MDAHALO (II)
Baada ya kumjaza jazba na kupoteza uelekeo, HC aka control ya mjadala
Hata pale Trump alipopaswa kumweka katika kona, alishindwa
Mbinu za Trump za kushambulia personality zilishindikana.
HC alikuwa mtulivu, na wapo 2,DT hakukufanya 'bullying' alizofanyia GOP
Trump aliingilia 'interrupts' mara 31 wakati Clinton anaongea.
Hili likajenga hoja ya 'temperament' ambayo HC ameitumia dhidi yake
HC alitumia fursa ya kuingiza hoja zake.
Trump alipoongelea suala la biashara, HC alimvuta kuongelea utajiri.
Trump akavutika, na hapo akashambuliwa kwa mambo mengi
Kwanza, kuonyesha Trump anataka Urais kwa model ya business zake
Alionyesha kuwa kuendesha uchumi katika siasa na biashara ni vitu tofauti
Pili, akaeleza jinsi Trump alivyofilisika katika vipindi kadhaa
Tatu, akachomeka suala la ubaguzi 'race' lililofanywa na Trump miaka mingi
DT alikiri na kusema makampuni mengi yalishtakiwa, alimaliza kesi bila kulipa
Hapa alikubali ubaguzi, hata kama kesi iliisha.
Akiwa na tatizo na watu wa rangi, hoja hii haikumsaidia
Ilipokuja suala la 'race' tayari alishajiweka katika nafasi ngumu.
Hakueleza 'law and order' inawezaje kuleta maalewano.
DT alitoa takwimu kuhusu uhalifu New York, wachambuzi wanasema, uhalifu unapungua si kama alivyosema
Aliongelea sana kuhusu Chicago na mauaji, HC akamchonganisha na weusi kwa kusema yapo mengi mazuri na si uhalifu tu kama DT anavyosema.
Hii hoja itatia katika fikra za weusi na itamsumbua DT kwa muda
Ilipounganishwa na hoja ya cheti cha kuazaliwa cha Obama, picha iliyoonekana ni mtu mwenye ubaguzi. Je, itaathiri hali ya mambo kwake?
Inaendelea..