Mbona bei ya kawaida sana hiyo. Dar tunalipia zaidi ya hiyo kwa unit moja na ni kawaida tu.
Unit moja ni lita 1,000 za maji. Wewe unatumiaje maji hebu tuambie. Sio unapiga kelele hapa kumbe nyumbani kuna uharibifu unaendelea.
Unakuta watoto wana mwaga mwaga maji hovyo, dada wa kazi hayupo makini,mke hajui kusimamia familia ufujaji umetawala. Mwisho wa mwezi idara ya maji wamekuletea bill yako unaanza kulalamika.
Chunguza mfumo wa maji hapo kwako. Anza na ripoti za usomaji wa mita. Kiwango cha unit unazotumia kila mwezi kipo sawa sawa kulingana na matumizi yako nyumbani?
Kama unit zinasoma nyingi kuliko matumizi halisi then ita fundi bomba kagua mifumo ya maji pengine inavuja au kuna upotevu unaosababishwa na uzembe wa matumizi mabaya.
Mtu anaingia chooni hajakojoa wala kukata gogo amejamba tu ,anavuta flusher mwaaaaaaaaaaah ana mwaga maji ya bure,lile drum la kuflush linabeba lita 10 kwa wastani ingawa zipo za ujazo mdogo ila nyingi ni lita 10,watu wakiwa wanaflush hovyo kwa siku watu wanaflush mara 50 then jua choo tu kwa siku kinakata nusu unit hapo haujaongeza matumizi mengine ya maji ya nyumbani.
So jikague.