Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

... inaendelea
Nafasi ya kwanza ilikuwa kubadili muundo wa bunge kwa kuchgua watu wenye uchungu na nchi hii, watu wanaofikiri mtu anawezaje kuishi kwa dola moja.

Ni kwa kupitia bunge pengine tusingeona haya wanayoyafanya viongozi wa bunge hili.
Tumetoa nafasi kwa genge la wahuni kuendeleza mtandao wao wa kulindana ndani ya seikali, katika bunge, vyombo vya sheria na vyombo vya dola.

Laiti kama tungekuwa a bunge linaloweza kupiga kura ya hapana tusingeona bajeti ya vocha za simu za vijana wanaotongozana ikiwa ndiyo chanzo cha mapato. Tumewakabidhi CCM kwa hiari na kwa hila.

Nafasi ya pili ilikuwa ni pale dola ilipoelewa kuwa umma unataka mabadiliko, mabadiliko ya katiba ili tuwe na mfumo unaokidhi haja na matakwa yetu. Tukashangaa kuona wapinzani na wananchi wakikubali genge lile lile lifanye mabadiliko ya katiba. Hebu fikiri miaka 50 hawakutaka iweje leo watake?

Mimi binafsi nawalaumu sana viongozi wa vyama vya upinzani hasa CDM. Hakika walikuwa na 'mass support' ya wananchi kuhusu utengenezaji wa katiba mpya.

Sijui waliingia mkenge gani na kuruhusu mchakato huo uendelee tukijua dhahiri shahiri kuwa wale wasiotaka mabadiliko na waliotufikisha hapa hawawezi kutukwamua.

Nilionya sana na kusema tume ya katiba inayoundwa na Rais na Mwenyekiti wa CCM haiwezi kutupatia kitu mbadala, ni mazingaombwe tu ya kuchezehsa mikono ili tuamini kuwa karatasi imekuwa pesa.
Ni mazingaombwe kama alivyowahi kusema ndugu yangu Mzee Mwanakijiji.

Kuna watu wenye hoja kuwa katiba pekee haiwezi kuwa suluhisho. Mimi napingana nao kwasababu midhali tumeshindwa kulivunja genge hili la 'wahalifu' kwa njia nyingine ikiwemo sanduku la kura, hatuna sababu ya kupoteza miaka 10 zaidi tukisubiri maajabu. Tumeshapoteza miaka 50 kwanini tuendelee kupoteza mingine?
Mimibaba anasema muda si mshiriki mzuri kwetu na tumeshapoteza, kwanini tufikir kupoteza zaidi

Tanzania kwasasa hatuhitaji kufufua viwanda, kuendeleza kilimo, kuhubiri kuhusu nguvu kazi au matumizi ya rasilimali zetu. Hatuhitaji elimu wala uvuvi, madini au nishati. Vyote hivyo vimekwama kwasababu genge la wahalifu limeshika mpini na sisi tumeshika makali. Njia mojawapo ni kutumia nguvu ya umma ili tupate muongozo utakaondoa kimya kimya hili genge huku tukiijenga nchi.

Wizi na uporaji pamoja na uhuni mpya wa kuuana ulioanza kushika kasi siyo matatizo yetu ni dalili za tatizo letu ambalo ni kukosa mfumo utakaombana kila mmoja kuanzia yule Mwanakijiji anayeiba kuku, Waziri anayesaini mikataba ya wizi na mkuu anayetuamnisha kuwa 'huu ni upepeo tu' utapita.

Hivyo ndivyo China walivyoweza, ndivyo Japan wanavyofanya, na ndivyo Marekani wanavyoendelea.
Nchi yao haiongozwi na mtu mmoja aliyelundikiwa madaraka na kuyatumia vibaya.
Matokeo ya kuwa na mfumo mbovu ni kuwa na viongozi dhaifu serikali dhaifu na nchi hovyo! huo ni ukweli hata kama unauma. Hapa ndipo tulipokwama!

Nihitimishe hapa kwa kusema, tunahitaji katiba mpya na kwa tume iliyopo tumebofoa sana! Katiba inayotokana na sisi wananchi ingetuwezesha kupata wananchi wanaowajibika, bunge linalowajibika, serikali inayowajibika, vyombo huru vya sheria na dola. Hapo tungevunja uti wa mgongo wa genge linaloiumiza nchi. Tungeweka misingi ya utaifa na thamani za taifa ili kila achukuae dola ajue huo ndio muongozo kinyume chake ni out na sheria kuchukua mkondo wake.

Endapo tungefanikiwa kwa hilo basi tungeweza kukaa na kuamua mfumo gani tunaoona unafaa kwa mazingira yetu na wala si copy and paste ya Ubepari au Ujamaa.

Kisha basi, tungekaa na kuangalia ili twende mbele ni kipi tukipe kipaumbele na ni vipi tutumie rasilimali zetu kuwasadia wananchi wetu. Hapo ndipo tungejadili kuhusu Ujinga, maradhi na Umasikini. Tungejadili sekta ya afya, elimu, madini nk zinatusaidiaje kujikwamua.

Ninasikitika kusema kwa bahati mbaya fursa zote mbili tumeshindwa kuzitumia.
Bado tuna nafasi kidogo sana hata hivyo ya kuwa 'empower' wananchi wetu kuhusu tatizo halisi na si dalili.
Tuna nafasi ya kusema katiba inayotengenezwa si yetu ni ya Rais na CCM. Tunanafasi ya kuwaambia wapinzani (CDM) kitendo cha kukubali tume inayowajibika kwa Rais na CCM ni usaliti na warejee kwenye 'drawing board'.

Tuangalie tatizo na si dalili. Kuumwa kichwa na homa siyo tatizo la mgonjwa wa malaria, tatizo ni kuwa wadudu wa malaria wameshambulia mfumo wa kawaida wa mwili wa mwanadamu. Vivyo hivyo, kukwama kwetu kimaendeleo, umasikini, ujinga, maradhi, uporaji na wizi hayo siyo matatizo, tatizo letu ni mfumo mbaya wa utawala ulioshambulia mfumo wa nchi yetu. Suluhu ya kwanza ni kutengeneza mfumo mpya wa utawala kwa muongozo mpya unaotokana na sisi

Tusemezane
 
Wakuu Nguruvi na Mimibaba:
Niwapongeze kwa hoja nzuri sana. Naomba nami kuchangia....
1. Si kweli kwamba Ubepari na Ujamaa ni njia tu za watawala kutawala watu! Labda sijawaelewa, ila hii ni mifumo ya maisha iliyobuniwa kuendesha nyanja za kuu za maisha, yaani Siasa, Uchumi na Utamaduni! Nadhani inaeleweka kwa uwazi kabisa.
2. Kudai kuwa hakuna mfumo tunaoweza kusema ni dawa ya matatizo yote-ni kusema kuwa kuna matatizo hayapaswi kuchukuliwa hatua zozote-yaachwe tu. Huku ni kujidunisha na kukataa tamaa. (hata hvyo nashukuru mwishoni umetambua nafasi yetu)
3. Mkuu Nguruvi, umetolea mfano kuwepo kwa viashiria vya ubepari katika nchi za kijamaa, na vile vya kijamaa kwa nchi za kibepari. Hilo lisitufunge. Kama kuna kushoto na kulia, ni wazi kuna kitovu(katikati), kichwa(juu) na miguu(chini)!
4. Nakubaliana nawe kwa 100% kwamba tulikuwa na mifumo yetu iliyojikita katika mazingira yetu...tena na nyakati zilizokuwepo! Swali, mifumo iliyopo inasadifu hilo? Kama laa kwanini tuendele kuwalaumu viongozi hali wao wanatekeleza matakwa ya mfumo? TAFAKARI, TUSEMEZANE,TUCHUKUE HATUA.
5. Kundi dogo limekaa Zanzibar kwa maslahi yao, ni kweli lakini tusiache kutambua kuwa zilikuwa hila za mataifa makubwa. Wenzetu waliokaa Zanzibar, mimi nawaita Malimbukeni na Punguani kwani waliisaliti mantiki ya UTU nafsini mwao, kwa tamaa za mioyo yao au uvivu na ufinyu wao wa kufikiri.
6. Tusiwashangae wananchi kwa kukaa kimya na kuwaogopa watu waliowaweka madarakani! Mental Slavery! Tujiulize mizizi ya utumwa huu: dini zenu, elimu yetu, sanaa zetu, siasa zenu, n.k. Mfano tunaiona watu wanashinda na kulala kwenye kumbi za starehe, wanajaa kwenye viwanja vya mpira kuliko kwenye mijadala na mikutano ya maendeleo yao! Wapo pia wanaoshnda makanisani muda wa kazi, mnaita uhuru wa kuabudu, wapo wasioenda shule ila madrasa, n.k. Sio jambo rahisi, ni lazima tuumize vichwa!
6. Bunge kuwa sehemu ya soga, udaku, mizaha na upuuzi. Niliacha kufuatilia Bunge tangu mwaka jana, kikao cha bajeti! Ni zaidi ya kilabu cha pombe za kienyeji!
Je, kwani hatujui chanzo? Tulitegemea nini hali mfumo unadai wenye kura nyingi ndio mbunge? Si ndio hao sasa! Raia hamjui hata mgombea, hajui hata maana ya neno sera, hajala siku ya pili, ana maradhi yanamsumbua, umasikini unamuandama, ni mtumwa wa fikra, yeye mwenyewe hajiamini na amejidunisha, eti anapewa haki ya kuchagua, UNADHANI ZAIDI YA HISIA ZAKE KIPI KINGINE KITAMSUKUMA KUMCHAGUA MTU! Ndio wale tunaowaona bungeni, wote ni zao la hisia za watanzania! Demokrasia si mfumo sahihi kwetu, hamuelewi!
7. HAKIKA wepesi wetu wa kusahau ni silaha ya genge la kuangamiza nchi-na huo ndio UTUMWA WA KIFIKRA, hatusahau kabisa, ila TUNAJIDUNISHA-TUNAJIONA SI CHOCHOTE KATIKA KULETA MABADILIKO. Tumetengenezwa kuwa hivyo, dini, elimu, sanaa, vyombo vya habari, n.k. Mnaita UHURU-HAKI ZA BINADAMU-kumbe ni HILA ZA WAZUNGU.
8. Tunaacha nafasi za kufanya mageuzi zinapita!
(a) Nafasi ya kubadili muundo wa bunge kwa kuchagua wenye uchungu-demokrasia haiwezi kufanya hili.(sababu zipo hapo juu) vilaza watatawala bungeni milele na milele. Na kamwe huwezi pata bunge linaloweza kusema hapana, kwani ni zao la mfumo mbovu-demokrasia!
(kumradhi, natumia simu) itaendelea....
 
.....inaendelea!
8. (b) Nafasi ya pili Kubadili Katiba-kama hatufahamu kuwa chanzo cha uozo (unyonge wetu) ni mfumo, basi ni kazi bure kuhangaika na katiba. Katiba yoyote chini ya demokrasia basi ni lazima itafungwa na kanuni na HILA za demokrasia. Tukae chini tusemezane, tuambiane ipi ni namna bora ya juishi...tuiundie katiba! Hatuwezi kuyafanya mageuzi kama mchezo wa kugiza, ni lazima tuumize vichwa, sio kirahisi rahisi! Libya na Misri tunaziona. Mageuzi ufanikiwa kutokana na uelewa na utayari wa watu, vyote hvyo vinaweza kufundishwa vikaeleweka kwa watu! UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO.
9. Kuwalaumu CDM, kunaonesha tumaini lako lipo kwao! Lakini 100% hakuna chama cha siasa zilizopo, kinachoweza kuletd ustawi kwetu! CDM ni wanademokrasia, hivyo siasa zao na matendo yao ni lazima zifungwe na sera, taratibu na HILA za Demokrasia! Ukikubali kuolewa, sharti ulale bila nguo! Tunaona HILA ya Demokrasia ilivyotumika kumuondoa spika wa bunge, Sitta. CDM watafanya nini? Hiyo ndio Demokrasia-utashangaa nini. Wakadai ni Haki za Binadamu-Usawa wa Kijinsia-Uhuru wa Kuchaguliwa-Mwenye kura nyingi ndio mshindi-matokeo yake Bunge ni soga, udaku na porojo! Bado tu mnaiamini demokrasia? Hizi HESABU! Hutoki kama hutotaka kuumiza kichwa!
TUFANYE NINI?
Kuna haja ya kuwepo kwa AZIMIO JIPYA! Lisimikwe na wananchi wenyewe, na si viongozi, wanasiasa, wapinzani, viongozi wa dini wala wajiitao wanaharakati. Ni wananchi! Tufiki maazimio yetu, tuundie katiba yetu! UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO! Pamoja sana wakuu wangu!
Mungu wetu yu tayarai kutupigania, anaita sasa!
 
Mkuu Mkandara:
1. Kuamini kwamba maisha ni aidha Ujamaa ama Ubepari tu, ni kosa kubwa kwangu! Ni utumwa wa kifikra, ni kujidunisha. (Tafadhali, usinifunge na ujamaa, ubepari, biblia wala kuruan, ila MANTIKI-UTU, nikiuamini kama ndio msingi mkuu wa maisha)
Kusoma sana vitabu na marejeo si bora sana kama kuwa na tafakari yako mwenyewe ya juu ya mambo uyasikiayo, uyaonayo, na uyahisiyo. Nautaja ubepari si kufanyia reference, ila kwa kuwa ndio mfumo uliopo!
2. Kinyume cha Ubepari si Udikteta kama unavyodai. (a) Mbadala wa ubepari si ujamaa tu, UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO. Tukiumiza vichwa, tunaweza. (b) Ipi ni tafsiri ya udikteta, kumuamuru mtu kufanya kazi ndio udikteta? Unadhani amri zilikuwa zinatolewa kwa maslahi ya mtu binafsi au umma? Kipi ni bora kuzidi maslahi ya umma?
3. Umesema Usawa hauwezi kuwepo, kwani tumeumbwa na tamaa ya kupigania ukuu. Kwanza nikubaliane nawe kuwa tumeumbwa na tamaa, lakini tuliwekewa msingi mkuu wa kuongoza hizo tamaa zetu, nao ni UTU! Mantiki ya UTU i nafsini mwa kila mtu, awe mchawi, mwizi, jambazi, ama laa, UTU umo nafsini mwake! Kutokuuishi, ni kujisaliti! Je, kuna mtu anayetenda ovu pasi nafsi yake kumsuta (kujishtukia)? Ni wazi hayupo! Sasa, kama zipo sheria zimetungwa makusudi kulinda tamaa mbaya za watu, kwanini zishindikane za kulinda tamaa nzuri? TUMEKUBALI KUKARIRISHWA, TUNASEMA HAIWEZEKANI. Lakini si katika misingi ya UTU. UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO.
4. Ni wazi kabisa samaki hakunjwi akikauka tayari. Mfumo umemruhusu Obama kuwa juu, lakini wangeamua wenyewe kubuni mfumo ambao usingemkweza, na ingewezekana.

Katika pita pita yangu kuna neno hili "UPENDO" na sentensi hii, "FROM EACH ACCORDING TO HIS ABILITY, TO EACH ACCORDING TO HIS NEEDS" Marx na Engles... maana kubwa sana ya tafsiri ya maisha imebebwa humo!
Ukifuga manyigu usishangae manundu na kukosa asali. Kama tunaamini kabisa kuwa mfumo uliopo ni sahihi, basi tusilaumu wala kupayuka juu ya chochote kiovu tukionacho...kwani tutakuwa tumekubali kuolewa, sharti tulale........!
Mungu wetu anaita sasa!
Mimi naona matumizi ya lugha ndio tunaposhindana zaidi ya kutaka kunielewa. Ningeshukuru sana kaa ungeeleza kitu gani unakipinga na ukweli ni upi..

Nini maana ya UBEPARI kama sio njia kuu za Production and Distribution ziwe mikononi mwa watu binafsi?..Na je unapowanyima wananchi uwezo wa kumiliki na kuziweka chini ya serikali sii ndio Udikteta wenyewe au Udikteta una tafsiri tofauti na kuweka mamlaka ya kumili chini ya Utawala iwe Usultan au Ujamaa?..

Ukweli ni upi?.. Ukweli jni kwamba Kabla ya Kukoloniwa mataifa yote iwe Russia, America China au Afrika wananchi walikuwa na haki miliki yaani individual rights na muhimu zaidi PROPERTY RIGHT. Kila mtu, ukoo, kabila au nasaba walimiliki mali hadi ardhi zao lakini walipoingi wakoloni walinyang;anywa haki hizo. Wenyeji wakapoteza rights zao na kutawaliwa.

Ujamaa umetokana na fikra za kujikomboa toka dhulma hizi za milki kiuchumi, lengo lilikuwa kurudisha haki walizonyang'anywa wananchi ...Ujamaa ulikuja kuondoa Ukoloni ambao walikuja kutuibia na kutunyonya na hivyo kuturudishia haki hizo kama haki yetu..

Tatizo lilikuja pale tulipoweza kuwaondoa Wakoloni tulijikuta tuna mali nyingi sana walizokwisha wekeza, mali za ziada zisizokuwa zetu. Hapo ndipo wabunifu wa falsafa wakaja na kamba za Common ownership, ambapo uchuimi wa nchi unakuwa held indivisibly badala ya individuals. Viongozi wetu kuwa ma trustees wetu na kizazi kijacho. Tuka neutralise Mtaji tulotaifisha toka kwa wakoloni na kutaka kila mmoja wetu a participate kuendeleza kilichopo ili tugawane mavuno sawa.. Hapa macho yetu wote ni kwenye mali ya Mkoloni aloziacha na sio tena kila mmoja wetu arudishiwe mali zetu tulonyang'angwa na mkoloni.

Serikali ikachukua nafasi ya zuia hizo na ikaendelea kuzuia hadi mali zetu wenyewe. Tukarudi ktk kutawaliwa tena kiuchumi na hivyo nasema Ujumaa ukawa ndio Unyonyaji wa ndani..tukanyimwa Haki zetu in the name of protection - tukihofia Ukoloni na Ukoloni mamboleo yaani kunyonywa kutoka nje.

Kwa hiyo tunaogopa kunyonywa kutoka nje tumejikuta tunanyonywa toka ndani na hawa walojiita Wajamaa kama tulivyokuwa tukiibiwa wakati wa mkoloni.. Ujamaa ulitunyioma indivudual rights esp. property right, Ujamaa haukubaliani na individuals rights ama Collective ownership isipokuwa iloyokuwa controlled na serikali tu..Hakuna mtu ktk Ujamaa anahaki ya kumiki ardhi, ardhi ni mali ya serikali na ndio hadi kesho tunaambiwa hivyo..

Ni hayo tu mkuu wangu sina sababu ya kuupandikiza Ubepari jina zuri isipokuwa tuwe makini sisi wenyewe kuelewa nini hasa maana ya Ubepari na kwa nini tunaipiga vita wakati kihaki Lillah kila mmoja wetu angependa turudi katika asili yetu ya kumiliki ardhi na mali bila kunyonyana..
 
JingalaFalsafa,
Hakuna mfumo tunaowweza seama ni panacea ya matatizo ya mwanadamu katika mataifa yaliyopo

Nimetoa mifano ya wakubwa wa dunia hii wanavyohangaika sasa kutafuta middle point.
Labda nikupe mifano ya hapa nyumbani Afrika mashariki. Hivi niambie ni nchi gani iliyobora kutokana na kufuata mikondo ya siasa za mrengo wa kulia au kushoto.

Tanzania ilikuwa inaegemea bawa la kushoto, Kenya na Malawi zikiwa bawa la kulia, sasa nipe tofauti za umasikini, ujinga, maradhi katika nchi hizo.

Hoja ya pili ni kuhusu CDM. Hakika sikuwa nimedhani kuwa CDM ndio wanaoweza kuleta mabadiliko.
Siku zote nimekuwa nikiamini kuwa mabadiliko ya kweli yanaletwa na wananchi wenyewe.
Lakini pia lazima uelewe kuwa mabadiliko si mkusanyiko wa watu au vurugu, ni lazima yaratibiwe katika utaratibu unaoeleweka. Suala la tume huru ya katiba lilikuwa ni duku duku la wananchi na wanaharakati.
Kwa bahati nzuri CDM walilichukua kama sehemu ya ilani ya uchaguzi wakisema ndani ya siku 100 utaratibu wa katiba mpya ungewekwa wazi.

CDM kwa kupitia wananchi wakaweka shinikizo lililowalazimu watawala wafikirie upya.
Hadi hapo wananchi wakaona CDM inawakilisha kiu yao na kupitia wao ambao wana nguvu ya kisiasa, mabadiliko tarajiwa yangefikiwa.Ukweli ni kuwa JK hakutishwa na CDM alitishwa na nguvu ya umma iliyokuwa nyuma ya CDM.

Naweza pia kusema hata wananchi walikosea kuwaamini wanasiasa.
Tukaona CDM wakienda Ikulu wakitoka na tabasamu, ghafla wakijawa na hasira na simanzi.
CDM walipaswa kumwelewa Kikwete mapema sana. Tahadhari nyingi zilitolewa na wao hawakuzizingatia.

Unajua suala hili lilopochukuliwa na chama cha upinzani tayari wananchi walikuwa wamefungwa mikono kisheria. Lolote nje ya utaratibu wa kisiasa lilikuwa ni vurugu kama wanavyodai. Kwahiyo CDM lazima ikubali jukumu la kushindwa kuwapatia wananchi kile walichokusudia na kujikuta wameingia katika mtego wa kisiasa.
 
JingalaFalsafa,
Hakuna mfumo tunaowweza seama ni panacea ya matatizo ya mwanadamu katika mataifa yaliyopo

Nimetoa mifano ya wakubwa wa dunia hii wanavyohangaika sasa kutafuta middle point.
Labda nikupe mifano ya hapa nyumbani Afrika mashariki. Hivi niambie ni nchi gani iliyobora kutokana na kufuata mikondo ya siasa za mrengo wa kulia au kushoto.

Tanzania ilikuwa inaegemea bawa la kushoto, Kenya na Malawi zikiwa bawa la kulia, sasa nipe tofauti za umasikini, ujinga, maradhi katika nchi hizo.

Hoja ya pili ni kuhusu CDM. Hakika sikuwa nimedhani kuwa CDM ndio wanaoweza kuleta mabadiliko.
Siku zote nimekuwa nikiamini kuwa mabadiliko ya kweli yanaletwa na wananchi wenyewe.
Lakini pia lazima uelewe kuwa mabadiliko si mkusanyiko wa watu au vurugu, ni lazima yaratibiwe katika utaratibu unaoeleweka. Suala la tume huru ya katiba lilikuwa ni duku duku la wananchi na wanaharakati.
Kwa bahati nzuri CDM walilichukua kama sehemu ya ilani ya uchaguzi wakisema ndani ya siku 100 utaratibu wa katiba mpya ungewekwa wazi.

CDM kwa kupitia wananchi wakaweka shinikizo lililowalazimu watawala wafikirie upya.
Hadi hapo wananchi wakaona CDM inawakilisha kiu yao na kupitia wao ambao wana nguvu ya kisiasa mabadiliko tarajiwa yangefikiwa.Ukweli ni kuwa JK hakutishwa na CDM alitishwa na nguvu ya umma iliyokuwa nyuma ya CDM.

Naweza pia kusema hata wananchi walikosea kuwaamini wanasiasa.
Tukaona wakienda Ikulu wakitoka na tabasamu, ghafla wakijawa na hasira na simanzi. CDM walipaswa kumwelewa Kikwete mapema sana. Thadhari nyingi zilitolewa na wao hawakuzizingatia.

Unajua suala hili lilopochukuliwa na chama cha upinzani tayari wananchi walikuwa wamefungwa mikono kisheria. Lolote nje ya utaratibu wa kisiasa lilikuwa ni vurugu kama wanavyodai. Kwahiyo CDM lazima ikubali jukumu la kushindwa kuwapatia wananchi kile walichokusudia nma kujikuta wameingia katika mtego wa kisiasa.

Nguruvi3, mtazamo wangu kwenye hili la katiba mpya na CDM ni kwamba heri nusu shari kuliko shari kamili. Na nakubaliana na hoja yako kwamba JK aliona mood ya wananchi iko upande wa CDM zaidi na hivyo kwenda opposite direction lisingekuwa jambo la busara.

Hata hivyo round ya kwanza ya muswada ilitoa 'hint' nia ovu na ujanjaujana wa CCM katika kuandaa katiba inayokidhi matakwa ya wananchi. Nafasi ya CDM kuonana na Jk ikulu iliboresha muswada kwa kiasi fulani lakini bado mambo mengi yamefumbiwa macho. Kama CDM wangeendelea kuweka brake kwenye round ya pili ya muswada there was a possibility process nzima ya kuandaa katiba mpya kuchelewa, wakubwa wangeanza kupiga danadana kwa kisingizio kuwa CDM wamekuwa kikwazo na risk yake ingekuwa kwenda kwenye uchaguzi 2015 kwa katiba ya sasa.

Na hapa ndipo nasema heri nusu shari kuliki shari kamili. Katiba inayoandaliwa sasa hivi itakuwa na matatizo mengi, lakini kuendelea kuwa na hii katiba ya sasa ni mbaya zaidi.

Jambo ambalo CDM wanaweza kusaidia kwa sasa ni kuongoza wananchi ili walau tupate 'minimum' toka kwenye hiyo katiba mpya moja ikiwa ni tume huru ya uchaguzi, police reform, mahakama huru na separation ya excutive na parliment. Tukiweza kupata hivyo, basi tutakuwa tumeanza safari nzuri ya kupata katiba mpya. Nasema safari kwa sababu katiba ya sasa kwa vyoyote vile itahitaji marekebesho makubwa within the next 4 fours. CCM pamoja na minyukano na mitandao mingi ya ndani bado hawawezi kutoa katiba ya watanzania, watatoa katiba ya CCM tu.
 
JingalaFalsafa,
Naomba unifafanunulie ikiwa ubepari na ujamaa si mifumo iliyobuniwa kutawala watu je hao waliobuni waliibuni kwa madhumuni gani? Kimsingi ukisoma historia ya mifumo hii iliasisiwa ili kuendesha maisha ya kila siku; Ujamaa na ubepari ni siasa, na siasa ndiyo inayotawala maisha yetu ya kila siku.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkandara;
Jaribu kufanya marejeo ya udikteta kuweka umiliki njia kuu chini ya serikali husika si udikteta; vipo vitu huwezi kuweka umiliki wake chini ya watu binafsi; na ndiyo sababu serikali kwa njia yoyote ile ni lazima iwe na mkono mathalani Marekani tumesema ndiyo mabepari lakini katika mfumo wao 20% ya njia kuu za uzalishaji inamilikiwa na serikali, na hata kwenye hiyo 80% bado serikali inatumia sheria na idara mbali mbali ilizounda ili ku control wamiliki wa hizo njia kuu za uzalishaji.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu Mkandara:
1. Hakuna apingae kuwa matatizo yetu yametokana na mfumo! Nachopinga ni kuamini ama kuaminisha watu kuwa ukombozi unaweza kuletwa na mfumo huo huo ulioleta machungu! Ni kupoteza muda! Ukweli ni huu: Mfumo sahihi ni lazima usadifu mazingira na nyakati za eneo mahususi. Tuna nafasi ya kuleta mabadiliko, kwa kukaa chini, wewe na mimi, tukapasua na tukaumiza vichwa, tukabuni mfumo unaosadifu maisha ya eneo letu! Hilo linawezekana ila tu ni kwa kuacha roho za ubinafsi za kujifikiria sisi, ila kizazi chetu kijacho. Tumeshazikwa hai na ubepari, tuwaepushe watoto wetu!
2. Ni kweli kuwa ubepari ni mahusiano ya kijamii na njia za uzalishaji mali...yaliyojikita katika falsafa ya umimi-ubinafsi. Kwangu mimi, msingi mkuu wa maisha ni UTU, ubinafsi ni sumu ya UTU. Kwa hiyo ndani ya Ubepari hakuna UTU...haufai.
3. Mkuu, tafsiri ya udikteta kwangu ni pale serikali yoyote inapofanya maamuzi ama vitendo vyake kwa kutozingatia misingi ya Haki za Binadamu, yaani kama demokrasia na uhuru. Ni Non-democratical actions taken by a govt. Ni upuuzi tu! Kama vile mababu zetu wenye hekima walipokufa wazungu walisema wanageuka kuwa "mizimu" hali wao ni "watakatifu" ni kuhalalisha hila na uovu wao! Ndio maana nasema "demokrasia ni mtego tu"
Gharama ya kulinda msingi mkuu wa maisha-UTU, haifananishwi na kitu chochote chini ya jua, hata uhai wa mtu...sembuse uhuru wa mtu kutekeleza tamaa na hisia zake? Pima mwenyewe, kati ya Usawa na Haki bora nini? UTU kwanza!
Mkuu Nguruvi3:
1. Ni wazi kuwa hakuna tangu uhuru nchi zetu zinajiangaisha na ubepari na ujamaa, lakini kila kona ni unyonge! Na ndio maana nasema "kuna haja za kuwa na namna yetu ya kuishi" UBUNIFU HAUJAWAI KUFIKA MWISHO!
2. Ni kweli mabadiliko lazima yaratibiwe kwa taratibu maalumu, sio kukurupuka. Na katika hilo, hatua ya kwanza kabisa ni kukomboa fikra zetu! Niambie, katiba mpya itawezaje hilo hali inafungwa na kanuni, taratibu na hila za mfumo mbovu uliopo? Kuichukia Demokrasia, simaanishi kuwepo kwa vita ya mapanga, ila ni mapigano ya akili-kichwani.
3. Pia ni kweli wananchi walikosea sana kuwaamini wanasiasa. Lakini tusisahau "Mental Slavery" vichwani mwao, mapenzi yao na hisia zao ndizo ziwaongozazo, hawajali MANTIKI. Na hayo ni matokeo ya mnachoita Haki za Binadamu. Ni mitego, akili nyingi sana kukubali japo inaonekana!
Mkuu Chama:
Nimekupata vizuri mkuu, ujamaa na ubepari hauna kingine ila kutawala nyanja za maisha za binadamu uchumi, siasa, na tamaduni. Sentensi ya kwanza ilisema kuwa ubepari na ujamaa ni njia za watawala kuwatawala watu, ndio maana nikapinga, kwani ni zaidi ya watawala na watawaliwa. Nadhani nimekuelewa mkuu.
Mungu wetu anaita"
 
Nguruvi3, mtazamo wangu kwenye hili la katiba mpya na CDM ni kwamba heri nusu shari kuliko shari kamili. Na nakubaliana na hoja yako kwamba JK aliona mood ya wananchi iko upande wa CDM zaidi na hivyo kwenda opposite direction lisingekuwa jambo la busara.

Hata hivyo round ya kwanza ya muswada ilitoa 'hint' nia ovu na ujanjaujana wa CCM katika kuandaa katiba inayokidhi matakwa ya wananchi. Nafasi ya CDM kuonana na Jk ikulu iliboresha muswada kwa kiasi fulani lakini bado mambo mengi yamefumbiwa macho. Kama CDM wangeendelea kuweka brake kwenye round ya pili ya muswada there was a possibility process nzima ya kuandaa katiba mpya kuchelewa, wakubwa wangeanza kupiga danadana kwa kisingizio kuwa CDM wamekuwa kikwazo na risk yake ingekuwa kwenda kwenye uchaguzi 2015 kwa katiba ya sasa.

Na hapa ndipo nasema heri nusu shari kuliki shari kamili. Katiba inayoandaliwa sasa hivi itakuwa na matatizo mengi, lakini kuendelea kuwa na hii katiba ya sasa ni mbaya zaidi.

Jambo ambalo CDM wanaweza kusaidia kwa sasa ni kuongoza wananchi ili walau tupate 'minimum' toka kwenye hiyo katiba mpya moja ikiwa ni tume huru ya uchaguzi, police reform, mahakama huru na separation ya excutive na parliment. Tukiweza kupata hivyo, basi tutakuwa tumeanza safari nzuri ya kupata katiba mpya. Nasema safari kwa sababu katiba ya sasa kwa vyoyote vile itahitaji marekebesho makubwa within the next 4 fours. CCM pamoja na minyukano na mitandao mingi ya ndani bado hawawezi kutoa katiba ya watanzania, watatoa katiba ya CCM tu.

JFM
Katika hili la katiba Chadema walikuwa wanapigania maslahi ya watanzania au maslahi yao kichama? Kwasababu sikumbuki ni lini Chadema wallitisha majadiliano na watanzania kuzungumzia mabadiliko ya katiba; na katika hayo walioyoenda kuyadili ikulu; yalikuwa na usiri gani? Kwasababu kama walikuwa wanapigania maslahi ya watanzania wangeweka bayana ni lipi wanalokwenda ongea na mh. Raisi; Chadema ni kukikundi tu cha watu ambao hawawakilishi maoni ya kila mtanzania; na haki haipiganiwi nusu nusu; ni afadhali kuendelea kupigania hicho unachodai ni haki yako kuliko kupigania nusu ambayo huna uhakika kama hata hiyo nusu yenyewe utaipata.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkandara;
Jaribu kufanya marejeo ya udikteta kuweka umiliki njia kuu chini ya serikali husika si udikteta; vipo vitu huwezi kuweka umiliki wake chini ya watu binafsi; na ndiyo sababu serikali kwa njia yoyote ile ni lazima iwe na mkono mathalani Marekani tumesema ndiyo mabepari lakini katika mfumo wao 20% ya njia kuu za uzalishaji inamilikiwa na serikali, na hata kwenye hiyo 80% bado serikali inatumia sheria na idara mbali mbali ilizounda ili ku control wamiliki wa hizo njia kuu za uzalishaji.

Chama
Gongo la mboto DSM
Unachozungumza ni sawa kabisa na hapo ndipo tunaweza jiuliza zaidi ni kwa kiasi gani serikali inatakiwa kuendesha NJIA KUU ambazo ni msingi wa maendeleo ya nchi na nadhani hata wakati wa utawala wa watemi wetu kulikuwepo na key segments ambazo zilishikiliwa na Mtemi ktk maendeleo ya Utawala wake kimaendeleo.
Kila nchi ina Commanding Heights zake zinazotakiwa kuwa chini ya serikali, naaamini kabisa kwamba hizi key segments of the national economy lazima ziwe mikononi mwa serikali maana sii jambo la mtu mmoja.

Sidhani kama kuna mtu anaweza kuchimba gas Songos, kuejnga reli, Bandari, Tanesco, Kiwila na kadhalika hivi ni vitu vinavyohitaji serikali kuweka dhamana yake tupatiwe mkopo ama kuwezeshwa. Hata Marekani kama ulivyosema wameshikilia hizo asilimia 20 kwa sababu hizi ni Commanding heights zao zinazohitaji nguvu ya serikali na sio watu binafsi kuzisimamisha lakini maajabu ya wajamaa wetu kina Mao hawa walishika kila kitu wakakaba hadi mkono uendao kinywani tukahesabiwa matonge.

Tatizo nilokuwa nalo mimi ni pale napoelewa kwamba Ujamaa ulikuwa nguvu ya pamoja kumondoa mkoloni ili turudishiwe kile tulochopoteza nacho ni individual rights..Right of private ownership iwe ardhi, shamba, mifugo, na properties nyinginezo as means of production tulimiliki sisi wenyewe. Ujamaa ulikuwa solution ya Ukoloni na tuliweza kuwaondoa kweli lakini ajabu ni kwamba Sii Russia, China au Cuba kote Ujamaa uliwaweka tena wananchi wake ktk kifungo kingine cha ndani kina Mao, Lenin na Castro wakijirundikia nguvu kubwa sana ambayo hata wananchi wenyewe walianza kujenga heshima ya woga badala ya kuwapenda..

Kwa hiyo nakuelewa vizuri Chama, na siitegemei kusikia mtu binafsi waliwahi kumiliki barabara, maziwa, mito na visima cha maji na usambazaji wake, wala sidhani kama kulikuwa na watu walimiliki mapori ya kuchungia ng'ombe ktk malisho hizi zilikuwa mali za Utawala.. Pia binafsi yangu kwa kutazama watu namazingira yetu naweza sema huduma zote muhimu (Maji, Umeme, Afya na Elimu) lazima zibakie chini ya serikali lakini muhimu wananchi warudishiwe kile walichopigania Uhuru kumwondoa mkoloni - Individual rights..
 
JFM
Katika hili la katiba Chadema walikuwa wanapigania maslahi ya watanzania au maslahi yao kichama? Kwasababu sikumbuki ni lini Chadema wallitisha majadiliano na watanzania kuzungumzia mabadiliko ya katiba; na katika hayo walioyoenda kuyadili ikulu; yalikuwa na usiri gani? Kwasababu kama walikuwa wanapigania maslahi ya watanzania wangeweka bayana ni lipi wanalokwenda ongea na mh. Raisi; Chadema ni kukikundi tu cha watu ambao hawawakilishi maoni ya kila mtanzania; na haki haipiganiwi nusu nusu; ni afadhali kuendelea kupigania hicho unachodai ni haki yako kuliko kupigania nusu ambayo huna uhakika kama hata hiyo nusu yenyewe utaipata.
Chama, Gongo la mboto DSM
Mkuu Chama ndio maana nikasema hata wananchi walifanya makosa kudhani CDM wangeweza kuendeleza harakati.

Lakini pia inabidi tuwape wananchi benefit of doubt kwa hili kwasababu baada ya kilio cha miaka mingi waliambiwa hapana. Miongoni mwa watu waliokataa katiba mpya ni Jaji Joesph Sinde Warioba aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali. Mwingine ni Andrew Chenge na Damian Lubuva.

Kilichowabana wananchi ni mahali pa kusemea kwasababu kwa utaratibu wa hovyo uliopo, hoja ni lazima iletwe bungeni. Bungeni kumejaa CCM wanaobaki kusema ndiooo miaka 50 sasa.

Watanzania hawana utaratibu wa kuingia mitaani, jambo linalowagharimu kwa baadhi ya nyakati hata kama ni utaratibu mzuri. Kwa hiyo fursa ya CDM ilipojitokeza ilikuwa kama 'platform' ambayo wananchi wangeweza kuingia mitaani kama watawala wangegoma. CCM wakaliona hilo mapema.

Kinachoshangaza hoja hii ya CDM ikatekwa nyara na CCM na CDM wakabaki kushangilia.
Hotuba ya JK ya mwezi december 2011 iliungwa mkono na upinzani kupitia Mbowe.
Kuanzia hapo wote wakaka kimya wakisubiri JK aweke mipango sawa.

Walishtukizwa walipogundua kuwa ilikuwa ni suala la photocopy ya katiba iliyokuwepo. Hapo wakachachamaa tena wakiungwa mkono na wananchi. Fursa hii ikapotea pale walipokwenda Ikulu na kutoka bila kusema wamejadiliana nini.

Kuanzia hapo tukaona mamlaka ya JK yakiwa makubwa sana. Fikiria, hivi kwanini tume iwajibike kwa rais?
Kama ulipitia mswada mzima wa kuundwa kwa tume ni dhahiri kuwa Jaji Warioba anaripoti kwa JK kuhusu maoni ya wananchi.Yaani Warioba aliyepinga katiba akiwa mwanasheria mkuu anaripoti kwa JK wa CCM isiyotaka katiba mpya!
Hapa ni nini kama si mazingaombwe.

Kwahiyo CDM walipoteza dhamana na fursa waliopewa na wananchi. Hii ilikuwa fursa muhimu kwa CDM kuonyesha kuwa wapo tayari kuuongoza umma wa Watanzania. Hawakuitumiafursa hiyo kikamilifu na imeacha maswali mengi yasiyojibiwa.

Hii pia inaendelea kujibu hoja nzito za Mimibaba kuwa tumekwama wapi na tuafanye nini. Kwa mtazamo wangu hapa ndipo tulipokwama. Narudia matatizo yetu ni matokeo ya mfumo mbovu unaozaa udhaifu wa uongozi.
Hadi tutakapokuwa na utaratibu wa kuendesha nchi kwa mipango na uongozi wa katiba mpya hatutaweza kujikwamua hata kidogo. Si kwa eneo lolote lile. Ndiyo maana nimeelezea hoja ya Mimibaba kuwa hapa ndipo tulipokwama na ndipo suluhisho linatakiwa lianzie.

Sasa wakati Mimibaba na ninamuunga mkono, anaposema muda si mshiriki wetu mzuri wa kufanya maamuzi na kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na hoja za mfumo gani unatufaa kama zinavyojadiliwa vema na Mkandara na JingalaFalsafa,
hutuwezi na hatuna nafasi ya kukubali nusu glass( half a glass) ya matumaini ya baadaye.
Hivyo Mkuu FJM kukubali nusu glass ni sawa na mwanamke kusema ' She has little pregnancy'.
Sidhani kuwa kuna kitu kinaitwa kamimba kidogo tu, ni ima mimba au hakuna mimba.

CDM lazima wakubali kuwa wameuchuuza umma kwa kiasi fulani na imeondoa credibility ya chama kwa kiasi fulani kwa kukubali nusu glass ya maziwa. Huu ni ukweli usio na utamu lakini tuite spade as spade and not a big spoon!
 
Unachozungumza ni sawa kabisa na hapo ndipo tunaweza jiuliza zaidi ni kwa kiasi gani serikali inatakiwa kuendesha NJIA KUU ambazo ni msingi wa maendeleo ya nchi na nadhani hata wakati wa utawala wa watemi wetu kulikuwepo na key segments ambazo zilishikiliwa na Mtemi ktk maendeleo ya Utawala wake kimaendeleo.
Kila nchi ina Commanding Heights zake zinazotakiwa kuwa chini ya serikali, naaamini kabisa kwamba hizi key segments of the national economy lazima ziwe mikononi mwa serikali maana sii jambo la mtu mmoja.

Sidhani kama kuna mtu anaweza kuchimba gas Songos, kuejnga reli, Bandari, Tanesco, Kiwila na kadhalika hivi ni vitu vinavyohitaji serikali kuweka dhamana yake tupatiwe mkopo ama kuwezeshwa. Hata Marekani kama ulivyosema wameshikilia hizo asilimia 20 kwa sababu hizi ni Commanding heights zao zinazohitaji nguvu ya serikali na sio watu binafsi kuzisimamisha lakini maajabu ya wajamaa wetu kina Mao hawa walishika kila kitu wakakaba hadi mkono uendao kinywani tukahesabiwa matonge.

Tatizo nilokuwa nalo mimi ni pale napoelewa kwamba Ujamaa ulikuwa nguvu ya pamoja kumondoa mkoloni ili turudishiwe kile tulochopoteza nacho ni individual rights..Right of private ownership iwe ardhi, shamba, mifugo, na properties nyinginezo as means of production tulimiliki sisi wenyewe. Ujamaa ulikuwa solution ya Ukoloni na tuliweza kuwaondoa kweli lakini ajabu ni kwamba Sii Russia, China au Cuba kote Ujamaa uliwaweka tena wananchi wake ktk kifungo kingine cha ndani kina Mao, Lenin na Castro wakijirundikia nguvu kubwa sana ambayo hata wananchi wenyewe walianza kujenga heshima ya woga badala ya kuwapenda..

Kwa hiyo nakuelewa vizuri Chama, na siitegemei kusikia mtu binafsi waliwahi kumiliki barabara, maziwa, mito na visima cha maji na usambazaji wake, wala sidhani kama kulikuwa na watu walimiliki mapori ya kuchungia ng'ombe ktk malisho hizi zilikuwa mali za Utawala.. Pia binafsi yangu kwa kutazama watu namazingira yetu naweza sema huduma zote muhimu (Maji, Umeme, Afya na Elimu) lazima zibakie chini ya serikali lakini muhimu wananchi warudishiwe kile walichopigania Uhuru kumwondoa mkoloni - Individual rights..

Mkuu Mkandara,
Matatizo tuliyo nayo Tanzania hayatokani na sera tulizokuwa nazo za ujamaa; kimsingi kuna za Afrika ambazo zilishabikia na kuukumbatia mfumo wa ubepari na leo hii zina matatizo makubwa ya kiuchumi kuliko Tanzania; matatizo makubwa yanayotukabili ni viongozi na wananchi kutokuheshimu misingi ya sheria; hata matatizo ya kiuchumi yanayozikabili nchi nyingi za magharibi ni watawala kutoheshimu misingi ya sheria ya ubepari; ujamaa ndiyo uliyoifanya Russia iwe ile ilivyo leo, huwezi kuyataja mafanikio ya kiuchumi ya China bila kumtaja Mao; hata Cuba bado kina Castro wanaheshimika kwasababu moja tu walianzisha mifumo ya ujamaa na wao wakaishi kama wajamaa; ubaya unakuja pale unapohubiri ujamaa wakati unaishi kibepari. Tatizo linatukabili si ujamaa wala ubepari ni viongozi kutokufuata na kuheshimu misingi ya sheria zilizopo. Kimsingi Tanzania kama nchi siasa za kibepari haziwezi kutuletea maendeleo kwa sababu nchi yetu ni masikini na hatuna matajiri wenye uwezo wa kuwekeza; labda kama tunataka kuiweka rehani nchi yetu; kama tungekuwa na matajiri wa kweli nadhani hata hizi ajali za meli zingekuwepo; ujamaa ulisisitiza zaidi kilimo; ukiangalia historia ya dunia mapinduzi ya kilimo ndiyo yaliyokuwa chachu ya mapinduzi makubwa ya kiuchumi; hata nchi za kibepari zinaendeleza sera za kilimo pamoja na kuwa tayari zimeshafanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi; Tanzania tumejiingiza kwenye mtego wa ukosefu wa ajira kwa sababu ya kutupilia mbali sera za kilimo, mkoloni aliweza kuweka miundo mbinu kwasababu aliheshimu sheria zilizokuwapo wakati huo; hivi sasa tupo huru hataufaidi matunda ya uhuru wetu kwasababu tumeshindwa kuheshimu sheria zetu. Mkuu hebu nifafanulie ni individial rights zipi unazozikosa sasa hivi? kwa sababu kumpiga mtu uliyemfumania na mkeo pia inaingia kwenye individual rights naomba ufafanue zaidi.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu Chama,
Nakubaliana nawe kuwa tatizo letu si ujamaa au ubepari! ni kuchanganyikiwa.
Yaani hatujielewi tunakwenda wapi au tunatoka wapi. Ni sawa na meli ndani ya bahari kuu inayoelea bila dira, ikitegemea upepo.

Huwa nasema kama ujamaa ni mbaya tuangalie Kenya na Malawi kwa ukaribu halafu tujiulize uzuri wa ubepari ni upi? Sina maana ya kusema ujamaa ni mzuri ninaweka point tu kuwa si ujamaa au ubepari ambao ni suluhisho la matatizo.

Umeongelea jambo moja tusilopenda kulisema, ambalo ni nidhamu. Sisi hatuhitaji kitu kingine zaidi ya nidhamu!
Nidhamu inajengwa kwa kuwa na mwongozo.

Mwongozo wetu ambao ndio katiba imetengenezwa kiasi kwamba ni kikundi cha watu wachache wanaoweza kuamua nini cha kufanya au kutofanya na sisi wananchi hatuna la ziada.

Mathalani, katika miaka 5 iliyopita Tanzania imepoteza pesa nyingi sana zaidi ya bajeti ya mwaka 1 wa fedha, kwa wizi, uporaji, misamaha ya kodi, ubadhirifu katika taasisi na mashirika n.k.

Fikiria ni hatua gani za kinidhamu zimechukuliwa dhidi ya wahusika. Kinyume chake wamekuwa wakipewa ulaji sehemu nyingine na kuendelea kulindana.
Sababu kubwa ni kuwa genge lina kitu kinachowalinda, kwamba wao wana sheria na wana umiliki wa mamlaka za nidhamu.

Angalia nchi zote zilizopiga hatua, kitu cha kwanza walichonacho ni nidhamu iliyojengwa katika misingi iliyokubaliwa na taifa na hapa nasema ni katiba.

Ninachotaka kusema ni kuwa kama hakuna nidhamu ya uongozi wa taifa kwa mwongozo wa taifa unaotokana na wananchi basi kuongelea umasikini, ujinga na maradhi ni kujidanganya.
Ndipo narudi kwa swali la Mimibaba kuwa tuanzie wapi? Nasema tutengeneza mwongozo utakaowazuia akina 'Makova' kuendelea kutudanganya miaka mingine 50.

Kwa bahati mbaya mwanya wa kutengeneza kitu hicho umeporwa na makova ili 'wakovalize'.
So sad!
 
Chama,
Maneno yako msumari na kuhusu Ujamaa lakini bado kidogo sana hamjanielewa..Nachosema mimi kuna maadui wetu wakubwa nao ni Ukoloni, Ukoloni Mamboleo na Ubeberu. Hawa ni maadui wa uchumi wa nchi zetu maskini lakini haipotezi umuhimu wa haki ya wananchi kumiliki njia za kiuchumi.

Asili ya Ujamaa haswa ilikuwa kupambana na haya maswala matatu sio Ubepari maana tulikuwa mapebari kabla ya kukoloniwa. Tatizo la Ujamaa na kwa nini tumeshindwa kwenda mbele ni kwamba Ujamaa umeshindwa kuwarudishia wananchi haki hiyo. Tumetoka ktk kupambana na ukoloni, tukaziba hata wananchi wenyewe kurudi ktk asili yao na kibaya zaidi leo tunaukaribisha ukoloni mamboleo kwa mikono miwili. Ujamaa was meant to protect us from them..Hivi leo hatuna tena Ujamaa labda vitabuni..

Matatizo ya nchi za Ulaya leo hii sio Ubepari in such isipokuwa kwa kushindwa kuendeleza Ukoloni mamboleo na Ubeberu... Katika kila zuri kuna mabaya yake hata iwe mapenzi kuna watu wanakufa kwa mapenzi, wanaongopa kwa mapenzi, wanajitajirisha kwa mapenzi, lakini haina maana mapenzi ni kitu kibaya, hii ni nature na haki ya kila kiumbe.. na labda nirudie tena kusema Ujamaa haukuja kuondoa Ubepari hapana, isipokuwa ulikuja kuondoa Ukoloni, Ukoloni mamboleo na kadhalika the Outside forces zilizokuja chukua chetu..Haihusiani kabisa na Mtanzania kuwa bepari maana tulikuwa mabepari before ila walipoingia wageni walichukua nguvu zetu za kiuchumi na Ujamaa ukasema tutakomesha kunyonywa, kuibiwa na kukandamizwa kiuchumi.

Leo hii Huko Ulaya wanaathirika kiuchumi sii kwa sababu ya Ubepari (watu kumiliki njia za uzalishaji) hapana isipokuwa ni kwamba Ukoloni mamboleo ulowawezesha kuzijenga nchi zao umewafikia wakati mgumu sana kwao kuziibia nchi za nje. Mataifa kama Greece, Spain, Italy, Portugal ni mataifa ambayo yalijengwa kwa Ukoloni na ubeberu lakini yameshindwa kutokana na kwamba wao wenyewe hawana meno tena ya Wakoloni mamboleo wala mabeberu. hawana nguvu ya Kijeshi, fedha, ushawishi ktk Technologia na kadhalika kuendelea kunyonya nchi maskini.

Tunachoshuhudia leo ni kuanguka kwa ukoloni mamboleo hasa kwa wale wanaoshindwa kujenga jeshi la kuendelea kunyonya mataifa mengine. Leo hii Nchi hizo wamekuwa tegemezi wao wenyewe sasa hivi wamefikia kunyonywa na kuwa soko la nchi matajiri. Tazama wanakopeshwa fedha ili iweje? kuziwezesha benki zao zi function na sii wananchi wake wapate ajira ama maisha bora..Hii siii kwa sababu ya Ubepari isipokuwa ni matokeo ya Ukoloni mamboleo pale simba anapokosa meno.

Kwa nchi maskini zinazoendelea kunyonywa zinadhoofika kiuchumi, na nchi tajiri zinazokosa meno ya kunyonya (hizo greece, Italy, Spain na Portugal) nazo zinadhoofika kiuchumi na zita collapse kiuchumi kwa sababu wanaingia ktk kundi la kunyonywa badala ya kuwa wanyonyaji..They lived by sword now they are dying by the sword..Sijui umenielewa hapo!

Adui wetu sisi alikuwa Ukoloni na sasa hivi ni ukoloni mamboleo, ubeberu na kadhalika na Ujamaa tunauhitaji kifikra kutulinda ktk maswala haya ya kutawaliwa na nguvu toka nje, lakini sio kwamba Ujamaa ulitakiwa kupambana na Ubepari - hapana. Kwa nini tunaita ukoloni mamboleo ndio Ubepari? kwa sababu wakoloni wote walitumia Ubepari ndani ya nchi zao na hatukupenda walotufanyia.. Wee subiri siku tukijua athari za Ukoloni mamboleo zikifanywa na Wachina sijui tutasema nini? maana tunawakaribisha tukidhani wao nafuu bila kujua kwamba adui wa Ujamaa wetu ni Ukoloni mamboleo..

As to say Mimi Mkandara kama nitakuwa mshenzi wa Tabia na ukajua huyu ni Muislaam basi kuna uwezekano mkubwa ukauchukia hata Uislaam wakati Uislaam haufundishi hivyo. Wakati Waturuki walipoivamia Ulaya walitumia Uislaam kama shahada ya kuziteka nchi hizo na wazungu waliuchukia Uislaam. Na baadaye Wakatoliki wakaziteka nchi kwa kutumia Ukatoliki (Crusaders) na watu wakawachukia Wakatoliki lakini in deep ukisoma vitabu vyao vinapingana na uharamia kama huu..
 
Wakuu Chama na Nguruvi3:
Kwanza nikiri kuona mwanga wa matumaini kwa hizi post zenu za mwisho. Ngoja nami nichangie:
1. Nidhamu 2. Inayojengwa muongozo 3. Yaani Katiba 4. Yenye kuamua kipi kifanyike na kipi kisifanyike.
Kwangu Nidhamu ni kutii, kuheshimu, kujali, kulinda, kuthamini, na kuamini! Yaani ni UZALENDO katika ngazi ya nchi! Mwenye nidhamu kwa nchi yake ni yule mzalendo!
Nidhamu (uzalendo) ni kweli kabisa unajengwa na Mongozo bora, yaani katiba. Katiba yenye kuegemea upande mmoja ni sumu kwa nidhamu! Mfano: Mtu hawezi kuonesha nidhamu kwa mtu anayempa mbwa wake mikate ale, hali yeye amekosa uji wa mwanae mgonjwa! Huwezi kumwambia mtu huyo atii sheria inayosema Haki kwa tajiri kulimbikiza pesa kwa anasa zake, hali yeye anaangaika japo mlo mmoja tu! Kumbe basi sheria pasipokuwa na MANTIKI NI BURE! Na hakuna Mantiki kuu duniani kama "UTU" Natamka tena kwa sauti kuu "U T U"
UTU ndio uwe muamuzi kwetu wa kuamua nini tufanye na nini tusifanye! Yaani tuishi, yaani taratibu zetu ziweje, yaani mifumo yetu iweje! UTU KWANZA!
Amini Amini Amini Nawaambia, MANTIKI YA UTU INAPOKIUKWA, BASI NI UNYAMA UNYAMA UNYAMA KILA KONA! Vilio na Unyonge, havitakoma kamwe! HAVITAKOMA!
Nakiri wazi kabisa, SIJAONA BAYA KATIKA UJAMAA! Nyerere alilia machozi ya damu moyoni mwake 1998, alipokuwa anahutubia Mei 1 Mbeya, alililia Azimio la Arusha, hakuona ubaya wake. "Dhana ya Kujitegemea" niliona chozi machoni mwake japo macho yake yalikuwa makavu! Aliuliza tumepata wapi "mjomba wa kumtegemea" hadi tukatae kujitegemea?
Azimio halikuandaa waumini, likajikuta likiiangukia mikononi mwa wanafiki, wakalisaliti! Ni wazi ilimuuma sana!
Lakini sisi tunaweza kuandaa Azimio Jipya, tukaandaa fikra za watoto wetu, tukaifanya iwe imani yao juu ya Mungu wetu na maisha yao! UTU tu ndio dhana inayoweza kueleweka na watu wote!

Mkuu wangu utanisamehe kuingilia hili japo sii haba tukubaliane kutokubaliana.. UTU ndio ulotufikisha hapa tulipo. UTU wetu kuwaamini wazungu na waarabu kama binadamu wanaostahili heshima na kupokewa kwa taadhima ndiko kulopekelea sisi kutawaliwa. UTU wetu ndio umetufikisha hapa tulipo leo kwa madai ya mezani wakati mafisadi hawatazami uzalendo wala kuuthamini UTU imefikia hadi watu wanasema kama wewe una mamatatizo sema wewe sio kila mtu..UTU una mipaka yake maadam unajua kuna maadui wa UTU na tumekanywa kujihadhari nao hata ktk vitabu vya dini imendika - Usimtendee mwenzako kile usichotaka wewe utendewe! lakini watu wanafanyiza wala bila msalie ni jukumu letu kujihadhari maana tumejifunza toka Uhuru, wakati wa Ujamaa na hata sasa hivi ktk madudu haya..

Sisi kama sisi ni lazima tuutukuze UTU wetu kwa kuelewa tuna maadui wetu nao ni ukoloni mamboleo kutoka nje na Ufisadi kutoka ndani. Ufisadi ni matunda ya kutojihadhari, kutoziba ufa sasa twaziba ukuta. Viongozi wetu wa leo wameisha sahau kabisa kwa nini tulikuwa Wajamaa miaka 6 baada ya kupata Uhuru. Leo tumeweza kuzaa wakoloni wa ndani ambao wanatumia silaha tulowapa (katiba) against sisi wenyewe.

Kama nilivyosema mwanzo kosa kubwa la Ujamaa huzaa Udikteta maana wananchi hawana mamlaka juu ya mali zao, hawana rights zaku own property isipokuwa kwa kugawiwa kama welfare, tulikuwa huru?. Binadamu sii rahisi kuthamini UTU pasipo kuwaondolea madaraka juu ya wengine, hivyo itawezekana tu kama tutayachukua mazuri ya Ujamaa tukaacha mabaya kisha tukachukua mazuri ya Ubepari tukaacha mabaya halafu regulations zinzwekwa kuwalinda wananchi with bila kupuuza mabaya na Ujamaa na Ubepari kwa wananchi ktk mazingira yetu..

Ikiwa nchi kama Canada na Nordic waliweza kuwalinda wananchi wao kwanza kwa ujamaa wao na kisha wakatumia haki za wananchi kumiliki wakaziba tobo zote za mirija na unyonyaji tusiseme haiwezekani maana mifano ipo..

Sisi kama sisi ni lazima katiba hii itazame upya nini athari za Ujamaa na nini athari za Ubepari usokuwa na regulations. UTU haupatikani bure na wala sii rahisi kwa kila mmoja wetu wapo watu watakao tumia nafsi walizopewa kwa faida zao. Ufisadi ni moja ya athari za nchi kukosa sheria, maana Uzalendo pekee hautoshi.

Ebu turudi nyuma kidogo kujiuliza tulkipigania UHURU - FREEDOM na nini? nini hasa sababu za kupigania uhuru maaa neno Uhuru pekee lina maana nyingi sana.. Kuna mwandishi mmoja aliandika hivi:-

Freedom is not empowerment. Empowerment is what the Serbs have in Bosnia. Anybody can grab a gun and be empowered. It's not entitlement. An entitlement is what people on welfare get, and how free are they?
It's not an endlessly expanding list of rights either - The "right" to education, the "right" to health care, the "right" to food and housing. That's not freedom, that's dependency. Those aren't rights, those are the rations of slavery!..

Duh sasa sisi tulipigania Uhuru upi?.. ukweli ni kwamba tulipigania Uhuru kutoka ktk kukoloniwa. Freedom from colonisation that's it..Haikutuhakikishia freedom nyinginezo na ndipo hoja yangu inapoingia kuhusu kukiuka right to owneship kuwa muhimu sana japokuwa ktk maandishi mengi ya haki za binadamu hutaikuta.

Tusidanganyane matatizo mengi ya nchi za Kijamaa na Kibapari zinatokana na haki hii inapokiukwa aidha kwa tajiri kuchukua cha maskini au serikali kuwazibia wananchi. Viongozi wengi wameanguka ni kutokana na kushindwa kuwalinda wananchi wake baada ya kuwanyima haki hizi hivyo kupoteza UTU wao. Each of us wonna own something..It's our right as long as it's ours na ndio maana tulifikiria kumwondoa mkoloni aliyechukua chetu. Na tutaendelea kuwachukia viongozi wetu kwa sababu tunakosa chetu wala sii mgao sawa wa keki ya Taifa.

Tunapofikia swala la sisi wenyewe tutaweza vipi kuendelea ni lazima tukubali ubepari ambao unarudishia fursa ya wananchi kumiliki njia za uzalishaji, sio serikali isipokuwa serikali itulinde sisi na kushika zile Commanding heights. Njia iko wazi kabisa muhimu ni kuweka regulations ambazo ni miiko na maadili kuwabana sana viongozi wetu kujihusisha na biashara badala ya kuweka sheria zinazowabana wananchi kumiliki mali ktk utajirisho..
 
Well said Mkandara, na hapa ndipo tatizo letu lilipo.
Duniani kote hata kule Ubepari ulipoota manyoya bado zile commanding height zinaheshimiwa sana.
Ukitaka kuona ukali wa mmarekani basi cheza na katiba yake. Maana yake ni kuwa fanya uwezalo lakini kuna mipaka ili kulinda haki za wengine na taifa.

Tumeona Obama akiweka regulations kule wall street, tumeona austerity measures kule ulaya nk.
Ukiziangalia zote zina lengo la kulinda mfumo wao wa ubepari bila exploitation iliyokithiri ya wananchi wake.

Margareth Thatcher alipobinafsisha kila sekta alikwenda mbali na kugusa mashirika kama ya reli na posta.
Hapo akawa amegusa baadhi ya commandnig heights za taifa na ndio ukawa mwisho wake.

Ukiangalia hapa kwetu tumebeba dhana ya ubepari kama ilivyo na kufikia mahali hata commanding height za taifa zikanyakuliwa na kufanyiwa mchezo. Tunaona viongozi wanavyotumia nyadhifa zao kuingia mikataba ya ajabu inayogusa thamani za taifa. Imefikia mahali hata njia kuu za uchumi ikiwemo ardhi sasa ni gawa gawa na mnada.

Njia ulizosema zipo wazi, hakika kwetu zimefungwa. Labda unifahamishe kidogo ni njia gani inayombana kiongozi wa Tanzania? Tumefuta miiko ya uongozi na kuweka kitu kinaitwa 'tume ya maadili'. Hii ni ze comedy maana hadi leo utaniambia imefanya kazi gani tunayoweza kusema imesimamia thamani za taifa.

Tukifika hapa ndipo nasema, tulipaswa na tunapaswa kuwa na mfumo mzuri wa kuwabana viongozi wasitumie fursa walizonazo kujinufaisha kwa mgongo wa ubepari na unyonyaji.

Kama ulivyosema kwavile hatuna regulations basi watu wanatumia fursa hiyo kuliangamiza taifa kwa kisingizio cha misingi ya ubepari ambayo ni soko huria. Soko huria kwetu limekuwa soko holela maana watu wanajifungia maofisini ili kuleta mgao wa umeme wauze mafuta yao yaliyopo bandarini.

Kabla hatujafikiri mfumo wowote ni lazima kwanza tuwe na misingi, mwongozo,maadili na thamani za taifa zikianishwa katika muongozo wetu sote ambao unambana kila mmoja wetu. Muongozo huo ni katiba inayotokana na sisi wananchi na si kundi lililokaa na kuandika pengine kwa kurubuniwa na wale wenye uchu wa unyonyaji.

Fursa hii ya kuandika katiba yetu tumeibofoa vibaya sana. Na hapa ndipo tulipaswa tuanzie.
 
Mkuu Mkandara:
Kwanza nakubali sana changamoto zako, hakika nazifurahia...ziko so critical!
1. Sipendi tukubaliane kutokubaliana! Tutakuwa tunawazika watoto wetu kabla hawajazaliwa. Ni lazima tutambue ukweli ni upi na kuafikiana, tukauwekea azimio la kuuishi na kuanza kuupigania! Sikumbuki vizuri maneno haya yalitamkwa na nani kati ya Aristoto na Sokarati, anasema "We are Discussing No Small Matters. But how We Ought to Live". Tumeshazikwa hai, je tuwaache watoto wetu nao? Je, tunakipenda kizazi chetu kijacho? Tunataka wajivunie nini kwetu? Je, tutakuwa kama Mkwawa na Kinjekitile? Je, tutaishi hata baada ya vifo vyetu kama hao?
"Maisha ni Furaha, kama haipo ni Upumbavu. Na hakuna Furaha ya Mtu ila Watu" UTU! Tukikaa chini, tukaamua kuumiza vichwa kwa pamoja, nadhani tunaweza na kutoka na suluhisho la haya yote!
2. Hakika kabisa napingana nawe kuwa UTU ndio uliotufikisha hapa! Hata siku moja UTU hauna zao baya, japo vitendo vyake vyaweza onwa ni vibaya (udikteta), udikteta haukwepeki katika kuendesha tamaa za binadamu, lakini matokeo yake ni furaha! UTU ni MANTIKI, MANTIKI ni UWIANO SAHIHI, UWIANO SAHIHI ni KUFIKIRIANA! Nyerere aliwahi kusema kuwa "Utii bila Uhuru ni Utumwa. Na Uhuru nao bila Nidhamu ni Wendawazimu" that says a sage! UTU sio Ujinga au Uzembe, Utu sio huruma au kusamehe pasipo mantiki! Utu sio upole pasipo mantiki! Utu sio kupenda pasipo mantiki! Utu sio Ukarimu pasipo Mantiki. Nilishawahi kusema kuwa Mantiki ya Utu inapaswa kutawala kila kitu chetu, uchumi, siasa na tamaduni, siioni kwenye dini zetu wala siasa zetu! Haipo! Imekiukwa! Unyonge wetu ulitokana na uzembe, ujinga au kuzidiwa nguvu! Kitendo cha babu kumkarimu mzungu sio UTU, ni ujinga-kutokufahamu-ignorance. Pima ipi ni Mantiki! Msidanganywe na dini zenu na mahubiri yao ya kinafiki juu ya UTU! Niulize swali labda: Kuna mamtiki gani ya mtu kubeba Dhaka mfukoni sh. 5000 akatoe kanisani au msikitini, hali jirani yake anakufa njaa na kukosa sh. 100/= tu ya panado? Njian anakutana na watoto wangapi wa mtaani asiwape? Anawajua masikini wangapi asiwajalie? Kuna wagonjwa wangapi asiwajalie? Wangapi hawajiwezi asiwape? Je, ikatokea mtu(mnayemuita mwizi) akampora hiyo pesa akaenda kumnunulia chakula na dawa yule afae njaa na homa! Yupi atakuwa na UTU? UTU si kutii sheria isiyokuwa na Mantiki!
Je, kuna Mantiki gani ya mchungaji ama shehe kupaki gari ya kifahari(luxury car) nje ya kanisa au msikiti hali kuwa amepita Manzese, Tandale amewaona waumini wake? Amepita Masikini na wagonjwa wangapi wasiojiweza hadi kufa akawasalia, asiwasaidie? Mkuu Mkandara, UTU ni MANTIKI KUU ya Maisha. "KUFIKIRIANA"
Na ndio maana napendekezwa usimikwe katika kila kitu chetu-LOGIC = HUMANITY.
Watu kuwakarimu wazungu ni baada ya kupumbazwa akili kwa kupindishiwa Mantiki ya UTU...kama leo tuzaniavyo UTU ni Haki za Binadamu, ni uzembe na ujinga unaotuzamisha kwenye shimo la Ukoloni Mamboleo, kama ujinga wa babu uliomzamisha kwenye shimo la Ukoloni.

Wangu naona hata hapa hukunielewa vizuri maana ya kusema Tukubali kutokubaliana.. Hii nikiwa na maana tuna nadharia mbili tofauti baina yangu na wewe ktk kiitikadi.. Mwenzangu umezama far left wkati mimi nimekuwa kati kulia kwa kutazama Watu na mazingira yalounda Utaifa wetu kiuchumi.. Kwa hiyo kuwa wewe kushoto nami kulia haina maana tunaacha watoto wetu hawana mwelekeo bali wachambue wenyewe ni mawazo gani watakubaliana nayo na bila shaka hatwa wao watatofautiana vile vile. Tena labda sijakwambia vizuri mimi ni mtetezi mkubwa sana wa siasa za mwalimu Nyerere na Ujamaa.. Ni mjamaa 100% kwa kazi ilotakiwa kama dawa vile Panador kwa kichwa na sio malaria. Nachofanya hapa ni kukosoa na kueleza makosa ya kimfumo na wapi tulipoharibu..

2. Hakika kabisa napingana nawe kuwa UTU ndio uliotufikisha hapa! Hata siku moja UTU hauna zao baya, japo vitendo vyake vyaweza onwa ni vibaya (udikteta), udikteta haukwepeki katika kuendesha tamaa za binadamu, lakini matokeo yake ni furaha! UTU ni MANTIKI, MANTIKI ni UWIANO SAHIHI, UWIANO SAHIHI ni KUFIKIRIANA! Nyerere aliwahi kusema kuwa "Utii bila Uhuru ni Utumwa. Na Uhuru nao bila Nidhamu ni Wendawazimu" that says a sage! UTU sio Ujinga au Uzembe, Utu sio huruma au kusamehe pasipo mantiki! Utu sio upole pasipo mantiki! Utu sio kupenda pasipo mantiki! Utu sio Ukarimu pasipo Mantiki. Nilishawahi kusema kuwa Mantiki ya Utu inapaswa kutawala kila kitu chetu, uchumi, siasa na tamaduni, siioni kwenye dini zetu wala siasa zetu! Haipo! Imekiukwa! Unyonge wetu ulitokana na uzembe, ujinga au kuzidiwa nguvu! Kitendo cha babu kumkarimu mzungu sio UTU, ni ujinga-kutokufahamu-ignorance. Pima ipi ni Mantiki! Msidanganywe na dini zenu na mahubiri yao ya kinafiki juu ya UTU! Niulize swali labda: Kuna mamtiki gani ya mtu kubeba Dhaka mfukoni sh. 5000 akatoe kanisani au msikitini, hali jirani yake anakufa njaa na kukosa sh. 100/= tu ya panado? Njian anakutana na watoto wangapi wa mtaani asiwape? Anawajua masikini wangapi asiwajalie? Kuna wagonjwa wangapi asiwajalie? Wangapi hawajiwezi asiwape? Je, ikatokea mtu(mnayemuita mwizi) akampora hiyo pesa akaenda kumnunulia chakula na dawa yule afae njaa na homa! Yupi atakuwa na UTU? UTU si kutii sheria isiyokuwa na Mantiki!
Je, kuna Mantiki gani ya mchungaji ama shehe kupaki gari ya kifahari(luxury car) nje ya kanisa au msikiti hali kuwa amepita Manzese, Tandale amewaona waumini wake? Amepita Masikini na wagonjwa wangapi wasiojiweza hadi kufa akawasalia, asiwasaidie? Mkuu Mkandara, UTU ni MANTIKI KUU ya Maisha. "KUFIKIRIANA"
Na ndio maana napendekezwa usimikwe katika kila kitu chetu-LOGIC = HUMANITY.
Watu kuwakarimu wazungu ni baada ya kupumbazwa akili kwa kupindishiwa Mantiki ya UTU...kama leo tuzaniavyo UTU ni Haki za Binadamu, ni uzembe na ujinga unaotuzamisha kwenye shimo la Ukoloni Mamboleo, kama ujinga wa babu uliomzamisha kwenye shimo la Ukoloni.
Mungu wetu anaita sasa!
Hii ya pili mkuu wangu ndio nasisitiza kutokubaliana na binadamu kuutumia UTU kama kigezo cha maisha bora wakati kuna wanyama pori wasokuwa na Ubinadamu. Na pengine umesahau kwamba Freedom yaani Uhuru ni sehemu ya UTU sasa kama utu huu hutaupata kwa amani ijawezekana kabisa nasi tukaupoteza utu wetu na kuingia vitani ktk kuutafuta UTU..

Na labda nifupishe tu maelezo ya tofauti baina yetu mimi na wewe kuhsu mfano wa Zaka uloutoa.. Kuna maana kubwa kupeleka kanisa au msikitini kwa sababu yule jirani yako unayempa hizo Tsh 100 haitampa chakula wala kipande cha mkate na chai na hata tuseme iwe Tsh 1000 bado kuna uwezekano kuwa unampa fedha za kwenda kulewa pombe na sii chakula halafu pia hujui kama tatizo lake ni chakula au kuna zaidi.. Fedha sii msingi isipokuwa kwa malengo ya kumkomboa.

Lakini kama utaipeleka hiyo Tsh 100 Kanisani au msikitini, huko kuna watu kama 200 wengine wamechangia hizo Tsh 100 na hivyo kuwa na Tsh 20,000 ambazo zitalisha sii mtu mmoja tu bali wengi na kwa wakati mmoja na watahakikisha wanapewa chakula na sio pombe. Kwa hiyo binafsi sadaka inasisitizwa kupelekwa msikitini au kanisani kwa maana yake..
Pamoja na yote haya binafsi yangu naamini ktk kumfundisha jirani yako uwezo wa yeye kujitegemea, kumwajiri, kumfundisha kuvua samaki badala ya kumpa kipande cha samaki..Na ukiwsha mwezesha umeomndoa mzigo huo machoni na ndio maana nasema sisi wote tunataka uhuru wa kumiliki mali zetu kuwezeshwa kuzalishaji badala ya kuwa wategemea zaka.
 
Back
Top Bottom