Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Nguruvi3,

Samahani kwa kutofafanua zaidi hili. Kuhusu Uzalendo, Kuhusu Uzalendo, sipingani na hoja zako, ni kwamba nina mtazamo wa ziada tu. Naomba nifafanue kidogo juu ya Utaifa. Sikuwa na maana kwamba all nationalists are gone, bado wapo wengi tu, and I believe you and I among them, and there are many other sisters and brothers of Nationalism ambao leaders the likes of Nyerere, Nkrumah, Samora Machell… made them (still do) proud of being Tanzanian, African…

When I say the project of Nationalism has stalled maana yangu ni kwamba: Kwanza, if you mention majina ya viongozi hawa to many of our university students (of Tanzanian origin) both at home and abroad, utakutana na one of the following:


  • Either, many have no interest to hear more;
  • Many do not recognize these names; or
  • Many have very marginal knowledge about these names…

So hilo ni la kwanza;

Pili, ni kwamba ingawa bado brothers and sisters of nationalism tupo, uweo wetu hauna maana sana kama viongozi wetu don't act the same way or enact policies zinazoendana na aspirations zetu. Tukumbuke kwamba Nationalism was an ideology in itself iliyolenga kutupatia self determination kisiasa, kiuchumi, na kijamii kama nilivyokwisha jadili juu ya TANU. Lakini kwa bahati mbaya sana, haikuchukua zaidi ya miaka 25 tokea uhuru kwa hizi hopes and aspirations zetu kuanza kupata msuko suko; Since then, ideology of domination spearheaded na Liberalization, Privatization, and Marketization has replaced our Ideology of Self Determination as it was envisaged by TANU.

Viongozi wetu baada ya Nyerere have simply aborted the Nationalism Project, and bear in mind, this project is a big threat to Liberalization, Privatization, and Marketization. Ndio maana hivi sasa, badala ya viongozi wetu kutumia muda mwingi kuwa karibu na wananchi (nationalists) na kuelewa matatizo yao, hence follow up with appropriate actions and policies, viongozi wanatumia more of their time and our resources to ‘wine and dine' with the "imperialists."
Nationalism has an ideology has been man slaughtered; the imperialists in association with wakala wao ambao kwa bahati mbaya sana ni hawa hawa wanasiasa/viongozi wetu, are just ridiculing Utaifa wetu:


  • Interests za nationalists ni kushinda vita dhidi ya our three main enemies of development Umaskini, Maradhi na Ujinga; Lakini eti tunaambiwa kwamba hilo linawezekana tukishirikiana na mapacha watatu wa imperialism Liberalization, Privatization, and Marketization?

That was my point – and I insist, our Nationalism project has been impaired, way beyond repair.
Ntarudi baadae kujaribu kujibu swali lako kuhusu the way forwad. Lakini lazima tuanze kwa kujitambua kwanza.
 
Pamoja sana wakuu wangu:
Mazingira yananifanya niwe mbali kidogo na Mnakasha, lakini tupo pamoja!
Mkuu Nguruvi3:
1. Binafsi kama mkuu wangu Mkandara sina jipya sana kuhusu EAC, kwangu ni kiini macho na kupotezeana muda! Hatuwezi kuwa wamoja kama kila mmoja wetu anamezea mate watoto wa mwenzake! Ni unafiki na mwisho wake ni Vita kali! Kikubwa kilichotakiwa kutufanya wamoja ni MANTIKI tu, nayo ni UAFRIKA wetu! Tumtengeneze mwana E. A. amthamini mwenzake kutoka taifa jingine kwa kutanguliza UAFRIKA kwanza, zaidi ya hapo ni BURE, sawa na kukimbiza upepo! Pia tusidanganyane, Hakuna Muungano nusu nusu, kwani unapoungana mikono tu pasi miguu, kuna wakati miguu yako itataka kwenda kaskazini na ile yangu kusini, na hapo ndipo mikono nayo itakaposhndwa kusimama katika umoja, itaachana tu. Kwa kuwa si kwa hiari, basi vidonda lazima vitokee! Tuwafanye wana EA watambue na kuuthamini Uafrika wao, hapo hatutakuwa na haja ya kujiuliza tuungane nini, bali itazaliwa nchi moja, serikali moja, tutabadilisha hata jina kutoka EA kupata linalojitegemea! Zaidi ya hapo ni Unafiki, huyu anafikiria aridhi ya yule, yule nguvu kazi, huyu soko, huyu teknolojia, huyu malighafi, nk. mwishowe ni Vita!
2. Kuhusu Katiba Mpya: Kwanza niseme wazi, sina tumaini huko. Na nitasema Katiba iweje na ifanye nini! Mkuu wangu Mchambuzi amenipa darasa zito kabisa kuhusu dhana ya Utaifa na Uzalendo, kwa kweli naafikiana nae 100%. Dhana hizi mbili zimepata anguko kuu, zimeporomoka mno! Ndio maana leo mtanzania haoni aibu kumsaidia mzungu kupitisha nyara zetu kimagendo mpakani, kusaini mikataba ya ulaghai dhidi ya rasilimali zetu, kununua bidhaa kutoka nje halikuwa viwandani kwetu ipo, kumthamini Dr. au mkandarasi kutoka nje hali kwetu wapo na tumetumia pesa nyingi kuwasomesha! Kumuuza mtanzania mwenzake ughaibuni ili apate pesa ya kwenda kwenye show ya muziki au mpira! Yote hayo yalipaswa kukemewa vikali na Katiba, kwani Katiba inapaswa kutuonesha tulipo na kule tutakapo kufika, na KUTUFUNGA na kutupitisha kwenye njia itakayotufikisha huko tunakotaka kufika! Hapa ndipo Katiba inapoonywa kujenga matabaka, mbinyo wa katiba usiwe kwa baidhi ya watu tu, kwani Chuki itajengeka kama sasa, tabaka tawaliwa na tawala, wenye nacho na wasionacho, nani afikirie kuipigania Tanzania yake iliyomuacha uchi na familia yake chini ya maboksi Tandale, hali kuwa kuna Manji na Mengi, Ndesamburo na Riz1, nk. Narudia tena "Katiba inayojali KITU na si UTU ni sumu kwa Uzalendo na Utaifa" ndicho kilichotukuta! Naamini kabisa, uwepo wa Tandale au Manzese, dhidi ya Masaki au Sinza, ni Kwa Mujibu wa Katiba! Sioni kitakachobadilisha hili, kwa SERA zizaazo katiba ni zile zile za CCM na Chadema na CUF, yaani Demokrasia!
Mtu makini huongozwa MANTIKI na si HISIA zake! Na Mantiki kuu kabisa ni UTU! KUFIKIRIANA, hapo Uzalendo na Utaifa utapatikana, vitu vya kwanza kabisa kwa Ustawi wa Taifa lolote! Tuna macho lakini hatuoni, masikio lakini hatusikii.
Mungu wetu anaita sasa!
 
JingalaFalasafa,
Hili neno au dhana UTU umeleiongelea sana.
Nilipouliza tunawezaje kwenda mbele kwa utaratibu unaokubalika, Mkandara akaja na bandiko lake zuri sana na kuelezea Nationalism na jinsi gani inaweza kufanyika.
Mchambuzi kaja na Nationalism na Patriot na kazielezea kwa umakini na kuzitofautisha.

Labda nikuuulize tena, tunawezaje kuwa na taifa na dhana ya UTU bila ku-document mahali, bila kuwa na utaratibu wa kuilanda dhana hiyo na bila kujua wananchi wanaielewaje dhana ya UTU.

Tunawezaje kuingiza dhana ya UTU vichwani mwa watu.
Na je UTU ni mfumo au ni msemo tu.

Labda iweke vizuri nawezakuwa sijakuelewa, how do you make 'UTU' as the policy of the nation
 
JingalaFalasafa,
Hili neno au dhana UTU umeleiongelea sana.
Nilipouliza tunawezaje kwenda mbele kwa utaratibu unaokubalika, Mkandara akaja na bandiko lake zuri sana na kuelezea Nationalism na jinsi gani inaweza kufanyika.
Mchambuzi kaja na Nationalism na Patriot na kazielezea kwa umakini na kuzitofautisha.

Labda nikuuulize tena, tunawezaje kuwa na taifa na dhana ya UTU bila ku-document mahali, bila kuwa na utaratibu wa kuilanda dhana hiyo na bila kujua wananchi wanaielewaje dhana ya UTU.

Tunawezaje kuingiza dhana ya UTU vichwani mwa watu.
Na je UTU ni mfumo au ni msemo tu.

Labda iweke vizuri nawezakuwa sijakuelewa, how do you make 'UTU' as the policy of the nation

Mkuu wangu Nguruvi3: Hakuna maana nyingine kuu ya UTU ila MANTIKI-LOGIC! Labda tuache kutumia neno UTU, ila tuseme kila tukifanyacho kiwe na MANTIKI, critical thinking-reasoning ni mama wa Logic! Tujiulize sasa, tukiishicho leo ni zao hilo? Je, MANTIKI inapatikana ndaniye? Neno UTU lisitusumbue! Kikubwa ni kuhoji mambo tu kwa kina! Je, kuna mantiki ya kuishi hiki na hiki? Mfano: kuna mantiki gani ya kuruhusu mtu kuwa na gari 10 hali jirani yake hana nguo wala chakula? Kuna mantiki gani ya kumzuia mtu binafsi kumiliki njia kuu za uchumi?
Sasa mimi katika kuhoji juu ya social life yetu, ukamilifu wa mantiki - logic ndio nimeupa jina UTU. Katka socialogy UTU ni MANTIKI na MANTIKI ni UTU! Kama unaona mantiki yoyote katika haya tuyaonayo leo, basi jua kuwa hicho ndicho nikiitacho UTU!
ANGALIZO:
Huwezi hoji mambo critically kama kuna upande umeegemea! MANTIKI hupatikana kutoka fikra huru zisizofungwa na chochote ila ujazo wa hoja! Narudia, MANTIKI ndicho nikiitacho UTU! MANTIKI(utu) hulindwa kwa MANTIKI%
Mungu wetu anaita sasa!
 
Mkuu wangu Nguruvi3: Hakuna maana nyingine kuu ya UTU ila MANTIKI-LOGIC! Labda tuache kutumia neno UTU, ila tuseme kila tukifanyacho kiwe na MANTIKI, critical thinking-reasoning ni mama wa Logic! Tujiulize sasa, tukiishicho leo ni zao hilo? Je, MANTIKI inapatikana ndaniye? Neno UTU lisitusumbue! Kikubwa ni kuhoji mambo tu kwa kina! Je, kuna mantiki ya kuishi hiki na hiki? Mfano: kuna mantiki gani ya kuruhusu mtu kuwa na gari 10 hali jirani yake hana nguo wala chakula? Kuna mantiki gani ya kumzuia mtu binafsi kumiliki njia kuu za uchumi?
Sasa mimi katika kuhoji juu ya social life yetu, ukamilifu wa mantiki - logic ndio nimeupa jina UTU. Katka socialogy UTU ni MANTIKI na MANTIKI ni UTU! Kama unaona mantiki yoyote katika haya tuyaonayo leo, basi jua kuwa hicho ndicho nikiitacho UTU!
ANGALIZO:
Huwezi hoji mambo critically kama kuna upande umeegemea! MANTIKI hupatikana kutoka fikra huru zisizofungwa na chochote ila ujazo wa hoja! Narudia, MANTIKI ndicho nikiitacho UTU! MANTIKI(utu) hulindwa kwa MANTIKI%
Mungu wetu anaita sasa!

Wakuu,
Hapana shaka mmekwishasikia kwamba utu ni falsafa ya muda mrefu katika jamii za kiafrika. Kama falsafa, inaeleza nafasi ya mtu mmoja mmoja katika jamii, pamoja na mahusiano ya kijamii kwa ujumla. Jamii za kusini mwa Afrika kwa mfano zina misemo; Umuntu gabantu, I am because we are, n.k.
Hakamiliki mtu bila kutengemaa kwa mahusiano yake na watu wengine. Mtu mwenye utu huthamini na kuheshimu hadhi ya kiumbe mwingine yeyote aitwaye mtu.
Jamii yenye utu, au angalau kiasi kikubwa cha utu ina uhaba wa vitendo viovu dhidi ya watu. Kama unathamini utu, huwezi kumdhalilisha mtu mwingine, kumtweza, kumwonea au kumdhulumu, n.k.
Kwa maana hiyo, vitendo vya ubaguzi, ufisadi, uwekaji watu katika madaraja, utumwa, n.k hufanywa na watu wasio na utu.
Jamii yenye utu kwa maana hiyo ina haki ya kijamii (social justice) [hapa fikiria pia dhana za social, political, na economic injustice]
Kwa kifupi, utu ni mfumo bora (ideal system) ambao jamii ikipenda inaweza kuujenga. Unajengeka katika misingi ambayo chama (fulani) cha kisiasa nchini Tanzania (kinachotaja UTU kwamba ndio itikadi yake)kinaibainisha kuwa, misingi ya utu ni UMUHIMUWaKE, yaani,
  • Usawa,
  • Maadili,
  • Udugu,
  • Haki,
  • Imani (trust),
  • Mabadiliko chanya,
  • Uhuru
  • Wajibu,
  • Kazi,
  • Endelevu (Sustainability)
Misingi hiyo huleta ustawi wa jamii katika nyanja zote (siasa, utamaduni, na uchumi)
 
Nguruvi3,
Mimi ningeshauri sana katika Ukumbi huu ama tuanzishe mwingine kuzungumzia Katiba yetu na pengine maswala yote tunayozungumza hapa yanaweza kupata ufumbuzi kutokana na michango yetu kuhusu katiba tunayoitaka sisi. Tusijali kinachoendelea na viongozi wetu ila sisi wenyewe tujiuliza tunaitaka katiba gani na pengine tuichukue ile ya zamani na kutazama kila kipengele wapi kuna makosa na wapi tunahitaji kuendeleza yale yaliyoasisiwa na viongozi wetu..

haya mambo yote tulozungumza hapa yatawezeshwa tu na KAYIBA tuitakayo..UTU, Utaifa na Uzalendo yanaweza tu kusimama ikiwa katiba yetu itayapa kipaumbele na ktk nafasi muhimu za mamlaka ya kiutawala kwa kuzingatia hisotira yetu... Tumeyaona mengi sana yakitendeka kinyume cha katiba iliyopo leo lakini kama kawaida yetu tumeiadhibu Katiba yenyewe kwa kusema ina mapungufu japokuwa binafsi yangu naamini sana tu kwamba ni sisi Watanzania tulokuwa na Mapungufu zaidi ya katiba yenyewe.. Maadam tumepoteza na wala hatujivunii UTAIFA wetu (uzawa wetu) hivyo sii rahisi kusisitiza hata UZALENDO. Hivyo, hata kama tutairekebisha katiba pasipo Utaifa na uzalendo bado tutarudi ktk hali ile ile ya kutafuta mchawi.

Ebu tujikumbushe kidogo hii sutra ya kwanza, imekuwaje hata utangulizi wa Katiba ya zamani umetushinda kuusimamisha?. Sura ya kwanza ya Katiba yetu ya mwaka 1977 inasema haya yafuatayo:-

UTANGULIZISURA YA KWANZAJAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA, WATU NASIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA
SEHEMU YA KWANZAJAMHURI YA MUUNGANO NA WATU​
1. Kutangaza Jamhuri ya Muungano.2. Eneo la Jamhuri ya Muungano.3. Tangazo la nchi yenye mfumo wa Vyama Vingi.4. Utekelezaji wa shughuli za Mamlaka ya Nchi.5. Haki ya kupiga kura.
SEHEMU YA PILIMALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MWELEKEOWA SHUGHULI ZA SERIKALI​
6. Ufafanuzi.7. Matumizi ya Masharti ya Sehemu ya Pili.8. Serikali na Watu.9. Ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea.10.[Imefutwa na Sheri Na. ……… ibara ya ……..].11.Haki ya kufanya kazi, kupata elimu, na nyinginezo.
SEHEMU YA TATUHAKI NA WAJIBU MUHIMU​
Haki ya Usawa​
12.Usawa wa Binadamu.13.Usawa mbele ya sheria.​
Haki ya Kuishi​
14.Haki ya kuwa hai.15.Haki ya uhuru wa mtu binafsi.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​
16.Haki ya faragha na ya usalama wa mtu.17.Uhuru wa mtu kwenda atakako.​
Haki ya Uhuru wa Mawazo​
18.Uhuru wa maoni.19.Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.20.Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine.21.Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.​
Haki ya Kufanya Kazi​
22.Haki ya kufanya kazi.23.Haki ya kumiliki mali.24.Haki ya kupata ujira wa haki.​
Wajibu wa Jamii​
25.Wajibu wa kushiriki kazini.26.Wajibu wa kutii sheria za nchi.27.Kulinda mali ya Umma.28.Ulinzi wa taifa.​
Masharti ya Jumla​
29.Haki na wajibu muhimu.30.Mipaka kwa haki, uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu.​
Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi​
31.Ukiukaji wa Haki na uhuru.​
32.Madaraka ya kutangaza hali ya hatari.
 
J
...Tunawezaje kuingiza dhana ya UTU vichwani mwa watu.
...Na je UTU ni mfumo au ni msemo tu.
...Labda iweke vizuri nawezakuwa sijakuelewa, how do you make 'UTU' as the policy of the nation


Naomba nichangie kidogo juu ya dhana hii ya UTU. Nia yangu sio kutoa majibu bali kuzidi kuchokoza mada kwani majibu kwa kweli sina. Kwa uelewa wangu, Utu ni zao la dhana ya UBINADAMU/HUMANITY; sasa ubinadamu kwa vile una mapungufu yake, hasa katika mazingira ya mahusiano kisiasa, kiuchumi na kijamii, hapo ndipo dhana ya utu ndio inapozaliwa ili kutenganisha ‘good human qualities' na ‘bad human qualities'; Kwahiyo maana ya utu in this sense ni ‘Good Human Qualities'. Ni hapa ndipo tatizo linakuja, e.g. ‘who calls the shots' kwamba hii ni GOOD na hii ni BAD? HAKIMU KATIKA HILI NI BINADAMU MWENYEWE!!

Je tofauti ya UTU ni nini, ni UNYAMA?

Binadamu ni tofauti sana na other living things, ndio maana ingawa mnyama wa porini kama Simba ameumbwa to survive kwa kuua kiumbe kingine chochote, sisi binadamu tuna mipaka, na tukivuka mipaka hii, tutapoteza sifa ya UTU na mara nyingine kuitwa ‘MNYAMA' – kwa maana ya kukosa 'good human qualities'.

Mimi nadhani chanzo cha mkanganyiko huu ni kwamba - binadamu hayupo sawa na viumbe hai vingine kama vile miti au wanyama wa porini kwani miti kwa mfano inajitunza yenyewe automatically kwa kutegemea mwanga, mvua n.k; na wanyama wa porini wanaishi/survive kwa kutegemea INSTINCT zaidi kuliko vitu vingine; lakini Binadamu akitegemea sana INSTINCT au what nature has to offer, kuna mawili: aidha hataweza ku survive, au akiweza ku survive, anaweza poteza sifa za ‘UTU'. Kwahiyo, ili ku-survive bila ya kupoteza sifa ya UTU, ni lazima atumie akili, lakini muhimu zaidi, survival yake hutegemea sana "REASON"; otherwise instincts peke yake haziwezi kumsaidia akaishi/survive kama kiumbe chenye sifa za UTU.

Naomba nitoe mfano mmoja. Binadamu akihisi tumbo linanguruma, kama ilivyo kwa simba, moja kwa moja akilii yake itamwambia kwamba hiyo ni njaa. Lakini tofauti na Simba ambae instincts zitamfanya akamate chochote kilicho nyama, akiue kisha ale, binadamu atahitaji kuwa more ‘rational', kwani instinct zake hazitamfanya atafute chakula kama ilivyotokea kwa Simba. Kwahiyo ili kufanikisha hili, ni lazima binadamu ategemee vitu vya ziada - hasa rationality (intellect), reason and morality (uwezo wa kuchambua what is right and what is wrong in the society), vinginevyo anapoteza sifa ya UTU, na kuwa kama wanyama wa porini au mimea.

Contradictions zilizopo...

Kwa kutumia rationality,reason and morality, binadamu atajitofautisha na wanyama na kutafuta kwa mfano ajira ili apate mshahara wa kumwezesha kula, kuvaa na kulipia pango. Swali linalofuata, ni je, binadamu mmoja kumwajiri mwingine na kumlipa mshahara ni part of human nature? Kama ni ndio, basi maana yake exploitation ni sehemu ya UTU. Lakini one could also argue kwamba binadamu mmoja kumuajiri mwingine sio human nature, na kufanya hivyo, mwajiri na mwajiriwa wote wanaondokwa na moja ya sifa ya UTU. Swali lingine linalofuata ni je, mfumo upi unathamini humanity zaidi – Ujamaa au Ubepari? Wapo wataosema ubepari kwa sababu unajali uhuru wa watu kujitafutia kwa kutumia akili yako, hivyo kula jasho lao, kitu ambacho kwa kiasi kikubwa kinakosekana kwenye Ujamaa. Lakini wapo ambao wataojenga hoja kwamba Ujamaa ndio unathamini zaidi UTU kuliko Ubepari kwa sababu kunakuwa na hali ya usawa katika umiliki wa ardhi, viwanda, migodi…, vitendea kazi na kile kinachozalishwa. Kwa maana nyingine, Ujamaa unapelekea more equitable economic production and distribution, income equality, hence social and human equality kuliko Ubepari - hivyo kuwa more UTU - centred kuliko Ubepari.

Swali lingine muhimu hapa ni je, kipimo cha Maendeleo/ Yard stick ya Maendeleo ni nini, Utajiri au Humanity? Je yote haya yanaweza kupatikana chini ya Ubepari? Chini ya Ujamaa?

Ni hayo tu ndio nilikuwa nayo kuhusu dhana ya UTU, hasa nia ikiwa ni kuchokoza tu mada, sio kutoa majibu.
 
"Uwezo wa kuchambua what is right and what is wrong in the society" au UTASHI! REASONING-CRITICAL THINKING-ARGUEMENTATION, huzaa LOGIC/MANTIKI, nayo ndiyo niitayo UTU!
Asante sana Mkuu wangu Mchambuzi, kwa kunisaidia kumeng'enya zaidi na kuileta karibu dhana hii katika kueleweka! Ulichokisema ndicho hasa nachokimaanisha kuhusu UTU!
1. Ni sahihi kabisa kusema kuwa binadamu ana "good and bad human qualities" tena hizi ni "innate/inborn". UTU na HULKA/MATAMANIO! Wanyama huongozwa na Hulka zao, lakini binadamu amejaliwa UTASHI, uwezo wa kujua jema na baya, hivyo anapokataa kutumia UTASHI wake, na kutumia HULKA zake, binadamu hugeuka kuwa mnyama! Binadamu ameumbwa na sifa za kujikweza, lakini mantiki inasema, kila kilicho juu kuna kikishikiliacho chini, kitoacho nguvu zake kukiweka kingine juu, ni Unyonyaji! Nimesema na sitaacha kusema, silaha kubwa kwa sasa ya HULKA za binadamu ni UHURU na HAKI (Uhalalishaji). Kama tunaamini kwamba tumeumbwa na Hulka, ambazo ndio sifa kuu ya UNYAMA, kwanini tung'ang'anie kuachwa huru pasi kufungwa? Nini ni zao la mtu kuachwa huru kufuata hulka zake? Je, si kama simba amkamatapo mama swala na kuacha kichanga chake cha siku moja? Kuna tofauti kwa wale walimbikizao utajiri nyumbani kwao hali kuwa hospitali hazina dawa? Mtaita Uhuru-haki, MANTIKI je? Wanatudanganya ni kupewa Fursa Sawa kushindana ili ku-boost maendeleo, inaingiaje akilini hii halikuwa tunajua fika tulikoloniwa? Wapo waliopata elimu mapema, barabara, hospitali, nk. kuna MANTIKI gani ya kuwaweka pamoja watu hao na mie kutoka unproductive area ya wakoloni ambako sikuona hospitali, shule, wala barabara, ETI tupiganie fursa ya soko la samaki au ajira? MANTIKI haipo hapo-yaan hakuna UTU hapo! Tunadhani ni kitatokea? Kama sio unyama? Kwanini nisihonge kupewa ajira? Au kuunda kundi kukwapua mali zako? Au kumtafuta sangoma kukufanya kichaa? Au kujinyonga kukwepa ugumu wa maisha? Au kutelekeza familia? Au kuanzisha machafuko? Hayo ni MATOKEO YA KUFUATA HULKA ZA WATU!
2. NI LAZIMA BINADAMU AFUNGWE, kamwe asiachwe huru! Matendo ya binadamu yote huongozwa na falsafa, mitazamo, itikadi, mila, imani, kanuni, sheria, taratibu, mienendo, desturi, mifumo, sera, nk, hayo ndiyo yamfungayo mtu, lakini kibaya zaidi hayo msingi mkuu huyasimamiayo ni UBINAFSI-Umimi-mimi kwanza, na ndio maana maisha yamekuwa ushenzi na upuuzi. Sasa ili binadamu asigeuke kuwa mnyama ni lazima mambo hayo juu yasimamiwe na msingi mkuu kabisa yaani MANTIKI, ndio niuitao UTU! Imani, itikadi zetu, n.k. zinapokosa MANTIKI, basi ni bure! Lakini zinapokuwa na MANTIKI, matendo yetu yataonesha hilo, na tutafungwa nazo!
Yaani kwa sasa TUNAFUNGWA na UBINAFSI zao la hulka zetu, na si MANTIKI zao la Utashi wetu!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Wanajamvi,
Kama alivyosema Mkandara, ni wakati sasa wa kutafakari nini watu wangedhani kibadilike,kiongezwe au kipunguzwe katika katiba:
-Kiuchumi, kisiasa na kijamii
-Kwa kuangalia mihimili ya mikuu mitatu na ule wa nne

KICHWA CHA HABARI KITAKUWA: NINI MTAZMO WA KATIBA MPYA

Karibuni
 
Mchambuzi,
Kwanza shukran sana ktk kuutafsiri UTU nahakika hakuna zaidi ya UTU wa binadamu isipokuwa uwezo wa kuchambua RIGHT and WRONG na hili lipo ktk maumbile ya binadamu wote likiitwa AKILI. Lazima nikubali ukweli kwamba mimi binafsi sielewi tafsiri sahihi ya neno AKILI kwa kiingereza ama lugha nyiingineyo zaidi ya kutumia neno SANITY.. maana sikubaliani na neno Intelligency ama mental capacity haya yanapunguza uzito wa maana ya neno hili maana wapo wanyama ni smart than us, na vipo viumbe wengi uwezo wa ku comprehend zaidi yetu, lakini kwa kutokuwa na Akili (reason of insanity) wanyama hawa hawana uwezo wa kuchambua right from wrong.

UTU kwa maana hiyo ni zaidi ya kufikiriana, kupendana na kadhalika maana hata wanyama wana uwezo huo lakini hawana AKILI inayotufanya ssi tuitwe Binadamu na viumbe tofauti na wengine wote hata yule nyani mwenye genetic DNA sijui 99.98 sawa na binadamu bado hana uwezo wa kuchambua..Na ndipo yale maneno matatu yanapochukua nafasi kubwa ktk uchambuzi na soundness of Judgment - 1. Freedom 2. Justice and 3. Equality. Tutabishana weee kuhusu haya matatu lakini kwa misingi ya kutazama what is right from wrong, mwisho wa siku tunaweza kubaliana kama sii wote basi wengi wetu the right thing is so and so..Japokuwa its very true ya kwamba what is around us mara nyingi sana hu influence our judgement..(WATU na MAZINGIRA)..
Nguruvi3,
Mkuu wangu naona swala la katiba kila mtu kalikwepa.. Na hapa pia nilitaka sana kuwasoma wenzangu lakini naona swala hizi zito sana ikiwa tatizo haswa ni SISI watanzania lakini tunajaribu kuziweka lawama hizi kwa katiba.. Ukisoma hiyo sura ya kwanza tu utagundua kwamba nusu kama sio robo tatu ya sehemu ya kwanza hadi ya tatu hazifuatwi..Na sii kwamba hazifuatwi tu bali naweza sema haziheshimiki kabisa ndipo jamaa zangu kina Zakumi na Willian J Malecela waliposema hatuhitaji miiko na Maadili isipokuwa kusimamisha Sheria.. Sasa tunajiuliza hizi sheria zitasimamishwa vipi ikiwa Katiba na sheria zake ni kizazi cha Miiko na Maadili ambayo hutafsiri thamani ya UTU wa wahusika?.

Hivi ni kweli kwamba ikiwa sio mwiko kwenu kula Mbwa japokuwa kuna sheria kikatiba inakataza kula Mbwa unafikiri kila Mphilipino anaweza kweli kuacha kula mbwa kwa sababu imekatazwa ktk katiba ya nchi. Ama unaanza na miiko kama India ambao mila zao zimeharamisha kula nyama ya ng'ombe hivyo ni rahisi kwao kuweka sheria ya kikatiba kutokula nyama ya ng'ombe na watu wakafuata!...narudi ale pale - Who are WE for real?
 
Mkuu Mkandara,
Nina uhakika watu wanakiu na hawajakwepa. Hoja ni nzito kama ulivyosema lakini sisi ndio Watanzania ni lazima tumeze kidonge kiwe na sukari au kichungu, we have to!


Tumesaha set a motion, let the ball roll on.
Kumbu kumbu zangu zinaonyesha sehemu nyingi mchambuzi amegusa katiba mara kadhaa akiinyoshea kidole, say something. Wanajamvi ukumbi huo
 
Mkuu Mkandara,
Nina uhakika watu wanakiu na hawajakwepa. Hoja ni nzito kama ulivyosema lakini sisi ndio Watanzania ni lazima tumeze kidonge kiwe na sukari au kichungu, we have to!


Tumesaha set a motion, let the ball roll on.
Kumbu kumbu zangu zinaonyesha sehemu nyingi mchambuzi amegusa katiba mara kadhaa akiinyoshea kidole, say something. Wanajamvi ukumbi huo

Hapa ndipo tupatapo shida kubwa!
Tunatofautiana Sera juu ya Mfumo, mbaya zaidi tunatofautiana juu ya mifumo yenyewe! Sasa, tukae chini tutunge katiba kwa sera zipi? Kwa mfumo upi? Kwa Falsafa ipi? Kila mahali kuna Ukinzani, katiba ijigawe vipi? Je, si kujaribu kutwanga maji kwenye kinu?
KAMA KWELI TUNA NIA YA DHATI KUMUINUA MWANAAFRIKA WA TANZANIA, NI SHARTI KUANZA CHINI. Tupate Falsafa itakayounda Mfumo, utakaokuwa na Sera zake zitakazohitaji kurasimishwa na kuitwa Sheria, na sheria hizo ndio KATIBA yenyewe!
BUMBUWAZI KWANGU:
1. Tunaunda Katiba kwa Falsafa zipi, na Zimekubaliwa na nani, kwa vigezo gani?
2. Tunaunda Katiba kwa Mfumo upi, na umekubaliwa na nani, kwa vigezo gani?
3. Tunaunda katiba kwa sera zipi, na zimekubaliwa na nani, kwa vigezo gani?
NAHOFU kuhangaika na matawi hali namwagia maji mizizi! Naogopa kumvisha chui ngozi ya kondoo kwani HAKIKA hasara yake ni juu ya damu ya watoto wangu mwenyewe, NAOGOPA!
Naogopa kufuga manyigu, hali hitaji langu ni asali!
Nahofu kuinafiki na kusaliti nafsi yangu!
Bado kuna HAJA YA KUKAA CHINI na kufanya Ubunifu wa hali ya juu kabisa! Tunaweza! Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu. UBUNIFU HAUJAWAHI KUFIKA MWISHO, TUNAYO NAFASI.
Mungu wetu yu hai, anaita sasa!
 
JingalaFalasa,
Ndiyo maana hasa ya mjadala. Baada ya kuuliza maswali hayo, wewe unafiiri ingekuwaje kwa mtiririko huo huo wa maswali.
 
Mimi nitarudia kusema kwamba hapa tulipofikia sii mahala pa kujadili UJAMAA Vs UBEPARI kwa kutazama tafsiri tulizofundishwa isipokuwa kwa tafsiri zetu wenyewe kulingana na mazingira yetu.. We can't go back to UJAMAA ambao tunaelewa fika ulikuwa ni mfumo usioendana na UWEZO wa mwanadamu bali fikra za kum tame binadamu awe mbora zaidi ya Ubinadamu wake jambo ambalo haliwezekani..kama nilivyokwisha sema Ubepari ni mfumo wa Kiuchumi unaolenga wananchi kumiliki uchumi huo na sio serikali,

Tofauti na Ujamaa ambao ulilenga kupambana na makoloni wlaokuja kutuibia mali zetu. NIna hakika kabisa wala sii uzushi kama Wakoloni wangekuja nchini na kuwekeza nchini pasipo kuiba chochote na kupeleka makwao basi Uhuru wetu ungekuwa na tafsiri tofauti kabisa. pengine tungepigania Uhuru kama South Africa, ule Uhuru wa bendera kupingana na ubaguzi wa Apartheid (kama ungekuwepo) ama Uhuru wa Wakikuyu kama wa Kenyatta na Maumau.

Ningependa sana kuandika mengi kuhusu Mabaya ya Ujamaa lakini nadhani sina muda huo kwa leo isipokuwa nachoweza kusema ni kwamba Ujamaa ulitufungia gerezani kwa kuhofia Mabeberu (Imperialists) Ukajaribu kutufunga kamba za shingo bila kujali vipaji vyetu, Utofauti wetu wa maumbile, imani, nguvukazi nakadhalika kiasi kwamba watu walilazimishwa kulima wakati sii wakulima. hata elimu tulilazimishwa kuchukua masomo kwa kupimwa na si mapenzi yetu..Ujamaa ulishindwa kufahamu kwamba ili tufanikiwe ni lazima falsafa yenye iwafahamu kwanza wananchi ni WATU wa aina gani..halafu inajengwa misingi ya maisha yao kutokana na wao sio kuwa na mfumo ulotungwa Urusi ama Ulaya kisha unakuja upandikiza Afrika. Ni sawa na kujaribu kupanda mti wa Christmas Dodoma ukitegema utastawi..

Na wala sii kweli kwamba Ujamaa Unalenga kuleta Freedom, haki na Usawa wa watu wake isipokuwa Ujamaa ni jibu la kuondoakana na Ukoloni kutokana na experience ya wazee wetu kuibiwa maliasili zetu. Ujamaa Ulishindikana kwa sababu Ujamaa haukulenga kuleta maendeleo isipokuwa kuzuia kutawaliwa, kunyonywa, kunyanyaswa na kuibiwa mali zetu..Na ndio maana nchi zote za Kijamaa hapakuwa na freedom ya watu, hapakuwa na haki kwa watu wake wala usawa kwa watu wake na kibaya zaidi hawakuwa na maendeleo isipokuwa walijikita ktk kukidhi tu mahitaji yao bila kutegemea nje. Ujamaa ulilenga zaidi kuikomboa ARDHI na kuwaweka wananchi wake salama dhidi ya wakoloni maana maendeleo ya watu huletwa na watu wenye nia na lengo la kuendelea. Hivyo nitakubalina nanyi tu ikiwa kipande hiki kitachukua nafasi ya kwanza ktk UTAMBULISHO wetu kuwa ni WATU waliotawaliwa na hawataki tena kutawaliwa kiuchumi..

Sisi Watanzania wa leo, aren't TOGETHER as Tanzanians.. hatuna introductory statement ya who we are! hatuna fundamental purposes wala guiding principles. Nitarudia tena kusema tumepoteza DIRA siku nyingi sana baada ya makosa ya mwalimu ktk Ujamaa ulotaka kukuza Uchumi tukashindwa.. Ujamaa haukuzi Uchumi isipokuwa Ujamaa ulikusudia kutulinda dhidi ya wageni wezi walokuja kuitawala nchi yetu kwa kutupatia mahitaji bora na muhimu ya maisha..Hivyo leo hii hatuna reliable evidence of our founding fathers intentions - hatuna! na baada ya kuja Azimio la Arusha ambalo lilichukua sura nyingine ya kuwaogopa hata wananchi wenyewe na hivyo kuwa regarded as Constitution's meaning and what Nyerere hoped the Constitution would achieve ndio tunachukulia kuwa guiding principals.

Ndio maana muda wote huwa nawarudisha ktk swali langu - WHO are WE?... maana inatakiwa tunaposema WE iwe reffered to as The people of Republic Tanzania na sio Linchi la Tanzania na mipaka yake.. Kwa hiyo tujiulize what are our common ground, our common goals ili tuwe na perfect Union na tuweze ku establish Freedom, Justice, insure equality na tranquility kwa watu wake sio kulinda mipaka ya nchi yetu pekee.. How tunaweza ku provide for, common defence, promote general Welfare, na to secure bahati na tuzo (maliasili na rasilimali) tujaaliwa na Mwenyezi Mungu kuwa jamii tulokuwa ktk Umoja wetu.

Pasipo kujielewa sisi ni kina nani, mtakesha na Katiba maana sijui hadi leo hii Wakristu, Waislaam, wapaganm Wahindi, Waarabu, weusi na makabila 120 wanawake kwa waume tunakutana wapi na vitu gani vinatuunganisha kama WATU na sii mipaka ya nchi iliyowekwa na mkoloni.

BTW:= Sipingani na UJAMAA ule ulokusudia maendeleo ya WATU pasipo kuwakazwa ama kuwaamrisha kuwa wasichokuwa. Naukubali tu Ujamaa ule unaotazama Umaskini, Ujinga na Maradhi kuwa ndio maadui wetu wakubwa hivyo kuufanya Ubepari kuwa secondary kwa sababu ubepari hukuza UCHUMI wa nchi wasiokuwa na adha kama zetu. As to say Ujamaa ni theory inayolenga kuboresha maisha na maendeleo ya WATU, as oppose to Ubepari ni WATU wanaokusudia kukuza Uchumi na maendeleo ya nchi..
 
JingalaFalasa,
Ndiyo maana hasa ya mjadala. Baada ya kuuliza maswali hayo, wewe unafiiri ingekuwaje kwa mtiririko huo huo wa maswali.

Nakuelewa Mkuu wangu Nguruvi3:
Pendekezo langu ni juu ya Kupata Falsafa sahihi kwanza, itakayozaa mfumo sahihi (sio lazima uwe ujamaa au ubepari), utakaozaa Sera sahihi ili kuunda KATIBA sahihi!
Hapo namaanisha kwamba, kwanza TUKAE CHINI TUTAFAKARI TUPATE FALSAFA YETU(mahusisi kwa MAZINGIRA na NYAKATI zetu). Tunapoanza ghafla na Katiba, tutakuwa tumeruka hatua 3, zitaendelea kutusumbu, kwani vitu hivi vinategemeana, vinapopishana UKINZANI utatokea! Itakuwa sawa na wale waliokuwa wanajenga Mnara wa Babeli. Huyu mfumo ukiweka tofali, katiba inaondoa, falsafa inalivunja kabisa!
Napenda sana kusema hivi, "tusijifikirie sisi binafsi, ila watoto wetu (kizazi chetu kijacho)" tuwajengee msingi, japo kwa kuwaachia Falsafa sahihi tu!
Mkuu Mkandara:
1. Kwanza nikubaliane nawe juu ya kutotegemea nani kasema nini kuhusu Ujamaa na Ubepari, ila tafsiri zao zitokane na tafakari zetu wenyewe!
2. Ujamaa ni mfumo usioendana na uwezo wa binadamu! Siamini hilo kamwe! Tupe vigezo. Mimi nitakwambia kwanini:
Turudi katika Falsafa kuu ya Ujamaa, "From each according to his ability. To each according to his needs" hapo ndipo ujamaa ulipolala! Niambie mkuu wangu, kipi kinashindikana hapo?
Kipi kipo juu ya uwezo wetu?
TUNAPOMTAZAMA BINADAMU tunagundua kuwa ameumbwa akiwa na pande kuu mbili, na zote zipo ndani ya uwezo wake kuzimiliki, kuzitendesha atakavyo! Nazo ni MANTIKI na HULKA, kwa kutumia UTASHI wetu mwanadamu anaweza kuchagua ama MANTIKI au HULKA kuongoza matendo yake!
Ni jukumu letu kuhoji Falsafa ya Ujamaa kama ni zao la Hulka zetu ama Mantiki!
Sipendi kurudia sana hapa, nitasema hivi tu "Falsafa kuu ya Ujamaa, ni KUFIKIRIANA, nayo ndio UTU, nao ndio UUWIANO SAHIHI, nayo ndio MANTIKI yenyewe, iliyomo chini ya mamlaka na uwezo wa binadamu kwa kuongozwa na UTASHI wake!
Mtu makini huongozwa na Mantiki ya mambo na si Hisia zake!
3. Sikuelewi mkuu wangu unaposema Ubepari ni mfumo tu wa kiuchumi, unaoruhusu Umiliki mali binafsi. Hivi kuna uchumi pasi siasa na utamaduni? Ni wazi HAKUNA! Ubepari ni mfumo wa maisha, kiuchumi una "Private ownership" kisiasa una "Democracy" na kitamaduni una "Freedom-Modernization", hivyo vitatu havikinzani, vinatembea pamoja.
Ni lazima kuumiza vichwa, hizi HESABU wanawaafrika wenzangu wa Tanzania! Ubepari ni "MWANGA MWEUSI" ole kwa wautumaniao kuwaongoza!
4. "Ujamaa ulitufunga gerezani kwa kuhofu mabeberu".
Kwanza sikubaliani nawe. Pia nikuulize, kama ujamaa ulilenga kutulinda dhidi ya mabeberu na ukoloni wao, Je, hatuna haja nao tena? Kwa ubeberu umeisha? Ukoloni nao? Je, huoni haja ya kuuishi Ujamaa kujilinda na ubeberu na ukoloni? Je, bado unaamini tupo huru? Au lini beberu alibadilika kuwa rafiki yetu sasa, tusione haja ya kujilinda nae?
Hizi HESABU, tumeingia kichwa kichwa!

5. Kama tafsiri za maneno HAKI, UHURU na USAWA ni hizi tuambiwazo kwa misingi ya Demokrasia, basi ni sahihi kabisa kusema Ujamaa haulengi kuleta Uhuru, Usawa na Haki!
Swali, je Kuna MANTIKI yoyote juu ya tafsiri zilizopo za maneno hayo matatu? Tukumbuke pia kuwa, MANTIKI ni KUFIKIRIANA-KUTOKINZANA!
Ni lazima tuchimbue mizizi!
6. "Ujamaa haukulenga kuleta Maendeleo"
Hata tafsiri ya Maendeleo kwa mujibu wa ubepari ni tofauti sana na ile ya Ujamaa! Hivyo kama maendeleo yenyewe ndio kama yale ya A. Kusini, basi kweli si lengo la ujamaa! Kwani kipimo cha Maendeleo katika Ujamaa ni UTU, hali kuwa katika Ubepari ni KITU.
Mungu wetu anaita sasa!
 
NINI MTAZAMO WA KATIBA MPYA

Mkandara,umesema kwanza nilzima tujitabue sisi ni akina nani kwanza.
Mchakato ndio huo unaendelea, unadhani tujitambue vipi kwanza kwa mtazamo wako wakati katiba inaandikwa.
Nadhami wakati ndio huu na tuanze kwa kujitambua

JingaLaFalsafa, unasema tumeruka hatua 3 kufikia kuandika katiba mpya. Kwa vovyote iwavyo ni lazima tuwe na katiba iwe hii ya sasa au itakayoandikwa. Hata kama hatukubali utaratibu kama nisivyoukubali mwisho ni katiba kuandikwa.

Kama ungeambiwa ueleze kwa kifupi sana hatua zipi tumeruka ungeandikaje.
Pili, kwahiyo upo upande upi kwamba twende twende bila katiba, tutumie ya zamani huku tukizirudia hatua tulizopita, au tuwe na pa kuanzia japo si timilifu.
 
Nakuelewa Mkuu wangu Nguruvi3:
Pendekezo langu ni juu ya Kupata Falsafa sahihi kwanza, itakayozaa mfumo sahihi (sio lazima uwe ujamaa au ubepari), utakaozaa Sera sahihi ili kuunda KATIBA sahihi!
Hapo namaanisha kwamba, kwanza TUKAE CHINI TUTAFAKARI TUPATE FALSAFA YETU(mahusisi kwa MAZINGIRA na NYAKATI zetu). Tunapoanza ghafla na Katiba, tutakuwa tumeruka hatua 3, zitaendelea kutusumbu, kwani vitu hivi vinategemeana, vinapopishana UKINZANI utatokea! Itakuwa sawa na wale waliokuwa wanajenga Mnara wa Babeli. Huyu mfumo ukiweka tofali, katiba inaondoa, falsafa inalivunja kabisa!
Napenda sana kusema hivi, "tusijifikirie sisi binafsi, ila watoto wetu (kizazi chetu kijacho)" tuwajengee msingi, japo kwa kuwaachia Falsafa sahihi tu!
Mkuu Mkandara:
1. Kwanza nikubaliane nawe juu ya kutotegemea nani kasema nini kuhusu Ujamaa na Ubepari, ila tafsiri zao zitokane na tafakari zetu wenyewe!
2. Ujamaa ni mfumo usioendana na uwezo wa binadamu! Siamini hilo kamwe! Tupe vigezo. Mimi nitakwambia kwanini:
Turudi katika Falsafa kuu ya Ujamaa, "From each according to his ability. To each according to his needs" hapo ndipo ujamaa ulipolala! Niambie mkuu wangu, kipi kinashindikana hapo?
Kipi kipo juu ya uwezo wetu?
TUNAPOMTAZAMA BINADAMU tunagundua kuwa ameumbwa akiwa na pande kuu mbili, na zote zipo ndani ya uwezo wake kuzimiliki, kuzitendesha atakavyo! Nazo ni MANTIKI na HULKA, kwa kutumia UTASHI wetu mwanadamu anaweza kuchagua ama MANTIKI au HULKA kuongoza matendo yake!
Ni jukumu letu kuhoji Falsafa ya Ujamaa kama ni zao la Hulka zetu ama Mantiki!
Sipendi kurudia sana hapa, nitasema hivi tu "Falsafa kuu ya Ujamaa, ni KUFIKIRIANA, nayo ndio UTU, nao ndio UUWIANO SAHIHI, nayo ndio MANTIKI yenyewe, iliyomo chini ya mamlaka na uwezo wa binadamu kwa kuongozwa na UTASHI wake!
Mtu makini huongozwa na Mantiki ya mambo na si Hisia zake!
3. Sikuelewi mkuu wangu unaposema Ubepari ni mfumo tu wa kiuchumi, unaoruhusu Umiliki mali binafsi. Hivi kuna uchumi pasi siasa na utamaduni? Ni wazi HAKUNA! Ubepari ni mfumo wa maisha, kiuchumi una "Private ownership" kisiasa una "Democracy" na kitamaduni una "Freedom-Modernization", hivyo vitatu havikinzani, vinatembea pamoja.
Ni lazima kuumiza vichwa, hizi HESABU wanawaafrika wenzangu wa Tanzania! Ubepari ni "MWANGA MWEUSI" ole kwa wautumaniao kuwaongoza!
4. "Ujamaa ulitufunga gerezani kwa kuhofu mabeberu".
Kwanza sikubaliani nawe. Pia nikuulize, kama ujamaa ulilenga kutulinda dhidi ya mabeberu na ukoloni wao, Je, hatuna haja nao tena? Kwa ubeberu umeisha? Ukoloni nao? Je, huoni haja ya kuuishi Ujamaa kujilinda na ubeberu na ukoloni? Je, bado unaamini tupo huru? Au lini beberu alibadilika kuwa rafiki yetu sasa, tusione haja ya kujilinda nae?
Hizi HESABU, tumeingia kichwa kichwa!

5. Kama tafsiri za maneno HAKI, UHURU na USAWA ni hizi tuambiwazo kwa misingi ya Demokrasia, basi ni sahihi kabisa kusema Ujamaa haulengi kuleta Uhuru, Usawa na Haki!
Swali, je Kuna MANTIKI yoyote juu ya tafsiri zilizopo za maneno hayo matatu? Tukumbuke pia kuwa, MANTIKI ni KUFIKIRIANA-KUTOKINZANA!
Ni lazima tuchimbue mizizi!
6. "Ujamaa haukulenga kuleta Maendeleo"
Hata tafsiri ya Maendeleo kwa mujibu wa ubepari ni tofauti sana na ile ya Ujamaa! Hivyo kama maendeleo yenyewe ndio kama yale ya A. Kusini, basi kweli si lengo la ujamaa! Kwani kipimo cha Maendeleo katika Ujamaa ni UTU, hali kuwa katika Ubepari ni KITU.
Mungu wetu anaita sasa!
Shukran sana napenda sana mtu anasipokubaliana na mimi na akapenda kuua mtazamo wangu maana nisemayo yanatokana na sio tu elimu ya kuusoma Ujamaa bali pia experience niliyopitia na kujiuliza maswali haya..

1. nafikiri swali hili tumekubaliana..
2. Ujamaa ni mfumo usioendana na uwezo wa binadamu! Siamini hilo kamwe! Tupe vigezo.

Kwanza niseme kuwa wewe unazungumzia theory vitu visivyokuwepo ktk dunia hii in reality..Ni vitu vya kufiirika ambavyo watu wote tungependa iwe hivyo lakini hakuna kiti kama mhicho.. Halafu unaposema tu kwamba means of Production zinapo milikiwa na serikali (a system) ina maana kwamba ni serikali (mwenye mali) anayepanga vitu gani wazaliishe, hivyo haitazami kama familia, ukoo au kabila wana ujuzi ama wamejaaliwa ktk ufugaji, uvuvi ama Ukulima..Serikali ikiamua kilimo kwanza kupambana na njaa basi watu wote mnakusanywa na kupelekwa ktk kilimo. Ilitokea Russia, China, Ethiopia - you name it na hata sisi walikunywa watu na kutupwa ktk vijiji vya Ujamaa kwa malengo ya kuwafikisha huduma muhimu lakini nyuma ya pazia lile walilazimishwa kilimo cha pamoja, ufugaji wa pamoja na hata Uvuvi wa pamoja - Uongo?. Why all this ikiwa mkoloni, beberu sijui sultan kisha ondolewa nchini nasi tuko huru, Huo Uhuru uko wapi? - changamoto kwako..

ELIMU;- Kama wewe ulisoma enzi za mwalimu utakubaliana na mimi kwamba ulichaguliwa kuingia masomo ya Sayansi, Uhasibu ama art pasipo hiari wala maandaliszi isipokuwa wao walichagua nani aende wapi. Wapo watu waliopenda kusomea economics au sayansi hawakuweza kusoma isipokuwa Elimu walizopangiwa - Uongo? Kwa hiyo tuliwasomesha watu kutokana na mahitaji yetu kiasi kwamba hata failures wa kidato cha nne wasiokuwa na uwezo walichukuliwa ili kuwa walimu kufidia pengo kubwa la walimu kutokana na vita yetu ya kuondoa Ujinga.

KAZI:- Hata baada ya kuhitimu walipangiwa wapi wakafanye kazi hata kama kulikuwa hakuna facilities za kumwezesha kuifanya kazi na kibaya zaidi wengine walipewa madaraka yasiyohusiana kabisa na elimu zao ili mradi tu washike management kwa sababu ni wasomi. Mtu alosomea Udaktari alipewa Uwaziri/Ukatibu mkuu wizara ya maliasili au miundombinu au ukuu wa mkoa na alipigwa msasa kisiasa zaidi kumwelekeza utendaji wake wa kazi utalenga zaidi sera na ilani za chama - Uongo?

Sasa ebu nipe uuwiano wa haya tuloyaona yakitendeka na maneno haya:- "From each according to his ability. To each according to his needs' kisha utagundua kwamba ktk maneno haya Ujamaa umesahau skills za kila mmoja wetu, kila mmoja wetu has the say or decide what was to be produced kutokana na ujuzi wake; in what quality and by what methods ni kazi ya mjuzi au sio? The government not the producers decided what to produce and to whom it was to be distributed. Hivyo mnaweza kuzalisha machungwa mazuri sana na mali yote ikapelekwa Ikulu, kwa waziri au mkuu wa mkoa na ilikuwa ikitokea - Uongo?.

Mbali ya hapo Ujamaaa haupimi cost za uzalishaji, malipo ya nguvukazi zilotumika zitalipwa vipi isipokuwa wanafanya kazi kama siafu kumtumikia malkia, askari na governmnent officials ambao kazi yao kubwa ni ukiritimba na paperwork all day long wakizana maofisini. kazi ya mtu mmoja kwao itafanywa na watu sii chini ya watano kwa sababu tu wamesoma au wanachama wa chama tawala maana wazalishaji hawahakikishiwi dividends au mapato ya ziada kwa kazi kubwa waliyoifanya.

3. Kuhusu Ubepari na Siasa, mkuu wangu pengine bado hujanipata. Ukizungumzia Demokrasia hata Ujamaa wana demokrasia yao wao wakichagua viongozi wao na kuwa vichwa vya watu ndivyo vinawakilisha upinzani, sijui kama unakumbuka Kura za Nyumba na Jembe. Hityo kwao ndio ilikuwa Demokrasia wakati Ubepari demokrasia imekuja na Ujamaa ndani yake unazungumzia KUFIKIRIANA.. Kama umemsikia Obama jana utaelewa kwamba alikuwa akizungumzia Kurikiriana ktk Ujamaa wa kibepari The Democratic or rather say the left wing. hakuna lolote unalozungumzia hapa ambalo Progressive na Liberal hawalikubali lakini ktk experience yangu mfumo huu hulemaza watu ktk social welfare maana hakuna mtu anayependa kazi ikiwa kuna njia rahisi za kuishi.

Mkuu wangu naishi nchi ya Kibepari ambayo kwa miaka mingi Leiberal wamekuwa ktk madaraka na kila wanapochukua nchi watu hufurahia zaidi kutokana na program za kufikiriana. Wasio wagonjwa hutafuta maradhi wakae majumbani wakivuta fedha za bure pasipo kufanya kazi. pengine unasahau ya kwamba sisi binadamu pamoja na kuthamini UTU wetu tuna upande wa pili wa Mnyama mambao ukiwa Tamed basi hata kutafuta kazi hutapenda.. Yule Simba ukimchukua mdogo ukamweka ktk zizi lake na kumgawia nyama kila siku basi siku ukimchukua mwituni atakufa njaa. Problem ya Ujamaa ni nadharia isofikiria utashi wa mtu akiwa free kufanya maamuzi yake na ndio maana sehemu zote za Ujamaa watu walilazimishwa.

Niliwahi kusema Ujamaa ni sawa na Udikteta lazima utumie Udikteta ktk Ujamaa laa sivyo hutampata mtu hata mmoja. Kuna tofauti ndogo sana baina ya Ujamaa na facism maana hata Hitler pamoja na kuwa kulikuwa na private ownership alilazimisha watu binafsi kuzalisha ku feed Utawala wake watu walichukuliwa utumwa kuzalisha chakula, mali, vifaa vya kivita na kadhalika for the love of the country. Na Ujamaa wa kina Linen haukuwa na tofauti yoyote.

4. Ubebari Ulitufunga kwa kuogopa Mabeberu.. Pengine hili hujanielewa vizuri maana nilichokusudia kusema ni kwamba sisi wenyewe tuliwekwa lumande tusijue lolote nje ya mipaka yetu - Uongo? Tulizuiwa kusafiri unless unaenda kusoma nje, Tulizuiwa hata kununua gari au TV zikiitwa luxuries sii huko Urusi, China wala Tanzania, hivi kweli ndivyo Ujamaa una. Kwa sisi tuloishi miaka ya Ujamaa kisha tukabahatika kwenda nje tunaijua gereza nalozungumzia. Ebu nambie kwa mtu aloishi Kijiji cha Ujamaa (sijui kama uliwahi kuishi) unaweza kunambia tofauti yake wakati ule na mfungwa wa magereza?..Kwa nini tulizuiwa kusafiri nje pasipo kuwa na kibali ncha serikali na ueleze sababu ya kukupeleka nje ambayo iwaridhishe wao (viongozi). Hivi ndivyo inavyotakiwa kufikiriana?.

Nadhani inatosha kwa leo, nitaendelea kesho tukijaaliwa Inshallah!, ila nakuomba unifahamu tu ya kwamba mimi ni mpenzi sana wa mwalimu Nyerere kwa sababu naelewa Ujamaa wake ulilenga nini na kwa manufaa gani na hivyo nayazungumzia makosa ya picha nzima ya ujamaa..Kwa nini tusiuchambue Ujamaa wenyewe badala ya Nyerere na kujua tulikosea wapi?
 
Mkuu wangu Mkandara:
1. Umeuliza hivi "Kwanini tusiuchambue Ujamaa wenyewe badala ya Nyerere na kujua tulikosea wapi?" Hakika hili swali lilipaswa kuulizwa nami kwako! Labda sijakuelewa, lakini swali hilo linakufunga mwenyewe! Nakuomba usichelee kuuafiki ukweli, tupige hatua ya mbele!
MIMI mara zote nimetaka tujadili Falsafa kuu ya Ujamaa, na nimeileta hapa jamvini. Lakini bado Mkuu wangu umenishambulia kwa experience yako binafsi juu ya Nyerere! Wapi nimemtaja Nyerere kama mfano bora katika kuutetea Ujamaa? Na kushauri tuishi kama Nyerere? Binafsi namkubali sana Nyerere, lakini siachi kusema "KUNA SEHEMU NDOGO SANA, ALIBUGI, na ndiyo iliyomghalimu hadi leo watu wanapata pa kuongelea! Kosa la Nyerere ni kutaka matokeo ya Haraka, watu hawakuandaliwa kuuishi Ujamaa! Matokeo yake nguvu ikawa inatumika sana, japo nakiri SI DHAMBI KUTUMIA NGUVU KATIKA UJAMAA, pale tu MANTIKI inapoonekana! Lakini kweli kuna haja ya kuumwagia maji mti mkavu? Kwanini usiandae hayo maji kwa mbegu za huo mti?
Katika misingi ya Demokrasia kutumia nguvu, mmeambiwa na wazungu muite UDIKTETA, "Ndiooooooo, si wamesema wakubwa!"
Mkuu wangu Mkandara, uliyoyataja ni maovu ya Nyerere, tena ni kwa misingi ya Demokrasia uliyofungwa nayo lakini si MANTIKI, na wala si maovu ya Ujamaa, PINGA FALSAFA KUU YA UJAMAA, si Nyerere aliishi nini, au Lenin aliishi nini?
Pia nikuweke wazi tu, KUUA SI DHAMBI PALE MANTIKI INAPOKUWEPO, hata imani yako ya kiislamu inakufundisha hivyo, sembuse kumlazimisha mtu kufanya kazi fulani? Serikali ina uhaba wa chakula, eti tuache watu huru walime pamba, inaingiaje akilini hapo? Tuna uhaba wa madaktari, eti tumuache mtu huru akasomee urubani halikuwa tuna ndege moja na kiwanja kimoja tu. Ukimzuia, unaitwa Dikteta, basi kama ni hivyo dikteta ni kiongozi bora kabisa! HESABU ndugu zangu zimetushika! Lazima tuumize vichwa!
2. Sema Ujamaa una mfumo wake wa Siasa, si kusema Ujamaa una Demokrasia yake! Demokrasia ni "Bill of Rights", UHURU WA KUCHAGUA-HAKI-UHALALI Feki.
Hili haliitaji mjadala mkubwa sana. Ujamaa haujawahi kuwa na Demokrasia, ndio maana hata viongozi wake mnawaita "anti-democratic" - "dictators"
3. WHO ARE WE?
Sisi WAFU waliohai kaburini! Tumezikwa tungali hai! HESABU KALI MNO, zimetufungia kaburi! Si wewe Mkuu wangu Mkandara wala mimi japo na umri wangu mdogo, awezae kuliona jua milele, maana tumeshazikwa! Kujitutumua kusukuma kifusi ili tutoke, ni kujinafiki, kwani juu ya kaburi letu kuna zege nzito, na juu yake wapo walinzi, na sisi ni dhaifu wa mwili na imani! Ni wazi tutafia humu! Je, watoto wetu nao? HAPANA! Big NOOOOOOOO! Tuchonge ukuta wa kaburi tutoboe shimo refu litakaloenda kutokea mbali, ni miaka mingi itapita shimo kuisha, tutakufa na watazaliwa, wataendeleza shimo, mwishowe watafikia mwisho, wataliona jua! Mimi niko tayari kutoa mfupa wangu wa mguu utumike kuchimbia, kwani hatuna kifaa chochote!
Kila post nayotuma humu jamvini haijawah kukinzana na nyingine, na ndani yao zote imo imani hyo. "TUSIJIFIKIRIE SISI ila WATOTO WETU"
Ukitegemea kuliona jua mwenyewe, basi mawazo yangu kweli yatakuwa ni THEORY!
Habari njema ni hii...
Mungu wetu yu tayari Kutupigania vitani. Anaita sasa!
 
JingalaFalsafa,
Shukran, hapa kwa Nyerere na Ujamaa ndipo nwatuwengi wanaposhindwa unielewa na wewe mmoja wapo. Narudia tena kusema kwamba Nyerere was the great leader na mimi mshabiki wake mkubwa sana hivyo kama ungemshambulia yeye ningekwambia ni falsafa ya UJAMAA ndio ulotufikisha pale sio Nyerere. Hata kama angekuwa Reagan au Obama ktk mfumo ule tusingefika mahala. Huyo Huyo Nyerere kama angetawala mtawala ktk mfumo huu wa Ubepari pengine pia angeonekana mbovu vile vile kwa sababu ukitaama kwa undani UJAMAA na UBEPARI ni mbegu za maabara ambazo haziwezi kuota na kustawi Tanzania au Afrika kutokana na mazingira yetu.. Sijui kama naeleweka.

Hivyo Nyerere alijitahidi kadri ya uwezo wake kuweka misingi bora ya kuistawisha jamii yetu lakini kwa hofu ile ile ya WAJAMAA kuhusu Imperialist na ndio maana nimekupa mmifano ambayo imetokea nchi zote za Kijamaa na sio Tanzania pekee, hivyo sio swala la Nyerere bali la kimfumo.

Na pengine sijakueleza mazuri ya Ujamaa ndio maana unafikiria napingana na UJAMAA kwa ujumla wake bali napingana na yale yasiyoshabihiana na Watu pamoja na Mazingira yetu japokuwa concept nzima ilikuwa inamlenga mwananchi. Nakubaliana na Nyerere sehemu nyingi sana za Azimio la Arusha hasa kutambua Umaskini, Maradhi na Ujinga (WATU) kuwa ndio maadui wetu lakini vita ya kupambana na aadui hao ilishindikana kutokana na serikali kuwa mmiliki wa means of productions..Hivyo kuufanya Ujamaa uliopo ktk misingi ya Kibepari kama Democratic ama Progressive kuonekana bora zaidi ya ule wa Kirusi au Kichina ambao uliwafanya wananchi wake kuwa sawa na wafungwa kutokana na hofu kubwa tulojengwa kuhusu Imperialist.

nakumbuka zamani sana wakati tunakua maeneo ya Kibara kuna sehemu inaitwa Kitengule. Huko kulikuwa na Simba wengi tu. Katika makuzi yetu tulikuwa tukiogopa kutoka nje usiku na mara nyingi sana tulisikia Simba kaua mtu hivyo watu tunatoka na kumsaka Simba huyo hadi anauawa maana Simba mla watu jua ni mzee ambaye hawezi tena kuwinda wanyama isipokuwa easy prey kama binadamu..Tuliendelea kuwawinda na kuwaua wakati makuzi ya makazi ya binadamu nayo yakipanuka ktk maeneo ya mbuga kuwafukuza Simba na Wanyama wengine far east warudi ktk makazi yao huko Serengeti. Leo hii Kibara hadi Bunda watu wanaishi pasipo woga wa kuliwa na Simba na miji hiyo imekua sana na maendeleo yanaonekana.

Hii ndio concept yangu kuhusu Mabeberu, walikuja Afrika wakatuibia mali zetu kwenda kujenga makwao, kweli ni Ujamaa ndio ulotuamsha sote baada ya wazazi wetu kurudi toka vita ya Burma na Asia. Huko Warusi na Wachina waliisha sambaza fikra na falsafa ya Ujamaa ktk kujikomboa dhidi ya Ukoloni na ukoloni mamboleo. Nasi tukawafukuza Wakoloni kama hatua ya kwanza kwa malengo ya kuunda makazi makubwa ya waafrika - Pan African na kulinda mali zetu ili kuhakikisha Simba hao hawarudi makwetu. Lakini hatukwenda deep zaidi kutazama mabaya (athari) ya Ujamaa kama ambayo huwaweka wananchi ktk hofu zaidi ya kuogopana hata wao wenyewe. Ujamaaa ilikuwa ujasiri wa kuishi kwa hofu, Ujamaa ulitujenga nidhamu ya woga badala ya kuwa huru hivyo tukashindwa kupambana na madui wa ndani yaani Umaskini, Ujinga na Maradhi kwa hiari yetu isipokuwa kwa kupandikizwa fikra.

Maadui wa ndani ni Ujinga. Umaskini na Maradhi sio WATU na hata kama wapo hawa ni MAFISADI sio Mabeberu. Hawa ni wahujumu Uchumi sio Imperialist hivyo unaweka misingi tofauti ya ku deal nao tofauti na kuwafungia wananchi wote Gerezani kwa hofu ya MABEBERU na MAFISADI wakati Ubepari sio kizazi cha mahasidi hawa bali ni HULKA za wanadamu wanotaka kutumia njia za mkato kujipatia Utajiri..
Nitaendelea baadaye..
 
Back
Top Bottom