Zanzibar 2020 DW: Jussa anapendekeza kuundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani Zanzibar

Zanzibar 2020 DW: Jussa anapendekeza kuundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani Zanzibar

Alshaojiwa bwashee,na akasema wazi yeye hana maamuzi mpaka uongozi wa chama ukubaliane.
Alafu mie sio bwashee, alafu mwenyekiti wa chama husika alishaweka msimamo wazi, niseme Mimi maridhiano nayapenda Sana ila yazingatie yafuatayo
Kurudia uchaguzi
Tume huru
Katiba mpya
 
Jama tuwe na kawaida ya kuskiliza kabla ya kuchangia , mie niliona jana kwa twitter ya Ally Saleh ikabidi nitafute hayo mahojiano na dakika kumi zote sijaskia pahala Jussa anasema kuhusu hiyo serikali ya umoja wa kitaifa. kuna watu wanataka kuvuruga watu tu.
 
nikiona maneno ya hivi tena kutoka kwa wanasiasa wa upinzani nachoka kabisaa, sijui kama aliziona maiti za wale vijana wa Zanzibar waliouwa kikatili kabisa tare 27, 28 na 29 Oktoba
Ndiyo ujue yote ni maigizo, yaani mtu katobolewa utumbo hapelekwi polisi wala hospital ni kuchukuwa picha tu na kurusha mitandaoni.
 
Alafu mie sio bwashee, alafu mwenyekiti wa chama husika alishaweka msimamo wazi, niseme Mimi maridhiano nayapenda Sana ila yazingatie yafuatayo
Kurudia uchaguzi
Tume huru
Katiba mpya
Kurudia uchaguzi sahau kabisa.
katiba mpya angalau inawezekana japo kutakuwa na vigingi vingi.
 
Kurudia uchaguzi sahau kabisa.
katiba mpya angalau inawezekana japo kutakuwa na vigingi vingi.
Hivi mkuu kwa sauti ya pole ,mtu umeshinda tena kwa kishindo, wapigakura ni wale wale na unapendwa Sana,wakati watu wanakusingizia kwamba umeiba kura why usirudie uchaguzi ili uwakomeshe ki mdomo domo Chao,tena kwa kuweka tume huru,au kuomba hata UN wasimamie ili uwaonyeshe dunia jinsi unavyokubalika, Kama hili haliwezekaniki.

Basi ni marufuku ccm kusema mmeshinda kwa shindo, Hiko clear mkisema hamna pesa ya uchaguzi kila mwananchi achnge elf 20 ya uchaguzi kufika februali mwakani ,mtashangaa account ya hizi pesa itavimba sana
 
Hivi mkuu kwa sauti ya pole ,mtu umeshinda tena kwa kishindo, wapigakura ni wale wale na unapendwa Sana,wakati watu wanakusingizia kwamba umeiba kura why usirudie uchaguzi ili uwakomeshe ki mdomo domo Chao,tena kwa kuweka tume huru...
Uchaguzi haurudiwi, kama ni kususa msuse lakini uchaguzi kurudiwa ni haramu.
 
Njaa hizi zimezidi!
Jussa unamjua lakini... huyo ni mnazi wa upinzani wewe huingii kwake hata mara milioni, ameyaishi mapambano sio wewe upo mitandaoni huku, ukiona kasema hivyo ashawaza mbali... political calculations
 
Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, vyama vya upinzani vilipata wabunge wa majimbo wananne na wabunge wa viti maalum 19 na hivyo kuwa na wabunge 27. Kwa matokeo haya Maalim Seif naye kapata sifa ya kuwa makamu wa kwanza wa serikali ya Zanzibar.

Imekuwa ni kawaida tangia mwaka 1995 tulipoanza uchaguzi wa vyama vingi, kila uchaguzi mkuu vyama vya upinzani vimekuwa vikiyakataa matokeo ya chaguzi hizo kwa madai ya kuibiwa kura. Hata hivyo havijawahi kususia nafasi zake za ubunge na ruzuku vilivyotokana na chaguzi hizo isipokuwa za mwaka huu.

Mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi huu yaliyoonesha viongozi wakuu wa vyama hivi (Mbowe na Zitto) kuambulia hola kwenye majimbo yao, havikuwa na kigugumizi cho chote kutangaza kususia nafasi hizo 27 za ubunge. Lakini kwa suala la Maalimu Seif kususia nafasi ya umakamu wa kwanza wa raisi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ni kizungumukuti. Na hivyo hivyo kwenye kukataa ruzuku?

Kwa nini iwe hivyo? Kwa nini wabunge hawa wa viti maalum na wale 8 wa majimbo wadhurumiwe haki zao? Si walisema ni kazi na bata, sasa kwa nini mnawazuia hawa kwenda kula bata? Jamaani acheni roho mbaya. Bata na maendeleo hayana chama! Mkifanya hivyo mnakiua chama chenu completely!
 
Kwani nyie Mataga upinzani ukifa si ndiyo mtakuwa mmetimiza lengo? Sasa mko peke yenu bado mnataka nini cha zaidi?
 
Mosi; Seif hachaguliwi/haingii kua makam wakwanza kwa idadi ya wabunge?

Pili: Seif alisusia kuwa makam wa kwanza 2015 japo alistahili ni hakwenda kulamba mtu

Tatu hao wabunge27 unaowataja 3 CUF 3, ACT 1, CHADEMA 9 vitimaalum chadema wanachangia vipi Seif kuwa makamu wa kwanza
 
Kinachonifurahisha kuhusu wanasiasa wote Tanzania ni wanajali kuhusu wao tuu
 
Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha ACT Wazalendo Ismail Jussa Ladhu anaeuguza majeraha baada ya kupigwa walipokuwa wanafanya maandamano Visiwani Zanzibar katika Maandamano hayo ya tarehe 29 mwezi wa Oktoba yalikuwa ya amani ila maafisa wa usalama waliwavamia na kuwajeruhi baadhi ya viongozi wa upinzani...
Hata Picha yako inaonesha tu, kama siyo yule raia wa Ubeligiji Mtetezi wa haki za Mashoga Duniani na Muabudu kuzimu.

Hakuna nchi Duniani Zaidi ya Tanzania inayoheshimu Sheria na taratibu walizojiwekea toka enzi za Mababu zetu.

Ndiyo maana Wakoloni wote wanaamini maala salama pa kuishi na penye Matumaini ni Tanzania.
 
Hakuna nchi Duniani Zaidi ya Tanzania inayoheshimu Sheria na taratibu walizojiwekea toka enzi za Mababu zetu.
Ni kama mbuni tu,unaficha kichwa kwenye mchanga wakati tako zipo nje. unakuwa muongo kuliko hata uongo wenyewe.
 
Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha ACT Wazalendo Ismail Jussa Ladhu anaeuguza majeraha baada ya kupigwa walipokuwa wanafanya maandamano Visiwani Zanzibar katika Maandamano hayo ya tarehe 29 mwezi wa Oktoba yalikuwa ya amani ila maafisa wa usalama waliwavamia na kuwajeruhi baadhi ya viongozi wa upinzani.

Mwandishi wa DW, Thelma Mwadzaya amezungumza Kinagaubaga na Jussa kuhusu siasa za visiwani Zanzibar na Jussa anapendekeza kuundwe serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar.

My Take
Kuunda serikali na CCM hii hii au?

That would be fantastic. Wajenge Zanzibar pamoja badala ya kupoteza muda kupambana.
 
Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha ACT Wazalendo Ismail Jussa Ladhu anaeuguza majeraha baada ya kupigwa walipokuwa wanafanya maandamano Visiwani Zanzibar katika Maandamano hayo ya tarehe 29 mwezi wa Oktoba yalikuwa ya amani ila maafisa wa usalama waliwavamia na kuwajeruhi baadhi ya viongozi wa upinzani.

Mwandishi wa DW, Thelma Mwadzaya amezungumza Kinagaubaga na Jussa kuhusu siasa za visiwani Zanzibar na Jussa anapendekeza kuundwe serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar.

My Take
Kuunda serikali na CCM hii hii au?
Ni kwamba hiyo serikali ya umoja itaongozwa na ACT Wazalendo na Mwinyi kuwa makamu wa kwanza wa Rais.
 
Back
Top Bottom