Zanzibar 2020 DW: Jussa anapendekeza kuundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani Zanzibar

Zanzibar 2020 DW: Jussa anapendekeza kuundwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani Zanzibar

nikiona maneno ya hivi tena kutoka kwa wanasiasa wa upinzani nachoka kabisaa, sijui kama aliziona maiti za wale vijana wa Zanzibar waliouwa kikatili kabisa tare 27, 28 na 29 Oktoba
Hizi ni propaganda nyengine kutoka kwa watawala ili wawachanganye Watanzania akili

Unakumbuka hivi majuzi tu Watawala walitaka kugushi saini za Wabunge wa kuteuliwa kutoka Chadema,ili raia waone kuwa CDM wamekubali kutea Wabunge

Nimisikiliza hiyo Clip ya mahojiano ya Jusa na DW hamna kitu kama hicho
 
Mosi; Seif hachaguliwi/haingii kua makam wakwanza kwa idadi ya wabunge?

Pili: Seif alisusia kuwa makam wa kwanza 2015 japo alistahili ni hakwenda kulamba mtu

Tatu hao wabunge27 unaowataja 3 CUF 3, ACT 1, CHADEMA 9 vitimaalum chadema wanachangia vipi Seif kuwa makamu wa kwanza
Sifa inayotakiwa ni idadi ya kura alizopata kwenye uchaguzi mkuu. Ni lazima idadi hii iwe angalao 10% ya kura zote halali zilizopigwa na awe wa pili kwa wagombea wote wa urais walioshiriki uchaguzi huo. Mwaka 2015 alisusa uchaguzi huo. Wa pili kwa walioshiriki ugombea urais katika uchaguzi huo hakufikisha hiyo 10% ya kura, hivyo kukosa sifa ya kuwa makamu wa kwanza wa rais.
 
Kwanini hamuendi mahakamani kutafuta haki Kama mmeibiwa...mkiambiwa pelekeni ushahidi hata wa karatasi moja hamna...Sasa mnacholilia nini
Ukipitia posts mbalimbali humu ndani utagundua kuwa Watanzania wengi ni wajinga na hawafaham kinachoendelea ingawa wengi wao wanajifanya wajuaji sana.

Sasa wewe Matokeo ya Rais unayapingaje wakati Katiba haitoi hiyo Fursa?
 
Kumbe mnajua sheria jomba Kama ndio hivyo kwann mnatulalamikia humu mjengoni..inatuhusu Nini kwani humu Kuna mahakimu..hatuna haja
 
Mahakama gani hiyo? Mahakama ya Tanzania ni CCM, majaji ni CCM, wakili ni CCM, polisi ni CCM unamshitaki CCM na unategemea nini kitachotokea?
Ok kama ndio hivyo, shut upz..hatutaki tena kusikia kelele zinazohusiana...nendeni mkajipange upyaaa jomba, Safari hii wananchi wamewaadhibu Kali mno..msirudie Tena kuchezacheza
 
Safari hii sasa ni LAZIMA tujue maana ya ule msemo.... Mapinduziiiii......

Wasituchoshe hawa..,kutufanya wajinga wakati mipango wanapanga wao... Zitto yupo very specific

Tinasubiri..hatuwezi kuhukumu kwa sasa!! Subira yavuta kheri na akiba ya maneno huwa ni busara.
 
Kwanini hamuendi mahakamani kutafuta haki Kama mmeibiwa...mkiambiwa pelekeni ushahidi hata wa karatasi moja hamna...Sasa mnacholilia nini
Mbuzi akashtaki kwa fisi kwamba mtoto wake kapotelea nyumbani kwa chui au vipi? Sijui kichwani mmejaza funza???

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Serikali ya umoja wa Kitaifa na walioiba uchaguzi?

Kama wapinzani huko Zanzibar wana akili za kuku namna hii basi CCM iendelee kuwatandika tu maana hawana akili!
Wewe ni mshabiki tu wa upinzani wenye vyama ndiyo wenye maamuzi. Tuliza mshono dada!!
 
Ok kama ndio hivyo, shut upz..hatutaki tena kusikia kelele zinazohusiana...nendeni mkajipange upyaaa jomba, Safari hii wananchi wamewaadhibu Kali mno..msirudie Tena kuchezacheza
Grow up, kama huna la kusema la maana si ukae kimya tu!
 
Grow up, kama huna la kusema la maana si ukae kimya tu!
Sindano imekuingia nywiiii..msiwachukulie poa watanzania..Wana akili kuliko mnavyodhani...eti kuwakimbia na kutorokea nje na familia zenu ndio mnaona solution...hahahah ...watanzania Hawa waliwaona
Mliwakimbia wakati wa korona bungeni mlidhani Nani angewasemea matatizo yao
Mliwadhihaki nankuwaona wajinga kwa wao kuunga mkono maendeleo yaliyofanywa na Magufuli
Mliwashtaki wawekewe vikwazo na wazungu bila huruma yoyote..Lakini mlishindwa....
 
Hivi kweli Jussa amesema na kushauri haya? Kama kweli kasema basi leo ndio mie nahakikisha kweli wanasiasa woooooote wa Tanzania wanaweka mahitaji yao mbele na wanawatumia wananchi kufikia malengo yao tu!

Hivi Jussa amesahau ule msemo wa unakula na kipofu lakini humshiki mkono? Kuna manufaa gani yatakayofikiwa kwa kuwa na serikali ya umoja wa kimataifa Zanzibar? Si tuliwahi kuwa nayo huko nyuma? Nini kilipatikana na nini kilibadilika? Hakuna kilichobadilika punda alikuwa yule yule lilibadilika ni soji tu!

Siamini kiongozi kama Jussa ambae mwenyewe amepewa kichapo cha mbwa, anataka watu waliopewa vichapo vya mbwa na kujikuta na ulemavu wa milele, watu waliopoteza maisha yao, mali zao na nguvu zao, watu waliopoteza ndugu zao, wazee wao na watoto wao washau yote hayo na wakubali Seif sharif na viongozi wenzake wapewe nyadhifa katika serikali ya umoja wa kitaifa. Siamini Jussa anataka Wazanzibari wa ACT baada ya yote waliyoyafanya na maumivu yote waliyoyapata kwa sababu ya kuunga mkono chama cha ACT, Jussa yuko tayari kukaa meza moja na CCM. CCM hii hii ambayo iliidhinisha na kufumbia macho vipigo vya wanachama wa CUF.

To be honest hata sijui kwa nini nashangaa, ACT inaongozwa na Seif Sharif ambae ni mahiri sana katika kuwaendea kinyume wenzake kwa manufaa yake binafsi. Aliwaendea kinyume akina Aboud Jumbe na wenzake pale viongozi wa serikali ya Zanzibar (akiwemo Seif Sharif) walipokwenda kwa Nyerere kutaka Tanzania iwe na serikali tatu.

Sote tunajua aliwaendea kinyume mara tu alipoahidiwa na Nyerere kuwa atamtayarisha kuwa Rais wa zanzibar siku za mbeleni. Seif huyu huyu akaamua kuwaendea kinyume CCM baada ya kuona kuwa ahadi aliopewa na Nyerere haikuwa ya kweli na akaamua kuleta matata ndani ya chama na hatimae kufukuzwa CCM mwaka 1987.

Seif huyu huyu aliwaendea kinyume wazanzibari wenzake mwaka 2010 akiwa kiongozi wa CUF pale alipokubali kuingia katika serikali ya mseto na CCM ilhali wanachama wake walijitoa mhanga na kuhakikisha kuwa anashinda uchaguzi na alishinda. Alisahau kuwa watu wamepigwa, wamepoteza mali zao na wengine kuuliwa kwa sababu tu ya kutaka CUF ishinde, lakini alipoonyeshwa fupa tu, Seif alilirukia na kuchukua cheo cha chief of minister of zanzibar.

Na sasa anataka kufanya yale yale tena!!!!!!!!!
Umefanikiwa kuandika makala ndefu bila kutazama video yenyewe.
Usiwe mvivu, nenda katazame video mwenyewe ili uje ufute hili gazeti uliloshusha hapa.
 
Wengi mnaocomment hamjaitazama video yenyewe.
Amesema.kwenye mahojiano ni afadhali basi wafute mfumo wa vyama vingi kwasababu inaonekana badala ya ustawi wa kisiasa inakuwa ni uhasama na mauaji.
 
Sindano imekuingia nywiiii..msiwachukulie poa watanzania..Wana akili kuliko mnavyodhani...eti kuwakimbia na kutorokea nje na familia zenu ndio mnaona solution...hahahah ...watanzania Hawa waliwaona
Mliwakimbia wakati wa korona bungeni mlidhani Nani angewasemea matatizo yao
Mliwadhihaki nankuwaona wajinga kwa wao kuunga mkono maendeleo yaliyofanywa na Magufuli
Mliwashtaki wawekewe vikwazo na wazungu bila huruma yoyote..Lakini mlishindwa....
Ama kweli Tanzania imejaa majuha kalulu kama wewe! Unakuja hapa kwenye ukumbi wa siasana kuleta maneno ya kitoto tu. Hivi unadhani kila anae criticize serikali basi ni mwanachama cha upinzani? Unaishi maisha ya aina gani wewe hasa? Nakwambia tena Grow up! By the way dont bother replying this as i am going to ignore any of your posts. I dont have time to waste having conversation with someone is thick as a plank.
 
Umefanikiwa kuandika makala ndefu bila kutazama video yenyewe.
Usiwe mvivu, nenda katazame video mwenyewe ili uje ufute hili gazeti uliloshusha hapa.
Si uvivu, ila hii habari ilipotumwa mwanzo ilitumwa bila ya video clip. Video clip iliongezwa baadae. However nasimama na nilichokisema na sitofuta post yangu. Thank you.
 
Exactly, kutaka kushirikiana na wauaji ni ujuha kama ujuha mwingine, na hauvumiliki.
Mwenzetu ameshaona fursa ya kuwa kwenye baraza! Kazi kweli kweli! Hawa ndio wapinzani wetu tulio nao!
 
Wazanzibari wana high IQ ni wacha Mungu na siyo animalistic kama wewe, wanaelewa umuhimu wa kuishi pamoja, Nani watu waungwana, ...
 
Mjumbe wa kamati kuu ya chama cha ACT Wazalendo Ismail Jussa Ladhu anaeuguza majeraha baada ya kupigwa walipokuwa wanafanya maandamano Visiwani Zanzibar katika Maandamano hayo ya tarehe 29 mwezi wa Oktoba yalikuwa ya amani ila maafisa wa usalama waliwavamia na kuwajeruhi baadhi ya viongozi wa upinzani.

Mwandishi wa DW, Thelma Mwadzaya amezungumza Kinagaubaga na Jussa kuhusu siasa za visiwani Zanzibar na Jussa anapendekeza kuundwe serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar.

My Take
Kuunda serikali na CCM hii hii au?

Update:
Mahojiano ya Jussa na DW (Sauti)
View attachment 1624824
Kwanza anataka iundwe mara ngapi wakati Mzee Maalim Seif anasubiriwa aapishwe kama Makamu wa Kwanza wa Rais pamoja na kupendekeza baadhi ya watu wake kuingia kwenye Baraza la Mawaziri?
 
Ha hataki kususa kama ilivyokuwa 2015?

Waache wasuse kama walivyofanya kipindi cha awamu ya Rais mstaafu Dr Shein, familia zao ziendelee ku - flip Tanzanian burgers (kupita maamri/maandazi) kwa kipindi kingine cha miaka mitano (till 2025)!!! Maalim Seif hataki nafasi ya umakamo wa kwanza wa Rais - let it remain vacant.
 
Kwanini hamuendi mahakamani kutafuta haki Kama mmeibiwa...mkiambiwa pelekeni ushahidi hata wa karatasi moja hamna...Sasa mnacholilia nini
Waende mahakamani? You guy, you must be crazy 😦😦
 
Back
Top Bottom