha, kama haipo ni Upuuzi. Na hakuna Furaha ya mtu ila Watu. = UTU.
Mungu wetu anaita sasa!
 
Mkuu Mkandara
Kwa ufafanuzi tu Azimio la Zanzibar liliruhusu viongozi kumiliki mali halali sio kwa njia za wizi; kilichoruhusiwa baada ya kuwatumikia wananchi kisiasa wanachama/viongozi wanaweza kujishughulisha kwenye shughuli halali za kiuchumi; hii ilitokana na kwamba wanasiasa kabla kabla ya Azimio la Zanzibar walibanwa na sheria na wengi wao waliishia kuishi maisha ya dhiki baada ya utumishi wao wa kisiasa; kuhusu utajiri wa hao matajiri wetu ni kitendawili; MAFIA walisema WHENEVER THERE IS GREAT FORTUNE THERE MUST BE A CRIME BEHIND IT; kama unakumbuka kabla ya benki ya NBC kusitisha shughuli zake mdaiwa na 2 alikuwa ni Reginald Mengi chini ya kampuni yake kama nakumbuka iliitwa Kalamu Ltd deni lilikuwa ni mamilion kwa ujumla ukijumlisha madeni ya kampuni za Mengi ilikuwa ni mabilioni swali la msingi je pesa zililipwa? Nina uhakika 100% deni halikulipwa huo ni mfano mmoja tu wa hawa matajiri wetu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Lazima nikiri baada ya kupitia michango ya humu pamoja na yangu nimejikuta najiuliza "focus" yetu hasa ni kujadili kila kitu na kuacha hapo au kujadili suala moja na kufikia muafaka. Pia nikiri kuwa michango humu ina mantiki na virutubisho vya akili ingawaje mmh kuna kaharufu ka kutambua kasoro na lawama kuliko "solutions" ambazo mtu utasaidika nazo. Najua tulivyoathirika na uelewa tegemezi.

Naomba nichangie kwa kifupi moja baada ya lingine niliyo yapata kwenye michango humu; maana mambo ni mengi na mimi kwa muda sikuwepo kwenye jamvi hili.

Pan Africanism

Hapa naomba niwakumbushe mtu mnae mjua sana anaitwa Jenerali Ulimwengu. Huyu alittumwa na chama na nchi kwenye ofisi ambazo zilikuwa zimejikita kuendeleza hili wazo huko Afrika ya kaskazini. Maana yake pan africanism ilikuwa a very strong movement yenye malengo mengi yaliyofanikiwa na yapo yaliyotekwa nyara. Lakini haina maana ilizikabiri changamoto zilizokuwa zinajukana vizuri nazo ukoloni na ukoloni mambo leo. Naona la ukoloni uliondolewa kwa kubadilishana na ukoloni mambo leo.

Dhumuni kubwa la kuondo ukoloni liliingia doa pale viongozi/watawala wetu walipoingia kichwa kichwa kukumbatia pande za kiitikadi zinazopingana. Nchi nyingi za kiafrica zilishawishika kujitambulisha na itikadi za ulaya mashariki kupinga ubepari kuwa ni unyama. Lakini wakiwa madarakani walionja tamu na chungu ya ubepari. Waliowekwa kwenye kapu la mabepari walisifiwa na kupewa misaada(Zawadi/Rushwa). Wenzangu na mimi walioukataa/waliokomaa angalau kwa maneno yao tu walikosa misaada na kushambuliwa kwenye vyombo dola za magharibi.

Hapa nisisitize kuwa vita iliyoonekana ni kujitambulisha au kupangwa kwenye kati ya hizi pande mbili. Vita ambayo viongozi wengi hawakuihimili ni ile isiyoonekana ya kuathirika kiubongo wa kufanya maamuzi ya manufaa kwa nchi zao. Athari hii ya akili ndiyo iliua Pan Africanism na kurutubisha ukoloni mambo leo. Ushahidi uchumi wetu kati ya 1967 hadi 1977 ulikuwa mzuri sana, baada ya hapo ukaporomoka ghafla. Zaidi ya kuporomoka fikra za mageuzi(reforms) ilijikita na kuondoa dhana yote ya utaifa na kujisalimisha kwenye taasisi za magharibi IMF, WB. Mbinu iliyotumika ni kupotezea mfumo wetu uliokuwa umefikia kuwa na data za kutosha kufikia tathmini na kuanza upya kwa majiribio nje ya uwezo wetu.

Kwa hiyo kuanzia hiyo 1977 tumeshudia yafuatayo:-

1. Kuzaliwa CCM 2. Kufa kwa EAC, 3. Vita kali na Uganda, 4. Kubadirika kwa sera karibu zote kwa kisingizio kuwa hazikuwepo kabisa eg elimu. uchumi, afya etc.

Tulichokipata kibaya nionavyo mimi 1. Kubadika Mind set yetu kuwa ya kutokujiamini 2. Kupoteza mwelekeo wa kujitegemea na kuwa tegemezi 3. Maamuzi mengi yahusuyo nchi kuamuliwa nje ya nchi. 4. Viongozi watawala wasio na msimamo. Lakini huo ndio UKOLONI MAMBO LEO.

Baada ya kuathirika kwa Pan Africanism tumeshudia rasilimali za Africa zikichangamkiwa na mabepari na viongozi wetu wakineemeka na kuwasahau wananchi. Ikaingia wimbo wa demokrasia tuliouimba kama kasuku. Hapa nachelea kujiuliza haya yote na baada ya miaka zaidi ya 20 kwenye maisha bila Pan Africanism, uchumi huria, vyama vingi, elimu duni, migogoro kila mahali akili yetu inafikiria nini?

VYAMA VINGI

Sitazungumzia chama/vyama na itikadi zake, nitajikita kwenye wazo la kuwepo vyama, uongozi, utawala na mind set. Tunajua mara baada ya uhuru tulikuwa na vyama vingi. Kwa nje vilikuwepo kuwasilisha mawazo mbadala ya uendeshaji wa nchi. Kwa ndani vilielemea itikadi za nje. Ila walikuwepo wanachama waliofikiria utaifa. Naomba ugundue hapo ukinzano ni lazima uwepo. Tukaja kwenye chama kimoja kwa nje lakini kwa ndani vyama vingi kwa sababu za kimaslahi ya ndani na nje. Nasema hivyo kwa sababu akina Kambona, Mkapa na wengine hawakuwa waumini wa itikadi ya chama hicho. Akina Babu, Ngombale Mwilu walikuwa kambi nyingine kwenye chama/vyama hivyo hivyo.

Agenda ya chama kimoja 1967 - 1977 ilieleweka na wananchi kielimu, uchumi hata kiusalama. 1977 nakuendelea, wananchi hatukuelewa agenda za viongozi/watawala juu ya mstakabali wa maendeleo yetu. Mbaya zaidi tulianza kuathirika kifikra kwa sababu tuliyoelezwa na watawala/viongozi hatukuwa na uwezo wa kuvitafuna bali kuvimeza. Na kwa bahati mbaya adui namba 1 MUDA hakusubiri. Rasilimali namba moja MUDA hatukuambatana naye. Walioweza akina Prof. Lipumba wakaingia kutufanyia mageuzi ya uchumi baada ya kina Mtei kupishana na Mw. Nyerere. Haya yote yalizaa mahitaji ya vyama vingi ili kuwepo mawazo na mikakati mbadala. Kwa kweli haikuwa rahisi kuepuka haya.

Kama kawaida ya wenye mtindio wa fikra, haikujalisha hivi vyama vinaanzishwa kukidhi mbadala uliokusudiwa. Watawala na si viongozi walihakikisha vyama vikiwa na njaa vinapewa mfupa wakati minofu inabaki kwa wenyewe. Ndiyo kuibuka kwa UPANDIKIZI. Sisi wananchi tulikuwa kwenye hali gani ya utambuzi wa uwakilishi na uelewa wetu wa kinachoendelea? Jibu ni kuwa hali mbaya bila kujitambua wala kuelewa. Kwa sababu nyenzo kubwa ya nguvu ya fikra ilishaporwa na elimu duni na watawala dhalili.

Haya toka 1992 tumeshuhudia hivi vyama vingi. Nafasi ya kuvibaini ubora wa hivi vyama imekuwa adhimu, kifupi kubaini huko kumehodhiwa na watawala. Binafsi lazima nikiri nimeshindwa kubaini kipi chama kinaweza kukidhi mahitaji yangu na nchi ninayoitarajia. Sababu kubwa vyote vinaeleweka kwenye kunyooshea kidole "symptoms" za matatizo bila kujikita/kubaini tatizo lenyewe. Kwangu mimi masuala katika umuhimu ni Elimu Bora si Bora Elimu, Uchumi Imara si Uchumi Huria, Ulipaji Kodi si ukwepaji Kodi, Uongozi Bora si Bora Uongozi nk. Niambieni kipi chama kilijokita kujibainisha na haya? Najua changamoto kubwa ya utamu wa madaraka unaweza kuwa kikwazo lakini umakini hauzuiwi na hilo.

MATABAKA

Kwa sasa matabaka ya kila aina yako dhahiri kama walionacho na wasionacho, wenye chama na wanachama, wenye maamuzi na wanaoamuliwa; wenye elimu bora na wenye bora elimu, madaktari na watumishi wengine. Yote haya yanaielemea serikali. Sasa serikali si yetu wote kwa ajili yetu wote bali ni serikali ya CCM kwa ajili ya CCM. Wanapoamka kudai sehemu ya serikali hiyo basi mgongano na migogoro ni lazima. Kwa nini basi sisi wote tusijiunge na CCM ili nasi tuwe sehemu hiyo? Haiwezekani kwa sababu usisahau CCM ina wenyewe. Kwa hiyo vyama vingine vina nafasi nje ya wenyewe wa CCM. Kwa bahati mbaya vinaitwa vyama pinzani. Suala la msingi vina sera gani kuhusiana na haya matabaka maana haitoshi kulalamikia kuwepo kwa matabaka. Inahitajika sera, mkakati na rasilimali kuyakabili hata kuyapunguza haya matabaka. HAYA MATABAKA YAMEJENGEKA KWA HIYO CHAMA CHOCHOTE MAKINI kitaibua sera na mikakati na kusimamia rasilimali ya nchi kutokomeza haya matabaka ili tusipigane na kuuana TUFAIDI MATUNDA YA NCHI.

MFUMO WA UTAWALA NA UONGOZI

Piga ua mafanikio na matatizo yetu kama nchi yanasababishwa na kutatuliwa na mfumo wa utawala na uongozi. Ni tunu ya ubinadamu na hasa ustaarabu kuwa na aina ya utawala na uongozi. Huu ndiyo unaitwa mfumo. Kwa historia tu tumefikia kiwango cha ustaarabu ambao unatupa jukumu na wajibu wa kujiamulia aina ya mfumo wa utawala na uongozi. Hapa nasisitiza uwingi wetu na uelewa wetu tuna maamuzi ya hatma ya aina ya utawala na uongozi tunaoutaka. Fursa zinaweza kuwa zinabinywa na wenzetu kwenye nafasi za uongozi na utawala. Hapo ndipo nasisitiza kama binafsi, wewe na mimi na sisi wote tunaweza kubaini na kuainisha na kutambua fursa tuliyo nayo katika mazingira haya hata kama tumebanwa namna gani. Hapa nasema hivyo kwa sababu wananchi wanalalamika, viongozi wanalalamika, watawala wanalalamika hata Rais wa nchi analalamika kiasi ambacho hajui ni kwa nini nchi ni maskini. Tumekuwa tunaomba kusaidiwa toka uhuru, je hilo siyo tatizo linalitokana na kasoro za utawala na uongozi wetu?

Naomba wote tuelimishane angalau tubaini na tuainishe hizi kasoro na kupendekeza suluhisho. Hapo hapo tuchangiane jukumu na wajibu wetu binafsi. NI CHANGAMOTO KWELI KWELI LAKINI HILO LITATUWEKA KWENYE NJIA YA KUJIKOMBOA.

Maoni yangu juu ya mfumo wa utawala ulivyo, naona si mmbaya kiasi hicho tunavyolalamikia, tatizo lipo kwenye mfumo wa uongozi. Viongozi kwa makusudi au kwa kutokujua hawatutazami wananchi kwanza kuhusiana na mahitaji yetu yanayosababisha malalamiko, migogoro na kuzoroteka kwa uchumu na kwa hiyo huduma za jamii. Mimi naainisha, na kutambua kuwa mfumo wa kuwapata viongozi una kasoro. Moja ya sababu ni kuwa sisi tulio na jukumu la kuchagua viongozi tuna kasoro. Hatujui dhamana tuliyo nayo ya uchaguzi wa kiongozi bora, hatuupi changamoto mfumo mzima wa uchaguzi kwa sababu ya ukomo wa uwezo wetu wa kutoa hoja zisizopingika kufanikisha hilo. Fursa tunazo finyu lakina hatuitumii. Ni matumaini yangu kuwa mara tukifanikisha hili, tutaurekebisha mfumo wa utawala bila jasho.

MATUKIO

Labda nianze kusema kuwa umasikini, hali mbaya ya uchumi uendeshwaji wa mihili mingine ya dola, utawala na uongozi unahusika na kila tukio. Mgogoro kati ya madakari na serikali ni tukio la karibuni. Kuna ukweli kuwa MTU AKIFIKIA MWISHO WA KUFIKIRI, ANAISHIA KUTUMIA MABAVU. Hii wala si falsafa bali ni maumbile ya binadamu. Tuonapo matukio haya yote, tujiulize fikra zetu za maamuzi ya busara zipo kwenye kiwango gani? Kwa nini hali ya mambo iko kama ilivyo. KWANGU MIMI OMBWE LA UONGOZI NI HILO. Tusiende mbali na kupoteza muda kuwanyooshea vidole wahusika bali MMOJA MMOJA AANZE KUCHUKUA HATUA.

Najua ni changamoto kweli kweli kuyatafisiri na kuyahusisha haya ya akina Richmond, Dowans, akina Manji Bahresa Chavda ya Katiba Mpya nk. Nakuhakikishia yana uhusiano. Nakushauri wewe binafsi baada ya kuyatakari haya niliyoyandika maana ni mawazo yangu kutokana na ninachokijua na akili yangu ilivyochambua fanya uchambuzi wako na utafiti ujiridhishe halafu chukua hatua wewe binafsi kulingana na FURSA iliyo mbele yako hata kama ni ndogo na finyu

HITIMISHO

KWANGU MIMI HIZI NDIZO DURU ZA SIASA TUCHANGIE
 
Duru za siasa,

Tunaendea na historia ya marais waliyopita nchni Misri, Nasser aliwaita baadhi ya viongozi wakiarabu mjini Cairo katika juhudi za kumpatanisha Mfalme Hussein na Yasser Arafat ambao wakati huo walikuwa kama paka na chui ugomvi wao ulifikia kileleni baada ya ya Wapalesitna kuziteka nyara ndege tatu, moja ya shirika la ndege la Uswiss aina ya DC-8, ndege ya pili boeing 707 ya shirika la ndege TWA na ndege ya tatu ya shirika la ndege la Uingereza la BOAC ya aina ya VC-10 na kuziliazimisha kutua uwanja wa Dawson, ulio maili kama thalathini kutoka Amman.

Serikali ya Jordan haikukubali, jeshi la Jordan lilizipiga mabomu kambi kadhaa za wakimbizi Wakipalestina nchini Jordan, vikosi vya jeshi la Ukombozi la Palestina vilikuwa Syria, vilivuka mpaka vikaingia Jordan na kuelekea Amman. vilishika maeneo kadhaa ya Jordan na kutangaza kuwa ni maeneo yaliyokombolewa.

Nasser alipata mshutuko mkubwa wa moyo baada ya kumalizika mkutano huo wa kuleta suluhu baina ya Mfalme Hussein na Arafat. aliondoshwa kwenye ukumbi wa mkutano na kupelekwa nyumbani kwake ambako alifariki muda mfupi baadaye...Hapajapata kutokea na penngine hapatatokea tena watu milioni tano wakilia na wengine wakilia kwa kwikwi kwa pamoja kama ulimwengu ulivyowashuhudia wakazi wa Cairo wakati wa mazishi ya Nasser na si Wamisri tu waliolia Mfalme Hussein alilia kama mtoto mchanga alizimia mara mbili. Arafat alitokwa na machozi huku mdomo wake ukitetemeka alipokuwa akimsomea dua...Gazeti la Al Ahram la Misri liliandika Nasser amefariki ulimwengu mzima unaomboleza.

Pengo la Nasser likaja kuzimbwa na Anwar Sadat kwa kuifuata katiba ya nchi. Sadat hakuwa na haiba wala mvuto kama aliokuwa nao Nasser. Katika kujijenga na kujaribu kujifanya kiongozi tofauti Sadat alianza kuzitenga sera za Nasser...moja ya matokeo yake ni kubadili polepole kwa sura ya Cairo. Mashirika ya umma yakajiuza kwa watu binafsi na ubepari wa kiholela ukaanza kutia mizizi bei za bidhaa, hasa vyakula zikanza kupanda... Jan, mwaka 1977 Sadat aliongeza maradufu bei ya mkate. Wakazi wa Cairo walichemka wakamiminika barabarani kama kawaida yao wakichoma moto magari na kuvunja maduka ghadhabu zao ziliwashangaza hata wao wenyewe.

Sadat alikuwa hajui jinsi Wamisri walivyokuwa wakiishi katika ufukara majeshi yalipambana na fujo za waandamanaji Cairo kwa mabomu ya kutoa machozi na kuwapiga risasi wapinzani watu wengi walikufa... Sadat akaanza kuwaona wananchi wenzake wa Misri watoto na yeye baba yao, Oktoba 6 mwaka 1973 Sadat alipata mafanikio makubwa pale jeshi lake lilipoyashambulia kwa ghafla majeshi ya Israel na kuyaondoa kutoka eneo la mfereji wa Suez ambalo Israel ililiteka ilipozishambilia nchi za Misri na Jordan mwaka 1967.

Tutaendelea....
 
Wakuu zangu,

Nadhani sasa kidogo tunaanza kuchanga mada au niseme hoja zetu. Mh. Nguruvi3 Ningeomba kama unaweza kusubiri tukimaliza moja kuchangia kabla hujatupa changamoto jingine na nadhani nasi pia tujikite na moja kwanza labda tu jingine litokane na la kwanza kwa Mfano tunazungumzia Pan Africanism halafu jina la Nasser linajitokeza na mtu anataka kujua zaidi kuhusu Mtu huyu..

Kuna issue sasa hivi Jingalafalsafa ameliweka kuhusiana na Ubepari - Capitalism (tumetoka nje) lakini ningependa sana kulizugmzia hili muda wake maana ipo haja kubwa sana ya kuelimishana juu ya Ubepari maana ndio maji tunayoyakoga leo hii.. Hivi kweli Watanzana wanaujua Ubepari au tumefungishiwa kitu kinachoitwa Ubepari lakini sii Ubepari kulingana na hoja ya JingalaFalsafa.

Nina hakika wengi wetu tumesoma sana vitabu vya wajamaa, tumehifadhi elimu kubwa ya upande wa kushoto lakini sidhani kama tumejizatiti ndani ya elimu ya Ubepari na kuelewa nini faradhi, sunna vs haramu na makuruh. Sisi wengine tulipitia somo la Siasa na kuingia ndani zaidi tukaamini na ilibaki tu kuuabudu lakini kama dini inatakiwa uzame ktk ukweli wa mafundisho, matukio na hadithi kuweza kujua umefungwa kamba wapi na ukweli ni upi kwa kutazama pia mapungufu yanayozungumzwa upande wako ..Labda nimuache tu ndugu yangu kwa Kupingana na dhana inayosema Ubepari = Pigania kunyonya kwa namna yoyote.
Na hilo la Ubepari upo wa namna mbili.
(a) Ule wa taifa kunyonya taifa(nauita External Capitalism)
(b) Ni ule wa mzawa kumnyonya mzawa( Internal Capitalism.

Hii sii kweli kabisa na labda nikuanzie na kusema kwamba kinyume cha Ubepari ni Udikteta. I mean Ujamaa = Udikteta. Kama serikali inavyowaweka watu wake ktk walfare ili wabakie ktk hali hiyo miaka yote ya maisha yao kama tegemezi while viongozi wao ni matajiri wanaokula mezani. Mifano yake ni mibaya kuliko Ubepari kwa sababu sisi binadamu tumekosa Imani kidini na tumekosa Uzalendo Kisiasa.

Tumewaona kina Kim, Castro, Mingistu, Mao na wengineo hawa wote walikuwa madikteta wakubwa tena naweza sema walikuwa kama MaPharaoh wakiishi wao kwa raha mustarehe wakati wananchi wao wakimenyeka. Sisi Waafrika tulikuwa nafuu na wabora zaidi Afrika wakati tunajenga Pan Africanism miaka ya 60s kuliko tulipoingilia siasa za hawa wageni. Ujamaa wa kikomunist ni Utumwa, unatumia zaidi rasilimali watu kama nguvukazi kuwa kipimo cha kibaba cha mavuno tokana na uzalishaji. Haikuwa lazima kabisa maana tuna machines na Robots ktk dunia ya ubunifu na kuumiza vichwa kuisaka elimu..

Hivyo, Ujamaa wa Kikomunist ulitazama zaidi kugawa rasilimali za nchi kutokana na mchango wa nguvu yako ktk uzalishaji na that's why tuliona huko China shamba la ekari 10 wanalima watu 100 wanakijiji wakati they could have used tractor moja na dereva mmoja lakini itikadi itagomba.. Ujamaa wa kikumunist ulikuwa sii creative, hawakuwa wabunifu zaidi ya kutumia mitulinga na kuridhishanana ndio tuloyafanya hata sisi kazi ya mtu mmoja ilifanywa na watu 20 iwe Bima au Ofisi ya rais.

Sina maana mbaya kuhusu Ujamaa na Kujitegemea lakini lazima tukubali kwamba kuna makosa yalifanyika kuiga itikadi za jamii zilizokwisha endelea wakitaka kuchukua Utajiri ulokwisha simamishwa. Then Russia walikuwa tayari industrialised, China, Cuba yaani hizi nchi zilikuwa Heaven za wakati ule wananchi wake wakichungulia tu dirishani tofauti na sisi tuloingia Ujamaa wakati hatuna hata kiwanda. Itikadi ya Ukomunist lengo lake lilikuwa kutaifisha Utajiri wa Wakoloni na wageni kuzirudisha mikononi mwa wananchi kama Mugabe anavyodai ardhi toka kwa Makaburu haina maana kilimo ni lazima kuwepo na uuwiano wa watu kumiliki..

Ubepari sio utamaduni wa wageni, Ubepari haukuiletwa Afrika na wazungu bali ulikuwepo na ndio ulokuwa - Ujamaa wa Kiafrika. Nitaeleza kwa kirefu zaidi nitakapo pata muda. Ikumbukwe tu ya kwamba sisi Waafrika wenyewe tulikuwa Mabepari kabla ya mzungu wala wakoloni kuingia Afrika. Ubepari wetu ulikuwa wa kurithishana mali toka wazazi kwa wanawe, Mababu wa wajukuu lakini kila mmoja wetu aliweza kumiliki mali zake hasa akisha kuoa ama kuolewa..

Na serikali (Watemi) ilikuwa na jukumu la kuwalinda wananchi wake kutokana na ukoo au kabila husika lakini kila familia ilimiliki mali zake toka ardhi, nyumba, mazao ya kilimo, mifugo au mitumbwi na nyavu za Uvuvi. Economic system yetu ilikuwa based on private ownership na sii mali za Mtemi au serikali yake. Njiia zote za uzalishaji toka ubunifu, uwekezaji hadi ujenzi wa mtaji na mali ulitazama faida - Jinsi ya Utajirisho zaidi ya kugawana mapato sawa kwa kabila zima.

Hatukuwahi kuwa na serikali ya MaChief au Watemi walo control uzalishaji iwe ukulima, ufugaji au uvuvi bali wananchi wenyewe.. All they did ni kuweka Policies ambazo ziliwa protect wananchi, kulinda Uhuru wao(freedom) dhidi ya maadui au wageni, kutoa haki sawa (justice) na kudumisha AMANI baina yao na makabila.

Ila moja tu ambalo halikuwepo ktk mila na desturi zetu ilikuwa Equality. Kinadharia tunachanganya sana kati ya kuleta EQUALITY while in fact all human being are CREATED equal. Huko mbele ndiko tunakoachana. Na ktk uhadsidi wetu ndio dini zikarudi na kuitaka Equality baina yetu, sio siasa. Huu ni mtihani mkubwa ambao tumeshindwa wote japokuwa tunaamini. USAWA haupo hata ktk uhalisia wa dini zetu, Ujamaa au Ubepari.

Na binafsi yangu sintoamini ktk dunia hii kunaweza tokea Usawa - Haiwezekani, maana binadamu tumeumbwa na tamaa na juu ya tamaa zote Madaraka imechukua nafasi ya kwanza..We all strive to be someone respected, admired and above all cheered for - Mheshimiwa. Ukisimama makofi, mayowe na vifijo makes us feel uungu mtu..Sasa unakuwaje sawa na huyu Mheshimiwa au kuwa treated sawa na Mheshimiwa?..na ktk vita hii huwezi kupata USAWA maana kuna failures- usawa utoke wapi...

Obama hawezi kuwa sawa au kuwa treated sawa na hata makamu wake acha mbali raia wa kawaida iwe kwa mahitaji yake au dream zake. Hatuwezi ku treat kila mmoja wetu sawa na mwingine maana kia mmoja wetu ana tabia, hulka na malengo tofauti.. MUme na Mke, mzazi na mtoto, Mwalimu na mwanafunzi - huu Usawa tunaoutaka na unapiganiwa hata na dini zetu (kiislaam) ni mtihani mkubwa ambao hauwezi kupatikana chini ya Ujamaa au Ubepari.

Binadamu wote ni sawa ni kitendawili ambacho hakina majibu isipokuwa imebakia kwenye kuumbwa kwetu maana sisi wote imani yetu ya dini ni dhaifu na hatuwezi kuleta usawa tunaozungumzia kila siku. Kama kuna Mungu mmoja nasi wote tunaamini kuwepo kwa nguvu ya Mungu ktk uumbwaji wa dunia, ulimwengu, vilivyomo na maajabu yake inakuwaje tuna imani nyingi na tofauti za dini zinazokinzana?

Something isn't right! Vivyo hivyo ukirudi ktk Ubepari na Ujamaa utakuta kwamba sisi imani zetu za Uzalendo ni dhaifu na Mungu katuumba kula kwa jasho letu, hivyo hizi siasa zote zinatafsiriwa upya na kupewa maana nyingine tofauti na biblia au vitabu vya Mungu. Ubepari ndio mfumo wa maisha ya binadamu ilisemwa ktk Biblia na hata Quran na kuna miiko na maadili yake. Kuna regulations ambazo tunatakiwa kuzifuata ili mali na utajiri wetu usitupeleke kusiko takiwa - Individually.. How we gonna organize ourselve kurahisisha mahitaji yetu ni mtihani mwingine..
 
Mkuu Mkandara, naafiki hoja ya kuendelea na mnakasha huu kama ulivyoshauri aya ya kwanza hapo juu.
Wakuu wote tunashukuru sana kwa mjadala mzuri wenye vitu vinavyoshibisha vichwa!
Tuendelee na mnakasha, ni mtamu sana!
Nina kahawa na kashata hapa jamvini nawasoma wakuu taratiibu
 
Mkuu Mkandara:
1. Kuamini kwamba maisha ni aidha Ujamaa ama Ubepari tu, ni kosa kubwa kwangu! Ni utumwa wa kifikra, ni kujidunisha. (Tafadhali, usinifunge na ujamaa, ubepari, biblia wala kuruan, ila MANTIKI-UTU, nikiuamini kama ndio msingi mkuu wa maisha)
Kusoma sana vitabu na marejeo si bora sana kama kuwa na tafakari yako mwenyewe ya juu ya mambo uyasikiayo, uyaonayo, na uyahisiyo. Nautaja ubepari si kufanyia reference, ila kwa kuwa ndio mfumo uliopo!
2. Kinyume cha Ubepari si Udikteta kama unavyodai. (a) Mbadala wa ubepari si ujamaa tu, UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO. Tukiumiza vichwa, tunaweza. (b) Ipi ni tafsiri ya udikteta, kumuamuru mtu kufanya kazi ndio udikteta? Unadhani amri zilikuwa zinatolewa kwa maslahi ya mtu binafsi au umma? Kipi ni bora kuzidi maslahi ya umma?
3. Umesema Usawa hauwezi kuwepo, kwani tumeumbwa na tamaa ya kupigania ukuu. Kwanza nikubaliane nawe kuwa tumeumbwa na tamaa, lakini tuliwekewa msingi mkuu wa kuongoza hizo tamaa zetu, nao ni UTU! Mantiki ya UTU i nafsini mwa kila mtu, awe mchawi, mwizi, jambazi, ama laa, UTU umo nafsini mwake! Kutokuuishi, ni kujisaliti! Je, kuna mtu anayetenda ovu pasi nafsi yake kumsuta (kujishtukia)? Ni wazi hayupo! Sasa, kama zipo sheria zimetungwa makusudi kulinda tamaa mbaya za watu, kwanini zishindikane za kulinda tamaa nzuri? TUMEKUBALI KUKARIRISHWA, TUNASEMA HAIWEZEKANI. Lakini si katika misingi ya UTU. UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO.
4. Ni wazi kabisa samaki hakunjwi akikauka tayari. Mfumo umemruhusu Obama kuwa juu, lakini wangeamua wenyewe kubuni mfumo ambao usingemkweza, na ingewezekana.

Katika pita pita yangu kuna neno hili "UPENDO" na sentensi hii, "FROM EACH ACCORDING TO HIS ABILITY, TO EACH ACCORDING TO HIS NEEDS" Marx na Engles... maana kubwa sana ya tafsiri ya maisha imebebwa humo!
Ukifuga manyigu usishangae manundu na kukosa asali. Kama tunaamini kabisa kuwa mfumo uliopo ni sahihi, basi tusilaumu wala kupayuka juu ya chochote kiovu tukionacho...kwani tutakuwa tumekubali kuolewa, sharti tulale........!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Mkuu Mkandara, naafiki hoja ya kuendelea na mnakasha huu kama ulivyoshauri aya ya kwanza hapo juu.
Wakuu wote tunashukuru sana kwa mjadala mzuri wenye vitu vinavyoshibisha vichwa!
Tuendelee na mnakasha, ni mtamu sana!
Nina kahawa na kashata hapa jamvini nawasoma wakuu taratiibu
Shukran, maana zipo hoja nyingi sana uloziandika nyuma hatukupata muda wa kuziongelea kwa mapana..Binafsi yangu napenda sana kusoma tofauti zetu kimtazamo zaidi ya kufanana kwani hapo hujifunza zaidi..

Ritz,
Kuhusu Misri inasemekana ni koloni la Marekani toka kuondolewa kwa Nasser na walipata na wanaendelea kupewa misaada mikubwa nadhani ni nchi ya pili baada ya Israel.. Hivi sasa itakuwaje?
 
kwakweli ushauri wako 100% nakubaliana na wewe, Hata jk ameitwa Dhaifu ama kwa kuchelwea kutoa maamuzi ama kukaa kimya kwenye issue ambayo watu wanategemea kitu
 
Mkuu Mimibaba, ningependa nichangie hoja zako nzito katika bandiko# 198 na nkidokoa huku na kule kutoka kwa wanajamvi wengine kwasababu kuna hoja zinakinzana na zingine zinashabihiana.

Wakoloni walipoondoka walijua vema hazina kubwa iliyopo Afrika kwahiyo waliweka mikakati ya kurudi kwa mlango wa nyuma. Labda nitoe mfano tu kuwa Wajerumani wanaifahamu Tanganyika pengine kuliko tunavyoijua. Wakati wa ubinafsishaji wa TRC wao waliingia katika zabuni wakiwa na nondo zote. Walijua kila 'calvert' na ugumu wa daraja husika.

Kwa muktadha huo Pan Africanism ilikuwa ni tishio kubwa na kila jitihada zilifanyika hilo lisiwezekane. Unakumbuka Mapinduzi yaliyokuwepo kila uchao katika miaka ya 1970 na 1980. Wasukaji wakubwa wa mbinu hizo walikuwa nchi za magharibi. Baada ya kuumaliza mkakati wa Pan Africanism kwa kusimika vibaraka wao hapo wakatangaza kuzisusia nchi zinazofanya mapinduzi. Nguvu ya Pan Africanism ikafa kwasababu viongozi walikuwa wanaishi maisha ya kujihami na hakukuwa na muda wa kufikiri kuhusu Afrika nyingine.Kwa maneno mengine 'If you can beat them, join them'

Kuhusu uchumi wetu kuwa mzuri miaka ya 1967-1977, pamoja na sababu zingine ulizotaja, bado tunabaki na ukweli kuwa kuanguka kwa soko la mkonge, kahawa na pamba vilichangia sana kuturudisha nyuma. Haya hayakutokea kwa bahati mbaya, ilikuwa ni mbinu ya kudhoofisha nchi zetu na kweli ilifanya kazi.

Hapo ndipo hoja yako ya sisi kupoteza mwelekeo ilipoingia, na kuaminishwa kumeza kila litokalo WB, IMF n.k.
Tulipoteza mwelekeo kwasababu hatukuweza kufikiri kuwa tungeweza kulima mpunga, mahindi n.k na bado uchumi ukawa imara. Pengine tungekuwa tunalisha Afrika kwasasa.

Tukaacha kilimo cha asili cha umwagialiji tukisubiri wataalamu waje watufundishe. Hapa ndipo nakubaliana na Mkandara kuwa badala ya kukifanya kilimo chetu cha asili kuwa cha kisasa tukarukia kilimo ili mradi kilimo.

Hadi sasa hatujajifunza kutokana na makosa ya huko nyuma. Kilimo kwanza ni dhana ninayoikataa sana. Watanzania wanaweza kulima tena kilimo cha kisasa kabisa katika mazingira yetu. Kule kwetu kuna miefereji ya asili ya kilimo cha umwagiliaji iliyopo kwa miaka 150 sasa. Lakini leo hakuna anyeitumia na njaa ni kila siku. Ni kwanini? Sababu ni kuwa kilimo hakilipi kama shughuli nyingine.

Badala ya kilimo kwanza cha wanasiasa serikali ingefanya jambo moja, kuandaa mazingira mazuri ya kumwezesha mkulima kunufaika na kilimo, hapo wangeagiza matrekta wao wenyewe na si kutegemea tenda za rushwa.

Kilimo kwanza ni mradi wa ulaji tu. Siamini ninaposikia kuwa Rais wetu ameahidiwa mapesa ya kilimo huko Marekani. Hatuhitaji pesa tunahitaji mipango ongofu na nyoofu. Hapa tena nakubaliana na Mimibaba kuwa tatizo letu limejikita katika uongozi. Hatuna uongozi unaojua nini Watanzania wanahitaji na nini ni tatizo la Watanzania.

Kuhusu nini vyama vingi vinaweza kuleta badala ya CCM, hapa nadhani tutavionea vyama hasa vya upinzani.
Tutavionea kwasababu havijapata fursa ya kutuonyesha vinaweza au la. Kule Kenya tunaona kasi waliyo nayo na hata jirani zetu wa Zambia.

Nikupe mfano, nimesoma ilani ya uchaguzi ya CDM na nina nakala yake, hakika kuna mambo wameyaeleza na kama wangepewa fursa basi tungekuwa katika nafasi nzuri ya kuwahukumu au kuwapongeza.

Wameongelea suala la mapato na vyanzo, wameongelea bajeti ya sigara bia na vocha za simu kuwa haifa na siyo endelevu. Wamesema mengi ambayo kama wangeyatekeleza hakika tungesogea toka hapa tulipo.

Ingawa inabaki dhana ya kufikirika jambo moja nililojifunza ni kuwa kuna mbadala wa mawazo, na wao upinzani umeleta changamoto sana.Kwahiyo tusiwahukumu kwa kosa la kutopewa nafasi kwanza, lakini pia tuangalie mipango yao.
Kwasasa naweza kusema kuwa ubunifu wa upinzani ni mkubwa kuliko wa chama tawala miaka 50 baada ya uhuru.

Sasa Mimibaba, ametoa changamoto, tujiulize, tuanishe na tutoe suluhu ya changamoto zinazotukabili kila mmoja kwa mtazamo wake. Kama alivyosema ni changamoto lakini ipo mbele yetu sote watanzania, hatuna muda wa kusubiri tena, na hapo ndipo nitakapoendelea napo.......
Itaendelea
 
Mkuu Mkandara;
mifumo yote ubepari na ujamaa imebuniwa kwa lengo moja tu kumtawala binadamu; usawa wa binadamu haupo na wala hautokuwepo, ujamaa sio suluhisho la ubepari lengo kuu hasa ni kuhakikisha upo uwiano wa mgawanyo wa mali miongoni mwa wananchi husika; labda tuangalie mabadiliko ya kiuchumi yanayoendelea hivi sasa duniani, ni kwa nini China imepiga hatua kubwa kiuchumi kwa kufuata sera za ujamaa, na kwa nini North Korea ni wajamaa lakini ni masikini; je ni kwa nini nchi nyingi za ulaya ambazo ni washiriki na wafuasi wakubwa wa sera za kibepari hivi zipo kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi; swali la pili tunalopaswa kujiuliza katika mabadiliko haya ya kiuchumi yanayotokea China je ni kila mchina ananufaika na ukuaji huu wa uchumu? je katika matatizo ya kuichumi yanayozikabili nchi za ulaya mathalani waathirika ni wote au ni sehemu tu ya wananchi wao? Ukiangalia viini vya mfumo yote ubepari unadai kila mtu ataendelea kiuchumi kwa juhudi zake binafsi, ujamaa umedai juhudi za pamoja ndio kiini cha maendeleo; swali la tatu kujiuliza ni kwanini katika nchi za kibepari matajiri ni 1% tu je hawa 99% ni wavivu au hawana miundo mbinu ya kutafuta huo utajiri? je katika huo ujamaa ni kweli mgawanyo unafanywa katika misingi ya haki bila upendeleo? Hakuna mfumo sahihi kwenye maisha, kinachofanyika ni kuangalia leo nini kifanyike ili kumtawala binadamu; hivi sasa tunaelekea zaidi kwenye Darwin theory survival of the fittest

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Inaendelea....
Kabala hatujaendelea na bandiko# 205, katika mjadala huu kuna hoja za Mkandara na JingalaFalsafa zinazohusiana na mada iliyopo. Labda nichangie tu kidogo kwa mtazamo nilionao.

Ubepari au Ujamaa ni njia tu za watawala kuwatawala watu kama alivyosema Mkandara.
Ukiangalia katika dunia ya leo hakuna mfumo tunaoweza kusema ni 'panacea' yaani dawa ya matatizo yote.
Nchi za Magaharibi zenye kudhani ubepari ndiyo njia ya kumkwamua mwanadamu kwa hakika hazifanyi hivyo.
Marekani ina mgogoro wa sekta ya afya. Wakati mabepari wakisema kila mtu aangalie utaratibu wake, wapo wanaounga mkono jitihada za kuwa na universal health care. Je universal healthcare siyo mfano wa ujamaa kwa siri!

Huko huko Marekani kuna mjadala wa kupunguza kodi kwa wale wenye kipato fulani kama siyo kuondoa kabisa.Je, hapo si ujamaa? Maana Ubepari kama alivyosema Ngongo ni survival of the fittest!

Hata ulaya magharibi wana program zinazokinzana na dhana ya ubepari ni kwa vile haweziweki wazi.
Kwa upande mwingine Uchina ambao ni Wajamaa waliokomaa sasa wameachia. Nao wanadaii soko huru na ushindani wa kibiashara. China imeacha kuzuia watu kumiliki utajiri kinyume na misingi ya falsafa yao. Matajiri wakubwa duniani leo wengi wanatoka china na ni hao ndio wananunua soko la Nyumba ulaya na Marekani. Ndio wamiliki wa viwanda kama Volvo na biashara nyingine. Hata ndani ya uchina sasa mambo yamebadilika na mfumo wa ujamaa umezua maswali

Sisi tulikuwa na mifumo yetu ya kiutawala. Mifumo hiyo ilijikita katika mazingira tuliyonayo na ilifaa kwa mahali husika. Mfumo kama wa Watemi ulikuwa si rahisi kusema ni wa Kibepari au kiujamaa. Tatizo ni pale tupoamua kuagiza kila kitu kwa neno demokrasia.

Tukifika hapo ndipo swali la Mimibaba linapoingia, je, tatizo letu hasa ni nini?
Kwa mtazamo wangu usiotofautiana na wake ni kuwa tatizo la Tanzania si rasilimali au rasilimali watu.
Tatizo letu ni Uongozi wa nchi. Huko nyuma tulifaulu kujenga misingi ya utu na umoja wa kitaifa mambo tunayojivunia. Badala ya kuendeleza mazuri ili tujijenge kiuchumi na kijamii, kundi dogo likaamua kwa makusudi kabisa kuiteka nchi kwa kutumia siasa.

Ili kufanikisha na kukamilisha mpango wao, kundi hilo likakaa ZNZ na kuua hata miiko ya uongozi.
Tumeshahudia makundi yakiiba chetu ili yajiufaishe kisiasa, tumeona kuhasimiana kiasi cha kuunda magenge ya kuuana kisa tofauti za kisiasa au hata za kibiashara.
Wakati hayo yakitokea wenye dhamana wamekaa kimya kuogopa waliowapeleka madarakani.

Mfumo mzima wa serikali umekuwa wa kihuni tu, kuwadanganya wananchi kama tulivyodanganywa kuhusu suala la utekwaji wa Daktari. Tumeona bajeti zikipigwa photocopy bila ubunifu wa aina yoyote. Tumeona bunge ambalo ndilo sehemu ya wananchi kusemea likigeuzwa kuwa genge la soga.

Hoja muhimu za kitaifa zikifunikwa chini ya kapeti kulinda wakubwa ndani ya bunge.
Vyombo vya dola kufanya kazi za kulinda genge husika na si wananchi.
Sheria zikiwabana vibaka wa kuku na kuwaachia magwiji yanaoiba sehemu ya bajeti ya taifa tena yakiwa ndani ya nyadhifa.

Katika hali hiyo hakuna kiongozi anyefikiri nini aifanyie nchi yake, wote wamejikita katika magenge, kama si serikalini basi ni bungeni au kwenye vyama. Hakuna fikra mpya na si ajabu kusikia 'kilimo kwanza' na tenda za matrekta zikipewa wezi.

Hivi tatizo letu ni matrekta au zaidi ya hapo. Ukimuuliza mkulima wa nyanya kipera anayeuza tenga la nyanya kwa sh 1500 atakupa jibu gani. Tumeona shule zikijengwa ilimradi zikimu tarakimu za uchaguzi hata kama madarasa yamegeuzwa madanguro ya mabinti na vijana kuvinunurisha viwili wili vyao kimahaba. Nani anajali!

Mimibaba kauliza suluhu ya haya ni nini? Hakika suluhu ya haya ni lazima itoke kwa wananchi wenyewe.
Katika historia ya ulimwengu hakuna dola ya kidemokrasia, kifalme au ya kidikteta iliyowahi kushinda nguvu ya umma.

Kwa bahati mbaya sana Watanzania ni watu wepesi sana kusahau hata kama wanajua kuwa wanachotendewa si haki.
Hii ndiyo silaha genge la kuiangamiza nchi imekuwa ikiitumia. Fikiria kidogo tu matukio ya wiki mbili na uongo ulivyosahaulika. Fikiria jinsi bunge na serikali eti vimeshindwa kuwashughulikia wahalifu kwasababu uchunguzi unaendelea. Fikiria kashafa na matukio kama ya gongo la mboto, kuzama meli yanavyopita bila mtu kuwajibika n.k.n.k.

Ni kwa muktadha huo nafasi adhimu na adimu tunashindwa kuzitumia ili kubadili mwelekeo wa nchi inayoelekea porini.
Nafasi iliyojitokeza hivi karibuni imenyakuliwa na genge la wahuni na sisi tupo kimya tukitegemea majaaliwa ya mwenyezi mungu.

Nasi hiyo ni ipi?
Inaendelea......
 
Back
Top Bottom