DUWASA-Dodoma punguzeni bei ya maji

DUWASA-Dodoma punguzeni bei ya maji

Wacha nao hao hiyo ni bei ndogo ya maji yaani 1500 unauziwa ndoo 50 za lita 20 kila moja
We mburula,unayosema ndogo,unalinganisha na nani na WA kipato Gani? Don't generalize issue!
 
We mburula,unayosema ndogo,unalinganisha na nani na WA kipato Gani? Don't generalize issue!
Masikini uswahilini wananunua ndoo moja ya maji kwa sh 100 hadi sh 200 kwa ndoo ya lita 20 sasa wewe huoni hiyo bei ya serikali ni chini sana au ujui hesabu..tena wananua na kuyachota kwa gharama ya mchotaji au house girl nk na gharama ya mikokoteni juu... nyinyi mna lalamikia maji ambayo unafungua bomba tu bila ya gharama ya kuyateka day by day
 
Mkuu Nina mke na watoto 3, ninanunua maji Kwa dumu la Lita 20 Kwa sh 500 ,ninalipa bill ya umeme Kwa mwezi sh 18000 ,sijawahi lia lia mtandaoni,wewe mzembe tu
Shida Yako unajifikiria wewe tuu,ninapotoa mada,naangalia na wengine,ndivyo nilivyofundishwa Toka utoto,usijedhani Nina shida ya hizo habari mkuu, nenda taratibu!
 
Kwa taarifa yako unit moja ni sawa na ndio 50 za lita ishirini na unachajiwa kwa 1500/=.....ulitaka upewe maji bure ????....Sasa ukae kwa kutulia zinakuja mita za pre-paid hapo ndio utahamia HOMBOLO ukatumie maji ya bwawani.
Sawa,itapendeza mkuu!
 
Masikini uswahilini wananunua ndoo moja ya maji kwa sh 100 hadi sh 200 kwa ndoo ya lita 20 sasa wewe huoni hiyo bei ya serikali ni chini sana au ujui hesabu..tena wananua na kuyachota kwa gharama ya mchotaji au house girl nk na gharama ya monotonic juu nyinyi mna lalamikia maji ambayo unafungua bomba tu bila ya gharama ya kuyateka day by day
Utakuwa Anduje,si kwa misifa hii!
 
Shida Yako unajifikiria wewe tuu,ninapotoa mada,naangalia na wengine,ndivyo nilivyofundishwa Toka utoto,usijedhani Nina shida ya hizo habari mkuu, nenda taratibu!
Watu Gani unawaongelea wewe,kama unalalama juu ya maji ya Bomba vipi sisi tunaotumia maji ya kwenye vidumu,ulitakiwa kama kweli unawasemeq watu ungeongelea sisi tunaotumia maji ya vidumu
 
Kama elfu Moja na mia Tano(1,500).
Mbona bei ya kawaida sana hiyo. Dar tunalipia zaidi ya hiyo kwa unit moja na ni kawaida tu.

Unit moja ni lita 1,000 za maji. Wewe unatumiaje maji hebu tuambie. Sio unapiga kelele hapa kumbe nyumbani kuna uharibifu unaendelea.

Unakuta watoto wana mwaga mwaga maji hovyo, dada wa kazi hayupo makini,mke hajui kusimamia familia ufujaji umetawala. Mwisho wa mwezi idara ya maji wamekuletea bill yako unaanza kulalamika.

Chunguza mfumo wa maji hapo kwako. Anza na ripoti za usomaji wa mita. Kiwango cha unit unazotumia kila mwezi kipo sawa sawa kulingana na matumizi yako nyumbani?

Kama unit zinasoma nyingi kuliko matumizi halisi then ita fundi bomba kagua mifumo ya maji pengine inavuja au kuna upotevu unaosababishwa na uzembe wa matumizi mabaya.

Mtu anaingia chooni hajakojoa wala kukata gogo amejamba tu ,anavuta flusher mwaaaaaaaaaaah ana mwaga maji ya bure,lile drum la kuflush linabeba lita 10 kwa wastani ingawa zipo za ujazo mdogo ila nyingi ni lita 10,watu wakiwa wanaflush hovyo kwa siku watu wanaflush mara 50 then jua choo tu kwa siku kinakata nusu unit hapo haujaongeza matumizi mengine ya maji ya nyumbani.

So jikague.
 
Acha kulalama mwanamme,huku niliko dumu moja la Lita 20 ni sh 500/ wewe unakuja na kilio Cha Lita 1000 Kwa shilingi 15,000+ wakati huo ni maji safi na salama!!!
Ndio maana mnakufa mapema,Kisa kuitwa mwanaume!Sifa za kitoto,toa hoja,huko kuuziwa hizo bei juu hao uliowataja,unadhani wanapenda?
 
Back
Top Bottom