Ukisoma kwenye details za business licence, Aliance business council wako specified kama Business Manager, na hata office set up yao inaonekana ni virtual office na kwa maelezo yao ni kwamba anatumia hapo office akihitaji hujamaliz8a kuwa ni bure, kuna contracts analipia service n.k, kitu ambacho ni cha kawaida kabisa katika ku run biashara na kupunguza gharama hasa ukiwa una operate kwenye nchi nyingi huwezi kuweka wafanyakazi kila mahali
Mimi ningependa kufahamu ni vipi haswa kawapiga ZBC ama anaitumia Azam kuipiga ZBC, Suala la yeye kutumia ofisi za Azam kuna shida gani?kama ni consultant wao wameamua kumpa ofisi afanye kazi
Sababu una nia ya kufahamu wacha nikusaidie.
Kwa sababu ya nature ya nchi, UAE inavutia wakazi wengi wa duniani kuwekeza na kufanya biashara huko.
Sababu ya sababu ya wingi serikali yao haijihusishi moja kwa moja na usajiri wa makampuni kama ilivyo Brela huku kwetu.
Bali inatumia makampuni binafsi kama agents wa kusajiri makampuni kwa niaba ya serikali.
Hivyo ABC haifanyi biashara ya kukodisha ofisi.
Na umeuliza juu ya virtual office.
DV International anasema wao ni kampuni ya kufanya supply ya goods, hauwezi kuwa unasaupply goods, au hardwares na ukasema unafanya virtual office, hii sio just consulting. Ni biashara ya kussuply products.
Ambapo nature ya kampuni hiyo lazima iwe na office, showroom na ikiwezekana workshop. Zaidi ya yote lazima iwe na staff ambao ni professionals katika kazi wanazofanya.
Sasa kuitumia Azam kuna kuja namna hii.
Broadcast Manager wa Azam ndie alimleta Huyu mtu na wanashirikiana, sababu yeye ni mgeni huenda aliushawishi uongozi wa Azam kuwa hiyo kampuni ina uwezo na ikaweza aminika na kupata kazi Azam. Kumbuka Azam ni private company, inaponunua haifuati sheria ya manunuzi ya umma, hivyo mtu unayemuamini akikupa reference ni rahisi kufanya manunuzi.
Sasa baada ya kufanya kazi waliyofanya Azam wakaplot namna ya kufanya kazi na ZBC.
Sasa ZBC ni shirika la umma, huwezi tu kwenda kwa mtu kununua bila kufanya mchakato wa utangazaji wa Zabuni.
Sasa kinachoonekana kupitia ushawishi wa huyu jamaa wa Azam waliweza fanya lobbying na kukiuka sheria hiyo na kumpa jamaa kazi kadhaa kama Single source. Kitu ambacho ni kinyume cha sheria za manunuzi ya umma.
Sasa ili jamaa kuwaaminisha ZBC kuwa ana uwezo basi kama alivyotaka fanya kwa mtu wangu anawaambia wakutane Azam, ambapo kuna uwezekano akawaonyesha hadi vitu ambavyo yeye hakufanya ili kuwaaminisha ni kampuni kubwa na inafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi aliyosajiriwa na za nchi husika.