@Mchambuzi shukuran tena kwa darsa hili lakini binafsi yangu nalitazama tofauti swala zima..Binafsi sikubaliani kabisa na ukweli kwamba Imperiarist inahusiana na Liberalization, Privatization, na Marketization isipokuwa ktk mazingira tuliyopo sisi na sio kufuata yaliyoandikwa vitabuni dhidi ya Imperialism.Nguruvi3,
Samahani kwa kutofafanua zaidi hili. Kuhusu Uzalendo, Kuhusu Uzalendo, sipingani na hoja zako, ni kwamba nina mtazamo wa ziada tu. Naomba nifafanue kidogo juu ya Utaifa. Sikuwa na maana kwamba all nationalists are gone, bado wapo wengi tu, and I believe you and I among them, and there are many other sisters and brothers of Nationalism ambao leaders the likes of Nyerere, Nkrumah, Samora Machell… made them (still do) proud of being Tanzanian, African…
When I say the project of Nationalism has stalled maana yangu ni kwamba: Kwanza, if you mention majina ya viongozi hawa to many of our university students (of Tanzanian origin) both at home and abroad, utakutana na one of the following:
- Either, many have no interest to hear more;
- Many do not recognize these names; or
- Many have very marginal knowledge about these names…
So hilo ni la kwanza;
Pili, ni kwamba ingawa bado brothers and sisters of nationalism tupo, uweo wetu hauna maana sana kama viongozi wetu don't act the same way or enact policies zinazoendana na aspirations zetu. Tukumbuke kwamba Nationalism was an ideology in itself iliyolenga kutupatia self determination kisiasa, kiuchumi, na kijamii kama nilivyokwisha jadili juu ya TANU. Lakini kwa bahati mbaya sana, haikuchukua zaidi ya miaka 25 tokea uhuru kwa hizi hopes and aspirations zetu kuanza kupata msuko suko; Since then, ideology of domination spearheaded na Liberalization, Privatization, and Marketization has replaced our Ideology of Self Determination as it was envisaged by TANU.
Viongozi wetu baada ya Nyerere have simply aborted the Nationalism Project, and bear in mind, this project is a big threat to Liberalization, Privatization, and Marketization. Ndio maana hivi sasa, badala ya viongozi wetu kutumia muda mwingi kuwa karibu na wananchi (nationalists) na kuelewa matatizo yao, hence follow up with appropriate actions and policies, viongozi wanatumia more of their time and our resources to ‘wine and dine' with the "imperialists."
Nationalism has an ideology has been man slaughtered; the imperialists in association with wakala wao ambao kwa bahati mbaya sana ni hawa hawa wanasiasa/viongozi wetu, are just ridiculing Utaifa wetu:
- Interests za nationalists ni kushinda vita dhidi ya our three main enemies of development Umaskini, Maradhi na Ujinga; Lakini eti tunaambiwa kwamba hilo linawezekana tukishirikiana na mapacha watatu wa imperialism Liberalization, Privatization, and Marketization?
That was my point – and I insist, our Nationalism project has been impaired, way beyond repair.
Ntarudi baadae kujaribu kujibu swali lako kuhusu the way forwad. Lakini lazima tuanze kwa kujitambua kwanza.
Umuhimu wa Liberalization, Privatization, na Marketization unatokana na mazingira tuliyopo sisi na sio kutazama wageni nje. kama kuna government restrictions ambazo ziliwakwaza wananchi ktk uzalishaji na usambazaji lazima tuzitazame upya na kuziondoa (deregulation) ama kuzipatia unafuu (relaxations) ili kujenga policies zinazolingana na mazingira yetu kiuchumi na Kijamaii.
Mkuu hoja kubwa ya vitu hivyo ni kuondoa madaraka makubwa walokabidhiwa serikali KUTAWALA hadi masiha ya wananchi wake wenyewe na ndio maana nasema Ujamaa uliogopa mabeberu (imerialists) kiasi kwamba ikaanza hata kuogopa wananchi wake wenyewe.
Hakuna sababu kabisa ya serikali kumzuia raia wake kumiliki ardhi au mali ikiwa lengo la Kupigania uhuru ilikuwa kurudisha mali hizo kwa wananchi wake. Sioni sababu ya Serikali kumiliki na kusimamia njia zote za uzalishaji ikiwa adui yetu Imperialist aliishwa ondoka na kurudishwa makwao sasa unapopingana na Liberalization, Privatization, and Marketization kama somo ina maana tunapingana na haya kutoka ndani na sio Mabeberu tena.
Sasa labda niwauliza Imperialist waliporudi makwao bado walikuwa wakiwaibia wananchi wao wenyewe au bado hutafuta mawindo ya nyama zao nchi za nje (easy prey) na kuwekeza ktk mfumo wa Ukoloni mamboleo. tena sasa hivi wamekuwa wakilinda kabisa hizo interest kwa kuweka majeshi, kutoa misaada na mikopo inayoweka ktk madeni makubwa zaidi..Imperialism haifanyiki Uingereza wa Marekani wao wanakuja kutuibia sisi na kujenga makwao and they are loving it.
Wewe unayeogopa kuibiwa kwa nini isitumie somo zima la Liberalization, Privatization, and Marketization ndani ili kutengeneza policies ambazo zitatuwezesha sisi uundwaji wa market system inayowalenga wananchi wenyewe na mazingira yetu sio kuendelea kuogopa Imperialist ambao hawapo tena nchini na hatuwezi kuwamaliza maana ndio kizazi chao kinachotakiwa sisi ni kuwasoma wao zaidi jinsi wanavyoweza jificha ktk nyasi kwa kutumia rangi zao kutumaliza..
I mean kama Imperialist ingekuwa mbaya hivyo mbona wao hawaibiani kiasi hicho (Simba hawezi kumla Simba mwenzake anaweza tu kumuua). Uchumi wa Uingereza ni ujanja ujanja tu kuiba nchi za nje na Linchi linakuwa tena wakiwa na social program kwa wananchi wake baabu kubwa na nyingi kuwashinda Urusi, China na Tanzania combined..as to say, Simba ni mnayama hatari na mbaya kwa wanyama wengine lakini sio kwa watoto wake mwenyewe..Natinalism ni pamoja na sisi kujifahamu kama ni Swala na riziki zetu zinapatikana vipi sio kufikiria tu kuliwa na Simba hivyo tunajifungia ndani na kufungwa kama nguruwe au ng'ombe wa kizungu.
Nitarudia kusema hawa ni sawa na SIMBA anayekwenda kuwinda mapori yetu (utandawazi) ya maliasili na rasilimali ili kuwalisha watoto wake. Huwezi kumuogopa Simba kiasi kwamba ukaanza kuogopa hata Swala wenzako ktk ulaji wa nyasi..Swala wataendelea kuhama kutafuta nyasi na Simba wataendelea kuwafuata Swala waendako hivyo tahadhari yetu ni kutazama tulipo sisi kama Simba wanaweza kusogea, lakini isituzuie hata sisi kula nyasi kwa hofu ya kulana sisi wenyewe. Hata kama tungeungana Afrika nzima (Pan Afrika) bado tungehitaji kuweka mfumo wa kiuchumi unaolingana na sisi na kila nchi ingetakiwa kuweka unafuu ama marekebisho ktk policies zake ili kutuwezesha kufanya biashara baina yetu na sio kuibiana. Ni makosa makubwa kwa serikali kumiliki na kuendesha njia za uzalishaji kwa hofu ya mabeberu..