Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Duru za Siasa Special: Mgogoro kambi ya Upinzani (CHADEMA)

Mkuu Mkandara
Nikushukuru kwa ujenzi wa hoja zako. Nipitie baadhi kwa kiasi nitakachojaaliwa.

1. Suala la Kafulila ZZK hakupinga kufukuzwa kwasababu ya kupoteza jimbo.
Motive behind Kafulila ilikuwa ni uongozi wa kikanda na ukabila ili Zitto apate mwanya
.

Tuhuma hizo zilipaswa kukemewa na ZZK kabla ya kupinga hatua. Zitto hakuzikemea ikimaanisha alikubaliana. Leo tunajua ule ulikuwa mwanzo wa 'waraka' ingeshangaza Zitto kuwatosa vijana wake.

Kafulila alipinga kubadilishwa nafasi,mabadiliko yaliyolenga kuondoa chokochoko kwa mtindo wa kuvumiliana. Mwisho Kafulila akaona hana namna nzuri ya kuishi CDM akajitoa na wala hakufukuzwa.

Chama kinachopigania kuondoa uzembe na kuchukua hatua kikimewanyooshea kidole CCM hakipaswi kuogopa kupoteza jimbo kwasababu ya mtu fulani.

Ni kutokana na hilo pengine watanzania wakaona CDM ni mbadala wa CCM na kukiunga mkono katika maeneo mengine ambako CDM ilikuwa haijulikani.

Kusema kuwa kuna kupoteza jimbo na kusahau kuwa hiyo ni sehemu ya political investment sidhani kuwa ni sahihi.

Marehemu Sokoine alipendwa si kwasababu aliwakumbatia wenzake bali alisimama kidete kwa kilicho sahihi.Kuendelea kuishi na watu wasioamini katika kile wanachokisema au kukitetea ni aina ya unafiki.

2. Lowasa hakuachwa CCM kwasababu ya kulinda chama.
Ameachwa CCM kwasababu ya kulindwa na swahiba wake.

Kikao cha NEC Butiama kilichowashirikisha marais wastaafu ukiacha mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, wadhamini wa CCM kiliazimia kuwafukuza akina Lowasa.
Mkutano wa kwanza uliotoa azimio ulikuwa wa Makongoro na wenyeviti wa mikoa.

Aliyeahirisha kikao ni mwenyekiti wa CCM na aliyepiga hoja dana dana alikuwa mzee Ngunge na Yusuph. Dhana kwamba walimwacha ili kulinda siri zao si sahihi, aliachwa na mwenyekiti ili kulinda siri zao kwasababu 'hawakukutana barabarani'

Haya unayoyasikia ya akina Nape na Mangula ni 'pre-lude' ya kile kinachokuja siku za karibuni.
Yote ya akina Lowasa yataibuka upya kwasababu ni jipu lililovia, bado lina usaha na halijatumbuliwa.

3. Kwamba kamati kuu imekurupuka hilo nakubaliana nalo.
Kulihitajika umakini zaidi. Kwa mfano, kulikuwa na sababu gani za Slaa na Mbowe kwenda Kigoma na Mwanza wakati gogoro linaunguruma na bila suluhisho.

Kuwavua uongozi ilikuwa hatua ya mwanzo ingawa iligubikwa na jazaba.
Hata hivyo lazima tukumbuke kuwa Zitto hakutaka kuhudhuria kikao jambo lililo wa provoke zaidi wajumbe na pengine kupoteza mwelekeo.

Hoja yangu siku zote ni kuwa ili kumaliza gogoro ilitakiwa tume huru kwani ingekuja na ukweli.
Hilo halikuzingatiwa na kutoa nafasi kwa mahakama ambapo mambo mengi zaidi yatajitokeza.

4. Kwamba Zitto yu 'ICU' na hivyo anapigania roho yake kisiasa hilo sikubaliani nalo.
Zitto yupo mtaani anadunda kwa kasi kubwa tu. Angekuwa ICU asingekwenda kwenye vyombo vya habari na mikoani kuhutubia mikutano.

Pengine ukimya ungesaidia zaidi watu kurudisha nyoyo zao na kusema kijana anakua 'aachwe abalehe'. Lakini uniambie yu ICU wakati anazidi kubomoa CDM!
Huko ICU watu wanapumulia mashine, yeye anatembea na mashine, ICU gani hiyo Mkandara!

5. Kuhusu hoja za Mzee Mwanakijiji kumtaka ajivue uanachama, kama nilivyomuelewa kwa tafsiri yangu binafsi ni kuwa ZZK yupo 'mahututi kisiasa'

Utaalam unaonyesha yupo katika vegetative state, kwamba mwili wa kisiasa upo lakini brain imekufa. Mwanakijiji anamaanisha ZZK wa vegetative state sasa ni wakati akubali life support iondolewe.

Mantiki ni kuwa kila mtu 'anapigania roho yake' akiwa wodini, lakini kwa hili la ZZK, manesi, madaktari, ndugu jamaa na marafiki hata wanaokuja kusalimia wagonjwa wa jirani wamechoka kuuguza.
Wanasema mgonjwa sasa ni wakati aondoke ili 'bwana atoe bwana atwae' maisha yaendelee.

5. CDM ndio waliopiga ngoma za kupunga mapepo na wachawi wamekuja.
Kama wasingepiga madebe wachawi wasingesogelea.

Kuwalaumu wachawi wanaofuata ngoma za mapepo ni makosa, kwanini asilaumiwe mpiga zumari na ngoma kwa kuita wachawi ili hali walijua ngoma za mapepo huvuta wachawi?

Ngoma ikipigwa kila atakaye kucheza hucheza, lakini kila ngoma ina mwenyewe na mwenye ngoma ya sasa ni Zitto.

Tabia yake ya kutembea na manyanga, kukutwa na viungo, kuvaa vibwenda usiku japo hajawahi kukamatwa na kidhibiti ni ushahidi kuwa ngoma inayoleta wachawi anaijua na kamba utaalamu huo anao.

Ushanfahamu mkubwa!

(Katika mazingira ya utata post hii ilihama na kwenda kule kwa uzi wa Paco)
 
Mkuu wangu wanisoma lakini huelewi kabisa nachokisema mimi kwa maana unajenga hoja tofauti kabisa na maswali yangu. Nitakueleza vizuri maana mimi ninazo kumbukumbu vizuri sana.

1.Kafulila - Bora pitia hapa ktk mtandao nilokuwa mwanachama pia Wanabidii ujikumbushe vizuri.https://groups.google.com/forum/#!topic/wanabidii/7oCTnBCxxi0

2. Lowassa ameachwa CCM kwa sababu ya kukilinda Chama, wewe Chadema iweje uyajue ya CCM wakati inajulikana wazi kwamba Lowassa ndiye mlezi wa Chama. Hivi kweli wewe unaamini Lowassa angefukuzwa CCNM leo tungekuwa tukibishana humu kuhusu hatma ya chama hicho?. Lowassa halindwi na mtu isipokuwa yeye ndio anawalinda wengi iwe kamati na baraza kuu la CCM. Ndiye hupitisha majina ya wagombea ubunge na pengine mawaziri na manaibu. Sii mdogo kama unavyofikiria maana ni katika Mtandao. Hawatupani, wanakumbuka walikotoka, wako wapi na wanamkwensa wapi hata kkama ni mafisadi.

3.Tumekubaliana na maadam umelikubali hili sielewi kwa nini bado unabisha maana hil hili ndio chimbuko la sisi kutokubaliana wala sii kwa sababu ni ZZK. hatua hizi zingechukuliwa hata kwa Mnyika nisingekubaliana nazo wakati kwenu pengine mngebadilika.

4. Zitto kuwa ICU ina maana ya kwamba Zitto Kisiasa yupo hatarini kumalizwa, kisha nyang'anywa vyeo vyote vya chama, haruhusiwi kufanya mikutano kwa jna la chama na kadhalika.. Hii ni sawa na kumalizwa kisiasa kilichobakia ni roho yake yaani uanachama. kama bado hujanielewa basi itakuwa vigumu sana kufafanua zaidi. Zitto hayupo ktk hali unayodai maana kama angekuwa, asingewapa shida mkaumiza vichwa maana mnachotaka ni unafuu wa kukwepa maswali magumu. Huko nje tayari tumesha athirika vya kutosha maana Hospital yetu inaonyesha wazi mtu alivunjia mguu anataka kufanyiwa Operation ya kichwa.. mnachosoma ni report tu hamtaki kumwona mgonjwa mwenyewe... Mnafikiria zaidi kukinusuru chama kwa kuficha maovu ya uongozi kama walivyokuwa CCM jambo ambalo mimi sikubalianni nalo. Jibuni tuhuma zenu kwanza ili Zitto asutwe, lakini sikubaliani kabisana kanuni zinazoficha uhalifu na ufujaji wa fedha za Umma kisha mnatumia waraka na Uhaini kuwa ndio sababu.

5. Kama wewe umekubaliana na namba 3 inakuwaje uziite ngoma za kupunga pepo ilihali ni makosa kupiga ngoma za kichawi mchana kweupe pale jangwani? Maadam ni ngoma kila mtu anayejisikia kucheza atacheza na hilo ndiolo linalotokea sasa hivi. CDM walitakiwa kuyafanya yote haya ktk vikao vyake wakifuata kanuni za chama zinasema nini. Kukiuka nkanuni kwa sababu mtuhumiwa alikiuka kanuni ni dalili mbaya sana ya utovu wa nidhamu kwa chama kizima. na ndio maana kina Lema wako huru kumtukana kiongozi yeyote na wasiwajibishwe.

Maadam ngoma mloipiga ni LEKA DUTIGITE mtawapata wengi wenye asili ya Kimanyema maana ngoma hizo huko Nyanda za juu huaminiwa ni ya Kichawi,!Hivyo Zitto atakuja kavaa hayo manyanga, na viungo maana ni ngoma yao ya asili (ngoma hiyo inaitwa - Kutokubali kuendeshwa na mtu..).
 
Mkuu Mkandara
Kwanza unaponiambia ni CDM unazidi kuniongezea vyama vya siasa ninavyonasibishwa navyo.
CUF walipokuwa na mgogoro niliandika sana kama nilivyoandika wakati wa CCM kuvuana magamba na kote huko nikaitwa ngangari na kagamba.
Sina sababu za kukinusuru CDM kwasababu sina masilahi ya aina yoyote zaidi na yale ya Utanzanania na uananchi.

Kuhusu Kafulika, inawezekana kumbu kumbu zangu zipo kombo.
Ningeomba unifahamishe alifukuzwa kwa lini na utaratibu gani ulitumika.

Kuhusu suala la ZZK nashangaa hapo mwisho umesema mambo ya CDM yangemalizwa katika vikao! Hakika hiyo ndiyo kauli ya wengi na kama tunakubaliana na hilo basi sote tusimame pamoja kulaani waraka kwasababu waraka haukuwa ndani ya vikao vya CDM.

Hakuna kuchagua mambo ya vikao na mambo ya 'ukombozi'.
Unless uniambie sababu zingine nabaki kukubaliana nawe kuhusu vikao na ningefurahi kama ungekubaliana nami kuhusu uharam wa waraka.

Hili la ZZK kuleta madhara kwa CDM, kwa wanachama na wapenzi wa CDM ni tatizo na linawasononesha.

Kwa ZZK hicho ndicho amekitafuta kwa muda mrefu sana.
Kama angekuwa mtu wa kujifunza vurugu 3 za mwanzo zilitosha kumfundisha kuwa anaua chama chake kama ni mtiifu, kwa mtazamo wa haraka haui chama anatimiza ndoto zake.

Kama ataamua kuzamisha meli na mzigo hilo ni juu yake na CDM, hakuna ubishi.
Mara ya 4 hii anakwenda kinyume na utaratibu Mkandara anaopendekeza wa vikao lakini Mkandara huyo huyo anarudi na kusema hapana! kuna issue zinatakiwa ziandikiwe waraka wa siri.
 
Nguruvi3,

Ahaa pengine hujaisoma vizuri lakini hiyo chat page imejieleza wazi ya kwamba Kafulila alienguliwa nafasi yake ya Uongozi ktk kikao kilichofanyika Dodoma na yeye aliwaita waandishi wa habari baada ya Dr.Slaa kumwambia kilichotokea. Katika kukumbushana, jaribu fuata mtiririko wake, isome hadi chini, imejieleza vizuri tu.

Watu wangu mnakurupuka kutaka kuzungumzia hatua ya pili ya kupokonrwa ZZK Uanachama mkiiweka kando sehemu hii ya kwanza - Kuachishwa madaraka yote alokuwa nayo pasipo kufuata kanuni za chama, mkitumia tu Uhaini ambao hadi sasa hivi hatufahamu ZZK alihusika vipi isipokuwa kupitia magazetini na dhana inayotumika onayotokana na karibu wake na wahusika. Ni dhana hiyo hiyo inatumika kumhusisha na CCM kutokana na ukaribu wake na JK au viongozi wa CCM. Hivyo yeyote alokuwa karibu na ZZK ama kupewa support na ZZK mna question - KULIKONI?.

Kuhusu waraka nimekuuliza toka mwanzo hukunijibu. Ikiwa wajumbe wote 33 wa kamati kuu ni viongozi wa chama nawe hukubaliani na uongozi wao utaandika vipi waraka wa mageuzi na timu hiyo hiyo? na katika vikao gani haswa ikiwa ni wao wanao kifisadi chama? Labda nirudie hivi, ikiwa wewe ni Polisi ma imetokea umemwona mkuu wa kituo na askari wake wameshiriki ktk ujambazi na sheria inakutaka wewe ukaripoti Kituoni kwako. Je, wewe utaenda kwa mkulu wako ku report?

Kumbe basi taratibu za Kisiasa ziko hivi, ikiwa mjumbe ama wajumbe wanaona chama ama nchi inaongozwa vibaya na inapelekwa kinyume cha miiko na maadili ya chama, Kuna Udikteta ama Uhafidhina kinyume cha itikadi na sera za chama, mjumbe/wajumbe wanaweza tu kutoa lawama zake/zao ktk vikao vya chama na zisipo sikilizwa ana/wanaruhusiwa kujipanga kushiriki ktk uchaguzi ujao.

1.Mashtaka 11 ya ZZK 10 yanahusu Kugombea ueneyekiti ambao tumemuona ZZK akiutaka toka mwaka 2009, in fact 2008 na akapigwa chini akichukua form tu.
2. Swala la magesabu ya chama na Posho, Zitto kayazungumzia toka zamani na hata Lema alisema wazi hilo la Posho lilikuwa swala la Chama Zitto akaliteka. Sasa wao wamefanya nini baada ya kutekwa? hawataki kuachia Posho za vikao! wanachukukia kwa nini asiwatonye mahesabu yatakaguliwa na GAC ina maana hatukuwa na ufanisi ktk utunzi wa mahesabu wala up to date!

3. Je, madai yao kina Kitila kuhusu viongozi? - hatuna jibu hata moja! hawakanushi wala kukubali na haitakiwi kuzungumziwa maana anayeshtakiwa ni ZZK sio Uongozi wala Kamati kuu!.. sasa kweli ulitegemea mtu kuandaa waraka kama huu ktk vikao, sijui vikao gani?

Mkuu hakuna sheria wala kanuni inayosema ni wakati gani mwanachama/wanachama wanatakiwa kuadaa nia ya mageuzi isipokuwa tunaelewa ni wakati gani kampeni zinatakiwa kuanza...Mwenyekiti Mbowe hakutokea mbinguni, huyu aliandaliwa, alifunzwa na kufundwa kwa maandalizi ya kuja kuongoza chama. Na kwa maandalizi yake haikuwa kupitia vikao vya chama bali wale walomtunuku nakuona kipaji chake. Hakuna alosema ama kutaka kujua maandalizi hayo yalianza lini?

Huku nyuma nimekuambia wazi kabisa ya kwamba WARAKA hauna tatizo ikiwa swala lenyewe linahusu Ufisadi na linahitaji mageuzi ya uongozi sio Itikadi ama sera za chama. Mkuu wangu haiwezekani Msouth kupinga Apartheid, ukataka kufanya mageuzi ati kwa kupitia vikao vya chama cha Makaburu, ama kupitia Ofisi ya rais. Pengine nyie mnayaona haya madai ya kina Kitila ni madogo lakini kwangu binafsi sii madogo hata kidogo na kama tungeendelea hivi hivi pasipo huo waraka nina hakika CDM ingefanya vibaya sana mwaka 2015 kwa sababu hatukujua yalokuwa nyuma ya pazia.

Sasa pengine baada ya kutajwa na madudu kujulikana, pengine uongozi utajirekebisha na kutambua ya kwamba hakuna siri ya watu wawili na ZZK ni bangusilo tu tumesha achwa uchi wa nyama. Mkuu wangu mimi mutoto wa Mujini huwa nazisoma alama za nyakati kabla hata hazijatoa nuru... Ni sawa kabisa nikwambie leo hao Yanga Afrika wameenda shamba (UTURUKI) kufanya nini? hutanielewa zaidi ya kuwa ati mazoezi ya mpira! Usiyaone ya kuwa huko Uturuki kwenyewe ni winter, baridi kali minus 10 kila siku ya Mungu.. Je, hayo mazoezi ni mazoezi gani haswa! kwani hakuna nchi za joto ambazo Yanga wanaweza kwenda wakati kama huu ikiwa ni lazima. Hapo hujisemea Mhhhhh! halafu naunganisha shamba kuna nini haswa?.. UNGA na kama kawaida ya JKN Airport wachezaji wetu wakirudi toka nje huwa hawapigwi search ya nguvu - hukuliona hilo - sherehe tupu!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mkandara
Kuna mahali tumekutana baadaye unaniruka tena. Tumekubaliana kuwa mambo ya vyama vya siasa kama CDM yamalizwe katika vikao vya chama. Kwa msingi huo waraka haukutakiwa kuwepo kwasababu ni nje ya utaratibu wa vikao vya chama na kama ililazimu uwepo basi ulitakiwa uwe addressed kwa vikao vya chamaé Hilo halikufanyika kilichotokea ni waraka wa siri ambao maudhui yake tu yanatia kinyaa.

Kuhusu wajumbe 33 na kwamba ilikuwa ni vigumu kuongelea suala hilo, nimeeleza huko nyuma kuwa ZZK alikuwa na fursa tatu kubwa za kufanikisha mambo yake tena akiungwa mkono na wanachama wengi wa CDM
1. Alitakiwa alieleze wazi katika vikao na kuonyesha kuwa
a) Kama hatasikilizwe atajiuzulu nafasi zake
b) Kuwashawishi wajumbe wajiuzulu nafasi zao kama sehemu ya kupinga uendeshaji mbaya

2. ZZK kujiuzulu bila kutoa malalamiko katika vikao na malalamiko yake ayafikishe kwa mahakama ya wanachama

3. ZZK kususia vikao vyote vinavyohusu mambo ya chama, shughuli za chama na kueleza kwanini anafaya hivyo.

ZZK na wenzake hawakuchukua hatua zozote, walichokifanya ilikuwa u-spy ili kutekeleza mipango yao nje ya utaratibu wa CDM au taasisi nyingine yenye nidhamu.

Kushindwa kwao kutenda hayo hakuwapi haki ya kufanya mambo ya kufarakanisha wanachama kwa njia za siri
Kitendo cha kutumia mitandao ya jamii kueleza mambo ya waraka ni uhuni kwa viongozi na hasa wenye elimu kama zao.

Waraka hata kama una maudhui mazuri kisiasi gani bado unabaki kuwa hovyo.
Unapokuwa na maandazi matamu ukayafunga katika magazeti yenye matope uzuri wa maandazi hayo haupo tena.Ukiusoma waraka kuna kejeli na matusi ambayo hayakupaswa kuwemo.

Ushiriki wa ZZK umesemwa na Kitila, alikuwa briefed, kimazingira ZZK alishaanza kutekeleza mkakati. Unachokitaka kukisikia ni nyaraka na kusahau kuwa laptop ya mwigamba ilijaa habari za akina `Chadema Mpya` n.k. mawasiliano yalikuwepo hilo halina ubishi.

ZZK alishiriki kwa Kafulila, Juliana na Masalia na kote hakuna ushahidi wa maandishi kuhusu kushiriki kwake, lakini upo ushahidi wa yeye kushiriki tena kama mfadhili wa vurugu hizo.
Leo hamjui Ben Saanane bado unaamini ZZK anaweza kukueleza jambo ukamwamini.

Kama unahalalisha waraka, sijui kwanini unakataa mipango ya nyuma aliyoshiriki,sielewi mkuu.
Vipi umuone ni shujaa wakati unasahau matimbwili ya nyuma ambayo hayakuwa katika vikao.

Na mwisho, nadhani uongozi hauwezi kujibu na haupaswi kujibu mambo vichochoroni yenye chembe za mipasho.

Waraka ulikuwa wa siri haukufanyika katika vikao unavyovisema, leo vipi ulaumu uongozi kujibu tuhuma za watu walioamua kukaa pembeni na kuleta mtafaraku.
Mkuu soma yafuatayo kwanza
`Kiwango cha elimu cha mpinzani wetu ni magumashi

''Mpinzaniwetu ni mgumu sana katika kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwonakama si mwenzao kiumri na kifedha, wanawake humwona kama malaya anayependakutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona kama mtu anayedhalilishahata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni waziwazi hata kuvunja ndoa si ya kwaketu bali hata za watu wengine

''Mpinzaniwetu hana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii,utamaduni, michezo, nk. Si tuelimu yake ya darasani ni ya magumashi bali piavipaji na akili ya kuzaliwa havijaonekana katika maisha yake''

Zitto ni kiongozi ....amekuwa ndiyemwakilishi pekee aliyeongoza katika kuibua kashfa nyingi na nzito za ubadhirifundani ya serikali hata kufikia mawaziri kadhaa kufukuzwa kazi''

Ungekuwa wewe Mkandara ndiye uongozi ungejibu nini
 
Nimefurahishwa sana na mjadala huu unavyoendelea na hasa kwa michango inayotolewa na wakuu wawili Mkandara na Nguruvi3...nawaomba mzidi kumwaga nondo, asanteni sana. Kwa kuwa mimi toka mwanzo nilikiri upungufu wangu kwa kuchagua upande toka mapema, natanguliza samahani kama mchango wangu huu kiduchu utaonekana haukidhi kiwango kilichooneshwa ndani ya huu mjadala muhimu. Huu waraka tunaoujadili nimeusoma kwa makini sana; nimeusoma zaidi ya mara moja na kila nikiusoma najikuta najiuliza maswali kadhaa kuhusu hasa lengo la waraka...je lengo kuu ni kuimarisha chama au kudhoofisha chama! Najiuliza hili swali kwa sababu hata nikitafakari vipi sioni namna mipango/njama hii ya siri hata kama ingeweza kufanikiwa, chama kingebaki salama.

Hapa chini nitanukuu vifungu kadhaa ambavyo naamini vinazua maswali badala ya kutoa jawabu kama kweli waandaaji wa waraka walikuwa na nia njema na Chadema, swali kuu ni timing, why now! Pengine hali hii ingeeleweka kama ingejitokeza mara tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kama ilivyotabiriwa na wenye wivu na hofu...Chadema kusambaratika baada ya kushindwa Uchaguzi! But against all odds, Chadema imezidi kuimarika na kuwa tishio kwa status quo day in and day out na sasa tukiwa tunakaribia uchaguzi mwingine 2015 waraka unajitokeza! Waraka unaouponda uongozi uliopo kwa dhihaka na kejeli; uongozi ambao ndio umeleta mafanikio makubwa tunayoyashuhudia...duh, utadhani waraka umeandaliwa na mahasimu wa Chadema...kumbe ni viongozi wa juu ndani ya Chadema wanaoshiriki kwenye vikao vinavyotoa maamuzi! Haya twende;
Tunayemtaka said:
Ni mvumilivu sana. Katika jitahada za wakuu waliopo kuhakikisha wanaendelea kukalia viti vyao, wamejitahidi sana kumpaka matope lakini amevumilia. Mahali ambapo wengine wangeshakata tamaa na kuhama taasisi, yeye alibaki kuvumilia mpaka imefikia wana taasisi wa ngazi za chini waliokuwa wanadanganywa kwamba mtu huyu ni msaliti, wameanza sasa kushtuka
Ni vigumu kuamini kwamba wahusika wa huu waraka ni sehemu ya uongozi...tena viongozi wa juu! Kwa ustaarabu na akili za kawaida kiongozi anayefikia hali kama hii, ana mawili; kujipima na kama nafsi inamsuta katika ushiriki wa pamoja na wenzake, ama anajirudi au anajiuzulu. Pamoja na hilo kama madai kuwa hata waliokuwa wanadanganywa kwamba huyu mtu ni msaliti wameanza kushtuka, hofu gani inawazuia kuachia nafasi zao ndani ya uongozi ili kujitenga na maamuzi wasiyoyaafiki. Hapo watakuwa japo na uhalali wa kuushutumu uongozi uliopo waziwazi na mathalan wanaowaunga mkono wapo kama wanavyodai, kwa nini kificho?
Tunayemtaka said:
Kuna wakati tunayemtaka hu-respond kwa taharuki kubwa dhidi ya mashambulizi yanayoelekezwa kwake jambo linalomfanya achukue maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati huo. Kwa kifupi kuna wakati tunayemtaka huonekana kufanya maamuzi kwa emotion zaidi badala ya kutulia kwanza na kutafakari kwa kina ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri kwa wenzake kabla ya kurespond. Jambo lililoelezwa katika ‘d' hapo juu humfanya tunayemtaka wakati mwingine kuonekana ana jazba sana kwa sababu akishataharuki na kuchukua maamuzi akingali kwenye taharuki huwa ni rahisi sana kuonekana anajibu mapigo kwa jazba sana.
Nashindwa kuwaelewa waandaaji wa waraka, hivi "tunayemtaka" bado ni yule yule? Au bado anatafutwa mwingine! Utakaaje chini na kuandaa waraka wa kutekeleza mapinduzi (?) ya uongozi wakati tayari una wasiwasi kama unayemtaka anakidhi sifa ambazo inadaiwa uongozi uliopo hauna? Lakini la msingi zaidi ni je haya mapinduzi yalikuwa yanapangwa kutekelezwa lini; mwaka jana, mwaka huu au mwaka wa Uchaguzi?
Ustahimilivu said:
yaliyotajwa katika ‘d' na ‘e' hapo juu yanaashiria tunayemtaka si mstahimilivu sana sifa ambayo inahitajika sana kwa kiongozi.
Hayo ni maneno ya waandaaji wasomi wanaopanga kwa siri kufanikisha mabadiliko katika uongozi yatakayoiwezesha Chadema kufanya vizuri katika uchaguzi mwaka ujao! Ajabu ni kwamba wanaanza kwa kukiri kuwa wanayemtaka hana ustahimilivu, sifa ambayo wanadai inahitajika sana tu kwa kiongozi!
Uwazi said:
Katika taasisi zetu hizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi wazi hata kama ni mema ama ni haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo. Kuna mambo ambayo ni haki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damu kutoka upande mwingine wa utawala, nk.
Nimejaribu kuutafuta huu uwazi unaoongelewa hapa lakini siuoni. Ninauona ni ushauri kwa tunayemtaka kuepuka kufanya mambo wazi wazi hata kama ni mema ama ni haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo! Kwamba kiongozi kama huyo ndiye anafaa ni jambo lisilo rahisi kueleweka katika karne hii ya utandawazi...kama kuna nia njema, huo usiri ni wa nini!
Siri said:
Lakini mambo hayo ni muhimu wakati mwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwa unaowaongoza.
Astaghfirulah!
Mkakati No. 1 said:
Tunahitaji kutekeleza mkakati huu kwa siri kubwa ili mkuu aliyepo aendelee kubweteka na ndiyo maana hata lugha iliyotumika ni ndani hapa ni ya pekee. Tunahitaji tunayemtaka asionekane kama kuna kitu anafanya na tunafurahi kwamba kuna wakati alitangaza kwamba hana nia ya kugombea tena waliopo wanatosha. Ikitokea vyombo vya habari vikamuuliza tena hiyo ndiyo iwe kauli yake ili kuendelea kumfanya mkuu aliyepo asihangaike na hivyo kuja kummaliza kirahisi.
Kwangu huu sio mkakati tena wenye nia njema; makakati ambao moja ya silaha yake kuu ni udanganyifu? makakati ambao silaha yake ni fitina na uongo? Napata taabu kuamini huu waraka ulitayarishwa na wanaojiita wasomi, wanaodhani ni wao tu wanaweza kuielewa lugha iliyotumika...hapana kwa lugha yoyote ile sisiti kuuita waraka huu kwa jina lake kamili, waraka wa hujuma. Kwamba waendelee na nyadhifa zao, wakikuhudhuria vikao vya chama na kukubaliana na maamuzi yanayofikiwa kinafiki ili wasishtukiwe, ni dhambi isiyovumilika na isiyosameheka. Kwamba katika kufanikisha malengo yao wawe tayari kuvaa ngozi ya kondoo kumbe ni mbwa mwitu...a leader cannot go lower than this and still feel he/she deserves any iota of respect!
Mkakati No. 2 said:
Aidha katika utekelezaji wa mkakati kama tutakavyoeleza hapo baadaye, tunayemtaka atajitenga mbali asionekane hata kuwa karibu na sisi. Vikao vyetu na yeye vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi ikiwezekana hata nchi jirani.
Hapa waandaaji wa waraka wanaonekana wakidhani wanaishi kwenye nchi ya kusadikika na siyo dunia yetu hii ambapo hata kuta zina masikio. Faragha yote hii ya nini? Kukutania hadi nchi jirani kupanga kuupindua uongozi wa Chadema? Ningeelewa kama wangekuwa wanafanya njama za kuipindua serikali lakini hii ya kupindua uongozi wa chama cha siasa kisicho na dola, chama cha upinzani ambacho ndio kwanza kinajijenga ili kiweze kutwaa madaraka? Hofu yote hii inatoka wapi? Je kweli Chadema inatisha kiasi hicho? No wonder ndani ya CCM watu hawalali! Lazima kuna kitu hapa kinafichwa na sidhani kama huu woga wa waandaaji unasababishwa na Chadema, kuna kitu zaidi na hapa ndipo dhana ya usaliti unapodhihirika na kudhihirishwa.
Fursa No. 1 said:
Dini: Kwa kuwa ni mwislamu. Hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu.
Hoja ile ile na wimbo ule ule unaoimbwa na mahasimu wale wale wa Chadema...Udini.
Fursa No.2 said:
Ukabila: Kujitokeza kwa tunayemtaka kutaonekana kama fursa kwa wanataasisi kufanya mabadiliko makubwa na kuua kabisa ile propaganda ya kwamba taasisi yetu ni ya kabila fulani ama eneo fulani kwa kufanya reference kwa uongozi wa taasisi.
Hoja ile ile na wimbo ule ule unaoimbwa na mahasimu wale wale wa Chadema...Ukabila.
Fursa No. 3 said:
Elimu: Elimu ndogo na duni aliyenayo mpinzani wetu ambaye ndiye mkuu wa taasisi yetu kwa sasa. Kwa sasa ni kiongozi pekee katika nchi yetu anayeongoza taasisi kubwa asiye na elimu ya shahada huku taasisi yetu ikiwa inaongoza kwa kuwa na wasomi waliobobea katika kila nyanja. Hii ni kejeli hasa kwetu sisi ambao tumekuwa tukiwasema wenzetu kwamba ‘akili ndogo' inaongoza akili kubwa. Kimsingi tumekuwa tukijisema kwa kukubali
kuongozwa na mtu mwenye akili ndogo.
Kwa maneno hayo hapo juu wamezidi kuonesha upungufu mkubwa katika kufikisha ujumbe wao na nia ya waraka na kama ningekuwa wao, baada ya huu waraka kuanikwa, ningekaa kimya kwa aibu. Wanaweza wakaamini wanamdhalilisha Kiongozi wao Mkuu lakini hapa kwa kweli wanawadhalilisha maelfu kwa mamilioni ya Watanzania walioweka matumaini yao kwa Chadema. Nitashangaa kama MwanaChadema halisi anaweza kupingana na hatua iliyochukuliwa na uongozi ya kuwavua madaraka hawa ambao mimi Mag3 sisiti kuwaita wasaliti. Kama kuna walilofanikiwa hawa wasaliti ni hilo la kuipa CCM fimbo. Hata hivyo naamini kwa namna ile ile Chadema iliweza kupitia tanuru moja baada ya nyingine na kuvuka salama na tanuru hii itavuka ikiwa imara zaidi.
 
Mkuu Mag3
Ahsante sana kwa mchango wako
Nimewahi kuuliza mara nyingi kuwa waandika waraka wengekuwa madarakani, je njia wanazozitumia wangekubaliana nazo?

Mkuu Mchambuzi kaeleza kuwa kwa contents na context waraka una matatizo makubwa.
Ninashukuru kuwa umekuja na kunyumbulisha zaidi matatizo mengine ya waraka kwa mtazamo mwingine unaofikirisha sana kwa anayeliangalia tatizo la CDM kwa ukweli .

Mkuu Mkandara tupo naye sehemu kubwa tu tunapoachana ni pale anaposema njia zilizotumika zilikuwa sahihi. Nimemuuliza kama njia nyingine ziliwahi kutumika, amenipa majibu nusu.
Mathalan, nilisema kuwa akina 'waraka na ZZK ' walikuwa na nafasi zifuatazo

1. Kueleza matatizo katika vikao jambo inalotetewa kuwa agenda zilizuiwa. Hiingii akilini kuwa hata kwenye OAB za vikao hilo halikujadiliwa. Hata hivyo kulikuwa na nafasi nyingine

2. Kujiuzulu nafasi zao kama sehemu ya kuonyesha kuwa kulikuwa na tatizo. Njia hiyo ingeamsha curiosity kwa wanachama wao nini kinaendelea.

3. Nafasi ya mwisho ilikuwa kuwashawishi wajumbe waelewe tatizo ili lipate msukumo.

4. Na nafasi ya mwisho ilikuwa kueleza katika mikutano ya ndani na wanachama wao kuhusu hali ilivyo katika chama chao.

Hizo ndizo njia za uwazi na kidemokrasia za kuikomboa CDM yao. Na hakika wangeungwa mkono kwa kuelewa kuwa tofauti ya mawazo ni jambo lisiloepukika katika siasa za vyama vingi.

Njia ya kuandika waraka wa siri wenye upungufu wa kisomi ilikuwa ni dhalili.
Maudhui ya waraka hayana chembe ya kampeni hata kidogo, wala kiashirio cha mageuzi.
Ni sentiments na personal attack ambazo sidhani kama ni tatizo la CDM kama taasisi.

Tatizo la wanaCDM baadhi wamelewa mapenzi na hivyo kutafuta namna ya kuhalalisha hata ubaya.
Hili la waraka halihusiani na chuki ni tatizo la baadhi ya watu kutaka madaraka.

Ambitions za madaraka si jambo baya kama zinafuta taratibu. Waandika waraka hawakufuata taratibu walikuja na mapinduzi.

Uchaguzi unakuja ilikuwa ni wao kuachia ngazi za uongozi na kujipanga kama timu ya upinzani ndani ya CDM kwa sera na maono. Hawakukubali hilo wakaamua kufanya makosa zaidi ya kuwa katika uongozi wasiokubaliana nao. Huo ni unafiki na usaliti.

Nashindwa kuelewa sijui kwanini wanaCDM hawakubali ukweli, yaani baadhi wapo katika state of denial.

Hilo ndilo linaiumiza CDM kwasasa vinginevyo wangeliona tatizo na kulikubali tatizo kama lilivyo leo wangekuwa katika kampeni zao dhidi ya mahasimu wao.

Hilo halitokei kwasababu mvutano umekithiri, mvutano usio na sababu kwasababu ukweli unaonekana.
 
Last edited by a moderator:
Nimeyatafakari haya Maneno ya Zitto kwa kweli yamenifanya nifikirie kama WAS ZITTO Serious in Politics

Slaa hakuwahi kutangaza nia ya kugombea Urais wakati wowote ule wa maisha yake. Mwaka 2010 Tulimwomba kama chama. Chama kinaweza kumwomba tena na tukifikia mwafaka ndio atakuwa huyo na sote lazima tumwunge mkono. Mimi nimetangaza kwa kuwa ninautaka Urais na hivyo nakiomba chama kiniteue. Pia chama kina viongozi wengine wazuri tu. Tundu Lissu na Mnyika wamesema hawautaki Urais. Ndugu Mbowe yeye hajasema kama anautaka au la. Kumbuka hata mwaka 2005 Mbowe tulimlazimisha, yeye alitaka aendelee kuwa Mbunge wa Hai. Sisi tukamwambia kuwa lazima abebe chama. Nakumbuka mimi binafsi niligombana naye maana aliposema yeye atagombea Hai, nikamwuliza kwa chama gani? Maana kama hutaki kukibeba chama kwenye Urais tutachukua kadi yetu. Ndio! Nilimwambia hivyo kwenye secretariat ya chama. Akakasirika kweli, lakini baadaye alinielewa na mafanikio tuliyoyapata ni makubwa sana baada yeye kugombea. Kwa hiyo hiyo School of Thought ni hisia tu za watu. CHADEMA ina watu wengi sana wenye uwezo wa kuwa maRais. Kitila Mkumbo mnamwonaje? Au mpaka watu wawe Bungeni. Huyu ni hazina ya chama na nchi. Chama kinaweza kusema, Zitto hapana, mwunge mkono Kitila. Nitafanya hivyo. The Party deploys for or against your wishes and every member must oblige a JUST deployment. I will.
 
Nguruvi3,

Ahaa pengine hujaisoma vizuri lakini hiyo chat page imejieleza wazi ya kwamba Kafulila alienguliwa nafasi yake ya Uongozi ktk kikao kilichofanyika Dodoma na yeye aliwaita waandishi wa habari baada ya Dr.Slaa kumwambia kilichotokea. Katika kukumbushana, jaribu fuata mtiririko wake, isome hadi chini, imejieleza vizuri tu.

Watu wangu mnakurupuka kutaka kuzungumzia hatua ya pili ya kupokonrwa ZZK Uanachama mkiiweka kando sehemu hii ya kwanza - Kuachishwa madaraka yote alokuwa nayo pasipo kufuata kanuni za chama, mkitumia tu Uhaini ambao hadi sasa hivi hatufahamu ZZK alihusika vipi isipokuwa kupitia magazetini na dhana inayotumika onayotokana na karibu wake na wahusika. Ni dhana hiyo hiyo inatumika kumhusisha na CCM kutokana na ukaribu wake na JK au viongozi wa CCM. Hivyo yeyote alokuwa karibu na ZZK ama kupewa support na ZZK mna question - KULIKONI?.

Kuhusu waraka nimekuuliza toka mwanzo hukunijibu. Ikiwa wajumbe wote 33 wa kamati kuu ni viongozi wa chama nawe hukubaliani na uongozi wao utaandika vipi waraka wa mageuzi na timu hiyo hiyo? na katika vikao gani haswa ikiwa ni wao wanao kifisadi chama? Labda nirudie hivi, ikiwa wewe ni Polisi ma imetokea umemwona mkuu wa kituo na askari wake wameshiriki ktk ujambazi na sheria inakutaka wewe ukaripoti Kituoni kwako. Je, wewe utaenda kwa mkulu wako ku report?

Kumbe basi taratibu za Kisiasa ziko hivi, ikiwa mjumbe ama wajumbe wanaona chama ama nchi inaongozwa vibaya na inapelekwa kinyume cha miiko na maadili ya chama, Kuna Udikteta ama Uhafidhina kinyume cha itikadi na sera za chama, mjumbe/wajumbe wanaweza tu kutoa lawama zake/zao ktk vikao vya chama na zisipo sikilizwa ana/wanaruhusiwa kujipanga kushiriki ktk uchaguzi ujao.

1.Mashtaka 11 ya ZZK 10 yanahusu Kugombea ueneyekiti ambao tumemuona ZZK akiutaka toka mwaka 2009, in fact 2008 na akapigwa chini akichukua form tu.
2. Swala la magesabu ya chama na Posho, Zitto kayazungumzia toka zamani na hata Lema alisema wazi hilo la Posho lilikuwa swala la Chama Zitto akaliteka. Sasa wao wamefanya nini baada ya kutekwa? hawataki kuachia Posho za vikao! wanachukukia kwa nini asiwatonye mahesabu yatakaguliwa na GAC ina maana hatukuwa na ufanisi ktk utunzi wa mahesabu wala up to date!

3. Je, madai yao kina Kitila kuhusu viongozi? - hatuna jibu hata moja! hawakanushi wala kukubali na haitakiwi kuzungumziwa maana anayeshtakiwa ni ZZK sio Uongozi wala Kamati kuu!.. sasa kweli ulitegemea mtu kuandaa waraka kama huu ktk vikao, sijui vikao gani?

Mkuu hakuna sheria wala kanuni inayosema ni wakati gani mwanachama/wanachama wanatakiwa kuadaa nia ya mageuzi isipokuwa tunaelewa ni wakati gani kampeni zinatakiwa kuanza...Mwenyekiti Mbowe hakutokea mbinguni, huyu aliandaliwa, alifunzwa na kufundwa kwa maandalizi ya kuja kuongoza chama. Na kwa maandalizi yake haikuwa kupitia vikao vya chama bali wale walomtunuku nakuona kipaji chake. Hakuna alosema ama kutaka kujua maandalizi hayo yalianza lini?

Huku nyuma nimekuambia wazi kabisa ya kwamba WARAKA hauna tatizo ikiwa swala lenyewe linahusu Ufisadi na linahitaji mageuzi ya uongozi sio Itikadi ama sera za chama. Mkuu wangu haiwezekani Msouth kupinga Apartheid, ukataka kufanya mageuzi ati kwa kupitia vikao vya chama cha Makaburu, ama kupitia Ofisi ya rais. Pengine nyie mnayaona haya madai ya kina Kitila ni madogo lakini kwangu binafsi sii madogo hata kidogo na kama tungeendelea hivi hivi pasipo huo waraka nina hakika CDM ingefanya vibaya sana mwaka 2015 kwa sababu hatukujua yalokuwa nyuma ya pazia.

Sasa pengine baada ya kutajwa na madudu kujulikana, pengine uongozi utajirekebisha na kutambua ya kwamba hakuna siri ya watu wawili na ZZK ni bangusilo tu tumesha achwa uchi wa nyama. Mkuu wangu mimi mutoto wa Mujini huwa nazisoma alama za nyakati kabla hata hazijatoa nuru... Ni sawa kabisa nikwambie leo hao Yanga Afrika wameenda shamba (UTURUKI) kufanya nini? hutanielewa zaidi ya kuwa ati mazoezi ya mpira! Usiyaone ya kuwa huko Uturuki kwenyewe ni winter, baridi kali minus 10 kila siku ya Mungu.. Je, hayo mazoezi ni mazoezi gani haswa! kwani hakuna nchi za joto ambazo Yanga wanaweza kwenda wakati kama huu ikiwa ni lazima. Hapo hujisemea Mhhhhh! halafu naunganisha shamba kuna nini haswa?.. UNGA na kama kawaida ya JKN Airport wachezaji wetu wakirudi toka nje huwa hawapigwi search ya nguvu - hukuliona hilo - sherehe tupu!

Uko sahihi mkuu,wanachokitaka kina Nguruvi3 hakiwezekani katika taasisi nyingi za kiafrika,mkubwa hasemwi
 
Last edited by a moderator:
ZZK NA KITILA KUANZISHA CHAMA KIPYA??!!

Makala hii ni kwa hisani ya gazeti la Raia Mwema
ITACHUKUA muda kuelewa nini hasa kilichokikumba Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA) hadi kikashindwa kutatua mgogoro wa uongozi na hatimaye kuingiza nchi katika kizungumkuti cha kisiasa tunachokishuhudia leo. Binafsi, kama mmoja ya wahusika wakubwa katika mgogoro huu nimepokea pole, lawama, na kwa kiasi fulani hongera kwa kumudu kuhimili mikikimikiki iliyonikumba. Nimepokea pole kutokana na misukosuko niliyokumbana nayo katika sakata hili hadi kufikia kufukuzwa uanachama.
Hili si jambo dogo katika maisha ya binadamu. Kufukuzwa katika ushirika wowote ni jambo linalosababisha mfadhaiko na ninazipokea pole nilizopewa kwa unyenyekevu. Ninashukuru pia kwa wale walionitia moyo kwamba hii ni ajali katika safari na nisikate tamaa katika kutoa mchango wangu katika harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Nami nawaahidi kwamba bado nipo imara na nitaendelea kushiriki kikamilifu katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa hapa nchini, ndani na nje ya vyama vya siasa.
Walionipa lawama ni wale waliokubaliana mia kwa mia na viongozi wa CHADEMA waliotujengea taswira ya usaliti na uhaini kwa chama kwa uamuzi wetu wa kuandaa mkakati wa kushinda uchaguzi ndani ya CHADEMA; mkakati ambao ulikuja kutafsiriwa kama mkakati wa mapinduzi ya uongozi halali ndani ya chama. Na kwa kuwa viongozi waliongea sana na kulirudia jambo hili mara kwa mara, na kwa kuwa jamii yetu imejengwa katika kuamini uongozi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, wapo watu wengi ambao wameafikiana na tafsiri ya uongozi kwamba waraka ule ulikuwa ni mkakati wa mapinduzi na haukuwa na nia njema.
Wapo pia wananchi walionilaumu kama sehemu ya uongozi wa chama kwa kushindwa kuyamaliza mambo yetu ndani ya chama. Na wengine wamenilaumu kwa kutokuwa na moyo wa kubali yaishe, kwamba ningekubali kosa, hata kama siamini kwamba ni kosa, ili niombe msamaha yaishe, tusonge mbele. Natamani ingekuwa rahisi hivi na kwamba kungekuwa na nia njema kwa pande zote mbili, pengine neno samahani lingetosha kumaliza mgogoro huu.
Kwa sababu hii nazipokea lawama zote kwa unyenyekevu pia na ninakubali kwamba nimeshiriki, bila kutarajia, kusababisha usumbufu na kutatiza tamanio na tumaini la mamilioni ya Watanzania katika kuitoa CCM madarakani. Hata hivyo, taswira ya mgogoro huu ni pana kuliko inavyoonekana na pengine tutapata nafasi nzuri zaidi mbele kueleza vizuri kilichotokea katika maandishi ili watu waelewe na waielewe CHADEMA na viongozi wake vizuri, na kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
Sitarajii katika makala haya kukidhi kiu ya watu wengi wanaotamani kujua ukweli wa mgogoro ndani ya CHADEMA na pengine mimi siye mtu sahihi kueleza jambo hili kwa kuwa nina maslahi ya moja kwa moja. Ninatoa changamoto kwa watafiti wa sayansi ya siasa kulifanyia utafiti jambo hili na kuliweka bayana, ili watu wapate kujifunza na kulijua vizuri.
Nieleze tu kwamba mgogoro huu unatukumbusha kuwa, pamoja na kwamba tupo katika mfumo wa vyama vingi, bado tumeendelea kuukumbatia utamaduni wa chama kimoja. Kwa hiyo tuna vyama vingi vya siasa, lakini vyama hivi bado vinakumbatia utamaduni wa chama kimoja. Utamaduni wa chama kimoja ni utamaduni hodhi na wa kiimla. Uongozi katika utamaduni wa chama kimoja unapatikana kwa njia za uteule, ukiwahusisha watu wachache wateule. Utamaduni wa chama kimoja unakataa ushindani wa wazi. Katika utamaduni wa chama kimoja kutamani cheo fulani ndani ya chama na katika serikali ni ulafi na uroho wa madaraka. Ndio maana vyama vyetu vyote vikubwa hapa nchini vinakataza na kukemea wanachama wao kutamani na kutangaza nia ya kuwania madaraka makubwa kama vile urais au uenyeviti wa vyama.
Kutamani madaraka peke yake kunakatazwa, achilia mbali kuandaa mkakati wa kushinda nafasi unayoitamani. Na hili ndilo kosa tulilolifanya. Tulikuwa wajinga sana kudhani kwamba tupo katika mfumo na utamaduni wa vyama vingi ambapo mtu yupo huru kutamani cheo chochote katika chama chake cha siasa, na kutengeneza mikakati ya kushinda cheo hicho katika uchaguzi huru ndani ya chama. Tulikuwa wajinga kwa kujaribu kuachana na utamaduni wa kuvizia cheo na kujifanya hutaki wakati unataka.
‘Msaliti' mwenzetu Zitto Kabwe alianza siku nyingi mwaka 2009 kwa uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama bila kupata ridhaa ya wazee wa chama. Alikuwa mjinga kudhani kwamba uongozi katika mfumo wa chama kimoja unapatikana kwa kujaza fomu na kuomba kura. Nami nilikuwa mjinga nisiyeelewa kwa kumuunga mkono na kumtaka asonge mbele katika nia yake hiyo. Hakuishia hapo, Zitto Kabwe akafanya ujinga mwingine kwa kutamani na hatimaye kutangaza kugombea urais kupitia chama chake. Huu nao ulikuwa ni usaliti kwa utamaduni wetu wa chama kimoja, kwa sababu katika utamaduni huu nafasi kama hii ni ya kiteule na wateule na wateuaji wapo.
Ninapokubali kupokea lawama katika kushiriki kusababisha mgogoro unaoendelea ndani ya CHADEMA, naomba nami niwarushie lawama tele wanachama na mashabiki wa chama hiki, na wapenda mabadiliko kwa ujumla. Nawarushia lawama wanachama na washabiki wa CHADEMA kwa kuwashabikia viongozi wa chama chao katika kukinyonga chama. Viongozi wa chama hiki wamefanya makosa mengi na makubwa hadi kusababisha mgogoro ufike ulipofika, lakini wanachama na mashabiki wa chama wamekuwa wakishwashangilia katika kila hatua walioifanya. Kwa hiyo lawama ya kwanza kwa wanachama na mashabiki ni pale walipokubali kugeuzwa kuwa mashabiki wa viongozi ndani ya chama badala ya kuwa mashabiki wa chama. Na kwa kuwa ushabiki hupofusha macho na akili, mashabiki wa viongozi hawatofautishi kati ya uongozi na chama. Ni kama vile wamedanganywa na viongozi waliopo na wakakubali kudanganyika, kwamba uongozi wa chama ndio chama, na chama ndio uongozi!
Ni kwa sababu ya ushabiki kwa viongozi, ndio maana ilifika mahala wanachama na mashabiki wa CHADEMA wakagawanyika katika makundi ya washabikia viongozi, na chama kikakosa watu wa kukishabikia na hapo kikajikuta hakina mlinzi.
Makosa yaliyofanywa na uongozi na wanachama wa CHADEMA unafanana sana na makosa yaliyofanywa na viongozi na wanachama wa NCCR Mageuzi miaka ya tisini. Kama inavyotokea kwa CHADEMA leo, wanachama wa NCCR Mageuzi waligeuka kuwa mashabiki wa viongozi, kundi moja likimshabikia Mrema na kundi jingine likiwashabikia akina Marando. Kwa kudhani kwamba chama kilikuwa imara sana, kundi la akina Marando likaamua kumfukuza Mrema likiamini kwamba alikuwa hana madhara yoyote kwa sababu chama kilishaimarika mno, wakisahau kwamba msingi wa ufuasi ulijengwa kwa viongozi na sio kwa chama.
Mrema alipotimka, akatimka na mashabiki wake. Hicho ndicho kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Kuna watu wenye mtazamo finyu wanaamini kwamba chama hiki ni imara sana kwa sasa kiasi kwamba hata wakimfukuza Zitto kitaendelea kubaki imara. Wamesahau kwamba wamejenga ufuasi kwa viongozi, na hivyo watakapomfukuza Zitto atatimka na wafuasi wake na chama kitayumba. Wangekuwa na mtazamo mpana wa kimantiki, na kama wangekuwa ni watu wa kujifunza, viongozi wa CHADEMA wangelimaliza sakata la Zitto ambalo sasa lipo mahakamani kwa njia ya usuluhishi kimya kimya kama walivyofanya NCCR kwa Kafulila. Lakini kwa sababu ya upofu unaoendelea unaotokana na kugubikwa na ulevi wa utamaduni wa chama kimoja kwa upande mmoja, na ulevi wa umaarufu kwa upande mwingine, hawatakubali yaishe nje ya Mahakama, na hatimaye watamfukuza Zitto. Wakishakumfukuza Zitto atatimka na mashabiki wake, chama kitayumba na kutoa unafuu kwa CCM. Katika mazingira haya tunahitaji sana mbadala wa CCM na CHADEMA.
Makala hii imeandikwa na Kitila mkumbo ambaye ndiye mwandishi mkuu wa waraka.

Ukimsoma kwa undani utaona halalamiki kuhusu waraka wala kuutetea.
Anachokifanya ni kuonyesha kuwa Zitto ameonewa kwasababu ya kutaka ueneyekiti.

Hiyo ndiyo kauli za ZZK na Kitila na ushahidi mwingine wa kimazingira kuwa wawili hawa wapo same page na waraka walishaanza kuufanyia kazi.

Kuna kitu ambacho wengi hawakielewi kuhusu waraka huu.
Anachofanya hapo Kitila ni kuitisha CDM ifanye kile ambacho NCCR imekifanya kumaliza mgogoro. Kitila amesahau kuwa mara 4 ZZK ameshaonywa kuhusu usaliti na kuyamaliza kimya, je hilo lilitoa suluhisho?

Pili, anatisha kuhusu wafuasi wa ZZK kutimka naye.
Hapa si kwamba anatisha, anachokifanya ni kuwaambia wafuasi wawe tayari kuondoka na ZZK.

Makala hii ni dalili kuwa ZZK na Kitila wapo mbioni kuanzisha chama chao.
Ukisoma kichwa cha habari na maudhui utashindwa kuelewa, kwa sisi wengine tunajua kuwa hii ni baragumu la chama kipaya.

Kitila hawezi kuitaka CDM imalize mgogoro kimya wakati huo akisema kunahitajika mbala wa CCM na CDM.

Kwa ufupi ZZK na Kitila wapo katika maandalizi ya kuanzisha chama chao, wanachokifanya ni kuhakikisha wanaibomoa CDM.
Mchambuzi Makandara Tuko Pasco Mag3 platozoom zumbemkuu Zinedine AshaDii Mzee Mwanakijiji Kichuguu FJM Mwita Maranya Ben Saanane Ritz @Nape nauye
 
Mkuu Nguruvi3, kama utakumbuka baada tuu ya kuibuka mgogoro huu, nilisisitiza tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tuwe more objective ba tusitake sides besides side ya ukweli halisi!. Nakumbuka kama nilikutuhumu for taking sides, and here you come again with the same side ya upande uliouchagua!.

Swali la msingi nililouliza tangu day one!, ule waraka ni uhaini kweli?!. Walipanga kufanya mapinduzi, au waliounda "a winning coalition" ili uchaguzi ukiitwa wamfungulia chaguo lao chances za kushinda!.

Andiko la Kitila nimelisoma na kulisoma na kulisoma, kiukweli nimemkubali!. Anachofanya sasa, ni kuwa mkweli kabisa kuwa kuwa Chadema imetumainiwa sana kuwa ndio chama mbadala!. Kwa wote wenye macho na masikio, waliishaiona Chadema inamatatizo ya kuiongozi kabla hata ya hili tifu na tumeijadili sana humu!.

Lengo la waraka ule ni ku address some serious issues na kuweka uongozi capable wa kuchukulia ikulu 2015. Baada ya hili kushindikana, amekuwa mkweli kabisa na kwanza kusema, kama bado mnaitumainia Chadema hii hii inayokwenda kumfukuza Zitto, then kwa 2015, hakuna kitu!. Watu serious wote wameisha jua kwa uchaguzi wa 2015, Chadema iliyopo as it is now, minus Zitto, ni hakuna kitu!. Ameshauri tupate chama kingine serious cha upinzani cha kuingoa CCM madarakani na sio Chadema!.

Ule waraka ulikuwa ni waraka wa kweli wenye very genuine na serious issues!. Chadema inafunika kombe kwa kuwatimua waandika waraka, ili tuu mwanaharamu apite badala ya kuziadress hizo issues, na wanataka kujiplease wakishamfukuza Zitto, they'll be very safe kuendesha chama kama saccos fulani!, no way, some of the truth members of Chadema akiwemo Prof. Beregu, hawatakubali!. Na hapo the game will be on again!.

Pasco.
 
Mkuu kabla sijajibu hoja zako nikuulize swali. Je njia zilizotumika za ule waraka zilikuwa sahihi?
 
Pasco,
Thanks yaani sijui kama hawa wanajisoma vizuri na kisha kulinganisha hoja zao na waraka wenyewe ama wanapotezea tu maana mapungufu yaliyopo wao wanayaona kama ni kashfa wakati mimi hapa nimeyaona kama UKWELI wa hali halisi na ipo haja kubwa ya Chadema kujiangalia upya.

Kuna watu humu wamekuwa wakiuliza kwa nini Zitto kafanya haya wakati huu?. Hili swali linachekesha kamma sii kushangaza maana waloutoa waraka huu ni viongozi wetu ambao wamekuja utoa wakati ambao chama kilitakiwa kufanya uchaguzi wa viongozi. Sasa mimi nikisema pengine wamefanya hivyo ili kuahirisha uchaguzi Je, nitakuwa nimekosea?

halafu basi nimemuuliza Nguruvi3, anionyeshe hata sehemu moja ya waraka huo ambayo inaonyesha mchango wa Zitto ktk ujenzi wa waraka ama mpango mzima. hakwana isipokuwa tunasikia toka kwa viongozi hawa hawa kuwa magazetini ya kwamba Zitto alihusika na alijua kuhusu mpango mzima na ushahidi wanao. sasa kama ushahidi mnao kwa nini mnatumia waraka ambao ni mkakati tu wa kujiandaa na uchaguzi ulotakiwa kufanyika November mwaka huo?..

Ni muda gani hawa jamaa walitakiwa kuanza kumuandaa kiongozi wanayefikiria anafaa kuchukua nafasi ya Mwenyekiti ama naibu wake? maana tunaanza na uandalizi kisha ndio inmakuja kampeni. Haiwezekani watu waanze maandalizi ya mgombea wakati wa kampeni - Haiwezekani, Kwanza nia, ari halafu tunatazama uwezo kama upo mtu anajitokeza kuchukua form. Halafu ndipo anasubiri ruksa wakati wa kampeni.

Mkuu wangu ulivyousoma waraka ndivyo nilivyoelewa mimi. Hakuna jambo baya kwa watu kupingana na uongozi unaokijenga chama kinyume vha malengo ya hadhi ya chama na Upinzani. Hadi sasa Chadema imejikita sana ktk kutafuta wanachama! CDM ni chama cha Upinzani ambacho hatua moja tu kufikia kuchukua nchi tofauti na NCCR ama CUF.. Wanachama wa nini haswa ikiwa kura za wananchi ndizo zinazokuweka IKULU?.

Uanachama ni Hiari ya mtu akipendezewa na mrengo na sera za chama anajiunga nacho, kisha atumiwe ktk michango na kazi za kujitolea ili kukijenga chama na huwezi kumfukuza bali anajitoa mwenyewe, wanayefukuzwa ni viongozi na watu walopewa mamlaka fulani sio Uanachama. Halafu leo CDM ni chama RASMI cha Upimzani (sijui kama wanaelewa uzito wa neno hili kisiasa) lakini bado tunafanya mikakati ya kukijenga chama kwa kupokonyana wananchama na CCM ya nini badala ya kuitafuta IKULU?. Hiyo CCM ilikuwa na wanachama wangapi iwe 1995, 2001, 2005 au 2010 hawafiki Mil 2 ktk nchi yenye wapiga kura Mil. 12 ila CCM inawafikia wapiga kura kwa takrima na hata kutangaza majukumu ya kiutawala kuwa ni wao tu wanaweza kufikisha kwa wananchi. Huo waraka ukiusoma kwa makini umetuchamba makalio vizuri sana kama asemavyo Mzee ES na Nyani giledi!

Halafu walivyokuwa wajanja wanaogopa kabisa kuyazungumzia yote yalokuwa ktk waraka isipokuwa wanachagua vipengele vyenye kashfa kuonyesha utovu wa nidhamu. Halafu hawa hawa wenye madai ya utovu wa ndhamu wanasema Zitto ni sehemu ya uongozi kwa nini hakuwashirikisha wengine wakati naye katukanwa!. Jamani UTOVU wa NIDHAAMU kwa VIONGOZI una maana moja tu ya kwamba wewe uko CHINI YAO. Na sijui mtu alokuwa chini ya kiongozi mwenzake ataweza vipi KUTII kwa kumwambia kiongozi wake kuwa ni fisadi na dhaifu ilihali anajua kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi. Halafu basi matusi yote alopewa Zitto ktk waraka huo huo wanazikubali, hapo hakuna utovu wa nidhamu maana Zitto ndivyo alivyo tena basi wameacha mengine ya kwamba Zitto hana hekima wala busara. Eeeeh, huu ni waraka ulo andaliwa na Zitto!.

Mimi nawaomba waniambie huyo Kitila na sii Zitto angeanza vipi ktk kikao cha chama kuzungumzia haya yote yalokuwa ktk waraka huu na viongozi hao wakayapokea kama hoja ama malalamiko yanayotakia kufanyiwa kazi. Jamani unawatuhumu viongozi wako kwa wizi na ubadhilifu, hivi utaweza vipi kuanzisha hoja hii ktk kikao cha chama?. Si watakumaliza hapo hapo kama Kolimba!

Mimi nawaomba hata mmoja wao ajitokeze hapa baada ya kuusoma waraka kisha atwambie huyo Kitila alitakiwa kusema vipi pasipo utovu wa nidhamu akiyatoa mashtaka yote haya mbele ya kamati kuu. Hata siku moja ya Nyani huwezi kumpelekea nyani au ngedele wangesulubiwa kama alivyoadhirika Mnauye na swala la magamba. Kifupi kumchinja kuku uwani kwako ama kumpelekea machinjioni haibadilishi standard ya nyama. Kitila ngetuhumiwa kwa hila mbaya na utovu wa Nidhamu kama walivyotuhumiwa sasa hivi. Tuliyaona kwa Kafulila na wengine ambao hawakufanya siri japo kweli walikuwa na makosa. Hivyo vikao sio suluhisho bali ni utaratibu wenye kuhodhi nidhamu ya woga!

Mimi nitaendelea kuamini kwamba Zitto amechomolewa kwa sababu hatakiwi tu. Hakuna ushahidi wowote unaonionyesha kwamba Zitto alikuwa na mpango wa kupindua chama bali kuna kundi la kina Kitila ambao waliona udhaifu wa viongozi wetu ma walitaka kufanya mageuzi (change) ya uongozi ambao utazingatia zaidi uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Aidha Mbowe na Dr.Slaa kweli wana mapungufu hayo mimi sijui lakini nina hakika Kitila anaelewa zaidi yetu sote.
 
Last edited by a moderator:
With a light touch!

Lengo la waraka ule ni ku address some serious issues na kuweka uongozi capable wa kuchukulia ikulu 2015.
Bila shaka kwa uongozi capable lengo la waraka ni moja tu, uongozi wa Zitto Kabwe! Bila Zitto sahau Ikulu.
Baada ya hili kushindikana, amekuwa mkweli kabisa na kwanza kusema, kama bado mnaitumainia Chadema hii hii inayokwenda kumfukuza Zitto, then kwa 2015, hakuna kitu!.
Kwa hiyo Zitto si wa kuguswa! Kwa Kitila, kumgusa Zitto, Chadema imejichimbia kaburi na kuzika matumaini ya wanachama wake.
Watu serious wote wameisha jua kwa uchaguzi wa 2015, Chadema iliyopo as it is now, minus Zitto, ni hakuna kitu!.
Watu wote serious wanajua kuwa bila Zitto, Chadema si lolote si chochote. Chadema haiwezekani bila Zitto!
Ameshauri tupate chama kingine serious cha upinzani cha kuingoa CCM madarakani na sio Chadema!.
Eti kwa Chama chochote serious cha upinzani ili kiweze kuing'oa CCM madarakani, Zitto anahitajika!

Ha, ha, haa Pasco, can you see how ridiculous all this sounds? Kweli akutukanaye, hakuchagulii tusi.
 
Nguruvi3,

Siku zote nimekua nikitaka kuchangia hii mada nakwama. Nakwama sababu ni na mengi ya kusema na ningependa niyaseme kwa mpangilio bila kuacha kipengele ambacho kwangu naona ni muhimu kuelezea mtazamo wangu, na muhimu zaidi ni mimi kupaswa kusoma hoja za wadau humu ambazo ninaamini sana zipo enlightening... Hili linaweza hata kunisaidia kuepuka kuzungumza hoja ambayo imeshajadiliwa na hivyo kuturudisha nyuma bila sababu za msingi.

Kwa haraka naweza changia mtazamo wangu juu ya swali lako hili ingawa lipo Directed kwa Pasco.

Swali lako la "Je njia zilizotumika za ule waraka zilikuwa sahihi?" Jibu linategemea unatumia vigezo vipi kuelewa malengo ya waraka (bila kuangalia nani kauandika); bali kwa kuzingatia nia ya waraka wenyewe.

1. Tukifuata What is right and wrong, njia zilizotumiwa waraka si sahihi; ndiyo jibu linalotakiwa na linatolewa Universally na wengi hasa ambao ni devoted na CHADEMA, iwe wanachama, wanaharakati ama viongozi wa Chama.

2. Tukifuata hali halisi njia zilizotumika kuandaa huo waraka zinajitetea tokana na Utendaji, Reactions na misimamo ya Viongozi wa Chadema; Kwa nini?

- Ukiusoma huo Waraka unatoka picha kuwa Viongozi wa juu wa Chama hawataki kupokea mawazo yoyote yale ambayo yapo kinyume na msimamo/mtazamo wao. Viongozi wa juu (Namaanisha Mbowe & Slaa plus) wanachukuliwa kama wao si watu wa kukosea bali wengine.

- Ukiusoma waraka unakuta kuna baadhi ya shutuma ambazo zimelengwa kwa baadhi ya Viongozi ambao ni msingi ndani ya Chama; Kiongozi yeyote anae fanya vitu kinyume na taratibu hawezi kukubali kuwa exposed ama kujadiliwa na Viongozi & Wajumbe. Ikiwa ana nguvu ya kuzuia hilo atajitahidi kwa namna yoyote. Take note Shutuma hizo hadi dakika hii nyingine hazijagusiwa kabisa.

- Tokana na Activities za kichama na Viongozi wa Chama wa Chadema inaonyesha wazi kuwa hawajajipanga na kuna mvurugano wa hali ya juu. Hiyo ni kioo kuwa kuna uwezekano mkubwa uongozi ni mbovu na umeshindwa kukiendesha chama na kujijenga badala yake kipo Pilot mode ya kubomoa. Just imagine taasisi kubwa kama Chadema ipange kikao cha Kamati kuu then isitishe kikao baada ya mahakama kusitisha ZZK kujadiliwa. Nguruvi kuwa Chadema hawana agenda nyingine kabisa zaidi ya Zitto?

- Kitila Mkumbo anaweza kuwa considered kuwa ni msaliti kwa baadhi hadi dakika hii; ila hilo haliepushi ukweli kuwa kwa kiasi kikubwa alikua akifahamika na kuheshimika kwa uwezo wake wa kupambanua issues za msingi, na alikua aki portray ni mtu ambae anajua ni nini anafaya. Hili lilinifanya niwashangae sana Viongozi wakubwa wa Chadema walipofanya maamuzi ya haraka ya kwenda public badala ya kukaa na akina Kitila kutafuta tatizo na kulitatua.

Naomba niwe wazi kuwa bado inanishangaza mijadala inayoendelea kujadili uwepo wa Zitto Chadema, na ile yote ambayo bado inajadili kama abaki ama atoke. Sijui wenzangu wanalitazama vipi, ila so far mtazamo wangu ni kuwa haijalishi... Chadema wajipange (Ni suala ambalo wamekua wakiambiwa toka kitambo hivyo kuniaminisha kua wamesha chemka; kujipanga kunawashinda). Waache kutumia nguvu nyingi na kupoteza mda kwa ku concetrate on Zitto. Mana imeshakuwa wazi jitihada, nguvu na malengo ya Zitto so far ni 'One man Army'; ana strategies za msingi ila zote zilizolenga kwa manufaa yake mwenyewe, na watu anao wawakilisha lakini siyo Chadema at large. For ni wazi hakuna uwezekano huo tena.

Zitto in Chadema ama out of Chadema haina maana tena kwa misingi kuwa (a) Akirudi, hakuna namna yoyote ile kuwa mambo yataka sawa na wote watakuwa kama wamoja kujenga Chama ama kuweza kufikia goal moja kama chama. Ikiwa tu kabla ya all these 'exposee' hawakuwa wamoja; seuzi leo hii? (b) Zitto nje ya Chadema ni sawa tu na Zitto akiendelea kuwa ndani ya Chadema. (Hapa nazungumzia kwa maslahi ya Chama cha Demokrasia as a whole na si ile ya Ego's za nani zaidi ndani ya Chama). Chadema waacha kufikiria in terms of people, wafikirie in terms of an Institution.

Nimekusoma katika post nyingi rafiki yangu, na namna ambavyo naona (maybe am wrong mana sijasoma post zote); inakua kana kwamba umeelemea kuangalia one side of the coin (makosa ya akina Kitila Mkumbo katika kuuandaa huo waraka). Msingi hapa mie naona ni kuutazama Waraka wenyewe kipengele kwa kipengele, kutazama nyenendo za viongozi waliokua wamelengwa (na hata kwenda beyond kwa wale ambao hawajatajwa). Iangaliwe content ya waraka, 'is it valid?' then vitu kama sababu za uandalizi ni rahisi to determine sababu zilizo nyuma ya pazia.

Hayo ni yangu kwa uchache.
 
Pasco,
Thanks yaani sijui kama hawa wanajisoma vizuri na kisha kulinganisha hoja zao na waraka wenyewe ama wanapotezea tu maana mapungufu yaliyopo wao wanayaona kama ni kashfa wakati mimi hapa nimeyaona kama UKWELI wa hali halisi na ipo haja kubwa ya Chadema kujiangalia upya.

Kuna watu humu wamekuwa wakiuliza kwa nini Zitto kafanya haya wakati huu?. Hili swali linachekesha kamma sii kushangaza maana waloutoa waraka huu ni viongozi wetu ambao wamekuja utoa wakati ambao chama kilitakiwa kufanya uchaguzi wa viongozi. Sasa mimi nikisema pengine wamefanya hivyo ili kuahirisha uchaguzi Je, nitakuwa nimekosea?

halafu basi nimemuuliza Nguruvi3, anionyeshe hata sehemu moja ya waraka huo ambayo inaonyesha mchango wa Zitto ktk ujenzi wa waraka ama mpango mzima. hakwana isipokuwa tunasikia toka kwa viongozi hawa hawa kuwa magazetini ya kwamba Zitto alihusika na alijua kuhusu mpango mzima na ushahidi wanao. sasa kama ushahidi mnao kwa nini mnatumia waraka ambao ni mkakati tu wa kujiandaa na uchaguzi ulotakiwa kufanyika November mwaka huo?..

Ni muda gani hawa jamaa walitakiwa kuanza kumuandaa kiongozi wanayefikiria anafaa kuchukua nafasi ya Mwenyekiti ama naibu wake? maana tunaanza na uandalizi kisha ndio inmakuja kampeni. Haiwezekani watu waanze maandalizi ya mgombea wakati wa kampeni - Haiwezekani, Kwanza nia, ari halafu tunatazama uwezo kama upo mtu anajitokeza kuchukua form. Halafu ndipo anasubiri ruksa wakati wa kampeni.

Mkuu wangu ulivyousoma waraka ndivyo nilivyoelewa mimi. Hakuna jambo baya kwa watu kupingana na uongozi unaokijenga chama kinyume vha malengo ya hadhi ya chama na Upinzani. Hadi sasa Chadema imejikita sana ktk kutafuta wanachama! CDM ni chama cha Upinzani ambacho hatua moja tu kufikia kuchukua nchi tofauti na NCCR ama CUF.. Wanachama wa nini haswa ikiwa kura za wananchi ndizo zinazokuweka IKULU?.

Uanachama ni Hiari ya mtu akipendezewa na mrengo na sera za chama anajiunga nacho, kisha atumiwe ktk michango na kazi za kujitolea ili kukijenga chama na huwezi kumfukuza bali anajitoa mwenyewe, wanayefukuzwa ni viongozi na watu walopewa mamlaka fulani sio Uanachama. Halafu leo CDM ni chama RASMI cha Upimzani (sijui kama wanaelewa uzito wa neno hili kisiasa) lakini bado tunafanya mikakati ya kukijenga chama kwa kupokonyana wananchama na CCM ya nini badala ya kuitafuta IKULU?. Hiyo CCM ilikuwa na wanachama wangapi iwe 1995, 2001, 2005 au 2010 hawafiki Mil 2 ktk nchi yenye wapiga kura Mil. 12 ila CCM inawafikia wapiga kura kwa takrima na hata kutangaza majukumu ya kiutawala kuwa ni wao tu wanaweza kufikisha kwa wananchi. Huo waraka ukiusoma kwa makini umetuchamba makalio vizuri sana kama asemavyo Mzee ES na Nyani giledi!

Halafu walivyokuwa wajanja wanaogopa kabisa kuyazungumzia yote yalokuwa ktk waraka isipokuwa wanachagua vipengele vyenye kashfa kuonyesha utovu wa nidhamu. Halafu hawa hawa wenye madai ya utovu wa ndhamu wanasema Zitto ni sehemu ya uongozi kwa nini hakuwashirikisha wengine wakati naye katukanwa!. Jamani UTOVU wa NIDHAAMU kwa VIONGOZI una maana moja tu ya kwamba wewe uko CHINI YAO. Na sijui mtu alokuwa chini ya kiongozi mwenzake ataweza vipi KUTII kwa kumwambia kiongozi wake kuwa ni fisadi na dhaifu ilihali anajua kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi. Halafu basi matusi yote alopewa Zitto ktk waraka huo huo wanazikubali, hapo hakuna utovu wa nidhamu maana Zitto ndivyo alivyo tena basi wameacha mengine ya kwamba Zitto hana hekima wala busara. Eeeeh, huu ni waraka ulo andaliwa na Zitto!.

Mimi nawaomba waniambie huyo Kitila na sii Zitto angeanza vipi ktk kikao cha chama kuzungumzia haya yote yalokuwa ktk waraka huu na viongozi hao wakayapokea kama hoja ama malalamiko yanayotakia kufanyiwa kazi. Jamani unawatuhumu viongozi wako kwa wizi na ubadhilifu, hivi utaweza vipi kuanzisha hoja hii ktk kikao cha chama?. Si watakumaliza hapo hapo kama Kolimba!

Mimi nawaomba hata mmoja wao ajitokeze hapa baada ya kuusoma waraka kisha atwambie huyo Kitila alitakiwa kusema vipi pasipo utovu wa nidhamu akiyatoa mashtaka yote haya mbele ya kamati kuu. Hata siku moja ya Nyani huwezi kumpelekea nyani au ngedele wangesulubiwa kama alivyoadhirika Mnauye na swala la magamba. Kifupi kumchinja kuku uwani kwako ama kumpelekea machinjioni haibadilishi standard ya nyama. Kitila ngetuhumiwa kwa hila mbaya na utovu wa Nidhamu kama walivyotuhumiwa sasa hivi. Tuliyaona kwa Kafulila na wengine ambao hawakufanya siri japo kweli walikuwa na makosa. Hivyo vikao sio suluhisho bali ni utaratibu wenye kuhodhi nidhamu ya woga!

Mimi nitaendelea kuamini kwamba Zitto amechomolewa kwa sababu hatakiwi tu. Hakuna ushahidi wowote unaonionyesha kwamba Zitto alikuwa na mpango wa kupindua chama bali kuna kundi la kina Kitila ambao waliona udhaifu wa viongozi wetu ma walitaka kufanya mageuzi (change) ya uongozi ambao utazingatia zaidi uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Aidha Mbowe na Dr.Slaa kweli wana mapungufu hayo mimi sijui lakini nina hakika Kitila anaelewa zaidi yetu sote.

Mkandara umenena sina hata la kuongeza,kweli kama kutukwana hata Zitto katukwana na Waraka"Ukweli ni Kama nyota gizani"
 
Last edited by a moderator:
Iangaliwe content ya waraka, 'is it valid?' then vitu kama sababu za uandalizi ni rahisi to determine sababu zilizo nyuma ya pazia.

Asante sana Dada AshaDii, leo nimeona mchango "neutral" usioushabikia upande. Hakika nimetumia muda kusoma post yako hadi chungu kikaungua (don't be gender-sensitive).
Wengi wetu kwenye huu uzi wanzungusha maneno lakini wako biased; nilishamweleza Mkuu Nguruvi3 juu ya hili mwanzoni nilipochangia na ligi yao na Bob Mkandara haitapata mshindi kwani wote mitazamo yao katika hili ni tofauti kabisa. Nafurahi Kaka Pasco wa JF kwani yeye tangia mwanzo anarusha mawe bila kupepesa macho, shikilia hapo hapo.

Kwa uzoefu mdogo nilionao katika uongozi wa taasisi, kuna vitu viwili; "growing pains" na "founder member syndrome" na haya yote yamrjionyesha katika ukuaji wa vyama vya siasa katika miaka 20 iliyopita.
Sitopenda kurudia magumu waliyoyapitia vyama hivi hadi kufika hapa walipo, na wote tunajua wale walishindwa kuhimili misukosuko, vyama vimebakia kwenye makaratasi bila kuwa na impact yoyote kwenye jamii wanayodai kuiwakilisha.

Hili la "founder member syndrome" ndio tatizo kubwa kwa sasa. Waanzilishi wa taasisi hizi walikuwa na vision yao juu ya wanakotaka kuelekea, wame-sacrifice muda na mali katika ujenzi wa taasisi hizi na inakuwa vigumu sana kukubali wanachama waliokuja juzijuzi kujaribu kushawishi juu ya mwenendo wa taasisi "zao", na "TRESHOLD" iko hapa.
 
Mkuu wangu nikwambie kitu.

Kama Viongozi wa Chadema wangetumia ushahidi wa kuhusika kwa Zitto kufanya Mapinduzi ya uongozi na kukiua chama ningemrushia madongo kisawa sawa lakini kutumia huu waraka ambao kila naposoma sioni kabisa mahala Zitto amehusika kuutunga ama kuuandaa hapo ndipo naposhindwa Uzalendo.

Halafu basi kama alivyosema AshaDii inategemea mtu unautazama vipi huu waraka maana ni rahisi kusema njia walotumia haikuwa halali. Mimi nimewahi kufuatilia sana msuguano wa Mbowe na Zitto toka zamani na naelewa makosa yako wapi na kilichofanyika. Wengi wanasoma tu humu JF na kua na judgement zao lakini Zitto amejaribu sana KUAMINIWA lakini haikuwezekana. Na hasira zake za kutoaminika ndizo zilizomsukuma kuwa na jeuri. nadhani umewahi kunisoma ktk Ushauri wangu kwa Zitto nilouweka humu JF na hii ni baada ya kufanya utafiti wangu ninafsi.

Mimi sidhani kama Uadui upo baina ya Mbowe na Zitto isipokuwa hawa watu wamechezewa ule mchezo wa kitoto wa PUTA, kwanza unaambiwa PUTA kisha vuka msitari, ukivuka tu jamaa wa upande wa pili anaambiwa duh jamaa kakutukania mama yako! - hapo hakuna salama tena Ngumi za kuua mtu zinaanza!..

Kwa maana hiyo kuvuka msitari ni kumvunjia mtu heshima na unapoputa unataka ushindani halali lakini kwa walio andaa wanataka results tofauti maana kinachopelekwa upande wa pili ni tofauti kabisa - Kakutukania mama yako! inakuwa sii mchezo tena ila ngumi za ukweli.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom