Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

@Mag3,pana post yako hapo nyuma ulifafanua swala la Fact checks na ukatolea mfano wa swala la vita ya Iraq,swala hilo nimeliona limeibuka na bahati nzuri sana Analyst wa CNN kaligundua na kamuumbua Trump.
Big up sana Mag3 na @Nguruvi3,mlichopredict Ndio exactly kimetokea kwenye Mdahalo wa leo,imebidi nirudi nyuma kusoma analysis zenu tena na nimebaki kushangaa,as if you knew exactly what is going to happen [emoji119][emoji119]
 
Ha haa haaaa!! Nimeangalia mdahalo mpaka nimejikuta namuonea huruma bi clinton. Trump akiwa anaongea anajiamini sana,anaongea hana pressure kabisa mpaka anavutia..!! Ngoja nisubiri tathimini ya nguruvi3.

Ha ha ha magode really,au unaamua tu kutufurahisha,ki ukweli sikutegemea sana Trump kufanya vizuri katika mdahalo huu,lakini pia sikutatajia kama angefanya VIBAYA KIASI HIKI.GOP hapa walichemka big tyme na najua wanajuta kupoteza miaka mingine tena 4
 
Kwa mujibu wa CNN Clinton kafanya vizuri kwenye mdahalo huu, kura zinaonyesha ni 62% kwa 27%, na hata kuhusu sera za nche naona Mwanamama Hillary alijipanga, Trump kwa mdhalo huu kdg kayumba kwa maoni yangu inabidi midahalo miwili ijayo ajipange sana.

Clinton sio mzuri sana kwa hoja, ila udhaifu wa Trump naona umempa ahueni na kumfanya aonekane ni bora zaidi, maanaTrump anaonekana facts zinasumbua anakuwa kama hayuko well informed
 
Haaa haaa ukisikia mahaba ndio hayo🙂.
Mkuu usuwaamini sana CNN HC ni mgombea wa mainstream media na CNN ni member wa mainstream media. Subiri tathimini ktk vyanzo vingine baada ya leo..!! Hao akina Mag3 ni team HC..umeziona coment alizoweka mag3 za tweeter?? Hivi unategemea mtu wa clinton ataandika nini!!? Km ni suala la kushangilia wakati wa mdahalo lipo wazi,wafuasi wa HC walikuwa 73% na wa DT walikuwa 27%. Lkn mdahalo umefuatiliwa na zaidi ya watu milioni 100. Hiyo tathimini ya baada tu ya mdahalo CNN wameifanyia wapi!!??
 
TATHMINI YA MDAHALO (I)

Mdahalo wa jana umetupa mwanga wenzetu wanavyofanya vetting ya viongozi

Hillary Clinton alichukua wiki kujiandaa, Trump alichukua siku mbili

Kama mtakumbuka, tulisema mdahalo wa Urais ngazi iliyopo si na primaries.

Kwa Republican walikuwepo wagombea zaidi ya 10 katika primaries
Mdahalo kwa sehemu kubwa ulikuwa unavurgwa kwa kila mmoja kuingilia

Jana ilikuwa tofauti na ilionyesha;
Kwamba, ngazi ya Urais mgombea lazima ajiandae

Trump kutofanya maandalizi kumemgharimu katika mdahalo.

Dakika 30 za mwanzo. Kauli za kufungua mdahalo zilionyesha Clinton akizungumzia suala la uchumi kwa upana wake.

Trump akahamisha suala na kuingiza hoja za biashara na mkataba wa TPP. Ilikuwa ni move nzuri sana kwani alimweka Clinton katika kujilinda

Clinton akatumia uzoefu wa mijadala kuhakikisha anamtibuaTrump wakati yeye akieleza sera zake. Trump akaingia katika mtego

Hoja iliyomtibua Trump ni suala la kodi. Kama tulivyosema, Trump alikwenda akiwa amejifunza na si kujiandaa kuhusu hoja.

Clinton alifanya homework ya kujua IRS hawana katazo la kuonyesha ''tax file'' wakati mteja akikaguliwa. Hoja ya Trump kuwa yupo katika audit ikafa.

Trump akasema ataonyesha kodi Clinton akitoa emails.

Ni kuanzia hapo, Trump akapoteza pumzi na uelekeo na dakika 60 zilizobaki akawa vulnerable kwa mambo mengi.

Inaendelea
 
MDAHALO (II)

Baada ya kumjaza jazba na kupoteza uelekeo, HC aka control ya mjadala
Hata pale Trump alipopaswa kumweka katika kona, alishindwa

Mbinu za Trump za kushambulia personality zilishindikana.
HC alikuwa mtulivu, na wapo 2,DT hakukufanya 'bullying' alizofanyia GOP

Trump aliingilia 'interrupts' mara 31 wakati Clinton anaongea.

Hili likajenga hoja ya 'temperament' ambayo HC ameitumia dhidi yake

HC alitumia fursa ya kuingiza hoja zake.
Trump alipoongelea suala la biashara, HC alimvuta kuongelea utajiri.

Trump akavutika, na hapo akashambuliwa kwa mambo mengi

Kwanza, kuonyesha Trump anataka Urais kwa model ya business zake

Alionyesha kuwa kuendesha uchumi katika siasa na biashara ni vitu tofauti

Pili, akaeleza jinsi Trump alivyofilisika katika vipindi kadhaa

Tatu, akachomeka suala la ubaguzi 'race' lililofanywa na Trump miaka mingi

DT alikiri na kusema makampuni mengi yalishtakiwa, alimaliza kesi bila kulipa

Hapa alikubali ubaguzi, hata kama kesi iliisha.
Akiwa na tatizo na watu wa rangi, hoja hii haikumsaidia

Ilipokuja suala la 'race' tayari alishajiweka katika nafasi ngumu.
Hakueleza 'law and order' inawezaje kuleta maalewano.

DT alitoa takwimu kuhusu uhalifu New York, wachambuzi wanasema, uhalifu unapungua si kama alivyosema

Aliongelea sana kuhusu Chicago na mauaji, HC akamchonganisha na weusi kwa kusema yapo mengi mazuri na si uhalifu tu kama DT anavyosema.

Hii hoja itatia katika fikra za weusi na itamsumbua DT kwa muda

Ilipounganishwa na hoja ya cheti cha kuazaliwa cha Obama, picha iliyoonekana ni mtu mwenye ubaguzi. Je, itaathiri hali ya mambo kwake?

Inaendelea..
 
MDAHALO (III)

Kuna nyakati Trump (DT) alifanya kitu kinaitwa 'unforced error'
Kwamba, hoja zilimrudi kwasababu hakuwa na maandalizi ya kukabiliana nazo

Hili lilionekana katika siasa za nje. DT aliongelea deal ya Iran kuwa ni mbovu. HC alimuuliza kama ni mbovu mbadala wake ni upi? DT Hakuwa na jibu

Unforced error nyingine ni pale aliposea HC alikuwa nyumbani wiki nzima
HC alimjibu 'ni kweli kwasababu anajiandaa kuwa Rais'

Unforced error: DT alipoulizwa kuhusu stamina ya HC
HC alimjibu kuwa 'hadi atakapotembea nchi 142 kiserikali na ku testify kwa masaa 11 mbele ya kamati, DT ndipo ataongelea stamina na DT'

HC akaingiza hoja ya Trump kuhusu suala la 'haonekani kuwa Rais' na kulihusisha na mwanamke (Alicia Machado) aliyekuwa abused na DT kwa kutumia wingi wa Latino. Akasema mama huyo ata vote Dcember!

Unforced error: DT aliongelea NATO na ulipaji wa ada
HC alizungumzia kwa ujumla na kuwahakikishia washirika msimamo wake
Aliongea katika kile kinachoitwa 'presidential'

Unforced error: DT alizungumzia ubovu wa miundo mbinu kama viwanja
HC akaliunganisha na ulipaji kodi, kwamba ni mibaya kwasababu watu kama DT hawalipi kodi. DT akalazimika kuliacha

Hizi unforced error si kuwa ni hoja za makosa, bali hoja zinazomtia mtu kitanzi yeye mwenyewe. Kilichotakiwa kwa DT ni kufafanua kwa sera

Kwahiyo unaweza kuona DT alikuwa na hoja katika mistari, hakuwa na details
Maandalizi ya HC kwa kuangalia mikanda ya video vilimsaidia sana
Kuna nayakati alikuwa na majibu mafupi lakini yenye mantiki

Trump akiwa 'spinning room'

Inaendelea
 
MDAHALO (IV)

Ikumbukwe katika mdahalo wagombea walipewa tiketi sawa za kualika watu wao. Halafu zipo zilizotolewa na kamati ya midahalo ya Urais, na mwisho za wenye ukumbi wa Chuo kikuu

Nyuma ya ukumbi kuna vyumba,wagombea kuongea na waandishi habari.
Vinaitwa 'spin room', wapiga debe huweka sawa kauli za wagombea

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, DT alikwenda mwenyewe ''spin room''
Huko alieleza mengi na kumshambulia moderator kwa kuegemea upande HC

Alilamikia microphone kutokuwa katika hali nzuri

DT anauliza mbona suala la email, kashfa za Benghaz na FBI halikuulizwa?

Suala la email liliulizwa, HC alilijibu kwa ufupi kwa kukiri makosa.

Kwavile DT hana uzoefu au hakujiandaa, alishindwa kuliunganisha na masuala mengi ikiwemo Benghaz na FBI. Kumlaumu mchokoza mada si sahihi

DT ana dhima ya kulirefusha suala,alidhani HC kukiri inatosha kumpa pointi.

Mwaka 2008 Obama alimtuhumu HC kwa vita ya Iraq, na kila mara ali 'invoke' kifundi kwasababu ilikuwa 'selling point yake' hakusubiri mchokoza mada.

Na hapo ndipo DT alipokuwa vulnerable

Hii ina ukweli kuwa katika primairies aliokolewa na mijadala nje ya hoja.

Hivyo, uwezo wake wa kuingiza hoja(kuchomekea) ni mdogo

Je, survey na fact checks zinasemaje?

Inaendelea sehemu ya mwisho
 
MDAHALO (V)

Kabla hatujasonga mbele, tunaweza kuona namna Hillary alivyokuwa amejiandaa ''flawless'' Trump akihangaika katika hoja

Kwa mfano, hoja ya ISIS iliingia, na wengi walitarajia ni sehemu kubwa ya sera za GOP na Trump angeieleza vema

Mtakumbuka tulisema baada ya mashambulio ya kigaidi, NY, NJ, MN kura za maoni zingebadilka. Ndivyo ilivyotokea siku za karibuni,Trump akiwa na momentum na Hillary akiwa hajapoteza bali haongezi

Trump akajikuta anavutika katika hoja za HC bila kutetea misimamo yake

Mwisho wa mjadala ikaulizwa, wagombea watakubali anaposhinda mwingine?

HC: Alisema demokrasia ya Marekani ni kuheshimu maamuzi ya wananchi

DT: Akaanza kuzungumzia wahamiaji 800 au 1800 kwa mujibu wake, walipewa uraia kwa makosa. Ni kweli hilo limetokea wiki chache zilizopita

Ilibidi aulizwe tena kama takubali iwapo HC atashinda, ndipo akasema 'ndiyo'

Hapa ndipo utaona DT ima hana weledi wa kutosha, hana uzoefu wa mijadala au hakujiandaa. Alipouzungumzia hoja ya ISIS ilikuwa muafaka kuchomeka suala la uraia kwa makosa! hakufanya hivyo

Matokeo yake ikaonekana kana kwamba hakuelewa swali, au amesahau alichotaka kusema kabla ya kufikia tamati.

Tofuati utaiona wakati HC alipoingiza hoja ya nyuklia na kumhusisha na DT kwamba mikono ile haifai kushika nuclear code.

Hakukuwa na swali lakini wenyewe wanasema ali 'invoke' kwa maana kuchomekea

Itaendelea mwisho
 
REALITY CHECK(RC)

Wataalam na wachambuzi wa vyombo mbali mbali wamepitia kauli za wagombea kubaini ukweli au uongo

DT: Hillary aliunga mkono mkataba wa biashara unaoujulikana kama TPP
HC: Hakusema ni golden std, bali aliunga mkono mkataba huo
RC: Ni kweli alisema mkataba huo ulikuwa golden std

DT: Obama/Hillary waliondoa majeshi mapema Iraq na kupelekea ISIS
HC: Aliyeandaa mpango wa kuondoa majeshi alikuwa George Bush
RC: Ni kweli mpango huo ulikuwepo Obama akiingia oval ofisi

DT: Clinton hakushughulikia ISIS maisha yake yote na miaka 30 kazini
HC: Alishiriki kukabiliana na ISIS ikiwemo kumuondoa Osama
RC: ISIS haikuwepo miaka 10 iliyopita, madai ya Trump si kweli

HC: Trump alipewa pesa na baba yake kama mtaji kama milioni 14
DT: Alipokea $1 M kutoka kwa baba yake
RC: Alirithi pesa na mali za baba yake pia

HC: Clinton hakubaliani na climate change akisema ni uzushi wa china
DT: Akanusha hakusema hivyo
RC: Mwaka 2012 DT ali tweet kuhusiana na climate change na China

DT: Utajiri wake ni takribani Bilioni 10
RC: Kwa mujibu wa Forbes, utajiri ni 4.5 Bilion

DT: Mauji katika mji wa NY yameongezeka baada kusitishwa'stop & frisk'
HC: Mauaji yamepungua, na stop and frisk ilikuwa na ubaguzi
RC: Kwa takwimu za 2015 mauaji yamepungua 4% ingawa yaliongezeka 2014

Inaendelea...
 
NANI ALISHINDA MDAHALO?
Kwa vigezo vyote na maoni ynayoendelea kutolewa Clinton alikuwa mshindi
Kwanza, alifanikiwa kutengeneza kesi ya Trump ya 'abuser, liar and racist'

Alionyesha abuse kwa wanawake(Machado),alivyowadhulumu wafanyakazi

HC akaonyesha alivyo muongo si kwa suala la kodi bali mengi

Aakatumbukiza suala la race ambalo alifanikiwa kumweka DT on defense

HC alikuwa na details nyingi na well informed kuhusu mambo ya dunia

Tatizo
HC alishindwa kutumia fursa kuonyesha udhaifu wa DT kimataifa kitaifa.

Hili linatokana na HC kuwa 'too presidential'

Aliongea kama Rais wa nchi wakati ni kipindi cha kuomba kura
Hakuweza kufanya effective connections kati yake na average person

Trump aliongelea biashara iliyoathiri battle states za Michagan na Pennsylvanian.
HC anaweza kuwafikia wengi, je 'needle will move?'' Penny na Michigan?

Advantage ya kuwa presidential ni alipowahikikishia 'allies' hasa wa NATO kuhusu msimamo 'wa USA' kwa mtazamo wake. DT alioonekana out of touch, foreign affairs

Kwa Trump, kitendo cha kurudia kauli ya 'umefanya hivyo miaka 30 mara nyingi' kimelenga kuonyesha HC ni status quo.

Kwa sehemu ya jamii inayohitaji mabadiliko hii ilikuwa 'selling' point kubwa

Mdahalo hautakuwa na impact mara moja, uta expose weakness and strength
Independents wataamua lakini pia watu wa rangi na jinsia ni factor

Kwa HC watu wa Bernie Sanders (millennial) bado hajaweza kuwaridhisha
Inapofanyika kura ya 'three way' wakijumuisha Johnson, HC anapoteza point

Hii maana yake millennial wa Sander wanakwenda kwa Johnson
Ni tatizo kubwa kwa HC, lazima atafute namna ya kuhamasisha

Baada ya mdahalo ambao DT amefanya vibaya, ndio mwisho?
Jibu ni hapana, ipo mijadala 2 zaidi inayokuja

Historia inaonyesha Reagan alivurunda wa kwanza,wa pili akaende WH.
2012 Obama alivuruga wa kwanza, wapili ukamrudisha

Trump bado yupo na kampeni bado ni ngumu.

Kitakachojitokeza atakuwa nervous kwa maana ya kupoteza confidence na anaweza kwenda kivyake zaidi na si kwa ushauri na kupotea zaidi

Tusemezane
 
Meet Trump’s Polling Truthers Who Say the Numbers Are Lies...
Donald Trump is trailing badly in the polls, but not according to his most ardent fans who see the polls as just another tool of the liberal, lying media.


A fake PPP poll shows Trump beating Hillary in Florida by a margin of 74-9. Obviously the first REAL UNSKEWED POLL of the election! Visit: www.longroom.com


49048906.cached.jpg


Bill Mitchell - Trump for President!
Every four years amid the presidential election, another kind of popularity contest gets underway, one that selects the new members of the professional peanut gallery of pundits, writers, and (in the modern era, anyway) social media stars who, through persistence or dumb luck, find themselves in the odd and delicate position of influencing the public discourse. And with all of its idiosyncrasies, 2016 has ushered in a new kind of thought leader to the mainstream: the polling truther.

By Bill Mitchell’s account, this campaign season has been good for Bill Mitchell—and he hasn’t even had to leave the comfort of his home. Mitchell, who is 56 years old, is a resident of Charlotte, North Carolina. He looks like a real-estate agent from Mars with his gleaming silver hair, bushy black eyebrows, and unusually youthful face. An executive recruiter by trade, it’s his hobby of internet trolling that has turned him into an unlikely conservative star.

In the last year, Mitchell has amassed a following of tens of thousands of Twitter followers, nearly 70,000 and counting, who come for his insistence that, despite what nearly every poll says, Donald Trump will be elected president of the United States. And as of two months ago, he’s taking his message outside of social media, to online radio with a show on YourVoiceRadio.com, which he says has as many as several thousand listeners per episode.

According to Mitchell, and to the thousands of Trump supporters who hang on his words, mainstream polling is skewed to disenfranchise the “silent majority” of Americans who favor the Republican nominee’s ideas.

For proof that it’s all made up, Mitchell says you don’t have to look further than the size of the crowds each candidate commands. While Trump fills stadiums designed for monster truck rallies and rock concerts, Clinton tends to address audiences of a more modest size. A beltway pundit might call that an enthusiasm gap or simply a matter of staging, but Mitchell calls it a conspiracy.
 
Lkn mdahalo umefuatiliwa na zaidi ya watu milioni 100. Hiyo tathimini ya baada tu ya mdahalo CNN wameifanyia wapi!!??
Hapa naomba nitoke kidogo nje ya mjadala. Kwa kadri unavyoona wenzetu wanavyofanya mambo, ndivyo wanavyofanya kila eneo la maisha.
Kwa mfano, leo nimeona wataalam wa 'Body movement'

Wataalam hawa hutumiwa katika maeneo ya 'forensic' kama interrogation n.k. Wataalam wanaweza kujua position gani na ina maanisha nini. Jana wanasema Trump alikunywa maji mara 11 , Clinton 0 wakisema hiyo ilikuwa dalili ya nervousness kwa Trump. Wakaeleza kuanzia wanashikana mikono, wanajadiliana wanabishana n.k. Wataalam wameonyesha kila mmoja na jinsi alivyokuwa katika nyakati tofauti

Ndivyo ilivyokuwa katika kujua rating ya viewers. Kuanzia Jumamosi ilikadiriwa kutakuwa na watazamaji 75Milioni kwa television ''8'' zilizopewa right ya moja kwa moja.

Leo takwimu zimetoka idadi ni 84+Milioni. Rating ya TV haihitaji rocket science, in fact inafanyika automatic.Wanaweza ku break down kila TV , program na idadi ya viewers.
 
Hapa naomba nitoke kidogo nje ya mjadala. Kwa kadri unavyoona wenzetu wanavyofanya mambo, ndivyo wanavyofanya kila eneo la maisha.
Kwa mfano, leo nimeona wataalam wa 'Body movement'

Wataalam hawa hutumiwa katika maeneo ya 'forensic' kama interrogation n.k. Wataalam wanaweza kujua position gani na ina maanisha nini. Jana wanasema Trump alikunywa maji mara 11 , Clinton 0 wakisema hiyo ilikuwa dalili ya nervousness kwa Trump. Wakaeleza kuanzia wanashikana mikono, wanajadiliana wanabishana n.k. Wataalam wameonyesha kila mmoja na jinsi alivyokuwa katika nyakati tofauti

Ndivyo ilivyokuwa katika kujua rating ya viewers. Kuanzia Jumamosi ilikadiriwa kutakuwa na watazamaji 75Milioni kwa television ''8'' zilizopewa right ya moja kwa moja.

Leo takwimu zimetoka idadi ni 84+Milioni. Rating ya TV haihitaji rocket science, in fact inafanyika automatic.Wanaweza ku break down kila TV , program na idadi ya viewers.
Mkuu nguruvi3 kwanza sina tatizo na hiyo namba 84mil.+ ukishaweka hiyo + hakuna hoja tena hapo. Kwa uelewa wangu wanachoweza ku-break down ni idadi ya tv na kuweka wastani wa watazamaji kwa kila tv,kwa sababu ni ngumu kujua kila tv ilikuwa na watazamaji wangapi,ndo maana wameweka 84mil.+..
 
ALICIA MACHADO NA TRUMP

Mwisho wa mdahalo Trump aliulizwa kuhusu taswra ya Clinton kama Rais.
DT alijibu kuwa alichoongelea ni stamina na si taswira

Hillary Clinton akajibu kuhusu suala la stamina. Akachomeka hoja ambayo ni wazi alikuwa nayo na akisubiri muda muafaka kuisema

HC alisema tatizo la Trump kudhalilisha wanawake lipo.

Akatolea mfano wa 'Miss universe' kutoka Columbia Alicia Machado alivyo dhalilishwa na Trump baada ya kushinda taji, miss Universe ikiwa chini ya DT

Ilionekana kama Trump alitaka kukanusha, lilipotajwa jina hakukataa.
Muda wa mdahalo ulishakwisha na hakuwa na nafasi ya kujitetea

Jana Trump kaenda TV ya Fox kueleza matatizo aliyokuwa nayo na Machado.

Kwamba alikuwa 'mgumu' kikazi na aliongeza uzito takribani paundi 40.

Hilo limebadilisha maongezi. Alicia yupo katika TV kueleza alivyotendwa

Amekanusha madai ya paundi 40 akisema zilikuwa 10

Na kwamba DT alimwambia mbele ya waandishi, anakula kama mashine

Hoja hapa si nani alisema nini, bali Trump anavyoliendeleza jambo hili.

Kampeni imetafuta mazonge zonge ya siku za nyuma ya Alicia kumwonyesha ni mtu mbaya. Alicia haugombei Urais na hana cha kupoteza

Hili lina tatizo katika kampeni ya Trump.
Kwanza, linaingia katika jinsia na kupata sympathy ya wanawake.

Pili linaingia katika ''race'' kwamba ni kwasababu alikuwa Latino.

Tatu linaonyesha '' arrogance'' ya Trump kwa mtazamo huo

Katika kipindi hiki haikuwa muafaka kuwa na majadiliano na Machado.

Hili pia linatukumbusha ugomvi wa Trump na familia ya Khan

Ni jambo dogo, impact yake ni kubwa sana

Tusemezane
 
Tatizo la Trump either hana washauri wazuri au anao ila hawasikilizi na kufuata kile anachokiwaza kichwani kwake. Ukifuatilia wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa republicans unaweza kuona jinsi alivyokuwa akitupa vijembe na kejeli kwa wapinzani wake (Bush, Cruz etc) na somehow mbinu hio ikamsaidia kuungwa mkono.

Shida ni kwamba sasa hivi uwanja wa mapambano umebadilika; Sasa hivi anasimama dhidi ya mpinzani ambaye kwanza ana uzoefu wa kutosha kwenye midahalo ya aina hii (Alipambana na Obama miaka 8 iliyopita kutafuta mgombea wa democrats), pili anasimama dhidi ya mgombea ambaye ameonesha uzoefu wa kukabiliana na mishale inayorushwa upande wake bila kupoteza focus, na mwisho kabisa anasimama dhidi ya mgombea ambaye hawezi kumrushia vijembe vizito kama alivyowafanyia kina Cruz & Bush bila kumgharimu yeye mwenyewe kwamba ni "sexist" na mdhalilishaji wa kinamama! Na hapo ndipo anapokuwa na wakati mgumu na mbaya zaidi hata pale aliporushiwa tuhuma yeye akashindwa kuzijibu.

Kuelekea mdahalo wa pili Trump inabidi ajipange sawa sawa kwa kujikita kwenye hoja zaidi badala ya kutegemea vijembe maana hiyo mbinu haijamsaidia sana. Bila kubadilisha strategy atajikuta akifanya vibaya pia kwenye mdahalo wa pili na kuzidi kupigilia misumari kwenye jeneza lake na kufanya uchaguzi huu kumalizika mapema kwa first round knock out!
 
babytrump-jpg.409453

Tulia mwanangu tulia...safari bado ni ndefu!​
 
Wakuu mag3 na nguruvi3,mna maoni gani kuhusiana na kura ya turufu ya rais obama kwenye mswada wa JASTA,kukataliwa na bunge la congress,hakuna athari ya moja kwa moja kwenye uchaguzi wa november kwa wagombea hawa wanaochuana vikali!!?? Km mswada utabaki hivi na kuwa sheria,nani atanufaika kati ya Replican na Democrat na km wabunge watabatilisha uamzi wao nani atanufaika!!? Nimesoma mahali baadhi ya wabunge wa replican wameanza kujutia maamuzi yao. Hebu nipeni maoni yenu..
 
Back
Top Bottom