Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Nguruvi3,

Samahani kwa kutofafanua zaidi hili. Kuhusu Uzalendo, Kuhusu Uzalendo, sipingani na hoja zako, ni kwamba nina mtazamo wa ziada tu. Naomba nifafanue kidogo juu ya Utaifa. Sikuwa na maana kwamba all nationalists are gone, bado wapo wengi tu, and I believe you and I among them, and there are many other sisters and brothers of Nationalism ambao leaders the likes of Nyerere, Nkrumah, Samora Machell… made them (still do) proud of being Tanzanian, African…

When I say the project of Nationalism has stalled maana yangu ni kwamba: Kwanza, if you mention majina ya viongozi hawa to many of our university students (of Tanzanian origin) both at home and abroad, utakutana na one of the following:


  • Either, many have no interest to hear more;
  • Many do not recognize these names; or
  • Many have very marginal knowledge about these names…

So hilo ni la kwanza;

Pili, ni kwamba ingawa bado brothers and sisters of nationalism tupo, uweo wetu hauna maana sana kama viongozi wetu don't act the same way or enact policies zinazoendana na aspirations zetu. Tukumbuke kwamba Nationalism was an ideology in itself iliyolenga kutupatia self determination kisiasa, kiuchumi, na kijamii kama nilivyokwisha jadili juu ya TANU. Lakini kwa bahati mbaya sana, haikuchukua zaidi ya miaka 25 tokea uhuru kwa hizi hopes and aspirations zetu kuanza kupata msuko suko; Since then, ideology of domination spearheaded na Liberalization, Privatization, and Marketization has replaced our Ideology of Self Determination as it was envisaged by TANU.

Viongozi wetu baada ya Nyerere have simply aborted the Nationalism Project, and bear in mind, this project is a big threat to Liberalization, Privatization, and Marketization. Ndio maana hivi sasa, badala ya viongozi wetu kutumia muda mwingi kuwa karibu na wananchi (nationalists) na kuelewa matatizo yao, hence follow up with appropriate actions and policies, viongozi wanatumia more of their time and our resources to ‘wine and dine' with the "imperialists."
Nationalism has an ideology has been man slaughtered; the imperialists in association with wakala wao ambao kwa bahati mbaya sana ni hawa hawa wanasiasa/viongozi wetu, are just ridiculing Utaifa wetu:


  • Interests za nationalists ni kushinda vita dhidi ya our three main enemies of development Umaskini, Maradhi na Ujinga; Lakini eti tunaambiwa kwamba hilo linawezekana tukishirikiana na mapacha watatu wa imperialism Liberalization, Privatization, and Marketization?

That was my point – and I insist, our Nationalism project has been impaired, way beyond repair.
Ntarudi baadae kujaribu kujibu swali lako kuhusu the way forwad. Lakini lazima tuanze kwa kujitambua kwanza.
@Mchambuzi shukuran tena kwa darsa hili lakini binafsi yangu nalitazama tofauti swala zima..Binafsi sikubaliani kabisa na ukweli kwamba Imperiarist inahusiana na Liberalization, Privatization, na Marketization isipokuwa ktk mazingira tuliyopo sisi na sio kufuata yaliyoandikwa vitabuni dhidi ya Imperialism.

Umuhimu wa Liberalization, Privatization, na Marketization unatokana na mazingira tuliyopo sisi na sio kutazama wageni nje. kama kuna government restrictions ambazo ziliwakwaza wananchi ktk uzalishaji na usambazaji lazima tuzitazame upya na kuziondoa (deregulation) ama kuzipatia unafuu (relaxations) ili kujenga policies zinazolingana na mazingira yetu kiuchumi na Kijamaii.

Mkuu hoja kubwa ya vitu hivyo ni kuondoa madaraka makubwa walokabidhiwa serikali KUTAWALA hadi masiha ya wananchi wake wenyewe na ndio maana nasema Ujamaa uliogopa mabeberu (imerialists) kiasi kwamba ikaanza hata kuogopa wananchi wake wenyewe.

Hakuna sababu kabisa ya serikali kumzuia raia wake kumiliki ardhi au mali ikiwa lengo la Kupigania uhuru ilikuwa kurudisha mali hizo kwa wananchi wake. Sioni sababu ya Serikali kumiliki na kusimamia njia zote za uzalishaji ikiwa adui yetu Imperialist aliishwa ondoka na kurudishwa makwao sasa unapopingana na Liberalization, Privatization, and Marketization kama somo ina maana tunapingana na haya kutoka ndani na sio Mabeberu tena.

Sasa labda niwauliza Imperialist waliporudi makwao bado walikuwa wakiwaibia wananchi wao wenyewe au bado hutafuta mawindo ya nyama zao nchi za nje (easy prey) na kuwekeza ktk mfumo wa Ukoloni mamboleo. tena sasa hivi wamekuwa wakilinda kabisa hizo interest kwa kuweka majeshi, kutoa misaada na mikopo inayoweka ktk madeni makubwa zaidi..Imperialism haifanyiki Uingereza wa Marekani wao wanakuja kutuibia sisi na kujenga makwao and they are loving it.

Wewe unayeogopa kuibiwa kwa nini isitumie somo zima la Liberalization, Privatization, and Marketization ndani ili kutengeneza policies ambazo zitatuwezesha sisi uundwaji wa market system inayowalenga wananchi wenyewe na mazingira yetu sio kuendelea kuogopa Imperialist ambao hawapo tena nchini na hatuwezi kuwamaliza maana ndio kizazi chao kinachotakiwa sisi ni kuwasoma wao zaidi jinsi wanavyoweza jificha ktk nyasi kwa kutumia rangi zao kutumaliza..

I mean kama Imperialist ingekuwa mbaya hivyo mbona wao hawaibiani kiasi hicho (Simba hawezi kumla Simba mwenzake anaweza tu kumuua). Uchumi wa Uingereza ni ujanja ujanja tu kuiba nchi za nje na Linchi linakuwa tena wakiwa na social program kwa wananchi wake baabu kubwa na nyingi kuwashinda Urusi, China na Tanzania combined..as to say, Simba ni mnayama hatari na mbaya kwa wanyama wengine lakini sio kwa watoto wake mwenyewe..Natinalism ni pamoja na sisi kujifahamu kama ni Swala na riziki zetu zinapatikana vipi sio kufikiria tu kuliwa na Simba hivyo tunajifungia ndani na kufungwa kama nguruwe au ng'ombe wa kizungu.

Nitarudia kusema hawa ni sawa na SIMBA anayekwenda kuwinda mapori yetu (utandawazi) ya maliasili na rasilimali ili kuwalisha watoto wake. Huwezi kumuogopa Simba kiasi kwamba ukaanza kuogopa hata Swala wenzako ktk ulaji wa nyasi..Swala wataendelea kuhama kutafuta nyasi na Simba wataendelea kuwafuata Swala waendako hivyo tahadhari yetu ni kutazama tulipo sisi kama Simba wanaweza kusogea, lakini isituzuie hata sisi kula nyasi kwa hofu ya kulana sisi wenyewe. Hata kama tungeungana Afrika nzima (Pan Afrika) bado tungehitaji kuweka mfumo wa kiuchumi unaolingana na sisi na kila nchi ingetakiwa kuweka unafuu ama marekebisho ktk policies zake ili kutuwezesha kufanya biashara baina yetu na sio kuibiana. Ni makosa makubwa kwa serikali kumiliki na kuendesha njia za uzalishaji kwa hofu ya mabeberu..
 
Mchambuzi,
Kwanza shukran sana ktk kuutafsiri UTU nahakika hakuna zaidi ya UTU wa binadamu isipokuwa uwezo wa kuchambua RIGHT and WRONG na hili lipo ktk maumbile ya binadamu wote likiitwa AKILI. Lazima nikubali ukweli kwamba mimi binafsi sielewi tafsiri sahihi ya neno AKILI kwa kiingereza ama lugha nyiingineyo zaidi ya kutumia neno SANITY.. maana sikubaliani na neno Intelligency ama mental capacity haya yanapunguza uzito wa maana ya neno hili maana wapo wanyama ni smart than us, na vipo viumbe wengi uwezo wa ku comprehend zaidi yetu, lakini kwa kutokuwa na Akili (reason of insanity) wanyama hawa hawana uwezo wa kuchambua right from wrong.

UTU kwa maana hiyo ni zaidi ya kufikiriana, kupendana na kadhalika maana hata wanyama wana uwezo huo lakini hawana AKILI inayotufanya ssi tuitwe Binadamu na viumbe tofauti na wengine wote hata yule nyani mwenye genetic DNA sijui 99.98 sawa na binadamu bado hana uwezo wa kuchambua..Na ndipo yale maneno matatu yanapochukua nafasi kubwa ktk uchambuzi na soundness of Judgment - 1. Freedom 2. Justice and 3. Equality. Tutabishana weee kuhusu haya matatu lakini kwa misingi ya kutazama what is right from wrong, mwisho wa siku tunaweza kubaliana kama sii wote basi wengi wetu the right thing is so and so..Japokuwa its very true ya kwamba what is around us mara nyingi sana hu influence our judgement..(WATU na MAZINGIRA)..

Mkuu Mkandara,

Asante sana kwa mchango wako mzuri; hoja zako zime stimulate my thinking, na naomba nijadili kidogo ingawa sitakuwa na mtiririko au mpangilio mzuri sana.

Kwanza, ni kuhusu neno 'AKILI'; nakubaliana na wewe kwamba tafsiri ya neno 'AKILI' ina utata, lakini mimi nadhani utata juu ya neno hili bado ungekuwepo hata kama dunia nzima ingekuwa inazungumza lugha moja tu; hii ni kwa sababu, hakimu kuhusu nani ana akili na nani hana akili, ni binadamu mwenyewe; Kwa mfano, umetaja neno 'SANITY' ambalo kwa uelewa wa jumla jumla, maana ya ‘Sane' - ni pale mtu anapoonekana kwamba he/she has a ‘SOUND JUDGEMENT', au ni mtu aliye ‘FREE FROM MENTAL DISORDER', au mtu ambae yupo ‘REASONABLE'. Lakini swali linalofuatia ni kwamba, ON WHOSE TERMS? Kwa bahati mbaya, HAKIMU juu ya nani ni SANE nani INSANE ni BINADAMU MWENYEWE/MTU, ambae anahusishwa na dhana tuliyoijadili i.e. Katiba za nchi nyingi (hata kwetu) zinaposema kwamba kabla ya mtu kushika nafasi fulani fulani za uongozi, ni lazima awe na akili timamu; je, tuna uhakika gani katika asilimia mia moja kwamba huwa tunachagua viongozi SANE (wenye Sound Judgement, walio Reasonable, walio Free from Mental Disorder)?

Tukiwa bado katika dhana hii ya ‘SANITY', je wanaotoa hukumu kwamba fulani ni ‘SANE au ‘INSANE', je kuna universal definition? Watu wanaotoa hukumu hii, je wote wamepimwa viwango vyao vya SANITY katika mazingira yanayofanana ili hukumu zao ziwe ‘Standardized'? Kwa maana nyingine, je, anaetoa hukumu hiyo nchini Marekani, mwingine nchini Australia, Canada, Ufaransa n.k, je wote hawa tumewapima viwango vyao vya SANITY ili tuwe na a standardized way to judge sanity and insanity? Hapa tusisahau pia kwamba mtu kuwa SANE maana yake ni kwamba yupo REASONABLE, na kuwa REASONNABLE maana yake ni kwamba kuwa FAIR, FREE FROM BIAS, FREE FROM SELF INTEREST, DECEPTION…;

Suala lingine ambalo umelijadili ni kuhusu whether or not BINADAMU ni most the most intelligent creature. Nakubaliana na wewe kwamba binadamu sio the most intelligent creature na ushahidi upo wazi kabisa. Kwanza, sisi na wanyama wengine kama tembo, nyati, n.k, tunaishi kwa kutumia UBONGO, hivyo kufanya UBONGO kuwa the Common Denominator kwetu sote; Pili, tunafahamu kwamba tunaishi kwa kutegemea vitu vinaitwa FIVE SENSES, na hizi zinafanya pale tu zinaposhirikiana na UBONGO; Sasa tukijidadisi na wanyama wengine, WHO MAKES MORE SENSE OF THE WORLD? Je sisi tuna uwezo ‘to make more sense of the world around us that other animals? – kwa mfano when it comes to abilities to see under different circumstances (eyes), uwezo wa kusikia (ears), uwezo wa kunusa (smell) etc. Hakuna ubishi kwamba kuna wanyama wengi waliotuzidi katika haya;

Pia kuna suala la ‘COMMON SENSE', ambalo wanadamu tuna tabia ya kutumia dhana hii kama njia ya kujipima ubora wetu na binadamu wengine; maana ya Common Sense kwa ujumla wake ni sawa tu na ile ya SANITY i.e. kuwa na "SOUND JUDGEMENT" ambayo binadamu wote wanategemewa kuwa nayo ili kuasaidiana na changamoto katika mazingira wanayoishi. Je, who makes better judgement katika mazingira yake bila ya kuathiri mazingira hayo kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadae? Definitely ni wanyama kwani tofauti na wanyama wengine, Binadamusisi tupo SO CONSUMED WITH SHORT TERM ECONOMIC GAINS KULIKO KWA MFANO THE ECOSYSTEM AMBAYO NDIO MHIMILI WA MAISHA YETU; kwa mfano, tupo obsessed na OIL huku tukujua wazi madhara yake kwenye ecosystem, lakini muhimu zaidi, huku tukijua wazi kwamba tuna uwezo wa kutumia nishati mbadala kwa urahisi na kwa gharam ndogo zaidi lakini We lack a very low level of INTELLIGENCE to comprehend that, or TO MAKE SENSE OF SUCH LOGIC;

Mifano mingine ipo mingi tu, - kwa mfano tunajua fika kwamba kuna aina fulani ya vilevi au vyakula ambazvyo matumizi yake yan athari kubwa kwa afya zetu na za wale wanaotuzunguka; lakini tupo tayari kuja kugharamia afya zetu baadae, au hata kufa ili mradi tu in the short run, we enjoy/we get leisure from consuming such, jijengea social status ya namna fulani n.k.katika haya, hakuna kiwango chochote cha maana cha intelligence au logic; Pia katika suala la siasa/uongozi, unakuta kuna Mijitu ambayo jamii inawaona kwamba ni Intelligent, Sane, etc, lakini unakuta ni hao hao wanakuwa upande wenye nia ya kuchakachua Katiba mpya ili mradi tu wafanikishe their short term gains (money, power, respect), bila ya kujali kwamba madhara kwa vitukuu vyao na vizazi vyao vya baadae yatakuwa makubwa; Lakini bado ni mijitu hii hii ambayo kutwa tunaipigia makofi na kuifagilia kwamba wapo BRAINY kwa maana ya kwamba they have unusual/impressive/extraordinary level of intelligence;

Mwisho niseme tu kwamba binadamu tuna tabia moja ya ajabu sana – Mtu aki ‘Behave' kwa namna tusiyoipenda, tunamuondoa kwenye UTU na kusema wazi kabisa kwamba "He/She is Behaving like an Animal, wakati ukweli ni kwamba kama tulivyokwisha ona, we are not the most intelligent species; Tuna ushahidi tosha kwamba kuna wanyama wa porini na hata wa kufuga, chungu nzima ambao ‘they behave with more Grace, Dignity, Wisdom & Morality kuliko Sisi Binadamu; Na kama ulivyogusia suala la RIGHT & WRONG, ambalo ni suala la MORALITY, hii ndio the most important measure of INTELLIGENCE. Mbwa tunaofuga majumbani kwetu kwa mfano, wote ni CANNIBALS – kwani hata nyama ya mtu kwao ni Chakula, lakini ni mara chache sana kusikia mbwa amekula binadamu, which means mbwa wengi behave with more grace, dignity, wisdom, morality, na pia Intelligence and SANITY kuliko binadamu wengi. Ndio maana mtu akiniita ‘MBWA WEWE', na kudhania amenitusi, mara nyingi huwa najihisi UTU ZAIDI.
 
Mchambuzi,
Shukrani nyingi sana tena kwa darsa hili la kisayansi katika mapana ya kujitazama sisi Binadamu ktk UTU wetu na kujitofautisha na wanyama wengine wasokuwa na AKILI. Hili ni swala zito sana ikiwa tutatumia vichwa vyetu vilivyoelimika kutokana na hisia zetu wenyewe za utambuzi wa yale yaliyotuzunguka.. Hii ndio maana ya ELIMU ya viumbe lakini bado haiwezi kuitafsir siri kubwa ya Mwenyezi Mungu ktk hili neno AKILI. Na hapa ndipo mimi kwa fikra zangu hujaribu kujipa urahisi ktk kujitambua ili kuepuka sana kutafuta undani wa tafsiri nzima ya neno hili AKILI ambalo ndilo hasa msingi wa Ubinadamu wetu na hivyo kujikita bktk imani ya dini maana hakuna Elimu dunia inayoweza kukupa siri na jibu la AKILI - Hakuna.

Kwa msingi huo basi ndio maana mimi hutumia haya maneno matatu UHURU, HAKI na USAWA ambayo wanyama wengine hawawezi kuwa na hukumu nayo isipokuwa Binadamu. Niaminivyo mimi AKILI ni the most important measure ya UTU wetu tofauti na viumbe wengine wote na sii swala la intelijensia zaidi isipokuwa ni la hisia za mwanadamu. Kwa mfano naweza sema "Una akili sana wewe" kwa sababu umenijibu nitakavyo au navyofikira ndio jibu sawa, lakini jibu hilo lisiwe sawa kwa mtu mwingine na tukasema hana Akili maana haya sii matumizi ya akili. Hata wale wenye Ubunifu wa vitu ktk kukidhi mahitaji yetu huitwa wenye akili lakini nao bado ni hisia ya kiinteligensia inayowezekana hata kwa wanyama na viumbe wengine kulingana na mahitaji yao. Akili inatuwezesha tu kutofautisha wrong na right ktk mazingira ya imani, itifaki na ktk mazingira yetu.

Akili inasimama pekee ktk kutambua na kusisitiza what is morality RIGHT or WRONG kwa jamii husika. Akili ni hisia nyingine kabisa ambayo binadamu pekee ndio anayo na naweza sema hii ni The SIX SENSE ambayo mwanadamu pekee ndio kajaaliwa maana ni sisi binadamu tu tunaoweza kuumiza vichwa kwa kusema mathlan - "Kutembea Uchi ni morally wrong au right", Ushoga ni morally wrong au right na hivyo hufuatia kuweka madai ya UHURU, HAKI na USAWA kukidhi au kupinga hisia hizi kwa wahusika. Lakini hapo hapo haina maana kwamba WATU waliokataa kutembea Uchi au Ushoga basi hawa hawana AKILI zaidi ya wale waliokubali...Ndipo hapa mimi huingiza swala la Itifaki kuwa muhimu zaidi. Na lo hutokana na watu wenyewe kujitambua who they Are in the first place..

Nitarudi ktk mfano wa kundi la wanyama, Sisi Watanzania ktk Pori hili la dunia ya Utandawazi (Mbuga yetu) sisi ni Wanadamu gani?.Kuwa binadamu tu haitoshi hata kidogo maana wazungu wakoloni wale mabeberu nao ni binadamu kama sisi lakini somo hili la UTU wao wanalitazama tofauti na kwa maisha yao. Hili swala la kujitambua mkuu wangu ni muhimu sana kuji Identify who we are ktk kundi la binadamu wote maana ni lazima tufahamu Mabeberu (imperialist) wametuzunguka kama Simba wa Serengeti. Kuna Misimba ya Ulaya wakiwinda kwa ukoo na kizazi, Kuna Mifisi ya Kichina ambayo hushambulia kwa makundi (mande) na hula mnyama hata akiwa hai bado na kadhalika (the most brutal cannibal looks innocent kwa kicheko chake). Kuna Mimamba wa Kirusi na jingine baya zaidi ni serikali ambayo mimi nawaita Binadamu wanaojiita WAJAMAA watakulisha, wanakutunza na kuonyesha mapenzi makubwa kumbe wanasubiri unenepe tu wakuchinje (Tazama ng'ombe 50 millions are slaughtered everyday to feed us Human!).

Hivyo basi Tukisha jitambua sisi kina nani kama jamii ya Watanzania ktk kundi la msafara wa Waafrika basi ni rahisi kwetu kutafuta mbinu za kujilinda kama Nyati au nyumbu ambao maisha yao yote hutembea pamoja na kwa makundi makubwa sana ili kujilinda dhidi ya wanyama cannibals na pia Umoja wao ktk kutumia hisia zao kutafuta riziki za Mwenyezi Mungu.

Nitaendelea kusisitiza hili ktk mjadala huu wa katiba maana hatuwezi kuitunga katiba pasipo sisi wenyewe kujitambua kwanza sisi ni nani na Mazingira yetu yapo ktk global position ipi na nini fursa na riziki ambazo tumejaaliwa kuwa nazo kwa kipindi cha mzunguko wa mwaka au miaka kwa faida ya kizazi kijacho. Laa sivyo tutaendelea kujaeribu kuyabadilisha mazingira around us to suit us au tuwe kama Ulaya tukidhani ni maendeleo yetu kumbe ndio distruction kubwa ya ecosystem na kizazi kijacho..

Tukifikia maamuzi ya kujitambua kuwa sisi ni Nyati wala sio Swala au Nyumbu ktk dunia hii ya Utandawazi basi tunajiunga na Pundamilia, nyumbu na swala (Africa Union) ktk msafara wa kuyatafuta maendeleo lakini maslahi yetu sisi Nyati yanatangulia. Tutaweza kuwajua maadui zetu wakubwa kina nani, itifaki zetu sisi tofauti na zile za swala, Pundamilia na nyumbu, tumepewa vipaji gani kama nyati kimaumbile na kitamaduni na hapo ndipo mwanzo wa kujitambua. Wakati wa Nyerere tukisema - HEKIMA, UMOJA na AMANI, hizi ni NGAO zetu (wimbo wa Taifa) sijui ni lini tulipoteza kuthamini ngao hizi na kwa nini?. Hivyo napokosana na JingalaFalsafa ni pale anapotumia mapana ya neno UTU kuwatambua wanyama wote mwituni na kuwataka wote tutumie Unyama wetu wa kibinadamu ktk kuutukuza UTU wakati wale wenzetu ni Simba, wengine Mafisi, Mbwa mwitu na kadhalika japo wote tuna hisia hii ya SITA (AKILI)i ambayo kwao wanaitumia ktk ubinadamu wao ili kukidhi mahitaji na maendeleo yao.

Ni jukumu letu sisi kujitazama sisi na sio binadamu wote kwa fikra za kuwabadilisha. Uingereza, Marekani na nchi nyingi za Ulaya wataendelea kuwa Mabeberu (Imperialist) kwa sababu ndio njia pekee inayo wawezesha kupata maendeleo ya jamii yao na pengine yawezekana kuwa adui mkubwa wa UTU wa binadamu wote ni Maendeleo yenyewe.
 
Mkuu Mkandara,

Asante kwa mchango wako mzuri kwani unaamsha mjadala mzuri na muhimu sana kwa taifa letu. Naomba nianze kwa kusema kwamba mimi sina ugomvi na Ubepari kwani nina amini kwa dhati kabisa kwamba hakuna mfumo bora wa wealth creation kwa jamii/mataifa kuliko Ubepari, vinginevyo tutakuwa tunajidanganya. Tatizo langu kubwa ni kwamba NJIA tunazopitishwa sisi nchi maskini – mwendo wa kukimbizwa kimbizwa bila maandalizi ni njia za maangamizi. Historia inaelezea kwa uwazi kabisa jinsi gani mataifa yaliyofanikiwa na Ubepari yalifanye nini kufika yalipo leo, kwa mfano Marekani, Japan, na hata Asian Tigers (Korea ya Kusini, Malaysia n.k). Nadhani utakubaliana na mimi kwamba hawa wote walipitia njia tofauti na ile ambayo leo tunaelekezwa tufuate. Sidhani kama una mfano hata mmoja wan chi maskini ambayo imefanikiwa kwa kupitia njia tunayolazimishwa sisi. Hatuwezi kwenda popote kwani hatujafikia ‘take-off' stage ambayo inahitaji maandalizi makubwa (radical) na ya muda mrefu.

Kwa kweli inasikitisha kwamba wengi wetu tumenogewa na Ubepari na kuaminishwa kwamba ndugu zetu vijijini watakuja nufaika chini ya mfumo wa sasa. Kinachoendelea sasahivi ni Ubepari wa kisanii kwani ni mataifa yale yale yaliyotunyonya wakati wa ukoloni na their imperial companies kama Barclays, leo hii tumewarudishia tulichowanyanganya. Mwisho wa siku, wanaofaidika ni wakubwa wa huko nje pamoja na mawakala wao (wengi wao wakiwa ni viongozi/wanasiasa wetu), hawa wote wanashiriki katika ubepari from the CENTRE wakati walio wengi ushiriki wao ni from the PERIPHERY. Mkuu Mkandara, unakubaliana na mimi katika hili na kwamba hii ni moja ya sababu kubwa kwanini Ubepari utaendelea kuwa kiini macho kwa watanzania wengi almost indefinitely?

Wahenga wetu walinena kwamba – UKIONA VYAELEA, UJUE VIMEUNDWA. Mkuu, una mifano gani hai na endelevu ya kunipa kama kielelezo kwamba Ubepari katika nchi za dunia ya tatu, hasa Afrika umewaletea wananchi walio wengi faida? Mimi sidhani kama upo mfano wowote, na sababu kubwa ni kwamba tumekosa maandalizi ambayo yatatusaidia ‘to take off' na ubepari, na ukoloni mamboleo unafanya jitiada za makusudi to suppress that; Tumekuwa tunapewa hadith nyingi sana na wanazuoni mbali mbali na hata wanasiasa wetu kuzidakia riwaya hizi kwamba eti in the 1960s, tulikuwa sawa na Asian Tigers kimaendeleo (mfano South Korea), lakini wao wakawa makini zaidi na ndio maana leo wapo mbali.

Sehemu ya kwanza ya riwaya hii ina mashiko kidogo kwani South Korea in early 1960s ilikuwa 80% vijiji, na less than 20% of the population walijua kuandika na kusoma; lakini sehemu ya pili kwamba walikuwa makini zaidi yetu ni UWONGO; Huu ni upuuzi; hizi ni riwaya zinazolazimishwa ziwe UKWELI na its only the fools who buy them; Vinginevyo hakuna siri kwamba nchi kama South Korea zilijengwa kwa makusudi na mataifa ya magharibi kama njia kuu to contain spread of communism wakati wa cold war; Kilichokuwa kinaendelea South Korea kwa mfano ilikuwa ni State – Led Capitalism guided by the USA, UK… kama njia ya kudhibiti jamii hizi zisione ukomunisti una mvuto; Vinginevyo nchi kama South Korea hazikupitia Natural Process kuelekea Capitalism bali walibebwa bebwa, pakatwa pakatwa, na kulindwa mpaka walipofikia ‘take off' stage; Ugomvi wangu na Ubepari ndio hapo, kwamba waliopendelewa ndio tunaambiwa an wakubwa hawa kwamba tuwaige kwani wao ni mfano mzuri.

Naomba pia nijadili kidogo hoja yako kuhusu IMPERIALISM; Napingana na hoja yako kwamba imperialism haina uhusiano na Liberalization, Marketization and Privatization, kwani hizi ndio tools muhimu za kufanikisha imperialistic interests za mataifa makubwa katika nchi maskini. Sijui wewe unaielewaje dhana ya IMPERIALISM lakini kwa uelewa wangu, Imperialism was simply ‘a deliberate foreign policy that governed international relations huko karne za nyuma; Naposema mahusiano, sina maana ya DIPLOMACY, bali uhuni, uvamizi, utapeli n.k. Na hii haikuwa baina ya mataifa makubwa na madogo tu bali hata wao wenyewe (wakubwa);

Tumejifunza katika historia kwa mfano jinsi gani Ujerumani ilivamia majimbo ya Ufaransa ya ALSACE & LORRAINE, kwa nia ya kupora ardhi zenye madini na mizabibu; Vile vile mataifa makubwa haya yalifanya uhuni kama huu kwa jamii nyingine za mbali kama kwetu Africa; hiki kilikuwa ni kipindi cha PRIMITIVE ACCUMULATION OF CAPITAL ambapo hapakuwepo SHERIA ZA KIMATAIFA, UTARATIBU WA VISA KUINGIA TAIFA JINGINE, UMOJA WA MATAIFA, SUALA LA HAKI ZA BINADAMU, MAHAKAMA YA THE HAGUE n.k. It was all about the survival of the fittest. Players wakubwa katika hili walikuwa ni Uingereza, Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Hispania, Ureno, Ubelgiji n.k. Ni miaka ya baadae after wakubwa hawa kujiwekea all the necessary foundations to enjoy Ubepari, ndio wakaleta vitu kama Declaration of Human Rights, United Nations n.k; Ni dhahiri kwamba yangekuwepo haya wakati wa kipindi cha primitive accumulation of capital, pasingekuwepo na unfair treatment iliyojitokeza;

Vinginevyo IMPERIALISM ilikuwa ni sera iliyolenga ‘to extend RULE, CONTROL & DOMINATION, hasa dhidi ya jamii kama zetu Afrika, hasa KIUCHUMI, huku Politics and Culture zikitumika kama ideological tools kufanikisha lengo hili. Imperialism was an aggressive policy kwani they used force to extend authority, rule, control and domination outside their borders, na hata leo tunaona tabia zile zile huko Iraq, Libya n.k. Ndio maana napingana na wewe kwamba hakuna uhusiana baina ya Imperialism Liberalization, Marketization na Privatization. Sidhani kama leo hii mtu unaweza Foreign Policy za mataifa makubwa ya kibepari bila ya kujadili pia International Trade, Foreign Direct Investment & AID; vile vile, hauwezi kujadili foreign policy bila ya kujadili imperial interests za wakubwa ambazo bado zipo na zinatekelezwa na sera chini ya Liberalization, Marketization na Privatization.

Naomba nisisitize kuhusu ‘PRIMITIVE ACCUMULATION OF CAPITAL'. Karne za huko nyuma, kama nilivyogusia kidogo awali, dunia ilikuwa inaendeshwa kihuni huni na kibabe babe. Mataifa makubwa yalitumia kila aina ya ujanja ujanja na utapeli kujikusanyia mitaji, malighafi, nguvu kazi n.k, na mwaka huu 2012, bado hatujafikisha hata karne moja tangia wakubwa hawa wamalize vita vya wenyewe kwa wenyewe iliyotokana na uhuni huu. Lakini kikubwa ni kwamba wote walikuwa wanajitengenezea mazingira ya kuwa self sufficient, self reliant n.k ili waweze to take-off without crashing na mfumo wa ubepari; Kwa mfano, Ebu Jiulize, je ni kwanini Utumwa ulitokomezwa? Was it because walikuja gundua kwamba ni kinyume na haki za binadamu? Jibu ni hapana, the overriding reason was the invention of machines which made it cheaper kuliko kutumia human labour. Vinginevyo philanthropists, religious leaders walipiga kelele nyingi sana kwa miaka mingi sana, lakini haikubadili kitu; Jiulize, je why the Human Rights Declaration in 1948 and not in 1885?

Mimi nadhani majibu kwa maswali haya ni marahisi sana kwani Sheria za kimataifa n.k, vilikuja kuwa muhimu baada ya wakubwa kukubaliana kwamba tayari they have "an advantage" na sasa ili kuzuia malumbano baina yao ambayo yangeharibu walichovuna, na pia kuweka control kwa mataifa waliyoyachuna, ni muhimu kuanzisha UN System, Haki za Binadamu n.k, kwani singingejalisha sana kwa sababu wakubwa hawa tayari walikuwa wameshafikia ile THRESHOLD ya kuweza ‘to take off' na ubepari without crashing; Na kwa vile ile threshold wameshaifikia ndio maana ni rahisi kwa wao leo hii kuungana/kuwa wamoja kwa mfano "EU", huku wakiendelea kujitenga kwa mtindo ule ule imperialistic na kujiita 'G-8', huku yale mataifa ambayo wanaona yanaweza kuwa tishio wakiyakaribisha kwenye ligi daraja la pili inayoitwa "OECD" ili na wao wajione wamo, huku mataifa mengine madogo madogo yakiendelea kunyonywa kwa mtindo ule ule under PRIMITIVE ACCUMULATION OF CAPITAL, lakini this time around, wameipa hii capital accumulation a sexier approach ya kiini macho huku wakijua kwamba kwetu haian faida kama kwao - Liberalisation, Marketization na Privatization, na kuweka mivitu kama THE HAGUE etc ambako wanaohukumiwa ni wanyonge tu, na haitatokea mkubwa wa G-8 akapelekwa huko!!!!

Naomba nirudie tena kwamba I am not disqualifying Ubepari per se; nachohimiza ni kwamba, kutokana na historia kuwa unfair kwetu, tunahitaji kuwa na some sort of a guided capitalist system kama ilivyotokea kule Asian Tigers mpaka tufikie the ‘take off' stage, vinginevyo majority ya watanzania watabakia maskini indefinitely. Na ndio maana Mwalimu alikuja na Ujamaa kwani aliogopa Ubepari na uwoga huu ni justified kabisa; na kwa Mwalimu, Ujamaa was meant to be a temporary state, not permanent. Lakini kama nakusoma vizuti, unajaribu kutuaminisha kwamba sisi Tanzania we can LEAPFROG hatua zoooooooote za relations of production na kurukia behewa la Ubepari bila ya matayarisho au bila ya kupitia hatua walizopitia wenzetu, aidha naturally au kwa kupakatwa pakatwa kama ASIAN TIGERS; vinginevyo hatua walizopitia wakubwa hawa zilitawaliwa na kila aina ya uhalifu - umwagaji wa damu, unyang'anyi, utapeli, n.k, na hadi leo, kwa kiasi kikubwa sana, bila ya uhalifu huu ambao unapewa sexy names kama globalization, mataifa makubwa hayawezi kujisikia amani na huru chini ya Ubepari;

Kwa kumalizia naomba nikuulize pia je:


  • Since 1986 mpaka leo (miaka 26), ni dhahiri kwamba soko huria nchini Tanzania halijamtendea haki mwananchi wa kijijini, je unadhani ni kwa sababu gani?


  • Pia je, MAPACHA WATATU WA UBEPARI - Liberalization, Marketization & Privatization, tunawezaje kujenga URAFIKI & USHIRIKIANO baina ya mapacha hawa na MAADUI WATATU WA MAENDELEO Tanzania kwa miaka zaidi ya 50, UMASKINI, MARADHI na UJINGA ili taifa lisonge mbele?


  • Mwisho kwa ujumla wa hoja zangu, Je nini maoni yako kuhusu kauli ya Mwalimu (Mwongozo CCM, 1982):

"Ilidhihirika katika miaka hiyo ya mwanzo ya uhuru wa Tanganyika kuwa mgongano ulianza kujengeka kati ya matazamio ya wananchi jumla kwamba uhuru ungaliwaletea mabadiliko katika hali ya maisha yao na kwa haraka, na uwezo mdogo wa Serikali wa kukidhi haja za wananchi kulingana na matazamio yao. Mabadiliko makubwa ya mapato na hali ya maisha yaliyoonekana kwa wachache, viongozi na maafisa wa madaraka yaliyokuwa yanashikwa na wakoloni zamani, pamoja na vitendo vya baadhi ya viongozi na maafisa hawa vya kuanza kutumia nafasi zao kujitajirisha, viliimarisha mgongano huo. Tafsiri ya hali hii ilijitokeza wazi wakati umma ulianza kuwaita wale walioonekana wanafaidika kwa vyeo vya uhuru "Naizesheni" wakati wananchi waliobaki kuitwa Baba kabwela".
 
Mchambuzi,
Shukuran kwanza nianze na UBEAPARI. Kinachotukandamiza sisi sio Ubepari bali yaliyomo ndani ya Ubepari hivyo hata yaliyotrukandamiza sisi sio UJAMAA bali yaliyomo ndani ya Ujamaa kwa maana hiyo hayakulingana na watu na mazingira yetu. Sisis tulifundishwa Ujamaa ni hivi na Ubepari ni hicvi tukachukua kama vilivyo na ndio maana nasema tulipewa mbegu za Ulaya na kujaribu kuzipanda kwetu Afrika hivyo hazikuweza kuota.

Katika Ubepari tumeletewa Utandawazi na soko huria (hivi ni vipya havikuwepo zamani jaokuw ubepari ulikuwepo kabla. Hivi ni vitu ambavyo sisi hatukujiandaa navyo wala sio ktk maisha yetu ya kila siku. Mtu hujikuna anapofikia hivyo nachoweza kusema sio swala zima la Ubepari kuwa haramu kwetu isipokuwa tutazame upana wake na nafasi yetu sisi. Sisi ndio tuloibiwa mali zetu hivyo Ubepari wao lazima uliambatana na Imperialism. Walipigana hadi vita ktk kugawana majimbo ya Afrika na kama unavyoona sasa tuna matatizo ya mipaka baina ya Tanzania na Malawi na nchi kibao za Afrika bado zina migogoro yake ya mipaka kutokana na kutawaliwa. Bado nchi za kiafrika wanafikiria mipaka ya nchi ndio Utaifa wao badala ya uhuru kuwa ni wa watu wake na milki nya mali hizo..

Hivi kuna haramu gani kwa Mtanzania kumiliki mali au njia za uzalishaji na kuviuza, serikali ikakusanya kodi zake. Huyu Mtanzania atakuwaje ama kuitwaje Imperialist ikiwa anazalisha ndani anasambaza ndani na nje kwa wahitaji wa mali zake kulingana na soko na kuwekeza ndani nchini - Sidhani kama fikra za mtu ku own kitu kunamfanya awe Imperialist maana utamaduni huu tulikuwa nao hata kabla ya mkoloni kuvamia Afrika.. Wazee wetu walimiliki mashamba, mifugo na hata mashua za uvuvi na walanguzi walisambaza mali hizo wakiziuza kwa wananchi na hata ilijulikana wazi kabla ya ujio wa wazungu watu wa Asia na ghuba ya Arabuni hao Waajemi, washiraz, Wahindi, waburush na Wachina walikuja Afrika mashariki (zanzibar) kwa pepo za Monsoon kununua bidhaa zetu. Wakati huo tulifanya biashara na wageni lakini baada ya kutawaliwa mali zetu zilichukuliwa bure na tawala hizo na kuwa mali zao wenyewe wakazijenga nchi zao. Sisi tukaingia utumwani na toka hapo ndio picha ikabadilika.

Unapozungumzia swala la nchi yoyote maskini kufaidika na Ubepari kusema kweli huwezi kupata mfano ikiwa sisi bado tunaibiwa ktk Ukoloni mamboleo na sii Ubepari. Bado nchi za Ulaya zinategemea malighafi kutoka Afrika na makosa makubwa tuloyafanya ni kufikiria kwamba tulidai uhuru wa mipaka ya nchi zetu tuwe huru pasi kutawaliwa na wageni. Kumbe harakati za Uhuru wetu ziliasisiwa sii kwa kuondoa Utawala wa mzungu na kumweka mtu mweusi bali sisi wenyewe kuwa wamiliki wa maliasili na rasilimali zetu na haki ya kuzilinda.

Toka tumepata Uhuru nchi zote za kiafrika tumeshindwa kuzilinda maliasili na rasilimali zetu badala yake tumejigubika ktk Ukoloni mamboleo na kutazama sana mipaka na sovereignty ya nchi huru. Hata wale waliokataa kuibiwa (Ujamaa) nimezungumza wazi makosa yalifanyika wapi ktk kujidungia magereza wenyewe wasiweze kujiendeleza. Bado neno langu la leo ni kwamba Wananchi wenyewe WAZAWA ndio wanatakiwa kuwa wamiliki wa maliasili na rasilimali za Taifa. na ktk kujikinga na ukoloni mamboleo tulihitaji umoja wa nchi za Kiafrika kama wale nyati, Pundamilia na nyumbu wanavyotembea pamoja ktrk mbuga za Serengeti hii inapunguza sana kushambuliwa hovyo ama kuweka kinga kwao hata Simba anapojaribu kuwavamia hutafuta urahisi uko wapi..

baada ya kupoteza dira hiyo ndio maana nchi maskini zimeshindwa kuendelea halafu kama ulivyosema hatujafika bado ktk stage ya take off bado tunakabiriwa na Umaskini, Ujinga na Maradhi ambayo ni sawa na Ugonjwa. Hivyo inatakiwa tiba kwanza ili tupate nguvu ya kuanza kupiga hatua ya kwanza. Na maadam tumeshindwa hata kufuta umaskini, Ujinga na Maradhi karibu kwa nchi zote za kiafrika tutaendelea kubakia shimoni. Gari lilokwama ni lazima ulitoke kwanza shimoni kabla hamjafikiria kuanza safari upya, lkn tatizo la viongozi wetu wanaifanya safari hii kama marathon. Wao wanataka tukimbie hivyo hivyo pasipo kujali ulemavu wetu ktk sehemu hizi tatu.. hatutaweza kufika popote tairi linazunguka tu palepale...

Swala la Imperialist, kaa ulivyoelezea tafsiri yake utaona hakuna mahala panahusiana na Liberalization, Marketization and Privatization isipokuwa kwa mtazamo wao. Kwa hiyo kila waliloliweka ktk mfumo huu walijitazama wao na mahitaji yao hivyo haipotezi maana kwetu tukiyatumia maneno hayo hayo kwa wale wanaojikinga na Imperialism. Liberazation ni mtazamo dhidi ya kile kilichotangulia na hata kuna watu kama Khomein alipotaifisha mali zote za Shah yeye aliziweka ktk soko huria na kuuzia wafanyakazi wa mashirika hayo shares. Ubepari uliendelea kama kawa lakini ni wananchi wa Iran ndio walomiliki nmali za nchi hiyo lakini tofauti na sisi serikali ndio ilochukua mali zile na kuziweka ktk himaya yake. Imperialist inaweza kutafrika kwetu kama vile utawala wa CCM unavyoweza kutumia nafasi hii kujitajirisha wao lakini hatuwezi kusema hivyo. Hawa ni Mafisadi ni watu wanao hujumu uchumi wa nchi japokuwa uporaji wa mali kwa manufaa binafsi unafanana.

majibu ya maswali yako yote ni TUMEPOTEZA DIRA.. kama tungeendelea kupambana na Umaskini, Ujinga na Maradhi (haya mambo matatu yakawa kazi na jukumu kubwa la serikali)Wakati wananchi wenyewe wakiwa wakimiki maliasili na rasilimali zetu, wakilipa kodi na kuongeza uzalishaji ili kukidhi hata uhaba ulokuwepo nina hakika tungepiga hatua kubwa zaidi lakini bahati mbaya tumeingia ktk Ubepari pasipo kutajirishwa. Viwanda vilivyokuwepo viliuzwa kwa wageni ama kufilisiwa kwanza yakabakia magofu ilihali watanzania wenyewe hawana mtaji. Hivyo kutokana na umaskini wa wananchi na hasa wa kijijini kukosa hata mikopo ya ukulima, utajirisho ktk nafasi zao za uzalishaji ilitufiisha hadi tukaanza kula Mbegu zetu. nakumbuka kuna mbegu za mchele ambazo zilikuwepo miaka ya 1985 huipo tena bali zipo za maabala ambazo zinahitaji mbolea na ghali kwa mkulima maskini.

Maadam tumedharau Umaskini Ujinga na maradhi kuwa maadui wetu na haki ya kila Mtanzania na kuviweka sokoni kwa mwenye uwezo akasome, akatibiwe basi umaskini, Ujinga na maradhi havitaweza kwisha. Liberalization, Marketization and Privatization vina wezekana tu ktk sehemu ambazo sii RIGHT ya mwananchi kulingana na watu na Mazingira yetu. Hata ktk malezi ya kifamilia kuna yale ambayo ni haki ya mtoto na sio privilege na upo uhuru fulani lazima mtoto apewe ili makuzi ya utoto wake umwezeshe kuongeza vipaji, nguvu na furaha .

Kumjali mtoto haituzuii kuboresha tamaduni za malezi ambazo yalimfubaisha mtoto hata kama sii tamaduni zetu kama vile kwenda shule, kuifunza michezo, sanaa na kadhalika huingia ktk sehemu ya malezi bora na muhimu japokuwa mambo haya yatagharimu fedha..Ndio maana nasema wakati mwingine haya maendeleo yenyewe ndio adui wa maskini maana tunayataka lakini hatuna uwezo.
 
Pamoja sana Mkuu wangu Mchambuzi:
Nami niongezee kidogo kuhusu Ubepari au Ubeberu (japo nitapingwa)!
Falsafa kuu ya Ubepari ni "Private Ownership", ndio maana Mkuu Mkandara amekuwa haoni ubaya wa dhana hiyo! Lakini kumbe alipaswa kuanza kuichambua... ilikotokea wapi? Itaishije/itafanikishwaje? Na italeta matokeo gani kwa nani na nani?
Binafsi naamini kuna "bad and good human qualities"
zile ambazo ni mbaya huitwa HULKA na zile ambazo ni nzuri huitwa MANTIKI/UTU.
1. Tujiulize sasa wapi ilikotoka dhana hii kati ya HULKA na MANTIKI?
2. Ili kuifanya dhana hii kuwa hai, ni wazi lazima kuwe na "mechanisms" to make the concept sustainable! Binafsi ukiniuliza lini hasa Uberai ulianza, nitakujibu ni tangu Utumwa, Ukabaila, Ulanguzi, Uchumi wa Viwanda, Ubeberu/Ukoloni, Ukoloni Mamboleo hadi Utandawazi. Hizo ndio Running Forces za "Private Ownership". Logically, unaporuhusu dhana hii kuishi basi ni wazi Unaruhusu moja kwa moja Tabaka Tegemezi, kwani kuna wale watakaoshindwa katika ushindani wa Fursa! Hawa lazima watawategemea wale wa waliowahi au kushinda ule ushindani. Atalazimika kumtumikia mshindi aweze kuishi! Na ili mshindi asijekuwa tegemezi, ni lazima ahakikishe mtumishi wake anabaki kuwa mtumishi siku zote! Ndipo hapo ulipoibuka "UNYONYAJI". (Karl Marx alihoji juu ya "Value of Labour" kipi ni kipimo chake?)
Nitakulipa mshahara finyu ili kesho usije pata mtaji wako!
Nitapokea rushwa kulinda maslahi yangu!
Nitakuua kulinda maslahi yangu!
Nitakufanya mtumwa!
Nitakudharirisha kuutukuza Ukuu wangu! Lengo ni kulinda nafasi yangu niliyonayo! Nawe hutokubali tu, kwani nawe unapigania Private Ownership yako, utawinda nafasi yangu kila leo!
Utaniibia!
Utanifanyia fujo.
Utahujumu mali zangu!
Utanichukia. Hayo ndio MATUNDA ya "Private Ownership"
3. Niliwah kusema hapa, kuwa Ubepari ni "Kupigania Ukuu kwa njia yoyote- na hakuna kilichojuu pasi kushikizwa! Yaani uwepo wa mkoloni hutegemea sana uwepo wa mkoloniwa" katika social life yetu tunaita UNYONYAJI, yaani kutumia rasilimali ya mtu kujinufaisha binafsi. Hili linapotokea baina ya mtu na mtu, mimi huita INTERNAL CAPITALISM/EXPLOITATION. Na pale inapotokea Taifa kuwa juu ya taifa, mimi huita EXTERNAL CAPITALISM/EXPLOITATION. Hizi ni atua mbili katika ubepari, hakuna afikiaye hatua ya pili pasikupitia hatua ya kwanza ili kukusanya nguvu!
Sasa wenzetu magharibi wameshafiki hatua ya pili, kufika na uwepo wao hapo unategeme sana nafasi yetu hapa! Kunyanyuka kwetu ni kuanguka kwao! (then tunaleta mzaha, kwa kufikiria kitoto-bungeni watu wanaenda kusutana, katiba kama sheria za shule).
Sasa swali:
Sisi tunataka kufikia Take Off Stage, nani ni mnyonge wetu kumfanya ngazi na nguzo ya kutushikiza? Je, sio Malawi na Burundi? Je, hao si Waafrika wenzetu? Tunataka kuupeleka UAFRIKA WETU wapi, kwa ushawishi wa watu Wapumbavu wazungu? Je, hizo ni hulka zetu ama MANTIKI? Je, Malawi atakubali tumfanye daraja? NEVER! Atatukwamisha tu, kama sisi tutakavyomkwamisha yeye atakapotaka kutufanya daraja.
Tafsiri ya Maendeleo kwa mtu Mweusi ni UTU si KITU kama watufundishavyo wale WASHENZI ngozi nyeupe. UTU unajenga KITU lakini si KITU kwa UTU.
Mkuu Mkandara unasema tumepoteza Dira. Nami nakubali. Maswali!
-Ipi?
-Ilikuwa inatutoa wapi kwenda wapi?
-Kwa faida ya nani?
-JE, KUNA HAJA YA KUIGEUKIA TENA? Kwanini?
(Azimio Jipya, aligusia haja ya kuwa na Falsafa ya Taifa)
Haki na Uhuru ni Mbeleko ya Private Ownership nayo ni zao la Umimi ambao ni mama wa UNYONYAJI, rafiki wa rushwa, vita, ufisadi, nk.
.............
Mungu wetu anaita sasa!
 
JingalaFalsafa,
Nikuulize hivi wazee wetu hawakuwa na barter - system of exchange goods hapo zamani? Je hiyo haikuwa ktk Ubepari?..
 
Mkandara,

Shukrani mkuu. Umezungumza suala la msingi sana kwamba tunaumizwa/ibiwa na ukoloni mamboleo lakini sio Ubepari; Upo sahihi kabisa kwamba tatizo sio UBEPARI bali wale wanao practice ubepari kwa faida yao; Vinginevyo kwa kweli hakuna sehemu inayosema kwamba Ubepari ni unyonyaji, utapeli, unequal exchange or lolote linalofanana na hilo; pia hakuna sehemu yoyote inayoeleza kwamba Ubepari umetengwa kwa faida ya watu wa aina fulani, tabaka fulani, au jinsi fulani; Vinginevyo ubepari ni mfumo huru kuliko yote iliyowahi kutokea, na mfumo bora zaidi katika creation of wealth na prosperity ya wanadamu, kuliko mfumo mwingie wowote;

Tukitazama definition ya Ubepari, kwa kweli hatuoni sehemu yoyote inayokinzana na haya niliyojadili hapo juu. Kwa mfano, maana rahisi kabisa ya Ubeparii ni: Mfumo wa uchumi ambao chimbuko lake ni umiliki binafsi wa means of production (mashine, majengo, viwanda, vitendea kazi n.k) vinavyotumika kuzalisha mali (create wealth)/kuzalisha goods and services, lengo kuu likiwa ni kujitengenezea faida. Vile vile suala lingine muhimu ni kwamba Ubepari unahimiza sana "HAKI" katika umiliki wa mali (Property Rights).

Niliwahi soma kwenye makala moja ya Reginald Green [huyu alikuwa ni mtaalamu wa uchumi wa Mwalimu kwa miaka mingi kabla hajarudi kwao Ulaya] ambae alielezea ni jinsi gani hata BABA WA UBEPARI (father of Capitalism), Adam Smith alivyofafanua kuhusu ubepari kwamba nia yake sio kuwafanya watu kuwa mafukara: Green alimjadili Nyerere na Adam Smith kama ifuatavyo:

["Mwalimu's overriding concern in respect of Economics and Political Economy is very similar to one of Adam Smith's main concerns. Smith, who styled himself as a moral philosopher, believed for both practical and normative reasons that no nation could be great and prosperous if the majority of its people were poor and miserable. He contended that it was a primary duty in ‘moral economy' to enable them to escape from what we would not call absolute poverty, and that making this possible is the primary economic duty of the State. On the particular functions of the state, Smith and Nyerere (in very different contexts) certainly did not come to similar conclusions. Even so, Smith's very similar moral distaste for collusive behavior by entrepreneurs of self – enrichment and by economic power clusters turning the state into their tool is almost as robustly and repeatedly states as Nyerere's has been."]

Lakini mkuu, nini maoni yako juu ya jinsi gani tunaweza kugeuza madhara ambayo Walter Rodney aliyaweka wazi kwenye chapisho lake la: How Europe Underdeveloped Africa? Mambo aliyozungumza Rodney yanajionyesha kwa uwazi sana, na madhara ya mfumo huu ambao wahuni wachache walitumia ubepari kutunyonya, yanaonekana hadi leo katika nyanja sio ya uchumi tu bali pia kisiasa, kiutamaduni, kijamii n.k. Pengine moja ya njia ya kugeuza haya ni kwanza kuwa na Dira (kama ulivyogusia) ambayo itatusaida tujitambue, tunatokea wapi, tupo wapi, tunataka kwenda wapi na tufanye nini kufika huko. Vinginevyo katika hali ya sasa, bado hatuna majibu kwa yote haya.
 
JingaFalsafa,
Asante kwa mchango wako. Ni kweli, ulichokisema lazima utapata upinzani kutoka kwa wengi. Lakini mimi kimsingi nakubaliana na wewe mia kwa mia; lakini kama nilivyojadili hoja za Mkandara muda mchache uliopita, hakuna sehemu ambayo inasema kwamba Ubepari nia yake sio kutendea haki jamii au tabaka fulani fulani, kwani fursa zipo wazi kwa yeyote atakayeweza kukabiliana na ushindani ambao ndio moja ya asili ya mfumo huu;

Nakubaliana na wewe kwa maana moja kubwa: Europe Underdeveloped Africa kama njia ya kujiwekea mazingira mazuri ya kutawala dunia kiuchumi, huku wakitumia tools za kisiasa, kiutamaduni na kijamii. Umelielezea hili lakini kwa namna tofauti; Mkuu Jingafalsafa, je unakubaliana na hoja kwamba ubepari per se hauna tatizo, lakini tatizo ni players in the game? Inawezekana majibu yako yakawa kwamba Ubepari inherently ni mfumo usio na haki, usiotoa fursa kwa wote; Kama nipo sahihi, hoja hii ina mashiko, lakini tatizo langu linakuja hapa: Je, ili tuweze ku create wealth for our societies, mfumo gani mwingine ni bora? Ujamaa? au ubepari ambao katika hatua za awali inahitaji na sisi tupakatwe pakatwe kama walivyofanyiwa South Korea wakati wa Cold War?

Mimi nadhani mfumo mzuri kwetu ni ule wa Social Democracy ambao unakubali kuishi na ubepari lakini under one condition kwamba ubepari uwe tayari kukosolewa, na kuwa regulated so that no one is left behind.
 
Mkandara,

Shukrani mkuu. Umezungumza suala la msingi sana kwamba tunaumizwa/ibiwa na ukoloni mamboleo lakini sio Ubepari; Upo sahihi kabisa kwamba tatizo sio UBEPARI bali wale wanao practice ubepari kwa faida yao; Vinginevyo kwa kweli hakuna sehemu inayosema kwamba Ubepari ni unyonyaji, utapeli, unequal exchange or lolote linalofanana na hilo; pia hakuna sehemu yoyote inayoeleza kwamba Ubepari umetengwa kwa faida ya watu wa aina fulani, tabaka fulani, au jinsi fulani; Vinginevyo ubepari ni mfumo huru kuliko yote iliyowahi kutokea, na mfumo bora zaidi katika creation of wealth na prosperity ya wanadamu, kuliko mfumo mwingie wowote;

Tukitazama definition ya Ubepari, kwa kweli hatuoni sehemu yoyote inayokinzana na haya niliyojadili hapo juu. Kwa mfano, maana rahisi kabisa ya Ubeparii ni: Mfumo wa uchumi ambao chimbuko lake ni umiliki binafsi wa means of production (mashine, majengo, viwanda, vitendea kazi n.k) vinavyotumika kuzalisha mali (create wealth)/kuzalisha goods and services, lengo kuu likiwa ni kujitengenezea faida. Vile vile suala lingine muhimu ni kwamba Ubepari unahimiza sana "HAKI" katika umiliki wa mali (Property Rights).

Niliwahi soma kwenye makala moja ya Reginald Green [huyu alikuwa ni mtaalamu wa uchumi wa Mwalimu kwa miaka mingi kabla hajarudi kwao Ulaya] ambae alielezea ni jinsi gani hata BABA WA UBEPARI (father of Capitalism), Adam Smith alivyofafanua kuhusu ubepari kwamba nia yake sio kuwafanya watu kuwa mafukara: Green alimjadili Nyerere na Adam Smith kama ifuatavyo:

["Mwalimu's overriding concern in respect of Economics and Political Economy is very similar to one of Adam Smith's main concerns. Smith, who styled himself as a moral philosopher, believed for both practical and normative reasons that no nation could be great and prosperous if the majority of its people were poor and miserable. He contended that it was a primary duty in ‘moral economy' to enable them to escape from what we would not call absolute poverty, and that making this possible is the primary economic duty of the State. On the particular functions of the state, Smith and Nyerere (in very different contexts) certainly did not come to similar conclusions. Even so, Smith's very similar moral distaste for collusive behavior by entrepreneurs of self – enrichment and by economic power clusters turning the state into their tool is almost as robustly and repeatedly states as Nyerere's has been."]

Lakini mkuu, nini maoni yako juu ya jinsi gani tunaweza kugeuza madhara ambayo Walter Rodney aliyaweka wazi kwenye chapisho lake la: How Europe Underdeveloped Africa? Mambo aliyozungumza Rodney yanajionyesha kwa uwazi sana, na madhara ya mfumo huu ambao wahuni wachache walitumia ubepari kutunyonya, yanaonekana hadi leo katika nyanja sio ya uchumi tu bali pia kisiasa, kiutamaduni, kijamii n.k. Pengine moja ya njia ya kugeuza haya ni kwanza kuwa na Dira (kama ulivyogusia) ambayo itatusaida tujitambue, tunatokea wapi, tupo wapi, tunataka kwenda wapi na tufanye nini kufika huko. Vinginevyo katika hali ya sasa, bado hatuna majibu kwa yote haya.
Shukran sana mkuu wangu kwa kunielewa niliposimama mimi kuzungumzia Ubepari na sio kwamba nafagilia WANYONYAJI isipokuwa ktk maisha ya mwanadamu hakuna kitu kisichokuwa na madhara kama hakitakuwa controlled. Wanyonyaji wapo na wataendelea kuwepo ni jukumu letu kujihadhari nao kwa kuweka na kulinda ngome zetu..Mkuu wangu hata Ukila sana utavimbiwa na pengine kutapika na kuumwa. Unene pia sio mzuri pengine ni maradhi. Kuzaa watoto ni rehma lakini unaweza kuzaa toto jizi, kibaka na kadhalika kila kitu kinatakiwa kujali ethic na moral zinazotokana na nyie wenyewe..

Kusema kweli kwa Tanzania yetu hii na tulipo sasa sijui kama tunaweza tena kuepuka UNYONYAJI. Sioni kama kuna uwezekano wa kuwa na dira yoyote inayoweza kuepuka mbegu zilizopandwa na viongozi wetu kuruhusu Ukoloni mamboleo pengine itachukua another 500 year kwa vizazi vijavyo kushtuka na by then sijui tutakuwa tumebakiwa na kitu gani. Tatizo ni mind set zetu sisi wenyewe maana viongozi wetu ni reflection yetu sisi, ni baina yetu. Na nasema hivi kwa sababu sijaona chama chochote hata chama changu Chadema au kiongozi yeyote akirudi nyuma na kusema tulikosea wapi isipokuwa kila mtu anatazama tunakosea wapi ktk mwendo huu wa kunyonywa ila tunaweza vipi nasi kufaidika na unyonywaji..

Tunachosahau ni Umaskini, Ujinga na Maradhi kuwa vitu hivi haviwezi kuchanganywa na maendeleo ya nchi. Maneno mazito sana ya Reginald Green aliposema:- "It was a primary duty in ‘moral economy' to enable them to escape from what we would not call absolute poverty, and that making this possible is the primary economic duty of the State."

Mkuu wangu toka tumeacha kutazama The Primary ecomomic duty ya kumkomboa mwananchi kupambana kwanza toka ktk umaskini, Ujingana Maradhi na kufikiria tunaweza kwenda mbele sawa na wale wasiokuwa maskini, Wajinga na Maradhi - Tutaendelea vipi?. Let's face the truth, hivi unaweza nambia tuna wananchi wangapi wenye digree hata moja au diploma na ni asilimia ngapi ya jumla yetu. I bet hatufiki hata asilimia 10.. Sisi ndio chakula cha Ulaya na maendeleo yao, na ndio maana nazidi kusema sisi ni kama Nyati wa Serengeti tofauti na mzungu ambaye ni Simba na anajua chakuala chake ni Nyati. What I dont understand ni sisi kutofiiria Unyati wetu, chakula chetu, tunaweza vipi kuepuka kuliwa na Simba maana hata hao nyati seriengeti wasiokuwa na akili hutumia senses zao ku tafuta mbinu za kujilinda..

Iweje sisi kweli binadamu tuloumbwa na akili tunashindwa kuelewa kwamba nchi tajiri karibu zote Ulaya, Marekani na Asia wote ni wanyama wanaokula kutokana na sisi isipokuwa tunataka wao waelewe kwa kutumia UTU kuwa wanachokifanya sii Ubinadamu. I mean kama riziki ya binadamu hutoka kwa binadamu mwenzake unafikiri kweli wao wanataacha kutunyonya kwa sababu sisi tunafiiri sio Ubinadamu kutunyonya? au ni kazi yetu sisi kukabiliana na unyonyaji?

Hivi kweli unaweza kumwambia jizi usiniibie bwana unavyofanya sii vizuri kwa kufikiria Ubinadamu wako.. Jizi halijali ubinadamu na ndio maana linaitwa jizi.. kazi yetu sisi kuelewa kwamba tunanyonywa kwa sababu sisi ni Maskini, Wajinga na wenye Maradhi. halafu tunategema kwamba hawa hawa wanyonyaji wanaweza kutuondoa sisi ktk Umaskini na Ujinga wakati hicho ndicho kilema chetu kama yule ndama wa nyati.

Hawa wote wanyonyaji wanataka sisi tuendelee kuwa maskini, na wajinga kwa sababu ndivyo wanavyoweza kuziendeleza nchi zao. Na ndio maana waliondoa Barter system na ku replace na paper money yaani tulichokuwa nacho kukiondoa thamani na kuweka karatasi wanazotengeneza wao kuwa juu ya kila kitu. How can Gold, Almasi na madini yapimwe thamani yake kwa karatasi na sio tena kile tunachokihitaji sisi?. Hii haina Ubepari wala Ujamaa isipokuwa Ubeberu na jinsi hawa wenzetu wenye ELIMU walivyoweza ku manipulate utajiri wetu kuwa umaskini wetu halafu leo tunawaita wao kuja kuchima madini yetu na wengine hata kufungua ofisi za services nchini.

Leo hii inachekesha kuona services inachukua nafasi kubwa ktk GDP yetu nasikia sasa hivi imefika asilimia zaidi ya 50 kuliko kilimo ama madini.. Hii aibu kubwa sana maana services ni kuishi kiujanja ujanja kama walivyoweza kuishi Uingereza na Ufaransa..Sasa jiulize sisi tutaweza kwenda kumnyonya nani nje? waliyoyafanya waingereza au wafaransa hatuwezi maana hatuna Mtaji wala elimu..hivyo hizo services tuna imports mashirika ya nje kua kumnyonya mwananchi maana hakuna ktk services kinachotokana na uzalishaji wa Mtanzania na kama kipo ni asilimia ndogo sana.

Tutaweza tu kufanikiwa kaa tutarudi to the basics... vita yetu ktk kufuta Umaskini, Ujinga na Maradhi na hatuwezi kuvifuta hivi pasipo kurudia mistari ya mwalimu katika Azimio la Arusha. Vita ya Uchumi huru waliipigania kina mwalimu na tukafanikiwa ushindi na tukaingia vita ya Umaskini, Ujinga na maradhi lakini kabla hatujafanikiwa tumejikuta tumerudi ktk Kukoloniwa tena Kiuchumi na ndipo narudia kwamba tulipoteza DIRA yetu kuacha vita hiyo na kawaribisha wanyonyaji tena. Pengine tunamhitaji mtu kama Kagame au Meles Meles kulazimisha kurudi nyuma, nje ya hapo kwa navyowajua wadanganyika hakuna tumaini..
 
Wakuu wangu:
Tunapozungumzia Ubepari na falsafa yake ya "Private Ownership" ni sawa na tunapozungumzia Ukristo na falsafa yake ya "Upendo". Falsafa ya Upendo kwa wakristo huwafanya watu wawasamehe maadui zao, wawafie wenzao, wafie imani yao, watoe misaada, wahurumie, waheshimu, wajali, watii, wawe wamoja, nk. Yote hayo ndiyo Upendo wenyewe!
Basi ndivyo ilivyo kwa "Private Ownership" = Ubinafsi. Ukazaa Utumwa, ukabaila, Ulanguzi, Ubeberu/Ukoloni, Ukoloni Mamboleo, hadi Utandawazi tulionao leo! Katika ngazi ya mtu na mtu tutakutana na matendo haya, Wivu, Njama, Visasi, Wizi, Kijicho, Hujuma, Dhuluma, Hongo, Uroho, Ulafi, Uchoyo, Uadui, Ukatili, n.k. Hayo ndiyo yakamilishayo "INDIVIDUALISM" nayo ndiyo "Private Ownership/Ubepari"
Si lazima Ubepari useme kwamba utatendea Haki tabaka fulani, katika tafsiri yake ya nje" kwani tafsiri ya nje ya chochote kile, huwa tamu na yenye kuvutia! HAKI na UHURU-FURSA SAWA, ni maneno mazuri masikioni. Lakini hakika ni machungu Fikirani!
Mkuu Mchambuzi:
1. Hakika sikubaliani wazi kabisa kuwa Ubepari Per Se hauna tatizo, kwani nimesema hapa kuwa, ili mfumo kuwa kamilifu na bora kwa watu wake, basi hauna budi kusadifu mambo makuu matatu
1. MAZINGIRA
2. NYAKATI
3. MANTIKI, yaani UTU.
Ubepari umekosa vyote hivyo!
2. Mfumo gani ni bora katika ku-create wealth?
Kwanza kabisa ningependa kusema target yetu isiwe WEALTH, si sahihi-tutaumizwa na kuumizana! Na hapa ndipo Ubepari unakosa maana kabisa kwetu! Nimesema tayari kuwa, tafsiri ya Maendele kwa mtu mweusi ni UTU yaani MANTIKI na si KITU kama watuaminishavyo washenzi nguruwe wakufugwa!
UTU unajenga KITU, lakini kamwe KITU hakiwezi kujenga UTU, ila HULKA tu!
Sasa kipi ni bora? Je, ni HULKA ama MAMTIKI?
Tukitaka tu kujenga Utajiri, hatushindwi. Ila tu, ni kukubali kuuza UTU wetu! Kukiuka MANTIKI na kuishi Upuuzi na Ujinga! A. Kusini ni Matajiri zaidi yetu, lakini ipi ni thamani na nafasi ya mtu mweusi kule?
Hakika, kama unataka kuwa tajiri mapema kabisa, basi Jifikirie Binafsi, yaani interest zako tu...kuwa bepari!
3. Je, ni mfumo gani ni sahihi kwetu?
Hakika si swali jepesi. Tukae chini tuumize vichwa, tufanye Ubunifu juu ya namna tupaswavyo sio tupendavyo kuishi. MANTIKI kuongoza Tafakari/Ubunifu wetu! Nahofu kupika pamoja social elements with democratic elements, hazitoiva kamwe!
Zipo zitakazoziba hali kuna nyingine zinatoboa...ni KAZI BURE! Binafsi naikubali sana Falsafa ya Ujamaa, "From Each According to His Ability. To Each According to His Needs"
Mkuu wangu Mkandara:
Kwanza unanipa mkanganyiko lakini nadhani ni wakupelekea kuafikiana nami!
1. Sisi ni Kama Nyati na Simba atuwindae! Beberu dhidi ya rasilimali zetu. Sasa kwanini bado tung'anie kupita kwenye njia zilizotengenezwa na simba hali kuwa twafahamu kuna vizingiti vya makusudi? Hivi kuna asiyejua kuwa "Demokrasia, Uwekezaji, Ubinafsishaji, Soko Huria, n.k. ni mbeleko za Ukoloni Mamboleo? Mbona bado mnazipigia chapuo?
Tunategemea nini? Je, huko si ndiko kutumaini kumbembeleza beberu asitunyonye? Eti asituuzie bidhaa feki, asiingie nasi mikataba feki, asichochee vita, asipandikize mamluki wake, n.k. Mantiki ni Kukata mirija ya Ukoloni Mamboleo kama Demokrasia, si kumshawishi bepari kupitisha mali halali tu katika mrija wake. Dawa ni kukata mrija na kuung'oa kabisa, hiyo ndio MANTIKI, yaani UTU.
2. Utashangaaje kuwaita waje kuchimba madini yetu hali kuwa tunakubali Demokrasia? Je, hatujui kama Ubinafsisha na Uwekezaji ni baadhi ya principles za demokrasia? Naposema Ubepari ni Siasa na Utamadun pia, mtapinga, na kudai it's only about economics!
3. Tutashangaa vipi juu ya uwezo wetu wa Kunyonya nje hali kuwa tunakubali uwepo wa USHINDANA na kudai ni kuhmiza Maendeleo? Naposema HESABU ndio hizi. Ndio Demokrasia. Fursa Sawa. Sungura na kobe kuwashindanisha mbio sawa!
4. Turudi vip AA halikuwa tunataka kuwe na "Private Ownership"?
Tunatambua kwamba AA haikuwa na Bill of Rights hii ya leo? Je, TUPO TAYARI KUFUNGWA? Je, tunakubali, Uhuru uliohalalishwa na kuwa HAKI ni Upuuzi?
Pamoja sana!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa.
 
Mkuu wangu Mkandara:
Kwanza unanipa mkanganyiko lakini nadhani ni wakupelekea kuafikiana nami!
1. Sisi ni Kama Nyati na Simba atuwindae! Beberu dhidi ya rasilimali zetu. Sasa kwanini bado tung'anie kupita kwenye njia zilizotengenezwa na simba hali kuwa twafahamu kuna vizingiti vya makusudi? Hivi kuna asiyejua kuwa "Demokrasia, Uwekezaji, Ubinafsishaji, Soko Huria, n.k. ni mbeleko za Ukoloni Mamboleo? Mbona bado mnazipigia chapuo?
Tunategemea nini? Je, huko si ndiko kutumaini kumbembeleza beberu asitunyonye? Eti asituuzie bidhaa feki, asiingie nasi mikataba feki, asichochee vita, asipandikize mamluki wake, n.k. Mantiki ni Kukata mirija ya Ukoloni Mamboleo kama Demokrasia, si kumshawishi bepari kupitisha mali halali tu katika mrija wake. Dawa ni kukata mrija na kuung'oa kabisa, hiyo ndio MANTIKI, yaani UTU.
2. Utashangaaje kuwaita waje kuchimba madini yetu hali kuwa tunakubali Demokrasia? Je, hatujui kama Ubinafsisha na Uwekezaji ni baadhi ya principles za demokrasia? Naposema Ubepari ni Siasa na Utamaduni pia, mtapinga, na kudai it's only about economics!
3. Tutashangaa vipi juu ya uwezo wetu wa Kunyonya nje hali kuwa tunakubali uwepo wa USHINDANA na kudai ni kuhmiza Maendeleo? Naposema HESABU ndio hizi. Ndio Demokrasia. Fursa Sawa. Sungura na kobe kuwashindanisha mbio sawa!
4. Turudi vip AA halikuwa tunataka kuwe na "Private Ownership"?
Tunatambua kwamba AA haikuwa na Bill of Rights hii ya leo? Je, TUPO TAYARI KUFUNGWA? Je, tunakubali, Uhuru uliohalalishwa na kuwa HAKI ni Upuuzi?
Pamoja sana!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa.
Mkuu wangu nadhani bado hatujaelewana..Labda nirudi nyuma kidogo kukuonyehsa kwamba sisi wenyewe tulikuwa na Demokrasia yetu lakini sio hii ya wazungu, Tulikuwa na Uwekezaji wetu lakini sio huu wa wazungu, tulikuwa na Ubinafsishaji wetu sio huu wa wazungu na mwisho tulikuwa na Soko Huria letu ambalo sio hili la wazungu. Hivyo utagundua kwamba sisi kutokana na UJINGA wetu tumefundishwa kufikiria Demokrasia, Uwekezaji, Ubinafsishaji, Soko Huria ulo asisiwa na wazungu ni kwa ajili yetu. Ndio maana siku zote husema hii Elimu dunia tunayojifunza kuna mengi sio kw aajili yetu ila yao wao..

Kama navyomzungumzia Simba yeye huwafundisha wanawe jinsi ya kuwinda, kupata chakula na kujilinda kama Simba na Nyati vile vile anatakiwa kufanya Unyati wake ktk kujifunza namna kupata riziki zake na kujilinda japokuwa manano haya yanafanana haina maana hata mbinu zao zitakuwa sawa, maadui wao sawa na chakula chao sawa. Sisi kwa bahati mbaya tumechukua ya Simba ili kutafuta riziki kwa sababu elimu kwetu ni ya kuiga UTU wa mzungu badala ya kujielemisha sisi kulingana na mahitaji yetu ktk mazingira na nyakati zetu ambayo tunakubaliana sote kuwa huo wa kwetu ndio UTU wetu.

Hivyo mzungu yeye ana UTU wake na sisi tuna UTU wetu na huwezi kumwambia mzungu hana UTU akakuelewa, yeye kutokana na mazingira na nyakati zake hutuona sisi ndio hatuna UTU. Na pengine yeye ni mkweli zaidi kwa sababu sisi ndio tunajaribu kuishi kama wao wakati hatuna meno ya canines. Lakini pamoja na yote haya tukiamua kuishi kama sisi ktk mazingira na nyakati zetu hatuwezi kuacha Demokrasia, Uwekezaji, Ubinafsishaji, na soko Huria maana ndizo njia za mwanadamu (mnyama) hujitafutia riziki zake.

2. Sishangai kuhusu UWEKEZAJI wa wazungu ikiwa fikra za maisha yetu yanataka kuwa kama Simba anavyopata riziki zake badala ya sisi kuwa na ELIMU kulingana na sisi wenyewe na ktk mazingira yetu ili kupaa maendeleo. Yule Nyati wa Serengeti pamoja na kwamba wanyama wengine huvuka mto Mara kwenda upande wa pili, Nyati huwa havuki na Pundamilia au Nyumbu. Wao kama Nyati wamejiandalia maisha yao upande mmoja kulingana na mahitaji yao ktk mazingira na nyakati tofauti na sio kuwafuata Nyumbu au Pundamilia.

Sisi Watanzania tunaweza kabisa uwekezaji kwa ajili ya kizazi chetu iwe sisi ni Nyati au Swala na sio kujaribu kuwa kama Simba au Nyumbu. Tatizo ni kwamba hadi kesho we are into denial of who we are...Aidha hatujui sisi ni Binadamu wa aina gani au hatutaki Ubinadamu wetu ndio maana tunajichubua ngozi na kuvaa nywele za bandia. Wazungu wanajijua, Wachina wanajijua na hata Wahindi wanajijua na ndio maana hawaziachi mila na tamaduni zao. Sisi waigaji ndio tumetupa mila na tamaduni zetu na hivyo kujaribu kuwa kama wao - wonna be. Ni muhimu sana kuwekeza ktk kizazi chetu hivyo Demokrasia, Uwekezaji, Ubinafsishaji, Soko Huria lazima zitatokana na mahitaji yetu sisi wenyewe - Kama alivyokuwa akisema Nyerere ktk kuutetea Ujamaa.

3. Nitarudia tena kusema ya kwamba sisi hatutakiwi kuishi kama Simba, maana simba wanapowafunza watoto zao mbio ni kwa sababu ya kumkamata Nyati au swala lakini nasi tunachotakiwa kujifunza ni mbio za kumuepuka Simba..Sio tuseme mbio hazihitajiki kabisa isipokuwa kuifungia ktk handaki na tutafute njia za kupata riziki kutoka chini..Ukweli ni kwamba jatuwezi kuepuka mabeberu na wala sisi hatushindani mbio kama za Sungura na Kobe kama wanavyotaka tushindane ila tunashindana mbio sisi kwa kuhakikisha tunaweza kumkimbia Simba..

4. AA kwa fikra za mazingira na nyakati ilikuwa haina matatizo kabisa isipokuwa tu pale tulipoamua kujifungia gerezani. lakini kupambana na Umaskini, Ujinga na Maradhi ilikuwa ndio uwekezaji wetu kwa WATU na hatungeweza kuendelea pasipo kutazama uwanja wetu wa vita, ARDHI, WATU, Siasa SAFI na UONGOZI BORA.. Kuacha vita ya Umaskini, Ujinga na maradhi na kutojali misingi ya maendeleo yetu ndipo naposema tumepoteza DIRA...
 
Nguruvi3 JingalaFalsafa Azimiojipya AshaDii na wengineo.

Katika mfululizo wa makala hii nadhani tunaweza fikia mahala tukaipata common ground ktk UTU wa Mtanzania. Na lazima nikubali kwamba tunapopishana ni ktk tungo nzima ya Ubepari ambao binafsi yangu nimejaribu tu kuutazama ktk hali ambayo mwanadamu kujipatia riziki zake lakini undani wake umejengwa sio tu ktk misingi ya maendeleo ya kiuchumi bali pia huja na formation of oligopolies..

Itakuwa mimi mpumbavu sana kama sintozingatia Sisi kama sisi na Ubepari unatufaa vipi na hautufai vipi. Ujamaa unatufaa vipi na hautufai vipi hivyo kwa ujumla wa murengo hii miwili tunaweza kujua sisi tumesimama wapi na mnjia ipi ni bora ktk kuunda Dira itakayoongozana na UTU wetu..

Maadam kuna vitu hivi viwili muhimu ambavyo mfumo wowote wa Kiutawala lazima uvizingatie kutokana na UTU wetu basi bila shaka tutaweza kupata mfumo halisi unalingana na sisi na katika mazingitra na nyakati hizi.. Vitu hivi ni:- JAMII (Social) na UCHUMI (economics).. Ni lazima mfumo wa wa maisha yetu upambanue sisi ni watu gani..

Na bila shaka tukiweza jitazama na kugundua Umaskini wetu , Ujingana maradhi inatulazimu tukubali kwamba ktk social development Ubepari sio maji yetu kabisa. Mzazi maskini lazima ataambukiza umaskini kwa mwanaye na hivyo umaskini utaendendelea ku strickle down kwa vizazi vyake vyote vijavyo unless kuna uwezeshaji ktk jamii hiyo. Hivyo kwa mtoto maskini tutaweza vipi kumwondoa ktk umaskini pasipo kumkwaza mwingine?..Ndipo hapa napokuja na fikra za kwamba hili neno ambalo wanawake hulitumia sana ktk kuwezeshwa kwa nini tusitumie kama mwanzo wa fikra mpya za Mtanzania yeyote ya kwamba - TUKIWEZESHWA TUNAWEZA.

Naamini kabisa kwamba mtoto wa maskini hana upungufu wa akili isipokuwa ana upungufu wa Mtaji, na hivyo upungufu wa mali hauna maana yoyote ktk kupungua kwa akili na uwezo wa kuboresha maisha yake. Hapa nadhani nitamrudia mwalimu Nyerere na kukubaliana naye ktk Azimio la Arusha na kusema huduma za ELIMU na AFYA ni haki ya kila Mtanzania. Hii iwe our first ammendment na ili tuondokane na UMASKINI kila Mtanzania lazima awe na access ya kupata AJIRA, hivyo serikali yenyewe inalazimika kuwa wakala wa AJIRA nchini. Wizara ya kazi iwajibike kwa hali na mali ktk kusaidia vijana wetu wanaomaliza masomo wapate ajira, kuwa na social program zinazowasaidia wale wasiokuwa na kazi kuwaandaa na kuwatafutia kazi ktk mashirika binafsi hata iwe serikali kutoa baadhi ya fungu kufidia mshahara kwa miezi sita ya temporary employment sio kuleta wageni wachukue kazi zetu kwa madai kwamba hatujui kiingereza..

Kambi za JKT ziwe vituo vya mafunzo kwa vijana wetubadala ya kuwa kambi za mchakamchaka kuwajenga nidhamu ya woga badala ya kuwa kambi za kuwajenga moyo wa UJASIRIAMALI kwani huko nje ktk dunia watakayo ikuta ni ktk mazingira ya kiuchumi na nyakati za Ubeberu (The undeniable breeding ground of inequality)..

Ubepari kama njia ya kiuchumi sio social economic solution kwa watu wote na wala hatuwezi kuchukua kila kilichoasisiwa na wazungu kwa ajili yetu iwe Socialism au Communism..WE must have our own way...kulingana na sisi na wala sii kusema tu kuchukue kutoka Ujamaa na Ubepari isipokuwa sisi wenyewe kujitambua na kutafuta mfumo ulokuwa bora kwetu ili kujiandaa ktk kupambana na mazingira na nyakati zilizotuzunguka..
 
Pamoja sana mkuu wangu Mkandara:
1. Japo wewe umesema tulikuwa na Demokrasia yetu, lakini si hii ya wazungu. Siko mbali sana nawe, ila napenda kusema "tulikuwa na mfumo wetu wa siasa" haijalishi uliitwaje! Nachojua haukufuata kanuni na misingi ya mfumo huu wa siasa uliopo, yaani Demokrasia! Tuko pamoja kwa hilo!
2. Pia tulikuwa na Uwekezaji, Ubinafsishaji na Soko Huria letu, sina Hakika sana juu ya hili. Lakini nachojua hasa, uchumi wetu haukuwa kama ilivyo leo. Yaani haukufungwa na kanuni za kidemokrasia kama huu wa leo! Hivyo ni kusema wazi kuwa Tulikuwa na namna yetu ya kuendesha Uchumi wetu (biological and physical factors for Man's development)
Ni wazi kabisa juu ya hilo! Naungana nawe moja kwa moja.
3. Si kweli kwamba hatuwezi kuwakwepa mabeberu, TUNAWEZA kwa kupita kando ya mawindo yao, ila si kazi rahisi, ni HESABU kali zinahitajika, nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU!
3. Mkuu wangu, AA haijakamilika bado pasi kutufunga GEREZANI. Je, kifungo chake hakikuwa na maana? Hakifai tena?
Je kuna haja ya kukiondoa? Je, kikitoka AA itabaki kuwa AA na Uwezo wake wote?
Kuna maana yoyote ya kuachwa Huru?
4. "Katika Social Development Ubepari sio maji yetu kabisa". HAKIKA! Na huo ndio Ukweli wenyewe!
Na kwa mtu mweusi kipimo cha Maendeleo si KITU bali UTU. Tunaweza kujenga kitu tukiwa na UTU lakini hatuwezi kujenga UTU tukiwa na KITU!
5. TUWEZESHWE ili kwenda sawa! Swali nani wa kumuwezesha masikini hali umasikini wake umefanywa kuwa mtaji wa tajiri? Ni kama mzungu alipojenga madaraja usiku, tusiibe ujuzi ndivyo tulivyo sasa. Kwani si tunajua serikali si dubwana tu, bali ni watu ambao ni sisi wenyewe tuliojaa chuki, choyo, na HILA? Nani wa kutuwezesha? TUWEZESHANE wenyewe. Si kumsubiri mtu wa kutuwezesha...kumbe tunahtaji KUFIKIRIANA KWANZA!
6. Ni wazi NIMEKOSHWA vya kutosha na bandiko lako # 312. Naungana nawe mkono kwa 100%. Tunahitaji mfumo utakaotusadifu sisi kama sisi. Tunataka kupigana vita dhidi ya Unyonge wetu. Hapa ndipo tupaswapo kuumiza vichwa! Ni lazima tuumize vichwa kubuni mfumo sahihi. Maadamu tunaafikiana juu ya thamani ya UTU katika kuondoa Unyonge wetu. Basi ni pendekezo langu kuwa "namna yoyote ile tutakayoiona inafaa, basi ni lazima itufanye tupigane pamoja kama timu, na isiwe vita ya mtu mmoja mmoja" yaani TUKATAE aina yoyote ya utengano. TUPIGANE PAMOJA...NDIO USHINDI WETU!
Ubunifu Haujawahi kufika mwisho, tunayo nafasi. Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu. Tubuni mfumo utakaotufanya tupambane pamoja! Umoja ni Nguvu!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Pamoja sana mkuu wangu Mkandara:
1. Japo wewe umesema tulikuwa na Demokrasia yetu, lakini si hii ya wazungu. Siko mbali sana nawe, ila napenda kusema "tulikuwa na mfumo wetu wa siasa" haijalishi uliitwaje! Nachojua haukufuata kanuni na misingi ya mfumo huu wa siasa uliopo, yaani Demokrasia! Tuko pamoja kwa hilo!
2. Pia tulikuwa na Uwekezaji, Ubinafsishaji na Soko Huria letu, sina Hakika sana juu ya hili. Lakini nachojua hasa, uchumi wetu haukuwa kama ilivyo leo. Yaani haukufungwa na kanuni za kidemokrasia kama huu wa leo! Hivyo ni kusema wazi kuwa Tulikuwa na namna yetu ya kuendesha Uchumi wetu (biological and physical factors for Man's development)
Ni wazi kabisa juu ya hilo! Naungana nawe moja kwa moja.
3. Si kweli kwamba hatuwezi kuwakwepa mabeberu, TUNAWEZA kwa kupita kando ya mawindo yao, ila si kazi rahisi, ni HESABU kali zinahitajika, nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU!
3. Mkuu wangu, AA haijakamilika bado pasi kutufunga GEREZANI. Je, kifungo chake hakikuwa na maana? Hakifai tena?
Je kuna haja ya kukiondoa? Je, kikitoka AA itabaki kuwa AA na Uwezo wake wote?
Kuna maana yoyote ya kuachwa Huru?
4. "Katika Social Development Ubepari sio maji yetu kabisa". HAKIKA! Na huo ndio Ukweli wenyewe!
Na kwa mtu mweusi kipimo cha Maendeleo si KITU bali UTU. Tunaweza kujenga kitu tukiwa na UTU lakini hatuwezi kujenga UTU tukiwa na KITU!
5. TUWEZESHWE ili kwenda sawa! Swali nani wa kumuwezesha masikini hali umasikini wake umefanywa kuwa mtaji wa tajiri? Ni kama mzungu alipojenga madaraja usiku, tusiibe ujuzi ndivyo tulivyo sasa. Kwani si tunajua serikali si dubwana tu, bali ni watu ambao ni sisi wenyewe tuliojaa chuki, choyo, na HILA? Nani wa kutuwezesha? TUWEZESHANE wenyewe. Si kumsubiri mtu wa kutuwezesha...kumbe tunahtaji KUFIKIRIANA KWANZA!
6. Ni wazi NIMEKOSHWA vya kutosha na bandiko lako # 312. Naungana nawe mkono kwa 100%. Tunahitaji mfumo utakaotusadifu sisi kama sisi. Tunataka kupigana vita dhidi ya Unyonge wetu. Hapa ndipo tupaswapo kuumiza vichwa! Ni lazima tuumize vichwa kubuni mfumo sahihi. Maadamu tunaafikiana juu ya thamani ya UTU katika kuondoa Unyonge wetu. Basi ni pendekezo langu kuwa "namna yoyote ile tutakayoiona inafaa, basi ni lazima itufanye tupigane pamoja kama timu, na isiwe vita ya mtu mmoja mmoja" yaani TUKATAE aina yoyote ya utengano. TUPIGANE PAMOJA...NDIO USHINDI WETU!
Ubunifu Haujawahi kufika mwisho, tunayo nafasi. Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu. Tubuni mfumo utakaotufanya tupambane pamoja! Umoja ni Nguvu!
Mungu wetu anaita sasa!
Haswaaa mkuu ulikuwa wapi muda wote kunielewa yaani umeyaandika ktk fikra nilizokuwa nazo toka mwanzo isipokuwa tu nadhani tulipokosana na hii dhana ya UBEPARI wetu na huu uloandikwa na kina Smith. Ndio maana siku zote utanikuta kwa Nyerere lakini pia napinga ktk maamuzi yaliyofuatia kutokana tu na kuogopa Mabeberu, tukafungiwa ndani ya chumba ili tuishi hiuvyo na sio kujifunza namna ya kumuepuka beberu ktk ulinzi wa maliasili na rasilimali zetu. Ndio maana nikatumia mifano ya wanyama ktk kutafuta riziki zao. Hawa wanajua fika Simba wapo na wayaendelea kuwa Simba maana riziki yao inatokana na wao.. Hivyo hata wao wasiokuwa na akili wameweza kuepuka sana kuliwa na Simba japokuwa wapo ktk mbuga moja..

Tunaweza sana kuwaepuka Mabeberu maana pembe tunazo, mbio tunazo, mateke tunaweza na wala haitulazimu kuwinda kama wao..Hivyo basi sisi tuwe na mfumo wetu wa Kijamii (social) ambao mazuri mengi yapo ktk UJAMAA wetu na Inapofiia kiuchumi (economics) lazima pia tutazame UBEPARI ktk sehemu moja tu ya kwamba riziki yetu haitokani na sisi wenyewe, hata tukijifungia kiasi gani mwisho wake tutakulana wenyewe hii itapingana na dhana ya kiswahili isemayo - Riziki ya MTU inatokana na MTU. Hivyo kufanya dhana ya kufikiriana kuwa ngumu sana kuiweka ktk utekelezaji..

Hivyo maadam hatuwezi kulana wenyewe lazima riziki yetu itoke nje yetu iwe kula mimea au nyama lakini sio yetu wenyewe na ndio ktk ile KUFIKIRIANA.. Tukumbuke tu kwamba Mabeberu wataendelea kutuwinda usiku na mchana maana riziki zao zinatokana na sisi, Je, riziki yetu sisi inatokana na nini?. (Riziki ya MTU inatokana na MTU} Hapa ndipo umuhimu wa jina unapoweza kutazamwa. Ni mtazamo wangu tu..
 
Mkuu Mkandara:
Sijawahi kutoka nje ya hili ulilonena hapo juu. Siku zote nimekuwa nikiamini kuwa "MTU MWEUSI ANA MAZINGIRA NA NYAKATI mahususi kwa ajili ya maisha yake" Maana kwangu maisha ni Mazingira na Nyakati!
RIZIKI YA MTU INATOKANA NA MTU!
Hakika msemo huu unaweza kubeba dhana kuu moja yenye kugawanyika katika pande mbili tofauti-hasimu! "Riziki ya mtu inatokana na Mtu"
Dhana kuu iibukayo hapa ni "MAHUSIANO", baina ya mtu na mtu!
Yaani ili mtu aweze kupata ridhiki yake, ni lazima kuwe na uwepo wa mtu mwingne! Yaani mahusiano yangu na watu hfanya nipate ridhiki! Hapa ndipo yanapoibuka Mahusiano ya aina mbili.
1. MAHUSIANO YA PANDE MOJA:
Haya hujali zaidi ridhiki ya upande mmoja. Yaani mahusiano haya huwa na uzito tofauti. Msemo huu hutumika kuhalalisha Unyonge wetu katika ngazi ya Kimataifa, hadi mtu na mtu! Yaani mimi nitahakikisha ridhiki yangu inatoka mikononi mwako, lakini ridhiki yako haitatoka kwangu, utajua utakapoitoa.
Huu ni UBATILI. Ndivyo UBEPARI ulivyo. Matokeo yake mnyonge atataka kutumia nguvu kuchukua riziki yake kwa mwenye nguu, hali kadhalika mwenye nguvu atatumia nguvu kulinda riziki yake! Kila kitu kitaharibika. Maisha yatakosa maana tena!

1 MAHUSIANO YA PANDE MBILI: Mahusiano haya ni yenye kujali uwepo wa pande mbili. Yaani mtu na mtu!
Riziki yangu i mikononi mwako halikadhalika riziki yako i mikonon. Tafsiri hii ya pili huibua dhana ya KUTEGEMEANA. Na huo ndio UAFRIKA;
Sasa tuchague basi aidha 1 au 2.
Piziki ya mtu i mikono mwake mtu! TUFIKIRIANE KWANZA.
Ni lazima tupambane pamoja!
Mungu wetu anaita!
 
JingalaFalsafa,
Samahani hapa umeniacha nje tena.. Ebu nipe darsa na hili la pili la KUTEGEMEANA.. Tutategemeana vipi mtu kwa mtu ikiwa hakuna cha mtu - Private ownership maana hata barter system ya wazee wetu walikuwa wana own mali zao za uzalishaji. Najaribu kuitafakari hiyo riziki itatokanaje?
 
JingalaFalsafa,
Samahani hapa umeniacha nje tena.. Ebu nipe darsa na hili la pili la KUTEGEMEANA.. Tutategemeana vipi mtu kwa mtu ikiwa hakuna cha mtu - Private ownership maana hata barter system ya wazee wetu walikuwa wana own mali zao za uzalishaji. Najaribu kuitafakari hiyo riziki itatokanaje?

Ni hivi Mkuu wangu:
Ni lazima tutofautishe UTEGEMEZI na KUTEGEMEANA katika hili la mahusiano baina ya mtu na mtu!
Private Ownership haina KUTEGEMEANA bali UTEGEMEZI! Na mara zote Utegemezi huu huwa ni juu ya mwenye nacho dhidi ya mnyonge! Yaani kama mimi ninamiliki aridhi kubwa, nitategemea mnyonge aje alime kwangu nimlipe ili niendeleze shamba langu. Inapotokea nikakosa mnyonge wa kunilimia, ni wazi shamba litakufa.
Kwa mnyonge yeye si tegemezi kwa tajiri kwani hana apiganiacho kubaki nacho, ila ni kutoka chini kwenda juu...na katika hilo mnyonge hawezi kuwa tegemezi kwa tajiri ili afikie ustawi wa juu, kwani ni wazi tajiri hapendi ustawi wa mnyonge, ni kutishia ustawi wake!
Yaani mnyonge hana haja ya kumtegemea tajiri kulinda status yake, kwani haina mvuto kwake-anatamani kuutupa unyonge wake, wala mnyonge hana haja ya kumtegemea tajiri kumtoa pale alipo kwani uwepo wake pale ndio ustawi wake tajiri! Ni kichaa tu atakayejenga tumaini la kutuma barua ya maombi kwa raisi wa nchi akitaka apewe kiti cha uraisi.
Lakini hlo si kwa tajiri, tajiri anamtegemea mnyonge kulinda na kuboresha status yake. Yeye ni tegemezi siku zote! Na hlo ndio zao la Private Ownership!
2. KUTEGEMEANA:
Hii ni Kinyume na UTEGEMEZI. Ni uwepo wa mizani sahihi baina ya mtu na mtu! Yaani kama muhogo shambani, sina nguvu kuung'oa peke yangu, nahitaji mtu wa pili kuja kunisaidia! Sasa ili mahusiano yetu yasiangukie kwenye Utegemezi(uzani wa upande mmoja), ni lazima shamba na muhogo wake vimilikiwe kwa pamoja!
Hivyo, tunahitaji KUTEGEMEANA na si Kumtegemea mtu fulani?
Mungu wetu anaita!
 
Ni hivi Mkuu wangu:
Ni lazima tutofautishe UTEGEMEZI na KUTEGEMEANA katika hili la mahusiano baina ya mtu na mtu!
Private Ownership haina KUTEGEMEANA bali UTEGEMEZI! Na mara zote Utegemezi huu huwa ni juu ya mwenye nacho dhidi ya mnyonge! Yaani kama mimi ninamiliki aridhi kubwa, nitategemea mnyonge aje alime kwangu nimlipe ili niendeleze shamba langu. Inapotokea nikakosa mnyonge wa kunilimia, ni wazi shamba litakufa.
Kwa mnyonge yeye si tegemezi kwa tajiri kwani hana apiganiacho kubaki nacho, ila ni kutoka chini kwenda juu...na katika hilo mnyonge hawezi kuwa tegemezi kwa tajiri ili afikie ustawi wa juu, kwani ni wazi tajiri hapendi ustawi wa mnyonge, ni kutishia ustawi wake!
Yaani mnyonge hana haja ya kumtegemea tajiri kulinda status yake, kwani haina mvuto kwake-anatamani kuutupa unyonge wake, wala mnyonge hana haja ya kumtegemea tajiri kumtoa pale alipo kwani uwepo wake pale ndio ustawi wake tajiri! Ni kichaa tu atakayejenga tumaini la kutuma barua ya maombi kwa raisi wa nchi akitaka apewe kiti cha uraisi.
Lakini hlo si kwa tajiri, tajiri anamtegemea mnyonge kulinda na kuboresha status yake. Yeye ni tegemezi siku zote! Na hlo ndio zao la Private Ownership!
2. KUTEGEMEANA:
Hii ni Kinyume na UTEGEMEZI. Ni uwepo wa mizani sahihi baina ya mtu na mtu! Yaani kama muhogo shambani, sina nguvu kuung'oa peke yangu, nahitaji mtu wa pili kuja kunisaidia! Sasa ili mahusiano yetu yasiangukie kwenye Utegemezi(uzani wa upande mmoja), ni lazima shamba na muhogo wake vimilikiwe kwa pamoja!
Hivyo, tunahitaji KUTEGEMEANA na si Kumtegemea mtu fulani?
Mungu wetu anaita!
Kusema kweli bado kabisa ila nakuomba usifikirie nafanya kiburi cha ubishi kwa sababu nashindwa ku connect the two..Hata huo mfano wa Muhogo kumtegemea mtu kunisaidia kuung'oa hampi haki wala mamlaka ya ownership. Mhogo bado utakuwa wangu hivyo namtegemea yeye kwa msaada wake pale napouhitaji kama ilivyokuwa enzi za wazee wetu wakisaidiana. Lakini ownership bado inabakia ya mtu mmoja wao. Mtoto wangu atalelewa na kijiji kizima lakini haiwapi haki ya kuwa mtoto wao, huyu bado ni mwanangu mimi mwenye haki ya kurithi umaskini/utajiri wangu. Ndivyo navyoelewa kutegemeana..

Kwa maana hii tunategemeana kama wewe mvuvi basi kijiji kitakutegemea utaleta samaki wanazozihitaji kama vile wewe unavyohitaji kuku au Mhogo, hivyo wao watakuja na mali zao iwe muhogo, mpunga au kuku kubadilishana na maadam leo hii barter system haitumiki tena nitasema Tutauziana.. Kwa hiyo mkuu wangu kila mmoja wetu anakuwa na chake anakiingiza ktk soko letu (gulio) maana hatuwezi kuwa watu wote wavuvi, wafugaji au wakulima na wala sii watu wote tuna uwezo sawa iwe nguvukazi, azma au Uzalendo wa kujituma kazini. I still believe Kutegemeana inatokana na uwezo wa kila mtu wetu kuzalisha na kusambaza kulingana na mahitaji yetu na sii kila mali iwe ya wote. Hata mkono uendao kinywani kila mtu hutumia wake kwa kipimo chake cha shibe lkn mwendo huu basi itafika mahala tutasema tulishane kwa kupimiana.

There will always be Demand and Supply ktk kutegemeana na mzunguko huo ndio unajenga utamaduni wa kiuchumi kwa watu hao..Na hata ktk maisha mkuu wangu hatuwezi kutoka watu wote ktk Umaskini kwa wakati mmoja isipokuwa kwa mmoja mmoja kama wanavyofanya Wayahudi na Wahindi na makabila mengine yanayosaidiana (wakitegemeana) kufikia azma zao kiuchumi. Tunawaona wakija huku majuu na wakiishi 10 ktk nyumba moja lakini mmoja mmoja atatolewa mkishtuka wote matajiri kulio kugawana kila mnachokipata sawa huku ni kugawana umaskini na hatatoka mtu.. Amini maneno yangu..
 
Mkuu wangu Mkandara: Wala usitie shaka nami. Naheshimu na kufurahia sana michango yako! Ni wazi inaniongezea maarifa kwa kiasi kikubwa!
Kauli ya "Riziki ya Mtu i mikononi mwa Mtu!" Inavyoleta dhana kuu yaani MAHUSIANO, ambayo nayo yapo ya namna mbili...UTEGEMEZI na KUJITEGEMEA/KUTEGEMEANA....dhidi ya Private Ownership!
1. Tunapozungumzia UTEGEMEZI na KUJITEGEMEA ni wazi kuwa tunagusa moja kwa moja MAENDELEO YA BINADAMU, yaani USTAWI WETU!
(a) Malengo ya Utegemezi kwa mtu ni KULINDA Ustawi alionao na KUBORESHA Ustawi alionao. Hapa tunazungumzia "Nakutegemea ili nilinde nilichonacho na kukiboresha". Hapa ndio maana nikatoa mfano wa mmiliki wa muhogo asiyeweza kuung'oa peke yake. Ataniita mimi kabwela kumsaidia kung'oa mhogo. Yeye ni tegemezi kwangu, ananitegemea kulinda na kuboresha hadhi yake. Je, mimi namtegemea kwa lipi? Je, ni kulinda hadhi yangu (ukabwela wangu) na kuuboresha zaidi. Je, namtegemea mwenye mhogo kuboresha hali yangu ili kesho ASINITUME? Je, akikubali Kesho ni Nani atakayemsaidia kung'oa mhogo? Kweli napaswa kumtegemea mtu anayefaidika na unyonge wangu kuondoa unyonge wangu? Ni wazi hilo halipo. Na ndio maana nimeita ni MAHUSIANO YA PANDE MOJA...UTEGEMEZI. Chanzo chake ni kuwa na HADHI binafsi. Private Ownership! Huku ndiko tupatapo tafsiri ya maendeleo kuwa ni KITU na si UTU.
(b) Vile vile katika KUTEGEMEANA, malengo ni kulinda Ustawi Walionao na Kuuboresha! Hapa tunazungumzia "Tunategemeana ili tulinde na kuboresha tulichonacho" Ili kufanikisha ili lazima tuzungumzie "SISI" na si "MIMI"
Katika KUTEGEMEANA Ujuzi na Stadi tu ndio unavyoweza kusema anavyo fulani na fulani. Lakini Ujuzi wako wa kuvua samaki haukuhalalishii kumiliki bwawa au ziwa! Vile vile kwa mkulima, haumuhalalishii kudai shamba ni lake. Daktari nae hatathubutu kusema hospitali ni yake. Kwa kufanya hivyo tunaua Mahusiano ya Pande Moja, yaani Utegemezi. Kwani hakutakuwa na Private Ownership. Ila yataibuka Mauhusiano ya Pande Mbili. KUTEGEMEA/KUJITEGEMEA. Kutakuwa na Meza ya Pamoja ambayo mkulima ataleta ugali ili daktari, na mvuvi wale, at the expense of their Unity, but not what they offer. Mvuvi ataleta samaki mezani ili mkulima na daktari wale, at the expense of their Unity but not what they have, Daktari nae atawatibu mkulima na mvuvi at the expense of their Unity na si kwa sababu za kipi wameleta mezani. Na hata ikatokea mvuvi akakosa samaki siku hyo, hatafukuzwa mezani kujumuika na mkulima na daktari, kwani kuponi yake ni Umoja wake na wenzake vivyo hivyo kwa wengine, huko ndiko KUJITEGEMEA. Lakini katika UTEGEMEZI, mahusiano ya pande moja. Mtu hupata Kitu at the expense of what he offers, kama hana HAPATI. Huo ndio
Ubepari-Private Ownershipi.
Wanaotegemeana Wanajenga Nyumba ya Pamoja hawanyimani fito! Ni marufuku kabisa kuruhusu umiliki binafsi wa njia za uzalishaji mali, kwani inaweza kutokea mtu ana uwezo wa kulima lakini mtaji wa kupata shamba hana, ataishia kutegemewd kulinda na kuboresha hadhi za ya mwenye shamba.
2. Mkuu wangu. Mfano wako wa wahindi kumi haupaswi kutufanya tusahau kuwa kunyanyuka kwa wahindi kumi ni kudididimia kwa weusi 1000, yaani kudidimia kwetu ndio kunyanyuka kwao. Hao wahindi 10 wametufanya weusi 1000 kuwa ngazi ya kufikia mafanikio yao. Tukumbuke kuwa sisi tumefanywa kuwa the lowest race, hvyo wale wa juu yetu wanatukanyagia tu. Je, sisi tunapotaka kupita njia zao au kujifananisha nao Nani yupo chini yetu TUMFANYE NGAZI kama wao wanavyotufanya? Je, sisi kwa sisi? Je, kuna MANTIKI ya Tanzania kuinyonya na kuikandamiza Malawi? Mkenya kumdanya daraja mtanzania. Hivi ni kweli tunataka kufikia hatua ya kuudharirisha na Kutoujali tena Uafrika Wetu. BORA NIFE, ILA NISIISHI HILO.
Mungu wetu anaita sasa!
 
Back
Top Bottom